{"result":[{"id":2190,"sura":12,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0642\u062f\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0645\u062c\u0644\u062f","text":"Juzuu ya nne ya Taysir Al-Karim Ar-Rahman fi Tafsir Kalaam Ar-Rabb Al-Mannaan (Wepesishaji wa Mkarimu, Mwingi wa rehema, katika kutafsiri maneno ya Mola Mlezi, Mtoaji kwa wingi). cha mwandishi wake masikini kwa Mola wake Mlezi, Abdur-Rahman bin Nasir bin Abdullah As-Saadi, Mwenyezi Mungu amsamehe yeye na wazazi wake na Waislamu wote, Amin."},{"id":2191,"sura":12,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Yusuf bin Yaaqub, rehema na amani ziwe juu yao wote wawili"},{"id":2192,"sura":12,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Nayo iliteremka Makka"},{"id":2193,"sura":12,"from_aya":1,"to_aya":3,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Alif Lam Raa. Hizi ni Aya za Kitabu kinachobainisha. 2. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia. 3. Sisi tunasimulia simulizi nzuri zaidi kwa kukufunulia Qur-ani hii. Na ijapokuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa walioghafilika. "},{"id":2194,"sura":12,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Yeye Mtukufu anajulisha kuwa Aya za Qur-ani ni \u201cishara za Kitabu kinachobainisha.\u201d Yaani kilicho baninifu, kilicho wazi katika maneno yake, na maana zake."},{"id":2195,"sura":12,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Miongoni mwa kubainisha kwake na kuweka kwake wazi ni kwamba aliiteremsha kwa lugha ya Kiarabu, lugha tukufu zaidi na iliyo wazi kabisa, chenye kubainisha kweli zote zenye manufaa ambazo watu wanazihitaji. Na kubainisha huku kwote na kuweka wazi ni \"ili mpate kuzingatia.\" Yaani, kuelewa mipaka yake, misingi yake, matawi yake, amri zake na makatazo yake. Na mkiyafahamu hayo kwa yakini yenu, na nyoyo zenu zikasifika na kuyajua, hilo litasababisha matendo ya viungo na kuyafuata, na \"ili mpate kuzingatia.\u201d Yaani, akili zenu zizidi kwa sababu ya kurudiarudia kwa maana tukufu za juu katika akili zenu, kwa hivyo mkahama kutoka hali moja hadi nyingine iliyo ya juu zaidi kuiliko na iliyo kamili zaidi."},{"id":2196,"sura":12,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} \"Sisi tunasimulia simulizi nzuri zaidi.\" Na hilo ni kwa sababu ya ukweli wake, usahili wa maneno yake, na umaridadi wa maana zake, \"kwa kukufunulia Qur-ani hii.\" Yaani, kwa sababu ya yale yaliyomo ndani ya Qur\u2019ani hii ambayo tulikufunulia wewe na tukakufadhilisha wewe kwayo juu ya Mitume wengine wote. Na hiyo ni neema tupu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ihsan. \"Na ijapokuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa walioghafilika.\" Yaani, hukuwa unajua ni nini Kitabu wala imani kabla ya Mwenyezi Mungu kukufunulia wahyi, lakini tumekifanya kuwa ni nuru ambayo kwayo tunamwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na alipozisifu hadithi zilizomo ndani ya Qur-ani hii na kwamba ni hadithi nzuri kabisa, na hakuna hadithi katika kitabu chochote kama zilizomo katika Qur-ani hii,  akataja kisa cha Yusuf, na baba yake, na ndugu zake, hadithi ya ajabu na nzuri, kwa hivyo akasema:"},{"id":2197,"sura":12,"from_aya":4,"to_aya":6,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"4. Yusuf alipomwambia baba yake: Ewe baba yangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja, na jua, na mwezi. Nimeviota vikinisujudia. 5. (Baba) akasema: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wakaja kukufanyia njama. Hakika Shetani ni adui aliye dhahiri kwa mwanadamu. 6. Na hivyo ndivyo Mola wako Mlezi atakuteua na atakufundisha katika tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya ukoo wa Yaa'qub, kama alivyowatimizia hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima. "},{"id":2198,"sura":12,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0622\u064a\u0627\u062a","text":"Na jua kwamba Mwenyezi Mungu alitaja kwamba yeye anasimulia Mtume wake hadithi nzuri kabisa katika kitabu hiki, kisha akaitaja hadithi hii, na akaikunjua, na akataja yaliyotokea ndani yake, kwa hivyo ikajulikana kuwa ni hadithi timilifu, kamili, nzuri. Kwa hivyo, anayetaka kuikamilisha au kuifanya kuwa nzuri, kwa yale yaliyotajwa kutoka kwa Wana wa Israili, ambayo haifahamiki silisili ya wasimulizi wake wa upokezaji sahihi, na hata nyingi zake ni za uongo, basi yeye ni kama anamzibia pengowenyezi Mungu, na kukamilishia kitu ambacho anadai kuwa ni kipungufu. Na linakutosha kuwa jambo hili linafikia kiwango hiki cha ubaya. Hii ni kwa sababu nyongeza mbalimbali juu ya Sura hii za uongo na mambo mabaya mno yanayopingana na kile alichosimulia Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mambo mengi zimejaa katika tafsiri mbalimbali. Basi ni lazima kwa mja aelewe kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale aliyoyasimulia na aache chochote kisichokuwa hayo yasiyokuwa kutoka kwa Nabii \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake \u2013 kupitia njia ya maandiko yaliyopokewa kutoka kwake."},{"id":2199,"sura":12,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Basi kauli yake yeye Mtukufu: \"Yusuf alipomwambia baba yake\" Yaaqub bin Is-haq bin Ibrahim Al-Khalil, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, \"Ewe baba yangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja, na jua, na mwezi. Nimeviota vikinisujudia.\" Ndoto hii ilikuwa ni utangulizi wa cheo cha juu alichokifikia Yusuf, amani iwe juu yake katika Dunia na akhera. Na vile vile Mwenyezi Mungu anapotaka jambo katika mambo makubwa, anaweka utangulizi mbele yake uwe wa kuuandalia na kulirahisishia jambo lake, na kujiandaa na magumu yatakayompata mja, na kuwa ni kumfanyia mja upole, na wema. Basi Yakub akaifasiri kwamba hilo jua ni mama yake, na mwezi huo ni baba yake, na nyota zile ni ndugu zake, na kwamba hali zitambadilikia mpaka afikie hali ambayo watamnyenyekea na kumsujudia kwa heshima na taadhima, na kwamba hilo haliwi isipokuwa kwa sababu zitakazolitangulia, kama vile Mwenyezi Mungu kumchagua, na kukamilishia neema zake juu yake kwa elimu, na matendo, na kumuimarisha katika ardhi, na kwamba neema hii itajumuisha familia ya Yakub ambao walimsujudia, wakawa wafuasi wake katika hilo."},{"id":2200,"sura":12,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} Na ndiyo maana akasema: \"Na hivyo ndivyo Mola wako Mlezi atakuteua.\" Yaani, anakuteua na kukuchagua kwa sababu ya sifa kubwa na fadhila nzuri alizokuneemesha kwazo, \"na atakufundisha katika tafsiri ya mambo.\" Yaani, kutafsiri ndoto na kubainisha yale ambayo Hadithi za kweli zitaishia, kama vile vitabu vya mbinguni na mfano wa hayo. \"Na atatimiza neema zake juu yako\" katika dunia na Akhera, kwa kukupa kheri katika dunia na Akhera, \"kama alivyowatimizia hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq\" kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwa neema kubwa, pana, za kidini na za kidunia. \"Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima\" Yaani, elimu yake inazunguka mambo yote na yale yaliyomo ndani ya dhamiri za waja wake ya wema na mengineyo, kwa hivyo humpa kila mmoja kile kinachohitajiwa na hekima yake na sifa Zake. Kwani, Yeye ni Mwenye hekima, huweka vitu katika mahali pake na huviteremsha katika vyeo vyake."},{"id":2201,"sura":12,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} Na Yusuf alipofasiriwa maana yake, baba yake akamwambia: \"Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wakaja kukufanyia njama.\" Yaani,  kwa sababu ya husuda kutoka kwa nafsi zao, na kwamba wewe utakuwa raisi mtukufu juu yao. \"Hakika Shetani ni adui aliye dhahiri kwa mwanadamu.\" Hachoki naye usiku na mchana wala kwa siri wala kwa dhahiri. Kwa hivyo, kuwa mbali na sababu ambazo anapata kwazo mamlaka juu ya mja ni bora zaidi. Kwa hivyo, Yusuf akafuata amri ya baba yake, na hakujulisha ndugu zake kuhusu jambo hilo, bali aliwaficha hilo."},{"id":2202,"sura":12,"from_aya":7,"to_aya":9,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"7. Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara kwa wanaouliza. 8. Pale waliposema: Hakika Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, ilhali sisi ni kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yumo katika upotovu wa dhahiri. 9. Muueni Yusuf, au mtupeni nchi ya mbali ili uso wa baba yenu uwaelekee nyinyi tu. Na baada ya haya mtakuwa kaumu njema. "},{"id":2203,"sura":12,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Yeye Mtukufu anasema: \"Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara.\" Yaani, mazingatio na ushahidi mbalimbali juu ya mengi katika mambo mazuri yatafutwayo \"kwa wanaouliza.\" Yaani, kwa kila mtu ambaye aliuliza juu yake kwa maneno au kwa vitendo. Kwani, waulizaji ndio wanaonufaika na ishara mbalimbali na mazingatio. Na ama wale wanaopuuza, hao hawafaidiki na ishara wala visa ushahidi wa wazi."},{"id":2204,"sura":12,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"8. \"Pale waliposema\" kati yao \"hakika Yusuf na nduguye.\" Binyamini, ambaye ni ndugu yake wa kwa baba na mama. Na vinginevyo, wote ni ndugu tu \"wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, ilhali sisi ni kikundi chenye nguvu.\" Yaani, vipi anawaboresha wawili hao [juu yetu] kwa mapenzi na huruma? \"Hakika baba yetu yumo katika upotovu wa dhahiri;\" yaani, yuko katika kosa lililo wazi kwa kuwa amewapendelea wao wawili kuliko sisi bila ya sababu tunayoiona, wala kitu tunachokiona."},{"id":2205,"sura":12,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} \"Muueni Yusuf, au mtupeni nchi ya mbali.\" Yaani, mtoeni katika macho ya baba yake hadi katika ardhi ya mbali ambayo hataweza kumuona huko. Kwani, mkifanya moja ya mambo haya mawili; \"ili uso wa baba yenu uwaelekee nyinyi tu;\" yaani, atabakia akiwashughulikia nyinyi tu, na kuwaelekea nyinyi kwa huruma na upendo. Kwa maana, moyo wake ulishughulika na Yusuf kushughulika ambako hawapati wakati wa kuwa nanyi. \"Na baada ya haya mtakuwa;\" yaani, baada ya tendo hili, mtakuwa kaumu njema. Yaani, mtatubu kwa Mwenyezi Mungu na kumwomba msamaha baada ya dhambi zenu, kwa hivyo wakawa wameitanguliza azimio mbele ya kutubu kabla ya kufanya dhambi hiyo, ili kurahisisha kukifanya kitendo hicho, na kuondoa ubaya wake, na kutiana moyo."},{"id":2206,"sura":12,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"10. Akasema msemaji miongoni mwao: Msimuue Yusuf. Lakini mtumbukizeni ndani ya kisima. Baadhi ya wasafiri watakuja mwokota; ikiwa kweli mnataka kufanya."},{"id":2207,"sura":12,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} Yaani, \"Akasema msemaji\" miongoni mwa ndugu zake Yusuf ambao walitaka kumuua au kumfukuzia mbali \"Msimuuwe Yusuf\" kwa maana kumuua ni dhambi kubwa na mbaya zaidi. \nLakini yanayokusudiwa yanaweza patikana kwa kumpeleka mbali na baba yake bila ya kumuua, lakini fikieni jambo la kumweka mbali kwa kumtumbukiza \"ndani ya kisima\" na mumtishie kwamba asijulishe yeyote juu yenu, bali aseme kuwa yeye ni mtumwa anayemilikiwa, aliyetoroka [kwenu] ili aokotwe na \"baadhi ya wasafiri\" ambao wanasafiri kwenda sehemu za mbali ili wamhifadhi pamoja nao. Na mzungumzaji huyu ndiye wa maoni bora zaidi kati yao kuhusiana na Yusuf na mwema wao zaidi na mchamungu wao zaidi katika suala hili. Kwa maana, baadhi ya uovu ni mdogo zaidi kuliko baadhi yake na madhara mepesi huepukwa kwayo madhara makubwa; basi walipokubaliana juu ya maoni haya:"},{"id":2208,"sura":12,"from_aya":11,"to_aya":14,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"11. Wakasema: Ewe baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yusuf? Na hakika sisi ni wenye kumtakia heri! 12. Muachilie kesho pamoja nasi, ale kwa furaha na acheze, na bila ya shaka sisi tutamhifadhi. 13. Akasema: Kwa hakika inanihuzunisha kwamba nyinyi mwende naye, na ninahofia aje mbwa mwitu akamla ilhali nyinyi mmeghafilika naye. 14. Wakasema: Ikiwa mbwa mwitu atamla na ilhali sisi ni kundi lenye nguvu kabisa, basi bila ya shaka sisi tutakuwa tumehasirika. "},{"id":2209,"sura":12,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} Yaani, ndugu zake Yusuf kwa njia ya kuyafikia makusudio yao walimwambia baba yao: \"Ewe baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yusuf? Na hakika sisi ni wenye kumtakia heri!\" Yaani, kwa nini uingiwe na hofu kutoka kwetu juu ya Yusuf bila ya kuwepo sababu wala la kulazimisha hilo, ilhali sisi hakika \u201cni wenye kumtakia heri!\" Yaani, tunamhurumia na kumtakia yale tunayojitakia sisi wenyewe. Na hili linaashiria kwamba Yakub, amani iwe juu yake, hakuwa akimruhusu Yusuf aende pamoja na ndugu zake nyikani na mfano wake."},{"id":2210,"sura":12,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Basi walipoondoshea tuhuma yenye kuzuia asiachiliwe kwenda pamoja nao, wakamtajia katika mambo yenye masilahi kwa Yusuf na kwamba atatulia, jambo ambalo baba yake anampendea kwa kiasi ambacho kitamfanya amuachilie kwenda pamoja nao. Kwa hivyo, wakasema: \"Muachilie kesho pamoja nasi, ale kwa furaha na acheze.\" Yaani, atembee kwa raha jangwani na ajitulize \"na bila ya shaka sisi tutamhifadhi.\" Yaani, tutamtunza na kumlinda kutokana na madhara yoyote yanayomtaka."},{"id":2211,"sura":12,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Kwa hivyo akawajibu kwa kauli yake, \u201cKwa hakika inanihuzunisha kwamba nyinyi mwende naye.\" Yaani kwenda  kwenu pamoja naye kunanihuzunisha na kunaniwia vigumu. Kwa sababu, siwezi kuachana naye, hata kwa muda mfupi tu. Basi hili ndilo linalonizuia kumuachilia aende. \"Na\" kizuizi cha pili ni kwamba \"ninahofia aje mbwa mwitu akamla ilhali nyinyi mmeghafilika naye.\" Yaani, katika hali ya kughafilika kwenu naye, kwa sababu yeye ni mdogo, hawezi kujizuia na mbwa mwitu."},{"id":2212,"sura":12,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} \"Wakasema: ikiwa mbwa mwitu atamla na ilhali sisi ni kundi lenye nguvu kabisa.\" Yaani, kundi linalofanya bidii katika kuihifadhi; \"basi bila ya shaka sisi tutakuwa tumehasirika.\" Yaani, hakutakuwa na heri yoyote ndani yetu na hakutakuwa na faida yoyote itakayotarajiwa kutoka kwetu ikiwa mbwa mwitu atamla na tukashindwa juu yake. Basi walipomuandalia baba yao sababu za kumfanya amuachilie na kutokuwepo na kizuizi chochote, akaruhusu aachiliwe kwenda pamoja nao kwa ajili ya kujituliza."},{"id":2213,"sura":12,"from_aya":15,"to_aya":18,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"15. Basi walipokwenda naye, na wakakubaliana kwamba wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia Yusuf: Hakika utakuja waambia jambo lao hili, na wala wao hawatambui. 16. Wakamjia baba yao usiku wakilia. 17. Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapokuwa sisi ni wakweli. 18. Na walikuja na shati lake likiwa lina damu ya uongo. Akasema: Bali nafsi zenu zimewashawishi kutenda kitendo. Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayoyaeleza. "},{"id":2214,"sura":12,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15} Yaani, ndugu zake Yusuf walipokwenda pamoja na Yusuf baada ya baba yake kumpa ruhusa, wakaamua kumweka ndani ya kisima, kama msemaji wao aliyetangulia alivyosema, na walikuwa na uwezo juu ya yale waliyokubaliana juu yake, basi wakamfanyia kile walichoweza kufanya, na wakamtupa ndani ya kisima, kisha Mwenyezi Mungu akamfanyia huruma na akamfunulia wahyi ilhali yuko katika hali hiyo ngumu; \"Hakika utakuja waambia jambo lao hili, na wala wao hawatambui.\"  Yaani, utawalaumu na kuwajulisha juu ya jambo lao hili ilhali hawalitambui jambo hilo. Kwa hivyo, ndani yake kulikuwa na bishara njema kwake kwamba ataokoka kutoka katika yale aliyojipata ndani yake, na kwamba Mwenyezi Mungu atamkutanisha na familia yake na ndugu zake katika njia ya utukufu na kumwezesha katika ardhi."},{"id":2215,"sura":12,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} \"Wakamjia baba yao usiku wakilia\" ili kurudi kwao kuwe baada ya kurudi kwao kwa kawaida, na kilio chao kiwe ni ushahidi wao na uthibitisho wa ukweli wao."},{"id":2216,"sura":12,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"17. Basi wakasema, wakitoa udhuru wa uongo, \"Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana\" ima kwa miguu au kwa kurusha mishale, \"na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu\" kwa ajili ya kumpa muda na kumuacha apumzike. \"Basi mbwa mwitu akamla\" tulipokuwa mbali naye na tulipokuwa tunashindana. \"Lakini wewe hutatuamini ijapokuwa sisi ni wakweli.\" Yaani, tumetoa udhuru huu, lakini inaonekana wazi kwamba hutuamini. Kwa sababu, ya huzuni ulioko moyoni mwako juu ya Yusuf na huruma kubwa ulioyo nayo juu yake, lakini kutotuamini kwako hakutuzuii sisi kuomba msamaha kwa udhuru wa uhakika. Na haya yote ni yalikuwa kwa ajili ya kusisitiza udhuru wao."},{"id":2217,"sura":12,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} \"Na\" katika yale waliyoyasisitiza kwayo kauli yao hiyo ni kwamba, \"walikuja na shati lake likiwa lina damu ya uongo.\" Wakadai kuwa, ni damu ya Yusuf mbwa mwitu alipomla, lakini baba yao hakuwaamini kwa hilo, na \"akasema, bali nafsi zenu zimewashawishi kutenda kitendo.\" Yaani, nafsi zenu ziliwapambia jambo baya ili kunitenganisha naye. Kwa sababu aliona baadhi ya ushahidi na hali mbalimbali, na pia katika ndoto ya Yusuf ambayo alimsimulia ambayo ilimuonyesha kile alichosema. \"Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayoyaeleza.\" Yaani, ama mimi  nitafanya hima katika kufanya kazi yangu, nayo ni kwamba nitajitahidi kujisubirisha katika majaribio haya subira nzuri iliyosalimika kutokana na hasira na kuwalalamikia viumbe, na nitatafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika hili, siyo kwa nguvu zangu na uwezo wangu. Basi alijiahidi jambo hili, na akamlalamikia Muumba wake kwa kauli yake: \"Hakika mimi ninamlalamikia shida yangu na huzuni wangu Mwenyezi Mungu tu.\" Kwa sababu kumlalamikia Muumba hakupingani na subira nzuri. Kwa sababu nabii anapoahidi, anatimiza."},{"id":2218,"sura":12,"from_aya":19,"to_aya":20,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"19. Na ukaja msafara, kisha wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Alisema: Hii ni bishara njema! Huyu hapa mvulana! Wakamficha ili kumfanya ni bidhaa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema hayo wanayoyatenda. 20. Na wakamuuza kwa thamani duni, dirhamu za kuhesabika tu. Wala hawakuwa na haja naye. "},{"id":2219,"sura":12,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} Yaani, Yusuf alikaa ndani ya kisima hicho muda aliokaa mpaka \"ukaja msafara.\" Yaani, msafara uliokuwa unaenda Misri, \"kisha wakamtuma mchota maji wao.\" Yaani, mtangulizi wao ambaye anazunguka akiwatafutia maji, na kuyapima na kuyaandaa kwa kuwatayarisha hodhi na mengine mfano wake. \"Naye akatumbukiza\" mchota maji wao huyo \"ndoo yake\" kwa hivyo Yusuf, amani iwe juu yake, akaishikilia na akatoka nje. Kwa hivyo, mtekaji huyo akasema: \"Hii ni bishara njema! Huyu hapa mvulana!\" Yaani akafurahi na kusema: Huyu hapa mvulana mwenye thamani. \"Wakamficha ili kumfanya ni bidhaa.\""},{"id":2220,"sura":12,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Na ndugu zake walikuwa karibu naye, basi huo msafara ukamnunua kutoka kwao \"kwa thamani duni.\" Yaani, chache sana, ambayo ilifasiriwa na kauli yake \"dirhamu za kuhesabika tu. Wala hawakuwa na haja naye\" kwa sababu hawakuwa na lengo lolote naye isipokuwa kumuweka mbali na baba yake, na hawakuwa na nia ya kuchukua thamani yake. Na maana ya hili ni kwamba, msafara huo ulipompata, waliazimia kuficha jambo lake na wakamfanya miongoni mwa bidhaa zao walizokuwa nazo, mpaka ndugu zake walipowajia, kwa hivyo wakadai kuwa yeye ni mtumwa aliyetoroka kutoka kwao, basi wakamnunua kutoka kwao kwa thamani hiyo, na wakapata uhakikisho juu yake kutoka kwake kwamba hatatoroka, na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi."},{"id":2221,"sura":12,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"21. Na yule aliyemnunua huko Misri alimwambia mkewe: Mtengenezee makazi ya heshima huyu; huenda akatufaa au tukamfanya mwanetu. Basi hivyo ndivyo tulivyomuweka Yusuf imara katika ardhi ili tumfundishe kufasiri mambo. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini wengi wa watu hawajui."},{"id":2222,"sura":12,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} Yaani, msafara huo walipokwenda naye hadi Misri na wakamuuza huko, mheshimiwa fulani Misri akamnunua. Na alipomnunua, akapendezwa naye na akamuusia mke wake, akisema, \u201cMtengenezee makazi ya heshima huyu; huenda akatufaa au tukamfanya mwanetu.\" Yaani, ima atatunufaisha kama wanavyonufaisha watumwa kwa aina mbalimbali za huduma, na ima tutajifurahisha naye kama kuwafurahia watoto wetu. Na pengine hilo ni kwa sababu hawakuwa na mtoto. \"Basi hivyo ndivyo tulivyomuweka Yusuf imara katika ardhi.\" Yaani, kama tulivyoepesisha kwamba yule mheshimiwa wa Misri amnunue na amkirimu kukirimu huku, tulilifanya hili kuwa ni utangulizi wa kumuimarisha hapa ardhini kupitia njia hii \"ili tumfundishe kufasiri mambo\" ikiwa hatokuwa na kazi yoyote wala wasiwasi isipokuwa elimu tu. Hilo linakuwa ni mojawapo ya sababu ya kujifunza elimu nyingi, ikiwemo elimu ya hukumu mbalimbali na elimu ya kutafsiri mambo na mengineyo. \"Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake.\" Yaani, jambo lake Yeye Mtukufu ni yenye kutekelezeka na hakuna mwenye kubatilisha awezaye kuibatilisha, na hakuna mwenye kushinda awezaye kulishinda. \"Lakini wengi wa watu hawajui.\" Na ndiyo maana yanatokea kwao na wanafanya wanayoyafanya katika kushindana na hukumu za Mwenyezi Mungu za kimajaliwa, ilhali wao hawawezi na ni dhaifu zaidi kuliko hayo."},{"id":2223,"sura":12,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"22. Na alipofikia utu uzima wake, tukampa hukumu na elimu. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mazuri."},{"id":2224,"sura":12,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} Yaani, \"alipofikia\" Yusuf \"utu uzima;\" yaani, alipokamilika nguvu zake za kimaana na za kihisia na akawa anaweza kubeba majukumu mazito kama vile ya unabii na ujumbe \"tukampa hukumu na elimu.\" Yaani, tulimfanya kuwa Nabii, Mtume na mwanazuoni wamuabuduo Mola Mlezi wa viumbe wote. \"Na hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mazuri\" katika kumuabudu Muumba kwa kufanya juhudi na ikhlasi ndani yake, na kwa waja wa Mwenyezi Mungu kwa kuwafanyia ya manufaa na wema. Tunawapa elimu yenye manufaa miongoni mwa malipo juu ya uzuri wao. Na hili linashiria kwamba Yusuf alitimiza cheo cha ihsani, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akampa kuhukumu kati ya watu, na elimu nyingi, na unabii."},{"id":2225,"sura":12,"from_aya":23,"to_aya":29,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"23. Na yule bibi wa nyumba aliyokuwamo Yusuf akamtamani kinyume cha nafsi yake, na akafungafunga milango. Akamwambia: Njoo! Yusuf akasema: Audhubillahi (Najikinga na Mwenyezi Mungu!). Hakika Yeye ni Bwana wangu, aliniweka maskani nzuri, na hakika madhalimu hawafaulu. 24. Na hakika yule mwanamke alimtamani, na Yusuf angelimtamani lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi. Ilikuwa hivyo, ili tumuepushie mabaya na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walioteuliwa. 25. Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke akalirarua shati lake Yusuf kwa nyuma. Na wakamkuta bwana wake mlangoni. Mwanamke akasema: Hakuna malipo ya mwenye kutaka kumfanyia mabaya mkeo isipokuwa afungwe au kupewa adhabu chungu. 26. Yusuf akasema: Yeye ndiye aliyenitaka bila ya mimi kumtaka. Na shahidi aliyekuwa katika jamaa za mwanamke akasema: Ikiwa shati lake limechanwa kwa mbele, basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo. 27. Na ikiwa shati lake limechanwa kwa nyuma, basi mwanamke amesema uongo, naye Yusuf ni katika wakweli. 28. Basi yule bwana alipoona shati lake limechanwa kwa nyuma, akasema: Hakika haya ni katika vitimbi vyenu wanawake. Hakika vitimbi vyenu ni vikuu. 29. Yusuf! Achilia mbali haya. Na wewe, mwanamke, omba msamaha kwa dhambi zako. Hakika wewe ni katika waliofanya makosa. "},{"id":2226,"sura":12,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0622\u064a\u0627\u062a","text":"Mtihani huu mkubwa ni mkubwa zaidi kwa Yusuf kuliko mtihani wa ndugu zake, na subira yake juu yake kuna malipo makubwa zaidi kwa sababu kusubiri kwa hiari licha ya kuwepo kwa sababu nyingi za kufanya kitendo hicho. Kwa hivyo, akatanguliza upendo wa Mwenyezi Mungu mbele ya hilo. Na ama mtihani wake kutoka kwa ndugu zake, huo kusubiri juu yake ni subira ya lazima, ambao ni kama maradhi na machukizo ambayo humsibu mja bila ya hiyari yake, na wala hana pa kukimbilia isipokuwa kuwa tu na subira juu yake, kwa kutii au kuchukia."},{"id":2227,"sura":12,"from_aya":23,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23-24} Haya ni kwa sababu Yusuf, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alibaki mwenye kuheshimiwa katika nyumba ya yule mheshimiwa, na alikuwa na uzuri, na ukamilifu, na urembo kiasi kwamba ilimlazimu kwamba, \"Na yule bibi wa nyumba aliyokuwamo Yusuf akamtamani kinyume cha nafsi yake.\" Yaani, alikuwa mtumishi wake na alikuwa chini ya uendeshaji wake, na maskani yalikuwa mamoja ambapo ilikuwa rahisi kwake kutekeleza jambo la kuchukiza bila kutambuliwa na yeyote wala kuhisiwa na mwanadamu yeyote. \"Na\" msiba huo ukazidi kwa sababu \"alifungafunga milango\"  na mahali pale pakawa tupu, na wakasalimika kutokana na mtu yeyote kuwaingilia kwa sababu milango ilikuwa imefungwa. Na bibi huyo alikuwa amemuita kwa nafsi yake, akasema: \"Njoo!\" Yaani, fanya jambo linalochukiza na uje kwangu! Na pamoja na hayo alikuwa mgeni ambaye hawezi kuwa na adabu kama ile angekuwa nayo katika nchi yake na miongoni mwa wale wanaomjua, na alikuwa mfungwa chini ya mkono wake, na mwanamke huyo alikuwa bibi yake, naye alikuwa mzuri unaoita kile kilichoko huko, naye alikuwa barobaro mseja, na alikuwa amemtishia iwapo hatafanya alichomuamrisha kuwa atafungwa jela au adhabu chungu. Lakini akawa na subira katika  kutomuasi Mwenyezi Mungu pamoja na kuwepo sababu yenye nguvu ya kufanya hivyo ndani yake. Kwa sababu alikuwa ameazimia juu yake azimio ambalo aliliacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akayatanguliza matashi ya Mwenyezi Mungu mbele ya matashi ya nafsi yenye kuamrisha mabaya, na akaona katika ushahidi wa Mola wake Mlezi - ambao ni elimu aliyokuwa nayo na imani ambayo yalimlazimu kujieka mbali na kuacha maasia haya makubwa Mwenyezi na \"Yusuf akasema: Audhubillahi (Najikinga na Mwenyezi Mungu!)\" Yaani, najikinga kwa Mwenyezi Mungu kufanya kitendo hiki kibaya. Kwa sababu ni katika mambo yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu na kumtenga mtu naye, na kwa sababu ni hiyana dhidi ya bwana wangu, ambaye aliniweka maskani mazuri. Basi hainifailii nimkabili katika mkewe kwa mkabala mbaya zaidi, na hii ni katika dhuluma kubwa zaidi, na dhalimu hafaulu. Na muhtasari wa hayo ni kwamba aliweka vizuizi dhidi ya yeye kufanya kitendo hiki: kumcha Mungu, kuzingatia haki za bwana wake aliyemkirimu, na kujitunza dhidi ya dhuluma ambayo hafaulu mwenye kujihusisha nayo, na pia uthibitisho wa imani ambao Mwenyezi Mungu alimneemesha nao ambao uko moyoni mwake, ilimtaka kutekeleza maamrisho na kuepuka makemeo. Na chenye kukusanya hayo yote ni kwamba, Mwenyezi Mungu alimwondolea ubaya huo na uchafu, kwa sababu yeye ni miongoni mwa waja Wake ambao wanamfanyia yeye tu ibada zao; ambaye Mwenyezi Mungu aliwasafisha, na akawachagua na akawafanya kuwa kwa ajili Yake tu; na akawaneemesha kwa neema mbalimbali, na akawaepusha na machukizo ambayo kwayo wakawa katika bora zaidi wa viumbe Wake."},{"id":2228,"sura":12,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} Alipokataa kuitikia ombi lake baada ya kumshawishi kukubwa, akaenda ili amtoroke na aharakishe kutoka nje ya mlango ili ajinasue na ayatoroke majaribu hayo, lakini mwanamke huyo akamtangulia kwenda huko, na akaishikilia nguo yake, kwa hivyo akalirarua shati lake. Na walipofika mlangoni katika hali hiyo, wakamkuta bwana wake - yaani, mumewe - hapo mlangoni, na akaona jambo linalomsumbua sana, kwa hivyo mwanamke huyo akaharakisha kusema uongo, na kwamba kushawishi huko kulitoka kwa Yusuf. Akasema: \"Hakuna malipo ya mwenye kutaka kumfanyia mabaya mkeo\" wala hakusema: aliyemfanyia ubaya mkeo, kwa ajili ya kujitoa katika hatia na kumtoa Yusuf pia katika hatia ya kufanya kitendo hicho, lakini mzozo huo ulikuwa tu katika utashi na kushawishi; \"isipokuwa afungwe au kupewa adhabu chungu.\" Yaani, au aadhibiwe adhabu chungu."},{"id":2229,"sura":12,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} Basi Yusuf akajiweka mbali na yale aliyomsingizia, na \"akasema: Yeye ndiye aliyenitaka bila ya mimi kumtaka\" kwa hivyo kufikia hapo hali ya kila mmoja wao ikawa na uwezekano wa kuwa ndiyo ya ukweli, wala hakujua ni nani kati yao, isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiwekea haki na ukweli ushahidi mbalimbali na alama zinazoyaashiria, ambazo waja Wake wanaweza kuzijua au wasiweze kuzijua. Na katika suala hili Mwenyezi Mungu Mtukufu alineemesha kwamba ajulikane mkweli kati yao ili kumuondoa hatiani Nabii Wake na mteule wake, Yusuf, amani iwe juu yake. Kwa hivyo, akajitokeza shahidi kutoka kwa familia yake mwanamke huyo akatoa ushahidi kwa uthibitisho ambao mwenye kupatikana nao ndiye mkweli. Kwa hivyo akasema: \"Ikiwa shati lake limechanwa kwa mbele, basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo.\" Kwa sababu hilo linaashiria kuwa yeye ndiye aliyemjia, aliyemtaka, aliyemshambulia, na kwamba mwanamke huyo alitaka kumsukuma amuondokee,  kwa hivyo akalirarua shati lake kutokea upande huu."},{"id":2230,"sura":12,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} \"Na ikiwa shati lake limechanwa kwa nyuma, basi mwanamke amesema uongo, naye Yusuf ni katika wakweli.\" Kwa sababu, hilo linaashiria kukimbia kwake kutoka kwa mwanamke huyo, na kwamba mwanamke huyo ndiye aliyemtafuta, kwa hivyo akararua shati lake kutokea upande huu."},{"id":2231,"sura":12,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"28. \"Basi yule bwana alipoona shati lake limechanwa kwa nyuma\" akaijua kwa hilo ukweli wa Yusuf na kutokuwa kwake na hatia, na kwamba mwanamke huyo ndiye mwongo. Kwa hivyo, bwana wake akamwambia: \"Hakika haya ni katika vitimbi vyenu wanawake. Hakika vitimbi vyenu ni vikuu.\" Na je, kuna kubwa zaidi kuliko kitimbi hiki alichojiweka mbali kwacho kutokana na yale aliyoyataka na kuyafanya na kumtuhumu kwayo nabii wa Mwenyezi Mungu Yusuf, amani iwe juu yake?"},{"id":2232,"sura":12,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"29. Tena kisha bwana wake alipohakikisha ukweli wa jambo hili, Akamwambia Yusuf: \"Yusuf! Achilia mbali haya.\" Yaani, acha kulizungumzia hili, na lisahau, na usimtajie hili mtu yeyote ili kuisitiri familia yake. \"Na omba msamaha\" ewe mwanamke \"kwa dhambi zako. Hakika wewe ni katika waliofanya makosa.\" Basi akamwamrisha Yusuf kuyaachilia mbali, naye mkewe akamwamrisha kuomba msamaha na kutubia."},{"id":2233,"sura":12,"from_aya":30,"to_aya":35,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"30. Na wanawake wa mjini wakawa wanasema: Mke wa Mheshimiwa anamtamani mtumishi wake bila ya yeye kumtaka! Hakika mapenzi yamemuingia sana moyoni. Sisi hakika tunamwona yumo katika upotovu ulio dhahiri. 31. Basi aliposikia yule bibi masengenyo yao, aliwaita, na akawawekea matakia ya kuegemea, na akampa kila mmoja wao kisu. Akamwambia Yusuf: Tokeza mbele yao. Basi walipomwona, waliona ni kitu kikubwa kabisa, na wakajikatakata mikono yao. Wakasema: Hasha Lillahi! Huyu si mwanadamu. Huyu si isipokuwa Malaika mtukufu. 32. Yule bibi akasema: Huyu basi ndiye huyo mliyenilaumia! Na kweli mimi nilimtaka naye akakataa. Na asipofanya ninayomwamrisha, basi hapana shaka atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio duni kabisa. 33. Yusuf akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Ninapendelea kifungo kuliko haya anayoniitia. Na usiponiondoshea vitimbi vya wanawake, mimi nitaelekea kwao, na nitakuwa katika wajinga. 34. Basi Mola wake Mlezi akamwitikia, na akamwondoshea vitimbi vyao. Hakika Yeye ni Msikizi, Mwenye kujua vyema. 35. Kisha ikawadhihirikia baada ya kuona Ishara kuwa lazima wamfunge kwa muda. "},{"id":2234,"sura":12,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Inamaanisha kwamba habari hiyo ikawa maarufu na kuenea katika nchi, na wanawake wakazungumza juu yake, na wakaanza kumlaumu mwanamke wa mheshimiwa huyu na wanasema: \"Mke wa Mheshimiwa anamtamani mtumishi wake bila ya yeye kumtaka! Hakika mapenzi yamemuingia sana moyoni.\" Yaani, hili ni jambo baya! Yeye ni mwanamke wa cheo kikubwa, na mumewe ni wa cheo kikubwa pia, lakini pamoja na hayo hajaacha kuendelea kumtaka kimapenzi mtumishi wake ambaye yuko chini ya mkono wake na katika huduma yake bila ya yeye kumtaka kimapenzi, na tena pamoja na hayo kumpenda kwake kumemfika kiwango kikubwa sana. \"Hakika mapenzi yamemuingia sana moyoni.\" Yaani, mapenzi yake yamemfika ndani kabisa ya moyo wake. Na huu ndio upendo mkubwa zaidi unaowezekana. \"Sisi hakika tunamwona yumo katika upotovu ulio dhahiri.\" Kwa kuwa ilipatikana ndani yake hali hii ambayo haimfailii, ambayo ni hali inayomshushia hadhi yake na kumdunisha mbele ya watu."},{"id":2235,"sura":12,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} Na kauli hii kwa upande wao ilikuwa ni njama, na haikukusudiwa tu kumlaumu na kumkashifu, bali walitaka, kwa maneno haya, kufikia kumuona huyu Yusuf, ambaye naye mke wa mheshimiwa huyu alifitinishwa naye ili mke wa mheshimiwa huyu akasirike na awaonyeshe ili wamkubalie udhuru wake. Na ndiyo maana wakaiita njama, kwa hivyo akasema: \"Basi aliposikia yule bibi masengenyo yao, aliwaita\" yaani aliwaita nyumbani kwake kwa ajili ya  karamu, \"na akawawekea matakia ya kuegemea.\" Yaani, pahali palipoandaliwa kwa kila aina ya magodoro, mito, na vyakula vitamu. Na miongoni mwa vitu alivyoleta katika karamu hiyo ni chakula kilichohitaji kisu. Ima tunda la utruj au kitu kinginecho. \"Na akampa kila mmoja wao kisu\" ili wakate kwacho chakula hicho, \"na akamwambia\" Yusuf, \"Tokeza mbele yao,\" katika hali ya uzuri wake na urembo wake. \"Basi walipomwona, waliona ni kitu kikubwa kabisa\" katika vifua vyao na wakaona mandhari ya ajabu mno ambayo hawakuwahi kuona mfano wake. \"Na wakajikatakata mikono yao\" kwa sababu ya mshango kwa visu hivyo walivyokuwa navyo. \"Wakasema: Hasha Lillahi!' Yaani, wakamtakasa Mwenyezi Mungu, \"Huyu si mwanadamu. Huyu si isipokuwa Malaika mtukufu.\" Na hayo ni kwa sababu Yusuf alipewa uzuri wa ajabu mno, na nuru na urembo ambayo kwayo alikuwa ni ishara kwa watazamaji na mazingatia kwa wanaotafakari."},{"id":2236,"sura":12,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} Na ulipowadhihirikia uzuri dhahiri wa Yusuf, na wakapendezwa sana, na zikaonekana kwao udhuru nyingi zinazomuunga mkono mke wa mheshimiwa huyo, akataka kuwaonyesha uzuri wake wa ndani kwa kujisafisha kwake kukamilifu. Kwa hivyo akasema, akitangaza hilo na akieleza mapenzi yake makubwa, bila ya kujali, na tena kwa sababu lawama ile ya wanawake hao ilikuwa sasa imeondoka \"Na kweli mimi nilimtaka naye akakataa.\" Yaani, alikataa lakini yeye ataendelea kumtaka kimapenzi, na kupita kwa wakati hakukumzidishia isipokuwa mapenzi, na hamu, na wasiwasi, na shauku kubwa ya mapenzi. Na ndiyo maana akamwambia Yusuf mbele yao: \"Na asipofanya ninayomwamrisha, basi hapana shaka atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio duni kabisa.\n;\" ili amlazimishe kwa kumtishia huku kumfanya ayafikie alichokusudia kutoka kwake."},{"id":2237,"sura":12,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"33. Hapo, Yusuf akashikamana na Mola wake Mlezi, na akamwomba msaada katika vitimbi vyao hivi. Na \"akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Ninapendelea kifungo kuliko haya anayoniitia.\" Na haya yanaashiria kuwa wale wanawake walianza kumtia moyo Yusuf kwamba amtii bibi yake, na wakaanza kumfanyia njama katika hilo, lakini akapendelea jela na adhabu ya kiduniani kuliko starehe za sasa zenye kusababisha adhabu kubwa. \"Na usiponiondoshea vitimbi vya wanawake, mimi nitaelekea kwao.\" Yaani, nitaelekea kwao. Kwa maana, mimi ni dhaifu na mnyonge usiponilinda na ubaya huu, nitaelekea kwao. \"Na nitakuwa katika wajinga\" kwa maana huu ni ujinga, kwa kuwa ni kupendelea starehe ndogo ihuzunishayo kuliko starehe za mfululizo na matamanio mbalimbali katika Bustani za neema. Na anayependelea haya kuliko yale, basi ni nani mjinga zaidi yake? Kwa maana, elimu na akili vinaitia kutanguliza masilahi makubwa zaidi kati ya mawili hayo na starehe kubwa zaidi kati ya starehe mbili hizo, na hupendelea kile chenye mwisho wa kusifiwa."},{"id":2238,"sura":12,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} \"Basi Mola wake Mlezi akamwitikia\" alipomwomba dua, \"na akamwondoshea vitimbi vyao;\" kwa kuwa hakuacha kuendelea kumtaka kimapenzi na kutafuta msaada juu yake kwa njia yoyote aliyoweza kuipata mpaka akamkatisha tamaa, na Mwenyezi Mungu akamuepusha na njama zake. \"Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia yote\" anayoomba mwenye kuomba. \"Mwenye kujua yote\" ya makusudio mema na makusudio dhaifu yaliyohitaji kumzidishia msaada wake na upole wake. Basi haya ndiyo Mwenyezi Mungu alimwokoa kwayo Yusuf kutoka katika majaribio haya yaliyomzunguka na mtihani huu mkubwa."},{"id":2239,"sura":12,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} Na mabwana zake, basi habari hiyo ilipokuwa mashuhuri na ikabainika, na watu wakawa kati ya wanaokubali udhuru huo, na mwenye kulaumu, na kukashifu, \"ikawadhihirikia baada ya kuona Ishara hizo\" zinazoonyesha kutokuwa kwake na hatia, \"kuwa lazima wamfunge kwa muda.\" Yaani, ili habari hizo ziishe kwa hilo na watu wazisahau. Kwa maana, kitu kinapoenea, hakiachi kuendelea kutajwa, na kinaenea zinapokuwa sababu zake zingali zipo; lakini ikiwa sababu zake hazipo kinasahaulika. Basi waliona kwamba hilo lilikuwa ni kwa manufaa yao, kwa hivyo wakamtia gerezani."},{"id":2240,"sura":12,"from_aya":36,"to_aya":41,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"36. Na wakaingia gerezani pamoja naye vijana wawili. Mmoja wao akasema: Hakika mimi nimeota kuwa ninakamua mvinyo. Na mwingine akasema: Hakika mimi nimeota kuwa nimebeba mikate juu ya kichwa changu, na ndege wanakula kwayo. Hebu tuambie tafsiri yake, kwani sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri. 37. Akasema: hakitawajia chakula mtakachoruzukiwa isipokuwa nitawaambia hakika yake kabla ya kuwajia. Hayo ni katika yale aliyonifundisha Mola wangu Mlezi. Hakika mimi nimeacha mila ya kaumu wasiomuamini Mwenyezi Mungu, na wakawa wameikufuru Akhera. 38. Na nimefuata mila ya baba zangu, Ibrahim, na Is-haq, na Yaa'qub. Haikutufailia sisi kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote. Hiyo ni katika fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yetu na juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru. 39. Enyi wafungwa wenzangu wawili! Je, mabwana wengi tofautitofauti ni bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu? 40. Hamuabudu badala yake isipokuwa majina tu mliyowaita nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hakuna hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka. Lakini wengi wa watu hawajui. 41. Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu, yeye atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine, yeye atasulubiwa, na ndege watakula katika kichwa chake. Imekwisha katwa hukumu ya hilo jambo mlilokuwa mkiuliza. "},{"id":2241,"sura":12,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36} Yaani, \"na\" Yusuf alipoingia gerezani, \"wakaingia gerezani pamoja naye vijana wawili\" miongoni mwa wale walioingia humo. Kisha kila mmoja wao akaona ndoto, kwa hivyo wakamsimulia ndoto hizo Yusuf ili azifasiri. \"Mmoja wao akasema: Hakika mimi nimeota kuwa ninakamua mvinyo. Na mwingine akasema: Hakika mimi nimeota kuwa nimebeba mikate juu ya kichwa changu\" na mkate huo \"ndege wanakula kwayo. Hebu tuambie tafsiri yake.\" Yaani, tafsiri yake na namna mambo yao yatakavyoisha. Na kauli yao, \"kwani sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri.\" Yaani, wewe ni katika watu wafanyao mazuri kwa waja. Basi tufanyie mazuri katika kututafsiria ndoto zetu kama ulivyowafayia mazuri wasiokuwa sisi. Kwa hivyo, wakamuomba Yusuf kupitia uzuri wake."},{"id":2242,"sura":12,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37} Kwa hivyo, \"Akasema\" akiwaitikia maombi yao: \"Hakitawajia chakula mtakachoruzukiwa isipokuwa nitawaambia hakika yake kabla ya kuwajia.\" Yaani, basi mioyo yenu na itulie kwa maana nitaharakisha kufasiri ndoto zenu, na chakula chenu cha mchana au cha jioni jambo la kwanza kitakapowajia, isipokuwa nitakuwa nimewaambia hakika yake kabla ya kuwajia. Na huenda Yusuf, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikusudia kuwalingania kwenye imani katika hali hii ambayo ndani yake ilionekana haja yao, ili wito wake uwe wa kuwaathiri zaidi wa kukubaliwa zaidi nao. Kisha akasema, \"Hayo\" niliyowafasiria \"ni katika yale aliyonifundisha Mola wangu Mlezi.\" Yaani, hii ni katika elimu ya Mwenyezi Mungu aliyonifundisha na akanifanyia wema kwayo. Na hayo ni kwamba, \"Hakika mimi nimeacha mila ya kaumu wasiomwamini Mwenyezi Mungu, na wakawa wameikufuru Akhera.\" Na kuacha, kama kunavyokuwa kwa yule aliyeingia katika kitu kisha akakihama, pia kunakuwa kwa yule ambaye hakuingia humo hata kidogo. Kwa hivyo, haiwezi kusemwa kwamba Yusuf hapo awali alikuwa wa mila isiyokuwa ya Ibrahim."},{"id":2243,"sura":12,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} \"Na nimefuata mila ya baba zangu, Ibrahim, na Is-haq, na Yaa'qub\" kisha akaieleza mila hiyo kwa kauli yake \"Haikutufailia sisi.\" [Yaani, haikuwa inaendana nasi] \"kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote.\" Bali sisi tunampwekesha Mwenyezi Mungu kwa tauhidi na tunamfanyia yeye tu dini yetu na ibada. \"Hiyo ni katika fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yetu na juu ya watu.\" Yaani, hii ni katika bora zaidi miongoni mwa [neema] yake na ihsani yake juu yetu na juu ya wale ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa kama alivyotuongoa. Kwani, hakuna bora zaidi kuliko neema ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake kwa Uislamu na Dini iliyonyooka. Kwa hivyo, mwenye kuikubali na kuifuata, basi hiyo ni bahati yake, na atakuwa amepata neema kubwa zaidi na na fadhila tukufu zaidi; \"Lakini wengi wa watu hawashukuru.\" Na ndiyo maana neema na ihsani zinawajia, lakini hawazikubali na hawamtimizii Mwenyezi Mungu haki yake. Na katika hili kuna kutia moyo juu ya kushika njia ambayo yeye yuko juu yake kwa mbinu ambayo haifichiki. Kwa maana, wale vijana wawili alipokwisha jua kwamba walimuona kwa jicho la taadhima na heshima kubwa na kwamba alikuwa mwema na mwalimu, akawatajia kuwa hali hii niliyo nayo ni kwa sababu ya fadhila na ihsani ya Mwenyezi Mungu; kwa kuwa alinineemesha kwa kuacha ushirikina na kufuata mila ya baba zangu. Na kwa sababu ya haya ndio nikafikia kile mlichokiona, kwa hivyo mnapaswa kufuata kile nilichokifanya."},{"id":2244,"sura":12,"from_aya":39,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39} Kisha akawalingania kwa uwazi, akasema: \"Enyi wafungwa wenzangu wawili! Je, mabwana wengi tofautitofauti ni bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu?\" Yaani, je, mabwana wasio na uwezo na walio dhaifu ambao hawanufaishi wala hawadhuru wala hawapeani wala hawanyimi, nao wametofautiana kama vile miti, mawe, Malaika, wafu na aina nyinginezo za miungu wanayoichukua washirikina? Je, hao ndio bora au Mwenyezi Mungu ambaye ana sifa za ukamilifu, mmoja kwa dhati yake, na sifa Zake, na matendo Yake? Na Yeye hana mshirika yoyote katika lolote miongoni mwa hayo, Mwenye nguvu, ambaye vitu vyote viko chini ya nguvu zake na mamlaka yake. Kwa hivyo, chochote anachotaka, kinakuwa. Na asichotaka, hakiwi. hakuna mnyama yeyote isipokuwa amekikamata kwa nywele za mbele ya kichwa chake."},{"id":2245,"sura":12,"from_aya":40,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40} Na inavyojulikana ni kuwa yule ambaye hivyo ndivyo alivyo, na zilivyo sifa zake, ni bora zaidi kuliko miungu iliyo tofautitofauti, ambayo ni majina tu yasiyokuwa na ukamilifu wowote wala uwezo wa kutenda chochote. Na ndiyo maana akasema, \"Hamuabudu badala yake isipokuwa majina tu mliyowaita nyinyi na baba zenu.\" Yaani, mliwavalisha tu majina [na] mkawaita miungu, ilhali wao si chochote, wala hawana sifa yoyote ya uungu. \"Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote.\" Bali Mwenyezi Mungu aliteremsha uthibitisho wa kukataza kuiabudu, na kubainisha ubatili wake. Na ikiwa Mwenyezi Mungu hakuiteremshia uthibitisho wowote, hawawezi hao kuwa ndio njia wala sababu wala ushahidi kwa hilo. Kwa sababu hukumu \"ni ya mwenyezi Mungu\" peke yake. Yeye ndiye Mwenye kuamrisha na kukataza, na kutunga sheria na kutunga hukumu mbalimbali, na Yeye ndiye aliyewaamrisha \"msimuabudu yeyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka.\" Yaani, njia iliyonyooka inayofikisha kwenye kila heri. Na zisizokuwa hiyo miongoni mwa dini nyinginezo zote, hizo siyo nyoofu. Bali zilijipinda na zinafikisha kwenye kila uovu. \"Lakini wengi wa watu hawajui\" uhakika wa mambo. Vinginevyo, tofauti iliyopo kati ya kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila mshirika yeyote, na kumshirikisha ni jambo la dhahiri zaidi na bainifu zaidi kuliko mambo yote. Lakini kwa sababu ya kutokuwa na elimu kutoka kwa wengi wa watu juu ya hilo, yaliyotokea yale yaliyotokea ya ushirikina. Basi Yusuf, amani iwe juu yake, aliwalingania wale wafungwa wenzake wawili wamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kumfanyia yeye tu dini yao. Na inawezekana kwamba waliitikia na kufuata, basi neema ikatimia juu yao; na inawezekana kuwa hawakuacha kuwa katika ushirikina wao, kwa hilo hoja hiyo ikasimama juu yao."},{"id":2246,"sura":12,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41} Kisha - yeye amani iwe juu yake - akaanza kuzifasiri ndoto zao baada ya kuwaahidi hilo, akasema, \u201cEnyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu.\" Naye ni yule aliyeona kwamba anamnywesha bwana wake mvinyo. Basi yeye atatoka gerezani na kumnywesha \"bwana wake mvinyo.\" Yaani, atamnywesha mvinyo bwana wake ambaye alikuwa akimtumikia. Na hili linalazimu kwamba atatoka gerezani. \"Na ama yule mwingine\" naye ni yule aliyeona kwamba amebeba mikate juu ya kichwa changu, na ndege wanakula kwayo, \"yeye atasulubiwa, na ndege watakula katika kichwa chake\" kwa maana alifasiri mkate ule ambao ndege walikuwa wanaula kuwa ni nyama ya kichwa chake na mafuta yake na ubongo uliomo ndani yake, na kwamba hatazikwa na kuhifadhiwa kutokana na ndege. Bali atasulubishwa na kuwekwa mahali ambapo ndege wanaweza kumla. Kisha akawaambia kuwa tafsiri hii aliyowapa ni lazima itokee, kwa hivyo akasema, \"Imekwisha katwa hukumu ya hilo jambo mlilokuwa mkiuliza\"  juu ya tafsiri yake."},{"id":2247,"sura":12,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"42. Na akamwambia yule aliyejua kuwa ataokoka katika wawili hao: Nikumbuke kwa bwana wako. Lakini Shetani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake. Basi Yusuf akakaa gerezani miaka kadhaa."},{"id":2248,"sura":12,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} Yaani, Yusuf amani iwe juu yake \"Akasema\" akimwambia \"yule aliyejua kuwa ataokoka katika wawili hao\" naye ni yule aliyeona kuwa anakamua mvinyo, \"Nikumbuke kwa bwana wako.\" Yaani, mtajie mambo yangu na kisa changu, huenda akanihurumia na akanitoa katika hali niliyomo. \"Lakini Shetani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake.\" Yaani, Shetani akamsahaulisha yule aliyeokoka kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kukumbuka yale yatakayomkurubisha kwake. Na miongoni mwa hayo ni kusahau kwake kumkumbuka Yusuf ambaye alistahiki kulipwa kwa wema kamili zaidi, na hilo ni ili Mwenyezi Mungu alikamilishe jambo lake na majaliwa yake. \"Basi Yusuf akakaa gerezani miaka kadhaa\" na hiyo ni kuanzia miaka mitatu hadi tisa. Na ndiyo maana, ikasemwa kwamba alikaa humo miaka saba. Na Mwenyezi Mungu alipotaka kulikamilisha jambo lake na akaruhusu Yusuf kutoka gerezani, akaliwekea hilo sababu ya kumtoa Yusuf na kuliinua jambo lake, na kukiinua cheo chake, nayo ni ile ndoto ya mfalme."},{"id":2249,"sura":12,"from_aya":43,"to_aya":49,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"43. Na siku moja mfalme alisema: Hakika mimi nimeota ng'ombe saba wanene wanaliwa na ng'ombe saba waliokonda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu. Enyi waheshimiwa! Niambieni maana ya ndoto zangu, ikiwa nyinyi mnaweza kuagua ndoto. 44. Wakasema: Hizi ni ndoto zilizoparaganyika, wala sisi sio wenye kujua tafsiri ya ndoto hizi. 45. Hapo akasema yule aliyeokoka katika wale wawili na akakumbuka baada ya muda. Mimi nitawaambia tafsiri yake. Basi nitumeni. 46. Yusuf! Ewe mkweli! Tueleze ni nini maana ya ng'ombe saba wanene kuliwa na ng'ombe saba waliokonda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu, ili nirejee kwa watu ili wapate kujua. 47. Akasema: Mtalima miaka saba kwa juhudi. Kwa hivyo mtakachovuna,  kiwacheni katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mtachokula kwacho. 48. Kisha itakuja baadaye miaka saba ya shida itakayokula kile mlichoiwekea isipokuwa kidogo katika kile mtakachokihifadhi. 49. Kisha baada ya haya utakuja mwaka ambao katika mwaka huo watu watasaidiwa, na watakamua. "},{"id":2250,"sura":12,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0622\u064a\u0627\u062a","text":"Mungu Mwenyezi Mtukufu alipotaka kumtoa Yusuf gerezani, alimfanya Mfalme wa Misiri kuota ndoto hii ya ajabu, ambayo tafsiri yake inahusu taifa lote. Ili tafsiri yake iwe mikononi mwa Yusuf, ili fadhila yake idhihirike na ibainike elimu yake, jambo ambalo litampelekea kuinuka daraja katika nyumba hizi mbili. Na katika mipango ya Mwenyezi Mungu ni kwamba, aliyaota hayo mfalme ambaye mambo ya wale walio chini yake yanamrudia yeye; kwa sababu, masilahi yao yalifungamana naye. Na hilo ni kwamba, aliona ndoto iliyomhangaisha, kwa hivyo akawakusanya wanachuoni wa kaumu yake na wale wenye maoni miongoni mwao, na akasema:"},{"id":2251,"sura":12,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} \"Hakika mimi nimeota ng'ombe saba wanene wanaliwa na ng'ombe saba waliokonda.\" Na hili ni la kushangaza kwamba wale ng'ombe saba waliokonda ambao nguvu zilipunguka, wanawala wale ng'ombe saba walionona ambao walikuwa wana nguvu nyingi sana. \"Na\" nikaona \"mashuke saba mabichi\" yakiliwa na mashuke mengine saba makavu. \"Enyi waheshimiwa! Niambieni maana ya ndoto zangu\" kwa sababu, tafsiri ya hizo zote ni moja, na mwisho wake pia ni mmoja; \"ikiwa nyinyi mnaweza kuagua ndoto.\""},{"id":2252,"sura":12,"from_aya":44,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"44. Wakastaajabu, wala hawakumtambua uso wake; \"Na wakasema: Ni ndoto za bure.\" Yaani, ndoto ambazo hazina matokeo au tafsiri. Haya ni madai yao ya wasiyoyajua, na udhuru wao kwa yale ambayo si udhuru. Kisha wakasema: \"Na sisi si wenye kujua tafsiri ya ndoto.\" Yaani, tunatafsiri ndoto tu, lakini kuhusu ndoto zinazotoka kwa Shetani au kujiongelesha, hatuzifasiri. Walichanganya ujinga na yakini kuwa ni ndoto tu na kujipendekeza, kiasi kwamba hawakusema: Hatujui tafsiri yake! Haya ni miongoni mwa mambo ambayo hayafai kwa watu wa dini na Hijja. Hii pia ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu kwa Yusuf, amani iwe juu yake. Lau angeivuka mwanzo kabla ya kuiwasilisha kwa umma wa watu wake na wanachuoni wao, basi wasingeweza kufanya hivyo. Haikuwa na eneo hilo, lakini ilipowasilishwa mbele yao, hawakuweza kujibu, na mfalme alipendezwa nayo sana, hivyo Yusuf akavuka; walikuwa na nafasi kubwa. Huu ni mfano wa Mwenyezi Mungu kuonyesha ubora wa Adam juu ya Malaika kwa elimu baada ya kuwauliza lakini hawakujua, kisha akamuuliza Adam na akawafundisha majina ya kila kitu, hivyo kupata ongezeko la wema wake. Na kama vile wema wa mbora wa viumbe vyake, Muhammad - rehema na Amani zimshukie - itakavyodhihirika katika Kiyama, Mwenyezi Mungu atawafunulia viumbe kuombea Adam, kisha Nuhu, kisha Ibrahim, kisha Musa, kisha Yesu, amani iwe juu yao, wanaomba msamaha kwa hilo, kisha wakamjia Muhammad \u2013 rehema na amani ziwe juu yake. \u2013 Naye anasema: \u201cMimi ni kwa ajili yake.\u201d \u201cMimi ni kwa ajili yake.\u201d Basi anaomba dua kwa ajili ya watu wote, kisha anafikia ile nafasi yenye kusifika ambayo watu wa kale na wa mwisho wanamhusudu kwayo. Ametakasika ambaye wema wake ni wa hila na ambaye utoaji wake wa uadilifu na ihsani kwa wateule wake na watakatifu wake ni sahihi."},{"id":2253,"sura":12,"from_aya":45,"to_aya":45,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{45} \"Yule aliyesalimika akasema;\" yaani, kutoka kwa vijana wawili, naye ndiye aliyeona kuwa anakamua mvinyo, na ndiye Yusuf aliamrisha amkumbuke mbele ya Mola wake Mlezi, \"Na akakumbuka baada ya umati.\" Yaani, Yusuf alikumbuka yaliyompata katika tafsiri yake ya uoni wao na yale aliyompa nasaha, na akajua kwamba atawajibika kuifasiri ndoto hii baada ya muda wa miaka, hivyo akasema: \"Nitawajulisha kwa tafsiri yake, basi tuma,\" ili nimuulize Yusufu juu yake."},{"id":2254,"sura":12,"from_aya":46,"to_aya":46,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"46. \u200b\u200bBasi wakamtuma, naye akamjia. Na Yusufu hakumkemea kwa kusahau kwake, bali alisikiliza aliyomuuliza, na akamjibu juu ya hayo, na akasema: {Yusuf, ewe mkweli.\" Yaani, ni mkweli sana katika kauli na vitendo vyake. \"Tupe fatwa kuhusu ng'ombe saba wanene, wanaoliwa na saba waliokonda, na masuke saba mabichi na mengine kavu, ili niwarudie watu. ili wapate kujua.\" Kwa maana, wana hamu ya kutaka kujua usemi wake, nao ukawafanya wasistarehe."},{"id":2255,"sura":12,"from_aya":47,"to_aya":47,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{47} Basi Yusuf akawafasiri wale ng'ombe saba walionona na yale masuke saba mabichi kuwa ni miaka saba yenye rutuba, na wale ng'ombe saba waliokonda na masuke saba makavu kuwa ni miaka tasa. na utasa ni wakati kulima kunategemea juu yake, na kwamba ikiwa rutuba itatokea; mazao na mimea vilikuwa na nguvu, sura yake ilikuwa nzuri, na mazao yao yaliongezeka, na utasa ulikuwa kinyume chake. Ng'ombe ndio ambao ardhi ililimwa na mimea ilinyweshwa maji, na mashuke ya nafaka yalikuwa makubwa zaidi, na bora ya riziki. Aliyabainisha namna hii kutokana na kuwepo kwa tukio hilo, hivyo akaunganisha katika tafsiri yao usemi na marejeo ya wanayoyafanya na kuyatayarisha, kuanzia kupanga katika miaka ya uzazi hadi miaka ya tasa. Hivyo akasema: \"Utapanda mbegu muda wa miaka saba ya uvumilivu; Yaani: wanaofuatana, \"basi mnavyovuna;\" kutokana na mazao hayo, tawanyeni. Yaani, iache \"katika masikio yake\" kwa sababu imehifadhiwa kwa ajili yake na mbali na kuzingatiwa, \"isipokuwa kwa uchache tu wa mnavyokula. Yaani, pangeni [pia] chakula chenu katika miaka hii ya rutuba, kiwe kidogo; ili kile mnachoweka akiba kiongezeke, na manufaa yake na athari yake itakuzwa."},{"id":2256,"sura":12,"from_aya":48,"to_aya":48,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{48} \"Kisha inakuja baada ya hayo;\" yaani, baada ya hiyo miaka saba ya rutuba, \"taabu saba.\" Yaani, wanawake tasa, \"wanakula mnachowaruzuku.\" Yaani, watakula mlichoweka akiba, hata kiwe kingi, \"isipokuwa kidogo mnachokitia nguvu;\" yaani, wanamzuia kuwaomba."},{"id":2257,"sura":12,"from_aya":49,"to_aya":49,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{49} \"Kisha utakuja baada ya hayo; yaani, ile miaka  Saba Migumu \"mwaka ambao watu watanyewa, na humo watakama vinywaji.\" Yaani, ndani yake kuna mvua na mafuriko yatakuwa nyingi, na mawimbi yataongezeka, na vyakula vyao vikuu vitazidi mazao kiasi kwamba watakama  zabibu na mfano wake pamoja na chakula chao. Huenda dhana yake ya kuwepo mwaka huu wenye rutuba, ijapokuwa haijasemwa wazi wazi katika ndoto hiyo ya mfalme ni Kwa sababu inafahamika kutokana na [kukadiria] miaka saba ya dhiki kwamba mwaka unaofuata utaondoa shida zake. Na inavyojulikana ni kwamba ukame wenye kuendelea kwa miaka saba mfululizo hautoweki isipokuwa kwa mwaka wenye rutuba sana.  Vinginevyo, kwa kukadiria huku hakungekuwa na manufaa. Na yule mjumbe aliporudi kwa mfalme na watu, na akawajulisha kuhusu tafsiri ya Yusufu ya ndoto hiyo, walistaajabishwa na hilo, na wakafurahi kufurahi kukubwa sana."},{"id":2258,"sura":12,"from_aya":50,"to_aya":57,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"50. Na mfalme akasema: Nijieni naye! Basi mjumbe huyo alipomjia, Yusuf akasema: Rudi kwa bwana wako na umuulize wana nini wale wanawake waliojikatakata mikono yao. Hakika Mola wangu Mlezi anazijua vyema njama zao. 51. Mfalme alisema: Mlikuwa mna nini mlipomtaka Yusuf kinyume na nafsi yake? Wakasema: Hasha Lillahi (Mwenyezi Mungu apishe mbali!) Sisi hatukujua ubaya wowote kwake. Mke wa Mheshimiwa yule akasema: Sasa haki imedhihiri. Mimi ndiye niliyemtaka kinyume na nafsi yake, na hakika yeye ni katika wakweli. 52. Hayo ni ili ajue ya kwamba sikumfanyia hiyana alipokuwa hayupo, na ya kwamba Mwenyezi Mungu haziongoi njama za wahaini. 53. Nami sijitoi lawamani. Kwa hakika nafsi ni yenye kuamrisha mno mabaya, isipokuwa kile alichorehemu Mola wangu Mlezi. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu mno, Mwenye kurehemu sana. 54. Basi mfalme akasema, \"Nijieni naye, awe wangu mwenyewe hasa.\" Basi alipomsemesha, akasema, \"Hakika wewe leo umekwisha kuwa imara kwetu na umeaminika.\" 55. Yusuf akasema: Nifanye msimamizi wa hazina za nchi. Kwani hakika mimi ni mlinzi mzuri, mwenye elimu sana. 56. Basi hivyo ndivyo tulivyomuimarisha Yusuf katika ardhi, akawa anakaa humo popote anapotaka. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala hatupotezi malipo ya wafanyao mazuri. 57. Na hakika malipo ya Akhera ni bora zaidi, kwa wale walioamini na wakawa wanamcha Mungu. "},{"id":2259,"sura":12,"from_aya":50,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{50} Yeye Mtukufu anasema: \"Na mfalme akasema\" akiwaambia waliokuwa karibu naye: \"Nijieni naye.\" Yaani, Yusuf, amani iwe juu yake, kwa kumtoa gerezani na kumleta mbele yake. Basi mjumbe huyo alipomjia Yusuf na akumuamuru aje mbele ya mfalme, akakataa kuharakisha kutoka nje mpaka kutokuwa kwake na hatia kikamilifu. Na hili ni katika subira yake, na akili yake, na rai yake kamili. Kwa hivyo akamwambia mjumbe huyo: \"Rudi kwa bwana wako;\" yaani, mfalme huyo \"na umuulize wana nini wale wanawake waliojikatakata mikono yao.\u201d Yaani, muulizeni walikuwa na jambo gani na ni nini kisa chao? Kwani Jambo lao hilo liko dhahiri na wazi kabisa. \u201cHakika Mola wangu Mlezi anazijua vyema njama zao.\u201d"},{"id":2260,"sura":12,"from_aya":51,"to_aya":51,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"51. Basi wakamjia mfalme na akasema, \u201cMlikuwa mna nini mlipomtaka Yusuf kinyume na nafsi yake?\u201d Je, mliona kwake chochote cha kutia shaka? Basi wakamtoa katika hatia na \"wakasema: Hasha Lillahi (Mwenyezi Mungu apishe mbali!) Sisi hatukujua ubaya wowote kwake.\u201d Yaani, si ubaya machache wala mwingi. Basi hapo sababu iliyojengeka juu yake tuhuma hiyo ikaondoka, na hakikubakia isipokuwa kile alichokuwa nacho mke wa mheshimiwa yule. Kwa hivyo \u201cMke wa Mheshimiwa yule akasema: Sasa haki imedhihiri.\u201d Yaani, imetenganishwa na ikadhihirika baada kwamba tulikuwa tukimuwekea ubaya na tuhuma jambo lililomfanya Yusuf afungwe gerezani. \"Mimi ndiye niliyemtaka kinyume na nafsi yake, na hakika yeye ni katika wakweli\u201d katika kauli zake na kutokuwa kwake na hatia."},{"id":2261,"sura":12,"from_aya":52,"to_aya":52,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{52} \"Hiyo\" niliyokiri kwamba nilimtaka Yusuf \"ni ili ajue kwamba sikumfanyia hiyana kwa siri.\u201d Inawezekana kwamba alichomaanisha kwa hayo ni mumewe. Yaani, ili ajue kwamba nilipokiri kuwa nilimtaka Yusuf ni kwamba sikumfanyia hiyana kwa siri. Yaani, sikufanya isipokuwa kumtamani tu, wala sikukiharibu kitanda chake. Na inawezekana kwamba kinachomaanishwa na hili ni kwamba ili Yusuf ajue kwamba nilipokiri kuwa mimi ndiye niliyemtaka, na kwamba yeye ni mkweli sikumfanyia hiyana kwa siri. \u201cNa ya kwamba Mwenyezi Mungu haziongoi njama za wahaini.\u201d Kwa maana kila mhaini ni lazima hiyana yake na njama zake zimrudie yeye mwenyewe, na lazima hali yake itabainika."},{"id":2262,"sura":12,"from_aya":53,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"53. Kisha pindi maneno hayo yalipokuwa na aina fulani ya kujitakasa nafsi, na kwamba hakufanya dhambi yoyote kuhusiana na Yusuf, akarekebisha hilo, akasema, \u201cNami sijitoi lawamani.\u201d Yaani, sijitoi katika kule kumtaka kimapenzi, na azimio yangu kubwa juu ya hilo, na kuwania kwangu kukubwa juu yake, na njama zangu katika hilo. \"Kwa hakika nafsi ni yenye kuamrisha mno mabaya.\u201d Yaani, uchafu na dhambi nyingine zote. Kwa maana nafsi ni kipando cha Shetani, na kupitia hiyo ndiyo anamuingilia mwanadamu \"isipokuwa yule aliyerehemewa na Mola wangu Mlezi.\u201d Kwa hivyo akamuepusha na nafsi yake yenye kuamrisha mabaya mpaka nafsi yake ikawa tulivu kwa Mola wake Mlezi, na yenye kufuata mwenye kulingania kwenye uwongofu, na kumuasi mwenye kulingania kwenye maangamizo. Na hilo halitoki kwa nafsi yenyewe, bali ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema yake kwa mja wake. \"Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu mno, Mwenye kurehemu sana.\u201d Yaani, Yeye ni Mwenye kuwasamehe mno kwa yule anayethubutu kufanya madhambi na maasia akitubu na kurudi kwake, na ni Mwenye kurehemu sana kwa kuitikia toba yake na kumuwezesha kufanya matendo mema. Na hili ndilo lililo sahihi, kwamba haya ni katika maneno ya mke wa mheshimiwa huyo, na si katika maneno ya Yusuf. Kwa maana, muktadha uko katika maneno yake, naye Yusuf wakati huo alikuwa bado yuko gerezani kabla ya kufika hapo."},{"id":2263,"sura":12,"from_aya":54,"to_aya":54,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{54} Basi mfalme huyo na watu walipopata uhakika wa kutokuwa na hatia kabisa kwa Yusuf, mfalme akatuma mtu kumuendea Yusuf, na akasema, \u201cNijieni naye, awe wangu mwenyewe hasa.\u201d Yaani, nimfanye kuwa mahususi kwangu na aliye karibu nami. Kwa hivyo wakaja naye kwa utukufu na heshima, \u201cBasi alipomsemesha\u201d maneno yake yalimpendeza, na cheo chake kwake kikaongezeka, kwa hivyo akamwambia, \u201cHakika wewe leo umekwisha kuwa imara kwetu na umeaminika.\u201d Yaani, umeimarika, umeaminika juu ya siri mbalimbali."},{"id":2264,"sura":12,"from_aya":55,"to_aya":55,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{55} Basi Yusuf akasema, akitafuta masilahi ya uma, \u201cNifanye msimamizi wa hazina za nchi;\u201d yaani, hazina za mazao ya nchi na mavuno yake, kama mwakilishi, mlinzi na mwendeshaji. \"Kwani hakika mimi ni mlinzi mzuri, mwenye elimu sana.\u201d Yaani, mlinzi kwa yale ninayosimamia. Hakuna kinachoweza kupotea kwayo kwa kuyaweka mahali pasipokuwa pake. Na ninadhibitii vinavyoingia na vinavyotoka nje. Ninajua vyema jinsi ya kuviendesha, na kutoa, kuzuia, na kutenda vyema katika aina zote za utendaji. Na hili halikuwa kuwania kukubwa kwa Yusuf juu ya uongozi. Bali ni utashi wake tu kufikisha manufaa kwa umma. Na alijijua mwenyewe kuna anatosha hilo, na kwamba ni muaminifu, na kuhifadhi kiasi ambacho wao hawakuwa wanajua. Basi ndiyo maana, akamwomba mfalme ampe usimamizi wa hazina za nchi, kwa hivyo mfalme akamfanya kuwa msimamizi wa hazina za nchi."},{"id":2265,"sura":12,"from_aya":56,"to_aya":57,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{56-57} Yeye Mtukufu alisema: \"Basi hivyo ndivyo;\u201d yaani, kwa sababu hizi na utangulizi huu uliotajwa, \"tulivyomuimarisha Yusuf katika ardhi, akawa anakaa humo popote anapotaka\u201d katika maisha ya starehe, na neema kunjufu, na heshima pana. \u201cTunamfikishia rehema zetu tumtakaye;\u201d yaani, haya ni katika rehema ya Mwenyezi Mungu kwa Yusuf ambazo alimpa na akamuandikia. Na hilo halikufungamana tu na neema ya dunia hii. Kwani Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri. Naye Yusuf, amani iwe juu yake, ni miongoni mwa wakuu wa watenda mazuri. Basi ana mazuri katika dunia na Akhera pia ana mazuri, na ndiyo maana akasema: \"Na hakika malipo ya Akhera ni bora zaidi\u201d - kuliko malipo ya dunia \u201ckwa wale walioamini na wakawa wanamcha Mungu.\u201d Yaani, kwa yule aliyekusanya kati ya uchamungu na imani. Kwa hivyo, kwa uchamungu yanaachwa mambo yaliyoharamishwa miongoni mwa madhambi makubwa na madogo yake. Nayo imani kamili inapatikana kwa moyo kusadikisha yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha kukiaminiwa, na kufuatwa na matendo ya nyoyo na matendo ya viungo: yale ya wajibu na yale yanayopendekezwa."},{"id":2266,"sura":12,"from_aya":58,"to_aya":68,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"58. Wakaja ndugu zake Yusuf, na wakaingia alimokuwa. Yeye akawajua, na wao hawakumjua. 59. Na alipowatengenezea tayari haja yao, alisema: Nileteeni ndugu yenu wa kwa baba yenu. Je, hamuoni ya kwamba mimi hakika ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa wanaokirimu? 60. Na msiponijia naye, basi hamtapata kipimo chochote kwangu, wala msinikaribie. 61. Wakasema: Sisi tutamrai baba yake juu yake, na bila ya shaka tutafanya hilo. 62. Na Yusuf akawaambia watumishi wake: Tieni bidhaa zao katika mizigo yao, ili wazione watakaporudi kwa watu wao ili wapate kurejea tena. 63. Basi waliporejea kwa baba yao, walisema: Ewe baba yetu! Tumenyimwa chakula zaidi. Basi muachilie ndugu yetu pamoja nasi ili tupate kupimiwa. Nasi hakika tutamlinda. 64. Je, niwaamini juu yake isipokuwa kama nilivyowaamini kwa nduguye zamani? Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora zaidi wa kulinda, naye ndiye Mbora zaidi wa wanaorehemu. 65. Na walipofungua mizigo yao, wakakuta bidhaa zao wamerudishiwa. Wakasema: Ewe baba yetu! Tutake nini zaidi? Hizi bidhaa zetu tumerudishiwa. Wacha tuwaletee watu wetu chakula, na tutamlinda ndugu yetu, na tutaongeza shehena ya ngamia. Na hicho ni kipimo kidogo. 66. Akasema: Sitamuachilia pamoja nanyi mpaka mnipe agano kwa Mwenyezi Mungu kwamba lazima mtanijia naye isipokuwa ikiwa mtazungukwa. Basi walipompa agano yao, alisema: Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa tuyasemayo. 67. Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie kupitia mlango mmoja, bali ingieni kwa kupitia milango tofautitofauti. Wala mimi siwafai kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Hukumu haiko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu tu. Juu yake Yeye mimi nimetegemea, na juu yake Yeye na wategemee wanaotegemea. 68. Na walipoingilia pale alipowaamrisha baba yao, hakuwa wa kuwafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa ni haja tu iliyokuwa katika nafsi ya Yaa'qub aliyoitimiza. Na hakika yeye alikuwa na elimu kwa sababu tulimfundisha, lakini wengi wa watu hawajui. "},{"id":2267,"sura":12,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0622\u064a\u0627\u062a","text":"Yaani, Yusuf - amani iwe juu yake - aliposimamia hazina za nchi, aliziendesha kwa uendeshaji mzuri zaidi, kwa hivyo akapanda mazao mengi sana katika nchi yote ya Misri katika miaka ya rutuba, na akayatengenezea maghala makubwa, na akakusanya kutoka kwa watu kiasi kingi cha chakula na akavihifadhi na akavidhibiti kudhibiti kamili. Na miaka ya ukame ilipoingia, na ukaenea ukame huo mpaka Palestina, ambako Yaaqub na wanawe walikuwa wanakaa, Yaaqub akawatuma wanawe ili waende watafute chakula huko Misri."},{"id":2268,"sura":12,"from_aya":58,"to_aya":58,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"58. Basi wakaja \u201cndugu zake Yusuf, na wakaingia alimokuwa. Yeye akawajua, na wao hawakumjua.\u201d"},{"id":2269,"sura":12,"from_aya":59,"to_aya":59,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{59} \"Na alipowatengenezea tayari haja yao\u201d Yaani aliwapimia kama alivyokuwa anawapimia wengine. Na ulikuwa katika uendeshaji wake mzuri kwamba hampimii kila mmoja zaidi ya shehena nzima ya ngamia mmoja. Na alikuwa amewauliza kuhusu hali yao, nao wakamwambia kwamba walikuwa na kaka fulani huko kwa baba yake, naye alikuwa Binyamini, kwa hivyo akawaambia: \"Nileteeni ndugu yenu wa kwa baba yenu\u201d Kisha akawahimiza wamjie naye, akasema: \u201cHamuoni ya kwamba mimi hakika ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa wanaokirimu?\u201d Yaani katika kuwakaribisha wageni kwa ukarimu."},{"id":2270,"sura":12,"from_aya":60,"to_aya":60,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"60. Kisha akawatishia wasipokuja naye, akasema: \"Na msiponijia naye, basi hamtapata kipimo chochote kwangu, wala msinikaribie\u201d na hilo ni kwa sababu alijua ya kwamba watalazimika kumjia, kwamba hilo litawafanya waje naye."},{"id":2271,"sura":12,"from_aya":61,"to_aya":61,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{61} Wakasema: \"Sisi tutamrai baba yake juu yake\u201d Hili linaashiria kuwa Yaaqub, amani iwe juu yake, alikuwa akimpenda sana, wala hakuwa na subira juu ya kuwa mbali naye, na alikuwa akijifariji naye baada ya Yusuf, na ndiyo maana alihitaji kuraiwa juu ya kumuachilia aende pamoja nao. \u201cNa bila ya shaka tutafanya hilo\u201d ulilotuamrisha kufanya."},{"id":2272,"sura":12,"from_aya":62,"to_aya":62,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"62. Yusuf \u201cakawaambia watumishi wake\u201d waliokuwa wakimtumikia, \u201cTieni bidhaa zao.\u201d Yaani, thamani waliyolipa ili kununua kwayo chakula hicho, \"katika mizigo yao, ili wazione\u201d baada ya hayo ndani ya mizigo yao \"ili wapate kurejea tena\u201d kwa sababu ya kuona ugumu katika kuzichukua, kulingana na ilivyosemwa. Lakini la dhahiri ni kwamba alitaka kuwatia moyo kwamba atawatendea ihsani katika kuwapimia kipimo kamili, kisha kuwarudishia bidhaa zao kwa njia ambayo hawawezi kuhisi wala kutambua kilichokuwa kinakuja. Kwa maana kumfanyia mtu ihsani kunamlazimu yeye kumtimizia yule aliyemfanyia ihsani hiyo."},{"id":2273,"sura":12,"from_aya":63,"to_aya":63,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{63} \u201cBasi waliporejea kwa baba yao, walisema: Ewe baba yetu! Tumenyimwa chakula zaidi.\u201d Yaani: Ikiwa hutamuachilia ndugu yetu kwenda pamoja nasi. \u201cBasi muachilie ndugu yetu pamoja nasi ili tupate kupimiwa.\u201d Yaani, ili hilo liwe sababu sisi kupimiwa. Kisha wakamuahidi kumhifadhi, wakasema: \"Nasi hakika tutamlinda\u201d kutokana na kufikiwa na chochote anachochukia."},{"id":2274,"sura":12,"from_aya":64,"to_aya":64,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{64} Yaaqub amani iwe juu yake akawaambia: \u201cJe, niwaamini juu yake isipokuwa kama nilivyowaamini kwa nduguye zamani?\u201d Yaani, mlikwisha tangulia hapo awali kuweka ahadi kubwa kuliko hii kuhusiana na kumhifadhi Yusuf, lakini pamoja na hayo, hamkutimiza yale mliyofunga ahadi nayo kwa msisitizo, kwa hivyo siamini ahadi yenu na ulinzi wenu, lakini ninamwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu. \"Kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mbora zaidi wa kulinda, naye ndiye Mbora zaidi wa wanaorehemu.\u201d Yaani, anaijua hali yangu na nataraji kwamba atanirehemu, hivyo atamlinda na kumrudisha kwangu. Na ni kana kwamba kwa maneno haya alikuwa ameshakubali kumuachilia akwende pamoja nao."},{"id":2275,"sura":12,"from_aya":65,"to_aya":65,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"65. Basi \u201cwalipofungua mizigo yao, wakakuta bidhaa zao wamerudishiwa\u201d Huu ni ushahidi kwamba walikuwa wanajua kuwa Yusuf aliwarudishia kwa makusudi, na kwamba alitaka kuwapa hizo bidhaa kama mali. Kwa hivyo, wakamwambia baba yao wakimhimiza amuachilie ndugu yao pamoja nao: \"Ewe baba yetu! Tutake nini zaidi?\u201d Yaani, tutake kitu gani baada ya ukarimu huu mzuri, kwani alitupimia kwa ukamilifu na akaturudishia bidhaa zetu kwa njia [hii] njema inayojumuisha ikhlasi na maadili mema? \"Hizi bidhaa zetu tumerudishiwa. Wacha tuwaletee watu wetu chakula.\u201d Yaani: tukienda na ndugu yetu, itakuwa ni sababu ya yeye kutupimia, na tutawajia watu wetu na chakula kikuu wanchohitaji sana, \"na tutamlinda ndugu yetu, na tutaongeza shehena ya ngamia\u201d kwa kumuachilia aende pamoja nasi. Kwani yeye humpimia kila mtu shehena ya ngamia mmoja. \u201cNa hicho ni kipimo kidogo.\u201d Yaani, ni kipimo chepesi ambacho hakikudhuru. Kwa maana muda hautakuwa mrefu, na masilahi tayari yameshabainika."},{"id":2276,"sura":12,"from_aya":66,"to_aya":66,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{66} Yaaqub akawaambia, \u201cSitamuachilia pamoja nanyi mpaka mnipe agano kwa Mwenyezi Mungu.\u201d Yaani, agano nzito, na muape kwa Mwenyezi Mungu kwamba, \u201clazima mtanijia naye isipokuwa ikiwa mtazungukwa.\u201d Yaani: isipokuwa ikiwa mtapatwa na jambo ambalo hamna uwezo nalo, wala hamuwezi kulizuia. \"Basi walipompa agano yao\u201d kwa mujibu wa aliyoyasema na alivyotaka; \"Akasema: Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa tuyasemayo.\u201d Yaani, unatutosha ushuhuda Wake juu yetu, na ulinzi Wake, na dhamana Yake."},{"id":2277,"sura":12,"from_aya":67,"to_aya":67,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{67}. Basi alipomuachilia kwenda pamoja nao; akawausia watakapofika Misri, wasiingilie \u201ckupitia mlango mmoja, bali ingieni kwa kupitia milango tofautitofauti.\u201d Na hilo ni kwa sababu aliwahofia kijicho kwa sababu ya wingi wao na uzuri wa mandhari yao. Kwa sababu wao ni watoto wa mtu mmoja, na hii ndiyo sababu, \u201cna\u201d kama sivyo \u201csiwafai kitu mbele ya Mwenyezi Mungu\u201d  kwani majaliwa hayana budi kuwa. \"Hukumu haiko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu tu;\" yaani, hukumu ni yake, na amri ni amri yake. Kwa hivyo anachopitisha na akahukumu, basi lazima kitokee. \"Juu yake Yeye mimi nimetegemea;\u201d yaani, nimemtegemea Mwenyezi Mungu, si juu ya ile sababu yangu niliyowausia nayo. \"Na juu yake Yeye na wategemee wanaotegemea.\u201d Kwani kwa kumtegemea, kila linalotarajiwa linapatikana, na kila linalohofiwa linazuiliwa."},{"id":2278,"sura":12,"from_aya":68,"to_aya":68,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{68}. \u201cNa\u201d walipokwenda na \u201cwakaingilia pale alipowaamrisha baba yao, hakuwa\u201d kwa kitendo hicho \u201cakiwafaa kitu isipokuwa ni haja tu iliyokuwa katika nafsi ya Yaa'qub aliyoitimiza.\u201d Na hilo lilimlazimu kwa sababu ya huruma kubwa yake na upendo kwa watoto, kwa hivyo kwa hilo akapata kutulia na kutimiza kile kilicho katika fikira zake. Na huu haukuwa upungufu katika elimu yake. Kwani yeye ni miongoni mwa Mitume watukufu na wenye elimu wanaomuabudu Mwenyezi Mungu tu, na ndiyo maana akasema kumhusu: \"Na hakika yeye alikuwa na elimu;\u201d yaani, ana elimu nyingi, \"kwa sababu tulimfundisha,\" na si kutokana na uwezo wake na nguvu yake ndiyo aliyajua hayo. Bali ni kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na kufundisha kwake. \"Lakini wengi wa watu hawajui\u201d mwisho wa mambo na undani wa mambo. Na vile vile wanachuoni miongoni mwao, inafichikana kwao elimu nyingi, na hukumu zake na athari zake."},{"id":2279,"sura":12,"from_aya":69,"to_aya":79,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"69. Na walipoingia alimokuwa Yusuf, alimkumbatia nduguye na akasema: Mimi hakika ndiye yule nduguyo. Basi usihuzunike kwa yale waliyokuwa wakiyafanya. 70. Na alipokwisha watayarishia mahitaji yao, akakitia kikopo cha kunywea maji katika mzigo wa nduguye huyo, kisha mwenye kunadi akanadi: Enyi msafara! Hakika nyinyi ni wezi! 71. Wakasema huku wamegeuka kuwaelekea, \u201cKwani mmepoteza nini?\u201d 72. Wakasema: Tumepoteza kopo la mfalme. Na atakayenijia nalo, atapewa shehena nzima abebayo ngamia. Nami ni mdhamini juu ya hilo. 73. Wakasema: Tallahi! Hakika mlikwisha jua vyema kwamba sisi hatukuja kufanya uharibifu katika nchi hii, wala sisi si wezi. 74. Wakasema: Basi malipo yake ni nini ikiwa nyinyi ni waongo? 75. Wakasema: Malipo yake ni kwamba yule ambaye litapatikana katika shehena naye, basi huyo ndiye malipo yake. Hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu. 76. Basi akaanza na mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha akalitoa katika mzigo wa nduguye. Hivyo ndivyo tulivyompangia njama Yusuf. Hakuwa ni wa kumzuia nduguye kwa sheria ya mfalme huyo isipokuwa Mwenyezi Mungu akitaka. Tunamuinua daraja tumtakaye. Na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi. 77. Wakasema: Akiwa ameiba huyu, basi hakika nduguye vile vile aliiba hapo zamani. Lakini Yusuf akaliweka hilo kisiri katika moyo wake wala hakulionyesha kwao. Akasema: Nyinyi ndio mko katika pahali paovu zaidi, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi hayo mnayosingizia. 78. Wakasema: Ewe Mheshimiwa! Hakika huyu anaye baba mzee sana. Kwa hivyo mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri. 79. Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipokuwa yule tuliyemkuta naye kitu chetu. Hakika, basi tutakuwa ni wenye kudhulumu. "},{"id":2280,"sura":12,"from_aya":69,"to_aya":69,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{69} Yaani: ndugu zake Yusuf walipoingia alimokuwa Yusuf; \"alimkumbatia nduguye\u201d Yaani: ndugu yake wa kwa baba na mama, Binyamin, ambaye aliwaamuru waje naye, na akamtenga kutoka miongoni mwa ndugu zake, na akamjulisha uhakika wa mamb. Na \u201cakasema, \u2018Mimi hakika ndiye yule nduguyo. Basi usihuzunike kwa yale waliyokuwa wakiyafanya\u201d kwa sababu mwisho bora ni wetu. Kisha akamwambia kile alichotaka kufanya na hila atakayofanya ili abakie hapo kwake mpaka jambo hilo liishe."},{"id":2281,"sura":12,"from_aya":70,"to_aya":70,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{70} \"Na alipokwishawa tayarishia mahitaji yao;\u201d yaani, alimpimia kila mmoja wa ndugu zake, na miongoni mwao alikuwa ni ndugu yake huyu, \"akakitia kikopo cha kunywea maji\u201d nacho ni chombo kinachotumika kunywea maji na kupimia \u201ckatika mzigo wa nduguye huyo kisha\u201d wakaifunga mizigo yao hiyo. Na walipoondoka wakienda \u201cmwenye kunadi akanadi: Enyi msafara! Hakika nyinyi ni wezi!\u201d Na Huenda mwenye kunadi huyu hakujua uhakika wa jambo hilo."},{"id":2282,"sura":12,"from_aya":71,"to_aya":71,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{71} \"Wakasema\"; yaani, Ndugu zake Yusuf, \u201chuku wamegeuka kuwaelekea\" ili kuondoa tuhuma yoyote. Kwa maana, mwizi huwa hana hima kubwa zaidi isipokuwa kuondoka na kwenda mbali na yule aliyemuibia, ili kile alichoiba kiwe salama naye. Nao hawa walikuja huku wamewaelekea, na hawakuwa na hima yoyote isipokuwa kujiondolea tuhuma hiyo ambayo walitupiwa. Kwa hivyo wakasema katika hali hii: \"Kwani mmepoteza nini?\u201d Na hawakusema: Ni nini tumeiba? Kwa sababu ya uhakika wao kwamba hawana hatia yoyote ya wizi."},{"id":2283,"sura":12,"from_aya":72,"to_aya":72,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{72} \u201cWakasema: tumepoteza kopo la mfalme. Na atakayenijia nalo, atapewa shehena nzima abebayo ngamia.\u201d Kama malipo yake ya kulipata. \"Nami ni mdhamini juu ya hilo\u201d na haya aliyasema huyo mwenye kunadi aliyekuwa anakagua."},{"id":2284,"sura":12,"from_aya":73,"to_aya":73,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{73} \u201cWakasema: Tallahi! Hakika mlikwisha jua vyema kwamba sisi hatukuja kufanya uharibifu katika nchi hii\u201d kwa kila aina ya maasia, \u201cwala sisi si wezi.\u201d Kwa maana wizi ni katika aina kubwa zaidi ya uharibifu katika ardhi. Na waliapa kwa sababu ya kujua kwao kwamba wao si waharibifu wala wezi. Kwa sababu walijua kwamba walichunguza hali zao kile kinachoashiria usafi wao na uchamungu wao, na kwamba jambo hili haliwezi kutokea kwao kwa kujua kwa wale wanaowatuhumu. Na hii ndiyo mbinu ya ufasaha zaidi katika kukanusha tuhuma kuliko kama wangesema: Tallahi hatujafanya uharibifu katika ardhi, wala hatukuiba."},{"id":2285,"sura":12,"from_aya":74,"to_aya":74,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{74} \u201cWakasema: Basi malipo yake ni nini\u201d yaani malipo ya kitendo hiki. \"Ikiwa nyinyi ni waongo?\u201d Na kikapatikana pamoja nanyi."},{"id":2286,"sura":12,"from_aya":75,"to_aya":75,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{75} \u201cWakasema: Malipo yake ni kwamba yule ambaye litapatikana katika shehena naye, basi huyo ndiye malipo yake.\u201d Kwa namna ya kwamba yule aliyeibiwa amumiliki mwizi huyo. Na hili lilikuwa katika dini yao, kwamba mwizi inapothibitika kuwa ameiba, basi nakuwa ni miliki ya yule aliyeibiwa mali hiyo, na ndiyo maana wakasema, \u201cHivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu.\u201d"},{"id":2287,"sura":12,"from_aya":76,"to_aya":76,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{76} Basi mkaguzi huyo akaanza na mizigo yao kabla ya mzigo wa ndugu yake, ili iondoke shaka ya kufikiriwa kwamba hilo lilifanywa kimakusudi. Na wakati hakupata chochote katika mizigo yao, \"akalitoa katika mzigo wa nduguye\u201d na hakusema: alilipata au ndugu yake aliliiba, kwa kuzingatia ukweli halisi. Basi hapo Yusuf akatimiza alichotaka kwamba ndugu yake abaki pamoja naye kwa njia ambayo ndugu zake hawawezi kuhisi. Akasema Yeye Mtukufu: \"Hivyo ndivyo tulivyompangia njama Yusuf\u201d Yaani, tulimrahisishia njama hii, ambayo kwayo alifikia jambo ambalo si la kulaumiwa. \"Hakuwa ni wa kumzuia nduguye kwa sheria ya mfalme huyo\u201d kwa sababu si katika sheria yake kuwa mwizi amilikiwe, bali wao wana malipo mengine. Na ikiwa hukumu ya hilo ingerudishwa katika sheria ya mfalme huyo, basi Yusuf hangeweza kumbakisha nduguye pamoja naye, lakini alifanya wao wenyewe wapitishe hukumu hiyo ili kitimie kile alichotaka. Yeye Mtukufu alisema \"Tunamuinua daraja tumtakaye\u201d kwa elimu yenye manufaa na kujua njia zinazofikisha kwenye makusudio yake, kama tulivyoinua daraja za Yusuf. \"Na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi.\u201d Kwa hivyo, kila ajuaye juu yake kuna yule ambaye anajua zaidi yake mpaka elimu yote iishie kwa Mwenye kujua ya ghaibu na yanayoonekana."},{"id":2288,"sura":12,"from_aya":77,"to_aya":77,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"77. Basi ndugu zake Yusuf walipoona yale waliyoona; \"Wakasema: Akiiba huyu\u201d ndugu yetu, basi hili si jambo geni kwake, \"basi hakika nduguye vile vile aliiba hapo zamani\u201d wakimaanisha Yusuf, amani iwe juu yake, na makusudio yao kwa hilo ni kujiondoa lawamani, na kwamba huyu na nduguye wanaweza kuiba, na wao si ndugu zetu wa kwa baba na mama. Na katika hili kuna kuwapuuza kukubwa, na ndiyo maana \"Yusuf akaliweka hilo kisiri katika moyo wake wala hakulionyesha kwao.\u201d Yaani, hakuwajibu kwa sababu ya hayo waliyoyasema kwa wanayoyachukia, bali aliizuia hasira yake na akalificha jambo hilo ndani ya nafsi yake, na \u201cakasema\u201d katika nafsi yake \u201cNyinyi ndio mko katika hali paovu zaidi\u201d kwa kuwa mmetushutumu kwa yale ambayo nyinyi mko katika yaliyo maovu zaidi yake. \"Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi hayo mnayosingizia\u201d kuhusiana nasi kwa wizi mnaotutuhumu kwao ambao Mwenyezi Mungu anajua kwamba hatuna hatia yoyote katika hilo."},{"id":2289,"sura":12,"from_aya":78,"to_aya":78,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{78} Kisha wakampitisha katika njia ya kubembeleza ili huenda atamuachilia ndugu yao kwenda pamoja nao, kwa hivyo \u201cWakasema: Ewe Mheshimiwa! Hakika huyu anaye baba mzee sana.\u201d Yaani, huyo baba yake mzee hawezi kuwa na subira ya kukaa mbali naye, na itakuwa vigumu kwake kuachana naye. \"Kwa hivyo mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri.\u201d Basi tufanyie mazuri sisi na baba yetu kwa hilo."},{"id":2290,"sura":12,"from_aya":79,"to_aya":79,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{79} Kwa hivyo, Yusuf akasema: \"Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipokuwa yule tuliyemkuta naye kitu chetu.\u201d Yaani, hii ni dhuluma juu yetu ikiwa tutamchukua asiye na hatia kwa dhambi ya yule tuliyempata naye vitu vyetu, na hapa hakusema: aliyeiba. Haya yote, alikuwa anajaribu kujiweka mbali na uwongo. \"Hakika;\" Yaani, tukimchukua asiyekuwa yule tuliyevikuta vitu vyetu katika mizigo yake, basi \"tutakuwa ni wenye kudhulumu\" kwa kuwa tutakuwa tumeweka adhabu pasipokuwa mahali pake."},{"id":2291,"sura":12,"from_aya":80,"to_aya":83,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"80. Basi walipokata tamaa naye, wakenda kando kunong'ona. Mkubwa wao akasema: Je! Hamjui ya kwamba baba yenu amechukua ahadi kutoka kwenu kwa Mwenyezi Mungu, na kabla ya hapo namna mlivyokosa katika agano lenu juu ya Yusuf? Basi mimi sitatoka nchi hii mpaka baba yangu anipe ruhusa au Mwenyezi Mungu anihukumie. Na Yeye ndiye Mbora wa mahakimu. 81. Rudini kwa baba yenu, na mwambieni: Ee baba yetu! Hakika mwanao ameiba. Na sisi hatutoi ushahidi isipokuwa kwa tunayoyajua. Wala sisi hatukuwa wenye kuhifadhi mambo ya ghaibu. 82. Na uliza mji tuliokuwamo, na msafara tuliokuja nao. Na hakika sisi ni wakweli. 83. Akasema: Bali nafsi zenu zimewashawishi kwenye jambo fulani. Basi subira ni nzuri! Huenda Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja. Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima. "},{"id":2292,"sura":12,"from_aya":80,"to_aya":80,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{80} Yaani, ndugu zake Yusuf walipokata tamaa juu ya Yusuf kuwaruhusu kumchukua ndugu yao, \u201cwakaenda kando kunong'ona.\u201d Yaani, walikusanyika peke yao, na hakuna mtu mwingine asliyekuwa pamoja nao, na wakaanza kunong'onezana wao kwa wao. Kisha \"Mkubwa wao akasema: Je! Hamjui ya kwamba baba yenu amechukua ahadi kutoka kwenu kwa Mwenyezi Mungu\u201d kwamba mtamlinda na kwamba mtakuja naye isipokuwa ikiwa atazungukwa. \"Na kabla ya hapo namna mlivyokosa katika agano lenu juu ya Yusuf?\u201d Basi wakawakusanyikia Mambo mawili haya: kutotomiza kwenu agano kulikotangulia kuhusiana na Yusuf, na kushindwa kwenu kumleta ndugu yenu kulikofuata huku. Basi mimi Sina uso nitakaokabiliana nao baba yangu. \"Basi mimi sitatoka nchi hii;\u201d yaani, nitakaa katika nchi hii bila ya kuondoka humo, \u201cmpaka baba yangu anipe ruhusa au Mwenyezi Mungu anihukumie.\u201d Yaani, aniandikie kuja nyumbani peke yangu au pamoja na ndugu yangu, \"Na Yeye ndiye Mbora wa mahakimu.\u201d"},{"id":2293,"sura":12,"from_aya":81,"to_aya":81,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{81} Kisha akawausia yale watakayomwambia baba yao, akasema: \u201cRudini kwa baba yenu, na mwambieni: Ee baba yetu! Hakika mwanao ameiba.\u201d Yaani, akachukulia kwa sababu ya wizi wake na hatukufanikiwa kuja naye kwako pamoja na juhudi tulizoziweka katika hilo, na hali ni kwamba hatukushuhudia kitu tusichokijua, bali tulishuhudia tu yale tuliyoyajua. Kwa sababu tuliuona kopo likitolewa katika shehena yake. \"Wala sisi hatukuwa wenye kuhifadhi mambo ya ghaibu;\u201d yaani, lau tungekuwa tunaijua ghaibu, basi hatungewania mno na kufanya juhudi kuwa aende pamoja nasi, na hatungelipokupa ahadi zetu na maagano yetu, na hatukudhani jambo hili lingefikia namna lilivyofikia."},{"id":2294,"sura":12,"from_aya":82,"to_aya":82,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{82} \"Na uliza\" ikiwa una shaka na kauli yetu \"Mji tuliokuwamo na msafara tuliokuja nao.\u201d Hao waliona haya tuliyokuambia, \u201cNa hakika sisi ni wakweli\u201d wala hatukudanganya, wala hatukugeuza, wala hatukubadilisha, wala bali hii ndiyo hali halisi."},{"id":2295,"sura":12,"from_aya":83,"to_aya":83,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{83}. Basi waliporudi kwa baba yao na kumwambia habari hii, huzuni yake ikazidi na dhiki yake ikaongezeka maradufu, na akawatuhumu tena katika suala hili kama alivyowatuhumu katika lile la kwanza, na \"Akasema: Bali nafsi zenu zimewashawishi kwenye jambo fulani. Basi subira ni nzuri!\u201d Yaani, ninakimbilia juu ya hayo kwenye subira nzuri ambayo haiambatani na hasira, wala kupapatika, wala kuwalalamikia viumbe. Kisha akakimbilia katika kutafuta faraja wakati alipoona kwamba jambo hilo limekuwa kali sana na dhiki yake imekuwa mbaya zaidi, kwa hivyo akasema: \"Huenda Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja.\u201d Yaani, Yusuf, Binyamin, na yule ndugu yao mkubwa ambaye aliamua kukaa Misri. \"Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema\u201d ambaye anaijua hali yangu na haja yangu ya faraja yake na neema yake na dharura yangu juu ya ihsan yake \"Mwenye hekima.\" Ambaye alikiwekea kila kitu kipimo, na akaliwekea kila jambo mwisho wake kulingana na kile hekima Yake ya kiungu inahitaji."},{"id":2296,"sura":12,"from_aya":84,"to_aya":86,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"84. Naye akajitenga nao, na akasema: Ah! Huzuni wangu kubwa juu ya Yusuf! Na macho yake yakawa meupe kutokana na huzuni, na aliizuia bila ya kuidhirisha. 85. Wakasema: Tallahi! Huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa sana au uwe katika walioangamia. 86. Akasema: Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu tu sikitiko langu na huzuni wangu. Na ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi. "},{"id":2297,"sura":12,"from_aya":84,"to_aya":84,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{84} Yaani, Yaaqub, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akajitenga na wanawe baada ya wao kumwambia habari hii, na huzuni yake ikazidi, na macho yake yakawa meupe kutokana na huzuni ambayo iko moyoni mwake na mfadhaiko uliosababishia kulia sana, kwani macho yake yalikuwa meupe kutokana na hayo; \"na aliizuia bila ya kuidhirisha.\u201d Yaani, moyo wake ulijaa huzuni nyingi, \"Na akasema: Huzuni wangu kubwa juu ya Yusuf!\u201d Yaani ulimdhihirikia ule huzuni mkubwa wa zamani uliokuwa umefichika ndani yake, na pia shauku ya kudumu, na msiba huu mwepesi ukilinganishwa na ule wa kwanza ukamkumbusha ule msiba wa kwanza."},{"id":2298,"sura":12,"from_aya":85,"to_aya":85,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{85} Basi wanawe wakamwambia huku wakishangazwa na hali yake: \"Tallahi! Huachi kumkumbuka Yusuf;\u201d yaani, hutaacha kuendelea kumkumbuka Yusuf katika hali zako zote, \"mpaka uwe mgonjwa sana.\u201d Yaani, mpaka usiishe na usiweze hata kusonga wala kuzungumza \"au uwe katika walioangamia.\u201d Yaani, hautaacha kumkumbuka abadan maadamu bado unaweza kumkumbuka."},{"id":2299,"sura":12,"from_aya":86,"to_aya":86,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{86} Kisha Yakub akasema: \"Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu tu sikitiko langu na huzuni wangu.\u201d Yaani, yale maneno ninayoyadhihirisha na ule huzuni ulio katika moyo wangu. \"Kwa mwenyezi Mungu\" peke yake, si kwenu nyinyi wala kwa wasiokuwa nyinyi miongoni mwa viumbe vinginevyo. Basi semeni mtakalo, \"Na ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi\u201d kwamba atanirudishia hao wote, na yatafurahia macho yangu kwa kukutana nao."},{"id":2300,"sura":12,"from_aya":87,"to_aya":92,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"87. Enyi wanangu! Nendeni mumtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu makafiri. 88. Basi walipoingia alimokuwa Yusuf, wakasema: Ewe Mheshimiwa! Imetupata shida kubwa, sisi na ahali zetu. Na tumekujia na mali kidogo. Basi tutimizie tu kipimo na tupe sadaka. Hakika Mwenyezi Mungu huwalipa watoao sadaka. 89. Akasema: Je, mnajua yale mliyomfanyia Yusuf na nduguye mlipokuwa wajinga? 90. Wakasema: Kumbe hakika wewe ndiye Yusuf? Akasema: Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni ndugu yangu. Mwenyezi Mungu ametufanyia hisani. Hakika anayemcha Mungu na akasubiri, basi Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri. 91. Wakasema: Tallahi! Mwenyezi Mungu amekufadhilisha wewe kuliko sisi, na hakika sisi tulikuwa wenye kukosa. 92. Akasema: Leo hakuna lawama yoyote juu yenu. Mwenyezi Mungu atawasamehe, naye ni Mwingi wa kurehemu kuliko wote wanaorehemu. "},{"id":2301,"sura":12,"from_aya":87,"to_aya":87,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{87} Yaaqub, amani iwe juu yake, aliwaambia wanawe: \u201cEnyi wanangu! Nendeni mumtafute Yusuf na nduguye.\u201d Yaani, fanyeni hima na jitahidini kuwatafuta, \"wala msikate tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu\u201d kwa maana matumaini yanamlazimu mja kuwania na kujitahidi katika yale anayoyatarajia, na kukata tamaa kunamsababishia kuzembea na kufanya polepole. Na kitu kilicho bora zaidi ambacho waja wa Mwenyezi Mungu wanafaa kukitumaini ni fadhila yake, na ihsan yake na rehema yake, na faraja yake. \"Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu makafiri.\u201d Kwa kuwa, kwa sababu ya ukafiri wao wanaona kuwa rehema yake iko mbali, na kweli rehema yake iko mbali nao. Kwa hivyo msijifananishe na makafiri. Na hili lilionyesha kwamba matumaini ya mja juu ya rehema na faraja ya mja huwa kulingana na imani yake."},{"id":2302,"sura":12,"from_aya":88,"to_aya":88,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{88} Kwa hivyo, wakaenda, na walipoingia alimokuwa Yusuf, \u201cwakasema\u201d huku wamemnyenyekea \u201cEwe Mheshimiwa! Imetupata shida kubwa, sisi na ahali zetu. Na tumekujia na mali kidogo. Basi tupimie kipimo na tupe sadaka. Na tumekujia na mali kidogo.\u201d Yaani, mali duni inayotolewa bila ya kuitamani hata na haichukuliwi kama ni kitu chochote. \"Basi tutimizie tu kipimo;\u201d yaani, pamoja na kwamba thamani yake haitoshi, na tupe sadaka pia kwa kutuongezea zaidi ya inavyostahiki. \"Hakika Mwenyezi Mungu huwalipa watoao sadaka.\u201d Kwa malipo ya hapa duniani na Akhera."},{"id":2303,"sura":12,"from_aya":89,"to_aya":89,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{89} Na jambo hilo lilipokwisha na kufikia kilele chake, Yusuf akafanya huruma mkubwa sana kwao, na akajitambulisha kwao na akawalaumu, akasema: \"Je, mnajua yale mliyomfanyia Yusuf na nduguye?\u201d Ama Yusuf, basi ni dhahiri mno kile walichomfanyia, na ama nduguye, basi landa huenda - na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi \u2013 ni kauli yao, \" Akiwa ameiba huyu, basi hakika nduguye vile vile aliiba hapo zamani.\u201d Au ni kwamba sababu iliyomtenganisha yeye na baba yake wao ndio walikuwa sababu yake na msingi uliosababisha hilo \"mlipokuwa wajinga?\u201d Na hii ni aina fulani ya udhuru aliowakubalia kwa sababu ya ujinga wao au karipio kwao kwa kuwa walifanya kitendo cha wajinga, pamoja na kwamba hakiwafaili wala hakiendani nao."},{"id":2304,"sura":12,"from_aya":90,"to_aya":90,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{90}. Basi wakajua kwamba huyo aliyewaongelesha ni Yusuf, kwa hivyo wakasema: \"Kumbe hakika wewe ndiye Yusuf? Akasema: Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni ndugu yangu. Mwenyezi Mungu ametufanyia hisani.\u201d Kwa imani na uchamungu na kutuimarisha katika dunia. Na hayo ni kwa sababu ya subira na uchamungu, kwani \"Hakika anayemcha Mungu na akasubiri.\u201d Yaani, mwenye kujiepusha kufanya yale yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu na akasubiri juu ya maumivu na masaibu na juu ya maamrisho kuwa kuyatekeleza \"basi Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri.\u201d Kwa maana hayo ni katika mazuri, na Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa mwenye kufanya matendo mazuri."},{"id":2305,"sura":12,"from_aya":91,"to_aya":91,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{91} \"Wakasema: Tallahi! Mwenyezi Mungu amekufadhilisha wewe kuliko sisi.\u201d Yaani, amekufadhilisha wewe juu yetu kwa tabia nzuri na maumbile asili bora, nasi tulikufanyia ubaya mkubwa sana, na tukawania kukudhuru na kukuweka mbali na baba yako, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akakufadhilisha na akakuwezesha kufikia yote utakayo [na hakika sisi tulikuwa wenye kukosa. Na huku ndiko kukiri kosa kukubwa zaidi kwao juu ya uhalifu walioufanya dhidi ya Yusuf]."},{"id":2306,"sura":12,"from_aya":92,"to_aya":92,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{92} Yusuf, amani iwe juu yake, akawaambia kwa heshima na ukarimu mwingi: \"Leo hakuna lawama yoyote juu yenu;\u201d yaani, siwakaripii wala kuwalaumu, \"Mwenyezi Mungu atawasamehe, naye ni Mwingi wa kurehemu kuliko wote wanaorehemu.\u201d Basi akawasamehe msamaha kamili bila ya kuwashutumu kwa kutaja dhambi yao iliyotangulia, na akawaombea msamaha na rehema. Na hii ndiyo ihsani kubwa sana ambayo haifanywi isipokuwa na viumbe maalumu na wale walio bora miongoni mwa wateule."},{"id":2307,"sura":12,"from_aya":93,"to_aya":98,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"93. Nendeni na shati langu hili na mlitupe usoni mwa baba yangu, atakuwa mwenye kuona. Na mnijie na ahali zenu wote. 94. Na ulipoondoka tu msafara, baba yao akasema: Hakika mimi ninaipata harufu ya Yusuf, lau kuwa hamtanituhumu. 95. Wakasema: Tallahi! Hakika wewe bado ungali katika upotovu wako wa zamani. 96. Basi alipofika tu mbashiri huyo, akalitupa shati hilo usoni pake, basi akarejea kuona. Akasema: Je, sikuwaambia kuwa mimi ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi? 97. Wakasema: Ewe baba yetu! Tuombee msamaha kwa dhambi zetu. Hakika sisi tulikuwa katika waliokosa. 98. Akasema: Nitakuja waombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu sana. "},{"id":2308,"sura":12,"from_aya":93,"to_aya":93,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{93} Yaani, Yusuf, amani iwe juu yake, aliwaambia ndugu zake: \u201cNendeni na shati langu hili na mlitupe usoni mwa baba yangu, atakuwa mwenye kuona,\u201d kwa sababu kila ugonjwa una unatibiwa na kinyume chake. Basi shati hili lilipokuwa na athari za harufu ya Yusuf, ambayo iliujaza moyo wa baba yake kwa huzuni na hamu kubwa ambayo Mwenyezi Mungu tu ndiye anaijua vyema, alitaka ainuse ili roho yake imrudie, kisha nafsi yake imrudie, nafsi kuona kwake pia kumrudie. Na Mwenyezi Mungu ana hekima yake na siri mbalimbali katika hilo ambazo hawazijui waja wake, na Yusuf aliweza kujua kitu kuhusiana na jambo hili. \"Na mnijie na ahali zenu wote.\u201d Yaani, watoto wenu, na ukoo wenu, na wote wanaowafuta ili kukutana kwote kufanyike, na muondokewe na shida za maisha na ufinyu wa riziki."},{"id":2309,"sura":12,"from_aya":94,"to_aya":94,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{94} \"Na ulipoondoka tu msafara\u201d kutoka nchi ya Misri kuelekea nchi ya Palestina, Yaaqub akanusa harufu ya shati la Yusuf, kwa hivyo akasema: \u201cHakika mimi ninaipata harufu ya Yusuf, lau kuwa hamtanituhumu.\u201d Yaani, lau kuwa hamtanifanyia masihara na kudai kuwa maneno haya yamenitoka bila ya kuhisi. Kwa sababu aliona kusataajabu kwao hali yake, jambo lililomfanya kusema hivi."},{"id":2310,"sura":12,"from_aya":95,"to_aya":95,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{95} Basi yale aliyowadhania yakatokea, kwa hivyo wakasema: \u201cTallahi! Hakika wewe bado ungali katika upotovu wako wa zamani.\u201d Yaani, hujaacha bado kupotelea katika bahari yenye kina kirefu, hujui unachosema."},{"id":2311,"sura":12,"from_aya":96,"to_aya":96,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{96} \"Basi alipofika tu mbashiri huyo\u201d kwa bishara ya ukaribu wa kukutana na Yusuf, na ndugu zake, na baba yao, \u201cakalitupa\u201d yaani, shati hilo \u201cusoni pake, basi akarejea kuona.\u201d Yaani, alirudi katika hali yake ya awali ya kuona baada ya macho yake kuwa meupe kwa sababu ya huzuni, kisha akawaambia wale waliokuwa karibu naye miongoni mwa watoto wake na ahali zake ambao walikuwa wakiifanyia masihara rai yake na wakistaajabu naye, huku akiwa amewashinda juu yao na akijivunia neema ya Mwenyezi Mungu juu yake: \u201cSikuwaambia kuwa mimi ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi?\u201d Kwa kuwa nilikuwa ninatarajia kukutana na Yusuf, nikingoja kwisha kwa wasiwasi yangu kubwa, na msiba wangu, na huzuni."},{"id":2312,"sura":12,"from_aya":97,"to_aya":97,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{97}. Basi wakakiri dhambi zao, na wakafaulu kwa kufanya hivyo, na wakasema: \u201cEwe baba yetu! Tuombee msamaha kwa dhambi zetu. Hakika sisi tulikuwa katika waliokosa,\u201d kwa kuwa tulikufanyia yale tuliyokufanyia."},{"id":2313,"sura":12,"from_aya":98,"to_aya":98,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{98} Kwa hivyo \u201cakasema\u201d akiwajibu maombi yao na akiharakisha kuwaitikia: \"Nitakuja waombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu sana.\u201d Na matarajio yangu kwake ni kuwa atawasamehe na kurehemu na kuwafunika kwa rehema yake. Na ilisemwa: Alichelewesha kuwaombea msamaha mpaka masaa ya mwisho ya usiku ambao ndio wakati bora ili liwe kamili zaidi katika kuomba msamaha na karibu zaidi na kuitikiwa."},{"id":2314,"sura":12,"from_aya":99,"to_aya":100,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"99. Na wakati walipoingia alimokuwa Yusuf, aliwakumbatia wazazi wake na akasema: Ingieni Misri, Inshallah kwa amani. 100. Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi. Na wote wakaporomoka kumsujudia. Na akasema: Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani. Na Mola wangu Mlezi ameifanya kuwa kweli. Na Mwenyezi Mungu amenifanyia uzuri kunitoa gerezani, na akawaleta kutoka jangwani baada ya Shetani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole kwa alitakalo. Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima. "},{"id":2315,"sura":12,"from_aya":99,"to_aya":99,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{99}. Yaani, \u201cNa wakati\u201d Yaaqub na wanawe na jamaa zao wote walipojiandaa na wakaondoka kutoka katika nchi yao wakielekea kumfikia Yusuf huko Misri na kuishi huko, na walipomfikia, na \u201cwalipoingia alimokuwa Yusuf, aliwakumbatia wazazi wake.\u201d Yaani, aliwakumbatia na akawaweka hao wawili karibu sana naye, na akawaonyesha wema, ihsan, heshima, na utukufu mkubwa. \u201cNa akasema\u201d akiwaambia jamaa zake wote \u201cIngieni Misri, Inshallah kwa amani.\u201d Kutokana na kila machukizo yote na hofu zote. Basi wakaingia katika hali hii ya kufurahisha, na machovu na shida za maisha yakawaisha, na wakafurahia na kujisikia vizuri."},{"id":2316,"sura":12,"from_aya":100,"to_aya":100,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{100} \"Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi,\u201d yaani, juu ya kitanda cha mfalme na kiti mheshimiwa, \"Na wote wakaporomoka kumsujudia.\u201d Yaani, baba yake, mama yake, na ndugu zake walimsujudia kwa njia ya taadhima, na heshima na kutukuza. \"Na Akasema\" alipoona hali hii, na akaona kumsujudia kwao, \"Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani\u201d wakati alipoona nyota kumi na moja na jua na mwezi vinamsujudia. Basi hili ndilo kutokea kwake ambako kuliishia na kufikia. \"Na Mola wangu Mlezi ameifanya kuwa kweli\u201d na hakuifanya kuwa ndoto zilizochanganyikana. \"Na Mwenyezi Mungu amenifanyia uzuri\u201d mkubwa sana \u201ckunitoa gerezani, na akawaleta kutoka jangwani.\u201d Na hili ni katika upole wake na usemi wake mzuri, yeye amani iwe juu yake, ambapo aliitaja hali yake gerezani, lakini hakutaja hali yake ndani ya kisima, kwa sababu ya msamaha wake kamili kwa ndugu zake, na kwamba haitaji dhambi hiyo, na kwamba kuja kwenu kutoka jangwani ni katika ihsan ya mwenyezi Mungu kwangu. Na hakusema aliwatoa katika njaa na uchovu, wala hakusema: Aliwafanyia uzuri. Bali alisema: Alinifanyia uzuri. Kwa hivyo alifanya uzuri kumrudia yeye. Basi ni Mwingi wa baraka anayemteua kwa rehema yake amtakaye katika waja wake na akawatunuku rehema itokayo kwake, hakika Yeye ndiye Mwenye kutunuku \"baada ya Shetani kuchochea baina yangu na ndugu zangu.\u201d Na hakusema: Shetani aliwachochea ndugu zangu. Bali badala yake ni kana kwamba dhambi hiyo na ujinga huo umetoka katika pande zote mbili. Basi sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu ambaye alimhizi Shetani, akamuweka mbali, na akatuleta pamoja baada ya kutengana huko kugumu. \"Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole kwa alitakalo.\u201d Anamfikishia mja wema wake na ihsani yake kutokea mahali asipohisi, na humfikisha katika vyeo vya juu kutoka katika mambo anayoyachukia. \"Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema\u201d ambaye anajua mambo ya dhahiri na ya ndani na siri na dhamiri za waja wake. \u201cMwenye hekima\u201d katika kuviweka kwake vitu mahali pake na kuyaleta mambo katika nyakati zake yaliyoandikiwa."},{"id":2317,"sura":12,"from_aya":101,"to_aya":101,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"101. Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa katika ufalme, na umenifunza katika tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na niunganishe na walio wema."},{"id":2318,"sura":12,"from_aya":101,"to_aya":101,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{101} Mwenyezi Mungu alipomtimizia Yusuf yale aliyomtimizia kama vile kumuimarisha katika ardhi na utawala, na akayafurahisha macho yake kwa wazazi wake na ndugu zake, na baada ya elimu nyingi aliyopewa na Mwenyezi Mungu, akasema akiikiri neema ya Mwenyezi Mungu, akimshukuru kwa hilo, na akiomba uthabiti juu ya Uislamu, \u201cEwe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa katika ufalme\u201d na hayo ni kwa sababu alikuwa ni msimamizi wa hazina za ardhi na uendeshaji wake, na alikuwa waziri mkuu wa mfalme, \u201cna umenifunza katika tafsiri ya mambo.\u201d Yaani, ulinifundisha katika tafsiri ya mambo ya vitabu vilivyoteremshwa, na tafsiri ya ndoto na elimu nyinginezo. \u201cEwe Muumba wa mbingu na ardhi! ... Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu.\u201d Yaani, nidumishie Uislamu na uniimarishe juu yake mpaka unifishe ndani yake. Na hii haikuwa dua ya kujiharakishia kifo. \u201cNa niunganishe na walio wema\u201d miongoni mwa Manabii na walio wema na walio safi na walio bora."},{"id":2319,"sura":12,"from_aya":102,"to_aya":102,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"102. Hizo ni katika habari za ghaibu tulizokufunulia. Na hukuwa pamoja nao walipoazimia jambo lao hilo walipokuwa wanafanya njama zao."},{"id":2320,"sura":12,"from_aya":102,"to_aya":102,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{102} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomsimulia kisa hiki Muhammad \u2013 rehema na amani ya Mwenyezi Mungu zimfikie - Mwenyezi Mungu akamwambia: \"Hizo\" [Habari] ambazo tulikujulisha juu yake \"ni katika habari za ghaibu\u201d ambazo lau kuwa si sisi kukufunulia, basi hazingekufikia habari hizi kubwa. Kwa maana hukuwepo \"pamoja nao walipoazimia jambo lao hilo;\u201d yaani, wale ndugu zake Yusuf, \"walipokuwa wanafanya njama zao\u201d dhidi yake wakati walipofungiana ahadi kumtenganisha na baba yake katika hali ambayo hakuna awezaye kuijua isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala hawezi yeyote kuijua isipokuwa kwa kuelimishwa na Mwenyezi Mungu juu yake. Kama Yeye Mtukufu alivyosema aliposimulia kisa cha Musa na yaliyompata, akataja hali ambayo viumbe hawawezi kufikia kujua isipokuwa kwa wahyi wake, kwa hivyo akasema, \u201cWala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipompa Musa amri, wala hukuwa katika waliohudhuria.\u201d Mpaka mwisho wa Aya hii. Basi huu ndio ushahidi wa wazi kabisa kwamba mwenye kuzileta ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa uhakika."},{"id":2321,"sura":12,"from_aya":103,"to_aya":107,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"103. Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi. 104. Wala wewe huwaombi ujira kwa haya. Hayakuwa haya isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote. 105. Na ni ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazozipitia, lakini wao wanazipuuza. 106. Na wengi wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina. 107. Je, wana amani kuwa iwajie adhabu ya Mwenyezi Mungu ya kuwagubika, au iwajie Saa ya Qiyama kwa ghafla, na hali hawatambui? "},{"id":2322,"sura":12,"from_aya":103,"to_aya":103,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{103} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - Rehema na Amani ya Mwenyezi Mungu zimshukie - \"Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi\u201d kwa maana fikira zao na malengo yao yalikwisha haribika, kwa hivyo bidii ya wenye kunasihi haiwanufaishi hata kama hakuna vizuizi vyovyote, kwa njia ya kuwalingania katika yale yanayowafaa na kuwaepusha na maovu bila ya malipo yoyote wala badili, na hata wangewawekea ushahidi na ishara mbalimbali zinazoonyesha ukweli wao namna watakavyosimamisha."},{"id":2323,"sura":12,"from_aya":104,"to_aya":104,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{104} Na ndiyo maana akasema, \u201cWala wewe huwaombi ujira kwa haya. Hayakuwa haya isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote.\u201d Ambao watakumbuka kwa huo yenye kuwafaa ili wayafanye na yenye kuwadhuru ili wayaache."},{"id":2324,"sura":12,"from_aya":105,"to_aya":105,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{105} \"Na ni ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazozipitia\u201d zinazowaonyesha upweke wa Mwenyezi Mungu, \u201clakini wao wanazipuuza.\u201d"},{"id":2325,"sura":12,"from_aya":106,"to_aya":106,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{106} Na pamoja na haya, ikiwa watakiwa na baadhi ya imani, basi \u201cwengi wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina\u201d kwa kuwa hata kama wanakiri umola wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba Yeye ndiye Muumbaji, Mwenye kuruzuku na Mwendesha mambo yote, ila wao wanamshirikisha Mwenyezi Mungu katika uungu na upweke wake."},{"id":2326,"sura":12,"from_aya":107,"to_aya":107,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{107} Kwa hivyo hawa waliofikia hali hii, hawakubaki isipokuwa kwamba iwapate adhabu na mateso yawafikie kwa ghafla hali ya kuwa wako katika amani. Na ndiyo maana akasema: \"Wana amani;\u201d yaani, wale wanaofanya vitendo hivyo, wanaozipuuza Ishara za Mwenyezi Mungu, \u201ckuwa iwajie adhabu ya Mwenyezi Mungu ya kuwagubika.\u201d Yaani, adhabu itakayowafunika, na kuwajumuisha, na kuwaangamiza wote \"au iwajie Saa ya Qiyama kwa ghafla, na hali hawatambui?\u201d Kwa maana walikwisha jisababishia hayo. Basi na watubie kwa Mwenyezi Mungu na waache yale ambayo ndiyo sababu ya hayo."},{"id":2327,"sura":12,"from_aya":108,"to_aya":109,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"108. Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa ufahamu mzuri - mimi na wale wanaonifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina. 109. Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Je, hawakutembea katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo bora kwa wamchao Mungu. Basi hamtumii akili? "},{"id":2328,"sura":12,"from_aya":108,"to_aya":108,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{108} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad -rehema na amani ya Mwenyezi Mungu zimshukie: - \"Sema,\" uwaambie watu: \"Hii ndiyo njia yangu;\" yaani, njia yangu ninayoilingania, nayo ni njia inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na kwenye nyumba ya utukufu wake, ambayo inajumuisha kuijua haki na kuifanyia kazi na kuipendelea, na kumfanyia dini Mwenyezi Mungu peke yake bila mshirika yeyote. \"Ninalingania kwa Mwenyezi Mungu;\u201d yaani, ninawahimiza viumbe na waja wamfikie Mola wao Mlezi, na ninawatia moyo juu ya hilo, na ninawahofisha dhidi ya yale yatakayowaweka mbali naye, na pamoja na hayo, mimi ninafanya hayo \u201ckwa ufahamu mzuri\u201d na yakini kuhusu dini yangu bila shaka yoyote. Na vile vile \u201cwale wanaonifuata\u201d wanalingania kwa Mwenyezi Mungu kama vile ninavyolingania kwa ufahamu mzuri wa mambo yake. \"Na Mwenyezi Mungu ametakasika\u201d kutokana na yale aliyonasibishwa nayo miongoni mwa yale yasiyoufailia utukufu wake au kupingana na ukamilifu wake.  \"Wala mimi si katika washirikina\u201d katika mambo yangu yote, bali mimi ninamwabudu Mwenyezi Mungu kwa kumkusudia Yeye tu katika Dini yangu."},{"id":2329,"sura":12,"from_aya":109,"to_aya":109,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{109} Kisha Yeye Mtukufu akasema: \"Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipokuwa wanaume;\u201d yaani, hatukutuma Malaika wala wasiokuwa wao miongoni mwa aina mbalimbali za viumbe. Basi kwa nini kaumu yako wanastaajabu jambo la kukutuma wewe na wanadai kuwa wewe huna ubora wowote juu yao, basi una mfano mzuri kutoka kwa Mitume wa kabla yako, \"tuliowafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini.\u201d Yaani, siyo kutoka kwa wakazi wa jangwani, lakini kutoka kwa wakazi wa mijini, ambao ndio wana akili kamili zaidi na maoni mazuri, na ili hali yao ibainike na hali yao iwe wazi. \"Je, hawakutembea katika ardhi\u201d ikiwa hawasadiki kauli yako, \u201cwakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao?\u201d Jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaangamiza kwa sababu ya kukadhibisha kwao. Basi jihadharini kuendelea na yale waliyoendelea kuyafanya, yakawapata yale yaliyowapata. \"Na hakika nyumba ya Akhera;\u201d yaani, Pepo na vyote vilvyomo miongoni mwa starehe za kudumu \"ndiyo bora kwa wamchao Mungu\u201d katika kutekeleza amri zake na kujiepusha na makatazo yake. Kwa maana starehe za dunia zina mipaka, ni dhiki, na ni za kukatika, ilhali starehe za Akhera ni timilifu, kamili na hazina mwisho abadan bali zitaongezeka daima na kuendelea. Hicho ni kipawa kisicho na ukomo. \"Basi hamtumii akili?\u201d Yaani, mkayapendelea yale yaliyo bora kuliko yaliyo duni zaidi?"},{"id":2330,"sura":12,"from_aya":110,"to_aya":111,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"110. Hata Mitume walipokata tamaa (ya watu wao kuamini) na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, kwa hivyo wakaokolewa sawasawa tuwatakao. Na adhabu yetu haiwezi kurudishwa dhidi ya kaumu wahalifu. 111. Kwa hakika katika hadithi zao limo zingatio kwa wenye akili. Hazikuwa hadithi tu zilizozuliwa, bali ni za kusadikisha yale yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa kina wa kila kitu, na ni uwongofu na rehema kwa kaumu inayoamini. "},{"id":2331,"sura":12,"from_aya":110,"to_aya":110,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{110} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba Yeye hutuma Mitume watukufu, lakini kaumu wao wahalifu, walio duni wanawakadhibisha, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu huwapa muhula ili warejee kwenye haki, na Mwenyezi Mungu haachi kuendelea kuwapa muhula hadi hali ifikie ngumu sana dhidi ya Mitume, hadi kiwango kwamba Mitume pamoja na ukamilifu wa yakini yao na ukubwa wa kusadikisha kwao ahadi ya Mwenyezi Mungu na tishio lake, huenda ikawaingia mioyoni mwao aina fulani ya kukata tamaa na aina fulani ya udhaifu wa elimu na kusadikisha. Basi jambo likishafikia hali hii, \"hapo ikawajia nusura yetu, kwa hivyo wakaokolewa sawasawa tuwatakao\u201d nao ni Mitume wetu na wafuasi wao. \"Na adhabu yetu haiwezi kurudishwa dhidi ya kaumu wahalifu;\u201d yaani,  adhabu yetu hairudishwi dhidi ya yule anayefanya uhalifu na akamuasi Mwenyezi Mungu kwa ujasiri, basi hao hawana nguvu wala msaidizi yeyote."},{"id":2332,"sura":12,"from_aya":111,"to_aya":111,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{111} \"Kwa hakika katika hadithi zao;\u201d yaani, Hadithi za Manabii na Mitume na kaumu wao \"zingatio kwa wenye akili.\u201d Yaani, wanayazingatia watu wema na watu waovu, na kwamba anayefanya mfano wa kitendo chao, anapatwa na yale yaliyowapata ya heshima au fedheha. Na wanayazingatia pia kuhusiana na sifa alizo nazo Mwenyezi Mungu za ukamilifu na hekima kubwa, na kwamba Yeye ndiye Mungu ambaye hapana apasae kuabudiwa isipokuwa Yeye tu, bila mshirika yeyote. Na kauli yake, \u201cHazikuwa hadithi tu zilizozuliwa;\u201d yaani, haikuwa Qur-ani hii ambayo Mwenyezi Mungu aliwasimulia ndani yake habari za ghaibu ni katika hadithi za kuzuliwa na kutungwa tu; \"bali ni za kusadikisha yale yaliyo kabla yake\u201d miongoni mwa Vitabu vilivyotangulia kwa kuafikiana navyo na kuvishuhudia usahihi wake, \"na ufafanuzi wa kina wa kila kitu\u201d wanachohitaji waja katika misingi ya dini na matawi yake na ushahidi na hoja mbalimbali. \"Na ni uwongofu na rehema kwa kaumu inayoamini.\u201d Kwa sababu ya elimu ya kuijua haki na kuipendelea, wanapata uwongofu. Na kwa sababu ya malipo yao ya haraka na ya baadaye, wanapata rehema."},{"id":2333,"sura":12,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0641\u0635\u0644","text":"Mlango unaohusiana na kutaja baadhi ya mazingatia na faida zilizomo katika kisa hiki kikubwa, ambacho mwanzo wake Mwenyezi Mungu alisema, \u201cSisi tunakusimulia simulizi nzuri.\u201d Na akasema: \u201cHakika katika Yusuf na nduguze ziko ishara kwa wanaouliza.\u201d Na akasema mwisho wake: \"Kwa hakika katika hadithi zao limo zingatio kwa wenye akili\u201d zaidi ya yale manufaa yaliyotajwa ndani yake hapo awali. Basi miongoni mwake ni kwamba kisa hiki ni katika visa vizuri zaidi, vilivyo wazi zaidi, na villivyo bainifu zaidi. Kwa sababu ndani yake kuna aina mbalimbali za kuhama kutoka katika hali moja hadi nyingine, na kutoka katika mtihani mmoja hadi mtihani mwingine, na kutoka katika mtihani hadi katika mtihani na neema, na kutoka katika udhalilifu hadi katika utukufu, na kutoka katika utumwa hadi katika utawala, na kutoka katika kutengana na mgawanyiko hadi katika kukutana na kuungana, na kutoka katika huzuni hadi katika furaha, na kutoka katika ustawi hadi katika ukame, na kutoka katika ukame hadi katika ustawi, na kutoka katika dhiki hadi katika wasaa, na kutoka katika kupinga hadi katika kukiri. Basi ni mwingi wa baraka yule aliyekisimulia kwa uzuri, na aliyekifanya kuwa wazi, na kukibainisha. Na miongoni mwake ni kwamba ndani yake kuna msingi wa kisheria unaoruhusu kutafsiri ndoto. Kwa maana elimu ya kutafsiri ndoto ni katika elimu muhimu ambazo Mwenyezi Mungu humpa amtakaye katika waja wake, na kwamba mara nyingi tafsiri za ndoto hizi zinajengeka kwa jambo la kufailiana na kufanana katika jina na sifa. Kwa maana ndoto ya Yusuf ambayo aliona kuwa jua, mwezi, na nyota kumi na moja zilikuwa zinamsujudia,  namna ya uhusiano ni kwamba nuru hizi ni pambo na uzuri wa mbingu na zina manufaa kwake. Vile vile Manabii na wanachuoni ndio pambo na uzuri wa ardhi, na kupitia kwao watu huongoka katika giza mbalimbali kama wanavyoongoka kwa nuru hizi, na kwa sababu msingi wake ni baba yake na mama yake, na ndugu zake ni matawi yake. Basi inafaa zaidi kwamba msingi uwe mkubwa zaidi katika nuru na umbile kuliko kilicho tawi kwake. Basi ndiyo maana jua likawa mama yake, mwezi ukawa baba yake, na nyota zikawa ndugu zake. Na inafaa zaidi kwa kuwa katika kiarabu jua ni neno la kike, basi ndiyo maana likawa mama yake, na mwezi na sayari ni vya kiume, basi ndiyo vikawa baba yake na ndugu zake. Na pia kuna uhusiano kwamba mwenye kusujudu huwa anamtukuza na kumheshimu yule anayemsujudia. Naye anayesujudiwa anatukuzwa na kuheshimiwa sana. Kwa hivyo, hilo liliashiria kwamba Yusuf atatukuzwa na kuheshimiwa sana na wazazi wake na ndugu zake. Na ni lazima kutokana na hilo kwamba atachaguliwa na kuboreshwa katika elimu na fadhila zenye kulazimu kufanyika kwa hilo. Na ndiyo maana baba yake akamwambia: \"Na hivyo ndivyo Mola wako Mlezi atakuteua na atakufundisha katika tafsiri ya mambo.\u201d Na pia kuna uhusiano katika ndoto ya wale vijana wawili kwamba alifasiri ndoto ya yule aliyeona kwamba anakamua mvinyo, kwamba anayekamua mvinyo kwa kawaida huwa mtumishi kwa mtu mwingine, na kilichokamuliwa hicho huwa kimekusudiwa kwacho mtu mwingine. Kwa hivyo, akaifasiri kwa mwisho wake, nao ni kwamba atamnywesha bwana wake. Na hilo linajumuisha kutoka kwake jela. Na alifasiri ndoto ya yule aliyeona kwamba amebeba mkate juu ya kichwa chake na kwamba ndege wanakula kwa mkate huo kwamba ngozi ya kichwa chake, nyama, na ubongo ulio ndani yake kwamba amevibeba hivyo, na kwamba atawekwa mahali wazi kwa namna kwamba ndege wataweza kula katika kichwa chake. Kwa hivyo akaona kutokana na hali yake kwamba atauawa na kusulubishwa baada ya kifo chake na atawekwa mahali wazi kwa ajili ya ndege ili wale katika kichwa chake, na hilo haliwi isipokuwa kwa kusulubishwa tu baada ya kuuawa. Na aliifasiri ndoto ya mfalme ya ng\u2019ombe na masuke kwamba vinaashiria miaka yenye rutuba na miaka ya ukame. Na sababu ya uhusiano huu ni kwamba hali na maslahi ya raia yanahusiana na mfalme, na akitengenea, yanatengenea, na akiharibika, yanaharibika. Na vile vile miaka, kwayo kunakuwepo kutengenea kwa raia na kunyooka kwa mambo maisha au ukosefu wake. Na ama ng'ombe, hao wanatumika katika kuilima ardhi na kuinywesha maji. Kwa hivyo, mwaka ukiwa na rutuba, wananenepa, na ukiwa na ukame, wanakonda. Na vile vile masuke ya nafaka yanakuwa mengi na mabichi katika hali ya rotuba. Na katika hali ya ukame hupunguka na kukauka, na hilo ndilo zao bora zaidi la ardhi. Na miongoni mwake ni ule ushahidi uliomo juu ya usahihi wa unabii wa Muhammad \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake \u2013 kwa kuwa aliwahadithia kaumu yake kisa hiki kirefu ilhali hakusoma vitabu vya watu wa kale, wala hakusoma kwa yeyote ambaye kaumu yake wanamuona miongoni mwao asubuhi na jioni, naye alikuwa hajui kusoma wala kuandika, na kisa hiki kilikuwa kinakubaliana na yale yaliyo katika vitabu vilivyotangulia, na hukuwa pamoja nao walipoazimia jambo lao hilo walipokuwa wanafanya njama zao. Na miongoni mwake mtu ajiepushe na sababu za maovu na afiche yale yanayohofiwa kuwa ni madhara kwake kwa mujibu wa yale aliyomwambia Yaaqub Yusuf: \"[Ewe mwanangu!] Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wakaja kukufanyia njama.\u201d Na miongoni mwake ni inaruhusika kumtaja mtu jambo asilolipenda kwa njia ya kumshauri mwingine, kwa mujibu wa kauli yake \"wakaja kukufanyia njama\u201d Na miongoni mwake ni kwamba neema ya Mwenyezi Mungu juu ya mja ni neema pia juu ya wale wanaofungamana naye kama vile familia yake, jamaa zake, na marafiki wake, na kwamba labda neema hiyo inaweza kuwajumuisha na wakapata yale yaliyompata kwa sababu yake, kama alivyosema Yaaqub katika tafsiri yake ya ndoto ya Yusuf. \u201cNa hivyo ndivyo Mola wako Mlezi atakuteua na atakufundisha katika tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya ukoo wa Yaa'qub.\u201d Na neema hiyo ilipomkamilikia Yusuf, familia ya Yaaqub ikapata yale iliyopata miongoni mwa utukufu mwingi, kuimarishwa katika ardhi, na furaha na hali nzuri kwa sababu ya Yusuf. Na miongoni mwake ni kwamba uadilifu unahitajika katika mambo yote, si katika kiongozi kuamiliana na raia wake wala katika mengineyo, hata katika kuamiliana kwa mzazi na watoto wake katika upendo, upendeleo na mambo mengine; na kwamba katika kwenda kinyume katika hayo, jambo hilo linamvurugikia na hali zinamharibikia. Na ndiyo maana Yaaqub alipomtanguliza Yusuf kwa upendo na akampendelea kuliko ndugu zake, yakawapata yale yaliyowapata wao na baba yao na kaka yao. Na miongoni mwake ni kujihadhari na uovu wa madhambi, na kwamba dhambi moja inaitia dhambi nyingi, na halimtoshi mtendaji wake isipokuwa kwa kufanya makosa kadhaa. Kwani ndugu zake Yusuf walipotaka kumtenga na baba yake, walilifanyia hila za aina mbalimbali, na wakadanganya mara kadhaa, na wakamficha baba yao ukweli kuhusiana na shati lile na damu iliyokuwa juu yake, na kuhusu kuja kwao usiku huku wanalia. Na wala usikatae kwamba kulikuwa na kutafuta kwingi katika kipindi hicho, bali pengine hilo liliendelea hadi walipokutana na Yusuf, na kila walipotafuta, ukawa unafanyika udanganyifu ule uliofanyika na uzushi. Na huu ndio uovu wa dhambi na athari zake, zinazofuatana nayo, na zinazotangulia na zilizofuata baadaye. Na miongoni mwake ni kwamba kinachozingatiwa katika hali ya mja ni ukamilifu wa mwisho wake, sio upungufu wa mwanzo wake. Kwa maana wana wa Yaaqub, amani iwe juu yao, walifanya yale waliyofanya mwanzoni, ambayo ni katika sababu kubwa zaidi ya upungufu na lawama, kisha jambo lao hilo likamalizika na toba ya kweli na msamaha kamili kutoka kwa Yusuf na baba yao, na kuwaombea maghfira na rehema. Na mja akisamehe haki yake, basi Mwenyezi Mungu ndiye bora zaidi wa wanaorehemu. Na ndiyo maana katika kauli sahihi zaidi ni kwamba wao walikuwa manabii, kwa mujibu wa kauli yake Yeye Mtukufu: \"Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wanawe\u201d nao ni wale wana kumi na wawili wa Yaaqub na vizazi vyao. Na miongoni mwa yanayoonyesha hayo ni kuwa katika ndoto ya Yusuf aliona nyota zenye kung'aa. Na nyota zina nuru na uwongofu, ambao ni katika sifa za manabii. Na ikiwa wao si manabii, basi wao ni wanachuoni walioongoka. Na miongoni mwake ni yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyomneemesha kwayo Yusuf, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake miongoni mwa elimu, ustahimilivu, tabia njema, kulingatia kwa Mwenyezi Mungu na dini yake, msamaha wake kwa ndugu zake waliomtendea makosa, msamaha ambao yeye ndiye aliyetangulia kuwasamehe, na akakamilisha hilo kwa kutowakemea na kuwalaumu kwa sababu ya hilo, kisha wema wake mkubwa kwa wazazi wake na ihsani yake kwa ndugu zake, bali kwa viumbe vyote. Na miongoni mwake ni kwamba baadhi ya maovu ni madogo kuliko mengine, na kufanya ovu dogo kati ya mawili hayo ni bora kuliko kufanya kubwa zaidi kati yake. Kwa maana ndugu zake Yusuf walipokubaliana kumuua Yusuf au kumtupa nchi ya mbali, na msemaji fulani akasema miongoni mwao  \"Msimuuwe Yusuf. Lakini mtupeni ndani ya kisima.\u201d Maneno yake yalikuwa bora zaidi na mepesi kuliko yao, na kwa sababu yake, dhambi kubwa ya ndugu zake ikawa hafifu. Na miongoni mwake ni kwamba ikiwa kitu kitapitia mikono mbalimbali na kikawa sehemu ya mali na kisijulikane kwamba kilikuwa kwa njia isiyokuwa ya kisheria, basi ni kwamba hakuna dhambi kwa yule anayekichukua kwa kuuza au kununua kuhudumiwa nacho au kunufaika nacho au kukitumia. Kwa maana Yusuf, amani iwe juu yake - aliuzwa na ndugu zake kwa njia ya haramu na ambayo hairuhusiki, kisha msafara ukaenda naye hadi Misri, na wakamuuza huko na akabaki kwa bwana wake kama kijana mtumwa, na Mwenyezi Mungu akamwita huyo aliyemnunua kwamba ni bwana, naye alikuwa kwao katika hadhi ya mtumishi, mtumwa, mwenye kuheshimiwa. Na miongoni mwake ni kujihadhari kuwa peke yako na wanawake ambao inahofiwa kuwa watakutia katika majaribio, na pia kujihadhari na mapenzi ambayo yanahofiwa kuleta madhara. Kwa maana mke wa mheshimiwa yule alifanya yale aliyofanya kwa sababu ya kuwa kwao peke yao na Yusuf na kumpenda kwake kukubwa, ambayo hakuyaacha mpaka akamtongoza kule kumtongoza, kisha akamdanganyishia, basi akafungwa jela kwa muda mrefu kwa sababu yake. Na miongoni mwake azimio alilokuwa nalo Yusuf juu ya mwanamke huyo kisha akaliacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni katika yale yanayompandisha cheo kwa Mwenyezi Mungu akawa karibu mno. Kwa sababu azimio ni katika mambo ya nafsi yenye kuamrisha mabaya, na hilo ndilo umbile la aghalabu ya viumbe. Basi ilipolinganisha kati yake na kumpenda Mwenyezi Mungu na kumhofu, kumpenda na kumhofu Mwenyezi Mungu kulishinda msukumo wa nafsi na matamanio, kwa hivyo akawa miongoni mwa wale \u201cwalioogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na wakajizuilia nafsi na matamanio.\u201d Na miongoni mwa wale saba ambao Mwenyezi Mungu atawafunika chini ya kivuli chake Siku ambayo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli chake: Mmoja wao ni mwanaume aliyeitwa na mwanamke mwenye cheo na uzuri, lakini akasema: Hakika Mimi ninamuogopa Mwenyezi Mungu. Na azimio ambalo mja analaumiwa juu yake ni lile ambalo anakaa nalo, kisha likawa ameshaliamulia na hata labda likaambatana na kitendo. Na miongoni mwake ni kwamba yule ambaye Imani iliingia moyoni mwake, na akamsafishia Mwenyezi Mungu mambo yake yote, basi hakika Mwenyezi Mungu humlinda, kwa uthibitisho wa imani yake na ukweli wake katika kumkusudia Mwenyezi Mungu, kutokana na kila aina ya ubaya, machafu na sababu za maasia, ambayo hayo ni malipo ya imani yake na kumkusudia kwake Mwenyezi Mungu peke yake. Hayo ni kwa sababu ya kauli yake: \"Na Yusuf akawa na azimio naye lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi. Na ni hivyo ili tumuepushe na ubaya na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu waliosafishwa;\u201d kulingana na kisomo cha aliyeweka kasra chini ya lam. Na ama aliyeisoma kwa fatiha, basi neno hilo linamaanisha kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyemsafisha, na hilo linajumuisha yeye mwenyewe kuwa safi. Kwa hivyo, alivyomsafia Mwenyezi Mungu matendo yake, Mwenyezi Mungu akamsafisha, na akamuepusha na ubaya na uchafu. Na miongoni mwake ni kwamba mja akiona mahali ambapo kuna majaribio au sababu za kufanya maasia inapaswa apakimbie na apaepuke kiasi awezavyo. Kwa maana Yusuf, amani iwe juu yake, alipotongozwa na yule ambaye yeye alikuwa katika nyumba yake, alikimbia kitorokea mlangoni, ili aepuke uovu wake. Na miongoni mwake ni kwamba ishara za Ushahidi mbalimbali zinazingatiwa wakati kuna mchanganyiko katika jambo. Kwa hivyo, iwapo mwanamume na mkewe watagombana juu ya vyombo vya nyumbani mwao, basi chochote kinachofailiana na mwanamume, hicho kinakuwa cha wanaume, na kile kinachofailiana na kwa wanawake, basi hicho kinakuwa ni chake. Hilo ni kama hakuna ushahidi. Na inaingia katika mlango huu kutumia mtu mwenye ujuzi wa kuangalia mfanano wa watu wa ukoo mmoja, na pia kutumia athari mbalimali kunaingia katika hili. Kwa maana, yule shahidi wa Yusuf alishuhudia kwa kutumia ishara tu na akatoa hukumu kwa kutegemea hilo juu ya kurarua shati, na akalitumia kuraruka kwake kwa nyuma yake juu ya ukweli wa Yusuf na uwongo wa mwanamke huyo. Na katika yale yanayoashiria kanuni hii ni kwamba alitumia kuwepo kwa kopo lile katika mizigo ya nduguye kama ushahidi juu kumhukumu kwamba aliiba bila ya hoja ya ushahidi wala kukiri. Basi kwa kuzingatia hili, ikiwa kitu kilichoibiwa kitapatikana mikononi mwa mwizi, hasa ikiwa anajulikana katika kuiba, basi atahukumiwa kwa wizi huo, na hili ni la nguvu zaidi ya ushahidi. Vile vile ikiwa mtu atapatikana akitapika mvinyo, au mwanamke ambaye hana mume wala bwana akipatikana akiwa mjamzito, basi ataadhibiwa adhabu maalumu ya kisheria maadamu hakuna kizuizi cha kuzuia hilo. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaiita hukumu hii kuwa ni shahidi, akasema: \"Na shahidi kutoka kwa jamaa za mwanamke huyo akashuhudia.\u201d Na miongoni mwake ni ule uzuri wa dhahiri na uliofichika wa Yusuf. Uzuri wake wa dhahiri ulimlazimu mwanamke yule ambaye Yeye alikuwa ndani ya nyumba yake kile ulichomlazimu, na pia kwa wale wanawake aliowakusanya wakati walipomlaumu kwa hilo kiasi kwamba walijikata mikono yao na wakasema: \u201cHuyu si mwanaadamu. Hakuwa huyu isipokuwa ni Malaika mtukufu. Na ama uzuri wake wa ndani, basi ni kujiepusha kwake kukubwa na maasi pamoja na kuwepo kwa sababu nyingi za kuyafanya, na ushahidi wa mke wa mheshimiwa yule na wanawake wale juu ya kutokuwa kwake na hatia baada ya hapo, na ndiyo maana mke wa mheshima yule akasema, \"Na kweli mimi nilimtaka, naye akakataa.\u201d Na akasema baada ya hayo: \"Sasa haki imedhihiri. Mimi ndiye nilimtaka kinyume na nafsi yake, na hakika yeye ni katika wakweli.\u201d Na wanawake wale wakasema: \"Hasha Lillahi! Sisi hatukujua ubaya wowote kwake.\" Na miongoni mwake ni kwamba Yusuf, amani iwe juu yake, alichagua jela badala ya kufanya dhambi. Basi hivyo ndivyo mja anafaa kufanya anapojaribiwa na mambo mawili: ima kufanya maasia au adhabu ya kidunia, basi achague adhabu ya kidunia kuliko kufanya dhambi yenye kulazimu adhabu kali katika dunia na akhera. Basi kwa sababu ya hilo miongoni mwa alama za imani ni kwamba mja achukie kurudi katika ukafiri baada ya Mwenyezi Mungu kumuokoa kutokana nao, kama vile anavyochukia kutupwa ndani ya Moto. Na miongoni mwake ni kwamba mja anapaswa kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu na kujikinga kwa ngome yake wakati zinapopatikana sababu za maasia na ajiweke mbali na uwezo wake na nguvu zake kwa mujibu wa kauli ya Yusuf, amani imshukie: \"Na usiponiondoshea vitimbi vya wanawake mimi, nitaelekea kwao, na nitakuwa katika wajinga.\u201d Na miongoni mwake ni kwamba elimu na akili humwita mwenyewe katika kheri na kukataza maovu, na kwamba ujinga unamwita mwenyewe katika kukubaliana na matamanio ya nafsi yake, hata ikiwa ni uasi huo ni wenye kumdhuru mwenyewe. Na miongoni mwake ni kama mja anavyopaswa kumfanyia Mwenyzi Mungu uja katika nyakati nzuri, basi pia anapaswa kumfanyia katika nyakati za shida. Kwa maana Yusuf, amani iwe juu yake, hakuacha kulingania kwa Mwenyezi Mungu, na alipoingia gerezani,  aliendelea hivyo na akawalingania wale vijana wawili kwenye tawhidi na akawakataza shirki. Na kutokana na utambuzi wake nzuri yeye amani iwe juu yake, alipowaona kwamba wanaweza kuitikia wito wake kwa maana walikuwa na dhana nzuri naye, na wakamwambia: \"Hakika sisi tunakuona wewe ni miongoni mwa wafanyao mazuri\" na wakamjia ili awafasirie ndoto zao, na akaona kwamba walikuwa na shauku kubwa ya yeye kuwafasiria, akaona kwamba hiyo ni fursa na akaitumia vyema, kwa hivyo akawalingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kabla ya kuwafasiria ndoto zao ili aweze kufaulu zaidi katika kulifanikisha lengo lake na kukaribia zaidi kulifanikisha alilokuwa analitaka, aliwaeleza kwanza kwamba kilichomfikisha kwenye hali ya ukamilifu na elimu waliyomuona nayo ni imani yake, tauhidi yake, na kuacha kwake dini ya wasiomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na haya ni kuwaita katika hali, kisha akawalingania kwa maneno, na akabainisha uharibifu wa ushirikina na akatoa ushahidi juu ya hilo. Na miongoni mwake ni kuanza na muhimu zaidi, kisha muhimu zaidi, na kwamba ikiwa mufti ataulizwa, na ikawa mwenye kuuliza haja yake ni kubwa zaidi kuliko swali lake, basi anapaswa kumfundisha kile anachohitaji zaidi kabla ya kujibu swali lake. Hii ni alama ya ushauri wa mwalimu na ufahamu wake na uzuri wa kuongoza kwake na kufundisha kwake. Kwa maana Yusuf alipoulizwa na wale wavulana kuhusu ndoto zao, alitangulia kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu peke yake bila ya mshirika yeyote kabla ya kuwafasiria ndoto hizo. Na miongoni mwake ni kwamba mwenye kupatwa na machukizo na dhiki, basi hakuna ubaya kwake kutafuta msaada wa mtu ambaye ana uwezo wa kumuokoa au kujulisha wengine juu ya hali yake, na kwamba hili si kuwalalamikia viumbe. Kwa maana hili ni katika mambo ya kawaida ambayo ni kawaida ya watu kutafuta msaada kutoka kwa wenzao.Na ndiyo maana Yusuf akamwambia yule aliyedhania kuwa ataokoka kati ya wale vijana wawili: \u201cNikumbuke mbele ya bwana wako.\u201d Na miongoni mwake ni anapaswa na ni muhimu kwa mwalimu kutumia ikhlasi kamili katika ufundishaji wake, na kwamba asifanye ufundishaji wake kuwa njia ya kufidiwa na mtu yeyote kwa mali au heshima au manufaa, na kwamba asikatae kufundisha au kutokushauri iwapo muulizaji swali hafanyi alichotakiwa na mwalimu. Kwani Yusuf, amani iwe juu yake, alisema, na akamuusia mmoja wa vijana wale wawili amkumbuke kwa bwana wake, lakini hakumtaja na akasahau. Na ilipodhihiri haja yake ya kumuuliza Yusuf, Walimtuma mvulana huyo, naye akaja kwake akiuliza juu ya ndoto ile. Basi Yusuf hakumkemea wala kumkaripia kwa sababu ya kuacha kwake kumtaja, bali alimjibu swali lake kikamilifu kwa kila njia. Na miongoni mwake ni kwamba aliyeulizwa anafaa kumuongoza muulizaji kwenye jambo litakalomnufaisha kuhusiana na swali lake na kumuongoza kwenye njia itakayomnufaisha katika dini yake na dunia yake. Hii ni katika ukamilifu wa ushauri wake, ushupavu wa akili yake, na kuelekeza kwake kuzuri. Kwa maana Yusuf, amani iwe juu yake, hakupunguza katika kufasiri ndoto ya mfalme huyo. Bali aliwaelekeza \u2013 pamoja na hayo \u2013 juu ya kile watakachofanya katika miaka ile ya ukame kama vile kupanda mimea kwa wingi na wingi wa mavuno yake. Na miongoni mwake ni halaumiwi mtu kwa kujitahidi kujiepusha na tuhuma dhidi yake na kutaka kujiweka mbali nayo, bali anasifiwa kwa hilo. Kwa vile Yusuf alipokataa kutoka gerezani hadi ibainike kwao kwamba hakuwa na hatia katika kesi ya wanawake wale waliojikatakata mikono. Na miongoni mwake ni fadhila ya elimu, elimu ya hukumu mbalimbali na sheria, na elimu ya kufasiri ndoto, elimu ya uendeshaji na malezi, na kwamba ni bora zaidi kuliko sura ya dhahiri, hata kama itafikia uzuri wa Yusuf. Hii ni kwa kuwa kwa sababu ya uzuri wake, Yusuf alipatwa na majaribio hayo na kufungwa jela, na kwa sababu ya elimu yake alipata utukufu, na kuinuliwa hadhi ya juu, na kuwezeshwa katika dunia. Kwa maana kila heri hapa duniani na akhera ni moja ya athari za elimu. Na miongoni mwake ni kwamba elimu ya kutafsiri ndoto ni miongoni mwa elimu za kisheria, na kwamba mtu hulipwa kwa kujifunza kwake na kufundisha wengine, na kwamba kutafsiri ndoto kunaingia katika kutoa fatwa. Kwa sababu ya kauli yake kwa wale vijana wawili, \u201cImeamuliwa jambo mnalotaka fatwa,\u201d naye mfalme alisema: \"Nipeni fatwa kuhusu ndoto yangu,\" na yule kijana akamwambia Yusuf: \"Nipe sisi fatwa kuhusu ng'ombe saba...\" hadi mwisho wa Aya. Kwa hivyo hairuhusiki kutoa tafsri ya ndoto bila ya elimu. Na miongoni mwake ni kwamba hakuna ubaya kwa mtu kusema juu ya sifa za ukamilifu zilizoko ndani yake, kama vile elimu au matendo, ikiwa kuna masilahi katika hilo maadamu mja hakusudii kujionyesha kwa kufanya hivyo, na akawa amesalimika na uongo, kwa mujibu wa kauli ya Yusuf, \"Niweke kusimamia hazina za ardhi. Hakika mimi ni Mlinzi mzuri, Mwenye kujua sana.\" Kadhalika, mtu halaumiwi kwa kuomba uongozi ikiwa anayeomba huyo atafanya awezavyo katika haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, na kwamba hakuna ubaya wowote katika kuomba ikiwa yeye ni anautosha zaidi kuliko wengine. Na kile kinacholaumiwa ni ikiwa hatoshi, au kuna mwingine kama yeye au aliye juu zaidi yake, au hataki kusimamisha amri ya Mwenyezi Mungu kupitia uongozi huo. Basi kwa sababu ya mambo haya, anapaswa kukatazwa kuutafuta na kujiweka karibu nao. Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu ni mwenye kupeana kwa wingi na Mkarimu. Yeye humpa mja wake kheri kwa wingi katika dunia na Akhera, na kwamba kheri ya Akhera ina sababu mbili: Imani na uchamungu, na kwamba ni bora kuliko malipo ya dunia, na ufalme wake, na kwamba mja anapaswa kujiombea mwenyewe na kuitamanisha malipo ya Mwenyezi Mungu, na wala asimhuzunike akiwaona watu wa dunia hii na furaha zake, ilhali yeye hawezi kuzipata, bali anafaa kuifariji kwa malipo ya Akhera ya Mwenyezi Mungu na fadhila yake kubwa, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu, \u201cNa malipo ya Akhera ni bora kwa walioamini na wakawa wanamcha Mungu.\u201d Na miongoni mwake ni kwamba ikiwa nia katika kukusanya pamoja vyakula ni kuwafanyia watu ukunjufu ikiwa hakuna madhara yoyote yatakayowafika, basi hakuna ubaya wowote katika hilo. Kwa sababu Yusuf  aliwaamrisha kukusanya pamoja chakula na katika ile miaka ya rutuba ili wajitayarishe kwa ajili ya miaka ya ukame, na kwamba hili halipingani na kumtegemea Mwenyezi Mungu; bali mja anapaswa kumtegemea Mwenyezi Mungu na kufanya sababu za kumnufaisha katika dunia yake na akhera yake. Na miongoni mwake ni ule uendeshaji mambo mzuri wa Yusuf  alipochukua usimamizi wa hazina za nchi, mpaka mavuno yao yakawa mengi sana kiasi kwamba watu wa nchi za pande zingine wakaanza kwenda Misri kutafuta huko chakula. Kwa sababu walijua kwamba ni kingi huko, na tena hakuna kufikia kwamba hakuwa akimpimia mtu yeyote isipokuwa kiasi cha haja yake maalumu, au kidogo, hakuwa akimpa kila aliyekuja zaidi ya kipimo anachoweza beba ngamia mmoja. Na miongoni mwake ni uhalali wa kumpokea nyumbani mgeni, na kumkirimu na kwamba ni katika desturi za mitume, kwa mujibu wa kauli ya Yusuf  akiwaambia ndugu zake, \u201cJe, hamuoni kwamba mimi ninatimiza kipimo na mimi ni mbora wa wale wanaopokea wageni?\" Na miongoni mwake ni kwamba kuwa na dhana mbaya pamoja na kuwepo kwa ishara za ushahidi zinaoonyesha hilo, hakukatazwi wala si haramu. Kwa maana Yaaqub aliwaambia wanawe baada ya kukataa kumuachilia Yusuf  pamoja nao mpaka wakamrai sana, kisha akawaambia baada ya wao kumjia na kudai kwamba mbwa-mwitu amemla, \u201cBali nafsi zenu zimewashawishi kutenda kitendo.\u201d Naye akawaambia kuhusu yule ndugu wao mwingine, \u201cJe, niwaaminini kwa huyu isipokuwa kama nilivyowaamini kwa nduguye hapo zamani?\u201d Kisha Yusuf alipomzuia kwake na ndugu zake wakamjia baba yao, akawaambia, \u201cBali nafsi zenu zimewashawishi kutenda kitendo.\u201d Basi wao mwishowe, hata ikiwa hawakukosea, walifanya yale ambayo yalimsababisha baba yao kusema yale aliyoyasema bila ya kuwepo dhambi wala ubaya juu yake. Na miongoni mwake ni kwamba kutumia sababu za kuzuia kijicho na mambo mengine ya kuchukiza au kutumia sababu za kukiondoa baada ya kutokea kwake hakukatazwi, bali kunaruhusika, hata ingawa hakuna kinachotokea isipokuwa kwa hukumu na majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana sababu pia ni katika hukumu na majaliwa. Hili ni kwa sababu ya amri ya Yakub alipowaambia wanawe, \u201cEnyi wanangu, msiingilie kupitia mlango mmoja, bali ingilieni kupitia milango tofauti tofauti.\u201d Na miongoni mwake ni kuruhusiwa kutumia njama ambayo kwayo inafikiwa haki mbalimbali, na kwamba kujua njia zilizofichika zinazofikisha kwenye malengo yake ni katika jambo ambayo mja anasifiwa kwayo, na kilicho haramu ni kutumia njama za kuangusha wajibu au kufanya kitendo kilichoharamishwa. Na miongoni mwake ni kwamba, yeyote anayetaka kuwahadaa wengine katika jambo ambalo hataki watu wajue, basi na atumie njia isiyokuwa ya moja kwa moja ya kimaneno na kimatendo yenye kumzuia kudanganya. Kama alivyofanya Yusuf alipolitupa lile kopo katika mizigo ya kaka yake, kisha akazitoa humo kwa kufanya idhaniwe kuwa yeye ni mwizi, na wala hapakuwa na chochote ndani yake isipokuwa ishara tu ye kuwafanya kaka zake kufikirika kuwa kweli aliiba, kisha akasema baada ya hayo, \u201cMwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipokuwa yule tuliyemkuta naye kitu chetu.\u201d Wala hakusema, \u201cyule aliyeiba kitu chetu.\u201d Na vile vile, hakusema, \u201cHakika tumekuta kitu chetu kwake.\u201d Bali alitumia maneno ya jumla ambayo yanaweza kumaanisha yeye au wengineo, na hakukuwa na kosa lolote katika hilo. Lakini ndani yake kuna tu kupeana dhana kwamba ni mwizi, ili kusudi la sasa lipatikane, na kwamba abakie [pamoja] na kaka yake, na tena dhana hiyo iliondoka juu ya kaka yake baada ya hali halisi kubainika. Na miongoni mwake ni kwamba haijuzu kwa mtu kushuhudia isipokuwa kwa yale anayoyajua, na aliyoyathibitisha [ama] kwa uchunguzi au uzoefu wa mtu anayemwamini na ambaye nafsi yake imetulia. Kwa sababu walisema, \u201cNa sisi hatutoi ushahidi ila kwa tunayoyajua.\u201d Na miongoni mwake ni kwamba msiba huu mkubwa ambao Mwenyezi Mungu alimtia mtihani Mtume Wake na rafiki yake, Yaaqub, amani iwe juu yake. Ambapo aliamua kumtenga na mtoto wake Yusuf ambaye hakuweza kuachana naye hata saa moja, jambo hilo lilimhuzunisha sana, hivyo utengano kati yake na yeye ulifanyika kwa muda mrefu, si chini ya miaka thelathini, na Yakubu huzuni haikutoka moyoni mwake katika kipindi hiki. \u201cNa macho yake yakawa meupe kwa huzuni aliyokuwa akiizuia.\u201d Basi jambo lilizidi kuwa kali kwake ilipofarikiana baina yake na mwanawe wa pili, nduguye Yusuf ambaye alikuwa mvumilivu kwa amri ya Mwenyezi Mungu na kutarajia malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, alikuwa amejiahidi subira nzuri, na hakuna shaka kwamba alitimiza yale aliyoahidi, na hili halipingani na kauli yake: \u201cHakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu sikitiko langu na huzuni yangu.\u201d Kulalamika kwa Mungu hakukatazi subira, bali kinachoikataa ni kulalamika kwa viumbe vilivyoumbwa. Na miongoni mwake ni kwamba unafuu huja na dhiki, na pamoja na shida huja urahisi. Maana majonzi ya Yakubu yalipozidi kuwa makali hata yalipokwisha, ndipo dhiki ilipotokea kwa jamaa ya Yakubu na madhara yakawapata; Wakati huo, Mungu aliruhusu kitulizo, na mkutano ulifanyika wakati wa hitaji na hitaji lake kuu, hivyo kutimiza thawabu na furaha.Ilijulikana kutokana na hilo kwamba Mungu huwajaribu marafiki zake kwa shida na ufanisi, shida na urahisi. Ili kujaribu uvumilivu wao na shukrani, na hivyo kuongeza imani yao, uhakika, na shukrani. Na miongoni mwake ni kwamba inajuzu kumjulisha mtu anayoyapata na anayoumwa, kama vile maradhi, umasikini na mengineyo bila ya kuchukizwa.  Kwa sababu ndugu zake Yusuf walisema: \"Ewe Mheshimiwa! Imetupata shida, sisi na watu wetu.\u201d Wala Yusuf hakuwakanusha hayo. Na miongoni mwake ni kwamba fadhila ya uchamungu na subira, na kwamba wema wote duniani na akhera ni moja ya athari za uchamungu na subira, na kwamba matokeo ya wale wanaozipokea ni matokeo bora zaidi. Kwa kauli yake: \u201cHakika Mwenyezi Mungu ametuneemesha. Hakika anayemcha Mungu na akasubiri, basi hakika Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri.\u201d Na miongoni mwake ni kwamba Yule ambaye Mungu amempa baraka baada ya dhiki, umaskini, na hali mbaya anapaswa kukiri baraka za Mungu juu yake, na bado akumbuke hali yake ya mwanzo. Acha akushukuru kila anapotaja. Kwa mujibu wa maneno ya Yusuf, amani iwe juu yake: \"Na Mwenyezi Mungu amenifanyia wema kunitoa gerezani, na akawaleta kutoka jangwani. \" Na miongoni mwake ni kwamba Fadhili kuu za Mungu kwa Yusuf; ambapo alimhamisha katika hali hizo, na kumletea shida na dhiki; ili kumfikisha kwenye malengo ya juu na viwango vya juu. Na miongoni mwake ni kwamba mja anapaswa daima kumsifu Mungu ili aithibitishe imani yake, afanye sababu zinazohitajika kwa hilo, na amuombe Mungu mwisho mwema na ukamilisho wa baraka. Kwa mujibu wa kauli ya Yusuf, Rehema na Amani zimshukie: \"Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa utawala, na umenifunza tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na niunganishe na walio wema.\u201d Haya ndiyo Mwenyezi Mungu amerahisisha miongoni mwa faida na mazingatio katika kisa hiki kilichobarikiwa, na lazima zitamdhihirikia mwenye kutafakari mengine yasiyokuwa hayo. Basi tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu elimu yenye manufaa na matendo yanayokubalika, hakika Yeye ni Mpeanaji kwa wingi, Mkarimu. Imetimia tafsiri Surat Yusuf na baba yake na ndugu zake, Mwenyezi Mungu awafikishie rehema na amani. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu mola mlezi wa walimwengu wote."},{"id":2334,"sura":12,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"***"}]}