{"result":[{"id":2335,"sura":13,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Ra'd"},{"id":2336,"sura":13,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Nayo iliteremka Madina, na pia inasemekana kuwa iliteremka Makka"},{"id":2337,"sura":13,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":2338,"sura":13,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Alif Lam Mim Ra. Hizi ni Ishara za Kitabu. Na yale uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki. Lakini wengi wa watu hawaamini."},{"id":2339,"sura":13,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Yeye Mtukufu anajulisha kuwa Qur\u2019ani hii ni ishara za Kitabu zinazoonyesha kila wanachokihitaji waja katika misingi na matawi ya Dini, na kwamba yale yaliyoteremshwa kwa Mtume kutoka kwa Mola wake Mlezi ndiyo haki iliyo wazi. Kwa sababu habari zake ni za ukweli na amri zake na makatazo yake ni ya uadilifu, yanayoungwa mkono na ushahidi na hoja za mkato. Kwa hivyo mwenye kukielekea kwa kukisoma, basi anakuwa miongoni mwa wenye elimu juu ya haki ambao elimu yao hiyo inawasababishia kufanya kile ambacho Mwenyezi Mungu anapenda. \u201cLakini wengi wa watu [hawaamini]\u201d katika Qur\u2019ani hii: ima kwa sababu ya ujinga na kupeana tu mgongo na kutoijali, au kwa sababu ya ukaidi na dhuluma. Na ndiyo sababu hiyo, wengi wa watu hawafaidiki nayo, kwa sababu hawana sababu ya kuwafanya wafaidike."},{"id":2340,"sura":13,"from_aya":2,"to_aya":4,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"2. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua mbingu bila ya nguzo mnazoziona, kisha akainuka juu ya Kiti cha Enzi, na akatiisha jua na mwezi, kila kimoja kinakwenda kwa muda maalumu. Anaendesha mambo, na anazipambanua Ishara kwa kina ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu Mlezi. 3. Naye ndiye aliyeikunjua ardhi na akaweka humo milima mathubuti na mito. Na katika kila matunda akafanya jozi mbili la kiume na la kike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa kaumu wanaotafakari. 4. Na katika ardhi vimo vipande vilivyokaribiana, na zipo bustani za mizabibu, na mimea mingine, na mitende yenye kuchipua kwenye shina moja na isiyochipua kwenye shina moja, nayo inanyweshwa katika maji yale yale. Na tunaifanya baadhi yao kuwa bora kuliko mengine katika kula. Hakika katika hayo zimo ishara kwa kaumu wanaotia mambo akilini. "},{"id":2341,"sura":13,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya upekee wake katika uumbaji, uendeshaji mambo, ukuu, na mamlaka, jambo ambalo linaashiria kwamba Yeye peke yake ndiye anayepaswa kuabudiwa, ambaye haifai kufanya ibada isipokuwa kwa ajili yake tu. Kwa hivyo akasema, \u201cMwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua mbingu\u201d pamoja na ukubwa wake na upana wake, kwa uwezo wake mkubwa, \"bila ya nguzo mnazoziona.\u201d Yaani, hazina nguzo zozote kwa chini yake. Kwa maana zingekuwa zina nguzo, basi mngeliziona \u201ckisha\u201d baada ya kuziumba mbingu na ardhi, \u201cakainuka juu ya Kiti cha Enzi\u201d kikubwa, ambacho ndicho kiumbe cha juu zaidi. Aliinuka juu kuinuka kunakolingana na utukufu wake na ukamilifu wake, \u201cna akatiisha jua na mwezi\u201d kwa masilahi ya waja na masilahi ya mifugo yao na matunda yao. \"Kila kimoja\" yaani jua na mwezi, \"kinakwenda\" kwa uendeshaji wa Mwenye nguvu, Mwenye kujua yote \u201ckwa muda maalumu,\u201d kwa mwendo uliopangwa, havipumziki, wala havichoki mpaka utakapokuja muda uliowekwa. Ambayo ni muda ule Mwenyezi Mungu ataukunja ulimwengu huu na kuwahamisha hadi kwenye nyumba ya akhera, ambayo ndiyo nyumba ya makazi ya kudumu. Kisha Mwenyezi Mungu atazikunja mbingu na kuzibadilisha, na ataighairi ardhi na kuibadilisha. Nalo jua na mwezi atavikunjakunja, na [kuviunganisha] na vitatupwa ndani ya Moto. Ili wale wanaoviabudu waone kuwa hivyo havistahiki kuabudiwa, kwa hivyo watajuta majuto makubwa zaidi kwa sababu ya hilo, na ile wajue wale waliokufuru kwamba walikuwa waongo. Na kauli yake, \u201canaendesha mambo, na anazipambanua Ishara kwa kina.\u201d Huku ni kujumuisha kati ya uumbaji na amri. Yaani, Mwenyezi Mungu Mkuu ameinuka juu ya kiti cha ufalme, anaendesha mambo yote ya ulimwengu wa juu na wa chini. Kwa hivyo anaumba na kuruzuku, anatajirisha na kufukarisha, anawanyanyua baadhi ya watu na kuwadunisha wengine, anatukuza na kudhalilisha, anateremsha na kuinua, anakinga kutokana na vikwazo, anaondoa misiba, anatekeleza majaliwa katika nyakati zake ambazo alikwisha jua na kalamu yake ikayaandika; na anawatuma Malaika wake watukufu kuyaendesha yale aliyowafanya kuendesha. Na anateremsha Vitabu vya kiungu kwa Mitume wake, na anabainisha yale wanayohitaji waja wake katika sheria mbalimbali, maamrisho na makatazo, na anayabainisha kwa kina zaidi na kuyapambanua. \"ili\" kwa sababu ya yale aliyowatolewa miongoni mwa ishara mbalimbali za kiupeo na ishara za kiqur-ani, \"mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu Mlezi.\u201d Kwa maana, wingi wa ushahidi, na ubainifu wake na kuwa kwake wazi ni katika sababu za kupata yakini katika mambo yote ya kimungu, hasa katika itikadi kuu, kama vile ufufuo, na kupelekwa mahali pa hesabu, na kutolewa makaburini. Na pia, inajulikana kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye hekima. Yeye haumbi viumbe bure, wala haviachi bure. Kama vile alivyowatuma Mitume wake na akateremsha vitabu vyake kuamrisha na kuwakataza waja wake, basi ni lazima atawahamisha hadi katika nyumba ambayo kuna malipo yao, ili awalipe wafanyao mazuri kwa malipo mazuri zaidi, na awalipe wafanyao mabaya kwa ubaya wao."},{"id":2342,"sura":13,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} \"Naye ndiye aliyeikujua ardhi;\u201d yaani, aliiumba kwa ajili ya waja, akaipanua, akabariki ndani yake, akaitandaza kwa ajili ya waja, na akaweka ndani yake yale yenye manufaa kwao, \"akaweka humo milima mathubuti.\u201d Yaani, milima mikubwa, ili  isiyumbeyumbe  na viumbe. Kwa maana lau kuwa si milima, basi ingeyumbayumba na wakazi wake, kwa sababu iko juu ya mkondo wa maji, ambao haina uthabiti wowote wala kukaa tulivu isipokuwa kwa milima imara ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa vigingi vyake. Na akafanya humo \u201cmito\u201d yenye kuwanywesha wanadamu, mifugo yao na mimea yao. Basi akatoa kwayo heri nyingi katika miti, mimea na matunda, na ndiyo maana akasema: \"Na katika kila matunda akafanya jozi mbili la kiume na la kike;\u201d yaani, sampuli mbili katika wanavyovihitaji waja. \"Huufunika usiku juu ya mchana\u201d kwa hivyo peo za macho zinakuwa giza, na kila mnyama anarudi kwenye makazi yake, na kupumzika kutokana na taabu na uchovu wa mchana. Kisha wanapotimiza haja yao katika kulala, mchana unaufunika usiku; basi wanakuwa hivi wameingia asubuhi wakawa [wanaenea] katika kutafuta masilahi yao na matendo yao mchana. \u201cNa katika rehema zake ni kwamba amewafanyia usiku na mchana ili mpate kutulia humo na ili mtafute katika fadhila zake, ili mshukuru.\u201d \u201cHakika katika hayo zimo Ishara\u201d juu ya matakwa ya kiungu \u201ckwa kaumu wanaotafakari,\u201d juu yake na wanaziangalia kwa mtazamo wa kuzingatia wenye kunyesha kwamba aliyeziumba na kuziendesha na kuzibadilishabadilisha ni Mwenyezi Mungu ambaye hakuna mungu isipokuwa Yeye. Na hakuna muabudiwa asiyekuwa Yeye, na kwamba Yeye ni Mwenye kujua ghaibu na yanayoshuhudiwa, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu, na kwamba Yeye ni Muweza wa kila kitu, Mwenye hekima katika kila kitu, Msifika kwa alichokiumba na alichoamrisha, Mwenye baraka na Mtukufu."},{"id":2343,"sura":13,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} \"Na\" miongoni mwa ishara za ukamilifu wa uwezo wake na ufundi wake wa hali ya juu zaidi ni kwamba alifanya \"katika ardhi vimo vipande vilivyokaribiana na zipo bustani;\" ambayo ndani yake kuna kila aina ya miti ya mizabibu, na mitende, na mimea na visivyokuwa hivyo, na mitende, ambayo baadhi yake ni \"yenye kuchipua kwenye shina moja na isiyochipua kwenye shina moja\" kwa namna kwamba kila mti uko kivyake, na yote \"inanyweshwa katika maji yale yale\" na ardhi yake ni moja. \"Na tunaifanya baadhi yao kuwa bora kuliko mengine katika kula\" katika rangi, ladha, manufaa, na raha. Kwa hivyo, hii ardhi ni nzuri inaotesha malisho, nyasi nyingi, miti na mimea, na karibu yake kuna ardhi ambayo haioteshi malisho wala haishikilii maji, na hii nyingine inashikilia maji lakini haioti malisho. Na hii nyingine inaotesha [mimea na] miti lakini haioti malisho. Na haya matunda ni matamu na haya ni machungu na haya ni kati ya hayo. Basi je, utofauti huu ni yenyewe tu ndani yake na maumbile yake, au hilo ni kwa sababu ya majaliwa ya Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu? \"Hakika katika hayo zimo ishara kwa kaumu wanaotia mambo akilini.\" Yaani, kaumu wenye akili zinazowaongoza kwenye yale yanayowafaa na kuwaongoza katika yale yanayowafanya kunyooka na kuyafahamu maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake. Na ama wale wanaopeana mgongo na wala hawatumii akili zao, wao wanatangatanga na ni vipofu katika giza mbalimbali, na wanasitasita katika upotovu wao. Hawawezi kuongoka kufikia njia ya kwenda kwa Mola wao Mlezi, wala hawawezi kuelewa neno lake lolote."},{"id":2344,"sura":13,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"5. Na kama ukistaajabu, basi cha ajabu zaidi ni huo usemi wao: Je, tukishakuwa mchanga, kweli tutakuwa katika umbo jipya? Hao ndio waliomkufuru Mola wao Mlezi. Na hao ndio watakaokuwa na makongwa shingoni mwao, na hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu."},{"id":2345,"sura":13,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} Inawezekana kwamba maana ya kauli yake, \"Na kama ukistaajabu;\" yaani, ukistaajabu na ukuu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wingi wa ushahidi wa tauhidi, basi hakika la kustaajabisha zaidi ya hilo ni kukanusha kwa hao wanaokadhibisha na kukadhibisha kwao kufufuliwa na kusema kwao. \"Je, tukishakuwa mchanga, kweli tutakuwa katika umbo jipya?\" Yaani, hili haliwezekani kabisa kulingana na madai yao kwamba baada ya kuwa kwao udongo, kwamba Mwenyezi Mungu atawarudisha. Kwa kuwa, kwa sababu ya ujinga wao, walilinganisha uwezo wa Muumba yote na uwezo wa kiumbe, na walipoona jambo hili haliwezekani kwa uwezo wa kiumbe huyo, wakafikiri kwamba haliwezekani kwa uwezo wa Muumba yote, na wakasahau kwamba mwenyezi Mungu aliwaumba mara ya kwanza na hawakuwa chochote. Na inawezekana kwamba maana yake ni, kuwa hata ukistaajabishwa na maneno yao na kukadhibisha kwao kufufuliwa, basi hilo ni katika maajabu. Kwa maana yule anayebainishiwa ishara mbalimbali na akaona ndani yake ushahidi wa kukata juu ya kufufuliwa usiokubali shaka yoyote wala kusitasita, kisha akakakunusha hilo, basi hakika kauli yake ni miongoni mwa maajabu, lakini hilo halishangazi kutoka kwa wale \"waliomkufuru Mola wao Mlezi\" na wakakanusha upweke wake ambao ndio kitu kilicho dhahiri zaidi na kilicho wazi zaidi. \"Na hao ndio watakaokuwa na makongwa\" zinazowazuilia kuongoka, \"shingoni mwao\" kwa kuwa waliitwa kwenye Imani lakini hawakuamini, na wakawekewa mbele uwongofu lakini hawakuongoka, basi nyoyo zao zikapinduliwa kama adhabu kwa kuwa hawakuiamini mara ya kwanza. \"Na hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu\" na hawatatoka humo abadan."},{"id":2346,"sura":13,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"6. Na wanakuhimiza ulete mabaya kabla ya mazuri, hali ya kuwa zimekwisha pita kabla yao adhabu za kupigiwa mfano. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye msamaha kwa watu juu ya udhalimu wao. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mkali wa kuadhibu."},{"id":2347,"sura":13,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya ujinga wa wale waliomkadhibisha Mtume wake, wale wanaomshirikisha na wengine, ambao waliaidhiwa lakini hawakuaidhika, na ukasimamishwa ushahidi mbalimbali juu yao, lakini hawakufuata. Bali walikanusha hayo waziwazi na wakatumia kama ushahidi ustahamilivu wa Mwenyezi Mungu Mmoja, Mshindi juu yao na kwamba hakuwaharakishia adhabu kwa sababu ya dhambi zao, kwamba wao wako katika haki, kwa hivyo wakaanza kumharakisha Mtume kuwafikishia adhabu, na anasema msemaji wao: \"Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ndiyo ya haki kutoka kwako, basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tuletee adhabu yoyote iliyo chungu.\"  \"Na\" hali ni kwamba \"zimekwisha pita kabla yao adhabu za kupigiwa mfano.\" Yaani, matukio ya Mwenyezi Mungu na siku zake katika umma waliokadhibisha. Je, hawatafakari katika hali zao na kuacha ujinga wao? \"Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye msamaha kwa watu juu ya udhalimu wao.\" Yaani, haijaacha kuwateremkia waja wake heri yake na ihsani yake, na wema wake, na msamaha wake nao haujaacha kupanda kwake ushirikina wao na maasia yao. Wanamuasi, naye anawalingania kwenye mlango wake, na wanafanya uhalifu, lakini yeye hawanyimi heri yake na ihsani yake. Kwa hivyo, wakitubia kwake, basi Yeye ni kipenzi chao. Kwa sababu anawapenda wanaotubu na anawapenda wanaojitakasa. Na wasipotubia, basi yeye ndiye daktari wao. Anawajaribu kwa misiba ili awatakase kutokana na makosa yao. \u201cSema: Enyi waja wangu walijidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.\" \"Na hakika Mola wako Mlezi ni Mkali wa kuadhibu\" kwa yule ambaye haachi kuendelea kufanya madhambi, ambaye amekataa kutubu na kuomba msamaha, na kukimbilia kwa Mwenye nguvu, Mwingi sana wa kusamehe. Basi na wajihadhari waja kutokana na adhabu zake kwa wafanyao uhalifu. Kwa maana hakika mshiko wake ni mchungu sana na mkali."},{"id":2348,"sura":13,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"7. Na wale waliokufuru wanasema: Mbona hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Hakika wewe ni Mwonyaji tu, na kila kaumu ina wa kuwaongoza."},{"id":2349,"sura":13,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Yaani makafiri wanakupendekezea baadhi ya ishara wanazozitaka wao, na wanasema: \u201cMbona hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?\" Na wanaifanya kauli yao hii kuwa ni udhuru wao wa kutomuitikia Mtume, na hali ni kuwa yeye ni mwonyaji tu, wala hana lolote katika jambo hilo, na Mwenyezi Mungu ndiye anayeteremsha ishara mbalimbali. Na alimuunga mkono kwa ushahidi mbalimbali ulio wazi ambao haufichikani kwa wenye akili, na kwayo anaongoka yule ambaye ameikusudia haki. Na ama kafiri, ambaye kwa sababu ya dhuluma yake na ujinga wake anampendekezea Mwenyezi Mungu kuleta ishara mbalimbali, basi pendekezo lake hili ni batili uwongo, na uzushi. Kwa maana lau kuwa itamjia ishara yoyote ile, hataamini wala kuifuata. Kwa sababu hakukataa kuamini kwa sababu ya kukosa cha kumuonyesha usahihi wake; bali hilo ni kwa sababu ya matamanio ya nafsi yake na kufuata tamaa zake. \"Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.\" Yaani, mlinganiaji anayewalingania kwenye uwongofu kama vile Mitume na wafuasi wao, nao huwa na ushahidi na hoja mbalimbali pamoja nao zenye kuwaonyesha usahihi wa uwongofu walio nao."},{"id":2350,"sura":13,"from_aya":8,"to_aya":11,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"8. Mwenyezi Mungu anajua mimba abebayo kila cha kike, na kinachopunguka na kuzidi matumboni mwa uzazi. Na kila kitu kwake ni kwa kipimo. 9. Yeye ndiye Mwenye kujua ya ghaibu na yanayoonekana, Mkubwa, Mtukufu. 10. Ni sawa anayeficha kauli yake miongoni mwenu na anayeidhihirisha, na anayejibanza usiku na anayetembea jahara mchana. 11. Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa kaumu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anapowatakia kaumu ubaya, basi hakuna cha kuyazuia wala hawana mlinzi yeyote asiyekuwa Yeye. "},{"id":2351,"sura":13,"from_aya":8,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8 - 9} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu ujumla ya elimu yake, na upana wa kujua kwake, na kukizunguka kwake kila kitu, kwa hivyo akasema, \"Mwenyezi Mungu anajua mimba abebayo kila cha kike\" katika wanadamu na wengineo. \"Na kinachopunguka matumboni mwa uzaz;i\" yaani, ima kwa kuharibika kwa mimba au hupungua \"na kuzidi\" matumboni mwa uzazi na kuongezeka kwa ukubwa wa mimba. \"Na kila kitu kwake ni kwa kipimo\" hakitangulii kipimo hicho, wala hakichelewi, wala hakizidishi wala hakipungui isipokuwa kwa kile kinachohitajiwa na hekima na elimu yake. Kwa maana, hakika Yeye ndiye \"Mwenye kujua ya ghaibu na yanayoonekana, Mkubwa\" katika dhati Yake, majina yake, na sifa Zake, \"Mtukufu\" kwa viumbe vyake vyote kwa dhati Yake, na uwezo Wake, na ushindi Wake."},{"id":2352,"sura":13,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} \"Ni sawa\" katika elimu yake, na kusikia kwake, na kuona kwake, \"anayeficha kauli yake miongoni mwenu na anayeidhihirisha, na anayejibanza usiku.\" Yaani, mwenye kukaa mahali pa siri, \"na anayetembea jahara mchana.\" Na ilisemwa kuwa maana yake ni mwenye kuingia katika maficho yake mchana, ima ndani ya nyumba yake, pango, au mfano wa hayo."},{"id":2353,"sura":13,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} \"Kila mtu analo kundi la malaika\" wanaobadilishana zamu mchana na usiku, \"mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu.\" Yaani, wanaulinda mwili wake na roho yake kutokana na kila anayemtakia mabaya, na wanamhifadhia matendo yake, nao huwa pamoja naye daima. Kama vile elimu ya Mwenyezi Mungu inavyomzunguka, Mwenyezi Mungu amewatuma walinzi hawa juu ya waja wake ili hali zao na matendo yao yasifiche, na kwamba kisisahaulike kitu chochote. \"Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyo kwa kaumu\" miongoni mwa neema, ihsani, na maisha ya starehe, \"mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao\" kwa kutoka katika imani na kwenda kwenye ukafiri, na kutoka katika utiifu hadi katika uasi, au kutoka katika kushukuru neema za Mwenyezi Mungu hadi katika kujifahiri nazo, ambapo Mwenyezi Mungu hapo anawaondolea hayo. Na vivyo hivyo ikiwa waja watabadilisha yaliyo katika nafsi zao za ya uasi, kwenda katika kumtii Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atawabadilishia hali waliyokuwa nayo ya mashaka hadi kwenye heri, furaha, hali nzuri, na rehema. \"Na Mwenyezi Mungu anapowatakia kaumu ubaya;\" yaani, adhabu na ugumu, na jambo wanalolichukia, basi ni lazima mapenzi yake yatimie kwao, kwa maana yeye \u201chakuna cha kuyazuia\" na hakuna wa kumzuia, \u201cwala hawana mlinzi yeyote asiyekuwa Yeye,\" anayeweza kusimamia mambo yao na kuwaletea wanayoyapenda, na kuwazuia wanayoyachukia. Basi na watahadhari kudumu katika yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu, kwa kuhofu kwamba itawapata adhabu ambayo hairudishwi dhidi ya kaumu wahalifu."},{"id":2354,"sura":13,"from_aya":12,"to_aya":13,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"12. Yeye ndiye anayewaonyesha umeme kwa hofu na matumaini, na huyaanzisha mawingu mazito. 13. Na radi inamtakasa Mwenyezi Mungu kwa kumhimidi, na Malaika pia, kwa kumhofu. Naye hutuma mapigo ya radi na kumsibu kwayo amtakaye. Nao wanabishana kuhusiana na Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye Mwenye adhabu kali! "},{"id":2355,"sura":13,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Yeye Mtukufu anasema, \"Yeye ndiye anayewaonyesha umeme kwa hofu na matumaini.\" Yaani, inahofiwa kutoka kwake kupigwa na radi, kubomolewa, na aina nyengine za madhara juu ya baadhi ya matunda na mfano wake, na inatumainiwa heri yake na manufaa yake. \"Na huyaanzisha mawingu mazito\" yakija na mvua kubwa yenye manufaa kwa waja na ardhi."},{"id":2356,"sura":13,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} \"Na radi inamtakasa Mwenyezi Mungu kwa kumhimidi.\" Nayo ni ile sauti inayosikika kutoka katika mawingu yenye kuwasumbua waja. Nayo huwa imemnyenyekea Mola wake Mlezi, ikimtakasa kwa kumhimidi \"na\" wanamtakasa \"Malaika pia kwa kumhofu.\" Yaani, wao huwa wamemnyenyekea Mola wao Mlezi, wakiwa wamehofu mshiko wake. \"Naye hutuma mapigo ya radi\" nao ni moto unaotoka katika mawingu, \"na kumsibu kwayo amtakaye\" katika waja wake kulingana na apendavyo na atakavyo. \"Na Yeye ndiye Mwenye adhabu kali!\" Yaani, Yeye ndiye mwenye uwezo mkubwa na nguvu. Na hataki chochote isipokuwa hukifanya, wala hakuna chochote kinachomuwia kigumu, wala hampotei mwenye kukimbia. Na ikiwa Yeye pekee ndiye anayewafikishia waja mvua na mawingu ambayo ndani yake kuna asili ya riziki yao, na Yeye ndiye anayeendesha mambo, na viumbe vikubwa vinavyoogopewa na vinavyowasumbua waja vinamnyenyekea. Naye ni mwenye nguvu kubwa, basi Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake, bila mshirika yeyote, na ndiyo maana akasema:"},{"id":2357,"sura":13,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"14. Wa kuombwa kweli ni Yeye tu. Na hao wanaowaomba badala yake hawawajibu chochote; bali ni kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake, lakini hayakifikii. Na maombi ya makafiri hayako isipokuwa katika upotovu."},{"id":2358,"sura":13,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} Yaani, Mwenyezi Mungu peke yake ndiye \"Wa kuombwa kweli ni Yeye tu\" bila mshirika yeyote, na kumfanyia yeye tu Mtukufu dua ya kuomba kitu na dua ya ibada. Basi Yeye tu ndiye anayestahiki kuombwa dua, na hofu, matumaini, upendo, utashi, hofu kubwa, na kurudi kwake kwa sababu uungu wake ni wa haki, na uungu wa wengine ni wa batili. Basi \"hao wanaowaomba badala yake\" miongoni mwa masanamu na wenza ambao wao waliwafanya kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu \"hawawajibu chochote.\" Yaani, hawawaitikii wale wanaowaomba na kuwaabudu kwa kitu kidogo wala kikubwa, si katika mambo ya dunia wala ya Akhera. \"Kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji\" ambaye mikono yake haiwezi kuyafikia kwa sababu ya umbali wake \"ili yafike\" kwa kunyoosha viganja vyake kwenye maji hayo \"kinywani mwake,\" kwa maana ana kiu, na kutokana na kiu yake kali, anauchukua mkono wake na kuunyoosha kwenye maji ambayo hauwezi kuyafikia, kwa hivyo hawezi kuyafikia. Basi vile vile makafiri ambao wanawaomba waungu pamoja naye hawawaitikii kwa lolote wala hawawanufaishi katika nyakati zao za haja kubwa. Kwa sababu wao ni mafuqara, kama vile walivyo mafuqara wale waliowaomba. \"Hawamiliki hata uzito wa chembe  katika mbingu wala katika ardhi. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala Yeye hana msaidizi yeyote miongoni mwao.\" \"Na maombi ya makafiri hayako isipokuwa katika upotovu.\" Kwa sababu wale wanaowaomba kando na Mwenyezi Mungu ni batili, basi ibada zao na maombi yao yakabatilika. Kwa sababu njia inakuwa batili pale lengo lake linapobatilika. Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mfalme wa haki aliye wazi, ikawa kumuabudu yeye ndiyo haki inayomfungamanishia manufaa mwenye kufanya hivyo katika duniani na akhera. Na kufananisha kumuomba makafiri asiyekuwa Mwenyezi Mungu na mtu ambaye ananyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake ni miongoni mwa mifano mizuri zaidi. Kwa maana, hilo ni kufananisha na jambo lisilowezekana. Kwa kuwa kilichofananishwa nacho hakiwezekani. Na  kufungamanisha kitu na kile kisichowezekana ni katika njia bora zaidi za kukataa kitu. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, \"Hakika wale wanaozikufuru Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia Peponi mpaka apite ngamia katika tundu ya sindano.\""},{"id":2359,"sura":13,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"15. Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na katika ardhi kwa kutii na kwa lazima. Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni."},{"id":2360,"sura":13,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15} Yaani, vyote vilivyo katika mbingu na ardhi, vyote vimemtii Mola wao Mlezi, vinamsujudia \"kwa kutii na kwa lazima.\" Basi kwa kutii huwa ni yule anayesujudu na kunyenyekea kwa hiari kama vile waumini, nako kwa lazima ni kwa yule anayetakabari kufanya kumuabudu Mola wake Mlezi, lakini hali yake na maumbile yake ya asili vinamkadhibisha katika hilo. \"Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni;\" yaani, vivuli vya viumbe vinamsujudia Yeye mwanzo wa mchana na mwisho wake. Na kila kitu kinasujudu kulingana na hali yake, kama alivyosema Yeye Mtukufu \"Na hakuna kitu isipokuwa kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake.\" Kwa hivyo ikiwa viumbe vyote vinamsujudia Mola wao Mlezi kwa kupenda na kwa kutopenda, basi anakuwa yeye ndiye Mungu wa kweli, mwenye kuabudiwa na kusifiwa wa kweli. Na uungu wa wengine ni batili,na ndiyo maana akataja ubatili wake na akawekea hilo ushahidi kwa kauli yake:"},{"id":2361,"sura":13,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"16. Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao hawajimilikii manufaa yoyote wala madhara? Sema: Je, kipofu na mwenye kuona huwa sawa? Au je, huwa sawa giza na mwangaza? Au wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walioumba kama alivyoumba Yeye, na viumbe hivyo vikawachanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja, Mwenye kushinda!"},{"id":2362,"sura":13,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} Yaani, waambie hao wanaomshirikisha na masanamu na wenza. Wanaowapenda kama wanavyompenda Mwenyezi Mungu, na wanawatolea aina mbalimbali za sadaka na ibada: Je, zimepotea akili zenu mpaka mkajifanyia walinzi wengine badala yake, mkawa mnawafanya marafiki kwa kuwaabudu, ilhali wao hawastahiki hayo? Kwani wao \"hawajimilikii manufaa yoyote wala madhara?\" Na mnaacha kumfanyia urafiki Yule aliyekamilika katika majina na sifa, Mmiliki wa walio hai na wafu, ambaye mkononi mwake umo uumbaji na uendeshaji mambo, na kunufaisha na kudhuru. Basi haiwi sawa kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kumuabudu kwa wale wanaomshirikisha, kama vile hawi sawa kipofu na mwenye kuona, na kama vile haiwi \"sawa giza na mwangaza.\"  Na kama wana shaka na wamechanganyikiwa na wakamfanyia washirika, na wakadai kwamba hao wameumbwa kama kuumba kwake, na wakafanya kama kufanya kwake, basi waondolee mfanano huu na kuchanganyikiwa huku kwa ushahidi unaoashiria upweke wa Mungu katika umoja. Basi waambie: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, kwa maana haiwezekani kwa kitu chochote kujiumba chenyewe, na pia haiwezekani kuwepo bila ya Muumba, kwa hivyo ikabakia tu kwamba wana Mungu, Muumba ambaye hana mshirika yeyote katika uumbaji wake. Kwa sababu Yeye ndiye Mmoja, Mshindi. Kwa maana Umoja na ushindi havipatikani isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Kwa maana viumbe, kila kiumbe kina kiumbe kilicho juu yake ambacho kinakishinda. Kisha juu ya mshindi huyo kuna mshindi aliye juu zaidi yake, mpaka ushindi huu umalizikie kwa Aliye Mmoja, Mshindi.  Kwa hivyo, ushindi na upweke vinaambatana, na ni vya Mwenyezi Mungu tu peke yake. Kwa hivyo ikabainika kwa ushahidi wa kiakili wenye ushindi kwamba chenye kuombwa kando na Mwenyezi Mungu hakina chochote katika uumbaji wa viumbe, kwa hivyo kuabudiwa kwake ni batili."},{"id":2363,"sura":13,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"17. Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kiasi chake. Na mafuriko yakabeba mapovu yaliyokusanyika juu yake. Na kutokana na wanavyoyeyusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyopiga mifano ya haki na batili. Basi lile povu linapita kama takataka tu. Na ama kinachowafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga mifano."},{"id":2364,"sura":13,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} Mwenyezi Mungu akaufananisha uwongofu ulioteremshwa kwa Mtume wake kwa ajili ya uzima wa nyoyo na nafsi na maji aliyoyateremsha kwa ajili ya uhai wa mizimu. Alifananisha manufaa makubwa ya umma katika mwongozo ambao watu wanalazimishwa kupata na manufaa ya umma katika mvua. Alizifananisha nyoyo zinazobeba mwongozo na utofauti wake na mabonde ambamo mito inapita ndani yake. Bonde kubwa linalohifadhi maji mengi ni sawa na moyo mkubwa ulio na maarifa mengi, na bonde dogo linaloshika maji kidogo ni sawa na moyo mdogo unaoshika maarifa kidogo... na kadhalika. Amefananisha matamanio na mashaka yaliyomo ndani ya nyoyo pale ukweli unapowafikia na povu litokalo juu ya maji na juu ya vito vinavyowashwa moto vinavyokusudiwa kutakaswa na kutupwa, na kwamba vinabaki juu ya maji yanayoelea na kuyasumbua mpaka yanatoweka na kutoweka, na kilichobakia ni manufaa kwa watu wa maji safi na vito safi. Kadhalika, mashaka na matamanio, moyo huendelea kuwachukia na kujitahidi dhidi yao kwa hoja za kweli na madhubuti, mpaka yatoweke na kutoweka, na moyo ukabaki kuwa msafi na safi, usiokuwa na chochote ndani yake isipokuwa yale yanayowanufaisha watu kutokana na elimu ya haki, kuipendelea, na kuitamani. Uongo hutoweka na kuharibiwa na ukweli. \"Hakika uongo umetoweka, na akasema hapa: \"Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga mifano\" ili ukweli ubainike na uongo na uwongofu na upotofu."},{"id":2365,"sura":13,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"18. Wale waliomuitikia Mola wao Mlezi watapata mazuri. Na wale ambao hawakumuitikia, hata wangelikuwa na vyote vilivyomo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangelivitoa kujikombolea! Hao wana hesabu mbaya kabisa, na makao yao ni Jahannamu. Na hapo ni pahali pabaya mno pa kupumzikia!"},{"id":2366,"sura":13,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} Yeye Mtukufu alipobainisha haki kutokana na batili, akataja kuwa watu wamegawanyika makundi mawili: wale wanaomwitikia Mola wao Mlezi, basi akataja malipo ya hilo, na wale wasioitikia, basi akataja adhabu ya hilo pia, akasema: \"Wale waliomuitikia Mola wao Mlezi.\" Yaani, wale ambao nyoyo zao zilifuata elimu na imani, na viungo vyao vikafuata amri na makatazo, na wakawa wameafikiana na Mola wao Mlezi katika yale anayoyataka kutoka kwao, basi hao wana \"mazuri.\" Yaani, hali nzuri na malipo mazuri. Kwa hivyo wana sifa bora zaidi, matendo bora zaidi, na thawabu za haraka na za baadaye ambazo hakuna jicho limewahi kuziona, wala hakuna sikio lililowahi kusikia, wala hayakuwahi kupitia katika moyo wa mwanadamu yeyote. \"Na wale ambao hawakumuitikia\" baada ya kuwapigia mifano na kuwabainishia haki, wana hali isiyokuwa nzuri. Basi \"lau wangelikuwa na vyote vilivyomo katika ardhi na mfano wa hivyo\" vya dhahabu, fedha na vitu vingine, \"bila ya shaka wangelivitoa kujikombolea!\" Kutokana na adhabu ya Siku ya Kiyama, lakini havingekubaliwa kutoka kwao. Na hata wangewezaje kufanya hivyo? \"Hao wana hesabu mbaya kabisa\" ambayo ni hesabu itayajia mabaya waliyoyatanguliza na yale waliyoyapoteza katika haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake. Hayo yalikwisha andikwa juu yao. \"Na watasema: Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa isipokuwa hulidhibiti? Na watayakuta yote waliyoyatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.\" \"Na\" baada ya hesabu hii mbaya, \"makao yao ni Jahannamu\" ambayo imekusanya kila adhabu kama vile njaa kali, kiu kikali, Moto wenye mwako mkali, Zaqqum, Zamharir, na adh-Dhwarii', na yote ambayo Mwenyezi Mungu alitaja miongoni mwa aina mbalimbali za adhabu. \"Na hapo ni pahali pabaya mno pa kupumzikia.\""},{"id":2367,"sura":13,"from_aya":19,"to_aya":24,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"19. Je, anayejua ya kwamba yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki ni sawa na aliye kipofu? Hakika wenye akili tu ndio wanaokumbuka. 20. Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, wala hawavunji agano. 21. Na wale ambao huyaunga yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanamhofu Mola wao Mlezi, na wanaiogopa hesabu mbaya. 22. Na ambao husubiri kwa kuutaka uso wa Mola wao Mlezi, na wakasimamisha Swala, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika vile tulivyowapa; na wakayaondoa mabaya kwa mazuri. Hao ndio wana malipo ya Nyumba ya Akhera. 23. Nayo ni Bustani za milele, wataziingia wao na wale waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika watawaingilia katika kila mlango. 24. (Wakiwaambia) Assalamu Alaikum (Amani iwe juu yenu), kwa sababu ya vile mlivyosubiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera. "},{"id":2368,"sura":13,"from_aya":19,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19 - 20} Yeye Mtukufu Anasema akipambanua baina ya watu wa elimu na vitendo na kinyume chao: \"Anayejua ya kwamba yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki.\" Basi akalifahamu hilo na akalifanyia kazi, \"ni sawa na aliye kipofu?\" Ambaye hajui haki wala haitendei kazi?  Kuna tofauti kubwa kati yao kama ilivyo kati ya mbingu na ardhi. Basi mja anafaa zaidi kukumbuka na kutafakari ni lipi kati ya makundi mawili hayo ndiyo yenye hali nzuri zaidi na maishio bora zaidi, kwa hivyo akapendelea njia yake na akafuata nyuma ya kikundi chake, lakini sio kila mtu anakumbuka kile chenye kumnufaisha na kinachomdhuru. \"Hakika wenye akili tu ndio wanaokumbuka;\" yaani, wenye akili timamu na maoni kamili, ambao ndio kiini cha ulimwengu na walio bora zaidi katika wanadamu. Na ukiuliza kuhusu maelezo yao, basi hutapata bora zaidi kuliko maelezo aliyotoa Mwenyezi Mungu juu yao aliposema: \"Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu\" ambayo aliwakabidhi na akaahidiana nao kama vile kutekeleza haki zake kwa ukamilifu na kwa wingi. Kwa hivyo, kuzitimiza ni kutimizia haki zake ya kuzitimiza na kuwa na ikhlasi ndani yake. Na katika utimilifu wa kuzitekeleza ni kwamba \u201chawavunji agano.\" Yaani, agano ambalo walifunga na Mwenyezi Mungu juu yake, kwa hivyo yanaingia humo maagano yote, ahadi, viapo, na nadhiri ambazo waja wanazifunga, kwa hivyo mja hawezi kuwa miongoni mwa watu wenye akili ambao wana malipo makubwa isipokuwa kwa kuyatekeleza kwa ukamilifu na siyo kuzivunja au kuzipunja."},{"id":2369,"sura":13,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} \"Na wale ambao huyaunga yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe.\" Na hili ni jambo la jumla katika kila aliloamrisha Mwenyezi Mungu liungwe, kama vile kumuamini Yeye na Mtume wake, kumpenda Yeye, kumpenda Mtume wake, kunyenyekea, kumuabudu Yeye peke yake bila mshirika, na kumtii Mtume wake, na kuwaunga baba zao na mama zao kwa kuwafanyia wema kwa kauli na vitendo na kutowaasi, na kuwaunga jamaa wa karibu na watu wa ukoo kwa kuwafanyia ihsani kwa kauli na vitendo, na wanaunga mafungamano yaliyopo baina yao na bibi na bwana zao, marafiki zao, na wale waliowamiliki, kwa kutekeleza haki zao kikamilifu, miongoni mwa haki za kidini na za kidunia. Na sababu inayomfanya mja kuunga yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kwamba yaungwe ni kumhofu Mwenyezi Mungu na kuiogopa Siku ya Kiyama, na ndiyo maana akasema: \"Na wanamhofu Mola wao Mlezi.\" Yaani, wanamuogopa, kwa hivyo kumhofu huko na jambo la kumjia Siku ya hesabu vinawazuia kuthubutu kumuasi Mwenyezi Mungu au kutotekeleza kikamilifu katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha, wanahofu adhabu na wanatumaini malipo."},{"id":2370,"sura":13,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} \"Na ambao husubiri\" juu ya maamrisho kwa kuyatekeleza. Na kujizuia na makatazo na kuwa mbali nayo. Na kusubiri juu ya majaliwa machungu ya Mwenyezi Mungu kwa kutokasirika kwa sababu yake, lakini kwa sharti kwamba subira hiyo iwe \"kuutaka uso wa Mola wao Mlezi\" si kwa ajili ya mengineyo miongoni mwa malengo mabovu. Kwa maana hii ndiyo subira yenye manufaa, ambayo mja hujizuia nafsi yake kwayo akitafuta radhi za Mola wake Mlezi na kwa kutaraji kuwa karibu Naye na kupata malipo yake; nayo ni subira ambayo ni miongoni mwa sifa za watu wa imani. Na ama subira ambayo lengo lake ni uvumilivu na mwisho wake ni kiburi, basi hilo linatoka kwa watu wema na waovu, Muumini na kafiri, na subira hiyo siyo yenye kusifiwa kwa uhakika. \"Na wakasimamisha Swala\" pamoja na nguzo zake, masharti yake, na vikamilishi vyake, kwa nje na ndani. \"Na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika vile tulivyowapa\" Na kunaingia katika hili kutoa matumizi kwa wajibu kama vile zaka, kafara na kutoa matumizi yaliyopendekezwa, na wanatoa kwa siri na hadhara popote panapohitajika. \"Na wakayaondoa mabaya kwa mazuri;\" yaani, mwenye kuwafanyia ubaya kwa maneno au kwa kitendo, wao hawakabiliani naye kwa kitendo chake, bali wanakabiliana naye kwa kumfanyia wema, kwa hivyo wanampa mwenye kuwanyima, na wanamsamehe aliyewadhulumu, na wanamuunga aliyewakata, na wanatendea mazuri aliyewafanyia mabaya. Kwa hivyo, ikiwa wanamkabili anayewafanyia mabaya kwa wema, basi unafikiri wanamkabili vipi yule ambaye hakuwafanyia mabaya? \"Hao\" ambao wameelezwa kwa sifa hizi tukufu na matendo haya mazuri, \"wana malipo ya Nyumba ya Akhera.\""},{"id":2371,"sura":13,"from_aya":23,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23 - 24} Akayafafanua malipo hayo kwa kauli yake: \"Bustani za milele;\" yaani, mabusatani ya kudumu ambayo hawatatoka humo, wala hawatatafuta kwenda kwingine,  kwa maana hawaoni lengo lolote zaidi yake; kwa sababu ya neema iliyomo humo na furaha, ambayo kwayo mahitaji na malengo yanaisha. Na katika ukamilifu wa neema yake na furaha ya macho yao ni kwamba \"wataziingia wao na wale waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao.\" Wanaume, wanawake, na wake na wanaume zao, na vile vile wale ambao wako katika hali sawa na wao, marafiki, na wapendwa. Kwa sababu hawa pia ni katika waume au wake za na dhuria zao. \"Na Malaika watawaingilia katika kila mlango\" watawapongeza kwa usalama wao na utukufu wa Mwenyezi Mungu juu yao, na watasema: \"Assalamu Alaikum (Amani iwe juu yenu).\" Yaani, salamu na maamkizi yawe juu yenu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na hilo linajumuisha kutoweka kwa kila machukizo na linalazimu kupatikana kwa kila kipendwacho \"kwa sababu ya vile mlivyosubiri!\" Yaani, subira yenu ndiyo iliyowafikisha pahali hapa pa juu na mabustani ya thamani kubwa. \"Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera.\" Kwa hivyo, anafaa zaidi yule ambaye amejinasihi nafsi yake, nayo ikawa ina thamani kwake kupigana nayo ili huenda ikapata fungu katika sifa za watu wenye akili, na pengine ikapata nyumba hii ambayo ni matamanio ya nafsi na furaha ya roho ambayo inakusanya raha zote na furaha zote. Basi kwa mfano wake na wafanye wafanyaji, na katika hayo na washindane washindani."},{"id":2372,"sura":13,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"25. Na wale wanaovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga, na wanakata yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya uharibifu katika ardhi, hao wana laana, na wana Nyumba mbaya."},{"id":2373,"sura":13,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} Alipotaja hali ya watu wa Peponi, akataja kuwa watu wa Motoni ni kinyume cha yale aliyowaeleza nayo watu wa Peponi. Kwa hivyo akasema juu yao, \"Na wale wanaovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga.\" Yaani, baada ya kuwasisitizia ahadi hizo juu ya mikono ya Mitume wake na akazifanya kuwa kali zaidi, lakini wao hawakumkabili kwa kufuata na kujisalimisha; bali walimkabili kwa kumpa mgongo na kuvunja ahadi. \"Na wanakata yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe\" kwa hivyo hawakuunga yale yaliyo baina yao na Mola wao Mlezi kwa Imani na vitendo vyema, wala hawakuwaunga jamaa, wala hawakutimiza haki, bali walieneza uharibifu katika ardhi kwa ukafiri na maasia na kuzuia njia ya Mwenyezi Mungu na kutaka kuipotosha. \"Hao wana laana;\" yaani, kuwekwa mbali na kushutumiwa na Mwenyezi Mungu, Malaika wake na waja wake waumini. \"Na wana Nyumba mbaya\" ambayo ni Jahiim pamoja na yaliyomo miongoni mwa adhabu chungu."},{"id":2374,"sura":13,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"26. Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa kipimo. Na waliufurahia uhai wa dunia. Na uhai wa dunia kwa kulinganisha na Akhera si kitu isipokuwa ni starehe ndogo."},{"id":2375,"sura":13,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} Yaani Yeye pekee ndiye humpanulia na kumkunjulia riziki amtakaye, na kuikunja na kuifanya kuwa finyu kwa amtakaye. \"Na waliufurahia;\" yaani, makafiri \"uhai wa dunia\" furaha iliyowasababishia kutulia nao na kuisahau akhera, kwa sababu ya upungufu wa akili zao. \"Na uhai wa dunia kwa kulinganisha na Akhera si kitu isipokuwa ni starehe ndogo.\" Yaani, ni kitu duni cha kujistarehesha kwacho kidogo, kisha kinamuacha mwenyewe na baadaye kinafuatwa na taabu ndefu."},{"id":2376,"sura":13,"from_aya":27,"to_aya":29,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"27. Na wanasema wale waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye, na humwongoa anayerudi kwake. 28. Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Sikilizeni! Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndiyo nyoyo hutua! 29. Wale walioamini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri. "},{"id":2377,"sura":13,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba wale waliokufuru ishara za Mwenyezi Mungu ni wanamfanyia ukaidi Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wanapendekeza wakisema, \"Kwa nini hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?\" Na kwa wanadai kuwa lau kuwa zingewajia, basi wangeamini, lakini Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kauli yake, \"Sema: Hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye, na humwongoa anayerudi kwake.\" Yaani, mwenye kutafuta radhi zake kwa maana, uwongofu na upotofu haumo mikononi mwao mpaka wayafanye hayo kutegemea ishara mbalimbali. Na pamoja na hayo, wao ni waongo, kwani \"lau kuwa tungeliwateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeliamini, isipokuwa Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao wanafanya tu ujinga.\" Na si lazima kwa Mtume kuja na ishara ambazo wanazitaka wao na kuzipendekeza, bali akiwajia na Ishara inayobainisha yale aliyokuja nayo ya haki, hilo linatosha, na kusudi likapatikana, na linakuwa la kuwafaa zaidi kuliko kuuliza kwao ishara wanazozitaka wao. Kwa maana, lau kuwa zingewajia kulingana na walivyopendekeza, kisha wasiziamini, basi angewaharakishia adhabu."},{"id":2378,"sura":13,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Kisha Yeye Mtukufu akataja alama za Waumini, akasema: \"Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu;\" yaani, unaondoka wasiwasi wake na msukosuko wake, na hujiwa na furaha zake na raha zake. \"Sikilizeni! Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!\" Yaani, zinastahiki na zinafaa zaidi kutotulia kwa chochote kisichokuwa kumkumbuka. Kwani hakuna kitu kitamu zaidi mioyoni, wala cha kutamaniwa zaidi, wala kitamu zaidi kuliko kumpenda Muumba wake, kutulia kwa sababu yake, na kumjua Yeye, na kulingana na kiasi cha kumjua kwake, na kumpenda kwake, ndiyo kunakuwa kumkumbuka Yeye. Haya ni kama itasemwa kwamba kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni mja kumkumbuka Mola wake Mlezi kwa kumtakasa, na kusema hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kutoa takbira na mambo mengine. Na imesemwa kuwa kinachokusudiwa na kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni Kitabu chake alichokiteremsha kiwe ukumbusho kwa Waumini. Kwa hivyo, kwa mujibu wa maana unakuwa utulivu wa moyo kwa kujua maana za Qur\u2019an na hukumu zake, na kutulia kwa sababu ya hayo. Kwa maana hizo zinaonyesha haki iliyo wazi inayoungwa mkono na ushahidi na hoja, na kwa hayo mioyo hutulia. Kwani haitulii isipokuwa kwa yakini na elimu, na hilo limehakikishwa ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa njia iliyo timilifu na kamili zaidi. Na ama vitabu vinginevyo ambavyo havikirejelei, hivyo mioyo havitulii kwa sababu yake; bali haiachi kuwa na wasiwasi kwa sababu ya kupingana kwa ushahidi na kugongana kwa hukumu. \"Na lau kuwa ingekuwa inatoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka wangelikuta ndani yake hitilafu nyingi.\" Na haya yanajulikana kutoka katika habari za Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kukitafakari, na kutafakari aina nyinginezo za elimu, kwani atapata tofauti kubwa kati yake na hizo."},{"id":2379,"sura":13,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Kisha akasema yeye Mtukufu, \"Wale walioamini na wakatenda mema.\" Yaani, walimuamini Mwenyezi Mungu kwa nyoyo zao, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na wakaisadikisha imani hiyo kwa matendo mema. Matendo ya mioyo, kama vile upendo, hofu, na kumtumaini Mwenyezi Mungu. Na matendo ya viungo, kama vile swala na mfano wake. \"Watakuwa na raha na marejeo mazuri;\" yaani, wana hali nzuri na marejeo mazuri, na hayo ni kwa sababu watapata radhi ya Mwenyezi Mungu kuwatukuza katika dunia na akhera, na wana raha kamili na utulivu kamili, na miongoni mwao ni mti wa Tuuba uliomo ndani ya Pepo ambao mpanda farasi anaweza kwenda katika kivuli chake kwa muda wa miaka mia bila ya kukimaliza, kama ilivyokuja katika Hadithi sahihi."},{"id":2380,"sura":13,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"30. Ndivyo hivyo tulivyokutuma kwa umma ambao wamekwsiha pita kabla yao umma nyingine, ili uwasomee yale tuliyokufunulia, na wao wanamkufuru Rahmani (Mwingi wa Rehema)! Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Juu yake nimetegemea, na kwake ndiyo marejeo!"},{"id":2381,"sura":13,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. - \"Ndivyo hivyo tulivyokutuma\" kwa kaumu yako ili uwalinganie kwenye uwongofu. \"Wamekwsiha pita kabla yao umma nyingine\" ambao tuliwatumia Mitume wetu. Basi wewe si kitu kigeni miongoni mwa Mitume mpaka wakaukanusha utume wako, na wala husemi kwa kupenda kwako, bali unawasomea aya za Mwenyezi Mungu ambazo Mwenyezi Mungu alikufunulia, ambazo na zinazisafisha nyoyo, kuzitakasa nafsi, na hali ni kuwa kaumu yako wanamkufuru Mwingi wa Rehema, na hawakuikabili rehema yake na wema wake - ambazo kubwa zake zaidi ni kuwa tulikutuma kwao kama Mtume na tukakuteremshia kitabu - kwa kuzikubali na kushukuru. Lakini badala yake walizikabili kwa kuzipinga na kuzikataa. \"Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye.\" Na hili linajumuisha zile aina mbili za tauhid: Tauhidi ya uungu na tauhidi ya umola. Basi yeye ndiye mola wangu mlezi ambaye amenilea kwa neema zake tangu aliponiumba, naye ndiye Mungu wangu ambaye \"Juu yake nimetegemea\" katika mambo yangu yote na kwake Yeye ninarejea katika ibada zangu zote na mahitaji yangu."},{"id":2382,"sura":13,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"31. Na kama ingelikuwako Qur-ani inayoendeshewa milima, na kupasuliwa kwayo ardhi, na kusemeshwa kwayo wafu, (basi ingelikuwa Qur-ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua wale walioamini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa bila ya shaka angeliwaongoa watu wote? Na wale waliokufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa yale waliyoyatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ije ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake."},{"id":2383,"sura":13,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} Yeye Mtukufu Anasema akibainisha ubora wa Qur-ani hii Tukufu juu ya vitabu vingine vyote vilivyoteremshwa: \"Na kama ingelikuwako Qur-ani\" katika Vitabu vya kiungu \"itaendeshewa milima\" kutoka mahali pake, \"na kupasuliwa kwayo ardhi\" mabustani na mito, \"na kusemeshwa kwayo wafu\" basi ingekuwa Qur'ani hii. \"Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu\" yeye analeta ishara ambazo inazihitaji hekima yake. Basi wana nini hao wanaokadhibisha wanapendekeza ishara wanazozipendekeza wao? Je, wao na wengine wana chochote katika jambo hili? \"Je, hawajajua wale walioamini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa bila ya shaka angeliwaongoa watu wote?\" Basi na wajue kwamba Yeye ni Muweza wa kuwaongoa wote, lakini hataki hilo, bali humwongoa amtakaye na humpoteza amtakaye. \"Na wale waliokufuru hawaachi\" wanaendelea na ukafiri wao, wala hawazingatii wala hawaaidhiki. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anawafikishia maangamizi yanayowasibu katika makazi yao, au yanafika karibu nayo, ilhali wao wanaendelea tu na ukafiri wao. \"Mpaka ije ahadi ya Mwenyezi Mungu\" ambayo aliwaahidi ya kushuka kwa adhabu ya kuendelea isiyoweza kuondolewa. \"Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.\" Na hili ni tishio kwao na kuhofisha juu ya kuteremshwa kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu aliahidi kwa sababu ya ukafiri wao, ukaidi wao na dhulma yao."},{"id":2384,"sura":13,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"32. Na hakika walifanyiwa kejeli Mitume waliokuwa kabla yako. Na nikawapururia wale waliokufuru, kisha nikawashika! Basi ilikuwaje adhabu yangu!"},{"id":2385,"sura":13,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} Yeye Mtukufu anamwambia Mtume wake, akimuimarisha na kumfariji, \"Na hakika walifanyiwa kejeli Mitume waliokuwa kabla yako\" Wewe si Mtume wa kwanza kukadhibishwa na kuudhiwa. \"Na nikawapururia wale waliokufuru\" Mitume wao mpaka wakadhani kuwa hawataadhibiwa, \"kisha nikawashika\" kwa aina mbalimbali za adhabu. \"Basi ilikuwaje adhabu yangu!\" Ilikuwa adhabu kali na adhabu chungu. Basi wasidanganyike hao waliokukadhibisha na kukufanyia stihizai na kutupa kwetu muhula. Wao wana mfano kutoka kwa wale waliokuwa kabla ya miongoni mwa umma. Basi na wajihadhari waje kufanyiwa kama walivyofanyiwa hao."},{"id":2386,"sura":13,"from_aya":33,"to_aya":34,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"33. Je, anayeisimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma...? Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa na washirika! Sema watajeni. Au ndiyo mnampa habari ya yale asiyoyajua katika ardhi, au ni maneno matupu tu? Bali wale waliokufuru wamepambiwa njama zao na wamezuiliwa njia ya sawasawa. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, basi hana wa kumwongoa yeyote. 34. Wana adhabu katika uhai wa dunia, na adhabu ya Akhera hakuna shaka ndiyo ngumu zaidi. Na wala hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu. "},{"id":2387,"sura":13,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: \"Je, anayeisimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma...?\" Kwa malipo ya haraka na ya baadaye, kwa uadilifu na haki. Naye ni Mungu, Mwenye baraka, Mtukufu, ni kama yule asiyekuwa hivyo. Na ndiyo maana akasema: \"Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa na washirika!\" Ilhali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu Mmoja, wa kipekee, Mkusudiwa ambaye hana mshirika yeyote wala mwenza, wala aliye sawa naye. \"Sema\" uwaambie ikiwa ni wakweli. \"Watajeni\" ili mjue hali zao. \"Au ndio mnampa habari ya yale asiyoyajua katika ardhi\" kwa maana ikiwa Yeye ndiye anayeyajua ya ghaibu na yanayoshuhudiwa, naye anajua kwamba hana mshirika yeyote, itajulikana kwa hayo ubatili wa madai ya kwamba ana mshirika, na kwamba mko katika nafasi ya mwenye kumjulisha Mwenyezi Mungu kwamba ana mshirika ilhali hamjui, na hii ndiyo batili kuliko zote! Na ndiyo maana akasema: \"Au ni maneno matupu tu?'' Yaani, mwisho kabisa wa madai ya kwamba Yeye Mtukufu ana mshirika ni kwamba hilo linategemea maneno matupu tu yao. Na ama kiuhakika, hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna yeyote miongoni mwa viumbe anayestahiki kuabudiwa. Lakini \"wale waliokufuru wamepambiwa njama zao\" ambazo walizipanga. Nazo ni kufuru yao, na ushirikina wao na kukadhibisha kwao Aya za Mwenyezi Mungu \"wamezuiliwa njia ya sawasawa\" yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na makazi ya utukufu wake. \"Na yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, basi hana wa kumwongoa yeyote.\" Kwa sababu hakuna yeyote mwenye mamlaka katika jambo hili isipokuwa Mwenyezi Mungu."},{"id":2388,"sura":13,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} \"Wana adhabu katika uhai wa dunia, na adhabu ya Akhera hakuna shaka ndiyo ngumu zaidi\" kuliko adhabu ya dunia, kwa sababu ya ukali wake na kudumu kwake. \"Na wala hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu,\" anayeweza kuwalinda kutokana na adhabu ya [Mwenyezi Mungu]. Kwa kuwa adhabu yake anapoielekeza kwao, hakuna kinachoweza kuizuia."},{"id":2389,"sura":13,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"35. Mfano wa Bustani waliyoahidiwa wachamungu, kwa chini yake inapita mito, chakula chake ni cha daima, na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale waliomcha Mungu. Na mwisho wa makafiri ni Moto."},{"id":2390,"sura":13,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: \"Mfano wa Bustani waliyoahidiwa wachamungu\" wale walioacha yale aliyowakataza Mwenyezi Mungu, na wala hawapunguza katika yale aliyowaamrisha kuyafanya. Yaani, maelezo yake na uhalisia wake, ni kwamba \"kwa chini yake inapita mito\" mito ya asali, mito ya mvinyo, mito ya maziwa, na mito ya maji yapitayo si ndani ya sehemu iliyodidimia kwa kina ndani ya ardhi, nayo yananywesha bustani hizo na miti hiyo, na inazaa kila aina ya matunda. \"Chakula chake ni cha daima na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale waliomcha Mungu. Na mwisho wa makafiri ni Moto,\" basi ni tofauti ngapi zilizo wazi baina ya makundi haya mawili?"},{"id":2391,"sura":13,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"36. Na wale tuliowapa Kitabu wanayafurahia yale yaliyoteremshwa kwako. Na katika makundi mengine wapo wanaoyakataa baadhi yake. Sema: Hakika nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu tu, na wala nisimshirikishe. Kwake Yeye ndiko ninaitia na kwake Yeye ndiko marejeo."},{"id":2392,"sura":13,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: \"Na wale tuliowapa Kitabu;\" yaani, tuliwaneemesha kwacho, na tukawaneemesha kukijua \"wanayafurahia yale yaliyoteremshwa kwako\" kwa hivyo wanayaamini na kuyasadiki, na wanafurahia kuafikiana Vitabu vyenyewe kwa vyenyewe, na kusadikishana vyenyewe kwa vyenyewe. Na hii ndiyo hali ya wale walioamini miongoni mwa Watu wa Vitabu vile viwili. \"Na katika makundi mengine wapo wanaoyakataa baadhi yake.\" Yaani, katika makundi ya makafiri waliofanya vikundi dhidi ya haki kuna wale wanaokataa baadhi ya Qur-ani hii na hawayaamini. Kwa hivyo mwenye kuongoka, basi ni kwa ajili yake mwenyewe, na mwenye kupotea, basi hakika anapotea kwa hasara yake, wewe hakika ewe Muhammad, ni muonyaji tu mwenye kulingania kwa Mwenyezi Mungu. \"Sema: Hakika nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu tu, na wala nisimshirikishe.\" Yaani, nimeamrishwa nimuabudu kwa kumfanyia yeye peke yake tu dini. \"Kwake Yeye ndiko ninaitia na kwake Yeye ndiko marejeo\" yangu ambayo nitarejea, kisha atanilipa kwa yale niliyoyafanya ya kuilingania dini yake na kutekeleza yale niliyoamrishwa."},{"id":2393,"sura":13,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"37. Na ndivyo hivyo tumeiteremsha (Qur-ani hii kuwa ni) hukumu kwa lugha ya Kiarabu. Na ukifuata matamanio yao baada ya elimu hii iliyokujia, hutakuwa na rafiki yeyote wala mlinzi kando na Mwenyezi Mungu."},{"id":2394,"sura":13,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37} Yaani, hakika tuliiteremsha Qur-ani hii na Kitabu hiki, \"hukumu kwa lugha ya Kiarabu.\" Yaani, hukumu iliyo madhubuti kwa lugha iliyo wazi zaidi na yenye ufasaha zaidi ili asiingie shaka yoyote ndani yake wala mchanganyiko, na ili iwe sababu ya kukifuata hicho peke yake wala asibembelezwe yeyote kukifuata, wala kisifuatwe kilicho kinyume yake na yenye kukipinga miongoni mwa matamanio ya wale wasiojua. Na ndiyo maana akamtishia Mtume wake - pamoja na kwamba yeye amehifadhiwa hafanyi dhambi - ili iwe neema yake juu yake kwamba kumhifadhi, na ili umma wake uchukue kiigizo kutoka kwake katika hukumu mbalimbali, basi akasema: \"Na ukifuata matamanio yao baada ya elimu hii iliyokujia\" iliyo wazi, ambayo inakukataza kufuata matamanio yao. \"Hutakuwa na rafiki yeyote kando na Mwenyezi Mungu\" atakayekusimamia na kukuletea mambo uyapendayo \"wala mlinzi\" atakayekukinga kutokana na mambo yachukizayo."},{"id":2395,"sura":13,"from_aya":38,"to_aya":39,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"38. Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukawafanya wawe na wake na dhuria. Na haikuwa kwa Mtume yeyote kuleta ishara isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila kipindi kina hukumu yake iliyoandikwa. 39. Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya hukumu zote zilizoandikwa iko kwake. "},{"id":2396,"sura":13,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} Yaani, wewe si mtume wa kwanza kutumwa kwa watu hadi waushangae  utume wako. Hakika \"tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukawafanya wawe na wake na dhuria.\" Basi wasikutie doa adui zako ikiwa una wake na dhuria kama walivyokuwa ndugu zako miongoni mwa Mitume. Basi ni kwa kitu gani wanakukashifu kwa hayo, ilhali wanajua kwamba Mitume waliokuwa kabla yako walikuwa hivyo, isipokuwa tu kwa ajili ya kuepeana kwao mgongo kuovu na matamanio yao. Na wakikuomba ishara wanayoipendekeza wao, basi wewe huna chochote katika jambo hilo. Kwa maana, \"haikuwa kwa Mtume yeyote kuleta ishara isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu\" Na Mwenyezi Mungu haliruhusu hilo isipokuwa kwa wakati wake alioupitisha na kuuandika. \"Kila kipindi kina hukumu yake iliyoandikwa\" hakiitangulii hukumu hiyo iliyoandikwa wala hakichelewi zaidi yake. Kwa hivyo kuziharakisha kwao ishara au adhabu hakufanyi Mwenyezi Mungu kutanguliza au kuchelewesha alichoandika, pamoja na kwamba Yeye Mtukufu hufanya atakavyo."},{"id":2397,"sura":13,"from_aya":39,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39} \"Mwenyezi Mungu hufuta ayatakayo\" katika hukumu na majaliwa, \"na huthibitisha\" atakayo katika hayo. Na kufuta huku na kubadilisha huku si katika yale aliyotangulia kuyajua na ikayaandika kalamu yake. Hayo hayaingiwi na mabadiliko wala mageuzi, kwa sababu hilo haliwezekani kwa Mwenyezi Mungu kutokea upungufu wowote wala dosari katika elimu yake. Na ndiyo maana akasema: \"Na asili ya hukumu zote zilizoandikwa iko kwake.\" Yaani, ubao uliohifadhiwa ambao vitu vyote vinaurudia kwa maana huo ndio asili yake, nayo ni matawi yake na vipengele. Kwa hivyo, mageuzi na mabadiliko hutokea katika matawi na vipengele, kama vile matendo ya mchana na usiku ambayo Malaika huyaandika na Mwenyezi Mungu anawekea kuthibiti kwake sababu mbalimbali, na kufutwa kwake pia anakuwekea sababu mbalimbali pia, na sababu hizi hazizidi yale yaliyoandikwa katika Ubao Uliohifadhiwa. Kama vile Mwenyezi Mungu alivyofanya wema, kuunga jamaa, na ukarimu kuwa miongoni mwa njia za kurefusha umri na upana wa riziki, kama vile pia alivyofanya maasia kuwa sababu ya kuondoa baraka ya riziki na umri, na kama vile alivyofanya njia za kuokoka kutokana na maangamivu na maafa kuwa ndizo sababu za usalama; na akafanya kujitia katika hayo ndiyo sababu ya maafa. Basi Yeye ndiye anayeendesha mambo kulingana na uwezo wake na utashi wake. Na kile anachokiendesha miongoni mwa mambo hayahalifu yale aliyokwisha yajua na kuyaandika katika Ubao Uliohifadhiwa."},{"id":2398,"sura":13,"from_aya":40,"to_aya":41,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"40. Na ikiwa tutakuonyesha baadhi ya yale tuliyowaahidi au tukakufisha kabla yake, juu yako wewe ni kufikisha ujumbe tu na juu yetu ni hesabu. 41. Je, hawakuona kwamba tunaijia ardhi tukiipunguza kutokea nchani mwake? Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hakuna wa kurekebisha hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhesabu. "},{"id":2399,"sura":13,"from_aya":40,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: - Usiwaharakishie kufikiwa na adhabu waliyoahidiwa.  Kwa maana hata wakiendelea na upindukiaji wao na ukafiri wao, basi ni lazima yatawafika yale waliyoahidiwa. Ima tutakuonyesha adhabu hiyo katika dunia, kwa hivyo yafurahie hayo macho yako, au tukufishe kabla kuwafikishia adhabu hiyo. Na hiyo si kazi yako; \"juu yako wewe ni kufikisha ujumbe tu\" na kuwabainishia viumbe, \"na juu yetu ni hesabu.\" Basi tutawahesabu viumbe kwa yale waliyoyafanya katika yale yaliyo juu yao na yale waliyokosa kufanya vyema, na tutawalipa thawabu au kuwaadhibu."},{"id":2400,"sura":13,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41} Kisha akasema akiwaahidi adhabu wale wanaokadhibisha, \"Je, hawakuona kwamba tunaijia ardhi tukiipunguza kutokea nchani mwake?\" Hapa ilisemwa maana yake ni kuwaangamiza wale wanaokadhibisha na kuwafutilia mbali madhalimu. Na ilisemwa pia kwamba hilo ni kwa kuziteka nchi za washirikina na kuwapunguza katika mali zao na miili yao, na kauli zinginezo pia zilisemwa. Na kauli iliyo dhahiri - na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi - ni kwamba maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu anaziteka ardhi za wale wanaokadhibisha hawa na kuzifutilia mbali, na anazifikishia misiba kwenye ncha zake ili liwe onyo kwao kabla ya kufutilia mbali na upungufu, na tena Mwenyezi Mungu huwafikishia misiba ambayo hakuna yeyote anayeweza kuizuia. Na ndiyo maana akasema: \"Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hakuna wa kupinga hukumu yake,\" na inaingia katika hili hukumu yake ya kisheria na ya kimajaliwa, na ya kimalipo. Kwa hivyo, hukumu hizi ambazo Mwenyezi Mungu anazihukumu zinapatikana kwa sababu ya hekima ya hali ya juu zaidi na ubora mkubwa zaidi, hazina dosari yoyote wala upungufu; bali zimejengeka juu ya haki na uadilifu, na sifa njema. Kwa hivyo hawezi kuzirekebisha, na wala hakuna njia yoyote ya kuzitia dosari. Kinyume na hukumu ya asiyekuwa yeye, hiyo huenda ikaafikiana na usahihi au huenda isiafikiane nao. \"Naye ni Mwepesi wa kuhesabu\" kwa hivyo, wasiiharakishe adhabu, kwa maana kila kijacho, basi ki karibu."},{"id":2401,"sura":13,"from_aya":42,"to_aya":43,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"42. Na walipanga njama wale waliokuwa kabla yao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye njama zote. Yeye anajua kile inachochuma kila nafsi. Na makafiri watakuja jua ni ya nani nyumba ya mwisho Akhera! 43. Na wale waliokufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye elimu ya Kitabu. "},{"id":2402,"sura":13,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na walipanga njama wale waliokuwa kabla yao\" dhidi ya Mitume wao na haki waliyokuja nayo Mitume, lakini njama hizo hazikuwafaa kitu, wala hawakufanya lolote. Kwa maana hapo walikuwa wanapigana na Mwenyezi Mungu na kujitokeza dhidi yake, \"lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye njama zote.\" Yaani, hakuna yeyote awezaye kupanga njama isipokuwa kwa idhini yake na chini ya hukumu yake na majaliwa yake. Kwa hivyo, ikiwa wanapanga njama dhidi ya dini yake, basi njama yao hiyo itawarudia kwa kuambulia patupu na majuto. Kwa maana Mwenyezi Mungu \"anajua kile inachochuma kila nafsi\"  wasiwasi wake, utashi wake, na vitendo vyake vya dhahiri na vilivyofichika. Na njama lazima ni katika kuchuma kwake, kwa hivyo njama zao hizo hazifichikani kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo haiwezekani kwao kufanya njama zenye kuidhuru haki na watu wake na ikawanufaisha kitu. \"Na makafiri watakuja jua ni ya nani nyumba ya mwisho Akhera!\" Yaani, je, itakuwa yao au ya Mitume wake? Na inajulikana vyema kwamba mwisho mwema ni wa wachamungu, si wa ukafiri na matendo yake."},{"id":2403,"sura":13,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} \"Na wale waliokufuru wanasema: Wewe hukutumwa;\" yaani, wanakukadhibisha wewe na yale uliyotumwa nayo. \"Sema\" uwaambie ikiwa watataka shahidi juu ya hilo, \"Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi.\" Na ushahidi wake ni kwa maneno yake, na vitendo vyake, na kukiri kwake. Ama kauli yake, basi ni kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyafunua kwa yule wa kweli zaidi katika viumbe vyake miongoni mwa yale anayothibitisha kwayo ujumbe wake. Na ama kitendo chake, basi ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuunga mkono Mtume wake na akamnusuru nusura iliyokuwa nje ya uwezo wake na uwezo wa masahaba wake na wafuasi wake. Na huu ni ushahidi kutoka Kwake kwa vitendo na uungaji mkono. Na ama kukiri kwake, basi ni kwamba alimjulisha Mtume kuhusu yeye kuwa ni Mtume, na kwamba aliwaamrisha watu wamfuate. Kwa hivyo, mwenye kumfuata, basi huyo ana radhi za Mwenyezi Mungu na utukufu wake. Na asiyemfuata, basi huyo ana Moto na ghadhabu, na mali yake na damu yake ni halali kwa Mtume huyu, na Mwenyezi Mungu amemkubalia hilo. Kwa hivyo, angemdanganyishia uongo hata kidogo, basi angemharakishia adhabu. \"Na pia yule mwenye elimu ya Kitabu\" na hili linajumuisha wazuoni wote wa Watu wa Vitabu hivi viwili. Kwani wao wanamshuhudia Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - katika wale walioamini na wakaifuata haki, wanatangaza ushahidi huo ulio juu yake. Na mwenye kuficha hilo, basi kujulisha kwa Mwenyezi Mungu juu yake kwamba ana ushahidi kunatosha zaidi hata kuliko habari yake mwenyewe. Na hata kama hangekuwa na ushahidi, basi angekataa kumfanya yeye kuwa shahidi kwa hijja. Kwa hivyo, kunyamaza kwake kunaonyesha kuwa ana ushahidi uliofichwa. Na Mwenyezi Mungu aliamrisha kutafuta ushahidi wa Watu wa Kitabu kwa sababu wao ni watu wa jambo hili, na katika kila jambo ni watu wake tu ndio wanaotafuta ushahidi wao, na wale ambao wajua zaidi katika wale wasiokuwa wao. Tofauti na yule ambaye ni mgeni katika hilo, kama vile wasiojua kusoma na kuandika katika washirikina wa Kiarabu na wengineo. Basi hakuna faida yoyote katika kutafuta ushahidi wao kwa sababu ya ukosefu wao wa uzoefu wao na maarifa yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi."},{"id":2404,"sura":13,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya Surat Ra'd. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote."}]}