{"result":[{"id":1,"sura":1,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Suratul-Fatiha."},{"id":2,"sura":1,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Nayo iliteremka Makka"},{"id":3,"sura":1,"from_aya":1,"to_aya":7,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. 2. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu. 3. Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. 4. Mmiliki wa Siku ya Malipo. 5. Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada. 6. Tuongoze katika njia iliyonyooka. 7. Njia ya wale uliowaneemesha. Siyo ya wale waliokasirikiwa, wala waliopotea. "},{"id":4,"sura":1,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"(1) Yaani, ninaanza kwa kila Jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu neno: \u201cJina\u201d liko katika hali ya umoja, na limeunganishwa (na neno Mwenyezi Mungu). Kwa hivyo (huko kuunganisha) kunajumuisha majina mazuri yote. \"Allah (Mwenyezi Mungu)\" ni yule anayefanyiwa uungu, anayestahiki kuabudiwa yeye peke yake, kwa sababu anasifika kwa sifa za uungu, ambazo ni sifa kamilifu. \"Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu\" ni majina mawili yanayoonyesha kuwa yeye Mtukufu ni mwenye rehema kuu kunjufu, ambazo zimeenea  kila kitu, na zinazojumuisha kila kilicho hai. Na (Mwenyezi Mungu) aliwaandikia rehema zake wachamungu wanaowafuata Manabii wake na Mitume wake. Basi, hao wana rehema kabisa. Nao wasiokuwa wao wana fungu tu kwazo (yani katika rehema hizo). Na jua ya kwamba katika misingi waliyokubaliana juu yake wale watangulizi wema wa umma huu na maimamu wake ni kuamini katika majina ya Mwenyezi Mungu na Sifa zake, na hukumu za Sifa hizo. Kwa hivyo, wanaamini kwa mfano, kwamba yeye ni Rahman (Mwingi wa Rehema), Rahim (Mwenye Kurehemu), mwenye rehema ambazo anasifika kwazo, zinazofungamana na wanaorehemewa. Kwa hivyo, neema zote ni athari katika athari za rehema yake, na vivyo hivyo katika majina mengineyo yote. Inasemwa kuhusu (jina lake) Al-\u2018Aliim (Mwenye elimu) kuwa yeye ni Mjuzi, Mwenye elimu, anayejua kwayo kila kitu. Qadiir (Muweza) mwenye uwezo, anayeweza kila kitu."},{"id":5,"sura":1,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"(2) \"Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.\" Ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa sifa za ukamilifu, na kwa vitendo vyake vinavyozunguka kati ya kupeana fadhila na kufanya uadilifu. Kwa hivyo, ni zake sifa zote za ukamilifu kwa namna zote. \"Mola Mlezi wa viumbe wa walimwengu.\" Mola Mlezi ni yule anayewalea walimwengu wote - nao ni kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu - kwa kuwaumba, kuwaandalia ala, kuwaneemesha kwa neema kubwa ambazo lau kuwa watazipoteza, basi hawataendelea kuishi. Kwa hivyo, neema yoyote waliyo nayo ni kutoka kwake (Mwenyezi Mungu) Mtukufu. Na ulezi wake (Mwenyezi Mungu) Mtukufu kwa viumbe wake ni wa aina mbili: Wa kiujumla na mahususi. Ama wa kiujumla ni kuumba kwake viumbe, kuwapa riziki, na kuwaongoza katika yale yaliyo na masilahi yao ambayo ndani yake kuna kuendelea kwao kuishi katika dunia. Nao (ulezi wake) mahususi ni kulea kwake vipenzi wake; kwa kuwalea kwa imani, na kuwawezesha kuifikia (imani), na kuwakamilishia imani, na kuwaepushia yale yanayoweza kuwatoa katika imani, na vizuizi vinavyozuia kati yao na Yeye. Na uhakika wake ni kuwalea kwa kuwawezesha kufikia kila la heri, na kuwahifadhi kutokana na kila shari. Na huenda hii maana ndiyo siri iliyofanya dua nyingi za manabii kuwa na neno \"Mola Mlezi.\" Kwa maana, mahitaji yao yote yanaingia ndani ya ulezi wake mahususi. Kwa hivyo, kauli yake \"Mola Mlezi wa walimwengu\" ikaashiria upweke wake katika kuumba, kuendesha mambo, kuneemesha, na kujitosheleza kwake kikamilifu, na kumhitaji kwa viumbe kabisa na kwa namna zote na kuzingatia kwote."},{"id":6,"sura":1,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"(4) \"Mmiliki wa Siku ya Malipo.\" Al-Malik ni yule anayesifika na sifa ya kumiliki, ambayo miongoni mwa athari zake ni kuwa anaamrisha na kukataza, na analipa mazuri na anaadhibu, na anawaendesha wale anaowamiliki kwa kila aina ya kuendesha. Na amefungamanisha umiliki  na Siku ya Malipo, nayo ni Siku ya Qiyama, siku ambayo watu watahukumiwa ndani yake kwa matendo yao, mema yake na mabaya yake. Kwa sababu, siku hiyo, viumbe watadhihirikiwa katika sura kamili, ukamilifu wa umiliki wake, uadilifu wake, hekima yake, na kukatika kwa miliki za viumbe kwa kiasi kwamba siku hiyo; wafalme, raia, watumwa, na watu huru watakuwa sawa. Wote watatii kwa sababu ya ukuu wake, na watanyenyekea sababu ya Nguvu zake, wakingoja malipo yake, wakitaraji malipo yake mazuri, na wakihofu adhabu yake. Na kwa sababu hiyo, aliitaja hususan. Vinginevyo, yeye ndiye mmiliki wa Siku ya Malipo na siku nyinginezo."},{"id":7,"sura":1,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"(5) Na kauli yake, \"Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.\" Yaani, tunakufanyia wewe peke yako ibada zetu, na kukuomba msaada. Kwa sababu, kutanguliza mwathiriwa (yaani, \u201cWewe tu\u201d) kunamaanisha kuthibitisha kitu, nako ni kuthibitisha hukumu kwa aliyetajwa, na kumkanusha kwa mwingine asiyekuwa yeye. Ni kana kwamba anasema: \u201cTunakuabudu wewe, na wala hatumuabudu asiyekuwa Wewe. Na tunakuomba msaada, na wala hatumwombi msaada asiyekuwa Wewe.\u201d Na kutanguliza kutaja ibada kabla ya kuomba msaada ni katika mlango wa kutanguliza yaliyo ya jumla kabla ya yale mahususi, na kwa sababu ya kuzingatia kutanguliza haki yake (Mwenyezi Mungu) Mtukufu mbele ya haki ya mja wake. Na ibada ni neno linalojumuisha kila akipendacho Mwenyezi Mungu na anakiridhia katika vitendo na maneno, ya dhahiri na ya siri. Na kutaka msaada ni kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuleta manufaa, na kuyazuia yenye kudhuru pamoja na kumuamini Yeye katika kuyatafuta hayo. Na kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumwomba msaada ndiyo njia ya kufikia kufaulu kwa milele, na kuokoka kutokana na shari zote. Kwa hivyo, hakuna njia yoyote ya kuokoka isipokuwa kwa kuyafanya yote mawili. Na kwa hakika, ibada huwa ibada tu ikiwa itachukuliwa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, na kwa kukusudia kwayo kumridhisha Mwenyezi Mungu. Na kwa haya mambo mawili ndiyo ibada huwa. Na alitaja kuomba msaada baada ya ibada ijapokuwa kuomba msaada kunaingia humo (katika ibada); kwa sababu mja katika ibada zake zote anahitaji kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani, Mwenyezi Mungu asipomsaidia, hatapata anachotaka miongoni mwa kufanya maamrisho na kuacha makatazo."},{"id":8,"sura":1,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0622\u064a\u0627\u062a","text":"Kisha (Mwenyezi Mungu) Mtukufu akasema:"},{"id":9,"sura":1,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} \"Tuongoe katika njia iliyonyooka.\" Yaani tuonyeshe, tuongoze, na utuwezeshe kuifikia njia iliyonyooka. Nayo ni njia iliyo wazi inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na kwa Pepo yake. Nayo ni kujua haki na kuifanyia kazi. Basi tuongoze kuelekea kwenye hiyo njia, na utuongoze katika hiyo njia. Na kuongoza kuelekea kwenye hiyo njia ni kushikamana na dini ya Uislamu na kuacha zisizokuwa hiyo miongoni mwa dini. Nako kuongoza katika njia hiyo kunajumuisha kuongoka katika maelezo yote ya undani ya kidini, kwa elimu na vitendo. Na dua hii ni mojawapo ya dua zenye kujumuisha mno, na yenye kumnufaisha mja zaidi. Na ndiyo maana ni lazima kwa mtu amwombe Mwenyezi Mungu kwayo katika kila rakaa ya swala yake, kwa sababu yeye analihitaji hilo zaidi. Na njia hii iliyonyooka ndiyo:"},{"id":10,"sura":1,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} \u201cNjia ya wale uliowaneemesha\u201d miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi (watu wakweli), na Mashahidi, na Watu wema. \u201cSiyo\u201d njia ya \u201cwale waliokasirikiwa,\u201d wale waliojua haki na wakaiacha kama vile Mayahudi na mfano wao. Na siyo njia ya wale \u201cwaliopotea\u201d ambao waliacha haki kwa ujinga na upotovu kama vile Wakristo na mfano wao."},{"id":11,"sura":1,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Licha ya ufupi wake, sura hii imekusanya yale ambayo sura yoyote katika sura za Qur-ani haijakusanya. Imekusanya aina tatu za Tawhidi: Tawhidur-Rububiyya (kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika uungu wake) inachukuliwa kutoka kwa kauli yake \u201cMola Mlezi wa walimwengu.\u201d Na Tauhidul-Uluhiyya, ambayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika ibada inachukuliwa kutoka kwa neno \u201cAllah (Mwenyezi Mungu),\u201d na kutoka kwa kauli yake \u201cWewe tu tunakuabudu.\u201d Na Tawhidul-Asmaa was-Swifaat, ambayo ni kuthibitisha sifa za ukamilifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambazo alijithibitishia yeye Mwenyewe, na alizomthibitishia Mtume wake, bila Ta'atwil (kuzikanusha), wala Tamthil (kuzipigia mfano), wala Tashbih (kufananisha). Na neno \u201csifa njema zote\u201d ndilo limeashiria hilo kama ilivyotangulia. Na (sura hii pia) inajumuisha uthibitisho wa unabii katika kauli yake, \u201cTuongoe njia iliyonyooka\u201d, kwa sababu hilo haliwezekani bila ya kutuma ujumbe. Na ina uthibitisho wa malipo kwa matendo katika kauli yake \u201cMmiliki wa Siku ya Malipo\u201d, na kwamba malipo yatakuwa kwa uadilifu, kwa sababu neno \u201cdiin\u201d linamaanisha kulipa kwa uadilifu. Na inajumuisha uthibitisho wa Qadar (makadirio ya Mwenyezi Mungu), na kwamba mja ndiye mtendaji halisi, tofauti na Al-Qadariyya (wanaopinga kuwa mwanadamu anatenda kihalisi) na Al-Jabriyya (wanaosema kuwa mwanadamu hatendi chochote, lakini Mwenyezi Mungu ndiye humlazimisha kutenda). Bali inajumuisha jibu kwa watu wote wa bid\u2019a (wanaozua katika dini) na upotovu katika kauli yake \u201cTuongoe njia iliyonyooka;\u201d kwa sababu ni kujua haki na kuifanyia kazi. Na kila mwenye kuzua na kupotea, basi yeye yuko kinyume na hilo. Na inajumuisha kumpwekeshea Mwenyezi Mungu Mtukufu dini katika kumuabudu na kumuomba usaidizi, katika kauli yake; \u201cWewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.\u201d Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote."}]}