{"result":[{"id":1885,"sura":10,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Yunus"},{"id":1886,"sura":10,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Nayo iliteremka Makka"},{"id":1887,"sura":10,"from_aya":1,"to_aya":2,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Alif Lam Ra. Hizo ni Aya za Kitabu chenye hekima. 2. Je, imekuwa ajabu kwa watu kwamba tumemfunulia mwanamume kutokana nao kuwa, \u201cWaonye watu, na wabashirie wale walioamini ya kuwa wana cheo cha juu kwa Mola wao Mlezi?\u201d Wakasema makafiri, \u201cHakika huyu ni mchawi aliye dhahiri!\u201d "},{"id":1888,"sura":10,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Yeye Mtukufu Anasema, \u201cHizo ni Aya za Kitabu chenye hekima\u201d nacho ni Qur'ani hii iliyomo hekima na hukumu mbalimbali, ambayo Aya zake zinaonyesha uhakika wa kiimani na maamrisho na makatazo ya kisheria ambayo ni lazima juu ya umma wote kuipokea kwa kuridhia, na kukubali, na kufuata."},{"id":1889,"sura":10,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Na pamoja na haya, wengi wao walipeana mgongo, na wakakosa kujua, basi wakastaajabu, \u201ckwamba tumemfunulia mwanamume kutokana nao kuwa, \u201cWaonye watu\u201d adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wahofishe ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na wakumbushe Ishara za Mwenyezi Mungu, na wabashirie \u201cwale walioamini.\u201d Yaani, imani ya ukweli \u201ckuwa wana cheo cha juu kwa Mola wao Mlezi\u201d yaani, wana malipo mengi, na thawabu zilizohifadhiwa kwa Mola wao Mlezi kwa sababau ya matendo mema na ya ikhlasi waliyoyatanguliza. Basi makafiri wakamstaajabia mwanamume huyu mkubwa kustaajabu kulikowapelekea kumkufuru! Basi \"makafiri wakasema\" juu yake, \u201cHakika huyu ni mchawi aliye dhahiri!\u201d Yaani, mwenye uchawi ulio wazi, na haufichiki \u2013 kulingana na madai yao \u2013 kwa yeyote. Na hili ni katika upumbavu wao na ukaidi wao. Kwani walistaajabu kwa jambo ambalo si la kustaajabisha wala sio geni, bali kunashangaza ujinga wao na kutojua kwao masilahi yao. Vipi hawakumwamini Mtume huyu mtukufu ambaye Mwenyezi Mungu alimtuma kutokana nao wenyewe? Walimjua haki ya kumjua, lakini wakaukataa wito wake na wakawania kuibatilisha dini yake? Na Mwenyezi Mungu ataikamilisha nuru yake, hata kama makafiri watachukia."},{"id":1890,"sura":10,"from_aya":3,"to_aya":4,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"3. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, kisha akaimarika juu ya Kiti cha Enzi, anaendesha mambo yote. Hakuna mwombezi yeyote isipokuwa baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je, hamkumbuki? 4. Kwake Yeye tu ndiyo marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurejesha ili awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na wale waliokufuru, wana vinywaji vya maji ya moto, na adhabu chungu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyakufuru. "},{"id":1891,"sura":10,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} Yeye Mtukufu Anasema akibainisha umola wake, uungu wake, na ukuu wake, \u201cHakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita\u201d pamoja na kwamba anaweza kuziumba kwa muda mfupi sana, lakini kwa sababu ya hekima yake ya kiungu katika hilo, na kwa sababu Yeye ni mpole katika vitendo vyake. Na katika hekima yake, ndani yake ni kwamba aliziumba kwa haki na kwa ajili ya haki, ili ajulishe kuhusu majina yake na sifa zake, na ili afanyiwe Yeye tu ibada. \"Kisha\" baada ya kuziumba mbingu na ardhi \"akaimarika juu ya Kiti cha Enzi,\" kuimarika kunakolingana na ukuu wake. \"Anaendesha mambo yote\u201d katika ulimwengu wa juu na wa chini, kama vile kufisha na kuhuisha, na kuteremsha riziki, na kubadilisha masiku baina ya watu, na kuondoa madhara kwa wenye shida, na kuitikia maombi ya waombaji. Kwa hivyo, aina mbalimbali za uendeshaji vinashuka kutoka kwake na kupanda kwake, na viumbe vyote vinanyenyekea kwa utukufu wake na viko chini ya ukuu na mamlaka yake. \"Hakuna mwombezi yeyote isipokuwa baada ya idhini yake.\u201d Basi hakuna hata mmoja miongoni mwao anayeweza kuanza kufanya uombezi hata kama yeye ndiye mbora wa viumbe vyote mpaka Mwenyezi Mungu ampe idhini, na wala humpi idhini isipokuwa yule anayemridhia, na wala hawaridhii isipokuwa wenye ikhlasi na kumpwekesha Yeye. \"Huyo\" ambaye yuko hivi \"ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi.\u201d Yaani, Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye ambaye ana sifa ya uungu, ambayo inajumuisha sifa za ukamilifu, na sifa ya umola inayojumuisha sifa za matendo. \"Basi mwabuduni yeye.\" Yaani, mpwekesheni kwa yote mnayoweza miongoni mwa aina mbalimbali za uja. \u201cJe, hamkumbuki?\u201d Ushahidi mbalimbali unaoashiria kuwa Yeye pekee ndiye aabudiwaye, Msifiwa, Mwenye utukufu na heshima."},{"id":1892,"sura":10,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Alipotaja hukumu yake  ya kimajaliwa, ambayo ni uendeshaji wa jumla, na hukumu yake ya kidini, ambayo ni sheria yake, ambayo madhumuni yake na makusudio yake ni kumwabudu yeye peke yake, bila mshirika yeyote, akataja hukumu ya kimalipo, ambayo ni malipo yake kwa matendo baada ya kufa. Akasema: \"Kwake Yeye tu ndiyo marejeo yenu nyote.\u201d Yaani, atawakusanya baada ya kufa kwenu kwa ajili ya wakati na siku maalumu. \"Hakika Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurejesha\u201d kwa maana Mwenye uwezo wa kuanzisha uumbaji ni muweza wa kuurudisha. Na mwenye kuona kuanza kwake uumbaji kisha akakanusha kurudisha kwake uumbaji, basi hana akili, ni mwenye kukanusha mojawapo ya mawili yanayofanana, pamoja na kuthibitisha kwake kile kinachofaa zaidi ya hilo analolikanusha. Basi huu ni ushahidi ulio wazi wa kiakili juu ya kurudishwa kwa uumbaji (Siku ya Qiyama). Kisha akataja ushahidi wa kimaandiko, akasema: \"Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli;\u201d yaani, ni Ahadi yake ya ukweli, na ni lazima itimizwe, \u201cili awalipe kwa uadilifu wale walioamini\u201d kwa nyoyo zao yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu kuyaamini, \u201cna wakatenda mema\u201d kwa viungo vyao miongoni mwa wajibu mbalimbai na yale yanayopekezwa. \u201cKwa uadilifu,\u201d yaani: kwa imani yao na vitendo vyao, malipo ambayo alikwisha wabainishia waja wake na akajulisha kuwa hakuna nafsi yoyote inayojua waliyofichiwa miongoni mwa yale yafurahishayo macho. \"Na wale waliokufuru\u201d Aya za Mwenyezi Mungu, na wanawakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu, \u201cwana vinywaji vya maji ya moto\u201d yenye kubambua nyuso na kukata matumbo, \"na adhabu chungu\u201d kutoka kwa kila aina ya adhabu zinginezo \u201ckwa sababu ya yale waliyokuwa wakikufuru.\u201d Yaani, kwa sababu ya ukafiri wao na dhuluma yao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali wanajidhulumu wenyewe."},{"id":1893,"sura":10,"from_aya":5,"to_aya":6,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"5. Yeye ndiye aliyelijaalia jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo isipokuwa kwa haki. Anazipambanua Ishara kwa kaumu wanaojua. 6. Hakika katika kuhitalifiana usiku na mchana, na katika vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi, zipo Ishara kwa kaumu wamchao. "},{"id":1894,"sura":10,"from_aya":5,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5-6} Alipothibitisha umola wake na uungu wake, akataja ushahidi wa kiakili uliopo kwenye peo za macho zenye kuonyesha hili, na kuonyesha ukamilifu wake katika majina yake na sifa zake kama vile jua, mwezi, mbingu, ardhi, na vyote alivyoumba humo miongoni mwa viumbe wengine wote. Na akajulisha kuwa hizo ni Ishara \u201ckwa kaumu wanaojua\u201d na \u201ckwa kaumu wamchao\u201d kwa maana, Elimu huongoza kwenye kujua ushahidi ulio ndani yake, na jinsi ya kuondoa humo ushahidi kwa namna ya karibu zaidi. Na uchamungu husababisha matamanio ya heri katika moyo na kuhofu maovu, ambayo mawili haya yanatokana na ushahidi na hoja, elimu na yakini. Na muhtasari wa hayo ni kwamba uumbaji tu wa viumbe hawa kwa sifa hizi kunaonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na elimu yake, na uhai wake, na usimamia mambo yote wake, na uimara uliomo, na ustadi wake, na ubunifu mkubwa, na uzuri wake; yote yanaonyesha ukamilifu wa hekima ya Mwenyezi Mungu. Na uzuri wa kuumba kwake, na upana wa elimu yake, na aina mbalimbali za manufaa na masilahi yaliyo ndani yake, kama vile kulifanya jua kuwa mwangaza, na mwezi kuwa nuru ambavyo kwavyo yanapatikana manufaa ya dharura na mengineyo yanayotokea, hayo yanaashiria rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na utunzaji wake kwa waja wake, na upana wa wema wake na ihsani yake. Na mambo maalumu  yaliyomo yanaashiria mapenzi ya Mwenyezi Mungu na matashi yake yatekelezekanayo. Na hilo linaonyesha kwamba Yeye pekee ndiye Muabudiwa, Mpendwa, Msifiwa, Mwenye utukufu, heshima, na sifa kuu kuu, ambaye haifai kumtaka mwingine wala kumhofu isipokuwa Yeye, wala haifai kumfanyia dua safi isipokuwa Yeye. Si mwingineye miongoni mwa viumbe wanaolelewa, wanaomhitaji Mwenyezi Mungu katika mambo yao yote. Na katika aya hizi kuna kuhimiza na kutia moyo juu ya kutafakari viumbe vya Mwenyezi Mungu na kuwatazama kwa jicho la kuzingatia. Kwa maana kupitia hayo, utambuzi unakuwa mpana, na inazidi imani na akili, na maumbile yanaimarika. Na katika kupuuza hilo kuna kuyapuuza yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha, na kufunga kuongezeka kwa imani, na kudumaa kwa akili na maumbile."},{"id":1895,"sura":10,"from_aya":7,"to_aya":8,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"7. Hakika wale wasiotaraji kukutana nasi, na wakaridhia uhai wa dunia hii na wakatua nao, na wale walioghafilika na Ishara zetu. 8. Hao, makazi yao ni Motoni kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma. "},{"id":1896,"sura":10,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Yeye Mtukufu Anasema, \"Hakika wale wasiotaraji kukutana nasi;\u201d yaani, hawataki kukutana na Mwenyezi Mungu ambaye ndiye mkubwa zaidi ambaye watamanio wanatamani, na wa juu zaidi anayetumainiwa na wanaotumaini. Lakini wao walilipa mgongo, na hata huenda walilikadhibisha \u201cna wakaridhia uhai wa dunia hii\u201d badala ya Akhera, \"na wakatua nao.\u201d Yaani, waliyategemea, na wakayafanya kuwa ndio lengo la jambo lao na mwisho wa makusudio yao. Basi wakayatafuta kwa bidii, na wakashikana na starehe zake na matamanio yake, na wakazitafuta kwa njia yoyote ile ziwezavyo kupatikana, na kwa upande wowote ule zinapoonekania, wanaziendea haraka. Walielekeza matashi yao, na nia zao, na fikira zao, na matendo yao kwazo. Basi ni kana kwamba waliumbwa kubaki humo, na ni kana kwamba si nyumba ya kupitia tu ndani yake, ambayo wasafiri wanachukua humo masurufu kwa ajili ya nyumba ya milele ambayo humo ndiko wataenda wa mwanzo na wa mwisho, na ambayo kwa ajili ya neema zake na starehe walijiandaa wale waliofanikishwa \"na wale walioghafilika na Ishara zetu.\u201d Kwa hivyo hawafaidiki na ishara za kiqur-aani wala ishara za kiupeo na kinafsi. Na kuupa ushahidi mgongo kunalazimu kukipa mgongo na kughafilika na kile kinachoashiriwa, na kinachokusudiwa."},{"id":1897,"sura":10,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} \"Hao\" ambao hii ndiyo sifa yao \"makazi yao ni Motoni.\" Yaani, makao yao na maskani yao ambayo hawatatoka humo; \"kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma\u201d miongoni mwa ukafiri, na ushirikina, na aina mbalimbali za maasi."},{"id":1898,"sura":10,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"Na alipotaja adhabu yao, Akataja thawabu za watiifu, akasema:"},{"id":1899,"sura":10,"from_aya":9,"to_aya":10,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"9. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawaongoa kwa sababu ya Imani yao. Itapita mito kwa chini yao katika Mabustani yenye neema. 10. Wito wao humo utakuwa, \u201cSubhanaka Allahumma (Umetakasika Ee Mwenyezi Mungu!).\" Na maamkizi yao humo ni \"Salama.\" Na mwisho wa wito wao ni, \u201cAlhamdulillahi Rabbil 'aalamiin (Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote).\" "},{"id":1900,"sura":10,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} Yeye Mtukufu anasema: \"Hakika wale walioamini na wakatenda mema.\u201d Yaani walijumuisha kati ya imani na kutenda kwa mujibu wake na matakwa yake miongoni mwa matendo mema, yanayojumuisha matendo ya nyoyo na matendo ya viungo, kwa namna ya ikhlasi na kumfuata Mtume. \"Mola wao Mlezi atawaongoa kwa sababu ya Imani yao.\u201d Yaani, kwa sababu ya imani waliyo nayo, Mwenyezi Mungu anawalipa malipo makubwa kabisa ambayo ni uwongofu, na anawafundisha yenye kuwanufaisha, na anawaneemesha kwa matendo yanayotokana na uwongofu, na anawaongoa kuzizingatia ishara zake, na anawaongoa katika nyumba hii kwenye njia iliyonyooka, na kwenye njia iliyonyooka, na katika nyumba ya malipo kwenye njia ifikishayo kwenye mabustani yenye neema. Na ndiyo maana akasema: \"Itapita mito kwa chini yao\" daima \"katika Mabustani yenye neema.\u201d Mwenyezi Mungu alizifungamanisha na neema, kwa sababu zina neema kamili: neema ya moyo kwa furaha, uzuri, furaha, uchangamfu, kumuona Mwingi wa Rehema, kusikia maneno Yake, kufurahia kukubwa kwa sababu ya ridha yake na kuwa karibu naye na kukutana na wapendwa na ndugu, na kufurahia kukutana nao, na kusikia sauti za kuimba, na nyimbo za kupendeza, na mambo yatazamwayo yenye kufurahisha, na raha ya mwili kwa kila aina mbalimbali za vyakula, vinywaji, kujamiana, na mfano wa hayo ambayo nafsi haziyajui, wala hayajawahi kuingia akilini mwa mtu yeyote, wala kiwango ambacho wanaweza kuyaeleza waelezaji."},{"id":1901,"sura":10,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} \u201cWito wao humo utakuwa, \u201cSubhanaka Allahumma (Umetakasika Ee Mwenyezi Mungu!)\" Yaani, kumwabudu kwao humo Mwenyezi Mungu, mwanzo wake ni kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumuondolea mapungufu, na mwisho wake ni kumsifu Mwenyezi Mungu. Basi majukumu yaliwaondokea katika Nyumba ya Malipo, na kilichobakia tu juu yao ni raha kamili zaidi, ambayo ni raha zaidi kwao kuliko vyakula vitamu, tazama, nayo ni kumtaja Mwenyezi Mungu, ambako kwa huko mioyo hutulia na roho hufurahi, na ambako kwao kuko katika daraja la kupumua bila ya uzito wowote wala ugumu. \"Na\" ama maamkizi yao humu kati yao wanapokutana na kutembeleana ni \u201csalama.\u201d Yaani, usemi uliosalimika na upuuzi na dhambi, ambao unasifika kwamba ni \"salama.\" Na Ilisemwa katika tafsiri ya kauli yake, \u201cWito wao humo utakuwa, \u201cSubhanaka Allahumma (Umetakasika Ee Mwenyezi Mungu!)...\u201d mpaka mwisho wa Aya. Wakazi wa Peponi watakapohitaji chakula na vinywaji na mfano wake, wakasema, \u201cSubhanaka Allahumma (Umetakasika Ee Mwenyezi Mungu!)\" basi wanaletewa mara hiyo. Na wanapomaliza, wanasema, \u201cAlhamdulillahi Rabbil 'aalamiin (Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote).\""},{"id":1902,"sura":10,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"11. Na lau kama Mwenyezi Mungu angeliwafanyia watu haraka kuwaletea maovu kama wanavyojiharakishia kuletewa heri, basi bila ya shaka wangelikwisha timiziwa muda wao. Lakini tunawaacha wale wasiotaraji kukutana nasi wakihangaika katika upotovu wao."},{"id":1903,"sura":10,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} Na hili ni katika upole wake na wema wake kwa waja wake, kwamba ikiwa angewaharakishia maovu wanapofanya sababu zake, na akawaharakishia adhabu juu yake kama anavyowaharakishia heri wanapofanya sababu zake, \u201cbasi bila ya shaka wangelikwisha timiziwa muda wao.\u201d Yaani, adhabu ingewafutilia mbali. Lakini Yeye Mtukufu anawapa muhula wala hawapuuzi, na anasamehe nyingi katika haki zake. Basi   lau kuwa Mwenyezi Mungu angewaadhibu watu kwa mujibu wa dhuluma zao, basi asingelimwacha mnyama yeyote juu ya mgongo wake. Na inaingia katika hili kwamba mja anapowakasirikia watoto wake, au mkwe, mali yake, basi huenda akawaapiza kuapiza ambako lau kutakubaliwa wangeangamia na hilo lingelimdhuru kumdhuru kukubwa sana, lakini Yeye Mtukufu ni Mpole, Mwenye hekima. Na kauli yake: \"Lakini tunawaacha wale wasiotaraji kukutana nasi;\u201d yaani, wasioamini Akhera. Na kwa sababu ya hilo, hawajitayarishi kwa ajili yake wala hawafanyi yenye kuwaepusha na adhabu ya Mwenyezi Mungu, \"katika upotovu wao.\u201d Yaani, batili yao ambayo walivuka kwayo haki na mipaka \u201cwakihangaika;\u201d yaani, wanasitasita na kuchanganyikiwa bila ya kuongoka kwenye njia ya sawa, wala hawawezeshwi kufikia hoja iliyo imara. Na hiyo ni adhabu kwao kwa dhuluma yao na kukufuru kwao ishara za Mwenyezi Mungu."},{"id":1904,"sura":10,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"12. Na mtu akiguswa na shida, hutuomba naye kaegesha ubavu, au kakaa, au kasimama. Lakini tunapomwondoshea shida yake hiyo, huendelea kama kwamba hakuwahi kutuomba tumwondoshee shida iliyomgusa. Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapitilizao viwango yale waliyokuwa wakiyatenda."},{"id":1905,"sura":10,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Na huku ni kujulisha kuhusu umbile la mwanadamu namna alivyo, kwamba yanapomgusa madhara kama vile maradhi au msiba, ataomba dua kwa bidii, na kumwomba mwenyezi Mungu katika hali zake zote huku amesimama, na kuketi, na kulala chini, na atasisitiza katika dua yake hiyo ili Mwenyezi Mungu amwondolee madhara yake. \"Lakini tunapomwondoshea shida yake hiyo, huendelea kama kwamba hakuwahi kutuomba tumwondoshee shida iliyomgusa.\u201d Yaani, anaendelea kughafilika huku amempa mgongo Mola wake Mlezi, kana kwamba hakujiwa na madhara yoyote, na Mwenyezi Mungu akamuondolea. Basi Je, ni dhuluma gani iliyo kubwa zaidi kuliko dhuluma hii? Anamwomba Mwenyezi Mungu atimize kusudio lake. Basi anapompa hilo kusudio lake, haitazami haki ya Mola wake Mlezi, kana kwamba hakuna haki yoyote ya Mwenyezi Mungu juu yake? Na huku ni kupambiwa  na Shetani. Alimpambia yale ambayo ni ya kuchukiza na yaliyo mabaya katika akili na maumbile. \"Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapitilizao viwango yale waliyokuwa wakiyatenda.\u201d"},{"id":1906,"sura":10,"from_aya":13,"to_aya":14,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"13. Na hakika  tuliviangamiza vizazi vya kabla yenu walipo dhulumu, na waliwajia Mitume wao kwa Ishara zilizo wazi, lakini hawakuwa wenye kuamini. Hivyo ndivyo tunavyowalipa kaumu wahalifu. 14. Kisha tukawafanya nyinyi ndio wenye kushika pahala pao katika ardhi baada yao ili tuone jinsi mtakavyotenda. "},{"id":1907,"sura":10,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Yeye Mtukufu anajulisha kuwa aliziangamiza umma zilizotangulia kwa dhuluma yao na ukafiri wao baada ya kujiwa na ishara zilizo wazi juu ya mikono ya Mitume wao zikibainisha haki, lakini hawakuzifuata, wala hawakuamini. Kwa hivyo, akawafikishia adhabu yake ambayo haiwezi kurudishwa dhidi ya kila mhalifu anayeyafanyia ujasiri maharamisho ya Mwenyezi Mungu. Na hii ndiyo desturi yake katika umma zote."},{"id":1908,"sura":10,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} \u201cKisha tukawafanya nyinyi\u201d enyi mnaoongeleshwa \"ndio wenye kushika pahala pao katika ardhi baada yao ili tuone jinsi mtakavyotenda.\u201d Kwa hivyo, ikiwa nyinyi mtazingatia na mkawaidhika kwa wale waliokuwa kabla yenu, na mkafuata Ishara za Mwenyezi Mungu, na mkwasadiki Mitume wake, mtaokoka katika dunia na Akhera. Na mkitenda kama matendo ya madhalimu wa kabla yenu, atawafikishia yale aliyowafikishia wao. Na mwenye kuonya,  basi hakika atakuwa ashapata udhuru."},{"id":1909,"sura":10,"from_aya":15,"to_aya":17,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"15. Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji kukutana na Sisi husema, \u201cLeta Qur-aani isiyokuwa hii, au ibadilishe.\u201d Sema, \u201cHaiwi kwangu niibadilishe nitakavyo mimi mwenyewe. Mimi sifuati isipokuwa yale ninayofunuliwa kwa Wahyi. Hakika mimi ninahofu, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu. 16. Sema, \u201cMwenyezi Mungu angelitaka, nisingeliwasomea, wala nisingelikuwa mwenye kukijua zaidi yenu. Kwani nalikwisha kaa miongoni mwenu umri mzima kabla yake! Kwani, hamtii akilini?\u201d 17. Basi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu na akazikadhibisha Ishara zake? Hakika hawafaulu wahalifu. "},{"id":1910,"sura":10,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15} Yeye Mtukufu anataja ukaidi wa wale wanaomkadhibisha Mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - na kwamba wanaposomewa Aya za kiqur-aani zinazobainisha haki, wanazipa mgongo, na wanatafuta njia ya ukaidi, kisha wanasema kwa ujasiri na udhalimu, \u201cLeta Qur-ani isiyokuwa hii, au ibadilishe,\u201d basi Mwenyezi Mungu awatie mbali na rehema zake. Ni ujasiri ulioje huu wao dhidi ya Mwenyezi Mungu, na ni dhulumu kubwa iliyoje hii yao na kuzikataa Ishara zake! Ikiwa Mtume mtukufu huyu aliamrishwa na Mwenyezi Mungu awaambie, \u201cSema, \u201cHaiwi kwangu.\u201d Yaani, haifai wala haiendani nami, \u201cniibadilishe nitakavyo mimi mwenyewe\u201d kwani mimi ni mtume tu, na sina chochote katika jambo hilo. \u201cMimi sifuati isipokuwa yale ninayofunuliwa kwa Wahyi.\u201d Yaani, sina lolote isipokuwa hilo. Kwa maana, mimi ni mja niamrishwaye. \u201cHakika mimi ninahofu, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu.\u201d Hii ndiyo kauli ya kiumbe bora zaidi na adabu yake kwa maamrisho ya Mola wake Mlezi na ufunuo wake. Basi vipi wapumbavu hawa waliopotea, ambao walikusanya kati ya ujinga, upotofu, dhuluma, upinzani, ukaidi, na kumfanya Mola Mlezi walimwengu wote asiyeweza? Kwani hawahofu adhabu ya siku kuu? Kwa hivyo, Wakidai kuwa makusudio yao ni kwamba haki iwabainikie kwa ishara ambazo waliziomba, basi wao ni waongo katika hilo. Kwa maana, Mwenyezi Mungu alikwisha zibainisha Ishara wanazoamini mfano wake wanadamu, naye ndiye anayezileta jinsi atakavyozifuata hekima yake ya kiungu, na rehema zake kwa waja wake."},{"id":1911,"sura":10,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} { Sema, \u201cMwenyezi Mungu angelitaka, nisingeliwasomea, wala nisingelikuwa mwenye kukijua zaidi yenu. Kwani nalikwisha kaa miongoni mwenu umri mzima\u201d mrefu \u201ckabla yake!\u201d Yaani, kabla ya kuisoma na kabla ya nyinyi na mimi kuijua, wala haikunijia kwenye akili wala haikuingia katika fikira zangu. \"Kwani, hamtii akilini?\u201d Kwamba kuwa sikuitunga katika muda wa maisha yangu, wala hakikutokea kwangu chochote kinachoonyesha hivyo; basi nitaitunga baada ya hapo ilhali nimekaa miongoni mwenu muda mrefu, huku mnajua uhakika wa hali yangu kwamba mimi sijui kusoma na kuandika, wala sisomi, wala sijifunzi kutoka kwa yeyote. Kisha nikawajia na kitabu kikuu ambacho kiliwashinda wenye ufasaha na kikawapiku wanachuoni. Basi je, inawezekana baada ya hayo kwamba kiwe nimekitunga tu mimi mwenyewe? Au huu ni ushahidi wa uhakika kwamba ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima, Msifiwa? Na ikiwa mtatumia akili na fikira zenu, na akili zenu, na mkaitafakari hali yangu na hali ya kitabu hiki, basi mngekuwa na uhakika usiokubali shaka yoyote kwamba ni cha ukweli, na kwamba ndiyo haki ambayo baada yake hakuna isipokuwa upotofu. Lakini ikiwa mtakataa isipokuwa kukadhibisha na ukaidi, basi nyinyi hakuna shaka ni madhalimu."},{"id":1912,"sura":10,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} Na \u201cBasi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu na akazikadhibisha Ishara zake?\u201d Na kama ningekuwa ni wa kukitunga, basi ningelikuwa dhalimu zaidi ya watu wote, na nikakosa kufaulu, na hali yangu isingefichika kwenu. Lakini niliwajia na Ishara za Mwenyezi Mungu, nanyi mkazikadhibisha, basi dhuluma ikathibiti kwenu hasa, na hakuna budi kwamba mambo yenu yatapotelea mbali, wala hamtapata kufaulu maadamu mtaendelea kuwa hivyo. Na kauli yake: \"Wale wasiotaraji kukutana na Sisi husema...\u201d hadi mwisho wa Aya iliashiria kuwa kilichowapeleka kwenye ukaidi huu ambao ulitoka kwao ni kutokuamini kwao kukutana na Mwenyezi Mungu na kutokuwa kwao na matumaini kwake, na kwamba mwenye kuamini kukutana na Mwenyezi Mungu, basi ni lazima afuate kitabu hiki na kukiamini, kwa sababu ana makusudio mazuri."},{"id":1913,"sura":10,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"18. Nao, wanaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wale wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema, \u201cHawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu!\u201d Sema, \u201cJe, mnamwambia Mwenyezi Mungu yale asiyoyajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Ametakasika na ametukuka na hao wanaomshirikisha naye.\u201d"},{"id":1914,"sura":10,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} Yeye Mtukufu anasema: \"Na wanaabudu;\" Yaani, washirikina wanaomkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu \u2013 Rehema na Amani zimshukie \u2013 \"badala ya Mwenyezi Mungu wale wasiowadhuru wala kuwanufaisha.\u201c Yaani, hawawamilikii uzito wa chembe ya manufaa, wala hawawazuilii chochote. \"Na wanasema\u201d maneno yasiyo na ushahidi: \"Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu\u201d Yaani, wanawaabudu ili kuwakurubishe kwa Mwenyezi Mungu na wawafanyie uombezi kwake. Na hii ni kauli kutoka tu kwao wenyewe. Na ni kauli waliyoizua wao, na ndiyo maana Akasema, akibatilisha kauli yao hii: \"Sema, \u201cJe, mnamwambia Mwenyezi Mungu yale asiyoyajua ya katika mbingu wala katika ardhi?\u201d Yaani, Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mwenye kujua yote ambaye amekizunguka kwa elimu kila kitu kilicho katika mbingu na ardhi. na tayari alikwisha wajulisha kwamba hana mshirika yeyote wala hana mungu yeyote pamoja naye. Basi enyi kundi la washirikina mnadai kuwa anao washirika ndani yake. Kwani mnamwambia jambo ambalo limefichikana kwake lakini nyinyi mkalijua? Je, nyinyi ndio mnaojua au Mwenyezi Mungu? Basi Je, kuna kauli batili zaidi kuliko kauli hii inayojumuisha kwamba hawa wapotofu, wajinga, na wapumbavu ni wenye kujua zaidi kuliko Mola Mlezi wa walimwengu wote? Basi Mwenye akili na atosheke na kufikiria tu kauli hii; kwani atakuwa na uhakika juu ya ubovu wake na ubatili wake. \"Ametakasika na ametukuka na hao wanaomshirikisha naye.\u201d Yaani, ametakasika na ametukuka kuwa na mshirika au mwenza. Bali Yeye ni Mwenyezi Mungu, Mmoja, wa kipekee, Mkusudiwa ambaye hakuna Mungu katika mbingu na ardhi isipokuwa Yeye. Na kila muabudiwa katika ulimwengu wa juu na wa chini asiyekuwa Yeye ni batili, kiakili, na kisheria, na kimaumbile. \"Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa haki, na kwamba wale wanaowaomba badala yake, ni baatili, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Aliye Juu na ndiye Mkubwa.\u201c"},{"id":1915,"sura":10,"from_aya":19,"to_aya":20,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"19. Na watu hawakuwa isipokuwa Umma mmoja tu, kisha wakahitalifiana. Na lau kuwa si neno lililokwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, hapana shaka hukumu ingelikwisha katwa baina yao katika yale wanayohitalifiana. 20. Na wanasema, \u201cKwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?\u201d Sema, \u201cHakika mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu. Basi nyinyi ngojeni, na mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.\u201d "},{"id":1916,"sura":10,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} Yaani, \u201cNa watu hawakuwa isipokuwa Umma mmoja tu\u201d yaani, walikuwa wameafikiana juu ya Dini sahihi, lakini wakahitalifiana. \"Basi Mwenyezi Mungu akawatuma Manabii wabashiri na waonyaji. Na akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale waliyohitalifiana.\u201cNa lau kuwa si neno lililokwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi\u201d kwa kuwapa muhula waasi na kutowaharakishia adhabu kwa madhambi yao, \u201chapana shaka hukumu ingelikwisha katwa baina yao\u201d kwa kuwaokoa Waumini na kuwaangamiza makafiri wanaokadhibisha. Basi hili likawa ndilo la kutofautisha kati yao \u201ckatika yale wanayohitalifiana;\u201d lakini alitaka kuwapa mtihani na kuwajaribu wao kwa wao, ili abainike mkweli na mwongo."},{"id":1917,"sura":10,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} \"Na wanasema;\" yaani, hao wanaokadhibisha, wakaidi. \"Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?\u201d Wakimaanisha ishara wanazopendekeza wao ambazo wanazitaka wao. Kama vile kauli yao: \"Mbona hakuteremshiwa Malaika akawa mwonyaji pamoja naye...?\u201d Hadi mwisho wa aya hizi. Na kama kauli yake, \u201cNa walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchemi katika ardhi hii...\u201d hadi mwisho wa aya hizi. \"Basi sema\" uwaambie Wakikuomba Ishara: \"Hakika mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu.\u201d Yaani, Yeye ndiye amezizunguka kwa elimu hali za waja Wake, kwa hivyo anawaendesha kulingana na inavyohitaji elimu Yake kuhusiana nao, na hekima Yake ya ajabu. Na hakuna yeyote mwenye uendeshaji katika hukumu, wala ushahidi, wala lengo, wala sababu. \"Basi nyinyi ngojeni, na mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.\u201d Yaani, kila mmoja anamgonjelea mwenzake yale anayostahili. Basi ngojeni muone ni nani atakuwa na mwisho mwema."},{"id":1918,"sura":10,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"21. Na tunapowaonjesha watu rehema baada ya shida iliyowagusa, tazama, wanafanya njama katika Ishara zetu. Sema, \u201cMwenyezi Mungu ni Mwepesi zaidi wa kupanga njama. Hakika wajumbe wetu wanayaandika hayo mnayoyapangia njama.\u201d"},{"id":1919,"sura":10,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} Yeye Mtukufu Anasema: \"Na tunapowaonjesha watu rehema baada ya shida iliyowagusa\u201d kama vile afya baada ya maradhi, na utajiri baada ya umasikini, na amani baada ya hofu, wanasahau yale yaliyowasibu miongoni mwa madhara, na hawamshukuru Mwenyezi Mungu juu ya maisha hayo ya raha na rehema. Bali wanaendelea na upotofu wao na njama zao, na kwa sababu ya hili ndiyo akasema: \"Tazama, wanafanya njama katika Ishara zetu.\u201d Yaani, wanafanya bidii katika batili ili waibatilishe haki kwayo. \"Sema, \u201cMwenyezi Mungu ni Mwepesi zaidi wa kupanga njama\u201d kwa maana njama haiwafikii isipokuwa wenyewe. Basi makusudio yao yanawarudia wao wenyewe, wala hawakuepuka lawama, bali Malaika wanawaandikia yake wanayoyafanya, na Mwenyezi Mungu atawahesabu kwayo, kisha Mwenyezi Mungu atawalipa kwayo malipo kamili zaidi."},{"id":1920,"sura":10,"from_aya":22,"to_aya":23,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"22. Yeye ndiye anayewaendesha katika nchi kavu na baharini. Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri na wakaufurahia, upepo mkali ukayajia, na yakawajia mawimbi kutoka kila mahali, na wakaona kwamba wameshazungukwa, basi hapo wanamwomba Mwenyezi Mungu kwa kumpwekeshea yeye tu dini, \u201cUkituokoa na haya, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.\u201d 23. Lakini anapowaokoa, tazama, wanafanya jeuri tena katika ardhi bila ya haki. Enyi watu! Hakika jeuri zenu zitawadhuru nyinyi wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda. "},{"id":1921,"sura":10,"from_aya":22,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22-23} Yeye Mtukufu alipotaja kanuni ya jumla kuhusu hali za watu wakati wanapopatwa na rehema baada ya shida, na urahisi baada ya ugumu, akataja hali inayounga mkono hilo. Nayo ni hali yao katika bahari wakati wa michafuko yake kuhofu matokeo yake. Akasema: \"Yeye ndiye anayewaendesha katika nchi kavu na baharini\u201d kwa yale aliyowarahisishia miongoni mwa njia zinazoekwa kwa ajili yenu na akawaongoa kuzifikia. \"Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri\u201d zikiafikiana na wapendavyo, bila ya masumbuko wala ugumu, \"na wakaufurahia\" na wakawa na utulivu nao. Na huku wakiwa hivyo, ghafla ukawajia \u201cupepo mkali\u201d katika kuvuma kwake \u201cna yakawajia mawimbi kutoka kila mahali, na wakaona kwamba wameshazungukwa.\u201d Yaani, wakajua kuwa ni maangamivu, na wakati huo kukakatika kufungamana kwao na viumbe, na wakajua kuwa hakuna yeyote wa kuwaokoa na shida hii isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake. Wakamuomba \"kwa kumpwekeshea yeye tu dini\u201d na wakajiwekea ahadi kwa ufaradhinamna ya ulazima, na wakasema: \u201cUkituokoa na haya, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru. Na alipowaokoa, tazama, walikuwa wakifanya jeuri tena katika ardhi bila ya haki.\u201d Yaani, walisahau shida hiyo, dua hiyo, na yale waliyojiwekea kwa namna ya ulazima juu ya nafsi zao, kwa hivyo wakamshirikisha Mwenyezi Mungu wale waliokiri kuwa hawawezi kuwaepusha kutokana na shida wala kuwakinga kutokana na matatizo. Basi kwa nini hawakumpwekeshea Mwenyezi Mungu ibada katika wakati wa raha kama vile walivyompwekesha katika nyakati za shida? Lakini jeuri hii yanarejea madhara yake juu yao, na ndiyo maana akasema: \"Enyi watu! Hakika jeuri zenu zitawadhuru nyinyi wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu.\u201d Yaani, matarajio yenu ya mwisho kwa jeuri yenu hiyo na kuwa kwenu mbali na kumpwekesha Mwenyezi Mungu ni kwamba mpate kitu katika mabaki ya dunia na heshima yake chache, ambayo yataisha haraka, na yote yatapita, kisha mtaondoka myaache hata msipotaka. \"Kisha marejeo yenu ni kwetu\u201d katika Siku ya Qiyama, \"na hapo tutawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.\u201d Na katika hili kuna onyo kubwa kabisa kwao juu ya kuendelea na matendo yao hayo."},{"id":1922,"sura":10,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"24. Hakika mfano wa uhai wa dunia hii ni kama maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha mimea ya ardhi ikachanganyika nayo miongoni mwa vile wanayvovila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipokamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani kwamba wameshaiweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, kwa hivyo tukaifanya kama iliyofyekwa, kama kwamba haikuwapo jana. Hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara zetu kwa kaumu wanaotafakari."},{"id":1923,"sura":10,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} Na mfano huu ni katika mifano mizuri zaidi, ambao unaingiana sawa sawa na hali ya dunia hii; kwa maana, raha zake, na matamanio yake, na heshima yake, na mfano wa hayo yanampendeza mwenyewe yanapompendeza kwa muda mfupi, na yanapokamilika na yakatimia, yanafifia na kutoweka kwa mwenyewe au mwenyewe anayaacha. Kwa hivyo, akawa mikono mitupu bila ya hayo, huku amejaa moyo na wasiwasi mkubwa juu yake, na huzuni yake na majuto yake, basi hayo ni \"kama maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha mimea ya ardhi.\u201d Yaani, ikaota kutoka humo kila aina na jozi nzuri, \"miongoni mwa vile wanayvovila watu\u201d kama vile nafaka na matunda, \"na\" katika vile wanavyovila \"wanyama\" kama vile aina mbalimbali za nyasi na malisho ya sampuli tofauti tofauti. \"Mpaka ardhi ilipokamilika uzuri wake, na ikapambika;\u201d yaani, ikapambwa katika mwonekano wake na ikavalika kwa mapambo yake, kwa hivyo ikawa nzuri kwa watazamaji, na matembezi ya burudani kwa wafurahiao, na ishara kwa wenye kuona, kisha ukaanza kuiona katika mtazamo wa ajabu kama vile kijani, njano, nyeupe na mingineyo. \u201cNa wenyewe wakadhani kwamba wameshaiweza;\u201d yaani, wakawa na matumaini kwamba hayo yataendelea na kudumu, kwa sababu matashi yao yalisimamia hapo, na yale wanayoyatafuta yakaishia humo. Na walipokuwa katika hali hiyo, amri ya Mwenyezi Mungu ikaijia \u201cusiku au mchana, kwa hivyo tukaifanya kama iliyofyekwa, kama kwamba haikuwapo jana;\u201d basi hii ndiyo hali ya dunia hii mia kwa mia. \"Hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara zetu;\u201d yaani, tunazibainisha na kuziweka wazi kwa kuleta maana karibu na akili na kuzipigia mifano, \"kwa kaumu wanaotafakari.\u201d Yaani, wanatumia fikira zao katika yale yenye kuwanufaisha. Na ama aliyeghafilika, aliyepeana mgongo, basi huyu hazimnufaishi ishara, na kubainisha hakumuondolei shaka yake."},{"id":1924,"sura":10,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"Na Mwenyezi Mungu alipotaja hali ya dunia hii, na matokeo ya starehe zake, akatamanisha juu ya nyumba yenye kubakia, akasema:"},{"id":1925,"sura":10,"from_aya":25,"to_aya":26,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"25. Na Mwenyezi Mungu anaita kwenye Nyumba ya amani, na anamwongoa amtakaye kwenye Njia iliyonyooka. 26. Kwa wafanyao uzuri ni uzuri na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila. Hao ndio wenza  wa Pepo. Wao, humo watadumu. "},{"id":1926,"sura":10,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} Yeye Mtukufu aliwajumuisha waja wake katika kuwalingania kwenye nyumba ya amani, katika kuwahimiza juu yake na kuwatia moyo kufanya hivyo, na akafanya kuongoka kuwa maalumu kwa yule aliyetaka kumwokoa na kumchagua. Basi hii ni fadhila yake na wema wake, na Mwenyezi Mungu  humchagua kumpa rehema zake amtakaye. Na huo ndio uadilifu wake na hekima yake, na hakuna mwenye hoja yoyote dhidi yake baada ya kubainisha na kuwatuma Mitume. Na Mwenyezi Mungu aliita Pepo kuwa ni nyumba ya amani kwa sababu ya usalama wake kutokana na balaa zote na mapungufu. Na hilo ni kwa sababu ya ukamilifu wa starehe zake, na ukamilifu wake, na kubakia kwake, na uzuri wake kwa kila njia."},{"id":1927,"sura":10,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} Na alipolingania kwenye nyumba ya amani, ni kana kwamba nafsi zilipata shauku juu matendo yenye kusababisha hilo na yenye kuwafikisha huko, kwa hivyo akajulisha juu yake kwa kauli yake: \"Kwa wafanyao uzuri ni uzuri na zaidi.\u201d Yaani, kwa wale waliofanya mazuri katika kumwabudu Muumba, kwa kumuabudu kwa namna ya kumchunga na kumsafishia ibada, na kufanya yale waliyoweza kufanya kwayo, na wakawafanyia uzuri waja wa Mwenyezi Mungu kwa yale wanayoweza miongoni mwa uzuri wa kikauli na wa kimatendo kama vile kutoa mali kwa uzuri na kufanya uzuri wa kimwili, na kuamrisha mema na kukataza maovu, kuwafundisha wasiojua, na kuwanasihi wapeanano migongo, na mambo mengineyo miongoni mwa njia mbalimbali za wema na ihsani. Basi hawa waliofanya uzuri wana uzuri zaidi, ambayo ni Pepo kamili katika uzuri wake, na ziada, ambayo ni kuutazama uso wa Mwenyezi Mungu, Mtukufu, na kusikia maneno Yake, na kupata ridha yake, na kufurahia kuwa karibu naye. Na kwa hivyo wakapata kitu cha juu zaidi ambacho wanakitamani wenye kutamani, na wanakiomba wenye kuomba. Kisha akataja kuondokewa kwao na kile wanachokihofu, akasema: \"Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila.\u201d Yaani, hawatapatwa na machukizo kwa namna yoyote ile. Kwa sababu machukizo yanapompata mwanadamu, yanaonekana kwenye uso wake na anabadilika na anahuzunika. Na ama hawa, basi ni kama Mwenyezi Mungu alivyosema kuwahusu, \u201cUtatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema.\u201d Hao ndio wenza wa Pepo watakaokaa humo milele. Hawataenda popote pengine, wala hawataondoka, wala hawatabadilika."},{"id":1928,"sura":10,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"27. Na wale waliochuma mabaya, malipo ya baya ni kwa mfano wake, na watafunikwa na madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao ni kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio wenza wa Moto. Wao, humo watadumu."},{"id":1929,"sura":10,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} Alipowataja wenza wa Pepo, akawataja wenza wa Moto, kwa hivyo akataja kwamba bidhaa zao ambazo walizichuma katika dunia hii ndiyo matendo mabaya yenye kumkasirisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa aina mbalimbali za ukafiri, na ukadhibishaji, na aina mbalimbali za maasia, kwa hivyo malipo yao ni mabaya mfano wake. Yaani, malipo yatakayowawiya mabaya kulingana na yale waliyoyafanya miongoni mwa mabaya kulingana na hali zao tofauti tofauti. \"Na watafunikwa na madhila\u201d katika mioyo yao na hofu ya adhabu ya Mwenyezi Mungu ambayo hakuna yeyote awezaye kuwaondolea wala hakuna mlinzi yeyote awezaye kuwalinda kutokana nayo. Na madhila hayo yatafika katika sura zao za nje, mpaka yawe meusi katika nyuso zao \"kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio wenza wa Moto. Wao, humo watadumu;\u201d basi ni tofauti gani iliyopo kati ya makundi mawili haya? Na ni umbali ulioje kati yao? \"Zipo nyuso siku hiyo zitakazong'ara. Zikimwangalia Mola wao Mlezi. Na zipo nyuso siku hiyo zitakazokunjana. Zikijua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.\" \u201cSiku hiyo ziko nyuso zitakazonawiri. Zitacheka, zitafurahia. Na nyuso zingine siku hiyo zitakuwa na mavumbi. Giza totoro litazifunika. Hao ndio makafiri, waovu.\u201d"},{"id":1930,"sura":10,"from_aya":28,"to_aya":30,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"28. Na siku tutakapowakusanya wote, kisha tutawaambia wale walioshirikisha, \"Simameni pahali penu nyinyi na washirika wenu.\" Kisha tutatenganisha baina yao. Na hao washirika wao watasema, \"Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi.\" 29. Basi Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi baina yetu na nyinyi. Hakika sisi tulikuwa hatuna habari na ibada yenu. 30. Huko kila nafsi itayajua iliyoyatanguliza. Na watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa haki, na yote ya uongo waliyokuwa wakiyazua yatawapotea. "},{"id":1931,"sura":10,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Yeye Mtukufu anasema: \"Na siku tutakapowakusanya wote;\u201d yaani, tutakapowakusanya viumbe vyote kwa ajili ya miadi ya siku maalumu, na tutawahudhurisha washirikina na wale waliokuwa wakiabudu badala ya Mwenyezi Mungu. \u201cKisha tutawaambia wale walioshirikisha, \"Simameni pahali penu nyinyi na washirika wenu.\" Yaani, bakieni pahali penu ili ipate kufanyika hukumu na kupambanua baina yenu na wao. \u201cKisha tutatenganisha baina yao,\u201d yaani, tutawatenganisha kimwili na kimoyo, na kuwe na uadui mkubwa baina yao baada ya kwamba waliwapa katika dunia mapenzi ya dhati na juu zaidi, lakini mapenzi hayo na ulinzi yakageuka kuwa chuki na uadui. Na washirika wao wakajiweka mbali nao na wakasema, \"Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi.\" Kwa maana, sisi tunamtakasa Mwenyezi Mungu kuwa na mshirika yeyote au mwenza."},{"id":1932,"sura":10,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} \"Basi Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi baina yetu na nyinyi. Hakika sisi tulikuwa hatuna habari na ibada yenu.\u201d Hatukuwaamrisha kufanya hivyo, wala hatukuwaita kwa sababu yake, bali nyinyi mlimwabudu yule aliyewaita kwa ajili ya hilo.  Naye ni Shetani, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \u201cJe, sikuwaagiza enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani? Kwani yeye hakika ni adui dhahiri kwenu.\u201d Na akasema, \u201cNa siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia Malaika: Je, hawa walikuwa wakiwaabudu nyinyi? Watasema: Umetakasika. Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao. Bali wao walikuwa wakiwaabudu majini, wengi wao wakiwaamini hao.\u201d Kwa hivyo, Malaika watukufu, Manabii, mawalii (marafiki wa Mwenyezi Mungu), na mfano wao watajitenga na wale waliowaabudu Siku ya Qiyama, na watakataa madai ya kuwaita ili wawaabudu. Nao ni wakweli na wema katika hayo."},{"id":1933,"sura":10,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Basi hapo, washirikina watajuta majuto yasiyoweza kuelezeka, na watajua kiwango cha yale waliyotanguliza katika matendo, na yale waliyofanya hapo zamani miongoni mwa sifa mbaya, na itawabainikia siku hiyo kwamba walikuwa waongo, na kwamba walikuwa wakimsingizia Mwenyezi Mungu. Ibaada zao zitapotea, na waabudiwa wao watatoweka, na zitakakika sababu zao na njia zao, na ndiyo maana Akasema, \u201cHuko;\u201d yaani, katika Siku hiyo \u201ckila nafsi itayajua iliyoyatanguliza.\u201d Yaani, zitayachunguza matendo yake na yale ziliyoyachuma, na zitafuatwa na malipo, na zitalipwa kulingana nayo, ikiwa ni ya heri, basi ni heri. Na ikiwa ni maovu, basi ni kwa uovu. \u201cNa yote ya uongo waliyokuwa wakiyazua yatawapotea.\u201d Yale waliyokuwa wakisema kwamba wanayofanya ya ushirikina ndiyo ya sahihi , na kwamba wale wanaoabudu badala ya Mwenyezi Mungu watawanufaisha na kuwaondolea adhabu."},{"id":1934,"sura":10,"from_aya":31,"to_aya":33,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"31. Sema, \"Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhi? Au ni nani anayemiliki kusikia na kuona? Na ni nani atoaye kilicho hai kutoka kwa maiti, na atoaye maiti kutoka kwa kilicho hai? Na ni nani anayeyaendesha mambo yote?\" Basi watasema, \"Mwenyezi Mungu.\" Basi sema, \"Je, hamchi?\" 32. Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi wa haki. Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu? Basi ni vipi mnageuzwa? 33. Ndivyo hivyo kauli ya Mola wako Mlezi ilivyowathibitikia wale waliovuka mipaka ya kwamba hawataamini. "},{"id":1935,"sura":10,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} Yaani, waambie hawa ambao walimshirikisha Mwenyezi Mungu na yale ambayo hakuyateremshia uthibitisho wowote, ukitoa hoja dhidi yao kwa yale waliyoyakiri ya kupwekeka kwa Mwenyezi Mungu katika umola wake, juu ya yale waliyoyakataa ya kupwekeka kwa Mwenyezi Mungu katika uungu. \u201cSema, \"Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhi?\u201d Kwa kuteremsha riziki kutoka mbinguni, na kutoa aina zake katika ardhi, na kurahisisha sababu zake humo. \"Au ni nani anayemiliki kusikia na kuona?\u201d Yaani, ni nani aliyeviumba na ndiye mmiliki wake? Na alivitaja hivi hasa kwa sababu ni mbinu ya kukumbusha kilicho muhimu zaidi kwa kutaja kilicho chini yake, na kwa sababu ya ukamilifu wa cheo chake na manufaa yake. \"Na ni nani atoaye kilicho hai kutoka kwa maiti\" kama vile kutoa aina mbalimbali za miti na mimea kutoka kwa mbegu na kokwa, na kumtoa Muumini kutoka kwa kafiri, na ndege kutoka kwenye yai... na mfano wa hayo? Na atoaye maiti kutoka kwa kilicho hai;\u201d kinyume cha haya yaliyotajwa? \u201cNa ni nani anayeyaendesha mambo yote\" katika ulimwengu wa juu na wa chini? Na hili linajumuisha kila aina ya uendeshaji mambo wa kiungu. Kwa hivyo ukiwauliza kuhusu hayo, \"Basi watasema, \"Mwenyezi Mungu.\" Kwa sababu, wanayakiri hayo yote, na kwamba Mwenyezi Mungu hana mshirika yeyote katika kitu chochote miongoni mwa hayo yaliyotajwa. \"Basi sema\" uwaambie ukiwalazimisha kuikubali hoja hii, \"Je, hammchi\" Mwenyezi Mungu, na  mkamuabudu Yeye tu, bila mshirika yeyote, na muwaache wale mnaowaabudu badala yake miongoni mwa wenza na masanamu?"},{"id":1936,"sura":10,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} \u201cBasi huyo\u201d ambaye alijieleza mwenyewe kwa yale aliyojieleza, \u201cndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi.\u201d Yaani, afanyiwaye uungu, muabudiwa, msifiwa, mlezi wa viumbe vyote kwa neema zake, naye ndiye wa \u201chaki. Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?\u201d. Kwa maana, Yeye Mtukufu ndiye wa pekee tu katika kuumba, na kuendesha mambo ya vitu vyote, ambaye hakuna neema yoyote waliyo nayo waja isipokuwa ni kutoka kwake, wala haji na mazuri isipokuwa Yeye, wala hayazuii mabaya isipokuwa Yeye. Yeye ni Mwenye Majina mazuri zaidi na Sifa, kamilifu, kuu, tukufu na za heshima. \"Basi ni vipi mnageuzwa\u201d kutoka katika \u0301ibaada ya yule ambaye hizi ndizo sifa zake hadi kumuabudu yule asiyekuwa na chochote katika kuwepo kwake isipokuwa kutokuwepo, wala hajimilikii manufaa yoyote, wala madhara, wala mauti, wala uhai, wala ufufuo? Basi hana katika umiliki uzito wa chembe, wala hana ushirika kwa namna yoyote ile, wala hafanyi uombezi kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa idhini yake."},{"id":1937,"sura":10,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} Basi na aangamie mwenye kumshirikisha, na ole wake mwenye kumkufuru. Kwani, hakika wamepoteza akili zao baada ya kupoteza dini zao. Bali walipoteza dunia yao na akhera yao, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema kuwahusu, \u201cHivyo ndivyo kauli ya Mola wako Mlezi ilivyowathibitikia wale waliovuka mipaka ya kwamba hawataamini;\u201d baada ya Mwenyezi Mungu kuwaonyesha Ishara zake zilizo wazi, na hoja zake zinazong\u2019aa, ambazo zina mazingatio ndani yake kwa wenye akili, na mawaidha kwa wachamungu, na uwongofu kwa walimwengu."},{"id":1938,"sura":10,"from_aya":34,"to_aya":36,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"34. Sema: Je, yupo katika washirika wenu mwenye kuanzisha kuumba viumbe, kisha akavirejesha? Sema: Mwenyezi Mungu anaazisha kuumba viumbe, kisha anavirejesha. Basi ni vipi mnadanganywa? 35. Sema, \"Je, yupo yeyote katika washirika wenu mwenye kuongoa kwenye haki?\" Sema, \"Mwenyezi Mungu anaongoa kwenya haki.\" Basi, je, yule anayeongoa kwenye haki anastahiki zaidi kufuatwa au yule asiyeongoka isipokuwa akiongozwa? Basi nyinyi mna nini, mnahukumu namna gani? 36. Na wengi wao hawafuati isipokuwa dhana tu. Na hakika, dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi yote wanayoyatenda. "},{"id":1939,"sura":10,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} Yeye Mtukufu anasema akibainisha kutoweza kwa miungu ya washirikina na kutosifika kwayo na sifa zinazoweza kusababisha wachukuliwe kuwa miungu pamoja na Mwenyezi Mungu, \u201cSema: Je, yupo katika washirika wenu mwenye kuanzisha kuumba viumbe kisha akavirejesha?\u201d Na huku ni kuuliza swali kwenye maana ya kukanusha na kuthibitisha. Yaani hakuna yeyote katika wao anayeanzisha kuumba viumbe kisha akavirudisha tena. Na ni dhaifu zaidi kuliko hivyo, na hawana uwezo hata zaidi yake. \"Sema: Mwenyezi Mungu anaazisha kuumba viumbe, kisha anavirejesha\u201d bila ya kuwa na mshirika yeyote wala msaidizi katika hayo. \"Basi ni vipi mnadanganywa?\u201d Yaani, mnageuzwa na mnaondolewa katika kumuabudu yule wa kipekee katika kuanzisha uumbaji na kuurudisha hadi katika kuwaabudu wale wasioumba chochote, nao wanaumbwa."},{"id":1940,"sura":10,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} \"Sema, \"Je, yupo yeyote katika washirika wenu mwenye kuongoa kwenye haki?\" Kwa kubainisha kwake na kuelekeza kwake au kwa ufunuo (wahyi) wake na kuwezesha kwake? \u201cSema, \"Mwenyezi Mungu\" peke yake \"anaongoa\" kwenye haki kwa ushahidi na hoja na ufunuo na kuwezesha, na usaidizi wa kushika njia iliyonyooka zaidi. \"Au yule asiyeongoka;\u201d yaani, haongoki \"isipokuwa akiongozwa,\" kwa sababu ya kutojua kwake na kwa sababu ya upotofu wake. Nao ni hao washirika wao ambao hawaongoi wala hawaongoki isipokuwa wakiongozwa. \"Basi nyinyi mna nini, mnahukumu namna gani?\u201d Yaani, ni kitu gani kiliwafanya mnahukumu hukumu hii batili ya kwamba ni sahihi kumuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu baada ya kudhihirika kwa hoja na ushahidi kwamba hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake? Na inapobainika kwamba hakuna katika miungu yao wanayoiabudu pamoja na Mwenyezi Mungu sifa za kimaana wala sifa za kimatendo zinazolazimu waabudiwe pamoja na Mwenyezi Mungu, bali hao wanasifika kwa upungufu wenye kulazimu ubatili wa uungu wao; basi ni kwa kitu gani walifanywa kuwa waungu pamoja na Mwenyezi Mungu?"},{"id":1941,"sura":10,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36} Basi jibu ni kwamba, hakika haya ni katika upambaji mambo wa Shetani kwa mwanadamu, na ni uongo mbaya zaidi na upotovu mkubwa zaidi mpaka akayaamini, na akayazoea, na akafikiri kuwa ndiyo haki ilhali si kitu. Na ndiyo maana akasema, \u201cNa wala hawawafuati hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu washirika wake.\u201d  Yaani, hawawafuati kwa uhakika washirika wa Mwenyezi Mungu, kwa maana Mwenyezi Mungu kamwe hana mshirika yeyote, kiakili wala kimaandiko, bali wanafuata dhana tu. \u201cNa hakika, dhana haifai kitu mbele ya haki.\u201d Basi wakawaita kuwa ni miungu, na wakawaabudu pamoja na Mwenyezi Mungu. \u201cHayo si isipokuwa ni majina mliyowapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuteremsha uthibitisho wowote juu ya hayo.\u201d \"Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi yote wanayoyatenda,\u201d na atawalipa kwa hayo kwa adhabu kali sana."},{"id":1942,"sura":10,"from_aya":37,"to_aya":41,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"37. Na haikuwa Qur-ani hii ni ya kuzuliwa kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini ni usadikisho wa yale yaliyoitangulia, na ni maelezo ya kina ya Kitabu kisicho na shaka yoyote ndani yake, kutoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. 38. Ama ndiyo wanasema ameizua? Sema, \"Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite muwawezao, kando na Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli.\" 39. Bali waliyakadhibisha yale wasiyoyaelewa elimu yake vyema kabla hayajawajia maelezo yake. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu hao. 40. Na miongoni mwao kuna anayeiamini, na miongoni mwao kuna asiyeiamini. Na Mola wako Mlezi ndiye anawajua vyema waharibifu. 41. Na wakikukadhibisha, basi sema, \"Mimi nina matendo yangu, na nyinyi mna matendo yenu. Nyinyi mko mbali sana na yale ninayoyatenda, nami niko mbali sana na mnayoyatenda.\" "},{"id":1943,"sura":10,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37} Yeye Mtukufu Anasema, \u201cNa haikuwa Qur-ani hii ni ya kuzuliwa kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.\u201d Yaani, haiwezekani wala haifikiriwi kwamba azuliwe Mwenyezi Mungu [Mtukufu] Qur-ani hii. Kwa sababu ni Kitabu Kikuu ambacho hakifikiwi na batili kwa mbele yake wala kwa nyuma yake, ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima, Msifiwa zaidi. Nacho ni Kitabu ambacho lau kuwa wangekusanyika watu na majini ili walete mfano wake, basi hawangeleta mfano wake, hata kama wangesaidiana wao kwa wao. Nacho ni Kitabu ambacho alikizungumza kwacho Mola Mlezi wa walimwengu wote. Basi vipi ataweza binadamu yeyote kuzungumza kwa mfano wake au kitu cha karibu nacho ilhali maneno yanategemea ukuu wa mzungumzaji na sifa zake? Basi ikiwa yeyote anafanana na Mwenyezi Mungu katika ukuu wake na sifa za ukamilifu wake, angeweza kuleta mfano wa Qur-ani hii. Na hata kama tutajishusha tuyakubali uwezekano wa kuwepo hilo, na mtu akaizulia Mola Mlezi wa walimwengu wote, basi angemharakishia adhabu na akamfikishia mateso mara moja. Lakini Mwenyezi Mungu alikiteremsha Kitabu hiki kuwa ni rehema kwa walimwengu wote, na ni hoja juu ya waja wake wote. Alikiteremsha \u201ckisadikishe yale yaliyoitangulia\u201d miongoni mwa vitabu vya mbinguni vya Mwenyezi Mungu, kwa namna ya kwamba kiliafikiana navyo na kikavisadikisha kwa yale vilivyoyashuhudia, na vikabashiria kuteremka kwake, na ikawa kama vilivyojulisha. \"Na ni maelezo ya kina ya Kitabu\u201d kuhusu yaliyo halali na ya haramu, na hukumu za kidini, na za kimajaliwa, na habari za ukweli \u201ckisicho na shaka yoyote ndani yake, kutoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.\u201d Yaani, hakina shaka yoyote ndani yake kwa namna yoyote ile. Bali ni haki ya yakini, ni uteremsho kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambaye alivilea viumbe vyote kwa neema zake. Na katika kubwa zaidi ya malezi yake ni kwamba aliwateremshia kitabu hiki, ambacho kina masilahi yao ya kidini na ya kidunia, na kinajumuisha tabia njema, na matendo mazuri."},{"id":1944,"sura":10,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} \u201cAu ndiyo wanasema;\u201d yaani, wale waliomkadhibisha kwa ukaidi na dhuluma, \"ameizua\" Muhammad dhidi ya Mwenyezi Mungu na akaitunga yeye. \"Sema\" uwaambie ukiwalazimisha kufanya kitu fulani, ikiwa watakiweza, basi hayo waliyodai yatawezekana, na kama sivyo, basi kauli yao hiyo ni batili. \"Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite muwawezao, isipokuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli.\" Ili wawasaidie kuleta sura moja mfano wake. Lakini hili haliwezekani. Na kama lingewezekana, basi wangelidai kuwa wanaweza kufanya hivyo, na wangelileta mfano wake. Lakini pindi kutoweza kwao kulipobainika, ikabainika kuwa kile walichosema ni batili na hakina fungu lolote katika hoja."},{"id":1945,"sura":10,"from_aya":39,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39} Kilichowafanya waikadhibishe Qur-ani ambayo inajumuisha haki ambayo hakuna haki nyingi zaidi yake ni kwamba hawakuijua vyema. Kwa maana, lau wangeliijua vyema na wakaifahamu ipasavyo kufahamiwa, basi wangeliifuata kwa kuisadikisha. Na vile vile mpaka sasa haijawajia tafsiri yake, ambayo iliwaahidi kuwa atawateremshia adhabu, na kuwatia mateso. Na ukadhibishaji huu unaotoka kwao ni aina sawa na kule kukadhibisha kwa wale waliokuwa kabla yao. Na ndiyo maana akasema, \u201cHivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu hao.\u201d Nayo ni maangamizo ambayo hakubaki yeyote miongoni mwao. Basi na watahadhari hawa dhidi ya kuendelea na kukadhibisha kwao, wakapatwa na yale yaliyowapata umma waliokadhibisha na vizazi vilivyoangamizwa. Na katika hili kuna ushahidi juu ya kuthibitisha mambo kwanza, na kwamba mtu hafai kuharakisha kukubali kitu au kukikataa kabla ya kukijua vyema."},{"id":1946,"sura":10,"from_aya":40,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40} \u201cNa miongoni mwao kuna anayeiamini;\u201d yaani, Qur-ani na yale iliyokuja nayo, \"na miongoni mwao kuna asiyeiamini. Na Mola wako Mlezi ndiye anawajua vyema waharibifu.\u201d Na hao ndio wale wasioiamini kwa dhulma, na ukaidi, na uharibifu. Basi atawalipa kwa uharibifu wao adhabu kali kabisa."},{"id":1947,"sura":10,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41} \u201cNa wakikukadhibisha,\u201d basi wewe endelea katika kulingania kwako, wala hakuna chochote juu yako katika hesabu yao, wala hakuna chochote juu yao katika hesabu yako, kila mmoja ana matendo yake. \u201cBasi sema, \"Mimi nina matendo yangu, na nyinyi mna matendo yenu. Nyinyi hamna mko mbali sana na yale ninayoyatenda, nami niko mbali sana na mnayoyatenda.\" Kama alivyosema Yeye Mtukufu, \u201cMwenye kutenda mema, basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kutenda mabaya, basi ni juu yake mwenyewe.\u201d"},{"id":1948,"sura":10,"from_aya":42,"to_aya":44,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"42. Na miongoni mwao kuna wale wanaokusikiliza. Je, wewe unaweza wasikizisha viziwi hata kama hawatumii akili? 43. Na miongoni mwao kuna yule anayekutazama. Je, wewe unaweza kuwaongoa vipofu hata kama hawaoni? 44. Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote, lakini watu wenyewe wanazidhulumu nafsi zao. "},{"id":1949,"sura":10,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu baadhi ya waliomkadhibisha Mtume, na yale aliyokuja nayo: \"Na\" hakika \u201cmiongoni mwao kuna wale wanaokusikiliza\u201d ewe Nabii - Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - wakati unaposoma ufunuo, si kwa sababu ya kutaka kuongoka, bali ni kwa njia ya kufurahia tu, na kukadhibisha, na kutafuta makosa. Na kusikiliza huku si kwa kunufaisha wala si kwa kuwaletea watu wake heri yoyote. Na hakuna shaka kwamba ndiyo maana ukafungika kwao mlango wa mafanikio, na wakanyimwa katika faida ya kusikiliza. Na ndiyo maana akasema, \u201cJe, wewe unaweza wasikizisha viziwi hata kama hawatumii akili?\u201d Na mbinu hii ya kuuliza ni ile yenye maana ya kukanusha na kuthibitisha hilo. Yaani, huwezi kuwasikizisha viziwi ambao hawawezi kusikia kauli hata ukaisema kwa sauti kubwa, hasa ikiwa akili zao hazipo. Kwa hivyo, ikiwa haiwezekani kumsikizisha kiziwi ambaye haelewi maneno, basi wakadhibishaji hawa vile vile haiwezekani kwako kuwaskizisha kusikia ambako watanufaika nako. Ama kusikia hoja, basi hakika walikwisha yasikia yale yanayosimamisha hoja ya kukata ya Mwenyezi Mungu. Basi hii hapa njia kubwa miongoni mwa njia za kutafuta elimu tayari imejifunga kwao, ambayo ni njia ya yanayosikika ambayo yanahusiana na habari."},{"id":1950,"sura":10,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} Kisha akataja kufungika kwa njia ya pili, ambayo ni njia ya kutazama, akasema: \"Na miongoni mwao kuna yule anayekutazama\u201d lakini hakumnufaishi kitu kukutazama kwake, wala hakuzichunguza vyema hali zako. Kwa hivyo, kama vile usivyoweza kuwaongoa vipofu hata kama hawaoni, basi vile vile huwezi kuwaongoa watu hawa. Ikiwa akili zao, na kusikia kwao, na kuona kwao ambazo ndizo njia zinazofikisha kwenye kujua haki, basi iwapi njia ya kuwafikisha kwenye haki? Na ilionyesha kauli yake: \"Na miongoni mwao kuna yule anayekutazama\u201d hadi mwisho wa Aya ... kuwa kutazama hali ya Nabii - rehema na Amani za Mwenyezi mungu zimshukie - na mwongozo wake, na maadili yake, matendo yake, na anachokilingania ni katika ushahidi mkubwa zaidi juu ya ukweli wake na usahihi wa kile alichokuja nacho, na kwamba inamtosha mwenye utambuzi bila ya kuhitaji ushahidi mwingine."},{"id":1951,"sura":10,"from_aya":44,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{44} Na kauli yake, \u201cHakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote.\u201d Hawazidishii katika mabaya yao, wala hawapunguzii mazuri yao, \u201clakini watu wenyewe wanazidhulumu nafsi zao.\u201d Wanajiwa na haki, lakini hawaikubali, kwa hivyo Mwenyezi Mungu anawaadhibu baada ya hayo kwa kuifunga mioyo yao, na kuyaziba masikio yao na macho yao."},{"id":1952,"sura":10,"from_aya":45,"to_aya":45,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"45. Na Siku atakapowakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa isipokuwa saa moja tu katika mchana! Watatambuana. Hakika wamehasirika wale waliokadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuongoka."},{"id":1953,"sura":10,"from_aya":45,"to_aya":45,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{45} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya dunia kuisha haraka kwa dunia, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atakapowakusanya watu na akawajumuisha katika siku ambayo hakuna shaka juu yake, itakuwa ni kana kwamba hawakukaa isipokuwa saa moja tu katika mchana, na kana kwamba hawakupitiwa na furaha wala taabu. Nao watatambuana kama ilivyokuwa hali yao katika dunia hii. Na katika Siku hii wachamungu watapata faida, na watahasirika  \u201cwale waliokadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuongoka,\u201d kwenye njia iliyonyooka, na Dini madhubuti kwa maana walikosa starehe, na wakastahiki kuingia Motoni."},{"id":1954,"sura":10,"from_aya":46,"to_aya":46,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"46. Na ima tutakuonyesha baadhi ya yale tunayowaahidi, au tukufishe kabla yake, basi marejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa wanayoyafanya."},{"id":1955,"sura":10,"from_aya":46,"to_aya":46,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{46} Yaani, usihuzunike, ewe Mtume juu ya hawa wanaokadhibisha, wala usiharakishe kwa sababu yao. Kwani, hakika ni lazima watapatwa na adhabu ambayo tunawaahidi: ima katika dunia, na uione kwa macho yako na nafsi yako itulie kwa hilo, au katika Akhera baada ya kuwatimizia muda wao. Kwani, marejeo yao ni kwa Mwenyezi Mungu, naye atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda, [Mwenyezi Mungu] aliyadhibiti vyema, nao wakayasahau, na Mwenyezi Mungu ni shahidi juu ya kila kitu. Basi aya hii ina ahadi ya adhabu kali kwao, na kumfariji Mtume ambaye kaumu yake walimkadhibisha na wakamkaidi."},{"id":1956,"sura":10,"from_aya":47,"to_aya":49,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"47. Na kila umma una Mtume. Alipowajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawadhulumiwi. 48. Na wanasema, \u201cNi lini ahadi hii, ikiwa nyinyi ni wakweli? 49. Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda wao waliowekewa. Ukifika muda wao hawakawii hata saa moja wala hawatangulii. "},{"id":1957,"sura":10,"from_aya":47,"to_aya":47,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{47} Yeye Mtukufu anasema, \u201cNa kila umma\u201d miongoni mwa umma zilizopita \u201cuna Mtume\u201d anayewalingania kumpwekesha Mwenyezi Mungu na Dini yake. Basi anapowajia Mtume wao na Ishara mbalimbali, baadhi yao wanamsadiki, na wengine wanamkadhibisha, kisha Mwenyezi Mungu anahukumu baina yao kwa uadilifu kwa kuwaokoa Waumini na kuwaangamiza wakadhibishaji. Na hawadhulumiwi\u201d kwa kuadhibiwa kabla ya kutumwa Mtume na kubainisha hoja, au kwa kuadhibiwa si kwa kosa lao."},{"id":1958,"sura":10,"from_aya":48,"to_aya":49,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{48 - 49} Basi na watahadhari wale wanaokukadhibisha kujifananisha na umma walioangamizwa, kwa hivyo yakawapata yale yaliyowapata watu wale, wala wasione kwamba adhabu itachelewa na wakasema, \"Ni lini ahadi hii, ikiwa nyinyi ni wakweli?\" Kwani huu ni udhalimu kutoka kwao, kwa sababu walitaka hilo kutoka kwa Nabii \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. \u2013 Yeye hakika hana chochote katika jambo hili, bali juu yake ni kufikisha tu na kuwabainishia watu. Na ama hesabu yao na kuteremsha adhabu juu yao, basi hilo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mtukufu. Ataiteremsha juu yao utakapofika muda ambao aliliwekea hilo na wakati ambao alipitisha lifanyike ndani yake ambao unaafikiana na hekima Yake ya kiungu. Basi wakati huo unapokuja, hawawezi kukawia hata saa moja wala hawawezi kutangulia. Basi na watahadhari wanaokadhibisha kuiharakisha. Kwa maana wanaiharakisha adhabu ya Mwenyezi Mungu ambayo inapoteremka, basi adhabu yake haizuiliki dhidi ya kaumu wahalifu. Na kwa sababu hii akasema:"},{"id":1959,"sura":10,"from_aya":50,"to_aya":52,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"50. Sema, \u201cMnaonaje ikiwajia adhabu yake hiyo usiku au mchana. Basi wahalifu wanaharakisha nini?\u201d 51. Tena je, ikishatokea ndiyo mtaiamini? Je, sasa? Na ilhali mlikuwa mkiifanyia haraka? 52. Kisha wale waliodhulumu wataambiwa, \"Ionjeni adhabu ya kudumu. Kwani mtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyachuma?\" "},{"id":1960,"sura":10,"from_aya":50,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{50} Yeye Mtukufu anasema: \" Sema, \u201cMnaonaje ikiwajia adhabu yake hiyo usiku\u201d wakati wa kulala kwenu usiku, \u201cau mchana\u201d hali ya kuwa mmeghafilika? \u201cBasi wahalifu wanaharakisha nini?\u201d Yaani, ni bishara gani njema wanayoiharakishia? Na ni adhabu gani wanayoifanyia mbio?"},{"id":1961,"sura":10,"from_aya":51,"to_aya":51,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{51} \u201cTena je, ikishatokea ndiyo mtaiamini?\u201d Basi hakika Imani hiyo haifai kitu wakati inapofika adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wataambiwa wakikaripiwa na kulaumiwa katika hali ile ambayo walidai kuwa wameamini: \"Je, sasa?\" Ndiyo mnaamini katika hali ya shida na mashaka, \"Na ilhali mlikuwa mkiiharakishia?\" Kwa maana desturi ya Mwenyezi Mungu katika waja wake ni kwamba anawaridhia wanapomwomba radhi kabla ya kutokea kwa adhabu. Lakini inapotokea adhabu, kuamini kwa nafsi hapo hakutainufaisha kitu, kama alivyosema Yeye kuhusu Firauni alipotaka kuzama. \u201cAkasema, \u201cNimemini kuwa hakuna mungu isipokuwa yule waliyemwamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa Waislamu!\" Basi huyo ataambiwa, \u201cJe, sasa? Na ilhali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa waharibifu!\" Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, \u201cLakini imani yao haikuwa yenye kuwanufaisha kitu wakati walipoiona adhabu yetu. Hii ndiyo desturi ya Mwenyezi Mungu ambayo alikwisha pitisha kwa waja wake.\" Na hapa akasema, \"Tena je, ikishatokea ndio mtaiamini? Je, sasa?\" mnadai kuamini, \"Na ilhali mlikuwa mkiifanyia haraka?\" Basi haya ndiyo mikono yenu iliyafanya, na haya ndiyo mliyoyafanyia haraka."},{"id":1962,"sura":10,"from_aya":52,"to_aya":52,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{52} \"Kisha wale waliodhulumu wataambiwa\" wakati watakapolipwa matendo yao kikamilifu Siku ya Qiyama, \"Ionjeni adhabu ya kudumu.\" Yaani, adhabu ambayo mtadumu humo, wala hamtapunguziwa hata saa moja. \"Kwani, mtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyachuma,\" miongoni mwa kufuru, kukadhibisha, na maasia."},{"id":1963,"sura":10,"from_aya":53,"to_aya":56,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"53. Na wanakuuliza, \"Je, ni kweli hayo?\" Sema, \"Ehe! Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi! Hakika hayo ni kweli, na wala nyinyi hamtashinda.\" 54. Na lau kuwa kila nafsi iliyodhulumu inamiliki kila kilichomo katika ardhi, basi bila ya shaka ingejikomboa kwavyo. Na watakapoiona adhabu, wataficha majuto. Na itahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa. 55. Jueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Lakini wengi wao hawajui. 56. Yeye ndiye anayehuisha na anayefisha. Na kwake mtarejeshwa. "},{"id":1964,"sura":10,"from_aya":53,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{53} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, -  \"Na wanakuuliza, \"Je, ni kweli hayo?\" Yaani, hao wakadhibishaji wanataka kujua kutoka kwako kwa njia ya inda na ukaidi, si kwa njia kutaka kubainshiwa na kutafuta mwelekeo, \"Je, ni kweli hayo?\" Yaani, je ni sahihi kwamba waja watakusanywa pamoja na kufufuliwa baada ya kufa kwao kwa ajili ya Siku ya Kiyama, na kwamba waja watalipwa kwa matendo yao, ikiwa ni heri, basi kwa heri, na ikiwa maovu, basi kwa maovu? \"Sema,\" uwaambie ukiapa juu ya usahihi wake, na kwa kuweka ushahidi wazi na hoja juu ya hilo: \"Ehe! Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi! Hakika hayo ni kweli\" Hakuna shaka yoyote ndani yake wala mchanganyiko wowote ndani yake, \"na wala nyinyi hamtamshinda\" Mwenyezi Mungu kuwafufua. Kwani, kama alivyoanzisha kuwaumba nyinyi, nanyi hamkuwa kitu, basi vivyo hivyo atawarejesha mara nyingine ili awalipe kwa matendo yenu."},{"id":1965,"sura":10,"from_aya":54,"to_aya":54,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{54} \"Na\" atakapokuwa siku ya Qiyama, basi lau \"kuwa itamiliki kila nafsi iliyodhulumu\" kwa ukafiri na maasia vyote vilivyomo katika ardhi kama vile dhahabu, fedha na vitu vinginevyo, ili ajikomboe kwavyo kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu. \"Basi bila ya shaka ingejikomboa kwavyo\" lakini hilo halingelimnufaisha kwa maana manufaa, madhara, malipo na adhabu ni juu ya matendo mema na mabaya. \"Na wataficha,\" yaani, wale waliodhulumu, \"majuto watakapoiona adhabu.\" Yaani, watajuta kwa yale waliyoyatanguliza, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita. \"Na itahukumiwa baina yao kwa uadilifu;\" yaani, kwa uadilifu kamili ambao hauna dhuluma yoyote ndani yake wala ukandamizaji kwa namna yoyote ile."},{"id":1966,"sura":10,"from_aya":55,"to_aya":55,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{55} \"Jueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi.\" Anavihukumu kwa hukumu yake ya kidini na ya kimajaliwa. Na atawahukumu kwa hukumu yake ya kimalipo. Na ndiyo maana akasema, \"Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Lakini wengi wao hawajui.\" Basi kwa sababu ya hilo, hawajitayarishi kwa ajili ya kukutana na Mwenyezi Mungu, bali pengine hawakuamini hilo, ilhali ushahidi mwingi wa uhakika ulikwisha kuja juu ya hilo na hoja za kimaandiko na na za kiakili."},{"id":1967,"sura":10,"from_aya":56,"to_aya":56,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{56} \"Yeye ndiye anayehuisha na anayefisha.\" Yaani, Yeye ndiye anayeendesha kuhuisha, kufisha, na aina zote za uendeshaji, hana mshirika yeyote katika hayo. \"Na kwake mtarejeshwa\" Siku ya Qiyama, kisha atawalipa kwa matendo yenu, ya heri yake na maovu yake."},{"id":1968,"sura":10,"from_aya":57,"to_aya":58,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"57. Enyi watu! Yamekwisha wajia mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na poza ya yale yaliyo katika vifua, na uwongofu, na rehema kwa Waumini. 58. Sema, \"Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi na wafurahi kwa hayo. Hayo ndiyo bora kuliko hayo wanayoyakusanya. "},{"id":1969,"sura":10,"from_aya":57,"to_aya":57,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{57} Yeye Mtukufu Anasema akiwahimiza viumbe kukifuata Kitabu hiki kitukufu, kwa kutaja sifa zake nzuri za muhimu sana kwa waja. Akasema, \"Enyi watu! Yamekwisha wajia mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi;\" yaani, yanawaaidhi na yanawaonya juu ya matendo yenye kusababisha  ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, yenye kulazimu adhabu yake, na yanawatahadharisha juu yake kwa kubainisha athari zake na madhara yake, \"na poza ya yale yaliyo katika vifua.\" Nayo ni Qur'ani hii Tukufu, ambayo ni poza kwa yale yaliyo katika vifua miongoni mwa maradhi ya matamanio yanayozuia kuifuata sheria. Na maradhi ya shaka yanayotia doa katika elimu ya yakini. Kwani, yale yaliyo ndani yake ya mawaidha, kutia moyo, kuhofisha, ahadi nzuri na ahadi ya adhabu ni katika yale yanayomfanya mja awe na hamu na hofu. Na kukipatikana kutaka ndani yake heri na kuhofu maovu, na mawili hayo yakakuwa, kulingana na yale yanayoyajia kwa kujirudia katika maana za Qur-ani, basi hilo litamfanya mja kutanguliza matakwa ya Mwenyezi Mungu mbele ya matamanio ya nafsi yake; na yanakuwa yale yanayomridhisha  Mwenyezi Mungu ndiyo yanayopendwa zaidi kwa mja kuliko matamanio ya nafsi yake. Na vile vile yale yaliyomo miongoni mwa hoja mbalimbali na ushahidi ambazo Mwenyezi Mungu alizieleza kueleza kwa kina zaidi na akazibainisha kubainisha kuzuri zaidi jambo ambalo linaondoa shaka zenye kutoa doa katika haki na unafika kwa hayo viwango vya juu zaidi vya yakini. Na ikiwa moyo utakuwa salama kutokana na maradhi yake, na ukavaa nguo za salama, basi viungo vyote vinaufuata. Kwa kuwa hivyo vinatengenea kwa kutengenea kwake, na vinaharibiwa kwa kuharibika kwake. \"Na uwongofu, na rehema kwa Waumini.\" Na uwongofu ni kuijua haki na kuifanyia kazi. Nayo rehema ni yale yanatopatikana miongoni mwa heri na wema, na malipo ya haraka na ya baadaye kwa wanaoongoka kwayo. Basi uwongofu ndiyo njia bora zaidi, nayo rehema ndiyo malengo na matamanio kamili zaidi, lakini hawezi kulifikia hilo wala haliwi rehema isipokuwa kwa Waumini tu. Na ukipatikana uwongofu, nayo rehema inayotokana nayo ikaingia, yanapatikana mafanikio, na kufaulu, na faida, na furaha na raha."},{"id":1970,"sura":10,"from_aya":58,"to_aya":58,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{58} Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akaamrisha kufurahia hilo, akasema, Sema, \"Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu\" ambayo ni Qur-ani, ambayo ndiyo neema kubwa zaidi na fadhila ambazo Mwenyezi Mungu amewapa Waja Wake. Na rehema zake ni Dini, imani, kumuabudu Mwenyezi Mungu, kumpenda Yeye, na kumjua. \"Basi na wafurahi kwa hayo. Hayo ndiyo bora kuliko hayo wanayoyakusanya,\" miongoni mwa starehe za dunia na raha zake. Kwa hivyo, neema ya Dini, ambayo inaungana na furaha ya nyumba hizi mbili, haina uhusiano kati yake na kila kitu kilicho katika dunia hii, ambavyo vitatoweka na kuondoka hivi karibuni. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu aliamuru kufurahia fadhila yake na rehema zake, kwa sababu hilo ni katika yale yanayosababisha nafsi kukunjuka, na ukakamavu wake, na kushukuru kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na yenye kuipa nguvu, na hamu kubwa ya elimu na imani inayoitia kuyaongeza hayo. Na hii ni furaha inayosifiwa. Tofauti na kufurahia matamanio ya dunia hii na anasa zake, au kufurahia batili. Kwa maana hili linashutumiwa, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu kaumu ya Qaruni walipomwambia, \"Usijigambe kwa furaha! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaojigamba kwa furaha.\" Na kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema kuhusu wale waliofurahia yale waliyo nayo ya batili yanayopingana na yale ambayo waliyokuja nayo Mitume. \"Walipowajia Mitume wao kwa ushahidi ulio wazi, wakajitapa kwa elimu waliyo nayo.\""},{"id":1971,"sura":10,"from_aya":59,"to_aya":60,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"59. Sema: Je, munaonaje yale aliyowateremshia Mwenyezi Mungu katika zile riziki, basi mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali. Sema, \"Je, Mwenyezi Mungu aliwaruhusu, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?\" 60. Na ni nini dhana ya wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uongo Siku ya Qiyama? Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru. "},{"id":1972,"sura":10,"from_aya":59,"to_aya":59,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{59} Yeye Mtukufu Anasema akiwakanusha washirikina ambao walizua kuharamisha yale aliyohalalisha Mwenyezi Mungu na kuhalalisha yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, \"Sema: Je, mnaonaje yale aliyowateremshia Mwenyezi Mungu katika zile riziki.\" Yaani, aina mbalimbali za wanyama waliohalalishwa ambao Mwenyezi Mungu aliwafanya kuwa riziki kwao na rehema kwao. Waambie ukiwakaripia kwa kauli hii potofu: \"Je, Mwenyezi Mungu aliwaruhusu, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?\" Na inavyojulikana ni kuwa Mwenyezi Mungu hakuwapa ruhusa. Kwa hivyo ikajulikana kuwa walizua uongo."},{"id":1973,"sura":10,"from_aya":60,"to_aya":60,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{60} \"Na ni nini dhana ya wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uongo Siku ya Qiyama?\" Kwamba Mwenyezi Mungu atawaadhibu na kuwatesa. Yeye Mtukufu amesema, \"Na Siku ya Qiyama utawaona wale waliomdanganyishia Mwenyezi Mungu nyuso zao zimefanywa kuwa nyeusi.\" \"Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila juu ya watu\" wengi, na mwenye wema mwingi, lakini wengi wa watu hawashukuru; ima kwa kutozishukuru hasa, au kwa kujisaidia kwazo katika kumuasi. Na ima waharamishe kwazo, au wakatae yale aliyowaneemesha kwayo Mwenyezi Mungu waja wake. Na ni wachache tu miongoni mwao wanaoshukuru ambao wanazikiri neema hizo, na kumsifu Mwenyezi Mungu juu yake, na kujisaidia kwazo katika kumtii. Na Aya hii inatumika kama ushahidi juu ya kanuni ya msingi katika vyakula vyote ni kwamba ni halali, isipokuwa vile ambavyo Sheria alikataza. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwakanusha wale wanaoharamisha riziki ambayo aliwateremshia waja wake."},{"id":1974,"sura":10,"from_aya":61,"to_aya":61,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"61. Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur-ani, wala hamtendi kitendo chochote isipokuwa Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa isipokuwa kimo katika Kitabu kilicho wazi."},{"id":1975,"sura":10,"from_aya":61,"to_aya":61,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{61} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya ujumla wa kuona kwake na kujua kwake hali zote za waja wake katika harakati zao na utulivu wao. Na ndani ya hili kuna wito wa kumchunga Yeye daima, akasema: \"Na huwi katika jambo lolote.\" Yaani, hali yoyote miongoni mwa hali zako za kidini na za kidunia, \"wala husomi sehemu yoyote katika Qur-ani.\" Yaani, na chochote unachokisoma katika Qur\u2019ani ambayo Mwenyezi Mungu alikufunulia, \"wala hamtendi kitendo chochote\" kidogo au kikubwa, \"isipokuwa Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo.\" Yaani, wakati mnapoyaanza, na kuendelea kuyafanya. Basi mchungeni Mwenyezi Mungu katika vitendo vyenu, na vifanyeni kwa njia ya uaminifu na kujitahidi. Na jihadharini na yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani, Yeye anawaona na anajua dhahiri zenu na ndani zenu. \"Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi;\" yaani, hakifichiki juu ya kujua kwake, na kusikia kwake, na kuona kwake, na kushuhudia kwake \"chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa isipokuwa kimo katika Kitabu kilicho wazi.\" Yaani, amekwisha kizunguka kwa elimu yake, na kalamu yake ikayaandika. Na daraja mbili hizi katika daraja za hatima na mapitisho mara nyingi Mwenyezi Mungu huziunganisha pamoja, ambazo ni elimu inayozunguka vitu vyote, na kuandika kwake kunakozunguka matukio yote, kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo katika mbingu na ardhi? Hakika hayo yako katika Kitabu. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.\""},{"id":1976,"sura":10,"from_aya":62,"to_aya":64,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"62. Jueni kuwa vipenzi wa Mwenyezi Mungu hawana hofu yoyote juu yao wala hawatahuzunika. 63. Wale walioamini na wakawa wachaji. 64. Wao wana bishara njema katika uhai wa dunia na katika Akhera. Hakuna mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa. "},{"id":1977,"sura":10,"from_aya":62,"to_aya":62,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{62} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu marafiki wake na vipenzi wake, na anataja matendo yao, na sifa zao, na malipo yao. Akasema, \"Jueni kuwa vipenzi wa Mwenyezi Mungu hawana hofu yoyote juu yao\" kwa yale watakayoyapata miongoni mwa yale yaliyo mbele yao miongoni mwa yanayohofisha na mahangaiko. \"Wala hawatahuzunika\" juu ya yale waliyoyatanguliza, kwa sababu hawakutanguliza isipokuwa matendo mema. Na ikiwa hawana hofu yoyote juu yao wala hawatahuzunika, basi inawathibitikia amani, furaha, na heri nyingi ambayo haijui isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu."},{"id":1978,"sura":10,"from_aya":63,"to_aya":63,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"63. Kisha akataja sifa yao, akasema, \"wale walioamini\" Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na katika majaliwa, mema yake na mabaya yake, na wakaisadikisha imani yao kwa uchamungu kwa kutekeleza maamrisho na kuepuka makatazo. Kwa hivyo, kila ambaye ni Muumini, mchamungu, basi yeye ni kipenzi wa Mwenyezi Mungu."},{"id":1979,"sura":10,"from_aya":64,"to_aya":64,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{64} Na \"Wao wana bishara njema katika uhai wa dunia na katika Akhera\" Ama bishara katika dunia, hiyo ni sifa nzuri na upendo katika nyoyo za Waumini, na ndoto njema, na yale anayoyaona mja miongoni mwa upole wa Mwenyezi Mungu kwake, na kumsahihisha kwake matendo mazuri na tabia nzuri, na kumuondoa kwenye tabia mbaya. Na ama katika akhera, basi ya kwanza yake ni kubashiriwa wakati wa kuchukuliwa roho zao, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Hakika wale waliosema, \"Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao Malaika huwateremkia wakawaambia: Msihofu, wala msihuzunike. Nanyi pokeeni bishara ya Pepo ambayo mlikuwa mkiahidiwa.\"  Na ndani ya kaburi kuna bishara ya kuridhiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu na neema ya kudumu. Na katika Akhera kuna bishara kamili ya kuingia katika Mabustani ya neema na kuokoka na adhabu chungu. \"Hakuna mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu\" bali yale aliyoyaahidi Mwenyezi Mungu, basi hayo ni haki ambayo haiwezi kughairishwa wala kubadilishwa. Kwa sababu, Yeye ndiye Mkweli katika Anayoyasema, ambaye hakuna yeyote anayeweza kupingana Naye katika yale aliyojalia na kuyahukumu. \"Huko ndiko kufuzu kukubwa\" kwa sababu kunajumuisha wokovu kutokana na kila kinachoepukwa, na ushindi juu ya kila kitafutwacho, kipendwacho. Na alikufungia kufaulu katika hilo kwa sababu, hakuna kufaulu kwa wasiokuwa wenye imani na uchamungu. Na muhtasari wa hilo ni kuwa bishara hii njema inajumuisha kila heri, na malipo ambayo Mwenyezi Mungu ameiwekea katika dunia na akhera kwa sababu ya imani na uchamungu. Na ndiyo maana akaliacha hilo bila ya kulifungia."},{"id":1980,"sura":10,"from_aya":65,"to_aya":65,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"65. Wala yasikuhuzunishe maneno yao. Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema Mwenye kujua yote."},{"id":1981,"sura":10,"from_aya":65,"to_aya":65,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{65} Yaani, usihuzunishwe na maneno ya wale wanaokukadhibisha, ambayo kwayo wanafikia kukutia doa, na pia Dini yako. Kwa maana, maneno yao hayo hayawapi utukufu wala hayakudhuru hata kidogo. \"Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.\" Humpa huo amtakaye na humnyima amtakaye. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, \"Mwenye kutaka utukufu, basi utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.\" Yaani na autafute katika kumtii, kwa ushahidi wa kauli yake baada yake: \"Kwake Yeye hupanda neno zuri, na tendo jema Yeye hulitukuza.\" Na inavyojulikana ni kwamba wewe unamtii Mwenyezi Mungu, na kwamba utukufu ni wako na wa wafuasi wako kutoka kwa Mwenyezi Mungu. \"Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu, na Mtume wake, na Waumini.\" Na kauli yake, \"Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema Mwenye kujua yote.\" Yaani, kusikia kwake kulizunguka sauti zote, kwa hivyo hakifichiki kitu kwake. Na elimu yake imezunguka kila ya dhahiri na ya ndani. Basi hakifichikani kwake chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na mbingu, wala kidogo zaidi kuliko hicho wala kikubwa zaidi. Na Yeye Mtukufu anayasikia maneno yako na maneno ya maadui zako kukuhusu wewe. Na anayajua hayo kwa kina. Kwa hivyo tosheka na elimu ya Mwenyezi Mungu na kutosheleza kwake. Kwa hivyo, mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, basi Yeye anamtosha."},{"id":1982,"sura":10,"from_aya":66,"to_aya":67,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"66. Jueni kuwa ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Na wala hawawafuati washirika wowote hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu. Wao hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawasemi isipokuwa uongo. 67. Yeye ndiye aliyewajaalia usiku ili mtulie humo, na mchana wa kuonea. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kaumu wanaosikia. "},{"id":1983,"sura":10,"from_aya":66,"to_aya":66,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{66} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba Yeye ni vyake vilivyo katika mbingu na ardhi, kwa kuviumba, na kuvimiliki [navyo ni waja wake] ambavyo anaviendesha anavyotaka kwa hukumu zake. Kwani hivyo, vyote vinamilikiwa na Mwenyezi Mungu, vimetiishwa na vinaendeshwa, wala havistahiki chochote katika ibada wala si washirika wa Mwenyezi Mungu kwa namna yoyote ile. Na kwa sababu ya hili ndiyo akasema, \"Na wala hawawafuati washirika wowote hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu. Wao hawafuati isipokuwa dhana tu\" ambayo haisaidii chochote mbele ya haki; \"na hawasemi isipokuwa uongo \" katika hilo. Nalo ni uongo na masingizio. Kwa hivyo, ikiwa ni wakweli kwamba hao ni washirika wa Mwenyezi Mungu, basi na wadhihirishe sifa wanazostahiki kwazo uzito wa chembe katika ibada; lakini hawataweza. Basi Je, yuko yeyote miongoni mwao anayeumba chochote, au anayeruzuku, au anayemiliki chochote katika viumbe, au anayeendesha usiku na mchana ambao Mwenyezi Mungu aliufanya kuwa nguzo ya maisha ya mwanadamu?"},{"id":1984,"sura":10,"from_aya":67,"to_aya":67,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{67} Na \"Yeye ndiye aliyewajaalia usiku ili mtulie humo\" kwa kulala usingizi na kutulia kwa sababu ya giza ambalo linafunika uso wa ardhi. Kwa maana, ikiwa mwanga ungeendelea, basi hawangeburudika wala kutulia. \"Na\" Mwenyezi Mungu aliufanya \"mchana wa kuonea;\" yaani, kuwa na mwangaza wanaona kwa huo viumbe, kwa hivyo wanaweza kuendesha maisha yao na masilahi ya dini yao na dunia yao. \"Hakika katika haya zipo Ishara kwa kaumu wanaosikia,\" kutoka kwa Mwenyezi Mungu kusikia kwa kufahamu, na kukubali, na kutafuta mwelekeo, si kusikia kwa inda na ukaidi. Kwani katika hayo zipo ishara kwa kaumu wanaozisikia, ambao wanayatumia kama ushahidi kwamba Yeye pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa, na kwamba Yeye ndiye Mungu wa haki, na kwamba uungu wa chochote kisichokuwa Yeye ni batili, na kwamba Yeye ndiye Mpole, Mwenye kurehemu, Mwenye kujua yote, Mwenye hekima."},{"id":1985,"sura":10,"from_aya":68,"to_aya":70,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"68. Walisema, \"Mwenyezi Mungu alijifanyia mwana.\" Ametakasika! Yeye ndiye asiyehitajia kitu. Ni vyake vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Nyinyi hamna uthibitisho wowote wa haya! Je, mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyoyajua? 69. Sema, \"Hakika wale wanaomzulia uongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.\" 70. Hiyo ni starehe ya katika dunia tu, kisha marejeo yao ni kwetu. Kisha tutawaonjesha adhabu kali kwa sababu ya yale waliyokuwa wakikufuru. "},{"id":1986,"sura":10,"from_aya":68,"to_aya":68,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{68} Yeye Mtukufu anasema akijulisha kuhusu uongo wa washirikina juu ya Mola Mlezi wa walimwengu wote, \"Walisema, \"Mwenyezi Mungu alijifanyia mwana.\" Basi akajitaka nafsi yake na hayo kwa kusema: \"Ametakasika;\" yaani, amesafika kutokana na yale wanayoyasema madhalimu katika kumnasibisha na mapungufu na ametukuka utukufu mkubwa. Kisha akaliwekea hilo hoja kadhaa: moja yake ni kauli yake, \"Yeye ndiye asiyehitajia kitu.\" Yaani, kutohitaji kwote ni kwake, na aina mbalimbali za kutohitaji anazo yeye. Basi Yeye ndiye asiyehitaji ambako ni kutohitaji kukamilifu katika njia zote, na mazingatio yote, na kwa namna yoyote ile. Kwa hivyo, ikiwa yeye si mhitaji kwa njia yoyote ile, basi atajifanyia mwana kwa sababu gani? Je, ni kwa sababu ganianahitaji mwana? Basi hili linapingana na kutohitaji kwake. Kwa maana hajifanyii yeyote mwana isipokuwa kwa sababu ya upungufu katika kutohitaji kwake? Ushahidi wa pili ni kauli yake: \"Ni vyake vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Na hili ni neno la jumla, lenye kujumuisha. Hakitoki kwalo chochote kinachopatikana miongoni mwa wakazi wa mbinguni na ardhi. Vyote viliumbwa, na ni waja wanaomilikiwa. Na inavyojulikana ni kwamba sifa hii ya jumla inapingana na ukweli kwamba yeye ana mwana [miongoni mwao]. Kwa maana, mwana anakuwa wa aina sawa na mzazi wake, na hawi wa kuumbwa wala mmilikiwa. Kwa hivyo, kuvimiliki kwake vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi kwa ujumla kunapingana na kuwa kwavyo wana wake. Ushahidi wa tatu ni kauli yake \"Nyinyi hamna uthibitisho wowote wa haya!\" Yaani, Je, mnayo hoja yoyote na ushahidi wowote unaoonyesha kwamba Mwenyezi Mungu ana mwana? Na ikiwa wangelikuwa na ushahidi, basi wangeionyesha. Na alipowapa changamoto, na akawafanya washindwe kusimamisha ushahidi, ikajulikana ya kwamba yale wanayoyasema ni batili, na kwamba huko ni kusema bila ya elimu, na ndiyo maana akasema, \"mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyoyajua?\" Kwani, haya ni miongoni mwa mambo makubwa yaliyoharamishwa."},{"id":1987,"sura":10,"from_aya":69,"to_aya":70,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{69 - 70} \"Sema, \"Hakika wale wanaomzulia uongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.\" Yaani, hawatayafikia wanayoyatafuta, wala hawatapata malengo yao, bali watafurahia katika ukafiri wao na uongo wao katika dunia hii kwa muda mchache, kisha watakwenda kwa Mwenyezi Mungu na kurejea kwake, naye atawaonjesha \u201cadhabu kali kwa sababu ya yale waliyokuwa wakikufuru.\" Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali walizidhulumu nafsi zao wenyewe."},{"id":1988,"sura":10,"from_aya":71,"to_aya":73,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"71. Na wasomee habari za Nuhu alipowaambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Ikiwa ni kukubwa kwenu kukaa kwangu nanyi na kuwakumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, nyinyi likusanyeni  jambo lenu pamoja na washirika wenu, kisha jambo lenu hilo lisiwe la kufichikana kwenu, kisha nihukumuni, wala msinipe muhula. 72. Na mkigeuka, basi mimi sikuwaomba ujira wowote. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waislamu. 73.   Lakini wakamkadhibisha. Kwa hivyo tukamwokoa, pamoja na wale waliokuwa naye, katika jahazi. Na tukawafanya wao ndio waliobakia, na tukawazamisha wale waliozikadhibisha Ishara zetu. Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walioonywa. "},{"id":1989,"sura":10,"from_aya":71,"to_aya":71,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{71} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake: Na wasomee kaumu yako \"habari za Nuhu\" katika kulingania kwake kaumu yake wakati alipowalingania kwa Mwenyezi Mungu muda mrefu, na akakaa kati yao miaka elfu moja isipokuwa miaka hamsini, lakini hakukuwazidishia kulingania kwake huko isipokuwa kuvuka mipaka. Kwa hivyo, wakachoka naye, na wakakata tamaa. Lakini yeye, rehema na amani ziwe juu yake, hakufanya uvivu wala hakuacha kuwalingania. Akawaambia, \"Enyi kaumu yangu! Ikiwa ni kukubwa kwenu kukaa kwangu nanyi na kuwakumbusha kwangu Ishara za Mwenyezi Mungu.\" Yaani, ikiwa kukaa kwangu nanyi na kuwakumbusha kwangu yale yatakayowafaa kwa ishara za Mwenyezi Mungu ambazo ni ushahidi ulio wazi na bainifu yamekuwa magumu juu yenu, na yakawa makubwa juu yenu na mnataka kunifikishia mabaya au kuikataa haki \"basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu.\" Yaani, nimemtegemea Mwenyezi Mungu katika kuniondolea kila baya ninalokusudiwa kwalo, na kile ninachokilingania. Basi hili ndilo jeshi langu na silaha zangu. Nanyi basi leteni muwezayo yote miongoni mwa aina za silaha na idadi ya wasaidizi, \"kisha likusanyeni  jambo lenu pamoja\" nyinyi nyote na asibaki nyuma yeyote miongoni mwenu na wala msiache chochote katika juhudi zenu. \"Na\" waleteni \"washirika wenu\" ambao mlikuwa mkiwaabudu na mnawafanya kuwa marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, \"kisha jambo lenu hilo lisiwe la kufichikana kwenu.\" Yaani, msichanganyike katika hilo wala lisifichikane kwenu, bali na lidhihirike na liwe hadharani. \"Kisha nihukumuni;\" yaani, nihukumuni kwa adhabu na ubaya ambao uko katika uwezo wenu \"wala msinipe muhula.\" Yaani, msinipe muhula wa saa moja katika mchana. Basi huu ni ushahidi wa uhakika na ishara kubwa juu ya usahihi wa ujumbe wake na ukweli wa kile alichokuja nacho. Kwa maana, alikuwa yeye peke yake bila ya ukoo wa kumlinda wala majeshi wa kumhifadhi. Na alikuwa amewashambulia kaumu wake kwa kupumbaza rai zao, kuweka wazi uharibifu wa dini yao, na kuwatia dosari miungu yao. Nao walikuwa wamebeba chuki na uadui juu yake ambayo yalikuwa makubwa zaidi kuliko milima iliyo imara. Na pia walikuwa watu wenye uwezo na nguvu, naye akawaambia: Kusanyikeni nyinyi na washirika wenu na yeyote muwezaye, na wekeni wazi kila muwezalo miongoni mwa njama, kisha nifikishieni kama mnaweza kufanya hivyo; lakini hawakuweza kufanya lolote katika hayo. Kwa hivyo ikajulikana kwamba yeye ndiye mkweli kwa uhakika, nao ndio waongo katika yale wanayoyadai."},{"id":1990,"sura":10,"from_aya":72,"to_aya":72,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{72} Ndiyo maana akasema: \"Na mkigeuka\" mkayaacha yale niliyowalingania kwayo, basi hakuna sababu kwa kugeuka kwenu huko. Kwa sababu, imebainika kwamba nyinyi hamgeuki kutoka kwenye batili kwenda kwenye haki; bali mnageuka kutoka kwenye haki ambayo ushahidi ulisimama juu ya usahihi wake kwenda kwenye batili ambayo ushahidi ulisimama juu ya uharibifu wake. Lakini pamoja na haya, \"mimi sikuwaomba ujira wowote\" juu ya ulinganizi wangu na juu ya kuitikia kwenu ndiyo mseme: Huyu ametujia ili achukue mali zetu, kwa hivyo mkakataa kwa sababu ya hili. \"Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu.\" Yaani, sitaki thawabu na malipo isipokuwa kutoka Kwake. \"Na\" pia mimi hakika sikuwaamrisha jambo fulani, kisha nikawahalifu kwenda kinyume nalo. Bali \"nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waislamu;\" basi mimi ndiye wa kwanza kuingia na wa kwanza kufanya kile nilichowaamrisha."},{"id":1991,"sura":10,"from_aya":73,"to_aya":73,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{73} \"Lakini wakamkadhibisha\" baada ya kuwalingania usiku na mchana, kwa siri na hadharani, lakini kulingania kwake huko hakukuwazidishia isipokuwa kukimbia. \"Kwa hivyo tukamwokoa, pamoja na wale waliokuwa naye, katika jahazi,\" ambalo tulimwamrisha alijenge mbele ya macho yetu, na tukamwambia, \"Tanuri itakapofoka maji, basi beba humo kwa jozi dume na jike kutoka kwa kila aina, na ahali zako, isipokuwa wale ambao imekwisha tangulia kauli juu yao, na wale walioamini.\" Kwa hivyo, akafanya hivyo, basi Mwenyezi Mungu akaamrisha mbingu kumimina maji, na tukaipasua ardhi kwa chemchemi. Kwa hivyo, maji hayo yakakutana kwa jambo lililokwishapitishwa. Na tukambeba kwenye safina ya mbao na kamba, ikawa inakwenda mbele ya macho yetu. \"Na tukawafanya wao ndio waliobakia\" katika ardhi baada ya kuwaangamiza waliokadhibisha. Kisha Mwenyezi Mungu akabariki katika dhuria yake na akawafanya dhuria wake ndio wenye kubakia, na akawaeneza katika pande za ardhi, \"na tukawazamisha wale waliozikadhibisha Ishara zetu\" baada ya kubainisha huko na kusimamisha ushahidi. \"Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walioonywa.\" Nao ulikuwa maangamizo ya kuhizi, na laana ya kufuatana juu yao katika kila kizazi kitakachokuja baada yao. Hakitasikia kuwahusu isipokuwa lawama tu, wala hakitaona isipokuwa shutuma na kashfa. Basi na wajitahadhari hawa wanaokadhibisha yasije yakawapata yale yaliyowapata wale kaumu waliokadhibisha ya maangamizo, hizaya, na adhabu."},{"id":1992,"sura":10,"from_aya":74,"to_aya":74,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"74.   Kisha baada yake tukawatuma Mitume kwa kaumu zao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini hawakuwa wenye kuyaamini wale waliyoyakanusha kabla yake. Hivyo ndivyo tunavyoziziba nyoyo za wavukao mipaka."},{"id":1993,"sura":10,"from_aya":74,"to_aya":74,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{74} Yaani, kisha baada ya Nuhu, amani iwe juu yake, tukawatuma \"Mitume kwa kaumu zao\" wanaokadhibisha, ili wawalinganie kwenye uwongofu, na wawaonye dhidi ya sababu za maangamizo, \"wakawajia kwa Ishara zilizo wazi.\" Yaani, kila Nabii aliunga mkono ulinganizi wake kwa ishara zinazoonyesha usahihi wa kile alichokuja nacho. \"Lakini hawakuwa wenye kuyaamini wale waliyoyakanusha kabla yake.\" Yaani, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaadhibu kwa maana alipowajia Mtume, wakaharakisha kumkadhibisha, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akazifunga nyoyo zao na akawazuia kati yao na kuamini baada ya kwamba walikuwa wanaweza hilo. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, \" Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao kama vile hawakuiamini mara ya kwanza.\" Na ndiyo maana akasema hapa: \"Hivyo ndivyo tunavyoziziba nyoyo za wavukao mipaka.\" Yaani, tunaziziba, basi haziingiwi na heri yoyote. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walizidhulumu nafsi zao wenyewe kwa kukataa kwao haki ilipowajia na kule kukadhibisha kwao kwa mwanzo."},{"id":1994,"sura":10,"from_aya":75,"to_aya":93,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"75. Kisha baada yao tukamtuma Musa na Haruni kwa Firauni na waheshimiwa wake, kwa Ishara zetu. Wakatakabari, na wakawa kaumu wahalifu. 76. Basi ilipowajia haki kutoka kwetu, walisema: Hakika huu ni uchawi ulio dhahiri. 77. Akasema Musa, \"Je, mnasema hivi juu ya haki ilipowajia? Je, huu ni uchawi? Na wachawi hawafanikiwi!\" 78. Wakasema: Je, umetujia ili utuachishe tuliyowakuta nayo baba zetu, na mpate nyinyi wawili ukubwa katika ardhi? Wala sisi hatuwaamini nyinyi. 79. Na Firauni akasema: Nileteeni kila mchawi ajuaye zaidi! 80. Basi walipokuja wachawi hao, Musa akawaambia: Vitupeni mnavyovitupa! 81. Basi walipotupa, Musa akasema, \"Mliyoleta ndiyo uchawi. Hakika Mwenyezi Mungu ataubatilisha. Hakika Mwenyezi Mungu hayatengenezi matendo\u00a0ya\u00a0waharibifu. 82. Na Mwenyezi Mungu huihakikisha haki kwa maneno yake, hata wakichukia wahalifu. 83. Basi hawakumwamini Musa isipokuwa baadhi ya vijana kutoka kwa kaumu yake, kwa kumwogopa Firauni na wakuu wao wasiwatese. Kwani hakika Firauni alikuwa jeuri katika ardhi. Na kwa yakini alikuwa miongoni mwa waliopita kiasi. 84. Na Musa alisema: Enyi kaumu yangu! Ikiwa nyinyi mmemwamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni Yeye, ikiwa nyinyi ni Waislamu. 85. Wakasema: Tunamtegemea Mwenyezi Mungu. Ewe Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye kutiwa majaribio na hao kaumu madhalimu. 86. Na utuokoe kwa rehema yako kutokana na kaumu hawa makafiri. 87.  Na tukamteremshia wahyi Musa na ndugu yake kuwa: Watengenezeeni majumba kaumu yenu katika Misri na zifanyeni nyumba zenu ndimo mahali mwa ibada, na msimamishe Swala, na wabashirie Waumini. 88. Na Musa akasema: Mola wetu Mlezi! Hakika wewe umempa Firauni na wakuu wake mapambo na mali katika uhai wa dunia. Hivyo wanapoteza watu kutoka kwa njia yako. Mola wetu Mlezi! Zifutilie mbali mali hizo na zifunge nyoyo zao, wasiamini mpaka waione adhabu chungu. 89. Mwenyezi Mungu akasema: Hakika maombi yenu yamekubaliwa. Basi nyookeni, wala msifuate njia ya wale wasiojua. 90.   Tukawavusha bahari Wana wa Israili, naye Firauni na askari wake wakawafuata kwa dhulma na uadui. Mpaka kuzama kulipomfikia, akasema: Nimeamini kuwa hakuna mungu isipokuwa yule ambaye walimwamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa Waislamu. 91. Je, sasa? Na ilhali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa waharibifu? 92. Leo basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa wale walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu. 93. Na hakika tuliwaandalia Wana wa Israili makao mema, na tukawaruzuku katika vitu vizuri. Nao hawakuhitalifiana mpaka ilipowafikia elimu. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Qiyama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana. "},{"id":1995,"sura":10,"from_aya":75,"to_aya":75,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{75} Yaani: Kisha tukatuma baada ya Mitume hao ambao Mwenyezi Mungu aliwatuma kwa kaumu waliokadhibisha, walioangamizwa \"Musa\" Ibn Imran, aliyezungumza moja kwa moja na Mwingi wa rehema, mmoja wa Mitume wenye azimio kubwa miongoni mwa Mitume, na mmoja wa wakubwa wanaoigwa,  walioteremshiwa sheria zilizo kuu na pana. \"Na\" tukamfanya pamoja naye nduguye \"Harun\" kuwa msaidizi. Na tukawatuma \"kwa Firauni na waheshimiwa wake;\" yaani, wakuu wa nchi yake na viongozi wao. Kwa sababu wengineo wote wanawafuata viongozi, \"kwa Ishara zetu,\" zinazoonyesha ukweli wa yale aliyokuja nayo ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na kukataza kuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. \"Wakatakabari\" juu yake kwa dhulumu tu na jeuri baada ya kuwa na yakini nayo. \"Na wakawa kaumu wahalifu;\" yaani, sifa yao ni kufanya uhalifu na kukadhibisha."},{"id":1996,"sura":10,"from_aya":76,"to_aya":76,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{76} \"Basi ilipowajia haki kutoka kwetu\" ambayo ndiyo aina kubwa zaidi ya haki na tukufu yake zaidi. Nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye shingo zote zilimnyenyekea kwa sababu ya ukuu wake. Naye ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote, anayewalea viumbe wake wote kwa neema mbalimbali. Basi ilipowajia haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia mkono wa Musa, wakaikataa na hawakuikubali, na wakasema, \"Hakika huu ni uchawi ulio dhahiri.\" Hawakutosheka - Mwenyezi Mungu awalaani - kupeana kwao mgongo wala kuikataa haki, mpaka walipoifanya kuwa batili ya batili zote, ambayo ni uchawi ambao uhakika wake ni kufichika na kugeuza jambo. Bali waliifanya kuwa uchawi ulio dhahiri, ilhali hiyo ndiyo haki iliyo dhahiri."},{"id":1997,"sura":10,"from_aya":77,"to_aya":77,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{77} Na kwa sababu ya hili, \"Musa akawaambia\" akiwakaripia juu ya kukataa kwao haki, ambayo haikatai isipokuwa aliye dhalimu zaidi ya watu wote, \"Je, mnasema hivi juu ya haki ilipowajia?\" Yaani, je mnasema kuwa ni uchawi ulio wazi? \"Je, huu ni uchawi?\" Yaani, angalieni sifa zake na yaliyomo. Na kwa kufanya hivyo tu, mtu anakuwa na yakini kwamba ni haki. \"Na wachawi hawafanikiwi!\" Si katika dunia wala katika Akhera. Basi angalieni ni nani atakuwa na mwisho mwema, na ni nani atafanikiwa, na kufaulu kutakuwa katika mikono ya nani? Na baada ya hayo, wakajua na ikamdhihirikia kila mtu kuwa Musa, amani iwe juu yake, ndiye aliyefanikiwa, na akafuzu katika dunia na akhera."},{"id":1998,"sura":10,"from_aya":78,"to_aya":78,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{78} \"Wakamwambia Musa wakiikataa kwa sababu alisema jambo lisilokanushwa: Umetujia ili utuzuie na tuliyowakuta nayo baba zetu. Yaani, umetujia ili utuepushe na yale tuliyowakuta nayo baba zetu, ya ushirikina na ibada isiyokuwa Mwenyezi Mungu, na utuamrishe tumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila mshirika yeyote. Basi wakayafanya maneno ya baba zao wapotofu kuwa ni udhuru wa kukanusha haki aliyowaletea Musa. Na kauli yake, Na wewe utakuwa na kiburi katika ardhi.\" Yaani, na mlitujia kuwa viongozi na kututoa katika ardhi zetu? Huku ni kuficha kwa upande wao na kukuza dhidi ya ujinga wao na uchochezi baina ya watu wao wa kawaida kuwa na uadui na Musa na wasimwamini. Hii haiwezi kutumika kama ushahidi na wale wanaojua ukweli na kupambanua baina ya mambo. Kwa maana, hoja haziwezi kukanushwa isipokuwa kwa hoja na ushahidi. Na ama yule anayeleta haki; alijibu kauli yake kwa mambo kama haya: Inaonyesha kutoweza kwa muuzaji wake kuja na kile kinachokanusha kauli ambayo mpinzani wake alikuja nayo. Kwa sababu kama alikuwa na hoja; angeitaja, wala asingelikimbilia kusema kwake: Ulikusudia hivi na hivi au ulimaanisha hivi na hivi, sawa sawa na alichosema na kusema juu ya dhamira ya mpinzani wake au uongo. ijapokuwa Musa, rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa ni kila mwenye kujua hali yake na anachokiitia; Alijua kwamba hakuwa na lengo la kuinuliwa duniani, bali lengo lake lilikuwa sawa na lengo la Mitume wenzake, kuwaongoza viumbe na kuwaongoza kwa yale ambayo yatawanufaisha. Lakini ukweli wa mambo ni kama walivyoieleza waliposema: \"Na sisi si wenye kuamini kwenu.\" Yaani, kiburi na ukaidi, si kwa sababu ya ubatili wa yale waliyoyaleta Musa na Harun, wala kwa sababu ya kuishuku, wala kwa maana nyingine isipokuwa dhulma, uchokozi, na kutaka ubora ambao walimtuhumu Musa na Harun."},{"id":1999,"sura":10,"from_aya":79,"to_aya":79,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{79} \"Na Firauni akasema;\" kwa kuipinga Haki aliyoileta Musa na kuwashinda watu wake: \"Nileteeni kila mchawi mjuzi.\" Yaani, mwenye ujuzi katika uchawi na aliyebobea katika hilo. Kwa hiyo akatuma katika miji ya Misri wale waliomletea kila aina ya waganga wa rangi na tabaka mbalimbali."},{"id":2000,"sura":10,"from_aya":80,"to_aya":80,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{80} \"Na walipokuja wachawi\" ili kumshinda Musa, \"Musa akawaambia: Tupeni mnachotupa.\" Yaani, chochote mtakacho, siwabainishii chochote, kwa sababu yeye ana uhakika wa ushindi wake, asiwajali wao na wanacholeta."},{"id":2001,"sura":10,"from_aya":81,"to_aya":81,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{81} \"Na walipotupa\" kamba zao na fimbo zao walikuwa kama nyoka wanaorukaruka. \"Musa akasema: Mliyoleta ndiyo uchawi.\" Yaani,  huu ni uchawi wa kweli, mkubwa, lakini pamoja na ukubwa wake \"Mwenyezi Mungu ataubatilisha. Mwenyezi Mungu hatengenezi kazi za waharibifu.\" Kwa kufanya hivyo wanataka ushindi wa uongo dhidi ya ukweli, na ni ufisadi gani mkubwa kuliko huu? Na vivyo hivyo, kila mfisadi hufanya kitendo, kudanganya, kupanga njama, au kudanganya. Kazi yake itabatilika na kupunguzwa, na ikiwa kazi yake itakuzwa wakati fulani; imehukumiwa kuporomoka na ni sawa.Ama warekebishaji, ambao matendo yao yamekusudiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, nao ni vitendo vyenye manufaa na njia zilizoamrishwa zifanywe; Mungu daima husahihisha, kukuza na kuendeleza matendo yao."},{"id":2002,"sura":10,"from_aya":82,"to_aya":82,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"82. Basi Musa akaitupa fimbo yake, ikayashika yote waliyokuwa wakiyatenda, na uchawi wao ukabatilika, na uongo wao ukatoweka. \"Na\" kwa hakika, \"Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kustahiki zaidi haki kwa maneno yake, ijapokuwa wakosefu wanachukia.\" Basi wakatolewa wachawi ilipowabainikia Haki, na Firauni akawatishia kuwasulubisha na kukatwa mikono na miguu; lakini hawakujali hilo, na walibaki imara katika imani yao."},{"id":2003,"sura":10,"from_aya":83,"to_aya":83,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"83. Na ama Firauni na wakuu wake na wafuasi wao, hakuamini hata mmoja wao, bali waliendelea na dhulma yao, na kwa ajili hiyo akasema: \"Na hakuamini yeyote katika Musa ila dhuria wa watu wake.\" Yaani, vijana wa Wana wa Israili waliosubiri kwa hofu, iliposimama Imani katika nyoyo zao, \"kwa kumwogopa Firauni na wakuu wao wasije wakawatia fitina\" na katika dini yao. \"Na hakika Firauni alikuwa na kiburi katika ardhi. Yaani, ana dhuluma na ubabe ndani yake. Ni kweli kwamba wanapaswa kuogopa unyama wake, \"na\" hasa \"kwamba alikuwa miongoni mwa wafujaji.\" Yaani, wale wanaoruka mipaka kwa uadui na uadui. Na hekima - na Mwenyezi Mungu ndiye Ajuaye zaidi - juu ya ukweli kwamba ni watoto tu wa watu wake waliomwamini Musa ni kwamba dhuria na vijana wanakubali zaidi haki na wepesi zaidi kuinyenyekea. Tofauti na mashekhe na wengineo waliolelewa katika ukafiri; kwa sababu ya imani potovu zilizobaki mioyoni mwao, wako mbali zaidi na ukweli kuliko wengine."},{"id":2004,"sura":10,"from_aya":84,"to_aya":84,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{84} \"Na Musa akasema\" akiwausia watu wake wawe na subira na kuwakumbusha yale wanayoweza kutafuta msaada katika hayo; akasema: \"Enyi watu wangu, ikiwa nyinyi mmemwamini Mwenyezi Mungu,\" basi timizeni wajibu wa Imani na kwa Mwenyezi Mungu \"Mtegemee ikiwa nyinyi ni Waislamu.\" Yaani, walimtegemea, wakamwendea, na wakamwomba msaada."},{"id":2005,"sura":10,"from_aya":85,"to_aya":85,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{85} \"Na wakasema,\" wakiyazingatia hayo, \"Sisi tunamtegemea Mwenyezi Mungu, na Mola wetu Mlezi, usitufanye kuwa mtihani kwa watu madhalimu.\" Yaani, usiwape mamlaka juu yetu, wasije wakatutia majaribuni au wakatushinda, wakajaribiwa kwa hayo, na wakasema: Lau wangelikuwa katika Haki wasingelishindwa."},{"id":2006,"sura":10,"from_aya":86,"to_aya":86,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{86} \"Na utuokoe kwa rehema yako na kaumu makafiri\" ili tuepuke na shari yao na tushike Dini yetu kwa njia ambayo tutaziweka sheria zake, na kuzidhihirisha bila upinzani wala ubishi."},{"id":2007,"sura":10,"from_aya":87,"to_aya":87,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{87} \"Na tulimpelekea wahyi Musa na nduguye\" lilipofika jambo gumu kwa kaumu yao kutoka kwa Firauni na kaumu yake, na wakawa na bidii ya kuwatia katika dini yao, \"kwamba nyinyi mkae kwa ajili ya watu wenu katika Misri majumbani.\" Yaani, waamuru wajifanyie nyumba ili wajifiche, \"na kuzifanya nyumba zako zielekee uelekeo.\" Yaani, fanya iwe mahali unaposali kwa vile huwezi kufanya maombi katika makanisa na maduka ya umma. \"Na simamisheni Sala,\" kwani hiyo ni usaidizi katika kila jambo. \"Na wabashirie Waumini\" ushindi na usaidizi na udhihirisho wa Dini yao. Pamoja na shida kuna urahisi, pamoja na shida kuna urahisi. Wakati dhiki ikawa kali na jambo likawa gumu; Mungu ambariki na kumzidishia."},{"id":2008,"sura":10,"from_aya":88,"to_aya":88,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{88} Na Musa alipouona ukatili na upotovu wa Firauni na wakuu wake; akawaombea, na Harun akaamini dua yake, na akasema: \"Mola wetu Mlezi, hakika umempa Firauni na wasaidizi wake pambo\" na wanajipamba kwa aina mbali mbali za mapambo, na nguo, na nyumba zilizopambwa, na merikebu za kifahari, na watumishi, \"na mali\" kubwa \"katika maisha ya dunia, Mola wetu Mlezi, wasije wakapotea njia yako.\" Yaani, hawakuomba msaada katika mali zao ila kukupoteza katika Njia yako, basi wanapoteza na kupotea. \"Mola wetu Mlezi wafute mali zao}; Yaani, aliiangamiza kwa ajili yao, ima kwa kuiharibu au kwa kuigeuza mawe bila ya manufaa yoyote, \"na akazifanya nyoyo zao kuwa ngumu.\" Yaani, pimeni, \"basi hawataamini mpaka waione adhabu iumizayo.\" Amesema kwa kuwakasirikia kwa sababu ya kuthubutu kuvuka haramu ya Mwenyezi Mungu na wakawaharibu waja wa Mwenyezi Mungu na wakaiacha njia yake, na wakakamilisha ujuzi wake juu ya Mola wake Mlezi kwamba Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa yale waliyoyafanya kwa kuwafungia mlango wa imani."},{"id":2009,"sura":10,"from_aya":89,"to_aya":89,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{89} \"Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Imejibiwa dua yenu.\" Huu ni ushahidi kwamba Musa anaomba dua, na Harun anaiamini dua yake, na kwamba mwenye kuamini ni mshirika na mwenye kuomba katika dua hiyo. \"Basi simameni\" katika Dini yenu, na dumuni katika wito wenu, wala msifuate njia ya wasiojua.\" Yaani, Msifuate njia ya wajinga waliopotea, wanaokengeuka na njia iliyonyooka, na kufuata njia za Jahannamu."},{"id":2010,"sura":10,"from_aya":90,"to_aya":90,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{90} Mwenyezi Mungu akamwamuru Musa aende pamoja na Wana wa Israili usiku, na akamwambia kwamba watamfuata, na Firauni akapeleka makundi mijini akisema: Hakika hawa - yaani, Musa na watu wake - ni kikundi kidogo. Na hakika wao wana hasira na sisi. Sote tuko makini. Basi akawakusanya majeshi wake wa mbali wao na wa karibu wao, na akawafuata pamoja na askari wake licha ya maadui. Yaani, walitoka wakifanya uadui juu ya Musa na watu wake na waasi katika nchi, na upotofu ulipozidi, na dhambi ikawa kali, basi subiri adhabu. \"Tukawavusha wana wa Israili baharini,\" na hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa wahyi Musa alipofika baharini ili aipige kwa fimbo yake, basi akaipiga, na njia kumi na mbili zikapasuka, na wana wa Israeli wakaichukua; na akamwingiza Firauni na askari wao nyuma yao. Basi Musa na watu wake walipokwisha kuiacha bahari, na Firauni na askari wake wakaingia humo. Mungu aliiamuru bahari imwangukie Farao na askari wake, na kuwazamisha huku wana wa Israeli wakiwa wanatazama, mpaka Farao alipogundua kuzama huko na kuwa na uhakika wa kuangamizwa kwake. \"Akasema, \u201cNimeamini kwamba hakuna mungu ila yule ambaye wana wa Israili walimwamini.\" Naye ni Mungu, Mungu wa haki, ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye, \"na mimi ni miongoni mwa Waislamu.\" Yaani, wale waliosilimu katika Dini ya Mwenyezi Mungu na aliyoyaleta Musa."},{"id":2011,"sura":10,"from_aya":91,"to_aya":91,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{91} Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, akieleza kwamba imani hii katika hali hii haina manufaa kwake: \"Sasa\" nyinyi mmemwamini na mnamkiri Mtume wa Mwenyezi Mungu, \"na ukaasi kabla.\" Yaani umekuwa mkubwa katika dhambi, ukafiri na ukanushaji, \"na umekuwa miongoni mwa waharibifu;\" basi imani haitakufaa kama ilivyo desturi ya Mwenyezi Mungu kwamba ikiwa makafiri wataifikia hali hiyo ya faradhi, imani haitawafaa; Kwa sababu, imani yao imekuwa imani inayoonekana. Kama imani katika Ufufuo, na chenye manufaa ni imani katika ghaibu."},{"id":2012,"sura":10,"from_aya":92,"to_aya":92,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{92} \"Leo basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa wale walio nyuma yako.\" Wakasema wafasiri: Hakina Wana wa Israili kwa sababu ya hofu kubwa mioyoni mwao itokayo kwa Firauni, hawakuamini kumzamisha, na wakawa na shaka, basi Mwenyezi Mungu akaiamuru bahari imtupe kwenye jabali refu mwili wake; ili kuwa mfano na ishara kwao. \"Na watu wengi wameghafilika na Ishara zetu.\" Basi wanapita juu yao na hurudiwa, basi hawanufaiki nazo. Kwa sababu hawakubali, bali wale walio na akili na moyo wa sasa; kwani anaona miongoni mwa ishara za Mwenyezi Mungu ushahidi mkubwa wa ukweli wa yale waliyoambiwa Mitume."},{"id":2013,"sura":10,"from_aya":93,"to_aya":93,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{93} \"Na kwa yakini tuliwaweka Wana wa Israili katika makazi ya kweli.\" Yaani, Mwenyezi Mungu aliwateremsha na akawaweka katika maskani ya kaumu ya Firauni, na akawarithisha ardhi yao na majumba yao, \"na tukawaruzuku vitu vizuri\" miongoni mwa vyakula na vinywaji na vitu vingine. Hawakukhitalifiana\" katika Haki \"mpaka ilipowajia elimu\" ambayo iliwalazimu kukusanyika na kuungana, lakini baadhi yao wakadhulumu wao kwa wao, na ikawa kwa wengi. Baadhi yao wana utambulisho na makusudio yanayopingana na Haki, na kutoelewana kumetokea baina yao. \"Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyohitalifiana} kwa hukumu yake ya uadilifu inayotokana na ujuzi Wake na uweza Wake. Huu ndio ugonjwa unaofichuliwa kwa watu wa dini ya haki, ambayo ni kwamba Shetani akiwafanya washindwe kumtii kwa kuacha dini kabisa, anatafuta kuwasumbua na kuwajengea uadui na chuki, na hitilafu inayopelekea hilo hutokea, na kisha upotofu wa baadhi yao na uadui wao kwa wao kwa unasababisha kile ambacho ni mboni ya jicho. Ikiwa Mola wao ni Mmoja, basi Mtume wao ni mmoja, na Dini yao ni moja, na maslahi yao yanaafikiana. Basi, ni kwa sababu gani wanahitalifiana ambayo ingewafarakanisha, kutawanya mambo yao, kuvunja mafungamano na mfumo wao, ili baadhi ya maslahi yao ya kidini na ya kidunia yapotee, na baadhi ya dini zao wafe kwa sababu hiyo? Basi tunakuomba, Ewe Mola, uwafanyie wema waja wako waaminifu, uwaunganishe tena, uwatengenezee mpasuko wao, na uwarudishe walio karibu nao, ewe Mwenye Utukufu na Heshima!"},{"id":2014,"sura":10,"from_aya":94,"to_aya":95,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"94. Na ikiwa uko katika shaka juu yale tuliyokuteremshia, basi waulize wale wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe kabisa miongoni mwa wenye shaka. 95. Na kabisa usiwe miongoni mwa wale waliozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, ukawa katika waliohasiri. "},{"id":2015,"sura":10,"from_aya":94,"to_aya":94,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{94} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: -\"Na ikiwa uko katika shaka juu yale tuliyokuteremshia\" je ni sahihi au si sahihi, \"basi waulize wale wasomao Kitabu kabla yako.\" Yaani, waulize watu wa Vitabu waadilifu, na wanazuoni wenye msingi madhubuti. Kwa maana, wao hakika watakukiria ukweli wa yale ambayo yalijulisha na kuafikiana kwake na yale waliyo nayo. Na ikisemwa: Hakika Wengi katika Watu wa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Manasara, na pengine wengi wao walikuwa wamemkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wakampinga, na wakaukataa wito wake. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwamrisha Mtume wake awafanye kuwa mashahidi, na akaufanya ushahidi wao kuwa hoja juu ya yale aliyokuja nayo, na ushahidi juu ya usahihi wake. Basi linawezaje kuwa hivyo? Jibu la hili ni kwa namna mbalimbali: Miongoni mwake ni kwamba, ushahidi unapofungamanishwa na kundi au watu wa dhehebu fulani au mji fulani na mfano wao, basi huo unajumuisha watu waadilifu wakweli miongoni mwao. Na ama wasiokuwa wao, hata kama wao ndio wengi miongoni mwao, basi hao hawazingatiwi. Kwa maana, ushahidi umejengeka juu ya uadilifu na ukweli, na hilo tayari lilikwisha patikana katika kuamini kwa wengi wa marabi wao wamuabuduo Mola wao Mlezi tu, kama vile 'Abdullah bin Salam na wenzake, na wengi miongoni mwa wale waliosilimu katika wakati wa Nabii \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake \u2013 na makhalifa wake baada yao. Na miongoni mwake ni kwamba, Ushahidi wa Watu wa Kitabu kwa Mtume umejengeka juu ya kitabu chao, Taurati, ambayo wao wanajinasibisha nayo. Basi ikiwa kuna yale yanayoafikiana na Qur\u2019an katika Taurati, na yanaisadikisha, na yanaishuhudia kuwa ni ukweli, basi hata kama wataafikiana tangu wa mwanzo wao hadi wa mwisho wao juu ya kulikataa hilo, basi hilo halitatia doa katika yale aliyokuja nayo Mtume. Na miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwamrisha Mtume wake kutafuta ushahidi wa Watu wa Kitabu juu ya usahihi wa yale yaliyomjia, na akalidhihirisha hilo na akaliweka hadharani mbele ya mashahidi hao. Na inavyojulikana ni kwamba wengi wao walikuwa miongoni mwa watu wenye pupa zaidi juu ya kubatilisha wito wa Mtume Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - na lau wangelikuwa na cha kukanusha yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu, basi wangelikifichua, na kukidhihirisha, na kukibainisha. Lakini kwa kuwa hakukuwa na lolote kati ya hayo lililotokea, basi kukawa kutopinga kwa wapinzani, na maadui, na kukiri kwa anayepaswa kujibu, ni miongoni mwa ushahidi mkubwa zaidi juu ya usahihi na Qur-ani hii na ukweli wake. Na miongoni mwake ni kwamba, si wengi wa Watu wa Kitabu waliokataa wito wa Mtume, bali wengi wao waliuitikia na kuufuata kwa kujitolea na kwa hiari. Kwa maana, Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alitumwa kama Mtume ilhali wengi wa watu wa ardhi wenye dini ni Watu wa Kitabu, na Dini yake haikudumu kwa muda mrefu mpaka wakaifuata watu wengi wa Shaam, Misri, Iraqi na nchi jirani ambazo ndiyo makao ya Dini ya Watu wa Kitabu. Na wala hawakubakia isipokuwa watu wa uongozi tu ambao walipendelea uongozi wao kuliko haki na wale waliowafuata miongoni mwa watu wa kawaida wasiojua, wale waliowafuata dini yao kwa jina tu, si kwa kimaana, kama vile Wafrank, ambao ukweli wao ni kwamba wao ni watu wasiopenda dini ambao wamezikana dini zote za Mitume, bali wamejihusisha na dini ya Kikristo ili kuendeleza ufalme wao na kuficha uwongo wao. Hii pia inajulikana na wale wanaojua hali zao wazi na zinazoonekana. Na kauli yake: \"Kwa yakini imekwisha kujia haki,\" yaani, ambayo haina shaka yoyote ndani yake kwa namna yoyote ile, \"kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe kabisa miongoni mwa wenye shaka.\" Kama kauli yake Yeye Mtukufu, \"Kitabu kilichoteremshwa kwako, basi isiwe dhiki yoyote katika kifua chako kwa sababu yake.\""},{"id":2016,"sura":10,"from_aya":95,"to_aya":95,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{95} \"Na kabisa usiwe miongoni mwa wale waliozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, ukawa katika waliohasiri.\" Na muhtasari wa haya ni kwamba Mwenyezi Mungu alikataza mambo mawili: kuitilia shaka Qur-ani hii, na kusitasita juu yake. Na baya zaidi kuliko hayo ni kuikadhibisha. Nayo ndiyo ishara za wazi wazi za Mwenyezi Mungu, ambazo hazikubali kukadhibishwa kwa namna yoyote ile. Na alifungamanisha na hilo kupata hasara. Nayo ni kutokapa faida yoyote. Na hilo linakuwa kwa kukosa malipo katika dunia hii na Akhera, na kufikiwa na adhabu katika dunia hii na Akhera. Na kukataza kitu ni kuamrisha kinyume chake. Kwa hivyo inakuwa hii ni kuamrisha kuisadiki Qurani kikamilifu, na kuutuliza moyo juu yake, na kuielekea kwa kujifunza na kuitendea kazi. Na kwa hayo mja anakuwa miongoni mwa waliofaidika, ambao walipata mambo matukufu zaidi yatafutwayo, na matashi bora zaidi, na sifa (fadhila) kamili zaidi, na kuepushwa na hasara."},{"id":2017,"sura":10,"from_aya":96,"to_aya":97,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"96. Hakika wale ambao neno la Mola wako Mlezi limekwisha thibitika juu yao, hawataamini. 97. Hata kama itawajia kila Ishara, mpaka waione adhabu iliyo chungu. "},{"id":2018,"sura":10,"from_aya":96,"to_aya":97,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{96 - 97} Yeye Mtukufu Anasema, \"Hakika wale ambao neno la Mola wako Mlezi limekwisha thibitika juu yao.\" Yaani, wao ni miongoni mwa wale waliopotea, walioangamia, watu wa Motoni, lazima wafikie yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwajalia na akawahukumia. Kwa hivyo, hawataamini hata kama itawajia kila ishara. Na ishara haziwazidishii isipokuwa kuvuka mipaka na upotofu ju ya upotofu wao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali walizidhulumu nafsi zao wenyewe kwa kuikataa kwao haki ilipowajia mara ya kwanza. Basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa kuziziba nyoyo zao, kusikia kwao na kuona kwao, ili wasiamini mpaka waione adhabu chungu waliyoahidiwa. Na hapo watajua kwa yakini kabisa kwamba waliyo juu yake ndiyo upotofu, na kwamba yale waliyowajia nayo Mitume ndiyo haki. Lakini yatakuwa katika wakati ambao imani yao haiwezi kuwafaidi kitu. Siku hiyo haitawafaa wale waliodhulumu  udhuru wao, wala haitatakiwa toba yao. Ama ishara, hizo zinamfaa mwenye moyo au aliyetega sikio ilhali yupo anashuhudia."},{"id":2019,"sura":10,"from_aya":98,"to_aya":98,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"98. Basi kwa nini hakikuwepo kijiji kilichoamini, kwa hivyo Imani yake ikakifaa, isipokuwa kaumu ya Yunus? Walipoamini, tukawaondolea adhabu ya hizaya katika uhai wa dunia, na tukawastarehesha kwa muda."},{"id":2020,"sura":10,"from_aya":98,"to_aya":98,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{98} Yeye Mtukufu Anasema: \"Basi kwa nini hakikuwepo kijiji\" miongoni mwa vijiji vilivyokadhibisha, \"kilichoamini\" wakati kilipoiona adhabu, \"kwa hivyo Imani yake ikakifaa.\" Yaani, hakuna hata mmoja wao aliyefaidika na imani yake wakati alipoiona adhabu, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema hivi karibuni kuhusu Firauni, aliposema, \"Nimeamini kuwa hakuna mungu isipokuwa yule ambaye walimwamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.\" Lakini akaambiwa, \"Je, sasa? Na ilhali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa waharibifu\" na kama alivyosema Yeye Mtukufu \"basi walipoiona adhabu yetu, wakasema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni wa pekee, na tunaikataa miungu tuliyokuwa tukiishirikisha naye. Lakini imani yao haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati ambao walipokwisha iona adhabu yetu. Hii ndiyo desturi ya Mwenyezi Mungu ambayo ilikwishatangulia kwa waja wake.\" Na Yeye Mtukufu akasema: \u201cMpaka yanapomjia mmoja wao mauti, anasema, \"Mola wangu Mlezi! Nirudishe, ili nitende mema sasa badala ya yale niliyoyaacha.\" Wapi!\" Na hekima katika haya iko wazi. Kwani Imani ya kulazimishwa si imani ya kweli. Kwa maana lau yataondolewa kwake adhabu hiyo na jambo ambalo lilimlazimisha kuamini,  basi angerudi katika ukafiri. Na kauli yake: \"isipokuwa kaumu ya Yunus? Walipoamini, tukawaondolea adhabu ya hizaya katika uhai wa dunia, na tukawastarehesha kwa muda.\" Basi wao wameondolewa katika ujumla uliotangulia, na lazima hilo ni kwa sababu ya hekima kutoka kwa ajuaye zaidi mambo ya ghaibu na yanayoonekana ambayo haijatufikia na wala ufahamu wetu haukuifikia. Amesema Yeye Mtukufu: \"Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume...\" mpaka aliposema: \"Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi. Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.\" Na pengine hekima katika hilo ni kwamba wasiokuwa wao miongoni mwa wale walioangamizwa lau wangerudishwa, basi wangerejea katika yale waliyokatazwa. Na ama kaumu ya Yunus, hao Mwenyezi Mungu alijua zaidi kwamba imani yao itaendelea, bali iliendelea kihalisi, na wakadumu juu yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi."},{"id":2021,"sura":10,"from_aya":99,"to_aya":100,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"99. Na angelitaka Mola wako Mlezi, wangeliamini walio katika ardhi wote kwa pamoja.  Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini? 100. Na haiwi kwa nafsi kuamini isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu juu ya wale wasiotumia akili zao. "},{"id":2022,"sura":10,"from_aya":99,"to_aya":99,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{99} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - \"Na angelitaka Mola wako Mlezi, wangeliamini walio katika ardhi wote kwa pamoja\" kwa kuwafunulia wahyi wa kuamini na kuongoza  mioyo yao kwenye uchamungu. Kwani uwezo wake unaweza hilo, lakini hekima yake ilihitaji kwamba baadhi yao wawe waumini na baadhi yao wawe makafiri. \"Wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?\" Yaani, huwezi kufanya hivyo, na wala haliko katika uwezo wako wala uwezo wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu juu ya lolote katika hayo."},{"id":2023,"sura":10,"from_aya":100,"to_aya":100,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{100} \"Na haiwi kwa nafsi kuamini isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu\" kwa kutaka kwake, na mapenzi yake, na idhini yake ya kimajaliwa ya kisheria. Kwa hivyo, yeyote yule miongoni mwa viumbe anayelifailia hilo, imani yake inatakasika, na anamuwezesha na kumuongoza \"naye hujaalia adhabu.\" Yaani, uovu na upotofu \"juu ya wale wasiotumia akili\" kuhusiana na Mwenyezi Mungu na maamrisho yake na makatazo yake, wala hawazingatii nasaha zake na mawaidha yake."},{"id":2024,"sura":10,"from_aya":101,"to_aya":103,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"101. Sema: Angalieni yaliyo katika mbingu na ardhi! Na Ishara zote na maonyo hayawafai kitu kaumu wasioamini. 102. Basi, je, wanangojea jingine isipokuwa kama yale yaliyotokea siku za watu waliopita kabla yao? Sema: Ngojeni! Nami ni pamoja nanyi katika wanaongoja. 103. Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na wale walioamini. Ndio kama hivyo, inatustahiki kuwaokoa Waumini. "},{"id":2025,"sura":10,"from_aya":101,"to_aya":101,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{101} Yeye Mtukufu anawaita waja wake watazame vilivyo katika mbingu na ardhi, na kinachomaanishwa na hayo ni kutazama kwa kufikiri, na kuzingatia, na kutafakari yaliyo ndani yake, na yaliyojumuisha, na kutaka kubainishiwa. Kwani, katika hayo zipo Ishara kwa kaumu wanaoamini, na mazingatio kwa kaumu wenye yakini, zenye kuonyesha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye peke yake wa kuabudiwa, Msifiwa, Mwenye utukufu na ukarimu, na majina na sifa kuu. \"Na Ishara zote na maonyo hayawafai kitu kaumu wasioamini.\" Kwa maana, wao hawafaidiki na ishara, kwa sababu ya kupeana kwao mgongo, na ukaidi wao."},{"id":2026,"sura":10,"from_aya":102,"to_aya":103,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{102 - 103} \"Basi, je, wanangojea jingine isipokuwa kama yale yaliyotokea siku za watu waliopita kabla yao?\" Yaani, Je, wanangoja hawa wasioamini ishara za Mwenyezi Mungu baada ya kuwa kwake wazi isipokuwa mfano wa siku za wale waliopita kabla yao? Yaani, kuangamizwa na kuadhibiwa. Kwa maana, walifanya kama kufanya kuwao, na desturi ya mwenyezi mungu inapita katika wa mwanzo na mwisho. \"Sema: Ngojeni! Nami ni pamoja nanyi katika wanaongoja.\" Basi Mtakujajua ni nani atakuwa na mwisho mzuri na kuokoka katika dunia na Akhera. Na hayo si isipokuwa kwa Mitume na wafuasi wao tu, na ndio maana akasema: \"Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na wale walioamini\" kutokana na machukizo ya dunia na Akhera na shida zake. \"Ndio kama hivyo, inatustahiki\" na tumejiwajibisha juu ya nafsi yetu \"kuwaokoa Waumini.\" Kwa maana, hakika Mwenyezi Mungu huwakinga wale walioamini. Kwani kulingana na imani aliyo nayo mja, ndiyo  anapata kuokoka kutokana na machukizo."},{"id":2027,"sura":10,"from_aya":104,"to_aya":106,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"104. Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mko katika shaka juu ya Dini yangu, basi mimi siwaabudu mnaowaabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu. Lakini mimi namwabudu Mwenyezi Mungu anayewafisha. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waumini. 105. Na kwamba uuelekeze uso wako kwenye Dini ya kweli, kwa unyoofu wala kamwe usiwe katika washirikina. 106. Na wala usiombe badala ya Mwenyezi Mungu wale ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru. Na ukifanya hivyo, basi wewe hakika ni  miongoni mwa madhalimu. "},{"id":2028,"sura":10,"from_aya":104,"to_aya":104,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{104} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - bwana wa Mitume wote, na imamu wa wachamungu, na mbora wa wenye yakini; \"Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mko katika shaka juu ya Dini yangu,\" yaani, katika shaka na kuchanganyikiwa; basi mimi hakika siko katika shaka nayo, lakini nina elimu ya yakini kwamba ndiyo haki, na kwamba hao mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu ni batili, na nina ushahidi ulio wazi na hoja zinazong'aa juu ya hilo. Na ndiyo maana akasema: \"Basi mimi siwaabudu mnaowaabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu\" miongoni mwa wenza, na masanamu na wengineo. Kwa sababu hao hawaumbi, wala hawaruzuku, wala hawaendeshi kitu katika mambo, bali hao wameumbwa, wametiishwa, hawana chochote kinachohitaji waabudiwe. \"Lakini mimi namwabudu Mwenyezi Mungu anayewafisha.\" Yaani, yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye aliwaumba, na Yeye ndiye atawafisha, kisha atawafufua ili awalipe kwa matendo yenu. Kwani Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa, na kuswali kwa ajili yake, [na kumnyenyekea] na kusujudiwa. \"Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waumini.\""},{"id":2029,"sura":10,"from_aya":105,"to_aya":105,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{105} {Na kwamba uuelekeze uso wako kwenye Dini kwa unyoofu.\" Yaani,  mkusudie Mwenyezi Mungu tu katika matendo yako ya dhahiri na ya ndani, na usimamishe sheria zote za dini, \"kwa unyoofu;\" yaani, kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu na kukipa mgongo kinginecho. \"Wala kamwe usiwe miongoni mwa washirikina,\" si katika hali yao wala usiwe pamoja nao."},{"id":2030,"sura":10,"from_aya":106,"to_aya":106,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{106} \"Wala usiombe badala ya Mwenyezi Mungu wale ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru.\" Na hii sifa ya kila kiumbe kwamba hakinufaishi wala hakidhuru, bali mwenye kunufaisha na kudhuru ni Mwenyeezi Mungu Mtukufu. \"Na ukifanya hivyo;\" yaani, ukiomba badala ya Mwenyezi Mungu wale wasiokufaa wala kukudhuru; \"basi hakika wewe\" ni miongoni mwa \"madhalimu;\u201d yaani, wale wanaojidhuru nafsi zao kwa kuziangamiza. \nNa dhuluma hii ndiyo ushirikina, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Hakika ushirikina ni dhuluma iliyo kubwa.\" Na ikiwa mbora wa viumbe akiomba mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu,  anakuwa miongoni mwa madhalimu na washirikina, basi vipi kuhusu wengineo?"},{"id":2031,"sura":10,"from_aya":107,"to_aya":107,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"107. Na Mwenyezi Mungu akikugusa kwa madhara, basi hakuna wa kukuondolea isipokuwa Yeye. Na akikutakia heri, basi hakuna wa kurudisha fadhila yake. Humsibu kwayo amtakaye katika waja wake, na Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."},{"id":2032,"sura":10,"from_aya":107,"to_aya":107,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{107} Huu ni katika ushahidi mkubwa zaidi kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa. Kwani yeye tu ndiye mwenye kunufaisha, mwenye kudhuru, mwenye kupeana, mwenye kunyima, ambaye anapogusa kwa madhara kama vile umaskini, na maradhi na mengineyo, \"basi hakuna wa kukuondolea isipokuwa Yeye\" kwa sababu lau kuwa viumbe vingekusanyika ili kunufaisha kwa kitu fulani, basi havingenufaisha isipokuwa tu kwa kile alichokiandika Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa wangekusanyika ili kumdhuru yeyote, basi Hawangeweza chochote katika kumdhuru ikiwa [Mwenyezi Mungu] hakutaka hilo. Na ndio maana akasema: \"Na akikutakia heri, basi hakuna wa kurudisha fadhila yake\" Yaani hawezi yeyote miongoni mwa viumbe kurudisha fadhila yake na wema wake, kama alivyosema Yeye Mtukufu, \"Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu, basi hakuna wa kuizuia. Na anayoizuia, hakuna wa kuiachilia isipokuwa Yeye.\" \"Humsibu kwayo amtakaye katika waja wake\" yaani humchagua kumpa rehema zake amtakaye miongoni mwa viumbe vyake, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa. {Na Yeye ni Mwenye kusamehe\" makosa yote, ambaye humuwezesha mja wake kufikia sababu za maghufira, kisha mja anapozifanya, Mwenyezi Mungu humsamehe madhambi yake yote, makubwa yake na madogo yake. {Mwenye kurehemu} ambaye rehema yake imeenea kwa kila kitu, na ukarimu wake ulikifikia kila kitu kilichopo kwa namna kwamba hawawezi kujitosheleza bila ya wema wake kwa muda wa kupepesa jicho. Basi mja anapojua kwa ushahidi wa kukata kwamba Mwenyezi Mungu ndiye peke yake mwenye kuneemesha, na kuondoa adhabu, na kupeana mazuri, na kuondoa mabaya na balaa, na kwamba hakuna yeyote miongoni mwa viumbe aliye na chochote katika haya mkononi mwake isipokuwa yale aliyoyafanyisha Mwenyezi Mungu kupitia mikononi mwake. Basi atakuwa na yakini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa haki, na ya kwamba wale wanaowaomba badala yake ndio wa batili, na ndiyo maana alipobainisha ushahidi ulio wazi, akasema baada yake:"},{"id":2033,"sura":10,"from_aya":108,"to_aya":109,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"108. Sema: Enyi watu! Haki imekwisha wajia kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo, anayeongoka, basi anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anayepotea, basi anapotea kwa hasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu. 109. Na wewe fuata yale yanayofunuliwa kwako kwa wahyi. Na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na Yeye ndiye mbora wa mahakimu. "},{"id":2034,"sura":10,"from_aya":108,"to_aya":108,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{108} Yaani, \"Sema\": Ewe Mtume, wakati ushahidi ulipobainika, \"Enyi watu! Haki imekwisha wajia kutoka kwa Mola wenu Mlezi.\" Yaani, habari ya ukweli inayoungwa mkono na ushahidi, ambayo haina shaka yoyote juu yake kwa namna yoyote ile. Nayo imewafikia kutoka kwa Mola wenu Mlezi ambaye katika malezi yake makubwa zaidi juu yenu ni kwamba aliwateremshia hii Qur'ani ambayo ndani yake kuna ufafanuzi wa kila kitu, na ambayo ndani yake kuna aina mbalimbali za hukumu, na matakwa ya kiungu, na tabia zenye kuridhisha ambayo yote hayo yana malezi makubwa zaidi kwenu. Kwani, uwongofu umeshabainika kutokana na upotofu, na hakuna aliyesalia na shaka yoyote. \"Kwa hivyo, anayeongoka\" kwa uwongofu wa Mwenyezi Mungu, kwa kujua haki, na akaifahamu, na akaipendelea juu ya mengineyo, basi ni kwa faida ya nafsi yake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu si mhitaji wa waja wake, bali matunda ya matendo yao yanawarudiwa wao wenyewe. \"Na anayepotea\" mbali na uwongofu, kwa kupeana mgongo kujua haki au kuifanyia kazi, \"basi anapotea kwa hasara ya nafsi yake\" wala hamdhuru Mwenyezi Mungu chochote, basi hadhuru isipokuwa nafsi yake mwenyewe.  \"Na mimi si mwakilishi juu yenu.\" Basi nikawahifadhia matendo yenu na kuwahesabu juu yake; bali mimi kwenu ni mwonyaji aliye wazi, naye Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi juu yenu. Basi jiangalieni nafsi zenu maadamu bado mko katika kipindi cha kupewa muhula."},{"id":2035,"sura":10,"from_aya":109,"to_aya":109,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{109} {Na fuata} Ewe Mtume, yale yaliyoteremshwa kwako kwa matendo na kwa kujifunza, na katika hali zote, na katika kulingania kwayo \"{Na vimulia} juu ya hayo. Kwani hii ndiyo aina ya juu zaidi ya uvumilivu, na hakika mwisho wake ni wa kusifiwa. Kwa hivyo usiwe mvivu wala usilalamike. bali dumu juu ya hayo na usimame imara, {mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu} baina yako na yule anayekukadhibisha. {na Yeye ndiye mbora wa mahakimu\" Kwa maana hekima yake inajumuisha uadilifu kamili na kufanya haki ambayo unasifiwa. Naye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alitekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na akasimama imara kwenye njia iliyonyooka, mpaka Mwenyezi Mungu akaidhihirisha dini yake kuwa juu ya dini zote, na akamnusuru dhidi ya maadui zake kwa upanga na mkuki baada ya Mwenyezi Mungu kumnusuru kwa hoja na ushindi. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, kama unavyostahiki utukufu wake, ukuu wake, na ukamilifu wake, na upana wa wema wake."},{"id":2036,"sura":10,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imetimia Tafsiri ya Surat Yunus, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote."},{"id":2037,"sura":10,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}