{"result":[{"id":2584,"sura":16,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat An-Nahl"},{"id":2585,"sura":16,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Nayo iliteremka Makka"},{"id":2586,"sura":16,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":2587,"sura":16,"from_aya":1,"to_aya":2,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Amri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiiharakishe. Ametakasika na ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo. 2. Huwateremsha Malaika na ufunuo kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake kwamba onyeni kuwa hakuna mungu yeyote isipokuwa Mimi, basi nicheni Mimi. "},{"id":2588,"sura":16,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Mwenyezi anasema akionyesha ukaribu wa yale aliyoahidi kusisitiza kutokea kwake \"Amri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiiharakishe;\" kwa maana, inakuja. Na kila kijacho, basi kiko karibu. \"Ametakasika na ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo\" kama vile kumnasibisha na mshirika, mwana, mke, mwenye kufanana naye na vinginevyo miongoni mwa yale waliyomnasibisha nayo washirikina, ambayo hayaufailii utukufu wake au yanapingana na ukamilifu wake."},{"id":2589,"sura":16,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Na alipojitakasa na yale waliyomuelezea nayo maadui zake, akataja ufunuo ambao anauteremsha juu ya manabii wake miongoni mwa yale yanayopasa kufuatwa katika kutaja yale yanayofailia kunasibishwa na Mwenyezi Mungu miongoni mwa sifa za ukamilifu. Kwa hivyo akasema, \"Huwateremsha Malaika na ufunuo kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake\" katika wale anaowajua kwamba wanafailia hilo la kuubeba ujumbe wake. Na kiini cha wito wa wajumbe hao wote na pale inapozungukia miito hiyo ni kauli yake \"kwamba onyeni kuwa hakuna mungu yeyote isipokuwa Mimi.\" Yaani, kumjua Mwenyezi Mungu, na kumpwekesha katika sifa za ukuu, ambazo ni sifa za uungu, na kumwabudu yeye peke yake bila ya mshirika yeyote. Kwani hilo ndilo aliloteremsha kwalo vitabu vyake, na akawatuma Mitume wake, na akafanya sheria zote kulingania hilo, na kuhimiza, na kupambana na mwenye kulipiga vita, na akafanya kinyume chake."},{"id":2590,"sura":16,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"Kisha akataja ushahidi na hoja mbalimbali juu ya hilo, kwa hivyo akasema:"},{"id":2591,"sura":16,"from_aya":3,"to_aya":9,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"3. Ameziumba mbingu na dunia kwa Haki. Ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo. 4. Amemuumba mtu kwa tone la manii. Na tazama, akawa mshindani aliye dhahiri. 5. Na aliwaumbia wanyama. Katika hao mna vifaa vya kutia joto, na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala. 6. Na katika hao mnapata furaha pale mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi. 7. Nao hubeba mizigo yenu kupeleka kwenye miji msiyoweza kuifikia isipokuwa kwa mashaka ya nafsi. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu. 8. Na farasi, nyumbu, na punda ili muwapande, na wawe ni pambo. Na anaumba msivyovijua. 9. Na ni juu ya Mwenyezi Mungu kuelekeza Njia. Na zipo njia za upotovu. Na angelipenda, angeliwaongoa nyote. "},{"id":2592,"sura":16,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0622\u064a\u0627\u062a","text":"Sura hii inaitwa Sura ya neema. Kwa maana, Mwenyezi Mungu alitaja mwanzoni mwake misingi ya neema na kanuni zake, na mwishowe akataja vyenye kuzitimiza na kuzikamilisha."},{"id":2593,"sura":16,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} Kwa hivyo akajulisha kwamba \"Ameziumba mbingu na dunia\" ili waja watumie hilo kama ushahidi juu ya ukuu wa Muumba wake, na sifa zake za ukamilifu. Na wajue kwamba aliziumba ili ziwe makao ya waja wake wanaomwabudu kwa kile anachowaamuru miongoni mwa sheria mbalimbali, ambazo aliziteremsha juu ya ndimi za Mitume wake. Na kwa sababu hiyo akajitakasa kutokana na shirki na wale wanaomshirikisha, akasema: \"Ametukuka na hayo wanayoshirikisha nayo.\" Yaani, ametakasika na ni mkuu mno kuhusishwa na ushirikina wao huo. Kwa maana Yeye ndiye Mungu wa haki, ambaye ibada, upendo, na unyenyekevu havifai kufanywa isipokuwa kwa ajili yake tu."},{"id":2594,"sura":16,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Na alipotaja kuumbwa kwa mbingu [na dunia], akataja kuumbwa kwa vile vilivyo ndani ya viwili hivyo, na akaanza kwa kitukufu zaidi kati ya hivyo, ambacho ni mwanadamu, akasema: \"Amemuumba mtu kwa tone la manii\" na akaendelea kuliendesha na kulipandisha, na kulikuza mpaka likawa mwanadamu mkamilifu wa viungo vya nje na vya ndani. Na akamfunika kwa neema zake nyingi mpaka anapokamilika, anajifahiri na nafsi yake na kujiona. \"Na tazama, akawa mshindani aliye dhahiri.\" Inawezekana kwamba kinachomaanishwa ni kuwa yeye anakuwa mshindani wa Mola wake Mlezi, kwa kumkufuru, na kujadiliana na Mitume wake, na anakadhibisha ishara zake, na anasahau uumbaji wake wa kwanza, na neema ambazo Mwenyezi Mungu alimneemesha, naye akazitumia katika kumuasi. Na inawezekana kwamba maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu kutokana na tone la manii, kisha akaendelea kumhamisha kutoka katika hatua moja hadi nyingine, mpaka alipokuwa na akili timamu, mwenye ubongo na maoni, akaanza kubishana na kujadiliana na Mola wake Mlezi. Basi na mja amshukuru Mola wake Mlezi ambaye alimfikisha katika hali hii, ambayo yeye mwenyewe hawezi kufanya chochote katika hayo."},{"id":2595,"sura":16,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} \"Na aliwaumbia wanyama\" kwa ajili ya faida yenu na masilahi yenu. Na kati ya faida zake kubwa, ni kwamba \"Katika hao mna vifaa vya kutia joto\" kutokana na nguo, matandiko na nyumba mnazotengeneza kutoka kwa sufu zao, na manyoya yao, na nywele zao. \"Na\" katika hao pia kuna \"manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala.\""},{"id":2596,"sura":16,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} \"Na katika hao mnapata furaha pale mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi.\" Kwa sababu uzuri wake hauwarudii wao kwa chochote, lakini nyinyi ndio mnaojipamba kwao kama tu vile mnavyojipamba kwa nguo zenu, watoto, na wana wenu, na mali zenu na mnafurahishwa na hayo."},{"id":2597,"sura":16,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} \"Nao hubeba mizigo yenu\" mizito, na hata kukubeba nyinyi wenyewe, \"kupeleka kwenye miji msiyoweza kuifikia isipokuwa kwa mashaka ya nafsi\" Lakini Mwenyezi Mungu amewatiisha kwa ajili yenu. Basi baadhi yao mnawapanda, na baadhi yao kuna wale mnaobebea juu yao mnachotaka katika mizigo hadi katika miji za mbali na pande makubwa. \"Hakika Mola wenu Mlezi ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu.\" Kwa maana aliwatiishia wale mnaolazimika kuwa nao na kuwahaitaji zaidi. Basi ni zake sifa njema zote kama inavyoufailia utukufu wa uso wake, na ukuu wa mamlaka yake, na upana wa ukarimu wake, na wema wake."},{"id":2598,"sura":16,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} \"Na farasi, nyumbu, na punda\" mara mnawatumia katika kuwapanda kwa lazima na mara kwa ajili ya kutafuta uzuri na pambo, na hakutaja kuwala hawa, kwa sababu ni haramu kumla nyumbu na punda, na pia mara nyingi farasi hawaliwi, bali inakatazwa kuwachinja kwa ajili ya kuwala kwa kuhofia waje kukosekana. Vinginevyo, imethibiti katika Kitabu cha hadithi Sahihi kwamba Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - aliruhusu kula nyama ya farasi. \"Na anaumba msivyovijua\" katika vile vitakavyokuwa baada ya kuteremka kwa Qur-ani miongoni mwa vitu ambavyo viumbe wanavipanda katika nchi kavu, baharini, hewani, na wanavitumia katika faida zao na masilahi yao. Hivyo hakuvitaja kwa majina yake, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hakutaja katika Kitabu chake isipokuwa kile ambacho waja wake wanakijua au wanajua kinachofanana nacho. Na ama kile kisichokuwa na mfano wake, basi lau hicho kingetajwa, basi hawangekijua wala hawangefahamu makusudio yake. Ndiyo maana akataja msingi unaokusanya yale wanayoyajua na wasiyoyajua, kama alivyotaja neema za Peponi, na akataja humo kile tunachokijua na tunatazama mfano wake, kama vile mitende, mizabibu, makomamasi, na akataja kwa ujumla yale tusiyoyajua katika kauli yake \"Humo katika kila matunda zimo namna mbili.\" Basi vile vile hapa ametaja kile vile tunavyovijua miongoni mwa vipando, kama vile farasi, nyumbu, punda, ngamia, safina, na akajumuisha vinginevyo katika kauli yake, \"Na anaumba msivyovijua.\""},{"id":2599,"sura":16,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} Yeye Mtukufu alipotaja njia ya kihisia, na kwamba Mwenyezi Mungu amewafanyia waja kile wanachosafiri kwacho miongoni mwa ngamia na wengineo, akataja njia isiyo ya kihisia inayofikisha kwake. Akasema, \"Na ni juu ya Mwenyezi Mungu kuelekeza Njia\" ambayo ndiyo njia ya karibu zaidi na ya fupi zaidi, ifikishayo kwa Mwenyezi Mungu kwa utukufu wake. Na ama njia ya upotofu katika itikadi zake na matendo yake, ambayo ni kila njia inayopingana na njia yake iliyonyooka, basi hiyo inazuia kufika kwa Mwenyezi Mungu, na inafikisha katika nyumba ya taabu. Kwa hivyo wale walioongoka wakashika njia ile iliyonyooka kwa idhini ya Mola wao Mlezi, nao wapotovu wakapotea wakaiacha, na wakafuata njia za upotofu, \"Na angelipenda, angeliwaongoa nyote.\"  Lakini aliwaongoa baadhi kwa ukarimu wake na fadhila, na hakuwaongoa wengineo kwa hekima yake uadilifu wake."},{"id":2600,"sura":16,"from_aya":10,"to_aya":11,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"10. Yeye ndiye anayewateremshia maji kutoka mbinguni. Katika hayo nyinyi mnapata ya kunywa, na miti ya kulishia. 11. Kwa hayo Yeye anawaoteshea mimea, na mizaituni, na mitende, na mizabibu, na kila aina ya matunda. Hakika katika hayo ipo ishara kwa kaumu wanaotafakari. "},{"id":2601,"sura":16,"from_aya":10,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10 - 11} Yaani wanaotafakari kwa hayo juu ya ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu na rehema zake, ambaye alishusha maji haya kutoka kwa mawingu membamba mno, ambapo alifanya ndani yake maji mengi sana, na kwa hayo wanakunywa, na pia mifugo wao huyanywa, na humwagilia mashamba yao kwa hayo, kisha yanawatolea matunda mengi na neema nyingi sana."},{"id":2602,"sura":16,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"12. Na amewatiishia usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota zimetiishwa kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kaumu watumiao akili."},{"id":2603,"sura":16,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Yaani, aliwatiishia vitu hivi kwa manufaa yenu na aina mbalimbali za masilahi yenu, kiasi kwamba hamuwezi kukosa kuzihitaji abadan. Kwa maana, usiku mnakaa humo, na kulala, na kupumzika. Na mchana mnaenea katika maisha yenu na manufaa ya dini yenu na dunia yenu. Na kutokana na jua na mwezi mnapata mwangaza na mng'ao, na kuifanya miti kuwa vizuri, na matunda, na mimea, na kukausha unyevu, na kuondoa baridi yenye madhara kwa dunia na miili na mahitaji mengine ya lazima na ya kawaida yanayotegemea kuwepo kwa jua na mwezi. Na pia ndani ya hivyo na katika nyota kuna mapambo kwa mbingu na mwongozo katika giza la nchi kavu na baharini na kujua nyakati na kuhesabu nyakati. Hivyo vyote kuna ushahidi na ishara mbalimbali, na ndiyo maana akavikusanya katika kauli yake, \"Hakika katika hayo zipo ishara kwa kaumu watumiao akili.\" Yaani, wale ambao wana akili ambazo wanazitumia katika kuzingatia na kutafakari kile kilichoandaliwa kwa ajili yake. Zinafahamu kile kinachokiona na kukisikia, na si kama kuona kwa wale walioghafilika ambazo fungu lao katika kuangalia ni kama fungu la wanyama ambao hawana akili."},{"id":2604,"sura":16,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"13. Na vile alivyowaenezea katika ardhi vya rangi mbalimbali. Hakika katika hayo ipo ishara kwa kaumu wanaokumbuka."},{"id":2605,"sura":16,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Yaani, kila alichokieneza Mwenyezi Mungu na kuvitawanya kwa ajili ya waja wake katika vyote vilivyo juu ya uso wa ardhi kama vile wanyama, miti, mimea, na vitu vingine vya aina mbalimbali, na vyenye faida tofautitofauti, ni ishara juu ya ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu na ujumla wa ukarimu wema wake na upana na wema wake, na kwamba ni yeye haipasi kufanywa ibada isipokuwa kwa ajili yake peke yake bila ya kuwa na mshirika yeyote. \"Kwa kaumu wanaokumbuka.\" Yaani, wanakumbuka yenye kuwafaidi kama vile elimu yenye manufaa na wanatafakari katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwaita kuyatafakari ili wakumbuke kwa hilo kile ambacho ni ushahidi wake."},{"id":2606,"sura":16,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"14. Yeye ndiye aliyeitiisha bahari, ili kutokana na humo mpate kula nyama laini, na mtoe humo mapambo mnayoyavaa. Na utaona marikebu zikikata maji humo, ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru."},{"id":2607,"sura":16,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} Yaani, [na] yeye peke yake ambaye hana mshirika yeyote \"ndiye aliyeitiisha bahari\" na akaiandaa kwa faida zenu anuai; \"ili kutokana na humo mpate kula nyama laini\" na samaki na nyangumi ambaye wanamvua kutoka humo, \"na mtoe humo mapambo mnayoyavaa\" ili yawazidishe urembo na uzuri juu ya uzuri wenu. \"Na utaona marikebu zikikata maji humo\" kwa mbele yake na zikakwenda kutoka upande mmoja hadi mwingine zikiwabeba wasafiri, riziki zao, mizigo yao, na biashara zao ambazo kwazo wanatafuta riziki, na fadhila za Mwenyezi Mungu juu yao; \"na mpate kushukuru\" yule ambaye aliwarahisishia mambo haya na kuyaandaa na mumsifu Mwenyezi Mungu aliyewaneemesha kwa hivyo. Basi himidi njema zote ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na shukrani na sifa njema, ambapo aliwapa waja wake katika masilahi na faida zao zaidi ya kile wanachokiomba na juu zaidi ya kile wanachotamani, na hatuwezi kumsifu ipasavyo, lakini Yeye ni kama alivyojisifu mwenyewe."},{"id":2608,"sura":16,"from_aya":15,"to_aya":16,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"15. Na akaweka katika ardhi milima madhubuti ili ardhi isiyumbe yumbe nanyi. Na mito, na njia mbalimbali ili mpate kuongoka. 16. Na alama nyingine. Na kwa nyota wao wanajiongoza. "},{"id":2609,"sura":16,"from_aya":15,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15 - 16} Yaani, \"Na akaweka\" Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waja wake \"katika ardhi milima madhubuti\" ili isiyumbe yumbe nao ana kuwasumbua viumbe, ndiyo waweze kulima ardhi, na kujenga, na kutembea juu yake. Na katika rehema yake Yeye Mtukufu aliweka humo mito anayoiendesha kutoka ardhi ya mbali hadi ardhi ambayo inaihitaji kwa lazima katika kunywa kwao na kunywesha mifugo wao na mashamba yao. Kuna mito ya juu ya uso wa ardhi na mingine ndani ya ardhi ambayo wanaitoa nje kwa kuchimba mpaka waifikie kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu amewatiishia miongoni mwa ndoo za kutekea, na ala mbalimbali na mfano wake. Na katika rehema zake ni kwamba alifanya katika njia mbalimbali za kufikisha katika miji ya mbali \"ili mpate kuongoka\"  katika njia hizo, kiasi kwamba unaweza kupata ardhi iliyoshikamana kwa milima inayofuatana lakini Mwenyezi Mungu ameweka kati yake mapitio kwa wapitao."},{"id":2610,"sura":16,"from_aya":17,"to_aya":23,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"17. Ati yule anayeumba ni kama asiyeumba? Basi hebu hamkumbuki? 18. Na mkizihesabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira mno, Mwingi wa kurehemu. 19. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyaficha na mnayoyaweka hadharani. 20. Na wale wanaowaomba wasiokuwa Mwenyezi Mungu hawaumbi kitu, bali wao wameumbwa. 21. Ni wafu, si wahai, na wala hawajui watafufuliwa lini. 22. Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Lakini wale wasioiamini Akhera nyoyo zao zinakataa, nao wanatakabari. 23. Hakuna shaka kuwa hakika Mwenyezi Mungu anayajua yale wanayoyaficha na wanayoyaweka hadharani. Hakika, Yeye hawapendi wanaotakabari. "},{"id":2611,"sura":16,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja viumbe vikubwa alivyoviumba na neema za jumla alizoneemesha, akataja kwamba hakuna chochote kinachofanana naye, wala anayelingana naye wala mwenza. Akasema: \"Ati yule anayeumba\" viumbe vyote, naye hufanya atakavyo, \"ni kama asiyeumba\" chochote, si kidogo wala kingi? \"Basi hebu hamkumbuki\" mkajua kwamba aliye pekee katika uumbaji ana haki zaidi ya kuabudiwa kwa ibada zote? Kwa kuwa kama alivyo Mmoja katika uumbaji wake na uendeshaji wake, basi yeye ni Mmoja katika uungu wake, upweke wake, na kuabudiwa kwake. Na kama vile hakuwa na mshirika yeyote alipowaumba na akaumba wasiokuwa nyinyi, basi msimfanyie wenza katika ibada yake, bali mpwekesheeni Dini."},{"id":2612,"sura":16,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} \"Na mkizihesabu neema za Mwenyezi Mungu\" bila ya kumshukuru \"hamwezi kuzidhibiti\" achilia mbali kushukuru ipasavyo. Kwani neema zake za dhahiri na zilizofichika kwa waja wake ni nyingi kwa idadi ya kuchukua pumzi na kila muda unaopita, za kila aina ya neema miongoni mwa zile ambazo waja wanazijua na katika zile wasizozijua, na namna anavyowakinga kutokana na adhabu, basi ni nyingi zaidi kuzidhibiti. \"Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira mno, Mwingi wa kurehemu,\" anakubali kutoka kwenu hata kama kushukuru kidogo anapowaneemesha neema nyingi."},{"id":2613,"sura":16,"from_aya":19,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19 - 20} Kwa kama vile rehema zake ni pana, na ukarimu wake ni wa jumla, na msamaha wake unawajumuisha waja wote, basi elimu yake imewazunguka. Anajua kile wanachokificha na kile wanachokiweka hadharani, tofauti na wale wanaoabudiwa badala yake. Wao kwa hakika \"hawaumbi kitu\" kidogo au kingi, \"bali wao wameumbwa.\" Basi wataumba kitu pamoja na kwamba wao wenyewe wanahitaji kuumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu?"},{"id":2614,"sura":16,"from_aya":21,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21 - 22} Pamoja na hili, wao hawana chochote katika sifa za ukamilifu, wala elimu wala kinginecho. \"Ni wafu, si wahai\" Hawasikii, wala hawaoni, wala hawaelewi  chochote. Basi je, hawa wanaweza kufanywa miungu badala ya Mola Mlezi wa walimwengu wote? Basi na ziangamie akili za washirikina! Ni upotofu mkubwa ulioje huu wao! Na mbovu mkubwa ulioje huu wao! Kwa maana, zilipotea kuhusiana na kitu kilicho dhahiri zaidi katika ubovu wake, na wakatoshanisha kati vilivyo vipungufu kwa namna zote visivyokuwa na sifa zozote za ukamilifu wala hawawezi kufanya chochote na yule ambaye ni mkamilifu kwa namna zote. Kwa maana ana elimu inayozunguka vitu vyote, na uwezo wa jumla, na rehema pana ambayo ilijaza walimwengu wote, na sifa njema, na utukufu, ukubwa, na ukuu ambao hakuna yeyote katika viumbe anayeweza kuzunguka baadhi ya sifa zake. Na ndiyo maana akasema, \"Mungu wenu ni Mungu Mmoja\" ambaye ni Mwenyezi Mungu, wa Pekee, Mmoja, Mkusudiwa, ambaye hakuzaa, wala hakuzaliwa, wala hana chcochote kinacholingana naye. Basi nyoyo za watu wa imani na akili zilimtukuza, na zikampa taadhima, na zikampenda kwa upendo mkubwa, na wakamfanyia kila kitu walichoweza miongoni mwa mambo ya kuwaweka karibu naye ya kimwili na kimali, na matendo ya mioyo, na matendo ya viungo, na wakamsifu kwa majina yake mazuri zaidi na sifa zake na matendo yake matakatifu. Na \"wale wasioiamini Akhera nyoyo zao zinakataa\" jambo hili kubwa, ambalo halikatai isipokuwa kiumbe ambaye ndiye mkubwa zaidi kwa ujinga na ukaidi. Na hili jambo ni upweke wa Mwenyezi Mungu. \"Nao wanatakabari\" kumfanyia ibada."},{"id":2615,"sura":16,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} \"Hakuna shaka kuwa hakika Mwenyezi Mungu anayajua yale wanayoyaficha na wanayoyaweka hadharani\" katika matendo mabaya. \"Hakika, Yeye hawapendi wanaotakabari;\" bali anawachukia kuchukia kukubwa zaidi, na atawapa thawabu kwa aina sawa na matendo yao. \"Kwa hakika, wale ambao wanatakabari kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.\""},{"id":2616,"sura":16,"from_aya":24,"to_aya":29,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"24. Na wanapoambiwa, \"Ni nini alichoteremsha Mola wenu Mlezi?\" Husema: Hadithi za kubuni za wa mwanzo! 25. Ili wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Qiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanaowapoteza bila ya kujua. Angalia, ni mabaya mno hayo wanayoyabeba! 26. Walipanga njama wale waliokuwa kabla yao, naye Mwenyezi Mungu akayasukua majengo yao kwenye misingi, kwa hivyo dari zake zikawaporomoka juu yao, na adhabu ikawajia kutokea wasipohisi. 27. Kisha Siku ya Qiyama atawahizi na atasema: Wako wapi hao washirika wangu ambao kwao mlikuwa mkipinga (Manabii)? Watasema wale waliopewa elimu: Hakika leo ndiyo hizaya na ubaya vitawashukia makafiri. 28. Wale ambao Malaika huwafisha huku wamejidhulumu nafsi zao! Basi wanasalimu amri, waseme: Hatukuwa tukifanya ubaya wowote. (Wataambiwa). Hasha! Hakika Mwenyezi Mungu anajua sana mliyokuwa mkiyatenda. 29. Basi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni mabaya mno makazi ya wafanyao kiburi! "},{"id":2617,"sura":16,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} Mwenyezi Mungu anasema kuwajulisha juu ya ukali wa kukadhibisha kwa washirikina ishara za Mwenyezi Mungu: \"Na wanapoambiwa, \"Ni nini alichoteremsha Mola wenu Mlezi?\" Yaani, wanapoulizwa juu ya Qur-ani na Wahyi, ambao ndio neema kubwa zaidi ambayo Mwenyezi Mungu amewaneemesha waja, mnasemaje juu yake? Na je, mnashukuru neema hii na kuikiri, au mnaikufuru na kuifanyia ukaidi? Linakuwa jibu lao ni jibu baya na bovu zaidi. Wanasema juu yake: Ni \"Hadithi za kubuni za wa mwanzo!\" Yaani, uwongo ambao Muhammad alimzulia Mwenyezi Mungu, na ni hadithi tu za watu wa mwanzo ambazo watu hupitishana vizazi baada ya vizazi, ambazo baadhi yake ni ukweli na baadhi yake ni uwongo."},{"id":2618,"sura":16,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} Walisema maneno haya na wakawaita wafuasi wao kwa hayo, kwa hivyo wakabeba mzigo wao na mzigo wa wale wanaowafuata hadi Siku ya Qiyama. Na kauli yake \"na sehemu ya mizigo ya wale wanaowapoteza bila ya kujua.\" Yaani, mizigo ya wale wanaowaiga wao ambao hawajui chochote isipokuwa kile walichowaitia. Kwa hivyo watabeba dhambi ya kile walichowaitia. Na ama wale wanaojua, basi kila mmoja yuko kando na uhalifu wake, kwa sababu walijua walichokijua. \"Angalia, ni mabaya mno hayo wanayoyabeba!\" Yaani, ni mzigo mbaya mno walioubeba unaotia uzito juu ya migongo yao ambayo ni mizigo yao wenyewe na mizigo ya wale waliowapoteza."},{"id":2619,"sura":16,"from_aya":26,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26-27} \"Walipanga njama wale waliokuwa kabla yao\" dhidi ya Mitume wao, na wakafanya hila mbalimbali ili wakatae yale waliyowajia nayo, na wakajenga majumba makubwa kutoka kwa hila zao hizo. \"Naye Mwenyezi Mungu akayasukua majengo yao kwenye misingi;\" yaani, kikawa walichojenga hicho ni adhabu ambayo waliadhibiwa kwayo, \"na adhabu ikawajia kutokea wasipohisi.\" Na hilo ni kuwa walidhani kwamba majengo hayo yatawanufaisha na kuwalinda kutokana na adhabu, lakini ikawa adhabu yao ni katika kile walichojenga na kukiwekea msingi imara. Na huu ni katika mifano mizuri zaidi katika kubatilisha kwa Mwenyezi Mungu njama za maadui zake. Kwa maana, walifikiria na kutathmini yale ambayo Mitume waliwajia nacho walipowakadhibisha, kisha wakawawekea misingi na kanuni batili ambazo wanazirudia na wanakataa kwazo yale waliyokuja nayo Mitume. Na pia wakafanya hila za kuwafikishia machukizo na madhara kwa Mitume na wale waliowafuata. Lakini njama zao hizo zikawa msiba juu yao, na kukawa kupanga kwao dhidi yao ni uharibifu juu yao wenyewe. Hayo ni kwa sababu njama zao hizo ni mbaya, na njama mbaya hazimsibu isipokuwa mwenyewe aliyezifanya. Hii ni katika dunia hii, nayo adhabu ya Akhera ni ya kuhizi zaidi, na ndiyo maana akasema, \"Kisha Siku ya Qiyama atawahizi\" mbele ya viumbe vyote na atawabainishia uongo wao na kumsingizia kwao Mwenyezi Mungu. \"Na atasema, Wako wapi hao washirika wangu ambao kwao mlikuwa mkiwapinga (Manabii)?\" Yaani, mliokuwa mkipigana na kumfanyia Mwenyezi Mungu uadui na kundi lake kwa ajili yao, huku mkidai kuwa wao ni washirika wa Mwenyezi Mungu. Na atakapowauliza swali hili, hawatakuwa na jibu isipokuwa kukiri upotovu wao na kukubali ukaidi wao, kwa hivyo watasema, \"Wametupotea! Na watajishuhudia wenyewe kwamba walikuwa makafiri.\" \"Watasema wale waliopewa elimu;\" yaani, wanachuoni wamchao Mola wao Mlezi \"Hakika hizaya leo;\" yaani, Siku ya Qiyama. \"Na ubaya;\" yaani, adhabu \"vitawashukia makafiri.\" Na katika hili kuna fadhila ya wenye elimu, na kwamba wao ndio wasemao ya haki katika dunia hii, na Siku watakaposimama mashahidi, na kwamba maneno yao yatazingatiwa na Mwenyezi Mungu na viumbe wake."},{"id":2620,"sura":16,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Kisha akataja kile atakachowafanyia wakati wa kifo na katika Siku ya Qiyama, akasema, \"Wale ambao Malaika huwafisha huku wamejidhulumu!\" Yaani, wanawafisha katika hali hii ambayo udhalimu wao na upotovu wao umekithiri, na tayari ilikwisha julikana aina za adhabu, aibu, fedheha na kudunishwa ambavyo watapata katika mahali hapo. \"Basi wanasalimu amri\" na kukataa vile walivyokuwa wakiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, na watasema, \"Hatukuwa tukifanya ubaya wowote\" Lakini wataambiwa, \"Hasha!\" Mlikuwa mkifanya ubaya. \"Hakika Mwenyezi Mungu anajua sana mliyokuwa mkiyatenda.\" Basi kukataa kwenu huku hakutawanufaisha kwa chochote. Hili ni katika baadhi ya hali katika Siku ya Qiyama. Watayakataa yale waliyokuwa wakifanya katika dunia, wakidhani kwamba hilo litawafaidi. Lakini vitakaposhushudia dhidi yao viungo vyao na yakawa wazi yale waliyokuwa wakifanya, watakiri na kukubali, na ndiyo maana, hawataingia Motoni mpaka watakapokiri dhambi zao."},{"id":2621,"sura":16,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Basi watakapoingia katika milango ya Jahannam, kila mtendaji ataingilia katika mlango unaoifailia hali yake, kwa hivyo ni mabaya mno \"makazi ya wafanyao kiburi,\" ambayo ni Moto wa Jahannam. Kwa maana, hayo ni makazi ya huzuni na majuto, na nyumba ya mashaka na maumivu, na mahali pa wasiwasi kubwa sana na dhiki, na mahali pa kukasirikiwa na aliye hai Milele Msimamia yote Milele. Hawatapumzishwa adhabu yake, wala hawataondolewa hata siku moja ya adhabu yake chungu. Mola Mlezi, Mwingi wa kurehemu atawapa mgongo na atawaonjesha adhabu kubwa."},{"id":2622,"sura":16,"from_aya":30,"to_aya":32,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"30. Na wataambiwa wale waliomcha Mungu: Mola wenu Mlezi aliteremsha nini? Watasema: Heri. Kwa wale waliofanya mazuri katika dunia hii watapata mazuri. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi, na ni njema mno nyumba hiyo ya wachamungu. 31. Bustani za milele wataziingia; iwe inapita kwa chini yake mito. Humo watapata watakacho. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu awalipavyo wenye kumcha. 32. Wale ambao Malaika huwafisha katika hali nzuri, wanawaambia: Salama iwe juu yenu! Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda. "},{"id":2623,"sura":16,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Mwenyezi Mungu alipotaja kauli ya wale waliokadhibisha yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, akataja yale waliyosema wachamungu, na walikubali na kukiri kwamba kile alichoteremsha Mwenyezi Mungu ni neema na heri kubwa ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwayo waja wake. Kwa hivyo wakakubali neema hiyo, na wakaipokea kwa kuikubali na kuifuata. Na wakamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, kwa hivyo wakaijua na kuifanyia kazi. \"Kwa wale waliofanya mazuri\" katika kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakawafanyia uzuri waja wa Mwenyezi Mungu, basi hao wana \"mazuri katika dunia hii\" kama vile riziki pana, maisha mazuri, utulivu wa moyo, amani na furaha. \"Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi\" kuliko nyumba hii na vyote vilivyomo miongoni mwa aina mbalimbali za starehe na matamanio. Kwani dunia hii, furaha yake ni kidogo ambayo imejaa masaibu na ni yenye kukatika, kinyume na starehe za Akhera. Na ndiyo maana akasema, \"na ni njema mno nyumba hiyo ya wachamungu.\""},{"id":2624,"sura":16,"from_aya":31,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31-32} \"Bustani za milele wataziingia; iwe inapita kwa chini yake mito. Humo watapata watakacho.\" Yaani, haijalishi ni kiasi gani zitatamani nafsi zao na utashi wao ukafungamana nacho, watakipata hicho kwa njia kamili zaidi. Na haiwezekani kwamba waombe aina katika aina za starehe ambayo ina raha kwa mioyo na furaha ya  roho, isipokuwa kitawafikia hapo. Na ndiyo sababu Mwenyezi Mungu atawapa wakazi wa Peponi kila kitu wanachotamani kiasi kwamba atawakumbusha mambo mengine ya starehe ambayo hayakuwa hipitia mioyoni mwao. Basi ni mwingi wa baraka ambaye ukarimu wake hauna kikomo wala utoaji wake kwa wingi hauna mipaka, ambaye hakuna kitu kama mfano wake katika sifa za dhati yake na sifa za matendo yake na athari za sifa hizo na ukuu wa mfalme wake na mamlaka yake. {Hivyo, Mwenyezi Mungu huwalipa waadilifu}: Kwa sababu ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake; kwa kutekeleza kile alichowawekea cha wajibu na wajibu unaohusiana na moyo, mwili, na ulimi kutokana na haki yake na haki ya waja wake, na kwa kuacha kile alichowakataza Mwenyezi Mungu. \"Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu awalipavyo wenye kumcha,\" kwa sababu ya hasira ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake, kwa kutekeleza kile alichowawajibishia miongoni mwa mambo ya faradhi na ya wajibu zinazohusiana na moyo, mwili, na ulimi katika haki zake na haki za waja wake, na kwa kuacha yale aliyowakataza Mwenyezi Mungu. \"Wale ambao Malaika huwafisha\" huku wanaendelea na uchamungu wao huku wakiwa \"katika hali nzuri\" yaani, wakiwa safi waliosafishwa kutokana na kila upungufu na uchafu unaowaendea na kuharibu katika imani yao. Kwa hivyo mioyo yao ikawa mizuri kwa kumjua Mwenyezi Mungu na kumpenda. Na ndimi zao zikawa nzuri kwa kumtaja na kumsifu. Na viungo vyao vikawa vizuri kwa kumtii na kumfuata. \"Wanawaambia: Salama iwe juu yenu\" kutokana na kila janga, na tayari mmeokoka kutokana na kila mnayoyachukia. \"Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda\" kama vile kumwamini Mwenyezi Mungu na kufuata amri yake. Kwa maana matendo ndiyo sababu, kiini, na msingi wa kuingia Peponi na kuokoka kutokana na Moto. Na waliweza kufikia matendo hayo kwa rehema na neema ya Mwenyezi Mungu, siyo kwa uwezo wao na nguvu zao."},{"id":2625,"sura":16,"from_aya":33,"to_aya":34,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"33. Wanangojea jingine hawa isipokuwa Malaika wawafikie, au iwafikie amri ya Mola wako Mlezi? Kama hivyo, walitenda wale waliokuwa kabla yao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walijidhulumu wenyewe. 34. Basi yakawafikia mabaya ya yale waliyoyatenda, na yale waliyokuwa wakiyafanyia stihizai yakawazunguka. "},{"id":2626,"sura":16,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Je, wanangojea hawa ambao wamefikiwa na ishara lakini hawakuamini, na wakakumbushwa, lakini hawakukumbuka, \"isipokuwa Malaika wawafikie\" ili kuchukua roho zao, \"au iwafikie amri ya Mola wako Mlezi\" ya adhabu itakayowapata? Kwa maana, hakika wameshastahili kufikiwa nayo. \"Kama hivyo, walitenda wale waliokuwa kabla yao\" walikadhibisha na wakakufuru, kisha hawakuamini mpaka adhabu ilipowateremkia. \"Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu\" alipowaadhibu, \"lakini walijidhulumu wenyewe.\" Kwa maana hizo ziliumbwa ili kumwabudu Mwenyezi Mungu, ili yawe maishio yao ni katika utukufu wa Mwenyezi Mungu, lakini wakazidhulumu na wakaacha kile ziliumbwa kwa ajili yake, na wakaziweka katika uduni wa kudumu na taabu isiyoisha."},{"id":2627,"sura":16,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} \"Basi yakawafikia mabaya ya yale waliyoyatenda\" yaani, adhabu na athari za matendo yao, \"na yale waliyokuwa wakiyafanyia stihizai yakawazunguka\" kwa maana, walikuwa wanapoambiwa na Mitume wao kwamba wataadhibiwa, wanawafanyia stihizai na masihara. Kwa hivyo, jambo hilo walilolifanyia stihizai likawapata."},{"id":2628,"sura":16,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"35. Na washirikina walisema: Mwenyezi Mungu angelitaka, tusingeliabudu chochote badala yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeliharimisha chochote bila ya Yeye. Kama hivyo, walifanya wale waliokuwa kabla yao. Basi lipo lolote juu ya Mitume isipokuwa kufikisha tu kwa wazi?"},{"id":2629,"sura":16,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} Yaani, washirikina walitumia mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo ushahidi juu ya uhalali wa ushirikina wao, na kwamba Mwenyezi Mungu angelitaka, basi hawangemshirikisha na chochote wala hawangeliharimisha chochote katika wanyama hoa ambao amewahalalisha, kama vile Bahira, Wasila, Hami na mfano wa hao bila Yeye kusema hivyo. Na hii ni hoja batili. Kwa maana, ingekuwa ya kweli, basi Mwenyezi Mungu hangewaadhibu wale waliokuwa kabla yao pale walipomshirikisha, lakini aliwaadhibu adhabu kali sana. Na ikiwa alikuwa anayapenda hayo kwao, basi hangewaadhibu. Na makusudio yao katika hilo si isipokuwa kuikataa haki ambayo Mitume walikuja nayo. Vinginevyo, wanajua vyema kwamba hawana hoja yoyote dhidi ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana, Mwenyezi Mungu aliwaamuru na kuwakataza, na akawawezesha kufanya kile alichowajukumisha, na akawapa nguvu na utashi ambao matendo yao yanatokana nao. Kwa hivyo kutumia kwao hukumu na majaliwa ya Mwenyezi Mungu kama ushahidi ni batili ya batili zote. Na kila mtu anajua vyema kihisia kwamba mwanadamu ana uwezo wa kufanya kila kitu anachotaka na hakuna yeyote anayepinga hilo. Na hawa walichanganya kati ya kumkadhibisha Mwenyezi Mungu, na kuwakadhibisha Mitume wake, na kukadhibisha mambo ya kiakili na kihisia. \"Basi lipo lolote juu ya Mitume isipokuwa kufikisha tu kwa wazi\" ambako kunafikia nyoyo na asibakie yeyote na hoja yoyote dhidi ya Mwenyezi Mungu. Na wakati Mitume wanawafikishia amri ya Mola wao Mlezi na katazo lake - nao wakayapinga haya kwa kutumia hukumu ya Mwenyezi Mungu na majaliwa kama ushahidi - basi Mitume hawana lolote katika jambo hilo, bali hesabu yao iko tu kwa Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu, Mtukufu."},{"id":2630,"sura":16,"from_aya":36,"to_aya":37,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"36. Na hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo aliowaongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao uliwathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wale wanaokadhibisha. 37. Hata ukiwa na pupa juu ya kuongoka kwao, basi hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anayeshikilia kupotea. Wala hawatapata yeyote wa kuwanusuru. "},{"id":2631,"sura":16,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba hoja yake ilisimama juu ya umma zote, na kwamba hakuna umma wowote uliotangulia au uliochelewa isipokuwa Mwenyezi Mungu aliutumia mtume, nao wote wanakubaliana juu ya wito mmoja na dini moja, ambayo ni kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya mshirika yeyote. \"Kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.\" Kwa hivyo umma zikagawanyika kulingana na mwitikio wao kwa wito wa Mitume na kutoitikia kwao katika sehemu mbili: \"Basi kati yao wapo aliowaongoa Mwenyezi Mungu\" kwa hivyo wakawafuata Mitume kwa elimu na matendo. \"Na kati yao wapo ambao uliwathibitikia upotovu;\" kwa hivyo wakaifuata njia ya upotovu. \"Basi tembeeni katika ardhi\" kwa miili yenu na mioyo yenu, \"muangalie ulikuwaje mwisho wa wale wanaokadhibisha.\" Mtaona maajabu katika hayo, na hutampata mkadhibishaji yeyote isipokuwa ilikuwa adhabu yake ni kuangamia."},{"id":2632,"sura":16,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37} \"Hata ukiwa na pupa juu ya kuongoka kwao\" na ukafanya bidii yako kuwa kwa ajili ya hilo \"basi hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anayeshikilia kupotea.\" Na hata kama atafanya kila sababu, basi hawezi kumuongoa isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. \"Wala hawatapata yeyote wa kuwanusuru\" na kuwalinda kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu."},{"id":2633,"sura":16,"from_aya":38,"to_aya":40,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"38. Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa viapo vyao kwamba Mwenyezi Mungu hatamfufua aliyekufa. Kwani! Ni ahadi iliyo juu yake kikweli; lakini wengi  wa watu hawajui. 39. Ili awabainishie  yale waliyohitalifiana ndani yake, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo. 40. Hakika, kauli yetu kwa kitu tunapokitaka kiwe, ni kukiambia tu: Kuwa! Basi kinakuwa. "},{"id":2634,"sura":16,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} Anajulisha Yeye Mtukufu juu ya washirikina wanaomkadhibisha Mtume wake kwamba \"waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa viapo vyao\" juu ya kumkadhibisha Mwenyezi Mungu, na wakaapa kwamba Mwenyezi Mungu hatawafufua wafu, wala hawezi kuwahuisha baada ya kuwa mavumbi. Yeye Mtukufu alisema akiwakadhibisha, \"Kwani!\" Atawafufua na kuwakusanya katika Siku ambayo haina shaka yoyote juu yake. \"Ni ahadi iliyo juu yake kikweli.\" Hataivunja wala kuibadilisha, \"lakini wengi  wa watu hawajui.\" Na katika ujinga wao mkubwa ni kukataa kwao ufufuo na malipo."},{"id":2635,"sura":16,"from_aya":39,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39 - 40} Kisha akataja hekima katika malipo na ufufuo, akasema, \"Ili awabainishie  yale waliyohitalifiana ndani yake\" miongoni mwa masuala makubwa na madogo, kwa kubainisha uhakika wake na kuyaweka wazi. \"Na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo,\" [wakati] watayaona matendo yao watakuwa na majuto, na miungu wao ambao wanawaomba pamoja na Mwenyezi Mungu hawatawasaidia chochote wakati amri ya Mola wako Mlezi ilipokuja, na watakapoona kile wanachoabudu huku kikiwa kuni za Jahannam. Nalo jua na mwezi vitakunjwa, nazo nyota zitatawanyika, kisha itawawia wazi wale wanaoviabudu kwamba hivyo ni waja wa Mwenyezi Mungu waliotiishwa naye, na kwamba vinamhitaji Mwenyezi Mungu katika hali zote, na hayo siyo magumu wala mazito kwa Mwenyezi Mungu. Kwa maana, Yeye anapotaka kitu, anakiambia tu: kuwa, na linakuwa bila ya upinzani wala kukataa, bali linakuwa namna alivyotaka na kupenda."},{"id":2636,"sura":16,"from_aya":41,"to_aya":42,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"41. Na wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa, bila ya shaka tutawaweka katika maskani mazuri katika dunia; na katika ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; lau wangekuwa wanajua! 42. Wale waliosubiri na wakamtegemea Mola wao Mlezi. "},{"id":2637,"sura":16,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu fadhila za waumini wanaojaribiwa, \"wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.\" Yaani, katika njia yake na kutafuta radhi zake, \"baada ya kudhulumiwa\" kwa kuudhiwa, kujaribiwa na kaumu yao ili wawarudishe katika ukafiri na ushirikina. Kwa hivyo wakaacha miji yao na marafiki zao, na wakayahama hayo kwa ajili ya kumtii Mwingi wa rehema. Kwa hivyo akataja kwamba wana thawabu mbili: thawabu ya haraka katika dunia kama vile riziki pana, na maisha mazuri ambayo waliyaona kwa macho baada ya kuhama na kuwashinda maadui zao na wakaiteka miji na wakapata ngawira nyingi kutoka kwao. Kwa hivyo wakazifanya kuwa mali zao, na Mwenyezi Mungu akawapa mazuri katika dunia, \"na ujira wa Akhera\" aliyowaahidi juu ya ulimi wa Mtume wake ni bora na \"makubwa zaidi\" kuliko malipo ya dunia. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, \"Wale walioamini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waliofuzu. Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu. Watadumu humo milele. Hakika Mwenyezi Mungu kwake anayo malipo makubwa.\" Na kauli yake, \"lau wangekuwa wanajua\" malipo na thawabu zilizopo kwa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kumuamini na akahama katika njia yake, basi hakuna yeyote aliyeangalia kando na hayo!"},{"id":2638,"sura":16,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} Kisha akataja sifa za marafiki wake, akasema, \"Wale waliosubiri\" juu ya amri za Mwenyezi Mungu, na juu ya makatazo yake, na juu ya majaliwa ya machungu ya Mwenyezi Mungu, na juu ya kuudhiwa na kuteswa kwa sababu yake; \"na wakamtegemea Mola wao Mlezi\" katika kutekeleza ayapendayo wake, wala hawajitegemei wenyewe. Na kwa hayo mambo yao yanafaulu na hali zao zinanyooka. Kwa maana subira na kumtegemea Mwenyezi Mungu ndiyo yanamiliki vitu vyote. Na hakuna yeyote aliyekosa chochote cha heri isipokuwa ni kwa sababu ya kutosubiri kwake na kutofanya bidii kwake katika kile ninachotakiwa kutoka kwake au kwa sababu ya kutomtegemea kwake Mwenyezi Mungu."},{"id":2639,"sura":16,"from_aya":43,"to_aya":44,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"43. Nasi hatukuwatuma kabla yako isipokuwa watu wanaume tuliowapa Wahyi (Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui. 44. Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao, ili wapate kutafakari. "},{"id":2640,"sura":16,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -  \"Nasi hatukuwatuma kabla yako isipokuwa watu wanaume\" yaani wewe si kitu kipya miongoni mwa Mitume. Kwa maana hatukuwatuma Malaika kabla yako, bali tuliwatuma wanaume wakamilifu, siyo wanawake \"tuliowafunulia Wahyi\" wenye sheria na hukumu mbalimbali ambazo ni katika fadhila zake na wema wake juu ya waja wake, na Mitume hao hawakuleta chochote wao wenyewe. \"Basi waulizeni wenye ukumbusho;\" yaani, watu wa vitabu vilivyotangulia \"kama nyinyi hamjui\" habari za wa mwanzo, na mkatia shaka kwamba je, Mwenyezi Mungu aliwatuma wanaume? Basi waulizeni wenye elimu juu ya hayo. Wale walioteremshiwa Zaburi na hoja zilizo wazi, nao wakazijua na kuzifahamu. Wao wote walikwisha jua kwa uhakika kwamba Mwenyezi Mungu hakutuma isipokuwa wanaume aliowafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Kwa ujumla, aya hii inawasifia watu wenye elimu, na kwamba aina ya elimu ya juu kabisa ni kukijua Kitabu cha Mwenyezi Mungu alichokiteremsha. Kwa maana Mwenyezi Mungu alimuamrisha asiyejua kuwarudia wenye elimu katika matukio yote. Na ndani ya hili kuna kuwasifia wenye elimu kwamba ni waadilifu na kuwatakasa. Kwa maana, Mwenyezi Mungu aliamrisha kuwauliza, na kwamba kwa kufanya hivyo, mjinga anatoka katika lawama. Basi hilo likaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu aliwapa amana ya ufunuo wake na uteremsho wake, na kwamba wameamrishwa kujitakasa nafsi zao na kusifika na sifa za ukamilifu."},{"id":2641,"sura":16,"from_aya":44,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{44} Na walio bora zaidi katika wenye ukumbusho ni watu wa Qur-ani hii tukufu. Kwa maana, wao ndio watu wa ukumbusho kiuhakika, noa ndio wanaolifailia zaidi jina hili kuliko watu wengineo. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, \"Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho;\" yaani, Qur-ani hii ambayo ndani yake kuna ukumbusho wa wale wanayoyahitaji ya mambo ya dini yao na dunia yao, ya dhahiri na ya ndani. \"Ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao\" Na hili linajumuisha kubainisha matamshi yake na maana zake. \"ili wapate kutafakari\" kitabu hiki, na kutoa katika hazina zake na elimu zake kulingana na utayari wao na kukielekea kwake."},{"id":2642,"sura":16,"from_aya":45,"to_aya":47,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"45. Je wana amani wale wanaopanga njama mbaya kwamba Mwenyezi Mungu hatawadidimiza katika ardhi, na haitawafikia adhabu kutoka wasipohisi? 46. Au hatawashika katika harakati zao, na wala hawatamshinda? 47. Au hatawashika huku wana hofu? Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye huruma kubwa, Mwingi wa kurehemu. "},{"id":2643,"sura":16,"from_aya":45,"to_aya":47,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{45 - 47} Huku ni kuhofisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wenye kukufuru na kukadhibisha na aina mbalimbali za maasia kwamba, anaweza kuwachukua kwa adhabu katika hali ya kughafilika kwao hali ya kuwa hawahisi. Ima awachukue kwa adhabu ya kutokea juu yao, au kutokea chini yao kwa kuwadidimiza au mfano wake. Na ima iwajie huku wako katika harakati zao na shughuli zao hali ya kuwa hawafikirii adhabu kabisa. Na ima huku wana hofu juu ya adhabu. Basi hawawezi kumshinda Mwenyezi Mungu katika hali miongoni mwa hali hizi zote. Lakini wao wako chini ya mshiko wake, nywele za mbele ya vichwa vyao ziko mkononi mwake. Lakini hawaadhibu kwa sababu yeye ni Mwenye huruma kubwa, Mwingi wa kurehemu. Hawaharakishii adhabu waasi, bali huwapa muhula, na salama, na kuwaruzuku,  ilhali wao wanamuudhi yeye na wanawaudhi marafiki wake. Lakini pamoja na hayo, Yeye hufungulia milango ya toba, na anawaita waachane na mambo mabaya ambayo yanawadhuru, na anawaahidi kwa hilo heshima kubwa sana, na msamaha kwa dhambi walizofanya. Basi na astahi muhalifu Mola wake Mlezi kwamba awe anateremkiwa na neema zake kila wakati ilhali maasi yake nayo yanapanda kwa Mola wake Mlezi kila wakati. Na ajue kwamba Mwenyezi Mungu hupeana muhula na wala hapuuzi. Na kwamba anapomchukua, anamshika mshiko wa Mwenye nguvu, Mwenye uwezo. Basi na atubie kwake, na arejee kwake katika mambo yote. Kwa maana Yeye ni Mwenye huruma kubwa, Mwenye kurehemu. Basi na mtu aharakishe, tena aharakishe kuziendea rehema zake pana, na wema wake wa jumla, na kushika njia zifikishazo katika fadhila za Mola wake Mlezi, Mwingi wa kurehemu. Tazama! Nazo ni kumcha Yeye, na kutenda yale anayoyapenda na kuyaridhia."},{"id":2644,"sura":16,"from_aya":48,"to_aya":50,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"48. Je, hawavioni vitu alivyoviumba Mwenyezi Mungu, vivuli vyao vinaelekea kushotoni na kuliani, kumsujudia Mwenyezi Mungu na vikinyenyekea? 49. Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo katika mbingu na katika ardhi, miongoni mwa wanyama mpaka Malaika na wala havitakabari. 50. Vinamhofu Mola wao Mlezi aliye juu yao, na vinafanya vinavyoamrishwa. "},{"id":2645,"sura":16,"from_aya":48,"to_aya":48,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{48} Yeye Mtukufu anasema, \"Je, hawavioni;\" yaani, wale wanaoshuku upweke wa Mola wao Mlezi, ukuu wake, na ukamilifu wake, wakavitazama \"vitu alivyoviumba Mwenyezi Mungu;\" yaani, viumbe vyake vyote, na jinsi vivuli vyao \"vinaelekea kushotoni na kuliani, kumsujudia Mwenyezi Mungu\" huku vimedhalilika kwa sababu ya ukuu wake na utukufu wake, \"huku vikinyenyekea?\" Yaani, huku vimetiishwa, viko chini ya uendeshaji wake na ushindi wake. Hakuna hata mmoja wao isipokuwa nywele za mbele ya kichwa chake ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, naye ndiye anayekiendesha."},{"id":2646,"sura":16,"from_aya":49,"to_aya":49,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{49} \"Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo katika mbingu na katika ardhi, miongoni mwa wanyama\" kama vile wanayama wazungumzao na wasiozungumza, \"na malaika\" watukufu. Na aliwataja malaika kwa namna mahususi baada ya kuwataja kiujumla kwa sababu ya ubora wao na utukufu wao na wingi wa ibada zao, na ndiyo maana akasema, \"na wala havitakabari.\" Kumfanyia ibada, pamoja na wingi wao, na ukuu wa maadili yao na nguvu zao, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, \"Masihi hatajiinua juu zaidi akaacha kuwa mja wa Mwenyezi Mungu, wala Malaika waliowekwa karibu.\""},{"id":2647,"sura":16,"from_aya":50,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{50} \"Vinamhofu Mola wao Mlezi aliye juu yao.\" Alipowasifu kwa wingi wa utii wao na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, akawasifu kwamba wanamcha Mwenyezi Mungu aliye juu yao kwa dhati yake, na ushindi, na sifa kamilifu. Kwa hivyo wao wamedhalilika chini ya ushindi wake \"na vinafanya vinavyoamrishwa.\" Yaani, chochote ambacho Mwenyezi Mungu anaviamuru, basi vinakitekeleza kwa kupenda na kwa hiari. Na kusujudu kwa viumbe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni aina mbili: kusujudu kwa ulazima kunakoonyesha sifa zake za ukamilifu. Na hii linawahusu viumbe wote sawa awe muumini, kafiri, mwema, muovu, mnyama azungumzaye na wengineo. Na kusujudu kwa kwingine ni kusujudu kwa hiari ambako ni maalumu kwa vipenzi vyake na waja wake waumini miongoni mwa malaika na viumbe wengineo."},{"id":2648,"sura":16,"from_aya":51,"to_aya":55,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"51. Na Mwenyezi Mungu amesema: Msijifanyie miungu wawili! Hakika Yeye ndiye Mungu Mmoja tu. Basi niogopeni Mimi tu! 52. Na ni vyake Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Na Dini ni yake Yeye daima. Je, mnamcha mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu? 53. Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakiwagusa madhara, mnamyayatikia Yeye. 54. Na anapowaondoshea madhara hayo, mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi. 55. Wakizikataa neema tulizowapa. Basi stareheni. Mtakuja jua! "},{"id":2649,"sura":16,"from_aya":51,"to_aya":51,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{51} Yeye Mtukufu anaamuru kwamba aabudiwe Yeye peke yake bila mshirika yeyote. Na hili linatumiwa kama ushahidi juu ya upekee wake katika kuneemesha [na Umoja]. Kwa hivyo, akasema, \"Msijifanyie miungu wawili!\" Yaani, msimfanyie mshirika yeyote katika uungu wake. Kwa maana yeye \"Hakika ndiye Mungu Mmoja tu;\" katika sifa zake zake kuu, ni wa kipekee katika vitendo vyote. Na kama vile Yeye ni Mmoja tu katika dhati yake, majina yake, sifa zake, na vitendo vyake, basi na mumfanyie yeye tu ibada. Na ndiyo maana akasema, \"Basi niogopeni Mimi tu!\" Yaani, nihofuni na mtekeleze amri yangu, na muepuke makatazo yao bila ya kunishirikisha na kiumbe chochote; kwani vyote hivyo vinamilikiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu."},{"id":2650,"sura":16,"from_aya":52,"to_aya":52,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"\u201cNi vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, na Dini ni yake daima. Yaani, dini, ibada, na unyenyekevu nyakati zote ni vya Mungu peke yake, na uumbaji lazima uwe mkweli kwa Mungu na kuzama katika utumwa Wake. \"Je, nyinyi mnamuogopa asiyekuwa Mwenyezi Mungu;\" kutoka kwa watu wa ardhini au watu wa mbinguni? Hawana uwezo wa kukudhuru wala kukunufaisha, na Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeruzuku na kufadhili."},{"id":2651,"sura":16,"from_aya":53,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{53} \"Na neema yoyote mliyo nayo\" ya dhahiri na ya ndani \"inatoka kwa Mwenyezi Mungu\" na hakuna yeyote anayemshiriki katika hizo. \"Kisha yakiwagusa madhara\" kama vile umaskini, magonjwa na shida \"mnamyayatikia Yeye\" kwa dua na kumnyenyekea kwa sababu mnajua ya kwamba hakuna anayeweza kuzuia madhara na shida isipokuwa yeye tu. Kwa hivyo yule ambaye ni wa pekee katika kuwapa vile mnavyopenda, na kuondoa vile mnavyochukia, basi ndiye pekee ambaye anapaswa kuabudiwa."},{"id":2652,"sura":16,"from_aya":54,"to_aya":55,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{54 - 55} Lakini wengi wa watu wanajidhulumu wenyewe na wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu juu yao anapowaokoa kutoka katika shida - kwa hivyo wakawa katika nyakati nzuri, wanamshirikisha na baadhi ya viumbe wake walio maskini. Na ndiyo maana akasema, \"Wakiyakufuru yale tuliyowapa;\" kwa kuwaokoa kutoka katika shida na mashaka. \"Basi stareheni\" kidogo katika dunia yenu, \"Mtakuja jua\" mwisho wa kufuru yenu."},{"id":2653,"sura":16,"from_aya":56,"to_aya":60,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"56. Na hao ambao hata hawawajui wanawawekea sehemu katika vile tunavyowaruzuku. Tallahi! Bila ya shaka mtaulizwa kwa hayo mliyokuwa mnayazua! 57. Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu ati ana mabinti, Subhanahu (ametakasika)! Na wao wenyewe, ati ndiyo wawe na hayo wanayoyatamani! 58. Na mmoja wao akibashiriwa kwa msichana, uso wake unasalia umesawijika na akawa na huzuni mno. 59. Anajificha asionekane na watu kwa ubaya wa yule aliyebashiriwa! Je, akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama, ni ubaya mno wanavyohukumu! 60. Wale wasioiamini Akhera wana mfano mbaya mno, naye Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye mfano bora zaidi. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. "},{"id":2654,"sura":16,"from_aya":56,"to_aya":56,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{56} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu ujinga wa washirikina na udhalimu wao na kumsingizia kwao uongo Mwenyezi Mungu , na kwamba wanaziwekea sanamu zao - ambazo hazijui wala hazinufaishi wala hazidhuru, - fungu katika kile ambacho Mwenyezi Mungu amewaruzuku na akawaneemesha kwayo. Kwa hivyo wakajisaidia na riziki yake katika kumshirikisha na wengine, na wakajikurubisha kwayo mbele ya masanamu yaliyochongwa, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, \"Na walimwekea Mwenyezi Mungu fungu katika mimea na wanyama alioumba, wakasema: Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya washirikishwa wetu. Basi vile vilivyokuwa vya washirikishwa wao, havimfikii Mwenyezi Mungu...\" hadi mwisho wa Aya. \"Tallahi! Bila ya shaka mtaulizwa kwa hayo mliyokuwa mnayazua!\" Na mtaambiwa, \"Je, Mwenyezi Mungu aliwaruhusu, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?\" Na nini dhana ya wale wanaomzulia uongo Mwenyezi Mungu Siku ya Qiyama? Basi atawaadhibu adhabu kali zaidi kwa hilo."},{"id":2655,"sura":16,"from_aya":57,"to_aya":59,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{57 - 59} \"Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu ati ana mabinti\" ambapo walisema hivi kuhusu malaika ambao ni waja walio karibu na Mwenyezi Mungu: Wao ni mabinti wa Mwenyezi Mungu, \"Na wao wenyewe, ati ndiyo wawe na hayo wanayoyatamani!\" Yaani, wao wenyewe wanajitakia wana wa kiume, kiasi kwamba wanawachukia sana mabinti. Kwa hivyo mmoja wao alikuwa \"akibashiriwa kwa msichana, uso wake unasalia umesawijika\" kwa sababu ya dhiki iliyoyapata. \"Na akajizuia mno huzuni;\" yaani, anajizuia mno huzuni na majuto anapobashiriwa kuzaliwa mwana wa kike, kiasi kwamba anafedheheshwa mbele ya wenzake na anajificha asionekane na watu kwa ubaya wa yule aliyebashiriwa! Kisha anafikiria kwa mawazo yake mabovu kuhusu atakalomfanyia binti ambaye amebashiriwa.\"Je, akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongoni\" hali akiwa hai? Nako ni kule kuwauwa mabinti wachanga ambako Mwenyezi Mungu aliwakashifu washirikina juu yake. \"Tazama, ni ubaya mno wanavyohukumu!\" Ambapo walimuelezea Mwenyezi Mungu kwa njia ambayo haiufailii utukufu wake kwa kumnasibishia mwana. Tena hilo halikuwatosha hadi walipomnasibisha na sehemu mbaya zaidi kati ya sehemu hizo mbili, ambayo ni wanawake ambao wao wenyewe hawawapendi mno na wanawachukia. Basi vipi wanawanasibisha kwa Mwenyezi Mungu? Basi hukumu mbaya zaidi ni hukumu yao hiyo."},{"id":2656,"sura":16,"from_aya":60,"to_aya":60,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{60} Na pindi huu ulipokuwa miongoni mwa mifano mibaya ambayo maadui zake washirikina walimnasibishia Mwenyezi Mungu,  Yeye Mtukufu akasema, \"Wale wasioiamini Akhera wana mfano mbaya mno.\" Yaani, mfano usio wenye mapungufu na kasoro kamili. \"Naye Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye mfano bora zaidi\" Nayo ni kila sifa ya ukamilifu. Kwa hivyo, kila ukamilifu uliopo, basi Mwenyezi Mungu anaustahiki zaidi bila hilo kuhitaji upungufu kwa namna yoyote ile. Naye anao mfano bora zaidi katika nyoyo za vipenzi wake, ambao ni kumpa taadhima, utukufu, upendo, kumrudia, na kumjua. \"Naye ni Mwenye nguvu\" ambaye alishinda vitu vyote, na viumbe vyote vilijisalimisha kwake. \"Mwenye hekima\" ambaye anaweka vitu mahali pake, kwa hivyo haamrishi wala kufanya chochote isipokuwa kile anachosifiwa juu yake kwa sababu ya ukamilifu katika hilo."},{"id":2657,"sura":16,"from_aya":61,"to_aya":61,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"61. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwaadhibu watu kwa mujibu wa dhuluma zao, basi asingelimwacha juu yake hata mnyama mmoja. Lakini anawaahirisha mpaka muda uliowekwa. Na unapofika muda wao, hawatakawia hata saa moja wala hawatatangulia."},{"id":2658,"sura":16,"from_aya":61,"to_aya":61,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{61} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kile walichomzulia wadhalimu, akataja ukamilifu wa ustahamilivu wake na subira yake. Akasema, \"Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwaadhibu watu kwa mujibu wa dhuluma zao\" bila ya kuongezeka wala kupunguza, \"basi asingelimwacha juu yake.\" Yaani juu ya mgongo wa ardhi \"hata mnyama mmoja\" yaani, wangeangamia wafanyao maasia, na wengineo mingoni mwa aina mbalimbali za wanyama. Kwa maana, uovu wa maasia unateketeza mimea na viumbe."},{"id":2659,"sura":16,"from_aya":62,"to_aya":63,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"62. Na wanampa Mwenyezi Mungu wanavyovichukia wao, na ndimi zao zinasema uongo kwamba wao watapata mazuri zaidi. Hakuna shaka kwamba hakika wana Moto, na kwamba kwa yakini wataachwa humo. 63. Tallahi! Hakika tuliwatuma Mitume kwa umma zilizokuwa kabla yako, lakini Shetani akawapambia matendo yao. Kwa hivyo leo, yeye ndiye kipenzi chao msaidizi, nao wana adhabu chungu. "},{"id":2660,"sura":16,"from_aya":62,"to_aya":62,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{62} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba washirikina, \"wanampa Mwenyezi Mungu wanavyovichukia wao\" kama vile mabinti na sifa mbaya kwa ushirikina wa kuwafanyia baadhi ya viumbe kitu katika ibada. Navyo pia ni waja tu wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, kama vile wanavyochukia na kutoridhika kwamba watumwa wao - nao ni viumbe wa aina yao - kwamba wawe washirika wao katika kile alichowaruzuku Mwenyezi Mungu, basi vipi wanamfanyia washirika katika waja wake? \"Na\" wao pamoja na kosa hili kubwa, \"ndimi zao zinasema uongo kwamba wao watapata mazuri zaidi\" katika dunia na Akhera. Lakini Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kauli yake, \"Hakuna shaka kwamba hakika wana Moto, na kwamba kwa yakini wataachwa humo\" milele."},{"id":2661,"sura":16,"from_aya":63,"to_aya":63,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{63} Yeye Mtukufu alimbainishia Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwamba yeye si Mtume wa kwanza kukadhibiwa, akasema yeye Mtukufu, \"Tallahi! Hakika tuliwatuma Mitume kwa umma zilizokuwa kabla yako\" ili wawalinganie kumpwekesha Mwenyezi Mungu, \"lakini Shetani akawapambia matendo yao;\" kwa hivyo wakawakadhibisha Mitume hao, na wakadai kwamba hayo wanayofanya ndiyo haki inakayowaokoa kutokana na kila kichukizacho, na kwamba kile ambacho Mitume walilingania ni kinyume na hayo. Kwa hivyo, Shetani alipowapambia matendo yao, akawa yeye ndiye \"kipenzi chao msaidizi\" katika dunia, wakamtii, wakamfuata na wakamfanya kuwa kipenzi chao. \"Je, mnafanya yeye na dhuria zake kuwa wapenzi wasaidizi wenu badala yangu, ilhali wao ni adui zenu? Ni mbaya mno badala hii ya madhalimu.\" \"Nao wana adhabu chungu\" Akhera, kwa maana waliacha kumfanya Mwingi wa rehema kuwa ndiye kipenzi msaidizi wao na wakaridhia kumfanya Shetani kuwa ndiye kipenzi msaidizi wao, kwa hivyo walistahili adhabu ya kudunisha kwa sababu ya hilo."},{"id":2662,"sura":16,"from_aya":64,"to_aya":65,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"64. Na hatukukuteremshia Kitabu hiki isipokuwa ili uwabainishie yale ambayo wanahitalifiana ndani yake, na kiwe Uwongofu na Rehema kwa kaumu wanaoamini. 65. Na Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Kwa hakika, katika hayo imo Ishara kwa kaumu wanaosikia. "},{"id":2663,"sura":16,"from_aya":65,"to_aya":65,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{65} Yaani, kaumu wanaosikia mawaidha ya Mwenyezi Mungu na ukumbusho wake, kwa hivyo wanayatumia hayo kuwa ushahidi kwamba yeye Muabudiwa tu, ambaye haipaswi kumfanyia yeyote ibada isipokuwa Yeye tu. Kwa sababu yeye ndiye aliyeneemesha neema ya kuteremka mvua na kuotesha kila aina ya mimea, na pia yawe ushahidi kwamba yeye ni Muweza wa kila kitu, na kwamba yule aliyeihuisha ardhi baada ya kifo chake, anaweza kuwahuisha wafu, na kwamba yule aliyeueneza ukarimu huu ana rehema pana, na anapeana kwa wingi."},{"id":2664,"sura":16,"from_aya":66,"to_aya":67,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"66. Na hakika katika nyama hoa, mna mazingatio. Tunawanywesha katika vile vilivyomo matumboni mwao, vikatoka baina ya mavi na damu, maziwa safi, mazuri kwa wanywao. 67. Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ulevi na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa kaumu watumiao akili. "},{"id":2665,"sura":16,"from_aya":66,"to_aya":66,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{66} Yaani, \"hakika katika nyama hoa\" ambao Mwenyezi Mungu amewatiisha kwa ajili ya manufaa yenu, \"mna mazingatio\" ambayo mnayatumia kama ushahidi juu ya ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu na upana na wema wake, ambapo aliwanywesha kutokana na matumbo yao yaliyo na mavi na damu. Kwa hivyo akatoa kutokana na hivyo maziwa safi yasiyo na uchafu, yaliyo mazuri kwa wanywao, kwa sababu ya ladha yake, na kwa sababu hunywewa na kuliwa. Basi je, huu siyo isipokuwa uwezo wa kiungu usiokuwa mambo ya kawaida? Je, ni gani katika maumbile kinachogeuza lishe anayoila mnyama na kinywaji anachokinywa kama vile maji safi na chumvi vikawa maziwa safi ambayo ni mazuri kwa wanywao?"},{"id":2666,"sura":16,"from_aya":67,"to_aya":67,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{67} Yeye Mtukufu alifanya matunda ya mitende na zabibu kuwa na manufaa na masilahi kwa waja wake kama vile aina mbalimbali za riziki nzuri ambayo waja wake hula ikiwa laini na imeiva, iliyopo na iliyowekwa kama akiba, na kama chakula na kinywaji kinachotengenezwa kutoka kwa juisi yake na maji matamu ya matunda, na mvinyo ambao ulikuwa halali kabla ya hapo. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaharamisha vileo na akaweka badala yake vilivyo vizuri miongoni mwa maji matamu ya matunda na aina mbalimbali za vinywaji vitamu ambavyo vinaruhusiwa. Basi ndiyo maana wakasema baadhi yao kilichokusudiwa na 'Sakar' hapa ni chakula na kinywaji kitamu, na kauli hii ndiyo inayofailia zaidi kuliko kauli nyingine ile. \"Hakika katika hayo ipo Ishara kwa kaumu watumiao akili,\" katika maneno ya Mwenyezi Mungu kwamba yeye ni mkamilifu wa uwezo, ambapo alivitoa kutoka katika miti inayofanana na kuni, kisha zikawa mazao yenye ladha na matunda mazuri. Na pia wanazingatia ujumla wa rehema yake, ambapo aliwaenea waja wake wote kwa hayo na akawafanyia kuwa mepesi. Na pia wanazingatia kwamba yeye ndiye Mungu aabudiwaye peke yake, kwa maana Yeye ni wa pekee katika hayo."},{"id":2667,"sura":16,"from_aya":68,"to_aya":69,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"68. Na Mola wako Mlezi alimfunulia nyuki kwamba: Jitengenezee majumba yako katika milima, na katika miti, na katika vile wanavyojenga watu. 69. Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako Mlezi zilizofanywa nyepesi kuzipita. Na kutoka matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbalimbali; ndani yake kuna ponya kwa watu. Hakika katika haya ipo Ishara kwa kaumu wanaotafakari. "},{"id":2668,"sura":16,"from_aya":68,"to_aya":69,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{68 - 69} Yaani kaumu wanaotafakari kuhusu kuumbwa kwa nyuki huyu mdogo, ambaye Mwenyezi Mungu alimuongoza kwa mwongozo huu wa ajabu, na akamrahisishia malisho, na kisha kurudi kwenye nyumba zake ambazo walizitengeneza kwa mafundisho na mwongozo wa Mwenyezi Mungu kwake, na kisha kinatoka katika matumbo yake asali hii tamu ya rangi mbalimbali kulingana na tofauti iliyo katika ardhi yake na malisho yake. Ndani yake kuna ponya kwa watu kutokana na magonjwa mengi. Basi huu ni ushahidi juu ya ukamilifu wa utunzaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na ukamilifu wa upole wake kwa waja wake, na kwamba Yeye ndiye ambaye haipaswi kumpenda asiyekuwa yeye, wala kumuomba mwingineye."},{"id":2669,"sura":16,"from_aya":70,"to_aya":70,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"70. Na Mwenyezi Mungu aliwaumba; kisha atawafisha. Na miongoni mwenu wapo wanaorudishwa kwenye umri mbaya kabisa, hata akawa hajui kitu baada ya kuwa alikuwa anajua. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi, Muweza."},{"id":2670,"sura":16,"from_aya":70,"to_aya":70,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{70} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba yeye ndiye aliyeumba waja wake na akawahamisha katika uumbaji awamu baada ya awamu. Kisha baada ya kukamilisha muda wao, anawafisha. Na kuna wengine wao anawapa umri mrefu mpaka akarudishwa \"kwenye umri mbaya kabisa.\" Yaani, umri duni zaidi, ambao kwa huo mtu anafikia udhaifu wa nguvu za dhahiri na za ndani, mpaka akili ambayo ndiyo kiini cha mtu inazidi kuwa dhaifu, hivi kwamba anasahau kile alichokuwa anakijua, na akili yake inakuwa kama akili ya mtoto. Na ndiyo sababu akasema, \" hata akawa hajui kitu baada ya kuwa alikuwa anajua. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi, Muweza.\" yaani elimu yake na uwezo wake vimezunguka vitu vyote. Na katika hayo ni yale anayohamishwa kwayo mwanadamu kutoka awamu za kuumbwa kwake uumbaji mmoja hadi uumbaji mwingine, kama alivyosema Yeye Mtukufu, \" Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba kutokana na udhaifu, kisha akajaalia nguvu baada ya udhaifu, kisha akajaalia baada ya nguvu udhaifu tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye ajuaye zaidi, Mwenye uwezo zaidi.\""},{"id":2671,"sura":16,"from_aya":71,"to_aya":71,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"71. Na Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki. Na wale waliofadhilishwa hawarudishi riziki zao kwa wale iliowamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo. Basi je, wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?"},{"id":2672,"sura":16,"from_aya":71,"to_aya":71,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{71} Na huu ni katika ushahidi wa upweke wake na ubaya wa kumshirikisha. Yeye Mtukufu anasema kuwa kama vile mnavyoshiriki kwamba nyinyi ni viumbe mnaoruzukiwa, lakini Yeye Mtukufu, \"amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki.\" Kwa hivyo akawafanya miongoni mwenu kuwa huru wenye mali nyingi. Na miongoni mwenu kuna watumwa wao wasiomiliki kitu katika dunia. Kwa hivyo, kama vile mabwana zao, ambao Mwenyezi Mungu aliwafadhilisha juu yao katika riziki, hawawezi \"kurudisha riziki zao kwa wale iliowamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo\" na wanaona kwamba hili ni katika mambo yasiyowezekana. Basi vile vile wale mliowashirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu, hao kwa hakika ni waja, hawana chochote katika Ufalme uzito wa chembe. Basi vipi mnawafanya kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? Je, hii si katika dhuluma kubwa zaidi na kukataa neema za Mwenyezi Mungu? Kwa hivyo, ndiyo maana akasema, \"Basi je, wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?\" Kwa hivyo, ikiwa wangekiri neema hizo na wakazinasibisha na yule aliyewapa kuzisimamia, basi wasingemshirikisha na yeyote."},{"id":2673,"sura":16,"from_aya":72,"to_aya":72,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"72. Na Mwenyezi Mungu amewaumbia wake kutokana na nyinyi wenyewe, na akawajaalia kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akawaruzuku vitu vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na wanazikufuru neema za Mwenyezi Mungu?"},{"id":2674,"sura":16,"from_aya":72,"to_aya":72,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{72} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu neema yake kubwa kwa waja wake, ambapo aliwafanyia wake ili mpate utulivu kwao. Na akawafanyia kutoka kwa wake zao watoto ambao macho yao yanafurahi kwa sababu yao, ambao wanawahudumia, wanakidhi mahitaji yao na wanafaidika nao kwa njia nyingi, na akawaruzuku katika vitu vizuri kama vile vyakula, vinywaji, na neema za dhahiri ambazo waja hawawezi kuzidhibiti. \"Basi je, wanaamini upotovu na wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?\" Yaani, wanaamini batili ambayo haukuwa kitu cha kutajwa, kisha Mwenyezi Mungu akaifanya kuwepo, na tena kuwepo kwake huko hakutadumu isipokuwa itatoweka? Nayo haiumbi, wala hairuzuku, wala haiendeshi jambo lolote. Na hii linahusu vyote vinavyoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu kwa ujumla, kwani hivyo vyote ni batili. Basi vipi washirikina wanavichukua kuviabudu badala ya Mwenyezi Mungu? \"Wanazikufuru neema za Mwenyezi Mungu\" kwa kuzitumia katika kumuasi Mwenyezi Mungu na kumkufuru. Je, haya si chochote isipokuwa dhuluma kubwa zaidi, uovu mkubwa zaidi, na upumbavu mkubwa zaidi?"},{"id":2675,"sura":16,"from_aya":73,"to_aya":76,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"73. Na badala ya Mwenyezi Mungu wanawaabudu wasiowamilikia riziki kutoka mbinguni wala kwenye ardhi, wala hawawezi kitu. 74. Basi msimpigie Mwenyezi Mungu mifano. Hakika Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui. 75. Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtumwa aliyemilikiwa, asiyeweza kitu, na mwingine tuliyemruzuku riziki njema inayotoka kwetu, naye akawa anatoa katika riziki hiyo kwa siri na dhahiri. Je, hao watakuwa sawa? Alhamdu Lillahi (Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu)! Lakini wengi wao hawajui. 76. Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa wanaume wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo kwa mlezi wake. Popote anapomuelekeza, haleti heri yoyote. Je, huyo anaweza kuwa sawa na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko kwenye njia iliyonyooka? "},{"id":2676,"sura":16,"from_aya":73,"to_aya":74,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{73 - 74} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu ujinga na udhalimu wa washirikina kwamba wanaabudu badala yake miungu ambayo waliichukua kama washirika na Mwenyezi Mungu, ilhali miungu hao hawawamilikii riziki kutoka mbinguni na ardhini. Hawateremshi mvua wala riziki, wala hawaoteshi chochote katika mimea ya ardhi, wala hawamiliki uzito wa chembe katika mbingu na dunia, wala hawawezi ikiwa wangetaka. Kwa maana, asiyemiliki kitu huenda akawa na nguvu na uwezo wa kumfaidi mwenye kuhusiana naye, lakini hawa hawamiliki kitu wala hawana uwezo. Na hii ndiyo sifa ya miungu wao hao. Basi vipi waliwaweka pamoja na Mwenyezi Mungu na wakawafananisha na Mmiliki wa dunia na mbingu, ambaye ni wake ufalme wote, sifa njema zote, na nguvu zote. Na ndiyo maana akasema, \"Basi msimpigie Mwenyezi Mungu mifano\" inayojumuisha kusawazisha kati yake na viumbe vyake. \"Hakika Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.\" Basi hatupaswi kusema juu yake bila ya elimu. Na ni juu yetu pia kusikia mifano aliyopiga Yeye Ajuaye zaidi. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akapiga mifano miwili kumhusu yeye mwenyewe na vyote vinavyoabudiwa badala yake:"},{"id":2677,"sura":16,"from_aya":75,"to_aya":75,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{75} Mmoja wao ni mtumwa ambaye anamilikiwa, ambaye hajimiliki nafsi yake mwenyewe wala hamiliki chochote katika rasilimali za kidunia. Naye wa pili ni yule aliye huru, tajiri, ambaye Mwenyezi Mungu amemruzuku riziki nzuri ya kila aina ya mali, naye ni mkarimu apendaye kufanya hisani. Anatoa katika mali hiyo kwa siri na dhahiri. Je, huyu na yule ni sawa?!  Hawako sawa, pamoja na kwamba wote ni viumbe ambao si muhali wao kuwa sawa. Kwa hivyo, ikiwa hawako sawa, basi vipi kiumbe - ambaye ni mja ambaye asiyemiliki chochote wala hana nguvu wala uwezo, bali ni mhitaji kwa namna zote - atakuwa sawa na Mola Mlezi, Muumba, Mmiliki wa falme zote, Muweza wa yote?! Ndiyo maana alijisifu yeye tu kwa aina zote za sifa njema, akasema, \"Alhamdu Lillahi (Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu)!\" Na ni kana kwamba ilisemwa: Kama ni hivyo, basi kwa nini washirikina waliwasawazisha miungu yao na Mwenyezi Mungu? Akasema, \"Lakini wengi wao hawajui.\" Kwa maana, ikiwa wangejua elimu ya hakika, basi wasingethubutu kushirikisha huku kukubwa."},{"id":2678,"sura":16,"from_aya":76,"to_aya":76,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{76} Nao mfano wa pili ni mfano wa, \"Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote\" si kichache wala kingi, \"naye ni mzigo kwa mlezi wake\" yaani, mlezi wake anahudumia naye hawezi hata akajihudumia mwenyewe. Kwa hivyo, ana mapungufu kwa kila njia. Basi je, yuko sawa huyu na yule, \"anayeamrisha uadilifu, naye yuko kwenye njia iliyonyooka?\" Kwani, maneno yake ni ya uadilifu, na matendo yake yamenyooka. Kwa hivyo, kama vile hawawi sawa, basi hawi sawa yeyote mwenye kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, ambaye hana uwezo wa chochote cha masilahi yake. Kwani kama si Mwenyezi Mungu kumfanyia hivyo, asingeweza kufanya chochote katika hayo. Hivyo basi, hawezi kufanana, wala kuwa mwenza wa yule ambaye hasemi isipokuwa haki, na wala hafanyi isipokuwa yale anayosifiwa juu yake."},{"id":2679,"sura":16,"from_aya":77,"to_aya":77,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"77. Na siri zote za katika mbingu na ardhi ni za Mwenyezi Mungu. Wala halikuwa jambo la Saa (ya Qiyama) isipokuwa kama kupepesa kwa jicho, au chini zaidi ya hivyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu."},{"id":2680,"sura":16,"from_aya":77,"to_aya":77,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{77} Yaani, Yeye peke yake ndiye ajuaye ghaibu za mbingu na ardhi, na wala hakuna ajuaye yaliyofichikana na siri zote isipokuwa Yeye. Na katika hayo ni kujua kwake Saa ya Qiyama. Kwa hivyo, hakuna yeyote anayejua ni lini itakuja isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Na itakapokuja na ikadhihirika, haitakuwa, \"isipokuwa kama kupepesa kwa jicho, au chini zaidi ya hivyo.\" Kisha watu watasimama kutoka makaburini mwao kuiendea siku ya kufufuka kwao na kuenea kwao, na fursa zinapotea kwa yule atakayetaka kupewa muhula."},{"id":2681,"sura":16,"from_aya":78,"to_aya":78,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"78. Na Mwenyezi Mungu aliwatoa matumboni mwa mama zenu hali ya kuwa hamjui kitu, na akawajaalia masikio na macho na nyoyo ili mpate kushukuru."},{"id":2682,"sura":16,"from_aya":78,"to_aya":78,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{78} Yaani, yeye peke yake ndiye mwenye neema hii, ambapo \"aliwatoa matumboni mwa mama zenu hali ya kuwa hamjui kitu\" wala hamkuwa mnaweza chochote. Kisha, \"akawajaalia masikio na macho na nyoyo.\" Alivitaja viungo hivi vitatu hasa kwa sababu ya heshima yake na ubora wake, na kwa sababu hivyo ndiyo ufunguo wa kila elimu, na mja hawezi kuifikia elimu isipokuwa kupitia moja ya milango hii mitatu. Vinginevyo, ni yeye tu aliyewajaalia viungo vinginevyo vyote na nguvu dhahiri na za ndani na akawa anayakuza yote hayo kidogo kidogo hadi kila kitu kikafikia hali inayokifailia, ili waweze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutumia yale aliyowapa miongoni mwa viungo hivi katika kumtii Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, mwenye kuvitumia vinginevyo, basi vitakuwa ni hoja dhidi yake, na atakuwa ameikabili neema kwa njia mbaya zaidi."},{"id":2683,"sura":16,"from_aya":79,"to_aya":79,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"79. Je, hawawaoni ndege walivyotiishwa katika anga la mbingu? Hakuna mwenye kuwashika isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika katika haya zipo ishara kwa kaumu wanaoamini."},{"id":2684,"sura":16,"from_aya":79,"to_aya":79,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{79} Yaani, kwa sababu wao ndio wanaonufaika na Ishara za Mwenyezi Mungu, wanaotafakari katika yale yaliyowekewa ishara hizo. Na ama wengineo, hao hutazama kwao ni pumbao tu na kughafilika. Na ishara iliyo ndani yake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaumba na umbile linalofailia kupaa, kisha akawatiishia hewa hii nyembamba, kisha akawekea ndani yake nguvu nyingi za kufanya harakati zilizowawezesha kufanya hivyo. Na huu ni ushahidi juu ya hekima yake, elimu yake pana, utunzaji wake wa kiungu kwa viumbe vyake vyote, na ukamilifu wa uwezo wake, yeye Mwingi wa baraka, Mola Mlezi wa walimwengu wote."},{"id":2685,"sura":16,"from_aya":80,"to_aya":83,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"80. Na Mwenyezi Mungu amewajaalia majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amewajaalia ni kutokana na ngozi za wanyama, nyumba mnazoziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufi zao, na manyoya yao, na nywele zao, mnafanya vyombo na mapambo ya kutumia kwa muda. 81. Na Mwenyezi Mungu amewafanyia vivuli katika vitu alivyoviumba, na amewafanyia maskani milimani, na amewafanyia nguo za kuwakinga kutokana na joto, na nguo za kuwakinga katika vita vyenu. Ndivyo hivyo anawatimizia neema zake ili mpate kujisalimisha kwake. 82. Kwa hivyo, wakikengeuka, basi lililo juu yako wewe ni kufikisha ujumbe wazi wazi tu. 83. Wanazijua neema za Mwenyezi Mungu, kisha wanazikanusha, na wengi wao ni makafiri. "},{"id":2686,"sura":16,"from_aya":80,"to_aya":80,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{80} Yeye Mtukufu anawakumbusha waja wake juu ya neema zake, na anawataka kuzishukuru na kuzitambua. Alisema, \"Na Mwenyezi Mungu amewajaalia majumba yenu yawe ni maskani yenu\" katika nyumba, makasri na mfano wake, ambazo zinawahifadhi kutokana na joto na baridi, na zinawasitiri nyinyi na wana wenu, na vitu vyenu. Na mnajitengenezea katika maskani hayo nyumba na vyumba. Nyumba ambamo mna manufaa na masilahi yenu na faida zinginezo zinazoonekana. \"Na amewajaalia kutokana na ngozi za wanyama;\" ima kutokana na ngozi yenyewe, au vile vinavyomea kutokana nayo kama vile sufi, nywele, na manyoya \"nyumba mnazoziona nyepesi\" katika safari na maeneo mnayoshukia ambayo hamkusudii kuishi hapo, ili yawazuie kutokana na joto, baridi, na mvua, na yanazuia mizigo yenu kutokana na mvua. \"Na\" amewajaalia \"kutokana na sufi zao, na manyoya yao, na nywele zao, mnafanya vyombo.\" Na hivyo vinajumuisha kila kinachotengenezwa kutokana navyo kama vile vyombo, matandiko, mavazi na vitu vinginevyo. \"Na furaha kwa muda;\" yaani, mnafurahia kwavyo katika dunia hii na mnafaidika nayo. Basi hivi ni katika vitu ambavyo Mwenyezi Mungu amewafanya waja wake kuvitengeneza na kuvifanya."},{"id":2687,"sura":16,"from_aya":81,"to_aya":81,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{81} \"Na Mwenyezi Mungu amewafanyia vivuli katika vitu alivyoviumba;\" yaani, katika viumbe vyake ambavyo hamkuvitengeneza nyinyi, \"vivuli\" kama vile vivuli vya miti, milima, vilima, na mfano wake. \"Na amewafanyia maskani milimani;\" yaani, mapango yenye kuwahifadhi kutokana na joto, baridi, mvua, na maadui. \"Na amewafanyia nguo za kuwakinga kutokana na joto.\" Na Mwenyezi Mungu hakutaja baridi, kwa sababu ilitangulia kwamba mwanzoni mwa sura hii zimetajwa neema za kimsingi, na mwishoni mwake zimetajwa neema kamilishi na timilizi. Na kuzuia kutokana na baridi ni katika neema za kimsingi, na tayari alikwisha itaja mwanzoni mwa sura hii katika kauli yake, \"katika hao mna vifaa vya kutia joto, na manufaa mengineyo\" na \"nguo za kuwakinga katika vita vyenu\"  kama vile deraya za kawaida na deraya za vifungo, na mfano wake. \"Ndivyo hivyo anawatimizia neema zake\" ambapo aliwapa kwa wingi katika neema zake zisizowezekana kuhesabika \"ili\" mnapozikumbuka neema za Mwenyezi Mungu na kuziona zimewafunika katika kila njia, \"mtapata kujisalimisha kwake.\" Kwa sababu ya ukuu wake, na mfuate amri yake, na kuzitumia katika kumtii yule aliyewapa kuzisimamia. Kwa hivyo wingi wa neema ni katika sababu zinazowafanya waja kuzidisha shukrani na kumsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yake."},{"id":2688,"sura":16,"from_aya":82,"to_aya":82,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{82} Lakini wadhalimu walikataa isipokuwa uasi na ukaidi, na ndiyo sababu Mwenyezi Mungu akasema juu yao, \"Kwa hivyo, wakikengeuka\" wakamuacha Mwenyezi Mungu na wakaacha kumtii baada ya kukumbushwa neema zake na ishara zake, \"basi lilio juu yako wewe ni kufikisha ujumbe wazi wazi tu.\" Huna chochote katika kuwaongoa na kuwawezesha, lakini unatakiwa tu kuaidhi, kukumbusha, kuonya na kutahadharisha."},{"id":2689,"sura":16,"from_aya":83,"to_aya":83,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{83} Ukifanya kile unachopaswa kufanya, basi hesabu yao ni juu ya Mungu, wanaona sadaka na wanajua neema ya Mungu, lakini wanaikataa na kuikataa. \"Wengi wao ni makafiri; Hakuna mema ndani yao, na kinachowanufaisha ni mfululizo wa aya; kwa sababu ya upotovu wa hisia zao na nia zao mbaya, na wataona malipo ya Mungu kwa kila jabari mkaidi, mwenye kukufuru mno neema, mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mitume wake."},{"id":2690,"sura":16,"from_aya":84,"to_aya":87,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"84. Na siku tutakapomtoa shahidi kutoka katika kila umma, kisha hawataruhusiwa wale waliokufuru wala hawataachiliwa kutaka radhi. 85. Na wale waliodhulumu watakapoiona adhabu, hawatapunguziwa adhabu hiyo, wala hawatapewa muhula. 86. Na wale walioshirikisha watakapowaona hao waliowashirikisha na Mwenyezi Mungu, watasema: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio washirikishwa wetu ambao tulikuwa tukiwaomba badala yako. Lakini hao watawatupia kauli: Hakika nyinyi ni waongo! 87. Na siku hiyo watasalimu amri mbele ya Mwenyezi Mungu, na yatapotea yale waliyokuwa wakiyazua. "},{"id":2691,"sura":16,"from_aya":84,"to_aya":85,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{84-85} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya hali ya hawa ambao walikufuru katika Siku ya Qiyama, na kwamba hawatakubaliwa udhuru wowote wala hawataondolewa adhabu, na kwamba washirikishwa wao hao watawakataa, na watakiri wenyewe kwamba walikuwa makafiri na kwamba walimsingizia Mwenyezi Mungu. Alisema Yeye Mtukufu, \"Na siku tutakapomtoa shahidi kutoka katika kila umma\" ili ashuhudie juu yao matendo yao na kile walichomjibu kwacho mlinganiaji aliyekuwa analingania kwenye wongofu. Na shahidi huyu ambaye Mwenyezi Mungu atamtoa kwao atakuwa ndiye shahidi msafi zaidi na mwadilifu wao zaidi, na wao ni Mitume, ambao, watakaposhuhudia, basi itatimia hukumu juu yao. \"Kisha hawataruhusiwa wale waliokufuru\" ili waweke udhuru wao. Kwa maana kuweka kwao udhuru baada ya wao kwisha jua kwa yakini ubatili wa wayafanyayo ni udhuru muongo usioweza kuwasaidia kitu. Na pia wakiomba kurudi duaniani ili watekeleze ambayo hawakutekeleza vyema, hawajibiwi wala hawaridhiwi. Bali wanaanzishiwa adhabu kali ambayo hawatahafifishiwa, wala kupewa muhula kuanzia wanapoiona, kwa sababu hawana mazuri yoyote. Na matendo yao yatahesabiwa tu, na kudhibitiwa, na watafanywa kuyaungama, na watafedheheshwa."},{"id":2692,"sura":16,"from_aya":86,"to_aya":86,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{86} \"Na wale walioshirikisha watakapowaona hao waliowashirikisha na Mwenyezi Mungu\" Siku ya Qiyama, na wakajua ubatili wao, na wasiweze kukataa, \"watasema: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio washirikishwa wetu ambao tulikuwa tukiwaomba badala yako.\" Hawana manufaa yoyote wala maombezi, kwa hivyo wakaashiria wenyewe juu ya ubatili wao, na watawakufuru, na itatokea chuki na uadui kati yao. \"Lakini hao watawatupia kauli\" na washirikishwa wao hao wakiwaambia, \"Hakika nyinyi ni waongo!\" Ambapo mlitushirikisha na Mwenyezi Mungu na mkatuabudu pamoja naye, nasi hatukuwaamuru hayo, wala hatukudai kwamba tunastahili uungu. Kwa hivyo lawama ni kwenu."},{"id":2693,"sura":16,"from_aya":87,"to_aya":87,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{87} Basi hapo wakajisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, na wakainyenyekea hukumu yake, na wakajua kwamba wanastahiki kuadhibiwa, \"na yakapotea yale waliyokuwa wakiyazua\" Basi wakaingia Motoni ilhali nyoyo zao zikajawa na chuki kubwa juu ya nafsi zao wenyewe, na kumsifu Mola wao Mlezi, na kwamba Yeye hakuwaadhibu isipokuwa kwa yale waliyoyachuma."},{"id":2694,"sura":16,"from_aya":88,"to_aya":88,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"88. Wale waliokufuru na kuzuilia njia ya Mwenyezi Mungu, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu, kwa walivyokuwa wakifanya uharibifu."},{"id":2695,"sura":16,"from_aya":88,"to_aya":88,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{88} Kwa maana, wao wenyewe walikufuru, na wakakadhibisha ishara za Mwenyezi Mungu, na wakapigana dhidi ya Mitume wake, na wakawazuia watu kutoka kwa njia ya Mwenyezi Mungu, na wakawa walinganiaji kwenye upotofu, kwa hivyo wakastahili kuzidishiwa adhabu maradufu kama vile uhalifu wao uliongezeka maradufu, na kama vile walivyofanya uharibifu katika ardhi ya Mwenyezi Mungu."},{"id":2696,"sura":16,"from_aya":89,"to_aya":89,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"89. Na (waonye) siku tutakapomtoa shahidi katika kila umma kutokana na wao wenyewe, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hawa. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu."},{"id":2697,"sura":16,"from_aya":89,"to_aya":89,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{89} Alipotaja hapo katika yaliyotangulia kwamba atatoa shahidi katika kila umma, pia akataja hilo hapa, na akamtaja miongoni mwa Nabii huyu mtukufu tu. Akasema, \"na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hawa\" yaani, juu ya umma wako, ukiwashuhudia ya heri na maovu. Na hili ni katika ukamilifu wa uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwamba kila Mtume anashuhudia juu ya umma wake. kwa sababu yeye ndiye ajuaye zaidi matendo ya umma wake kuliko wengineo, na aliye mwadilifu zaidi na mwenye huruma zaidi kiasi kwamba hawezi kushuhudia juu yao isipokuwa kile wanachostahili. Na hii ni kama kauli yake yeye Mtukufu, \"Na vivyo hivyo tumewafanya muwe Umma wa wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu.\" Na amesema yeye Mtukufu, \"Basi itakuwa vipi tutakapoleta kutoka kwa kila umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi dhidi ya hawa? Siku hiyo watapenda wale waliokufuru na wakamuasi Mtume lau kuwa ardhi isawazishwe kwa wao.\" Na kuali yake, \"Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu\" kuhusiana na misingi ya dini na matawi yake, na kuhusiana na hukumu za nyumba hizi mbili, na kila kitu ambacho waja wanahitaji, basi kimeelezwa humo kwa ufafanuzi kamili, na kwa maneno yaliyo wazi na maana za wazi kabisa, kiasi kwamba yeye Mtukufu anarudia humo mambo makubwa ambayo moyo unahitaji kuyapitia kila wakati na kuyarudia kila saa. Na anayaonyesha kwa maneno tofauti tofauti na ushahidi anuai ili yakae mioyoni na kuzalisha heri na wema kulingana na uthabiti wake moyoni, na tena kiasi kwamba Yeye Mtukufu anaunganisha katika maneno machache yaliyo wazi, maana nyingi, basi yakawa maneno hayo ndiyo kanuni na msingi wake. Na lizingatie hili katika aya inayofuata aya hii, na aina mbalimbali za amri na makatazo zilizo ndani yake ambazo haziwezi kuwekewa mipaka. Na wakati Qur-ani hii ilipokuwa ni ufafanuzi wa kila kitu, ikawa ni hoja ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake wote, kwa hivyo hoja ya madhalimu ikakatika kwa hilo, na Waislamu wakafaidika nayo, kwa hivyo ikawa ni uwongofu kwao ambao wanaongoka kwayo katika mambo ya dini yao na dunia yao, na ni rehema ambayo wanapata kwayo kila heri katika dunia hii na Akhera. Na uwongofu ni kile walichopata kutokana na elimu yenye manufaa na matendo mema. Nayo rehema ni matokeo ya hayo miongoni mwa malipo ya dunia na Akhera, kama vile kutengenea kwa moyo, na wema wake, utulivu wake, na ukamilifu wa akili ambao hautimii isipokuwa tu kwa kuilea juu ya maana zake ambazo ndizo maana tukufu zaidi na za juu kabisa. Na rehema hiyo pia katika matendo matukufu, maadili mema, riziki pana, nusura dhidi ya maadui kwa maneno na matendo, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na utukufu wake mkubwa ambao hajui neema ya kudumu iliyomo isipokuwa Mola Mlezi, mwingi wa kurehemu."},{"id":2698,"sura":16,"from_aya":90,"to_aya":90,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"90. Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa, na anakataza uchafu, na uovu, na dhuluma. Anawaaidhi ili mpate kukumbuka."},{"id":2699,"sura":16,"from_aya":90,"to_aya":90,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{90} Na uadilifu ambao Mwenyezi Mungu aliamuru unajumuisha kufanya uadilifu katika haki yake na haki ya waja wake. Basi uadilifu katika hayo ni kutekeleza haki mbalimbali kikamilifu na kwa wingi. Kwamba mja atekeleze kile ambacho Mwenyezi Mungu alimuwajibishia miongoni mwa haki za kimali na za kimwili na zenye kuchanganya mbili hizo katika haki zake Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, na kwamba aamiliane na viumbe kwa uadilifu kamili. Kwa hivyo akatekeleza kila mlezi kile kilicho juu yake chini ya ulezi wake, sawa iwe ni katika usimamizi na uongozi mkuu, na usimamizi wa kutoa hukumu, na makamu wa kiongozi mkuu, na makamu wa mahakimu. Na uadilifu ni kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwafaradhishia katika Kitabu chake na juu ya ulimi wa Mtume wake na akawaamuru kuifuata. Na uadilifu katika miamala ni kutimiza yote yanayokulazimu katika mikataba ya kuuza, kununua, na mabadilishano mengineyo. Kwa hivyo haufai kuwapunja haki yoyote katika hayo, wala kuwadanganya, wala kuwahadaa, na kuwadhulumu. Na kufanya haki ni wajibu, lakini kufanya hisani pia ni jambo zuri linalopendekezwa. Na hilo ni kama vile kuwafaidi watu kwa mali, mwili, elimu, na aina nyinginezo za faida, hata kuwafanyia wema wanyama wanaoliwa na wengineo kunaingia humo. Na Mwenyezi Mungu alitaja kuwapa jamaa hasa, pamoja na kwamba wanaingia katika ujumla wa aya hii, ili kusisitiza haki yao na kukokoteza suala la kuwaunga, kuwafanyia wema, na kufanya bidii kubwa katika hilo. Na wanajumuishwa jamaa wote katika hilo, sawa wawe wa mbali wao au wa karibu wao, lakini kila mtu ambaye ni wa karibu zaidi, basi anastahili zaidi kufanyiwa wema. Na kauli yake, \"na anakataza uchafu.\" Nao ni kila dhambi kubwa ambayo ni chafu kulingana na sheria na silika, kama vile ushirikina, kuua bila ya haki, uzinzi, wizi, kujiona, kiburi, kudharau viumbe na yasiyokuwa hayo miongoni mwa uchafu. Na inaingia katika maovu kila dhambi na uasi unaohusiana na haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nayo dhuluma ni kila uvukaji mipaka kuhusiana na viumbe katika damu zao, mali zao, na heshima zao. Kwa hivyo, Aya hii imejumuisha maamrisho yote na makatazo yote, na hakikubakia chochote isipokuwa kinaingia ndani yake. Na vipengele vidogo vyote vinairudia kanuni hii, kwani kila jambo linalojumuisha uadilifu, au kufanya hisani, au kuwapa jamaa, basi hilo ni katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamuru. Na kila jambo ambalo linajumuisha uchafu, au uovu, au dhuluma, basi hilo ni katika yale ambayo Mwenyezi Mungu alikataza. Na kwa hayo ndio unajulikana uzuri wa yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamuru na ubaya wa yale ambayo alikataza. Na kwa hayo yanapaswa kupimwa maneno yote ya watu, na kuyarudishia hali zote. Basi ni mwingi wa baraka aliyeweka katika maneno yake uwongofu, uponyaji, nuru, kipambanuzi kati ya vitu vyote, na ndiyo sababu akasema, \"Anawaaidhi\" kwa yale aliyowabainishia katika kitabu chake, kwa maana amewaamrisha yale ambaye ndani yake kuna kutengenea kwenu kukubwa zaidi, na akawakataza yale ambayo ndani yake kuna madhara kwenu, \"ili mpate kuyakumbuka\" yale anayowaaidhi kwayo na mkayafahamu na kuyaelewa kwa hivyo mkatenda kwa mujibu wake, hivyo basi mkapata furaha ambayo hakuna huzuni wowote pamoja nayo."},{"id":2700,"sura":16,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"Na alipoamrisha yale ambayo ni wajibu katika asili ya sheria, akaamrisha kutimizwa kwa yale ambayo mja mwenyewe alijiwajibishia, akasema:"},{"id":2701,"sura":16,"from_aya":91,"to_aya":92,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"91. Na timizeni ahadi ya Mwenyezi Mungu mnapoahidi, wala msivunje viapo baada ya kuvifunga imara, ilihali mmekwisha mfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myafanyayo. 92. Wala msiwe kama mwanamke yule aliyeuzongoa uzi wake baada ya kwishausokota ukawa mgumu. Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa ati umma mmoja una nguvu zaidi kuliko mwingine? Hakika Mwenyezi Mungu anawajaribu kwa njia hiyo. Na bila ya shaka atawabainishia Siku ya Qiyama yale mliyokuwa mkihitalifiana ndani yake. "},{"id":2702,"sura":16,"from_aya":91,"to_aya":91,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{91} Hii linajumuisha mambo yote ambayo mja alimuahidi Mola wake Mlezi miongoni mwa ibada mbalimbali kama vile nadhiri na viapo ambavyo mja alivifunga ikiwa kuna wema katika kuvitimiza. Na pia linajumuisha mikataba aliyofunga yeye na wengine, kama vile maagano wanayofanya wafanyao mikataba, na kama vile ahadi anayompa mja wengine na akaisisitiza juu yake, basi ni lazima atimize yote hayo na kuyakamilisha awezavyo. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akakataza kuzivunja, akasema, \"wala msivunje viapo baada ya kuvifunga imara\" kwa kuvifunga kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Ilihali mmekwisha mfanya Mwenyezi Mungu\" enyi mfungao mikataba \"ndiye mdhamini wenu.\" Kwa hivyo si halali kwenu kutotekeleza yale mliyomfanya Mwenyezi Mungu kuwa ndiye mdhamini wenu, na hilo likawa ndani yake kuacha kumtukuza Mwenyezi Mungu na kumdharau. Na ilhali mwenzako aliridhia kiapo chako na uhakikisho ambao mlimfanya Mwenyezi Mungu kuwa ndiye mdhamini juu yake. Hivyo basi, kama alivyokuamini na akawa na dhana nzuri kwako, basi nawe mtimizie yale uliyosema na ukayasisitiza. \"Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myafanyayo,\" na atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake kulingana na nia yake na makusudio yake."},{"id":2703,"sura":16,"from_aya":92,"to_aya":92,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{92} \"Wala msiwe,\" katika kuvunja kwenu maagano kwa mithali mbaya na mbaya kabisa na ushahidi wa upumbavu wa wale wanaozitumia. Ambao ni \"kama mwanamke yule\" anayeusokota uzi wake ukawa mgumu, na pindi unapokuwa imara na ukatimia kama ulivyotakiwa kuwa, anaufumua na kuufanya kuwa, \"umezongoka.\" Basi akawa alitaabisha kuusokota, tena akataabika katika kuufumua na wala hakufaidika isipokuwa kuambulia patupu, taabu, upumbavu wa kiakili, na upungufu wa kimaoni. Basi hivyo ndivyo alivyo mwenye kuvunja agano lake. Anakuwa dhalimu, mjinga, mpumbavu, mpungufu wa dini, na uungwana. Na kauli yake, \"Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa ati umma mmoja una nguvu zaidi kuliko mwingine?\" Yaani, hali hii haiwafailii, kwamba mfunge viapo vya mkazo, kisha mkangojea fursa, ikiwa aliyevifunga ni dhaifu, asiyemuweza mwenzake huyo, anavitimiza siyo kwa sababu ya kuutukuza mkataba na kiapo hicho, lakini kwa sababu ya kutoweza kwake kuuvunjilia mbali. Na ikiwa ina nguvu, na anaona kwamba kuna masilahi ya kidunia katika kuuvunja, anauvunja bila ya kujali agano na kiapo cha Mwenyezi Mungu. Na hayo yote yanakuwa kulingana na matamanio ya nafsi roho na kuyatanguliza mbele ya makusudio ya Mwenyezi Mungu kwenu, na kuyatanguliza pia mbele ya uungwana wa kibinadamu na tabia zinazoridhiwa, kwa sababu tu kwamba umma mmoja ni wengi na wenye nguvu zaidi ya wenzao.  Haya ni majaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu na mtihani ambao [Mwenyezi Mungu] anawajaribu kwa huo, kwani aliweka sababu za kuwajaribia ambazo anamjaribu kwazo mkweli atimizaye kutokana na muovu mwana mashaka. \"Na bila ya shaka atawabainishia Siku ya Qiyama yale mliyokuwa mkikhitalifiana ndani yake.\" Kisha atamlipa kila mmoja kwa matendo yake, na atawahizi waliovunja ahadi zao."},{"id":2704,"sura":16,"from_aya":93,"to_aya":93,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"93. Na Mwenyezi Mungu angelitaka, kwa yakini angeliwafanya kuwa umma mmoja. Lakini anampoteza amtakaye, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa juu ya yale mliyokuwa mkiyatenda."},{"id":2705,"sura":16,"from_aya":93,"to_aya":93,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{93} Yaani, \"Mwenyezi Mungu angelitaka\" angeliwakusanya watu kwenye uwongofu na akawafanya kuwa, \"umma mmoja.\" Lakini Yeye Mtukufu ndiye pekee aongoaye, na apotoshaye. Na kuongoa kwake na kupotosha kwake ni katika vitendo vyake vinavyofuatana na elimu yake na hekima yake. Anampa uwongofu yule anayeustahili kwa fadhila zake, na anamnyima yule asiyeustahili kwa uadilifu wake, \"Na hakika mtaulizwa juu ya yale mliyokuwa mkiyatenda\" ya heri na maovu. Kisha atawalipa kwa hayo, malipo kamili zaidi na ya uadilifu zaidi."},{"id":2706,"sura":16,"from_aya":94,"to_aya":94,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"94. Wala msifanye viapo vyenu kuwa njia ya kudanganyana baina yenu, mguu ukaja teleza baada ya kuwa thabiti, na mkaonja mabaya kwa sababu ya kule kuzuilia kwenu Njia ya Mwenyezi Mungu, na mkapata adhabu kubwa."},{"id":2707,"sura":16,"from_aya":94,"to_aya":94,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{94} Yaani, \"Wala msifanye viapo vyenu\" na ahadi zenu na maagano yenu kufuatana na matamanio yenu, kiasi kwamba wakati wowote mnapotaka, mnavitimiza, na wakati wowote mnapotaka, mnavivunja. Kwa maana mkifanya hivyo, miguu yenu itateleza baada ya kuwa thabiti kwenye njia iliyonyooka. \"Na mkayaonja mabaya;\" yaani, adhabu ambayo itawawia mbaya na kuwahizi, \"kwa sababu ya kule kuzuilia kwenu Njia ya Mwenyezi Mungu\" kwa kuwa mlipotea nyinyi wenyewe na mkawapoteza wengine; \"na mkapata adhabu kubwa\" ambayo itazidishwa."},{"id":2708,"sura":16,"from_aya":95,"to_aya":97,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"95. Wala msinunue ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo. Hakika kilicho kwa Mwenyezi Mungu ndicho bora kwenu, ikiwa mnajua. 96. Mlivyo navyo vitakwisha, na vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyobakia. Na kwa yakini Sisi tutawapa wale waliosubiri ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda. 97. Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, hakika tutamhuisha uhai mwema, na hakika tutawapa ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda. "},{"id":2709,"sura":16,"from_aya":95,"to_aya":95,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{95} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawatahadharisha waja wake dhidi ya kuvunja ahadi na viapo kwa ajili ya mambo ya kidunia yasiyo na thamani, akasema, \"Wala msinunue ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo\" mnayopata kwa kuvunja ahadi na kutoitimiza. \"Hakika kilicho kwa Mwenyezi Mungu\" miongoni mwa thawabu za haraka na za baadaye kwa mwenye kupendelea radhi zake na akatimiza yale aliyomuahidi Mwenyezi Mungu, \"ndicho bora kwenu\" kuliko vitu visivyo na thamani vya kidunia vyenye kuondoka, \"ikiwa mnajua.\""},{"id":2710,"sura":16,"from_aya":96,"to_aya":96,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{96} Basi vipendeleeni vya kubakia juu ya vya kupotea. Kwa maana hakika vile, \"Mlivyo navyo\" - hata kama ni kingi namna gani - lazima vitakwisha na kutoweka. \"Na vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyobakia\" kwa kubakia kwake. \nHavitaisha wala havitapotea. Basi si mwenye akili atakayevipendelea vyenye kwisha visivyo na thamani  juu ya vyenye kubakia vyenye thamani. Na hii ni kama kauli yake yeye Mtukufu, \"Lakini nyinyi mnapendelea uhai wa dunia! Na Akhera ndiyo bora na yenye kudumu zaidi.\" \"Na vilivyoko kwa Mwenyezi Mungu ndivyo bora kwa walio wema.\" Na hili limo himizo na kutia moyo juu ya kujitenga na dunia, hasa kujitenga ambako ni lazima, kama vile kujitenga na yale yenye kumdhuru mja na yenye kumfanya kujishughulisha na kuacha yale ambayo Mwenyezi Mungu alimuwajibishia na kuyatanguliza mbele ya haki ya Mwenyezi Mungu. Basi huku ndiko kujitenga na dunia ambako ni kwa wajibu. Na katika yale yenye kumsababishia mja kujitenga na dunia ni yeye kuzikabili starehe za dunia na matamanio yake kwa heri za Akhera. Kwani atapata tofauti kubwa kushindana kukubwa, jambo ambalo litamfanya kulipendelea jambo la juu zaidi kati ya mawili hayo. Na kujitenga na dunia kunakosifika si kujitenga ili kufanya ibada zinazomhusu mtu mwenyewe tu, kama vile swala, saum, dhikri, na mifano ya hayo. Bali hawi mja mwenye kujitenga na dunia kujitenga sahihi mpaka ayafanye yale awezayo miongoni mwa yale alioyoamrishwa kufanya miongoni mwa maamrisho ya kisheria ya wazi na ya ndani, na pia alinganie kwa Mwenyezi Mungu na kwa dini yake kwa kauli na vitendo. Na kujitenga na dunia ambako kwa hakika ni kujitenga na yasiyofaidi katika dini na dunia, na kuwa na utashi mkubwa, na kufanya bidii katika kila yenye kunufaisha, \"Na kwa yakini Sisi tutawapa wale waliosubiri\" juu ya kumtii Mwenyezi Mungu na kujiepusha na kumuasi Yeye, na wakajitoa kabisa matamanio ya kidunia yenye kudhuru dini yao. \"Ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.\" Uzuri mmoja kwa mara kumi mfano wake hadi mizidisho mara mia saba hadi mizidisho mingi, kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa anayetenda mazuri."},{"id":2711,"sura":16,"from_aya":97,"to_aya":97,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{97} Basi ndiyo sababu, akataja malipo ya watendaji katika dunia na Akhera. Akasema, \"Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini\" kwa maana Imani ni sharti la matendo mema kuwa sahihi na kukubaliwa. Bali hayaitwi matendo mema isipokuwa kwa imani. Na pia imani inahitaji kutenda mema. Kwani, imani ni usadikisho thabiti wenye kuzaa matendo ya viungo ya wajibu na yapendekezwayo. Kwa hivyo mwenye kujumuisha kati ya imani na matendo mema, \"hakika tutamhuisha uhai mwema\" kwa kuufanya moyo wake kutua na kutulia kwa nafsi na kutoangalia yenye kuushawishi moyo wake na Mwenyezi Mungu atampa riziki nzuri halali kutoka asikotarajia, \"na hakika tutawapa\" katika Akhera, \"ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda\" miongoni mwa aina mbalimbali za starehe ambazo hakuna jicho lililowahi kuyaona, wala hakuna sikio lililowahi kuyasikia wala hayajawahi kupitia katika moyo wa binaadamu yeyote. Basi Mwenyezi Mungu atampa mazuri duniani na Akhera pia."},{"id":2712,"sura":16,"from_aya":98,"to_aya":100,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"98. Na unaposoma Qur-ani, mwombe Mwenyezi Mungu akulinde kutokana na Shetani aliyelaaniwa. 99. Hakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na wakamtegemea Mola wao Mlezi. 100. Hakika mamlaka yake yako juu ya wale wanaomfanya kuwa rafiki yao msaidizi, na wale wanaofanya ushirika naye. "},{"id":2713,"sura":16,"from_aya":98,"to_aya":100,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{98 - 100} Yaani, unapotaka kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, ambacho ndicho kitabu cha heshima zaidi kitukufu zaidi, na ambacho ndani yake kuna yenye kufanya mioyo kutengenea, na elimu nyingi, basi shetani hutia bidii zaidi dhidi ya mja anapotaka kuanza kufanya mambo mema. Kwa hivyo anafanya bidii kubwa kumuondoa katika makusudi yake na maana zake. Kwa hivyo, njia ya usalama kutokana na uovu wake ni kumkimbilia Mwenyezi Mungu na kutafuta kinga yake kutokana na uovu wake. Kwa hivyo msomaji na aseme, \"Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutoka na shetani aliyelaaniwa\" huku akitafakari maana yake, akitemgemea Mwenyezi Mungu kwa moyo wake katika kumuondoa karibu naye, akijitahidi katika kuzuia wasiwasi wake na fikira zake mbaya, akifanya bidii kufanya sababu yenye nguvu zaidi ya kumzuia, ambayo ni kujipamba kwa pambo la imani na kumtegemea Mwenyezi Mungu. Kwa maana, Shetani \"hana mamlaka juu ya wale walioamini na wakamtegemea Mola wao Mlezi\" peke yake, asiyekuwa na mshirika yeyote. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu anawazuia waumini wanaomtegemea kutokana na uovu Shetani naye anabaki hana njia yoyote ya kuwafikia. \"Hakika mamlaka yake yako juu ya wale wanaomfanya kuwa rafiki yao msaidizi\" na hilo huwa kwa kuacha kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa rafiki msaidizi, na kuingia katika utii wa Shetani, na kujiunga na kikundi chake. Basi wao wenyewe ndio waliomfanya kuwa rafiki yao msaidizi, naye akawachochea mchocheo mkubwa kuingia katika maasia, na akawaongoza kwelikweli kuingia motoni."},{"id":2714,"sura":16,"from_aya":101,"to_aya":102,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"101. Na tunapobadilisha Ishara pahala pa Ishara, na Mwenyezi Mungu anayajua anayoyateremsha, wanasema: Wewe si chochote ila ni mzushi tu, lakini wengi wao hawajui tu. 102. Sema: Ameiteremsha Roho mtakatifu kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa haki, ili awaimarishe wale walioamini, na kuwa ni uwongofu, na bishara kwa Waislamu. "},{"id":2715,"sura":16,"from_aya":101,"to_aya":101,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{101} Mwenyezi Mungu anataja kwamba wale wanaokadhibisha Qur-ani hii wanafuatilia tu yale wanayoyaona kuwa ni hoja kwao, ambayo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye hakimu mwenye hekima, anayetunga sheria na anabadilisha hukumu mahali pa nyingine kwa sababu ya hekima yake na rehema yake. Kwa hivyo, wakiona hilo, wanamkashifu Mtume na kile alichokuja nacho, na \"wanasema: Wewe si chochote ila ni mzushi tu\" Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, \"lakini wengi wao hawajui tu.\" Kwa maana wao ni wajinga, hawana elimu yoyote juu ya Mola wao Mlezi, wala sheria yake. Na inavyojulikana ni kwamba kukashifu kwa mjinga bila ya elimu hakuzingatiwi kabisa. Kwa maana, kukashifu kitu kunatokana na kukijua, na kile ambacho kinajumuisha, ambacho kinalazimu kisifiwe na kukashifiwa."},{"id":2716,"sura":16,"from_aya":102,"to_aya":102,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{102} Na ndiyo maana yeye Mtukufu akataja hekima yake katika suala hili, akasema, \"Sema: ameiteremsha hii Roho mtakatifu\" naye ni Jibril, Mjumbe Mtakatifu, ambaye ametakasika kutokana na kasoro zote, hiyana na mapungufu, \"kwa haki.\" Yaani, kushuka kwake ni kwa haki, nacho kinajumuisha haki katika habari zake, amri zake na makatazo yake. Basi hakuna njia yoyote kwa mtu yeyote kukikashifu kashfa iliyo sahihi. Kwa maana inapojulikana kwamba hicho ndiyo haki, itajulikana kwamba chenye kukipinga na kuwa kinyume nacho ni batili, \"ili awaimarishe wale walioamini\" wakati wa kuteremka kwa ishara zake na kuwajia mara kwa mara, kwa hivyo haiachi haki kuendelea kuifikia mioyo yao kidogo kidogo, hadi imani yao iwe thabiti zaidi kuliko milima imara. Pia, wanajua kwamba hiyo ndiyo haki, na anapoweka sheria ya hukumu fulani miongoni mwa hukumu mbalimbali, kisha akaifuta, wanajua kwamba ameibadilisha kwa kile kilicho mfano wake au kilicho bora zaidi yake kwao, na kwamba kuifuta ndiko kunafaa kwa sababu ya hekima ya kimungu na pia kufailia kwake kwa kiakili. \"Na kuwa ni uwongofu, na bishara kwa Waislamu;\" yaani, inawaongoza kwenye hakika za mambo, na inawabainishia haki kutokana na batili, na uwongofu kutokana na upotovu, na inawabashiria kwamba wana malipo mazuri, na kwamba watadumu humo milele. Pia, kila inapoteremka kidogo kidogo, ndivyo inakuwa mwongozo mkubwa zaidi na habari njema kwao kuliko ikiwa angewajia kwa jumla moja, na mawazo yakatawanyika ndani yake. Lakini Mwenyezi Mungu hushuka hukumu moja, na mara nyingine zaidi ya moja. Kwa hivyo, wanapoifahamu na wakaielewa, wanajua kilichokusudiwa nayo, na wakaifikiria vizuri, anashusha nyingine. Vivyo hivyo, na ndiyo maana, maswahaba - Mwenyezi Mungu awe radhi nao - walifikia kiwango kikubwa kwayo, na tabia zao na maumbile yao vikabadilika, na wakahamia kwenye tabia, ada, kurudi, na matendo ambayo kwayo waliwashinda wa mwanzo na wa mwisho. Basi ikawa inafaa zaidi kwa wale waliowafuata baada yao kujifunza vyema elimu zake na wajipambe kwa tabia zake, wajiangazie kwa nuru yake katika giza la upotovu na ujinga, na waifanye kuwa Imamu wao katika hali zote. Na kwa hayo, yatanyooka mambo yao ya kidini na ya kidunia."},{"id":2717,"sura":16,"from_aya":103,"to_aya":105,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"103. Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anayemfundisha. Lugha ya huyo wanayemuelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu iliyo bainifu. 104. Hakika wale wasioziamini Ishara za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hawaongoi, nao wana adhabu chungu. 105. Hakika wanazua uongo tu wale wasioziamini Ishara za Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waongo. "},{"id":2718,"sura":16,"from_aya":103,"to_aya":103,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{103} Yeye mtukufu anajulisha juu ya usemi wa washirikina wanaomkadhibisha Mtume wake, \"kwamba wanasema: Yuko mtu anayemfundisha\" kitabu hiki alichokuja nacho. Na mtu huyo wanayemkusudia ni wa lugha ya kigeni. \"Na hii\" Qur-ani \"ni lugha ya Kiarabu iliyo bainifu.\" Je, kauli hii inawezekana au hata ina nafasi yoyote katika uwezekano? Lakini mwongo anadanganya na wala hafikirii uongo wake utaisha aje? Kwa hivyo maneno yake yanakuwa na ukinzani na ubovu, jambo ambalo linalazimu kuikataa kwa kuifikiria tu."},{"id":2719,"sura":16,"from_aya":104,"to_aya":104,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{104} \"Hakika wale wasioziamini Ishara za Mwenyezi Mungu\" zinazoonesha ushahidi wa wazi juu ya haki iliyo bainifu, wao wanaukataa wala hawaukubali. \"Mwenyezi Mungu hawaongoi\" kwa kuwa walijiwa na uwongofu, lakini wakaukataa, kwa hivyo wakaadhibiwa kwa kunyimwa uwongofu huo, na kuachiliwa mbali bila kusaidiwa na Mwenyezi Mungu, \"nao wana adhabu chungu.\""},{"id":2720,"sura":16,"from_aya":105,"to_aya":105,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{105} \"Hakika wanazua uongo tu wale wasioziamini Ishara za Mwenyezi Mungu,\" kama vile wale wanaomfanyia ukaidi Mtume wake baada ya kujiwa na hoja zilizo wazi. \"Na hao ndio waongo\" peke yao. Ama Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - anayeziamini ishara za Mwenyezi Mungu, anayemnyenyekea Mola wake Mlezi, basi ni muhali amsingizie Mwenyezi Mungu na kumzulia yale ambayo hakusema. Basi maadui zake ndio waliomtuhumu kwa uongo ambao ndiyo sifa yao, lakini Mwenyezi Mungu akadhihirisha hizaya yao na akabainisha fedheha zao, basi ni zake yeye Mtukufu sifa njema."},{"id":2721,"sura":16,"from_aya":106,"to_aya":109,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"106. Anayemkufuru Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipokuwa yule aliyelazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini yule aliyekifungulia kifua chake ukafiri - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao wana adhabu kubwa. 107. Hayo ni kwa sababu wameupendelea uhai wa dunia hii kuliko Akhera, na kwa sababu Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu makafiri. 108. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu ameziziba nyoyo zao na masikio yao na macho yao. Na hao ndio walioghafilika. 109. Hakuna shaka ya kwamba hao ndio waliohasirika. "},{"id":2722,"sura":16,"from_aya":106,"to_aya":108,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{106 - 108} Yeye mukufu anajulisha juu ya hali mbaya ya wale waliomkufuru baada ya kumuamini, kwa hivyo akapofuka baada ya kwamba alikuwa ana uwezi wa kuona, na akarudi katika upotofu baada ya kwamba alikuwa ameongoka, na akakifungulia kifua chake ukafiri, na akauridhia, na akatulia nao, basi wana ghadhabu kubwa kutoka kwa Mola wao Mlezi, Mwingi wa kurehemu, ambaye anapokasirika, hakuna chochote kinachoweza kuizuia ghadhabu yake, na tena kila kitu kinawakasirikia hao. \"Na wao wana adhabu kubwa\" yenye kudumu milele. Na hilo ni kwa kuwa wao \"wameupendelea uhai wa dunia hii kuliko Akhera\" ambapo ya kwamba walirudi nyuma kwa visigino vyao kwa sababu ya tamaa ya kupata kitu katika vitu vya kidunia visivyokuwa na thamani, na kuitaka sana, na kuipa mgongo heri ya Akhera. Na walipochagua ukafiri badala ya imani, Mwenyezi Mungu akawazuia uongofu, kwa hivyo hakuwaongoa. Hili ni kwa sababu ukafiri ndio sifa yao, basi na Mwenyezi Mungu akafunga nyoyo zao, kwa hivyo heri yoyote haiwezi kuingia humo. Na pia akafunga masikio yao na macho yao, kwa hivyo hakipiti humo chochote cha kuwafaidi na kufikia nyoyo zao. Basi wakaenewa na kughafilika, na wakazungukwa na kuangushwa, na wakanyimwa rehema za Mwenyezi Mungu ambazo zimeenea kila kitu. Na hayo ni kwa sababu rehema zake ziliwajia, lakini wakazikataa, na zikaekwa mbele yao, lakini hawakuzikubali."},{"id":2723,"sura":16,"from_aya":109,"to_aya":109,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"\"Hakuna shaka ya kwamba hao ndio waliohasirika.\" Wale waliohasiri nafsi zao, mali zao, na familia zao Siku ya Qiyama, na wakakosa neema ya kudumu na wanapata adhabu chungu. Na hili ni kinyume na yule ambaye alilazimishwa kukufuru ilhali moyo wake umetua juu ya imani na anaitaka sana, basi yeye hana ubaya wowote juu yake wala dhambi, na anaruhusiwa kutamka neno la ukafiri anapolazimishwa kulitamka. Na hilo liliashiria kwamba maneno ya mtu aliyelazimishwa kutoa talaka, au kumtoa mtumwa huru, au kununua, au kuuza, au mikataba mingineyo, basi hayo hayazingatiwi wala hukumu ya kisheria haipatikani katika hali hizo. Kwa sababu ikiwa haadhibiwi juu ya neno la ukafiri ikiwa alilazimishwa, basi mambo mengineyo yanafailia na kustahiki zaidi."},{"id":2724,"sura":16,"from_aya":110,"to_aya":111,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"110. Kisha hakika Mola wako Mlezi, kwa wale waliohama makwao baada ya kuteswa, kisha wakapigania Dini na wakasubiri, bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu. 111. Siku ambayo kila nafsi itakuja ikijitetea, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyotenda, nao hawatadhulumiwa. "},{"id":2725,"sura":16,"from_aya":110,"to_aya":110,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{110} Yaani, kisha \"Mola wako Mlezi\" ambaye aliwalea waja wake wamkusudiaye yeye tu kwa upole wake na wema wake \"ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu;\" kwa wale waliohama katika njia yake, na akayaacha makazi yake, na mali zake akitafuta radhi za Mwenyezi Mungu, na akajaribiwa kwa sababu ya dini yake ili arudi katika ukafiri, lakini akawa imara juu ya imani yake, na akawa na yakini iliyo safi zaidi, kisha akapambana na maadui wa Mwenyezi Mungu ili awaingize  katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa ulimi wake na mkono, na akasubiri juu ya ibada hizi ngumu kwa wengi wa watu. Basi hizi ndizo sababu kubwa zaidi za kupata kwazo kipawa kikubwa na tunu bora zaidi, ambazo ni msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa madhambi, madogo yake na makubwa yake, ambazo zinajumuisha kuondoka kwa kila kitu kinachochukiwa, na pia kupata rehema yake kubwa, ambayo kwayo zilitengenea hali zao, na mambo ya dini yao na dunia yao yakanyooka, basi wana rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Qiyama."},{"id":2726,"sura":16,"from_aya":111,"to_aya":111,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{111} Wakati ambao \"kila nafsi itakuja ikijitetea,\" kila mmoja akisema, 'Nafsi yangu, nafsi yangu', na hatajali chochote isipokuwa nafsi yake. Basi katika siku hiyo mja atahitaji kupata walau uzito wa chembe ya heri. \"Na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyotenda\" ya heri na maovu. \"Nao hawatadhulumiwa\" kwa kuongezewa katika maovu yao, wala kupunguziwa katika mema yao. \"Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.\""},{"id":2727,"sura":16,"from_aya":112,"to_aya":113,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"112. Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji uliokuwa na amani na utulivu, riziki yake ikiufikia kwa wingi kutokea kila mahali. Lakini ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akauvika vazi la njaa na hofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya. 113. Na alikwisha wajia Mjumbe kutoka miongoni mwao. Lakini wakamkadhibisha; basi ikawachukua adhabu hali ya kuwa wamedhulumu. "},{"id":2728,"sura":16,"from_aya":112,"to_aya":113,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{112 - 113} Mji huu ni Makka tukufu, ambayo ilikuwa na amani, na utulivu, ambamo hakuna yeyote aliyefadhaishwa. Na watu wa kipindi cha Jahiliyya walikuwa wakiuheshimu, kiasi kwamba mmoja wao angemkuta mtu aliyemuua baba yake na kaka yake, lakini hangeweza kumfadhaisha pamoja na ukali wa hasira zao na majivuno ya Kiarabu. Kwa hivyo kukawa humo na amani kamili ambayo haikutokea kwa miji mingineyo. Na vile vile kulikuwa na riziki kunjufu. Ulikuwa mji ambapo hakukuwa na mimea wala miti, lakini Mwenyezi Mungu akaurahisishia riziki ambayo ilikuwa akiujia kutokea kila mahali. Kisha wakajiwa na Mtume kutoka miongoni mwao ambaye walijua uaminifu wake na ukweli wake. Akawalingania kwenye mambo kamilifu zaidi, na akawakataza mambo mabaya, lakini wakamkadhibisha na wakakufuru neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yao, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaonjesha kinyume cha walichokuwa ndani yake, na akawavisha \"vazi la njaa\" ambayo ni kinyume cha utele, \"na hofu\" ambayo ni kinyume cha amani. Na hayo ni kwa sababu ya matendo yao, ukafiri wao, na kutoshukuru kwao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu wenyewe."},{"id":2729,"sura":16,"from_aya":114,"to_aya":118,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"114. Basi kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, vilivyo halali na vizuri. Na shukuruni neema za Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu. 115. Hakika amewaharimishia tu nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliyechinjwa kwa ajili isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu. Lakini anayelazimishwa bila ya kuasi, wala kuvuka mipaka, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu. 116. Wala msiseme uongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hiki ni halali, na hiki ni haramu - mkimzulia uongo Mwenyezi Mungu. Hakika wale wanaomzulia uongo Mwenyezi Mungu hawatafaulu. 117. Ni starehe ndogo tu, nao wana adhabu chungu. 118. Na Mayahudi tuliwaharimishia yale tuliyokuhadithia zamani. Na Sisi hatukuwadhulumu, bali walikuwa wakijudhulumu wenyewe. "},{"id":2730,"sura":16,"from_aya":114,"to_aya":114,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{114} Yeye mtukufu anawaamuru waja wake kula vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu miongoni mwa wanyama, nafaka, matunda, na vinginevyo \"vilivyo halali na vizuri.\" Yaani, visiwe miongoni mwa vilivyoharamishwa na Mwenyezi Mungu au vya kunyang'anya na mfano wake. Basi vifurahieni vile alivyowaumbia Mwenyezi Mungu bila ya kupitiliza viwango wala kuvuka mipaka. \"Na shukuruni neema za Mwenyezi Mungu\" kwa kuzikiri kwa moyo, na  kumsifu Mwenyezi Mungu juu yale, na kuzitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu \"ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu.\" Yaani, ikiwa mnamfanyia Yeye peke yake ibada, basi msishukuru isipokuwa Yeye tu, wala msisahau neema zake juu yenu."},{"id":2731,"sura":16,"from_aya":115,"to_aya":115,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{115} \"Amewaharimishia.\" Vitu vinavyoleta madhara vimeharamishwa kwenu, navyo ni kama vile mzoga,hapa ni pamoja na kila kilichokufa kwa njia isiyo ya sahihi kisheria, isipokuwa mzoga wa nzige na samaki ambavyo vimeruhusiwa. \"Na damu\" iliyomwagika, Ama kwa ile inayobaki katika mishipa na nyama, haidhuru. \"Na nyama ya nguruwe\" kwa uchafu wake na ubaya wake, na hii inajumuisha nyama yake, mafuta yake, na sehemu zake zote. \"Na mnyama aliyechinjwa kwa ajili isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu;\" kama vile anayechinja kwa ajili ya masanamu, makaburi na kadhalika, kwa sababu lengo lake ni shirki. \"Lakini anayelazimishwa bila ya kuasi\" kwa kitu chochote kutokana na vilivyoharimishwa; wakati kuna haja halisi na mtu anaogopa kuangamia kama hatakula, basi hana dhambi ikiwa si mwenye uadui na wala si muasi. Yaani, ikiwa hana nia ya kula kitu kilichoharamishwa, na hawezi kupata chakula halali au amezidisha kiasi cha mahitaji ya lazima. Hii ndiyo ambayo ameharamisha Mwenyezi Mungu kati ya mubaah."},{"id":2732,"sura":16,"from_aya":116,"to_aya":116,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{116} \"Wala msiseme uongo,kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hiki ni halali, na hiki ni haramu.\" Yaani, msiharamishe wala msihalalishe kwa matakwa ya nafsi zenu yaliyo uongo na uzushi kwa Mwenyezi Mungu na mkasema yametoka kwake Yeye Mola; \"mkimzulia uongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanaomzulia uongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.\" Siyo duniani na siyo akhera, na hapana budi Mwenyezi Mungu atadhihirisha aibu yao."},{"id":2733,"sura":16,"from_aya":117,"to_aya":117,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{117} Na ikiwa watastarehe katika dunia; nayo ni \"starehe ndogo tu.\" Na marejeo yao ni Motoni, \"nao wana adhabu chungu.\""},{"id":2734,"sura":16,"from_aya":118,"to_aya":118,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{118} Mwenyezi Mungu, Mtukufu, ameharamisha kwetu vitu viovu kama fadhila kwetu na kinga dhidi ya mambo machafu. Kuhusu watu wa Kiyahudi, Mwenyezi Mungu amewaharamishia vitu vizuri ambavyo vilikuwa vimehalalishwa kwao kwa sababu ya dhuluma yao, kama adhabu kwao. Haya yameelezwa katika Surat al-An'am kwa maneno yake Mwenyezi Mungu, \"Na wale waliofuata dini ya kiyahudi tumewaharamishia kila mwenye kucha. Na katika ng'ombe na kondoo na mbuzi tumewaharamishia shahamu yao,isipokuwa ile iliyobeba migongo yao au matumbo yao, au iliyogandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyo kwa sababu ya uasi wao. Na bila ya shaka Sisi ndio wasema kweli.\""},{"id":2735,"sura":16,"from_aya":119,"to_aya":119,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"119. Kisha hakika Mola wako Mlezi kwa wale waliotenda mabaya kwa ujinga, kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mazuri; bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu."},{"id":2736,"sura":16,"from_aya":119,"to_aya":119,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{119} Hili ni himizo kutoka kwake kwa waja wake kutubu na kuwaita wamrudie. Kwa hivyo akajulisha kwamba mwenye kufanya ubaya, \"kwa ujinga\" bila kujua mwisho wa yale ambayo yatamletea, hata ikiwa amekusudia kutenda dhambi, basi ni lazima elimu iliyomo moyoni mwake itapunguka wakati wa kutenda dhambi hiyo. Kwa hivyo, atakapotubu na akatengenea kwa kuacha dhambi hiyo na akaijutia, na akarekebisha matendo yake, basi hakika Mwenyezi Mungu anamsamehe, na kumrehemu, na anakubali toba yake na anamrudisha katika hali yake ya kwanza au hali ya juu zaidi yake."},{"id":2737,"sura":16,"from_aya":120,"to_aya":123,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"120. Hakika Ibrahim alikuwa mfano mwema, mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, mnyoofu kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. 121. Mwenye kuzishukuru neema zake. Yeye alimteua, na akamwongoa kwenye Njia iliyonyooka. 122. Na tukampa mazuri katika dunia, naye hakika Akhera atakuwa miongoni mwa walio wema. 123. Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mnyoofu kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. "},{"id":2738,"sura":16,"from_aya":120,"to_aya":120,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{120} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu yale aliyomfadhilisha kwayo mwandani wake, Ibrahim - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na akampa yeye tu miongoni mwa fadhila za juu na sifa kamilifu. Akasema, \"Hakika Ibrahim alikuwa mfano mwema;\" yaani, imamu aliyekusanya sifa kamili za wema, kiongozi aliyeongoka, \"mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu.\" Yaani, mwenye kumtii Mola wake Mlezi, mwenye kumfanyia yeye tu Dini; \"mnyoofu\" katika kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa upendo, kurudi kwake, na uja, mwenye kumpa mgongo asiyekuwa yeye; \"wala hakuwa miongoni mwa washirikina\" katika kauli zake, na matendo yake, na hali zake zote. Kwa sababu yeye ndiye imamu wa wote wampwekeshao Mwenyezi Mungu, wanyoofu kwake."},{"id":2739,"sura":16,"from_aya":121,"to_aya":121,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{121} \"Mwenye kuzishukuru neema zake;\" yaani, Mwenyezi Mungu alimpa mazuri katika dunia, na akamneemesha kwa neema dhahiri na za ndani, naye alimshukuru juu yake, kwa hivyo matokeo ya sifa hizi nzuri yakawa ni kwamba Mola wake Mlezi, \"alimteua\" na akamfanya yeye tu kuwa mwandani wake, na akamfanya katika walio bora zaidi miongoni mwa viumbe wake, na waja wake wa hali ya juu zaidi walio karibu naye. \"Na akamwongoa kwenye Njia iliyonyooka;\" katika elimu yake na matendo yake, kwa hivyo akaijua haki na akaipendelea juu ya mengineyo."},{"id":2740,"sura":16,"from_aya":122,"to_aya":122,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"\"Na tukampa mazuri katika dunia.\" Riziki pana, mke mzuri, kizazi chema , na tabia ya kuridhisha. \"Naye hakika Akhera atakuwa miongoni mwa walio wema\" ambao wana vyeo vya juu, na ukaribu mkubwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu."},{"id":2741,"sura":16,"from_aya":123,"to_aya":123,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{123} Na kati ya fadhila zake kubwa ni kwamba Mwenyezi Mungu alimfunulia wahyi bwana wa viumbe wote na mkamilifu wao zaidi kwamba afuate mila ya Ibrahim na amuige yeye na umma wake."},{"id":2742,"sura":16,"from_aya":124,"to_aya":124,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"124. Hakika siku ya Sabato (Jumamosi) waliwekewa wale waliohitalifiana kuhusiana nayo. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya Qiyama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana."},{"id":2743,"sura":16,"from_aya":124,"to_aya":124,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{124} Mwenyezi  Mungu Mtukufu anasema, \"Hakika siku ya Sabato (Jumamosi) waliwekewa;\" yaani, walifaradhishiwa \"wale waliohitalifiana kuhusiana nayo,\" wakati walipopotea kuhusiana na siku ya Ijumaa. Na hao walikuwa Mayahudi kwa hivyo, kukawa kuhitilafiana kwao huko ni sababu ya kuwalazimu kuiheshimu na kuitukuza Sabato, vinginevyo ubora wa uhakika ulikuwa ni wa siku ya  Ijumaa, ambayo Mwenyezi Mungu aliuongoa umma huu kuiafiki. \"Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya Qiyama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana,\" ili awabainishie aliye katika haki na aliye katika batili, na anayestahiki kupata thawabu na ayestahiki adhabu."},{"id":2744,"sura":16,"from_aya":125,"to_aya":125,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"125. Lingania kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo nzuri zaidi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi yule aliyeipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi wale walioongoka."},{"id":2745,"sura":16,"from_aya":125,"to_aya":125,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{125} Yaani, na kuwe kulingania kwako viumbe, Mwislamu wao na kafiri wao katika njia ya Mola wako Mlezi, iliyonyooka inayojumuisha elimu yenye manufaa na matendo mema \"kwa hekima.\" Yaani, kila mtu kulingana na hali yake, ufahamu wake , kukubali kwake  na kufuata kwake. Na katika hekima ni kulingania kwa elimu si kwa ujinga, na kuanza na kilicho muhimu zaidi kisha kilicho muhimu zaidi, na kilicho karibu zaidi na akili na ufahamu, kile kinachokubalika zaidi kikamilifu, na kwa upole na ulaini. Kwa hivyo, akifuata kwa sababu ya hekima, basi ni sawa. Vinginevyo, na asonge naye katika kumlingania kwa mawaidha mazuri, nayo ni kuamrisha na kukataza yanayofungamana mawili hayo na kutia moyo na kutishia. Ima kwa kutaja manufaa yaliyomo katika maamrisho na kuyahesabu, na makatazo na madhara yake na kuyahesabu. Au ima kwa kutaja kukirimiwa kwa yule aliyesimamisha dini ya Mwenyezi Mungu, na    kudunishwa kwa yule ambaye hakuisimamisha. Au kwa kutaja yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia watiifu miongoni mwa malipo ya haraka na ya baadaye na yale aliyowaandalia waasi miongoni mwa adhabu ya haraka na ya baadaye. Na kama yule anayelinganiwa anaona kwamba yeye ndiye aliye katika haki, au kwamba analingania kwenye batili, basi huyo atajadiliwa kwa njia iliyo nzuri zaidi. Nazo ni njia ambazo zitachangia zaidi aitikie kiakili na kimaandiko matakatifu. Na katika hayo ni kumuekea hoja kwa ushahidi ule ule aliokuwa akiuitakidi kwani hilo ni karibu zaidi katika kufikia makusudio, na kwamba mjadala huo usizae mzozo au kutukanana utakaopoteza makusudio yake wala haitapatikana faida yake. Bali na yawe makusudio yake ni kuongoza viumbe kwenye haki na siyo kushindana, na mifano yake. Na kauli yake, \"Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi yule aliyeipotea Njia yake.\" Alijua sababu iliyompoteza, na alijua matendo yake yaliyotokana na upotovu wake, na atamlipa kwa hayo. \"Na Yeye ndiye anayewajua zaidi wale walioongoka.\" Alijua kwamba wao wanafailia kuongoka, kwa hivyo akawaongoa, kisha akawaneemesha, kwa hivyo akawachagua."},{"id":2746,"sura":16,"from_aya":126,"to_aya":128,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"126. Na mkilipiza, basi lipizeni sawa na vile mlivyoadhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanaosubiri. 127. Na subiri. Na kusubiri kwako kusiwe isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. Wala usiwahuzunikie, wala usiwe katika dhiki kwa njama wanazozifanya. 128. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na wale watendao mazuri. "},{"id":2747,"sura":16,"from_aya":126,"to_aya":126,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{126} Anasema Yeye Mtukufu akiruhusu kufanya uadilifu na akiitia kufanya kilicho bora zaidi na hisani, \"Na mkimlipiza\" aliyewafanyia ubaya kwa kauli na vitendo, \"basi lipizeni sawa na vile mlivyoadhibiwa,\" bila ya kuongeza chochote juu ya kile mlichofanyiwa.\" Na ikiwa mtasubiri\" mkaacha kuwaadhibu  na mkawasamehe uhalifu wao, \"basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanaosubiri\" kuliko kulipiza kisasi. Na yaliyo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwenu na ya mwisho mzuri zaidi, kama alivyosema yeye Mtukufu, \"Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yako kwa Mwenyezi Mungu.\""},{"id":2748,"sura":16,"from_aya":127,"to_aya":128,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{127 - 128} Kisha akamuamrisha Mtume wake kuwa na subira katika kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu katika hilo na wala asijitegemee nafsi yake. Akasema, \"Na subiri, na subira yako iko kwa Mwenyezi Mungu tu.\" Yeye ndiye anayewanusuru humo na kuwaweka imara. \"Wala usiwahuzunikie\" ukiwaita na hukuwaona wakikubali mwaliko wako; huzuni haikusaidii chochote. \"Wala msiwe katika dhiki.\" Yaani, dhiki na aibu \"kutokana na hila zao\" kwani vitimbi vyao vinawarudia, na wewe ni miongoni mwa wachamungu na wafanyao wema, na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamungu na wafanyao wema, kwa nusura yake, na kufaulu, na uwongofu. Na hao ndio walioogopa ukafiri na dhambi, na wakatenda mema katika kumwabudu Mwenyezi Mungu. Kwamba walimwabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba wanamwona; ikiwa hawamuoni, basi anawaona, na ihsani kwa viumbe ni kwa kuwanufaisha wao kwa kila njia. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie tuwe miongoni mwa watu wema na wafanyao wema."},{"id":2749,"sura":16,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya Surat An-Nahl. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu."},{"id":2750,"sura":16,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}