{"result":[{"id":3052,"sura":19,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Maryam"},{"id":3053,"sura":19,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Nayo iliteremka Madina"},{"id":3054,"sura":19,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":3055,"sura":19,"from_aya":1,"to_aya":6,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Kaf Ha Ya 'Ayn Swad. 2. Huu ni ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya. 3. Alipomwita Mola wake Mlezi kwa siri. 4. Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi, mifupa yangu imedhoofika, na kichwa kinametameta kwa mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe. 5. Na hakika mimi ninawahofia wasimamizi wa baada yangu. Na mke wangu ni tasa. Basi nitunuku mrithi kutoka kwako. 6. Anirithi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Na umjaalie ewe Mola wangu Mlezi awe mwenye kuridhisha. "},{"id":3056,"sura":19,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Yaani, huu \"ni ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya\" ambao tutakusimulia, na kuelezea kwa undani, ambao atajulisha kwa huo hali ya Nabii wake, Zakariya na athari zake njema na sifa zake nzuri. Kwa maana, katika kisa chake kuna mazingatio kwa wale ambao wanazingatia na kiigizo chema kwa wale wanaomfuata, na kwa sababu katika kuelezea kwa kina rehema zake kwa vipenzi wake na ni kwa sababu gani walipata hayo, ni katika yale yanayoitia kwa kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumtaja kwa wingi na kumjua na kujua sababu ya kufikisha kwake. Na hilo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimteua na kumchagua Zakariya, amani iwe juu yake, kwa ajili ya ujumbe wake, na akamteua kwa kumpa ufunuo wake. Basi akatekeleza hilo kama walivyotekeleza mfano wake miongoni mwa mitume, na akawalingania waja kwa Mola wake Mlezi, naye akawafundisha yale ambayo Mwenyezi Mungu alimfundisha, na akawa mshauri mwema kwao katika uhai wake na hata baada ya kifo chake kama ndugu zake miongoni mwa mitume na wale waliowafuata."},{"id":3057,"sura":19,"from_aya":3,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3 - 4} Alipojiona amedhoofika, na akahofu kwamba atakufa, na hakukuwa na yeyote wa kusimama pahali pake katika kuwalingania viumbe kwa Mola wao Mlezi na kuwapa ushauri mwema, akamlalamikia Mola wake Mlezi juu ya udhaifu wake wa dhahiri na uliofichikana, na akamwita mwito uliofichikana ili awe uwe kamili zaidi, na bora zaidi, na wa kumkusudia Mwenyezi Mungu tu kikamilifu. Akasema, \"Mola wangu Mlezi! Hakika mimi, mifupa yangu imedhoofika.\" Na wakati mifupa ambayo ndiyo nguzo ya mwili inapodhoofika, basi viungo vinginevyo vinadhoofika. \"Na kichwa kinametameta kwa mvi\" kwa sababu mvi ni ishara ya udhaifu na uzee, na ni mtume wa kifo, na mtangulizi wake, na mwonyaji wake. Kwa hivyo akamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa udhaifu wake na kutoweza kwake. Na hii ni katika njia zinazopendeza zaidi za kumuomba nazo Mwenyezi Mungu. Kwa sababu njia hii inaonyesha kujiweka mbali na uwezo wako na nguvu zako, na kufungamana kwa moyo na uwezo wa Mwenyezi Mungu na nguvu zake. \"Wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.\" Kwa hivyo, ewe Mola wangu Mlezi hutakuwa ni wa kuniacha niambulie patupu, wala kuniacha bila ya kuniitikia maombi. Bali hujaacha kuwa mwema kwangu, na kuniitikia dua yangu, na wema wako na ihsani yako haijaacha kuendelea kunifikia kwa mfululizo. Na hii ni njia ya kumuomba Mwenyezi Mungu kwa neema zake juu yake, na kuitikia kwake maombi yake ya awali. Kwa hivyo alimwomba yule ambaye hapo awali alikuwa amemfanyia mema kwamba amkamilishie wema wake katika siku zijazo."},{"id":3058,"sura":19,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5}\"Na hakika mimi ninawahofia wasimamizi wa baada yangu,\" juu ya Wana wa Israili baada ya kifo changu kwamba wasijetekeleza dini yako haki ya kuitekeleza, wala kuwalingania waja wako kwako. Na maana yake iliyo dhahiri ni kwamba hakuona miongoni mwao yeyote anayefaa zaidi kuwa kiongozi wao katika Dini. Na ndani ya hili kuna huruma ya Zakariya, amani iwe juu yake, na ushauri wake mzuri, na kwamba ombi lake kupata mwana siyo kama ombi la wengineo ambao makusudio yao ni masilahi ya kidunia tu, lakini yeye makusudio yake ni masilahi ya Dini na kuhofu kwamba inaweza kupotea. Na aliona wasiokuwa yeye kwamba hawafailii kwa hilo, naye nyumba yake ilikuwa miongoni mwa nyumba maarufu katika Dini na ni chimbuko la ujumbe wa Mwenyezi Mungu na yenye uwezekano mkubwa wa kuwa na heri ndani yake. Kwa hivyo akamwomba Mwenyezi Mungu ampe mwana ambaye ataisimamisha Dini baada yake, na akalalamika kwamba mke wake alikuwa tasa, na kwamba yeye mwenyewe alikuwa amefikia umri ambao ni nadra kuwa na matamanio ya kijinsia na kupata mwana. \"Basi nitunuku mrithi kutoka kwako.\""},{"id":3059,"sura":19,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} Na urithi huu ni urithi wa kidini, utume, elimu na matendo, na ndiyo maana akasema, \"Anirithi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Na umjaalie ewe Mola wangu Mlezi awe mwenye kuridhisha.\" Yaani, mja mwema ambaye utamridhia na kumfanya kupendwa waja wako. Na jumla ya hayo ni kwamba alimwomba Mwenyezi Mungu ampe mwana mwema wa kiume ambaye atasalia baada ya kifo chake na awe msimamizi baada yake, na pia awe nabii aliyeridhiwa kwa Mwenyezi Mungu na kwa viumbe vyake. Na huyu ndiye mwana bora zaidi. Na katika rehema za Mwenyezi Mungu kwa mja wake ni kwamba amruzuku mwana mwema aliyekusanya tabia njema na sifa nzuri. Kwa hivyo Mola wake Mlezi akamrehemu na akaitikia dua yake, na akasema:"},{"id":3060,"sura":19,"from_aya":7,"to_aya":11,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"7. (Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake. 8. Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Vipi nitakuwa na mwana na ilhali mke wangu ni tasa, na mimi nimeshafikia ukongwe katika uzee? 9. Akasema: Hivyo ndivyo alivyosema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu. Na hakika Mimi nilikwisha kuumba wewe zamani na wala hukuwa kitu. 10. Akasema: Mola wangu Mlezi nijaalie Ishara. Akasema: Ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa usiku tatu, na ilhali u mzima sawasawa. 11. Basi akawatokea kaumu yake kutoka mihirabuni. Akawaashiria kwamba: Msabihini Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni. "},{"id":3061,"sura":19,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Yaani, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa bishara njema kupitia Malaika kuhusu kuzaliwa kwa Yahya, na Mwenyezi Mungu mwenyewe ndiye aliyempa jina la Yahya, nalo lilikuwa jina lanalolingana na yule aliyeitwa kwalo. Yaani, atakuwa na uhai kwa kihisia, ndiyo iwe neema hivyo imetimia sawasawa. Na kwamba pia ataishi usio kuwa wa kihisia ambao ni uhai wa moyo na roho kwa wahyi, elimu na Dini. \"Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.\" Na pia maana yake inaweza kuwa: Hatukuwahi kumfanya yeyote kuwa mfano wake na sawa naye. Ndiyo hiyo iwe ni bishara njema hukusu ukamilifu wake na kusifika kwake kwa sifa nzuri, na kwamba anawashinda waliokuwa kabla yake. Lakini kulingana na maana hii, ujumla huu lazima atolewe ndani yake Ibrahim, Musa, na Nuhu amani iwe juu yao na mfano wao, miongoni mwa wale ambao ni bora zaidi ya Yahya bila shaka yoyote."},{"id":3062,"sura":19,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} Wakati huo, ilipomjia bishara njema hiyo ya huyu mwana aliyemuomba, alishangaa na kustaajabu, na akasema, \"Ewe Mola wangu Mlezi! Vipi nitakuwa na mwana\" ilhali mimi mwenyewe na hata mke wangu tuna kizuizi cha hilo? Na ni kana kwamba wakati alipokuwa anaomba hakuona kizuizi hiki akilini mwake kwa sababu ya nguvu ya kile kilicho ndani ya moyo wake na pupa yake kubwa juu ya kutaka mwana. Na katika hali hii wakati ilipokubaliwa dua yake, akashangazwa na hilo."},{"id":3063,"sura":19,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} Lakini Mwenyezi Mungu akamjibu kwa kauli yake, \"Hivyo ndivyo alivyosema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu.\" Yaani, jambo hili kawaida linashangaza, lakini katika desturi ya Mwenyezi Mungu na katika viumbe. Lakini uwezo wa Mwenyezi Mungu unaweza kumfanya apatikane bila ya sababu zake. Hilo ni rahisi kwake, na siyo gumu kuliko alivyomuumba yeye Zakariya hapo awali, na hakuwa kitu chochote."},{"id":3064,"sura":19,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} \"Akasema: Mola wangu Mlezi, nijaalie Ishara\" ili moyo wangu utulie kwayo, na hii siyo kwa sababu ya kuwa na shaka katika habari za Mwenyezi Mungu. Lakini ni kama vile kipenzi wa Mwenyezi Mungu (Ibrahim), amani iwe juu yake, alivyosema, \"Mola wangu Mlezi! Nionyeshe vipi unavyofufua wafu. Mwenyezi Mungu akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! Lakini ili moyo wangu utue.\" Kwa hivyo, akawa ameomba elimu zaidi na kufikia jicho la yakini baada ya kujua kwa yakini. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamuitikia ombi lake kama rehema kwake. \"Akasema Ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa usiku tatu, na ilhali u mzima sawasawa.\" Na katika aya nyingine, \"siku tatu, isipokuwa kwa kuashiria tu\" na maana yake ni sawa. Kwa sababu wakati mwingine alisema usiku, na wakati mwingine akasema siku. Na hili ni katika ishara za ajabu. Kwa maana, kumzuia kuzungumza kwa muda wa siku tatu na kutoweza kwake kufanya hivyo bila kuwa bubu wala balaa yoyote, bali alikuwa mzima sawasawa bila ya kuwa na upungufu wowote, ni katika ushahidi wa uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kimiujiza unaoenda kinyume na ada ya kawaida. Na tena pamoja na hayo alikuwa amezuiwa kuzungumza maneno yanayohusiana na wanadamu na kuwaongelesha. Lakini kumtakasa Mwenyezi Mungu [na kusema kuwa hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu] na dhikri na mfano wake, hayo hakuzuiwa kuyafanya. Na ndiyo maana, akasema katika aya nyingine, \"Na mdhukuru Mola wako Mlezi kwa wingi na mtakase jioni na asubuhi.\""},{"id":3065,"sura":19,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} Basi moyo wake ukatulia, na akafurahia kwa bishara njema hii kubwa, na akatekeleza amri ya Mwenyezi Mungu juu yake ya kumshukuru kwa kumuabudu na kumtaja. Basi akakaa katika mihrabu yake, na akatoka humo akawaendea kaumu yake \"akawaashiria kwa kumbukumbu na ishara, \"Akawaashiria kwamba: Msabihini Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni.\" Kwa sababu bishara njema ya kuzaliwa Yahya ina masilahi ya kidini kwao wote."},{"id":3066,"sura":19,"from_aya":12,"to_aya":15,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"12. Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hekima angali mtoto. 13. Na tukampa huruma itokayo kwetu, na utakaso, na akawa mchamungu. 14. Na akawa mwema kwa wazazi wake, wala hakuwa jabari muasi. 15. Na salama iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku ya kufa, na siku ya kufufuliwa. "},{"id":3067,"sura":19,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Maneno yaliyotangulia yaonyesha kuzaliwa kwa Yahya, ujana wake na malezi yake. Alipofikia hali ambapo anayaelewa maneno vizuri, Mwenyezi Mungu alimwamrisha achukue kitabu hicho kwa nguvu. Yaani, kwa kujitahidi katika kuhifadhi maneno yake na kufahamu maana yake na kufanyia kazi maamrisho yake na makatazo yake. Huku ndiko kuchukua kitabu kwa ukamilifu. Kwa hivyo, akatekeleza amri ya Mola wake Mlezi. Akakichukua kitabu hicho na akakihifadhi na kukielewa, na Mwenyezi Mungu akampa werevu na utambuzi mkubwa ambao haukupatikana asiyekuwa yeye. Na ndiyo maana akasema, \"Nasi tulimpa hekima angali mtoto\" [Yaani, kuzijua hukumu za Mwenyezi Mungu na kuhukumu kwazo hali ya kuwa bado angali mdogo]."},{"id":3068,"sura":19,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Na pia tulimpa \"huruma itokayo kwetu\" na upole ambayo kwayo mambo yake yalikuwa mepesi, na hali zake zikatengenea, na vitendo yake vikanyooka sawasawa. \"Na utakaso\" kutokana na balaa na madhambi. Kwa hivyo moyo wake ukasafika na akili yake ikatakasika. Na hayo yanajumuisha kutokuwepo sifa za kulaumiwa, na tabia mabaya, kuongezeka kwa tabia na sifa nzuri. Na ndiyo maana akasema, \"na akawa mchamungu\" kwa kufanya maamrisho na kuacha makatazo."},{"id":3069,"sura":19,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} Na yeyote ambaye ni muumini mchamungu, basi huyo anakuwa kipenzi cha Mwenyezi Mungu, na anakuwa katika wakazi wa Peponi ambayo imeandaliwa wachamungu, na atapata thawabu za kidunia  na akhera ambazo Mwenyezi Mungu huzilipa kwa sababu ya uchamungu. Na pia ilikuwa \"mwema kwa wazazi wake\" wala hakuwa na kuwaasi, wala wa kuwafanyia mabaya. Bali alikuwa mzuri kwao kwa kauli na matendo, \"wala hakuwa jabari muasi \" wa kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, wala kujiinua juu ya waja wa Mwenyezi Mungu wala wazazi wake. Bali alikuwa wa kujirudisha chini, mnyenyekevu, na wa kurudi kwa Mwenyezi Mungu daima. Kwa hivyo alijumuisha kati ya kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za viumbe wake."},{"id":3070,"sura":19,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15} Na ndiyo maana akapata salama kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika hali zake zote: mwanzo wake na mwisho wake. Na ndiyo maana akasema, \"Na salama iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku ya kufa, na siku ya kufufuliwa.\" Na hilo linalazimu kwamba alisalimika kutokana na Shetani, maovu, adhabu katika hali hizi tatu na kile kilicho kati yake, na kwamba yuko salama kutokana na Moto na mahangaiko, na kwamba ni katika wakazi wa nyumba ya salama. Basi rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na baba yake, na Mitume wengine wote, na atufanye katika wafuasi wao. Hakika Yeye ndiye mtoaji kwa wingi, Mkarimu."},{"id":3071,"sura":19,"from_aya":16,"to_aya":21,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"16. Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipojitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki. 17. Na akaweka pazia kujikinga nao. Basi tukamtumia Roho wetu, naye akajifananisha kwake sawa sawa na mtu. 18. (Maryamu) akasema: Hakika mimi ninajikinga kwa Mwingi wa rehema aniepushe nawe, ikiwa wewe ni mchamungu. 19. (Malaika huyo) akasema: Hakika mimi ni mtume tu kutoka kwa Mola wako Mlezi ili nikutunuku mwana aliyetakasika. 20. Akasema: Nitampataje mwana ilhali mtu yeyote hajawahi nigusa, wala sikuwahi kuwa kahaba? 21. (Malaika) akasema: Hivyo ndiyo alivyosema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na rehema kutoka kwetu, na hilo ni jambo lililokwisha hukumiwa. "},{"id":3072,"sura":19,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} Alipotaja kisa cha Zakariya na Yahya, na kikawa katika ishara za ajabu, akahamia katika kilicho cha ajabu zaidi yake, kwa njia ya hatua kwa hatua kutoka hali ya chini zaidi hadi juu zaidi. Akasema, \"Na mtaje katika Kitabu\" kitukufu \"Maryamu\" amani iwe juu yake. Na hili ni katika fadhila zake kuu zaidi, kwamba anatajwa katika kitabu kikuu ambacho Waislamu wanakisoma katika mashariki ya ardhi na magharibi yake. Na anatajwa humo kwa utajo mzuri zaidi na sifa bora zaidi, kama malipo kwa matendo yake bora na juhudi zake kamili. Pindi \"alipojitenga\"  na jamaa zake na kwenda \"mahali upande wa mashariki.\" Yaani, Masharaiki ambapo ni mbali sana nao."},{"id":3073,"sura":19,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} \"Na akaweka pazia kujikinga nao \" ili asalie peke yake kwa ajili ya kumuabudu Mola wake Mlezi katika hali ya unyenyekevu na udhalilifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hilo ni kwa ajili ya kutekeleza kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu. \"Na angalia pale Malaika waliposema: Ewe Maryamu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuteua, na akakutakasa, na akakutukuza kuliko wanawake wa walimwengu wote.\" Ewe Maryamu! Mnyenyekee Mola wako Mlezi na usujudu na uiname pamoja na wainamao.\" Na kauli yake, \"Basi tukamtumia Roho wetu\" naye ni Jibril, amani iwe juu yake, \"naye akajifananisha kwake sawa sawa na mtu.\" Yaani, mwanamume mkamilifu katika sura nzuri na mwonekano mzuri bila ya kuwa na dosari yoyote wala upungufu, kwa sababu hawezi Maryamu kuvumilia kumwona jinsi alivyo."},{"id":3074,"sura":19,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} Basi Maryamu alipomwona katika hali hii, ilhali alikuwa amejitenga mbali na familia yake na watu, huku amejiwekea pazia kutokana na watu wapendwa zaidi kwake, ambao ni familia yake, aliogopa kwamba huenda mwanamume alikuwa ameingia alimokuwa kwa ajili ya kumfanyia ubaya na kumtamani. Kwa hivyo akajikiga kwa Mola wake Mlezi na kujilinda kwake. Akamwambia, \"Hakika mimi ninajikinga kwa Mwingi wa rehema aniepushe nawe.\" Yaani, ninamkimbilia, na ninajihifadhi kwa rehema yake usije nitia ubaya. \"Ikiwa wewe ni mchamungu,\" basi acha kunijia na ubaya. Kwa hivyo alichanganya kati ya kujilinda kwa Mola wake Mlezi na kumuhofisha na kumuogopesha, na kumuamrisha kushikamana na uchamungu. Naye Maryamu alikuwa katika hali hiyo ya kuwa peke yake, na kuwa mbali na watu, naye alikuwa katika hali nzuri kabisa ya kibinadamu iliyokamilika tena iliyo sawasawa, na hakuwa amemuongelesha kwa baya lolote au hata kumtamani. Lakini hiyo ilikuwa tu hofu kutoka kwa Maryamu. Na hii ndiyo hali ya juu zaidi ya kujiweka safi na mbali na machafu, maovu na sababu zake. Na huku kujiweka safi hasa pamoja na kuwepo kwa pamoja kwa sababu za kufanya uchafu na kutokuwepo kizuizi cha kufanya uchafu huo ni katika matendo bora zaidi. Na ndiyo sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimsifu akasema, \"Na Maryamu binti wa Imrani, aliyeulinda ubikira wake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu.\" \"Na mwanamke aliyelinda uke wake, na tukampulizia katika roho yetu, na tukamfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu.\" Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akampa mwana kwa sababu ya kujihifadhi kwake kutokana na machafu ili awe ishara katika ishara za Mwenyezi Mungu na Mtume katika Mitume wake."},{"id":3075,"sura":19,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} Jibrili alipomuona akijiweka mbali na maovu, na akawa ana hofu, akasema, \"Hakika mimi ni mtume tu kutoka kwa Mola wako Mlezi\" na kazi yangu na shughuli yangu ni kufikisha ujumbe wa Mola wangu Mlezi kwako, \"ili nikutunuku mwana aliyetakasika.\" Na hii ni habari njema kubwa sana ya kupata mwana ambaye ametakasika. Kwa maana, utakasifu unalazimu kwamba amesafika kutokana na sifa mbaya na kusifika kwake na sifa nzuri."},{"id":3076,"sura":19,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Kwa hivyo, Maryamu akashangaa juu ya kupata mwana bila ya baba, akasema, \"Nitampataje mwana ilhali mtu yeyote hajawahi nigusa, wala mimi sijawahi kuwa kahaba?\" Na mtoto hapatikani isipokuwa kwa hayo."},{"id":3077,"sura":19,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} \"(Malaika) akasema: Hivyo ndiyo alivyosema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu,\" inayoonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwamba sababu zote haziathiri zenyewe tu, lakini huathiri kwa Mwenyezi Mungu kuzifanya ziathiri. Kwa hivyo Yeye huwaonyesha waja wake ukiukaji wa ada ya kawaida kuhusiana na sababu fulani za kawaida, ili wasisimamie tu kwenye sababu hizo, na wakakosa kumuangalia yule aliyeziweka na anayezisababisha. \"Na\" ili tumfanye kuwa yeye na kuzaliwa kwake\" ni rehema kutoka kwetu\" kwake, na kwa mama yake, na kwa watu. Ama rehema ya Mwenyezi Mungu kwake, ni kule kumteua Mwenyezi Mungu kwa kumpa ufunuo wake, na akamneemesha kwa yale aliyowaneemesha kwayo Mitume wenye stahamala kubwa. Na ama rehema yake kwa mama yake, ni ile fahari aliyopata na sifa nzuri, na manufaa makubwa.  Na ama rehema yake kwa watu, ni kwamba neema yake kubwa juu yao ni kwamba aliwatumia Mtume miongoni mwao anayewasomea Aya zake, na kuwatakasa, na kuwafundisha Kitabu na hekima, ili wamuamini, na wamtii, na wapate furaha ya dunia na akhera. Na kupatikana kwa Isa kwa njia hii \"lilikuwa jambo liliokwisha hukumiwa\" kitambo na halikuwa budi kutokea. Kwa hivyo Jibril, amani iwe juu yake, akapuliza katika nafasi ya kuingilia kichwa kwenye nguo."},{"id":3078,"sura":19,"from_aya":22,"to_aya":26,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"22. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali. 23. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya, na nikawa niliyesahaulika kabisa! 24. Kwa hivyo, akamnadi kutokea chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi ameshajaalia chini yako kijito kidogo cha maji! 25. Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. 26. Basi kula, na kunywa, na litulizie jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote, basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema, ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu yeyote. "},{"id":3079,"sura":19,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} Yaani, alipobeba mimba ya Isa, amani iwe juu yake, akahofu kukashifiwa, kwa hivyo akajitenga na watu pahali pa mbali."},{"id":3080,"sura":19,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} Wakati kuzaa kwake kulipokaribia, uchungu wa kuzaa ukamlazimisha kwenda kwenye shina la mtende. Na wakati uchungu huo wa kuzaa ulipomtia uchungu, pia uchungu wa kuwa peke yake bila ya chakula na kinywaji, na uchungu wa moyo wake kutokana na maneno ya watu, na akahofu kwamba hataweza kuwa na subira, akatamani kwamba angekuwa alikwisha kufa kabla ya tukio hili na akawa amesahaulika kabisa na hakumbukwi na yeyote. Na kutamani huku kulitokana na jambo hilo la kusumbua, lakini hakukuwa na heri yoyote wala masilahi katika kutamani kwake huku, bali heri yote na masilahi yalikuwa katika yale yaliyotokea hasa."},{"id":3081,"sura":19,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} Kisha Malaika akamtuliza hofu yake, na wasiwasi wake ukatulia, na akamwita kutokea chini yake. Na labda likuwa kutokea mahali palipo chini zaidi yake na akamwambia: Usihuzunike wala usiwe na wasiwasi kwa maana, \"Hakika Mola wako Mlezi ameshajaalia chini yako kijito kidogo cha maji\" ili unywe kutoka humo."},{"id":3082,"sura":19,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} \"Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu\" zenye manufaa."},{"id":3083,"sura":19,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} \"Basi kula\" tende, \"na kunywa\" kutoka mtoni, \"na litulize jicho lako\" kwa Issa. Na huu ndio utulivu wake katika suala la kuwa salama kutokana na uchungu wa kuzaa na kupata chakula na vinywaji vizuri. Na ama katika suala la maneno ya watu, akamuamrisha kwamba akimuona mtu yeyote, basi na aseme kwa ishara, \"Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema, ya kufunga.\" Yaani, kunyamaza, \"kwa hivyo leo sitosema na mtu yeyote\" haya ni ili asjipumzishe kutokana na maneno yao. Na siku hizo ilikuwa inajulikana kwao kwamba kunyamaza ni katika ibada za kisheria. Na hakuamrishwa kuwaongelesha katika suala hili na kujiondolea lawama, kwa sababu watu hawangemwamini, na tena hakuna faida yoyote katika kufanya hivyo, na ili kuwe kuondolewa kwake hatiani ni kupitia maneno ya Isa katika mlezi ni ushahidi mkubwa zaidi juu ya kutokuwa kwake na hatia. Na maana, mwanamke kuzaa mtoto bila mume na kudai kwamba hakutokana na mwanamume yeyote ni katika madai makubwa zaidi ambayo hata kama wataletwa mashahidi kadhaa, basi hangesadikiwa kwa hilo. Kwa hivyo ushahidi wa jambo hili lisilo la kawaida ukafanywa kutoka na jambo la aina yake, ambalo ni kuongea kwa Isa katika hali ya uchanga sana wake. Na ndiyo maana yeye Mtukufu akasema:"},{"id":3084,"sura":19,"from_aya":27,"to_aya":33,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"27. Basi akaenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu sana! 28. Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu mbaya, wala mama yako hakuwa kahaba. 29. Kwa hivyo, akamuashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeshe aliye bado mtoto mdogo yumo katika mlezi? 30. (Mtoto huyo) akasema: Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. 31. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Swala na Zaka maadamu ni hai. 32. Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. 33. Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayokufa, na siku nitakayofufuliwa kuwa hai. "},{"id":3085,"sura":19,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} Yaani, Maryamu alipokamilisha damu ya baada ya kuzaa, akaja na Isa kwa kaumu yake huku amembeba. Na hilo ni kwa sababu alijua kwamba yeye mwenyewe hana hatia, na kwamba yu safi. Basi akaja bila kujali na bila ya wasiwasi wowote. Wakasema, \u201cHakika umeleta kitu cha ajabu sana.\u201d Nao walimaanisha ukahaba kwa hilo - na Mwenyezi amuepushe na hilo."},{"id":3086,"sura":19,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Inaonekana dhahiri katika kuali yake, \"Ewe dada yake Harun\" kwamba Harun huyu ni kaka yake Maryamu wa kweli, na ndiyo maana wakamnasibisha Maryamu naye. [Nao walikuwa wakiitana kwa majina ya Manabii, na huyu si Harun bin Imran, kakaye Musa, kwa sababu kuna vizazi vingi sana kati yao]. \"Baba yako hakuwa mtu mbaya, wala mama yako hakuwa kahaba.\" Walikuwa watu wema waliosalimika na maovu, na hasa uovu huu ambao wanauashiria hapa. Nao wanamaanisha kwamba: Vipi umesifika na yale ambayo hawakusifika nayo wao, na ukafanya kitu ambacho hawakuwahi kukifanya? Na hilo ni kwa sababu kizazi mara nyingi wanatokana wao kwa wao kuhusiana na kutengenea na kinyume chake. Kwa hivyo wakastaajabu sana kulingana na yale yaliyothibiti katika nyoyo zao. Vipi akafanya hilo?"},{"id":3087,"sura":19,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} \"Kwa hivyo, akamuashiria (mtoto)\" ili wamuongeleshe. Na aliashiria hivyo kwa sababu aliamrishwa kwamba watu wakizungumza naye, aseme, \"Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema, ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu yeyote.\" Basi alipowaashiria kwamba wazungumze naye, wakastaajabishwa na hilo, na wakasema, \"Vipi tumsemeshe aliye bado mtoto mdogo yumo katika mlezi?\" Kwa sababu hilo si jambo la kawaida wala haikutokea kwa mtu yeyote katika umri huo."},{"id":3088,"sura":19,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Kisha Isa, amani iwe juu yake, akasema hali ya kuwa ni mtoto mdogo yuko katika mlezi, \"Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii.\" Kwa hivyo, akawaongelesha kujihusu kwamba ni mja, na kwamba hana sifa yoyote anayostahiki kwayo kuwa mungu au mwana wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ametukuka juu ya maneno ya Manaswara waliomhalifu Isa katika kauli yake, \"Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu\" pamoja na kwamba wanadai kwamba wanamfuata. \"Amenipa Kitabu;\" yaani, alikwisha pitisha kwamba atanipa Kitabu. \"Na amenifanya Nabii\" basi akajulisha kwamba yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu alimfundisha Kitabu na akamfanya miongoni mwa manabii wake. Zote hizi ni miongoni mwa sifa za ukamilifu ambazo Isa mwenyewe alikuwa nazo."},{"id":3089,"sura":19,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} Kisha akataja kukamilisha kwake wengine, akasema, \"Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo,\" na katika wakati wowote niwapo. Mwenyezi Mungu amejalia baraka ndani yangu kama vile kufundisha watu mema, kulingania kwake, kukataza maovu, na kulingania kwa Mwenyezi Mungu kwa maneno na vitendo vyake. Kwa hivyo, kila mwenye kujumuika naye, anapata baraka zake na anapata furaha kutoka kwake maadamu yu pamoja naye.  \"Na ameniusia Swala na Zaka maadamu ni hai.\" Yaani, ameniusia nitekeleze haki zake, ambazo kubwa zaidi zake ni kuswali, na haki za waja wake, ambazo tukufu zake zaidi ni zaka muda wa uhai wangu. Basi ninafuata wasia wa Mola wangu Mlezi kwa kuufanyia kazi, na kuutekeleza."},{"id":3090,"sura":19,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} Pia aliniusia nimtendee wema mama yangu, kwa kumfanyia ihsani kubwa zaidi, na nimfanyie yale anayofaa kufanyiwa. Kwa sababu ya heshima yake na fadhila zake, na kwa sababu yeye ni mama mzazi mwenye haki ya kuzaa na mengineyo yanayofungamana na haki hiyo. \"Wala hakunifanya niwe jeuri\" mwenye kutakabari mbele ya Mwenyezi Mungu, mwenye kuwadharau waja wake, \"muovu\" katika dunia yangu na vile vile Akhera yangu. Bali amenifanya niwe mtiifu kwake, mwenye kujiweka chini sana mbele yake, mwenye kumnyenyekea, mwenye kujidhalilisha na mnyenyekevu kwa waja wa Mwenyezi Mungu, niwe mzuri katika dunia na Akhera, mimi na atakayenifuata."},{"id":3091,"sura":19,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} Na alipofikia ukamilifu na sifa nzuri, akasema, \"Na amani iwe juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayokufa, na siku nitakayofufuliwa kuwa hai.\" Yaani, na kwa fadhila za Mola wangu Mlezi na ukarimu wake nilipata amani siku ya kuzaliwa kwangu, na siku ya kufa kwangu, na siku ya kufufuliwa kwangu kutokana na uovu na Shetani na adhabu. Na hili linalazimu usalama wake kutokana na mahangaiko na nyumba ya waovu, na kwamba yeye ni katika wakazi wa nyumba ya amani. Basi huu ni muujiza mkubwa na uthibitisho mkubwa kwamba hakika yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mja wake."},{"id":3092,"sura":19,"from_aya":34,"to_aya":36,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"34. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka. 35. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kujifanyia mwana, Subhanahu (Yeye ametakasika)! Anapolihukumia jambo, basi hakika huliambia tu: Kuwa! Na linakuwa. 36. Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo Njia iliyonyooka. "},{"id":3093,"sura":19,"from_aya":34,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34-35} Yaani, huyo ni yule aliyesifiwa kwa sifa hizo, Isa mwana wa Maryamu, bila ya shaka wala kusitasita kokote, bali \"ndiyo kauli ya haki\" na neno la Mwenyezi Mungu, ambaye hakuna neno ambalo ni la ukweli zaidi yake wala mazungumzo mazuri zaidi yake. Kwa hivyo, hii ndiyo habari ya yakini kuhusu Isa, amani iwe juu yake, na yote yaliyosemwa juu yake ambayo yanapingana na haya, hayo kwa hakika ni batili, na kiwango chake cha mwisho zaidi ni kwamba aliyeyasema ana shaka nayo na wala hana elimu yoyote kuhusiana nayo. Na ndiyo maana akasema, \"ambayo wanaifanyia shaka.\" Yaani, wanatia shaka na kusitasita, na wanabishana kwa kukisia tu. Na miongoni mwao kuna anayesema juu yake kuwa: Yeye ni Mungu, au mwana wa Mungu, au wa tatu katika watatu, lakini Mwenyezi Mungu ametukuka juu ya uzushi wao huo na kusema kwao uwongo huko. Basi \"Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kujifanyia mwana.\" Yaani, haifai wala haiendani naye. Kwa sababu hili ni katika mambo yasiyowezekana, kwa maana Yeye ndiye Mkwasi, Msifika, mmiliki wa wamilikiwa wote. Basi vipi anaweza kujichukulia mwana kutoka kwa wamilikiwa wake? \"Ametakasika\"; Yaani: Ametakasika kutokana na mtoto na upungufu, \"anapohukumia jambo\" miongoni mwa mambo madogo na makubwa, basi haliwezi kukataa wala kumuwia gumu. \"Yeye huliambia tu: Kuwa, na linakuwa.\" Basi ikiwa majaliwa yake na mapenzi yake yatatekelezeka katika ulimwengu wa juu na wa chini, basi vipi anaweza kuwa na mwana? Na ikiwa anapotaka kitu, anakiambia tu: Kuwa, na linakuwa, basi inawezaje kufikiriwa kwamba hawezi kumuumba Isa bila baba?"},{"id":3094,"sura":19,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36} Na ndiyo maana Isa mwenyewe akajulisha kuwa yeye ni mja tu anayelelewa kama waja wengine, akasema, \"Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi.\" Yeye ndiye aliyetuumba na akatutia sura, na akatekeleza uendeshaji wake kwetu, na alituelekeza kulingana na majaliwa yake. \"Basi mwabuduni Yeye\" kwa ikhlasi na jitahidini katika kurudi kwake. Na katika hili kuna kukiri upweke wa Mwenyezi Mungu katika umola na upweke wake katika uungu, na kutumia upweke wake katika umola kuwa ndiyo ushahidi wa upweke wake katika uungu. Na ndiyo maana akasema, \"Hii ndiyo njia iliyonyooka\" ya wastani inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hiyo ndiyo njia ya Mitume na wafuasi wao. Na isiyokuwa hii, basi hiyo ni miongoni mwa njia za ukengeufu na upotovu."},{"id":3095,"sura":19,"from_aya":37,"to_aya":38,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"37. Lakini makundi yakahitilafiana wao kwa wao. Basi ole wao hao waliokufuru kwa kuhudhuria Siku iliyo kuu! 38. Watasikia na wataona vizuri vilivyoje Siku watakayotujia! Lakini madhalimu sasa wamo katika upotovu ulio dhahiri. "},{"id":3096,"sura":19,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoeleza hali ya Isa mwana wa Maryamu, isiyo na shaka yoyote, wala kusitasita, akajulisha kwamba makundi yaliyopotoka miongoni mwa Mayahudi na Manaswara, na wengineo, bila kujali tabaka zao, yalitofautiana kuhusiana na Isa, amani iwe juu yake. Basi kuna aliyepindukia mipaka kuhusiana naye, na aliyemdunisha zaidi. Miongoni mwao kuna waliosema kuwa yeye ni Mwenyezi Mungu! Na kuna wale waliosema miongoni mwao kuwa yeye ni mwana wa Mwenyezi Mungu! Na miongoni mwao kuna waliosema kuwa yeye ni wa tatu kati ya watatu! Na miongoni mwao kuna wale ambao hawakumfanya kuwa mtume, bali walimzulia kwamba yeye ni mwana wa kahaba, kama vile Wayahudi! Na kauli zote za watu hawa ni batili, na rai zao ni mbovu, zimejengeka juu ya shaka, ukaidi, ushahidi mbovu, na tuhuma zisizo na uhakika wowote. Na watu wote hawa wanastahiki ahadi ya adhabu kali. Na ndiyo maana akasema, \"Basi ole wao hao waliokufuru\" Mwenyezi Mungu na Mitume wake na Vitabu vyake, kama vile Mayahudi na Manaswara wanaosemma kauli ya ukafiri kuhusiana na Isa, \"kwa kuhudhuria Siku iliyo kuu!\" Yaani, siku ya Qiyama, ambayo wataishuhudia wa kwanza na wa mwisho, wakazi wa mbinguni na wakazi wa ardhini, Muumba na viumbe, ambayo imejaa mitetemeko na hofu kubwa, yenye malipo juu ya matendo. Na wakati huo yatabainika yale waliyokuwa wakiyaficha na waliyokuwa wakiyadhihirisha."},{"id":3097,"sura":19,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} \"Watasikia na wataona vizuri vilivyoje Siku watakayotujia!\" Kisha watakiri ukafiri wao na ushirikina wao na maneno yao, na watasema, \"Mola wetu Mlezi! Tumeshaona, na tumeshasikia. Basi turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa.\" Kwa hivyo, Siku ya Qiyama ndiyo watakuwa na yakini juu ya uhakika wa hali zao. \"Lakini madhalimu sasa wamo katika upotovu ulio dhahiri\" wala hawana udhuru wowote wa upotovu huu. Kwa sababu wako baina ya mtu mkaidi ambaye alipotea baada ya kufahamu vyema na akaijua haki lakini akaikataa, na kati ya yule aliyepotea njia ya haki, na tena anaweza kuijua haki na usahihi, lakini ameridhika na upotovu wake na matendo yake mabaya, hafanyi bidii ya kujua haki kutokana na batili. Na tazama jinsi alivyosema, \"basi ole wao hao waliokufuru;\" baada ya kauli yake, \"Lakini makundi yakahitalifiana wao kwa wao.\" Wala hakusema, 'basi ole wao!' ili maneno hayo yayarudie makundi hayo yote. Kwa sababu miongoni mwa makundi hayo yaliyohitilafiana, kuna kundi [lililofuata usahihi] na likaafikiana na haki, na likasema kuhusiana na Isa kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa hivyo wakamuamini na kumfuata. Basi hawa ni waumini na hawaingii katika ahadi hii ya adhabu. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawaahidi makafiri tu ahadi hii ya adhabu."},{"id":3098,"sura":19,"from_aya":39,"to_aya":40,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"39. Na waonye siku ya majuto makubwa itapokatwa amri. Nao wamo katika ghafla, wala hawaamini. 40. Hakika Sisi ndio tutairithi ardhi na wale walio juu yake. Na kwetu watarejeshwa. "},{"id":3099,"sura":19,"from_aya":39,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39 - 40} Kuonya ni kujulisha kuhusiana na lenye kuhofisha na kujulisha kuhusu sifa zake kwa njia ya kutishia. Na jambo linalostahiki zaidi kuwaonya kwalo waja na kuwatisha ni siku ya majuto makubwa wakati amri itakapokatwa. Hapo watakusanywa wa mwanzo na wa mwisho katika mahali pamoja, na waulizwe juu ya matendo yao. Kwa hivyo, yule aliyemuamini Mwenyezi Mungu na akawafuata Mitume wake, atafurahia furaha ambayo hatateseka baada yake. Na ama yule ambaye hakumuamini Mwenyezi Mungu na akawafuata Mitume wake, atapata mateso ambayo hatawahi kufurahia baada yake, na atahasiri nafsi yake na familia yake. Basi hapo atajuta majuto makubwa ambayo mioyo inakatikakatika kwa sababu yake, na vifua vinavunjikavunjika kwa sababu yake. Na ni majuto gani makubwa zaidi kuliko kupoteza ridha ya Mwenyezi Mungu na Pepo yake, na kustahiki hasira zake na Moto kwa njia ambayo hawezi akarudi na akaendelea kufanya matendo, na wala hana njia yoyote ya kubadilisha hali yake kwa kurudi duniani? Basi haya ndiyo yako mbele yao, na ilhali wao katika dunia hii bado wameghafilika na jambo hili kubwa. Hata halipiti akilini mwao, kama lingepita, basi ingekuwa tu kwa njia ya kughafilika na kugubika na kuenewa na ulevi. Basi hawamwamini Mwenyezi Mungu, wala hawawafuati Mitume wake, na dunia yao imewasahaulisha, na matamanio yao ya kuisha na kukatika yakazuia kati yao na imani. Kwa maana, dunia na vyote vilivyomo kuanzia mwanzo wake hadi mwisho wake vitawaacha watu wake nao wataondoka humo, na Mwenyezi Mungu atairithi ardhi na vilivyomo ndani yake, na atawarejesha kwake, na atawalipa yale waliyoyafanya humo, kwa kile walichohasiri au kufaidi ndani yake. Kwa hivyo, mwenye kutenda mema, basi na amsifu Mwenyezi Mungu. Na atakayepata yasiyokuwa hayo, basi na asilaumu isipokuwa yeye mwenyewe."},{"id":3100,"sura":19,"from_aya":41,"to_aya":50,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"41 Na mtaje katika Kitabu Ibrahim. Hakika yeye alikuwa mkweli mno, na Nabii. 42. Alipomwambia baba yake: Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyosikia, na visivyoona, na visivyokufaa chochote? 43. Ewe baba yangu! Kwa yakini imenifikia elimu ambayo haikukujia wewe. Basi nifuate mimi, nami nitakuongoza Njia iliyo sawa. 44. Ewe baba yangu! Usimuabudu Shetani. Hakika Shetani ni mwenye kumuasi sana Mwingi wa rehema. 45. Ewe baba yangu! Hakika mimi ninahofu ije kupata adhabu inayotoka kwa Mwingi wa Rehema, ukaja kuwa mwenziwe Shetani. 46. (Baba) akasema: Je huitaki miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi, basi lazima nitakupiga mawe. Na niondokee mbali kwa muda! 47. (Ibrahim) akasema: Salamun 'alaika (Amani iwe juu yako)! Mimi nitakuombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ananihurumia sana. 48. Nami ninajitenga mbali nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na ninamwomba Mola wangu Mlezi; asaa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi. 49. Basi alipojitenga mbali nao na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tukamtunuku Is-haq na Yaaqub, na kila mmoja wao tukamfanya Nabii. 50. Na tukawatunuku katika rehema zetu na tukawajaalia kupewa sifa za kweli tukufu. "},{"id":3101,"sura":19,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0622\u064a\u0627\u062a","text":"Kitabu kikubwa, bora na cha juu kabisa ni kitabu hiki kilicho wazi na ukumbusho wa hekima. Ikiwa habari imetajwa ndani yake; ilikuwa ni habari ya kweli, yenye kustahiki zaidi, na yenye manufaa zaidi, hata kama amri na makatazo yalitajwa ndani yake. Ilikuwa ni amri na makatazo yenye rehema zaidi, ya haki, na ya haki, hata kama malipo, ahadi na tishio vilitajwa ndani yake. Ilikuwa ni haki kabisa, yenye kustahiki zaidi, na yenye dalili nyingi zaidi ya hekima. Aliwanyanyua hadhi na hadhi yao ya juu kwa sababu ya yale waliyoyafanya ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kumpenda, kurejea kwake, kutekeleza haki zake na haki za waja wake, kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kuwa na subira katika hayo, na vituo vilivyotukuka na vituo vya juu. Kwa hiyo Mungu alitaja katika surah hii kundi la manabii; Mwenyezi Mungu anamwamrisha Mtume wake kuwataja; Kwa sababu kuwataja kunamsifu Mwenyezi Mungu na wao, na kunawafafanulia fadhila zake na wema wake, na kuna kutia moyo kuwaamini, kuwapenda, na kuwaiga, hivyo akasema:"},{"id":3102,"sura":19,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41}\"Na mtaje katika Kitabu Ibrahim. Hakika yeye alikuwa mkweli mno na Nabii.\" Mwenyezi Mungu alimkusanyia ukweli na utume. Na alikuwa mkweli katika maneno yake, matendo yake, na hali zake, na anasadikisha kila alichoamrishwa kusadiki, na hilo linalazimu kwamba alikuwa na elimu kubwa yenye kuufikia moyo wake, yenye kuuathiri, yenye kuufanya kuwa na yakini, na kutenda matendo mema kamili. Na Ibrahim, amani iwe juu yake, ndiye mbora zaidi wa Mitume wote baada ya Muhammad \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie \u2013 na yeye ndiye baba wa tatu wa madhehebu bora, na ndiye ambaye Mwenyezi Mungu aliipa dhuria yake unabii na Kitabu. Naye ndiye aliyewalingania viumbe kwa Mwenyezi Mungu, na akavumilia mateso makubwa aliyopitiwa. Akawalingania walio karibu na walio mbali, na akafanya bidii katika kumlingania baba yake kiasi alivyoweza."},{"id":3103,"sura":19,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} Na Mwenyezi Mungu alitaja namna alivyokuwa anamrai, akasema, \"Alipomwambia baba yake\" akimwonyesha ubaya wa kuabudu masanamu: \"Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyosikia, na visivyoona, na visivyokufaa chochote?\" Yaani, kwa nini unaabudu masanamu ambayo yana upungufu wao wenyewe na hata katika matendo yao. Hawasikii, hawaoni, na hawana uwezo wa kumnufaisha mwenye kuwaabudu wala kumdhuru. Bali wao wenyewe hawajimilikii manufaa yoyote, wala hawawezi kuzuia chochote? Huu ni uthibitisho wa wazi unaoonyesha kwamba kuabudu kilicho kipungufu chenyewe na ni kipungufu pia katika vitendo vyake ni jambo baya katika akili na sheria. Na maonyo yake Ibrahim na ishara yake vikaonyesha kuwa anayepaswa kuabudiwa na ambaye ni vizuri kumfanyia hivyo ni yule ambaye ana ukamilifu. Ambaye hakuna neema yoyote inayowafikia waja isipokuwa kutoka kwake, wala hakuna anayewazuilia adhabu isipokuwa Yeye tu. Naye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu."},{"id":3104,"sura":19,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} \"Ewe baba yangu, kwa yakini imenifikia elimu ambayo haikukujia wewe.\" Yaani, ewe baba yangu, usinidharau na kusema: Mimi ni mwanao, nawe unacho kitu nisichokuwa nacho. Bali Mwenyezi Mungu amenipa elimu ambayo hakukupa wewe. Maana ya hilo ni kauli yake, \"Basi nifuate mimi, nami nitakuongoza njia sawa.\" Yaani, njia iliyonyooka, ya wastani. Ambayo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya mshirika yeyote, na kumtii yeye katika kila hali. Na katika maneno yake haya kuna kumuongelesha baba yake kwa njia nzuri ya upole na ulaini ambako hakufichiki. Kwa maana hakusema, 'Ewe baba yangu, mimi nina elimu ilhali wewe ni mjinga;' au 'Wewe huna elimu yoyote.' Bali alitumia njia yenye [kulazimu] kwamba mimi nina elimu na wewe pia una elimu, na ya kwamba elimu iliyonifikia haikukufikia wewe wala haikukujia. Kwa hivyo, unapaswa kufuata hoja na kujisalimisha kwayo."},{"id":3105,"sura":19,"from_aya":44,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{44} \"Ewe baba yangu, usimwabudu Shetani.\" Kwa sababu anayeabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi hakika amemuabudu Shetani, kama Yeye Mtukufu alivyosema, \"Je, Sikuchukua ahadi yenu, enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu?\" \"Hakika Shetani ni mwenye kumuasi sana Mwingi wa rehema.\" Kwa hivyo, mwenye kufuata nyayo zake, basi hakika atakuwa amemchukua kama kipenzi, na atakuwa amemuasi Mwenyezi Mungu kama Shetani. Na kufungamanisha uasi na jina la Mwingi wa rehema kunaashiria kwamba maasia humzuilia mja na rehema ya Mwenyezi Mungu na kumfungia milango yake. Kama vile utiifu pia ndiyo sababu kubwa zaidi ya kupata rehema zake."},{"id":3106,"sura":19,"from_aya":45,"to_aya":45,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"Ndiyo maana akasema, \"Ewe baba yangu! Hakika mimi ninahofu ije kupata adhabu inayotoka kwa Mwingi wa Rehema.\" Yaani, kwa sababu ya kuendelea kwako kuwa kafiri, na kuendelea kwako kuvuka mipaka; \"ukaja kuwa mwenziwe Shetani\" katika Dunia na Akhera, na ukawa katika daraja zake mbaya, na ukala katika malisho yake maovu. Kwa hivyo, Al-Khalil, amani iwe juu yake, akaenda hatua kwa hatua katika kumlingania baba yake kwa njia nyepesi zaidi kisha nyepesi zaidi. Alimjulisha kuhusu elimu yake, na kwamba hilo linalazimu unifuate mimi, na kwamba ukinitii, nitakuongoza kwenye njia iliyonyooka. Kisha akamkataza kumuabudu Shetani, na akamjulisha madhara yaliyo katika hilo. Kisha akamtahadharisha na adhabu na mateso ya Mwenyezi Mungu kama ataendelea na hali yake hiyo, na kwamba atakuwa kipenzi wa Shetani."},{"id":3107,"sura":19,"from_aya":46,"to_aya":46,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{46} Lakini kulingania huku hakukumuingia muovu huyu, na akajibu kwa jibu la mtu mjinga, akasema, \"Unaichukia miungu yangu, ewe Ibrahim?\" Basi akajigamba kwa miungu yake hiyo ambayo imetengenezwa kwa mawe, na masanamu, na akamlaumu Ibrahim kwa kutoitaka miungu yake hiyo. Na huu ni ujinga uliokithiri zaidi na ukafiri mbaya mno, kwa kujisifu na suala la kuabudu masanamu na kulingania yaabudiwe. \"Kama huachi\" kushutumu miungu yangu na kunilingania kumwabudu Mwenyezi Mungu. \"Basi lazima nitakupiga mawe\" ufe \"na niondokee mbali kwa muda!\" Yaani usizungumze nami kwa muda mrefu."},{"id":3108,"sura":19,"from_aya":47,"to_aya":47,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{47} Basi Al-Khalil akamjibu kwa jawabu la waja wa Mwingi wa rehema wakati wanapozungumzishwa na wajinga, na wala hakumtukana. Bali alisubiri na hakumkabili baba yake kwa yale anayoyachukia. Akasema, \"Amani iwe juu yako.\" Yaani, utakuwa salama kutokana na mimi kukutusi na kufanyia unayoyachukia. \"Mimi nitakuombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ananihurumia sana.\" Sitaacha kukuombea uwongofu na msamaha kwa Mwenyezi Mungu ili akuongoe uingie katika Uislamu, ambao kwa huo ndio msamaha unapatikana. Kwa maana Yeye ni mwenye huruma kubwa kwangu na ananijali sana. Basi akaendelea kumuombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu, akitumaini kwamba Mwenyezi Mungu atamuongoa. Na pindi ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, na kwamba hamfaidishi na chochote, akaacha kumuombea msamaha na akajieka mbali naye. Na Mwenyezi Mungu alituamrisha tufuate mila ya Ibrahim. Kwa hivyo, katika kufuata mila yake ni kufuata njia yake katika kulingania kwa Mwenyezi Mungu kwa njia ya elimu, hekima, upole, wepesi, na kutoka katika daraja moja hadi daraja lingine, na kuwa na subira kwa hayo, na kutochoka nayo, na kuyavumilia madhara ambayo mlinganizi anapata kutoka kwa viumbe kwa njia ya maneno na vitendo, na kukabiliana na hayo kwa msamaha na kuachilia mbali, na hata kufanya wema kwa maneno na vitendo."},{"id":3109,"sura":19,"from_aya":48,"to_aya":48,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{48} Alipokata tamaa na kaumu yake na baba yake, akasema, \"Nami ninajitenga mbali nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na ninamwomba Mola wangu Mlezi.\" Na hili linajumuisha dua ya kiibada na dua ya kuomba kitu, \"asaa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi.\" Yaani, huenda Mwenyezi Mungu atanifurahisha kwa kuitikia maombi yangu na kukubali matendo yangu. Na huu ndio wajibu wa yule aliyekata tamaa katika wale anaowalingania - nao wakafuata matamanio yao, na mawaidha yasiwaingie kitu. Kwa hivyo, wakaendelea kutangatanga kiupofu katika kuvuka kwao mipaka - kwamba ajishughulishe na kujitengeneza yeye mwenyewe, na ataraji kwamba Mola wake Mlezi atamkubalia, na ajiweke mbali na maovu na watu wake."},{"id":3110,"sura":19,"from_aya":49,"to_aya":49,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{49} Na kwa kuwa mtu kujitenga mji wake, na yale aliyoyazoea, na familia yake, na kaumu yake ni katika mambo magumu sana kwa nafsi yake kwa sababu ya mambo mengi yanayojulikana, ikiwa ni pamoja na kutengwa na wale ambao humtia nguvu na kuzidi idadi kwa hao, na ikawa kwamba mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humlipa kilicho bora zaidi ya hicho, naye Ibrahimu alijitenga na watu wake, basi Mwenyezi Mungu akasema kumhusu, \"Basi alipojitenga mbali nao na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tukamtunuku Is-haq na Yaaqub, na kila mmoja wao.\" Yaani, Is-haq na Yaaqub \"tukamfanya Nabii.\" Basi Ibrahim akapata heri, yeye na watu wema hawa waliotumwa kwa watu, ambao Mwenyezi Mungu aliwateua kwa wahyi wake, na akawachagua kwa ajili ya ujumbe wake, na akawateua miongoni mwa walimwengu."},{"id":3111,"sura":19,"from_aya":50,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{50} \"Na tukawatunuku\" Ibrahim na wanawe wawili, Is-haq na Yaaqub \"katika rehema zetu.\" Na hili linajumuisha rehema zote alizowatunuku Mwenyezi Mungu, kama vile elimu yenye manufaa, na matendo mema, na dhuria wengi walioenea, ambao Manabii na watu wengi miongoni mwao walikuwa wengi. \"Na tukawajaalia kupewa sifa za kweli tukufu.\" Na hii pia ni katika rehema aliyowatunuku. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alimuahidi kila mtenda mazuri kwamba atamuenezea sifa za kweli kulingana na uzuri wake. Na hawa ni miongoni mwa maimamu wa wafanyao mazuri, basi Mwenyezi Mungu akawaenezea sifa ya kweli, isiyo ya uongo, tukufu na isiyofichika. Kwani utajo wao ulijaa ulimwenguni, na nyoyo zilijaa kwa sifa zao na mapenzi kwao, na ndimi zikajaa kwazo, kwa hivyo akawa kiigizo kwa waigaji na maimamu kwa walioongoka, na utajo wao haujaacha kurudiwa mara kwa mara katika zama zote. Na hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa."},{"id":3112,"sura":19,"from_aya":51,"to_aya":53,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"51. Na mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii. 52. Na tulimwita upande wa kulia wa mlima na tukamsogeza kunong'ona naye. 53. Nasi kwa rehema zetu tukamtunuku kakaye, Harun, awe Nabii. "},{"id":3113,"sura":19,"from_aya":51,"to_aya":51,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{51} Yaani, mtaje katika Qur-ani hii tukufu Musa mwana wa Imran kwa njia ya kumtukuza, na kumpa taadhima, na kujulisha cheo chake kitukufu na tabia zake zilizokamilika. \"Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa.\" Na ilisomwa (mukhlaswan) kwa kutia fat\u1e25a kwenye lam, nalo ni lenye maana ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimteua, akamchagua juu ya walimwengu wote. Na likasomwa neno hilo kwa kasra, nalo ni lenye maana ya kwamba yeye ni \"mwenye kumkusudia tu\" Mwenyezi Mungu Mtukufu katika matendo yake yote, na maneno yake, na makusudio yake. Kwa hivyo akamsifu kwamba alikuwa akimkusudia Yeye tu katika hali zake zote. Na maana hizi mbili hazitenganishwi. Kwa maana, Mwenyezi Mungu alimteua kwa sababu yeye Musa alikuwa akimkusudia Yeye tu. Nako kumkusudia kwake huku kunalazimu kuchaguliwa kwake. Na hali bora zaidi ambayo mja anaweza kuelezewa nayo ni yeye kumkusudia tu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu kumteua. \"Na alikuwa ni Mtume, Nabii.\" Yaani, Mwenyezi Mungu alimuunganishia utume na unabii. Na utume unahitaji kufikisha maneno ya mtumaji, na kufikisha yale yote aliyoyaleta ya Sheria, madogo yake na makubwa yake. Nao unabii unahitaji kwamba Mwenyezi Mungu alimfunulia wahyi, na kumteua yeye tu kwa ufunuo huo. Basi unabii huwa baina yake na Mola wake Mlezi, nao utume huwa baina yake na viumbe."},{"id":3114,"sura":19,"from_aya":52,"to_aya":52,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{52} Bali Mwenyezi Mungu alimteua kwa aina tukufu zaidi na bora zaidi ya wahyi ambayo ni Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu kumuongelesha na kumuweka karibu naye. Kwa hivyo, akawa kwa hilo akateuliwa miongoni mwa Manabaii kwamba yeye ndiye yule aliyezungumza moja kwa moja na Mwingi wa rehema. Na ndiyo maana akasema, \"Na tulimwita upande wa kulia wa mlima.\" Yaani, upande wa kulia wa Musa wakati alipokuwa anasafiri, au maana yake ni upande wenye baraka zaidi. Kama inavyoashiriwa na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Hakika amebarikiwa aliye katika moto huu na walioko pembezoni mwake,\" \"na tukamsogeza kunong'ona naye.\" Na ndani ya hili kuna kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anazungumza, na kwamba aina za maneno hayo ni kama vile kunadi na kunong'ona, kama lilivyo dhehebu la Ahlus-Sunna wal-Jamaa. Na hili ni kinyume na wale waliolipinga hilo kama vile Jahmiyyah na Mu\u2019tazila na wote waliofuata njia yao."},{"id":3115,"sura":19,"from_aya":53,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{53} Na kauli yake, \"Nasi kwa rehema zetu tukamtunuku kakaye, Harun, awe Nabii.\" Na hii ni miongoni mwa fadhila kubwa zaidi za Musa, na ihsani yake na uaminifu wake kwa kaka yake, Harun. Nalo ni kwamba alimuomba Mola wake Mlezi amshirikishe pamoja naye katika jambo lake na kwamba amfanye awe Mtume kama yeye. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamuitikia hilo na akamtunuku kakaye, Harun, awe Nabii. Na unabii wa Harun uko chini ya unabii wa Musa, amani iwe juu yao. Basi Harun akamsaidia Musa katika jambo lake hilo."},{"id":3116,"sura":19,"from_aya":54,"to_aya":55,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"54. Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii. 55. Na alikuwa akiwaamrisha ahali zake Swala na Zaka, na alikuwa mbele ya Mola wake Mlezi mwenye kuridhiwa. "},{"id":3117,"sura":19,"from_aya":54,"to_aya":54,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{54} Yaani, mtaje katika Qur-ani Tukufu nabii huyu mkuu, ambaye taifa la Kiarabu lilitokana naye, ambalo ndilo taifa bora na tukufu zaidi. Ambalo ametokana nalo bwana wa mwana wa Adam. \"Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi.\" Yaani, hakuwa akitoa ahadi yoyote isipokuwa anaitekeleza kikamilifu. Na hili linajumuisha ahadi anayoifunga na Mwenyezi Mungu au anayoifunga na waja wake. Na ndiyo maana alipojiahidi kuwa na subira baba yake alipotaka kumchinja, akasema, \"utanikuta mimi, Inshallah (Mwenyezi Mungu akipenda), katika wanaosubiri.\" Akalitimiza hilo, na akamuwezesha baba yake kwamba amchinje, jambo ambalo ndilo msiba mkubwa zaidi unaoweza kumsibu mtu. Kisha akamsifia kwa sifa ya utume na unabii ambayo ndiyo neema kubwa zaidi za Mwenyezi Mungu juu ya mja wake, na akamfanya kuwa miongoni mwa viumbe wa daraja la juu kabisa."},{"id":3118,"sura":19,"from_aya":55,"to_aya":55,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{55} \"Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Swala na Zaka.\" Yaani, alikuwa akisimamisha amri ya Mwenyezi Mungu juu ya watu wake, kwa kuwaamrisha Swala yenye kukusudiwa kwayo anayeabudiwa tu. Na zaka ambayo inayojumuisha kuwafanyia wengine mazuri. Kwa hivyo, akaikamilisha nafsi yake na akawakamilisha wengine, hasa watu maalumu zaidi kwake, ambao ni ahali zake. Kwa sababu wao ndio wanaostahili zaidi kulinganiwa kuliko wengine. \"Na alikuwa mbele ya Mola wake Mlezi mwenye kuridhiwa.\" Na kwa sababu ya kutekeleza kwake yale anayoridhia Mola wake Mlezi na kufanya kwake bidii katika yale yanayomridhisha, Mwenyezi Mungu akamridhia na akamjaalia miongoni mwa waja wake maalumu na vipenzi vyake walio karibu sana naye. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamuwia radhi, naye akamridhia Mola wake Mlezi."},{"id":3119,"sura":19,"from_aya":56,"to_aya":57,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"56. Na mtaje katika Kitabu Idris. Hakika yeye alikuwa ni mkweli mno, Nabii. 57. Na tulimuinua mahali pa juu. "},{"id":3120,"sura":19,"from_aya":56,"to_aya":56,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{56} Yaani, taja katika Kitabu kwa njia ya heshima, na utukufu, na kwa kueleza sifa za ukamilifu za Idris. \"Hakika yeye alikuwa mkweli mno, Nabii.\" Mwenyezi Mungu alimkusanyia kati ya sifa ya ukweli mno kamili unaojumuisha kusadiki kukamilifu, elimu kamili, yakini madhubuti, na matendo mema, na kati ya kumteua kwa ajili ya ufunuo wake na akamchagua apeleke ujumbe wake kwa watu."},{"id":3121,"sura":19,"from_aya":57,"to_aya":57,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{57} \"Na tulimuinua mahali pa juu.\" Yaani, Mwenyezi Mungu alinyanyua utajo wake katika walimwengu na cheo chake miongoni mwa walio karibu naye, basi akawa mwenye utajo wa juu na cheo cha juu."},{"id":3122,"sura":19,"from_aya":58,"to_aya":58,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"58. Hao ndio aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii katika uzao wa Adam, na katika uzao wa wale tuliowabeba pamoja na Nuhu, na katika uzao wa Ibrahim na Israil, na katika wale tuliowaongoa na tukawateua. Wanaposomewa Aya za Mwingi wa rehema, huanguka kusujudu na kulia."},{"id":3123,"sura":19,"from_aya":58,"to_aya":58,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{58} Alipowataja Manabii hawa watukufu, na Mitume maalumu na akataja fadhila na daraja zao, akasema, \"Hao ndio aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii.\" Yaani, Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwa neema isiyoweza kufikiwa wala kupitwa kama vile unabii na utume. Na hao ndio tuliamrishwa kwamba tumuombe Mwenyezi Mungu atuongoe kwenye njia ya wale aliowaneemesha, na kwamba mwenye kumtii Mwenyezi Mungu, atakuwa \u201cpamoja na wale ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha miongoni mwa manabii...\u201d  hadi mwisho wa Aya. Na kwamba baadhi yao ni \u201cuzao wa Adam, na katika uzao wa wale tuliowabeba pamoja na Nuhu.\u201d Yaani, kutoka katika kizazi chake. \"Na katika uzao wa Ibrahim na Israil.\" Hizi ndizo nyumba bora zaidi katika walimwengu wote. Mwenyezi Mungu aliwateua na kuwachagua, na ilikuwa hali yao pale wanaposomewa Aya za Mwingi wa rehema, zilizojumuisha habari za ghaibu na sifa za Ajuaye zaidi ghaibu, na habari za Siku ya Mwisho, na ahadi nzuri na ahadi ya adhabu kali, \"huanguka kusujudu na kulia.\" Yaani, walikuwa wakizinyenyekea Aya za Mwenyezi Mungu, na zikawa zinaathiri katika nyoyo zao kwa kuwapa imani, kumtaka Mwenyezi Mungu na kumhofu, mambo yaliyowasababishia kulia, kurudi kwa Mwenyezi Mungu, na kumsujudia Mola wao Mlezi, na hawakuwa miongoni mwa wale ambao walipozisikia Aya za Mwenyezi Mungu, wanajifanya viziwi nazo na vipofu. Na katika kufungamanisha Aya na jina lake, Mwingi wa rehema, kuna ushahidi Aya zake ni katika rehema zake na ihsani yake kwa waja wake, ambapo aliwaongoa kwazo kwenye haki, akawafanya kuona kutokana na kuwa na upofu, akawaokoa kutoka katika upotovu, na akawafundisha baada ya kwamba walikuwa wajinga."},{"id":3124,"sura":19,"from_aya":59,"to_aya":63,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"59. Lakini wakaja baada yao wafuatizi waliipoteza Swala, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta malipo ya ubaya. 60. Isipokuwa mwenye kutubu, akaamini, na akatenda mema. Hao basi, wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa chochote. 61. Bustani za milele ambazo aliwaahidi Rahmani (Mwingi wa Rehema) waja wake katika ghaibu. Hakika Yeye ahadi yake hakuna shaka itafika. 62. Humo hawatasikia upuuzi wowote, isipokuwa Salama tu. Na watapata humo riziki zao asubuhi na jioni. 63. Hiyo ndiyo Pepo tutayowarithisha katika waja wetu wale waliokuwa wachamungu. "},{"id":3125,"sura":19,"from_aya":59,"to_aya":59,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{59} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowataja Manabii hawa, ambao ni wenye kumkusudia Yeye tu, wanaofuata yale yanayomridhisha Mola wao Mlezi, wenye kurudi kwake, akawataja wale waliokuja baada yao na wakabadilisha yale waliyoamrishwa, na kwamba walikuja \"baada yao wafuatizi\" waliorudi nyuma \"waliipoteza Swala\" ambayo waliamrishwa kuihifadhi na kuisimamisha. Lakini waliipuuza na kuipoteza. Na ikiwa waliipoteza Swala ambayo ndiyo nguzo ya dini na mizani ya imani na kumkusudia tu Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambayo ndilo tendo la wajibu zaidi na sifa ubora zaidi, basi walikuwa wenye kupoteza zaidi na kukataa zaidi mengineyo yasiyokuwa hiyo. Na sababu iliyowapelekea kufanya hivyo ni kwamba walifuata matamanio na utashi wa nafsi zake, kwa hivyo zikawa hima zao zimeelekezwa kwa hayo na kutangulizwa mbele ya haki za Mwenyezi Mungu. Basi ikatokana na hayo, kupoteza haki za Mwenyezi Mungu, na wakayaelekea matamanio ya nafsi zao wenyewe. Haijalishi yaliwaonekania vipi matamanio hayo, wao walikuwa wanayatafuta tu. Na wakawa wanayafuata hata yakiafikiana kwa njia gani. \"Basi watakuja kuta malipo ya ubaya.\" Yaani, adhabu kali maradufu."},{"id":3126,"sura":19,"from_aya":60,"to_aya":60,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{60} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawatoa baadhi katika hilo, akasema, \"Isipokuwa mwenye kutubu\" kutokana na ushirikina, uzushi na maasia, na akayaacha hayo, na akayajutia, na akaazimia azimio ya kweli kutoyafanya tena, \"na akaamini\" Mwenyezi Mungu, Malaika wake, Vitabu vyake, Mitume wake, na Siku ya Mwisho, \"na akatenda mema.\" Nayo ni matendo ambayo Mwenyezi Mungu aliyaweka katika sheria kupitia ndimi za Mitume wake, ikiwa yatakusudiwa kwayo uso wake, \"hao basi\" ambao walijumuisha kati ya toba, imani na matendo mema; \"wataingia Peponi,\" ambayo imejumuisha neema ya milele, maisha yaliyo salama, na kuwa karibu na Mola Mlezi Mkarimu zaidi, \"wala hawatadhulumiwa chochote\" katika matendo yao. Bali watayakuta yakiwa kamili, yenye malipo mengi, na idadi iliyozidishwa."},{"id":3127,"sura":19,"from_aya":61,"to_aya":61,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{61} Kisha akataja kuwa Pepo aliyowaahidi kuingia si kama Pepo nyinginezo, bali ni \"Bustani za milele\" zisizokuwa na taabu yoyote, wala kuondoka, wala kutoweka, kwa sababu ya upana wake na wingi wa heri, furaha, na uzuri ulio ndani yake; \"ambazo aliwaahidi Rahmani (Mwingi wa Rehema) waja wake katika siri.\" Alizifungamanisha na jina lake, Mwingi wa rehema, kwa sababu zina rehema na ihsani ambayo jicho halijawahi kuona, wala sikio halijawahi sikia, wala hazijawahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote. Naye Mtukufu aliziita 'rehema yake,' akasema, \"Na ama wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe, basi watakuwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu. Wao humo watadumu.\" Na pia kuzifungamanisha Pepo hizo na rehema yake kunaonyesha uendelevu wa furaha yake, na kwamba zitabakia maadamu rehema yake itabakia, ambayo ndiyo athari yake na sababu yake. Na waja waliokusudiwa katika Aya hii ni wale waja wanaomfanyia Yeye tu uungu, wale waliomuabudu na wakashikamana na sheria zake, basi uja ukawa ndiyo sifa yao, kama ilivyo katika kauli yake, \"Na waja wa Mwingi wa rehema\" na mfano wake. Tofauti na waja wake kwa sababu ya kuwamiliki kwake tu. Wale ambao hawakumwabudu. Hawa hata ingawa ni waja kwa sababu ya umola wake juu yao, kwa sababu Yeye ndiye aliyewaumba, akawaruzuku na akawaendesha, lakini hawaingii katika waja wanaomfanyia Yeye tu uungu. Nao huu ni uja anaoufanya mja kwa hiari yake, ambao mwenye kuufanya anasifiwa kwa sababu yake. Si kama uja wao ambao ni wa lazima, ambao hauna sifa yoyote ndani yake. Na kauli yake, \"katika ghaibu\" inawezekana kuwa inarejelea ahadi ya Mwingi wa rehema. Kwa hivyo, maana yake inakuwa ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwaahidi hilo ahadi ya ghaibu ambayo hawakuishuhudia wala kuiona, lakini wakaiamini, na wakaisadiki ghaibu yake, na wakaifanyia bidii ijapokuwa hawakuiona. Basi ingekuwa vipi ikiwa wangeiona? Wangekuwa ni wenye kuitafuta kwa bidii kubwa zaidi, na kuitaka vikubwa sana, na kuifanyia bidii kubwa zaidi. Na maana hii inawasifu kwa sababu ya kuamini kwao ghaibu, ambayo ndiyo imani yenye manufaa. Na inawezekana kwamba inarejelea waja wake. Yaani, wale waliomuabudu katika ghaibu bila ya kumuona. Basi hii ndiyo ibada yao ingawa hawakumuona. Na ikiwa wangemwona, basi wangemwabudu kwa bidii kubwa zaidi, na kurudi kwake kwa wingi, na wangempenda zaidi, na kuwa na hamu kubwa zaidi naye. Pia inawezekana kwamba maana yake ni: Bustani hizi ambazo Mwingi wa rehema aliwaahidi waja wake ni miongoni mwa mambo ambayo maelezo hayawezi kuyafahamu na hakuna yeyote anayeyajua isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, ndani ya maana hii kuna kutia hamu juu yake na kuzieleza kwa maelezo mazuri yenye kufurahisha nafsi na kumsisimua aliyetulia ili azitafute, na hili linakuwa kama kauli yake, \"Nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho - ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda.\" Na maana hizi zote ni sahihi na zilithibiti, lakini uwezekano wa kwanza ndio bora zaidi, kwa ushahidi wa kauli yake, \"Hakika Yeye ahadi yake hakuna shaka itafika.\" Kwa maana Yeye havunji ahadi yake, naye ndiye mkweli zaidi wa wanaosema."},{"id":3128,"sura":19,"from_aya":62,"to_aya":62,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{62} \"Humo hawatasikia upuuzi wowote\" wala mambo yenye kumfanya mtu kuwa na dhambi. Kwa hivyo, hawatasikia humo matusi, wala kutilia kitu dosari, wala kauli ya kumuasi Mwenyezi Mungu, au maneno ya kuhuzunisha \"isipokuwa Salama tu.\" Yaani, [isipokuwa] kauli ambazo ni salama kutokana na dosari yoyote. Humo kutakuwa tu na kumtaja Mwenyezi Mungu, na maamkizi, na maneno ya furaha na bishara njema, mazungumzo mazuri kati ya ndugu, kusikia muzungumzo ya Mwingi wa rehema, sauti za kupendeza za hurulaini, malaika na watoto wadogo, nyimbo za kupendeza mno, na maneno mazuri. Kwa sababu nyumba hiyo ni nyumba yenye salama. Hakuna ndani yake isipokuwa usalama kamili katika njia zote. \"Na watapata humo riziki zao\" miongoni mwa vyakula, vinywaji, na aina mbalimbali za starehe \"asubuhi na jioni.\" Yaani, zitaendelea popote pale watakapoomba na wakati wowote watakapotaka. Na katika ukamilifu wake, raha yake, na uzuri wake ni kwamba zitakuwa katika nyakati zinazojulikana, asubuhi na jioni. Ili kuongeza athari vikubwa na yatimie manufaa yake."},{"id":3129,"sura":19,"from_aya":63,"to_aya":63,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{63} Basi \"Hiyo ndiyo Pepo\" tuliyoieleza kuwa yaliyotajwa \"tutayowarithisha katika waja wetu wale waliokuwa wachamungu\" na tuifanye kuwa makazi yao ya kudumu, ambayo hawatatoka humo, wala hawatataka kuiacha kwenda kwingine. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Na kimbilieni kufutiwa dhambi kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi. Iliandaliwa kwa ajili ya wachamungu.\""},{"id":3130,"sura":19,"from_aya":64,"to_aya":65,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"64. (Nao watasema:) Wala hatuteremki isipokuwa kwa amri ya Mola wako Mlezi. Ni yake Yeye yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyomo katikati ya hayo. Na Mola wako Mlezi si mwenye kusahau. 65. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi muabudu Yeye tu, na usubiri katika kumuabudu. Je, unajua chochote kilicho sawa naye? "},{"id":3131,"sura":19,"from_aya":64,"to_aya":64,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{64} Siku moja Nabii  \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie \u2013  aliona kwamba Jibril, amani ziwe juu yake, hamteremkii mara kwa mara, akamwambia: Lau ungetujia mara nyingi zaidi ya unavyotujia. Hili lilikuwa kutokana na kuwa na shauku yake kubwa juu yake na kuwa kwake mpweke anapoondoka, na ili moyo wake utulie kwa kuteremka kwake. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha kwa ulimi wa Jibril: \"Wala hatuteremki isipokuwa kwa amri ya Mola wako Mlezi\" nasi wenyewe hatuna lolote katika suala hilo. Akituamrisha, tunaharakisha kutekeleza amri yake wala hatumuasi katika amri yake yoyote. Kama alivyosema juu yao, \"hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa.\" Kwa maana sisi ni waja tu tunaoamrishwa. \"Ni yake Yeye yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyomo katikati ya hayo.\" Yaani, ni yake yote mambo yaliyopita, yajayo, na ya sasa katika zama zote na mahali pote. Na ikishabainika kuwa jambo lote ni la Mwenyezi Mungu, na kwamba sisi ni waja tunaoendeshwa, basi jambo hilo linabakia kuwa kati ya je, hekima ya Mwenyezi Mungu inataka liwe, ndiyo alipitishe, au hailitaki, kwa hivyo akalichelewesha? Ndiyo maana akasema, \"Na Mola wako Mlezi si mwenye kusahau.\" Yaani, Mwenyezi Mungu si mwenye kukusahau au kukupuuza. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukukasirikia.\" Bali Yeye hakuacha kuendelea kuyajali mambo yako, na kukuendesha kufikia malipo yake na mipango yake mizuri. Yaani, ikiwa tutachelewa kuteremka katika wakati uliozoea, basi lisikuhuzunishe hilo wala lisitukie wasiwasi. Na jua ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyetaka hilo. Kwa sababu ana hekima fulani ndani yake."},{"id":3132,"sura":19,"from_aya":65,"to_aya":65,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{65} Kisha akatoa sababu ya upana wa elimu yake na kuwa kutosahau kwake kwamba Yeye ndiye \"Mola Mlezi wa mbingu na ardhi.\" Kwa hivyo, umola wake juu ya mbingu na ardhi, na kwamba viwili hivyo viko katika nidhamu nzuri zaidi iliyo kamili, ambao hauna kughafilika kokote, wala kupuuza, wala ubatili, ni uthibitisho wa uhakika juu ya elimu yake ya kujumuisha kila kitu. Basi usijishughulishe na hayo, bali ishughulishe nafsi yako na yale yanayokufaa na yenye matokeo mazuri kwako, nayo ni kumuabudu Yeye pekee bila ya mshirika yeyote. \"Na usubiri katika kumuabudu,\" na pambana na nafsi yako kwa hilo, na uitekeleze kwa ukamilifu kulingana na uwezo wako. Na katika kushughulika na ibada ya Mwenyezi Mungu kuna liwazo kwa mja dhidi ya mafungamano yote na matamanio. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Wala usivikodolee macho vile tulivyowastarehesha kwavyo baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya duniani, ili tuwajaribu katika hivyo...\" Mpaka aliposema, \"Na waamrishe ahali zako kuswali, na usubiri juu yake...\" hadi mwisho wa aya. \"Je, unajua chochote kilicho sawa naye?\" Yaani, je unajua chochote kilicho sawa na Mwenyezi Mungu, na chenye kufanana naye miongoni mwa viumbe? Na huku ni kuuliza swali kwenye maana ya kukanusha kunakojulikana tu kwa akili. Yaani, hujui yeyote mwenye jina kama lake wala mwenye kufanana naye. Kwa sababu Yeye ndiye Mola Mlezi, na wengineo wanalelewa naye, Muumba na wengineo wameumbwa, Asiyehitaji kwa njia zote, nao wengineo ni wahitaji kwa dhati zao katika njia zote. Yeye ni mkamilifu wa ukamilifu wote katika njia zote, na wasiokuwa yeye ni wapungufu na hawana ukamilifu wowote isipokuwa ule aliowapa Mwenyezi Mungu. Huu ni uthibitisho wa uhakika kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa, na kwamba kumwabudu Yeye ni haki, na kuabudu chochote badala yake ni batili. Na ndiyo maana akatuamrisha tumwabudu Yeye peke yake na kusubiri juu yake, na akatoa sababu ya [hilo] kwamba yeye ni mkamilifu na wa pekee katika ukuu na majina mazuri zaidi."},{"id":3133,"sura":19,"from_aya":66,"to_aya":67,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"66. Na mwanadamu husema: Hivyo, nitakapokufa, ni kweli nitafufuliwa niwe hai tena? 67. Je, hakumbuki mwanadamu ya kwamba hakika tulimuumba kabla, na wala hakuwa chochote? "},{"id":3134,"sura":19,"from_aya":66,"to_aya":66,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{66} Aliyekusudiwa na mwanadamu hapa ni kila mwenye kukana ufufuo anayeona kwamba haliwezi kutokea. Akawa anasema, akiuliza kwa njia kukanusha, ukaidi, na ukafiri, \"Hivyo, nitakapokufa, ni kweli nitafufuliwa niwe hai tena?\" Yaani, vipi Mwenyezi Mungu atanirudisha niwe hai baada ya mauti, na baada ya kuwa mifupa iliyokwishamung'unyika? Hili haliwezi kuwa wala hata haliingii akilini! Lakini hili ni kulingana na akili yake mbovu, na makusudio yake mabaya, na ukaidi wake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na vitabu vyake. Lakini angeangalia kwa mtazamo mdogo zaidi na kutafakari kudogo zaidi, angeona kwamba kupinga kwake Ufufuo ni jambo la upumbavu wa mwisho."},{"id":3135,"sura":19,"from_aya":67,"to_aya":67,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{67} Na ndiyo sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja uthibitisho wa mkato na ushahidi ulio wazi kwamba kila mtu anajua juu ya uwezekano wa kufufuliwa, hivyo akasema, \"Je, hakumbuki mwanadamu ya kwamba hakika tulimuumba kabla, na wala hakuwa chochote?\" Kwa hivyo, yule aliyeweza kumuumba baada ya kwamba hakuwepo, na wala hakuwa chochote cha kutajwa, kwani hawezi kumuumba baada ya kuchanikachanika, na kumkusanya baada ya kugawanyika? Na hili ni kama kauli yake, \"Na Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine.  Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake.\" Na katika kauli yake, \u201cJe, hakumbuki mwanadamu\" kuna wito juu ya kuzingatia, kwa ushahidi wa kimantiki kwa kutumia mazungumzo yenye upole mkubwa zaidi, na kwamba kukanusha kwa yule aliyekanusha hilo kunatokana na kughafilika kwake kuhusiana na hali yake ya mwanzo? Vinginevyo; ikiwa angeikumbuka na kuihudhurisha katika akili yake, basi hangekanusha hilo."},{"id":3136,"sura":19,"from_aya":68,"to_aya":70,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"68. Basi ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na mashetani. Kisha tutawahudhurisha kuizunguka Jahannamu huku wamepiga magoti! 69. Kisha kwa yakini tutaondoa kutoka katika kila kundi wale miongoni mwao waliozidi kumuasi Arrahmani (Mwingi wa Rehema). 70. Tena hakika Sisi tunawajua vyema zaidi wanaostahiki kuunguzwa humo. "},{"id":3137,"sura":19,"from_aya":68,"to_aya":68,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{68} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaapa - naye ndiye mkweli zaidi wa wale wanaosema - kwa umola wake kwamba hakika atawakusanya hawa wakanushaji wa ufufuo wao na mashetani wao, kisha atawakusanya kwa miadi ya siku inayojulikana. \"Kisha tutawahudhurisha kuizunguka Jahannamu huku wamepiga magoti,\" kutokana na ukubwa wa hofu kubwa, wingi wa mitetemeko, na hali mbaya, huku wakingojea hukumu ya Mkubwa, Mtukufu."},{"id":3138,"sura":19,"from_aya":69,"to_aya":69,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{69} Na ndiyo sababu akataja hukumu yake kuhusiana nao, akasema, \"Kisha kwa yakini tutaondoa katika kila kundi wale miongoni mwao waliozidi kumuasi Arrahmani (Mwingi wa Rahema).\" Yaani, kisha kwa yakini tutaondoa kutoka katika kila kundi miongoni mwa madhalimu, waliofanana katika dhuluma, ukafiri na uasi, wale wao waliozidi katika uasi, wenye dhuluma kubwa zaidi, wenye ukafiri mkubwa ili awatangulize kutiwa adhabu. Kisha hivyo hivyo atatangulizwa mwenye dhambi kubwa katika adhabu zaidi, kisha mwenye dhambi kubwa zaidi. Nao katika hali hiyo watalaaniana wao kwa wao, na wa mwisho wao atasema kuhusu wa mwanzo wao, \"Mola wetu Mlezi! Hawa ndio waliotupoteza. Basi wape adhabu ya Motoni marudufu. [Atasema: Kila mmoja ana marudufu, lakini nyinyi hamjui tu]. Na wa mwanzo wao atamwambia wa mwisho wao: Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora wowote kuliko sisi...\""},{"id":3139,"sura":19,"from_aya":70,"to_aya":70,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{70} Na yote haya yanafuatana na uadilifu wake, hekima yake, na elimu yake pana, na ndiyo maana akasema, \"Tena hakika Sisi tunawajua vyema zaidi wanaostahiki kuunguzwa humo.\" Yaani, elimu yetu imewazunguka wanaostahiki kuunguzwa humo Motoni. Na tayari tulikwisha wajua na tukayajua matendo yao, na kustahiki kwa matendo hayo adhabu, na fungu la matendo hayo katika adhabu."},{"id":3140,"sura":19,"from_aya":71,"to_aya":72,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"71. Wala hapana yeyote katika nyinyi isipokuwa ataifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako Mlezi ambayo lazima itimizwe. 72. Kisha tutawaokoa sawasawa wale waliomcha Mungu; na tutawaacha madhalimu humo huku wamepiga magoti. "},{"id":3141,"sura":19,"from_aya":71,"to_aya":71,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{71} Haya wanaongeleshwa kwayo viumbe wote, mwema wao na muovu wao, muumini wao na kafiri wao. Hakika, hakuna hata mmoja wao isipokuwa ataufikia Moto, ni hukumu aliyokwisha pitisha Mwenyezi Mungu mwenyewe, na akawatishia kwayo waja wake. Kwa hivyo, hakuna budi itatekelezeka wala hakuna cha kuiepusha kutokea. Na wanachuoni wamehitilafiana juu ya maana ya kuifikia. Basi ikasemwa kuifikia ni kule kuihudhuria kwa viumbe vyote ili kila mmoja wao aweze kusumbukana, kisha baadaye Mwenyezi Mungu atawaokoa sawasawa wachamungu. Na ilisemwa kwamba kuifikia ni kuingia humo, lakini kwa muumini moto huo utakuwa baridi na salama. Na ilisemwa kwamba kuufikia ni kule kupita kwenye Sirat, nayo ni njia nyembamba iliyoko juu ya Jahannam. Basi watu watapita juu yake kulingana na matendo yao. Miongoni mwao kuna wale watakaopita kama kufumba na kufumbua kwa macho, na kama upepo, na kama farasi waendao kwa kasi kubwa zaidi, na kama ngamia waendao kwa kasi kubwa zaidi. Na miongoni mwao kuna atakayekimbia juu yake, na kuna atakayetembea, na kuna atakayetambaa, na miongoni mwao kuna atakayenyakuliwa na kutupwa Motoni. Kila mmoja wao kulingana na uchamungu wake."},{"id":3142,"sura":19,"from_aya":72,"to_aya":72,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{72} Na ndiyo maana akasema, \"Kisha tutawaokoa sawasawa wale waliomcha Mungu\" Mtukufu kwa kutenda maamrisho na kujiepusha na haramu. \"Na tutawaacha madhalimu\" waliojidhulumu kwa ukafiri na maasia \"humo huku wamepiga magoti.\" Na haya, kwa sababu ya udhalimu wao na ukafiri wao, ikawa lazima juu yao kwamba wadumu humo, na adhabu ikawadhibitikia, na zikawakatikia njia zote."},{"id":3143,"sura":19,"from_aya":73,"to_aya":74,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"73. Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale waliokufuru huwaambia wale walioamini: Ni lipi katika makundi mawili haya lenye cheo kizuri na lilio zuri zaidi barazani? 74. Na kaumu ngapi tuliziangamiza zilizokuwa na mapambo mazuri zaidi na wazuri zaidi katika muonekano! "},{"id":3144,"sura":19,"from_aya":73,"to_aya":73,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{73} Yaani, wanaposomewa makafiri hawa Aya zetu zilizo wazi katika kuonyesha upweke wa Mwenyezi Mungu na ukweli wa Mitume wake, ambazo zinamlazimu mwenye kuzisikia kuwa na imani ya ukweli na yakini kubwa, wao wanakabiliana nazo kwa kinyume cha inavyowapasa kuamiliana nazo, na wakazifanyia stihizai, na yule mwenye kuziamini, na wakatumia hali yao nzuri katika dunia kuwa ni ushahidi kuwa wao ni bora kuliko Waumini. Wakasema wakiipinga haki, \"Ni lipi katika makundi mawili haya;\" sisi na Waumini ''lenye cheo kizuri\" katika dunia hii kama vile wingi wa mali, na matamanio ya juu zaidi \"na lilio zuri zaidi barazani?\" Kwa hivyo, wakatoa katika utangulizi huu mbovu, kwa kuwa wana mali nyingi zaidi na watoto, na kwamba wanayo mengi ya mahitaji yao ya kidunia, na kwamba mikusanyiko yao na mabaraza yao yamepambwa na kurembeshwa, ilhali waumini wako kinyume na hali hii, basi wakaona kwamba wao ni bora kuliko waumini!"},{"id":3145,"sura":19,"from_aya":74,"to_aya":74,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{74} Na ushahidi huu ni mbovu zaidi, na ni katika mbinu za kugeuza uhakika wa mambo. Vinginevyo, wingi wa mali, watoto, na muonekano mzuri mara nyingi huwa ni sababu ya kuangamia kwa mwenyewe, na kumtia mashakani, na katika uovu. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, \"Na kaumu ngapi tuliziangamiza zilizokuwa na mapambo mazuri zaidi.\" Yaani, wenye bidhaa kama vile vyombo, fanicha, nyumba, na mapambo, \"na wazuri zaidi katika muonekano!\" Yaani, wenye muonekano mzuri zaidi wa maisha yenye utajiri, furaha, raha, na sura nzuri. Kwa hivyo, ikiwa hawa walioangamia walikuwa bora zaidi yao katika mapambo na muonekano, na wala hayo hayakuwazuilia kufikiwa na adhabu, basi hawa wenye vichache zaidi yao, na ni wanyonge zaidi yao watawezaje kujilinda dhidi ya adhabu? \"Je, makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?\" Na ilijulikana kutokana na hili kwamba kutumia heri ya dunia kama ushahidi wa heri ya Akhera ni katika ushahidi mbovu zaidi na kwamba ni miongoni mwa njia za makafiri."},{"id":3146,"sura":19,"from_aya":75,"to_aya":75,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"75. Sema: Yule aliye katika upotofu, basi Arrahmani (Mwingi wa rahema) na amuongezee (muda, mali na mengineyo) mpaka atakapoona yale waliyoahidiwa - ima ni adhabu au ni Saa, hapo ndipo watakapojua ni nani mwenye makao maovu zaidi na mwenye jeshi dhaifu zaidi."},{"id":3147,"sura":19,"from_aya":75,"to_aya":75,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{75} Alipoutaja ushahidi wao wa batili, unaoonyesha ukubwa wa ukaidi wao na upotovu wao mkubwa zaidi, akajulisha hapa kwamba yeyote yule aliye katika upotovu, kwa kuuridhia yeye mwenyewe, na akautafuta kwa bidii, basi Mwenyezi Mungu humuongezea katika huo na kumzidishia kuupenda, iwe adhabu kwake kwa kuuchagua badala ya uwongofu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, ''Na walipokengeuka, Mwenyezi Mungu akazikengeusha nyoyo zao.'' ''Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao kama vile hawakuiamini mara ya kwanza. Kisha tutawaacha katika upotovu wao wakitangatanga kwa upofu...'' \"mpaka atakapoona.\" Yaani, hao waliosema, \"Ni lipi katika makundi mawili haya lenye cheo kizuri na lilio zuri zaidi barazani?\" \"Yale waliyoahidiwa - ima ni adhabu\" kwa kuwaua au kitu kinginecho, \"au ni Saa\" ambayo ndiyo mlango wa kwenda kulipwa juu ya matendo. \"Hapo ndipo watakapojua ni nani mwenye makao maovu zaidi na mwenye jeshi dhaifu zaidi.\" Na wakati huo ndipo itawabainikia ubatili wa madai yao, na kwamba ni madai ya kupotelea mbali tu, na watakuwa na yakini kuwa wao ni watu waovu na wenye jeshi dhaifu zaidi. Lakini elimu hii haitawafaidi chochote. Kwa sababu hawataweza kurudi katika dunia na wafanye yasiyokuwa mtendo yao ya kwanza."},{"id":3148,"sura":19,"from_aya":76,"to_aya":76,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"76. Na Mwenyezi Mungu huwazidishia wale walioongoka uwongofu. Na mema yenye kubakia ni bora katika malipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana marejeo mema."},{"id":3149,"sura":19,"from_aya":76,"to_aya":76,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{76} Alipotaja kuwa madhalimu wataongezewa katika upotovu wao, akataja kuwa atawazidishia wongofu walioongoka kwa sababu ya fadhila na rehema zake juu yao. Na uwongofu unajumuisha elimu yenye manufaa na matendo mema. Kwa hivyo kila mwenye kufuata njia ya elimu, imani na matendo mema, Mwenyezi Mungu atamzidishia katika hayo na kumfanyia wepesi na kumuongezea mambo mengine yasiyokuwa katika matendo yake mwenyewe. Na katika hili kuna ushahidi kwamba imani huongezeka na kupunguka, kama walivyosema hivyo watangulizi wema. Na hilo linaashiriwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Na wazidi Imani wale walioamini\", \"na wanaposomewa Aya zake, zinawazidishia Imani.\" Hili pia linaonyeshwa na hali halisi ya mambo. Kwa maana, imani ni kauli ya moyo na ulimi, na matendo ya moyo, ulimi na viungo. Na waumini wanatofautiana kutofautiana kukubwa sana katika mambo haya. Kisha akasema: \"Na matendo mema yenye kudumu.\" Yaani, matendo yaliyobakia ambayo hayakomi ikiwa mengine yatakoma, na mazuri hayatatoweka. Kuanzia sala, zaka, saumu, Hajj, Umra, kusoma, kusifu, kutukuza, kusifu, kutukuza, kufadhili viumbe, na vitendo vya moyo na mwili. Amali hizi \"ni bora kwa Mola wako Mlezi kwa malipo na bora kwa marejeo.\" Yaani, ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kwa malipo yake, na manufaa yake na marejeo yake ni mengi kwa wafanyao kazi, na hii ni chini ya kichwa cha kutumia upendeleo wenye ufanisi zaidi katika mengine yasiyo ya somo lake. Kwani hakuna jingine isipokuwa mema yenye kudumu yenye manufaa na malipo yake hayabaki kwa mwenye kuyatenda, wala hayafai, na tukio lake ni kutajwa kwa mema yenye kudumu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi kwamba alipotaja ya kuwa madhalimu walizifanya hali za dunia, kama vile fedha, watoto, cheo kizuri, na mfano wa hayo, kuwa ni dalili ya hali nzuri ya mmiliki wao. Niambie hapa kwamba jambo si kama walivyodai, bali kazi, ambayo ni jina la furaha na njia ya mafanikio, ni kufanya kazi na kile ambacho Mungu anakipenda na anaridhia nacho."},{"id":3150,"sura":19,"from_aya":77,"to_aya":80,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"77. Je, umemwona aliyezikufuru Ishara zetu na akasema: Kwa hakika mimi nitapewa mali na wana! 78. Kwani yeye amepata habari za ghaibu, au amechukua ahadi kwa Arrahmani (Mwingi wa Rehema)? 79. Hasha! Tutaandika anayoyasema, na tutamuongezea sawasawa katika adhabu. 80. Na tutamrithi hayo anayoyasema, na atatujia mtupu peke yake! "},{"id":3151,"sura":19,"from_aya":77,"to_aya":77,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{77} Yaani, je, hushangazwi na hali ya kafiri huyu aliyechanganya kati ya kukufuru kwake Ishara za Mwenyezi Mungu na madai yake makubwa ya kwamba katika akhera atapewa mali na watoto? Yaani, atakuwa miongoni mwa wakazi wa Peponi. Na hili ni miongoni mwa mambo ya ajabu sana. Kwa maana, ikiwa angekuwa anamwamini Mwenyezi Mungu na akadai madai haya, basi jambo hili lingekuwa rahisi. Na aya hii, hata kama iliteremka kuhusiana na kafiri mahususi, inajumuisha kila kafiri anayedai kwamba yuko katika haki na kwamba yeye ni miongoni mwa wakazi wa Peponi."},{"id":3152,"sura":19,"from_aya":78,"to_aya":78,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{78} Mwenyezi Mungu akasema kwa kumkemea na kumkadhibisha, \"Kwani yeye amepata habari za ghaibu?\" Yaani, elimu yake iliizunguka ghaibu mpaka akajua yatakayotokea, na kwamba miongoni mwa mambo yatakayotokea ni kuwa atapewa mali na watoto Siku ya Qiyama? \"Au amechukua ahadi kwa Arrahmani (Mwingi wa Rehema)\" ya kwamba atapata aliyoyasema? Yaani, hakuna lolote kati ya hayo lililotokea. Kwa hivyo ikajulikana kwamba anazua tu maneno haya, na kusema mambo ambayo hana elimu yoyote nayo. Na kugawanya huku na kurejea ni katika mbinu kubwa zaidi ziwezekanazo katika kulazimisha na kumsimamishia hoja. Kwani mwenye kudai kuwa atapata heri kwa Mwenyezi Mungu huko Akhera hatoki katika hali hizi. Ima kauli yake hiyo inatokana na kujua kwake ghaibu ya mambo yajayo, na tayari ilikwisha julikana kwamba hayo ni ya Mwenyezi Mungu peke yake. Kwa hivyo, hakuna yeyote ajuaye mambo ya ghaibu isipokuwa yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwajulisha Mitume wake. Au iwe kwamba alichukua ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kumwamini na kuwafuata Mitume wake, ambao Mwenyezi Mungu aliwaahidi wafanyao hivyo na akafunua kwamba hao ndio wenye kupata akhera, ambao wataokoka na kufaulu. Na mambo haya mawili yasipopatikana, basi inajulikana kwamba madai hake hayo ni batili."},{"id":3153,"sura":19,"from_aya":79,"to_aya":79,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{79} Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, \"Hasha!\" Yaani, jambo hili si kama alivyodai. Kwa maana, huyo aliyeyasema hana habari zozote za ghaibu, kwa sababu yeye ni kafiri asiye na elimu yoyote ya Mitume, na wala hakuchukua ahadi yoyote kwa Mwingi wa rehema. Kwa sababu ya ukafiri wake na kutoamini kwake. Lakini anastahiki kinyume cha ayasemayo, na hakika maneno yake yameandikwa na kuhifadhiwa ili alipwe kwayo na aadhibiwe. Na ndiyo maana akasema, \"Tutaandika anayoyasema, na tutamuongezea sawasawa katika adhabu.\" Yaani, tutamzidishia aina mbalimbali za adhabu kama alivyozidisha katika kukengeuka na kupotea."},{"id":3154,"sura":19,"from_aya":80,"to_aya":80,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{80} \"Na tutamrithi hayo anayoyasema.\" Yaani, tutamrithi mali yake na watoto wake, na atatoka katika dunia hii mtupu peke yake, bila ya mali, wala familia, wala wa kumnusuru na wa kumsaidia. \"Na atatujia peke yake!\" Na ataiona adhabu kali ambayo ni malipo ya madhalimu kama yeye."},{"id":3155,"sura":19,"from_aya":81,"to_aya":84,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"81. Na walichukua miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati iwape nguvu. 82. Sivyo kabisa! Wataikataa hiyo ibada yao, na watakuwa ndio dhidi yao. 83. Kwani huoni ya kwamba tumewatuma mashetani kwa makafiri wawachochee sawasawa? 84. Basi usiwafanyie haraka. Sisi tunawahisabia idadi ya siku zao. "},{"id":3156,"sura":19,"from_aya":83,"to_aya":83,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{83} Na hii ni miongoni mwa adhabu za makafiri kwamba pindi hawakujilinda kwa Mwenyezi Mungu na wala hawakushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu, bali walimshirikisha Yeye na wakawafanya maadui zake ndio vipenzi wao miongoni mwa mashetani, akawapa mamlaka mashetani hao juu yao na akawawea kuandamana nao. Basi mashetani hao wakawa wanawachochea sawasawa kufanya maasia, na wanashawishi sawasawa kufuru. Kwa hivyo wakawa wanawatia wasiwasi na kuwafunulia mambo na kuwapambia batili, na kuwaonyesha kwamba haki ni mbaya, basi yakaingia mapenzi ya batili ndani ya nyoyo zao na zikainywa sawasawa. Kwa hivyo, wakawa wanaifanyia bidii kama vile anavyoifanyia bidii mwana haki juu ya haki yake, kwa kuinusuru kwa jitihada yake, na kupigana kwa ajili yake. Na anapigana dhidi ya wana haki katika kuiteteka batili. Na yote haya ni malipo yake kwa kumfanya kipenzi huyo kipenzi wake ambaye ni adui yake Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu akampa mamlaka juu yake. Vinginevyo, ikiwa angemwamini Mwenyezi Mungu na kumtegemea, basi hangekuwa na mamlaka juu yake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Hakika yeye hana mamlaka yoyote juu ya wale walioamini na wakamtegemea Mola wao Mlezi. Hakika mamlaka yake yako juu ya wale wanaomfanya kuwa kipenzi chao, na wale wanaofanya ushirika naye.\""},{"id":3157,"sura":19,"from_aya":84,"to_aya":84,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{84} \"Basi usiwafanyie haraka\" hawa makafiri wanaotaka adhabu ije haraka. \"Sisi hakika tunawahesabia sawasawa.\" Kwa maana, wana siku za kuhesabika tu. Hawatazitangulia wala hawatakawia zaidi yake. Na tunawapa muhula, na kuwafanyia ustahamilivu kwa muda, ili wairudie amri ya Mwenyezi Mungu. Lakini ikiwa hayo hayatawafaidi kitu, tukawashika kama anavyoshika Mwenye nguvu, Mwenye uwezo."},{"id":3158,"sura":19,"from_aya":85,"to_aya":87,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"85. Siku tutakayowakusanya wachamungu kuwapeleka kwa Arrahmani (Mwingi wa rehema) kuwa ni wageni wake. 86. Na tukawaswaga wahalifu kwenda katika Jahannamu hali ya kuwa wana kiu. 87. Hawatakuwa na mamlaka ya uombezi isipokuwa yule aliyechukua ahadi kwa Arrahmani (Mwingi wa rehema). "},{"id":3159,"sura":19,"from_aya":85,"to_aya":85,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{85} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu tofauti iliyoko kati ya makundi haya mawili: wachamungu na wahalifu. Na kwamba wale wanaomcha Yeye kwa kujiepusha na ushirikina, uzushi na maasia, atawakusanya kwenye mahali pa kisimamo cha Qiyama kwa utukufu, heshima, na taadhima. Na kwamba marejeo yao ni Mwingi wa rehema, na makusudio yao ni Mwingi wa kutoa (Al-Mannan), kama wageni wake. Na mgeni lazima huwa moyoni mwake na matumaini na mawazo mazuri juu ya anayemuendea ugeni, kama inavyojulikana. Basi wachamungu watakwenda ugeni kwa Mwingi wa rehema, wakitaraji rehema yake na ihsani yake ya kujumuisha, na kufikia vipawa vyake katika nyumba ya radhi zake. Na hayo ni kwa sababu ya yale matendo waliyoyatanguliza kwa kumcha na kufuata yale anayoyaridhia, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaahidi thawabu hizo kwa ndimi za Mitume wake. Kwa hivyo wakaelekea kwa Mola wao Mlezi wakiwa wana utulivu juu ya hilo, wakiwa wana imani na fadhila zake."},{"id":3160,"sura":19,"from_aya":86,"to_aya":86,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{86} Na ama wahalifu, hao wataswagwa, \"kwenda katika Jahannamu hali ya kuwa wana kiu.\" Na hii ndiyo hali ya kutisha zaidi inayowezekana miongoni mwa hali, watakaposwagwa kwa njia ya udhalilifu na uduni kwenda katika jela kubwa zaidi na adhabu ya kutisha mno, ambayo ni Jahannam, hali ya kuwa wana kiu na wamechoka. Wataomba msaada, lakini hawatasaidiwa. Na wataomba dua, lakini hawatajibiwa. Na  wataomba uombezi, lakini hawatafanyia uombezi wowote."},{"id":3161,"sura":19,"from_aya":87,"to_aya":87,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{87} Na ndiyo maana akasema, \"Hawatakuwa na mamlaka ya uombezi\" kwa njia yoyote ile, kwa maana hilo ni la Mwenyezi Mungu Mtukufu tu. \"Sema: Uombezi wote ni wa Mwenyezi Mungu.\" Na tayari alikwisha julisha kwamba uombezi wa woambezi hautawafaa kitu, kwa sababu hawakuchukua ahadi kwake ya kumuamini Yeye na Mitume wake. Vinginevyo, mwenye kuchukua ahadi kwake, akamwamini Yeye na Mitume wake, na akawafuata, basi yeye ni miongoni mwa wale aliowaridhia Mwenyezi Mungu na atapata uombezi. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Wala hawamwombei uombezi yeyote isipokuwa yule ambaye Yeye anamridhia.\" Na Mwenyezi Mungu ameita kumuamini Yeye na kuwafuata Mitume wake kuwa ni ahadi. Kwa sababu aliahidi katika vitabu vyake na juu ya ndimi za Mitume wake malipo mazuri kwa anayewafuata."},{"id":3162,"sura":19,"from_aya":88,"to_aya":95,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"88. Na wao ati walisema kuwa Arrahmani (Mwingi wa rehema) alijifanyia mwana! 89. Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno! 90. Zinakaribia mbingu kulipuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande. 91. Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani (Mwingi wa rehema) ana mwana. 92. Wala Arrahmani (Mwingi wa rehema) hafailii kujichukulia mwana. 93. Hapana yeyote aliyemo mbinguni na ardhini isipokuwa atamjia Arrahmani (Mwingi wa rehema) kuwa ni mja wake. 94. Yeye hakika amewadhibiti na amewahesabu sawasawa. 95. Na kila mmoja wao atamjia Siku ya Qiyama peke yake. "},{"id":3163,"sura":19,"from_aya":88,"to_aya":88,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{88} Na huku ni kuonyesha ubaya zaidi na kuchukiza kwa kauli ya wanaofanya ukaidi na ukanushaji, ambao walidai kuwa Mwingi wa rehema alijifanyia mwana. Kama vile kauli ya Wakristo wanaosema: Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu, na Mayahudi wanaosema: Uzeir ni mwana wa Mwenyezi Mungu, na washirikina wanaosema: Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ametukuka kukutuka kukubwa juu ya maneno yao hayo."},{"id":3164,"sura":19,"from_aya":89,"to_aya":91,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{89-91} \"Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno!\" Na kwa sababu yake, \"Zinakaribia mbingu\" pamoja na ukubwa wake na uthabiti wake, \"kulipuka kwa hilo,  na ardhi kupasuka\" kwa sababu yake \"na milima kuanguka vipande vipande.\" Yaani, kwa sababu ya madai haya mabaya mno, viumbe hawa wanakaribia kupatwa na haya yaliyotajwa."},{"id":3165,"sura":19,"from_aya":92,"to_aya":92,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{92} Na hali ni kwamba \"Arrahmani (Mwingi wa rehema) hafailii kujichukulia mwana\" Kwa maana, Yeye kujichukulia mwana kunaashiria kwamba ana upungufu na anahitaji hilo, ilhali Yeye ndiye Mkwasi, Msifika. Na mwana pia ni wa aina sawa na baba yake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hana yeyote anayefanana naye, wala aliye sawa naye, wala anayelingana naye."},{"id":3166,"sura":19,"from_aya":93,"to_aya":93,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{93} \"Hapana yeyote aliyemo mbinguni na ardhini isipokuwa atamjia Arrahmani (Mwingi wa rehema) kuwa ni mja wake.\" Yaani, mdhalilifu, huku amefuata amri, bila ya kuasi chochote, wala kukataa. Sawa awe Malaika, au wanadamu, au majini au wengineo, wote hao wanamilikiwa na kuendeshwa naye, na hawana chochote katika umiliki wake, wala katika uendeshaji. Basi vipi atakuwa na mwana ilhali hii ndiyo hali yake na ukuu wa ufalme wake?"},{"id":3167,"sura":19,"from_aya":94,"to_aya":94,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{94} \"Yeye hakika amewadhibiti na amewahesabu sawasawa.\" Yaani elimu yake ilivizunguka viumbe vyote, wakazi wa mbinguni na ardhini, na akawahesabu na akahesabu matendo yao. Kwa hivyo, hapotezi, wala hasahau, wala hakifichikani kwake chochote cha kufichikana."},{"id":3168,"sura":19,"from_aya":95,"to_aya":95,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{95} \"Na kila mmoja wao atamjia Siku ya Qiyama peke yake\"\nbila ya watoto, wala mali, wala wasaidizi, na hayakuwa pamoja naye isipokuwa matendo yake tu, kisha Mwenyezi Mungu atamlipa vikamilifu hesabu yake. Ikiwa ni heri, basi itakuwa heri. Na ikiwa ni maovu, basi yatakuwa maovu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Na hakika mmetujia wapweke kama tulivyowaumba mara ya kwanza.\""},{"id":3169,"sura":19,"from_aya":96,"to_aya":96,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"96. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Arrahmani (Mwingi wa rehema) atawajaalia mapenzi."},{"id":3170,"sura":19,"from_aya":96,"to_aya":96,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{96} Hii ni miongoni mwa neema zake juu ya waja wake ambao waliunganisha kati ya imani na matendo mema, nayo ni kuwa aliwaahidi kwamba atawapa mapenzi katika nyoyo za vipenzi wake na wakazi wa mbinguni na ardhini. Na ikiwa wana mapenzi katika nyoyo hizo, mengi ya mambo yao yatawawia mepesi, na watapata heri nyingi, dua mbalimbali, mwongozo, kukubaliwa, na uongozi. Na ndiyo maana ikaja katika Hadithi sahihi kuwa: \"Hakika Mwenyezi Mungu anapompenda mja, anamnadi Jibril: Hakika Mimi ninampenda fulani, kwa hivyo mpende. Kwa hivyo Jibril anampenda, kisha ananadi kwa wakazi wa mbinguni: Hakika Mwenyezi Mungu anampenda fulani, kwa hivyo mpendeni, basi na watu mpendeni, kwa hivyo, wanampenda wakazi wa mbinguni, kisha akaandikiwa kukubaliwa duniani.\" Na Mwenyezi Mungu aliwafanyia mapenzi, kwa sababu walimuenzi na kumpenda, kwa hivyo akawafanya kupendwa na walio karibu zaidi naye, vipenzi wake."},{"id":3171,"sura":19,"from_aya":97,"to_aya":98,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"97. Na hakika tumeifanya nyepesi (Qur'ani) kwa ulimi wako, ili uwabashirie kwayo wachamungu, na uwaonye kwayo kaumu wagumu mno. 98. Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao. Je, unawaona hata mmoja katika wao au unasikia hata mnong'ono wao? "},{"id":3172,"sura":19,"from_aya":97,"to_aya":97,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{97}  Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu neema yake, na kwamba ameirahisisha Qur-ani hii Tukufu kwa ulimi wa Mtume Muhammad rehema na amani za Mwenyezi mungu zimshukie. Alirahisisha maneno yake na maana zake, ili yafikiwe malengo yaliyokusudiwa kwayo na kufaidika nayo, \"ili uwabashirie kwayo wachamungu\" kwa kuwatia moyo juu ya kinachobashiriwa kama vile thawabu ya haraka na ya baadaye, na kutaja sababu zinazolazimu kubashiriwa. \"Na uwaonye kwayo kaumu wagumu mno,\" katika batili yao, wenye ukafiri mkubwa mno, basi uwaonye ili hoja isimame juu yao, na ili njia ya sawasawa iwabainikie, kwa hivyo aangamie mwenye kuangamia kwa hoja iliyo wazi, na aishi mwenye kuishi kwa hoja ulio wazi."},{"id":3173,"sura":19,"from_aya":98,"to_aya":98,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{98} Kisha akawatishia kwa namna alivyowaangamiza wale waliokadhibisha kabla yao, akasema, \"Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao?\" Kama vile kaumu ya Nuhu, na 'Adi, na Thamud, na Firauni, na wengineo miongoni mwa wakaidi waliokadhibisha walipoendelea kuvuka mipaka, Mwenyezi Mungu akawaangamiza, kwa hivyo hakuna yeyote miongoni mwao aliyesalia nyuma. \"Je, unawaona hata mmoja katika wao au unasikia hata mnong'ono wao?\" Yaani, hakusalia yeyote miongoni mwao wala athari yao. Bali habari zao tu ndizo zilibakia ili ziwe ni mazingatio kwa wanaozingatia, na majina yao yakabaki kuwa ni khutba kwa wanaozingatia. Vile vile ili mazungumzo yao ya usiku yawe ni mawaidha kwa wasikilizao mawaidha."},{"id":3174,"sura":19,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya surat Maryamu na Sifa njema na shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu."},{"id":3175,"sura":19,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}