{"result":[{"id":4284,"sura":30,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsir ya Surat Ar-Rum"},{"id":4285,"sura":30,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Nayo iliteremka Makka"},{"id":4286,"sura":30,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu."},{"id":4287,"sura":30,"from_aya":1,"to_aya":7,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Alif Lam Mim 2. Warumi wameshindwa. 3. Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda. 4. Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. 5. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwingi kurehemu. 6. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini wengi wa watu hawajui. 7. Wanajua hali ya dhahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera. "},{"id":4288,"sura":30,"from_aya":1,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1 - 5} Waajemi na Warumi wakati huo walikuwa miongoni mwa nchi zenye nguvu zaidi duniani, na kulikuwa na vita na mapigano kati yao ambayo huwa kati ya nchi zinazokaribiana kwa nguvu. Waajemi walikuwa washirikina walikuwa wakiabudu moto, nao Warumi walikuwa watu wa Kitabu ambacho kilikuwa Taurati na Injili, na walikuwa karibu na Waislamu kuliko Waajemi, [kwa hivyo waumini] walikuwa wakitaka kwamba wao wawashinde Waajemi. Nao washirikina kwa sababu ya kushirikiana kwao na Waajemi katika ushirikina walikuwa wakipenda kwamba Waajemi wawashinde Warumi. Kwa hivyo Waajemi wakawashinda juu ya Warumi kwa ushindi ambao haukuumaliza ufalme wao, lakini ulifikia tu sehemu iliyokuwa karibu zaidi nao. kwa washirikina wa Makka wakafurahia hilo na Waislamu wakahuzunika. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaambia, na kuwaahidi kwamba Warumi watashinda Waajemi, \"Katika miaka michache\" tisa au minane na mfano wake, kwa muda usiozidi miaka kumi wala haipungui chini ya miaka mitatu. \"Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake.\" Kwa hivyo, ushindi na nusura hautokani tu kwa kuwepo kwa sababu zake. Bali ni lazima ufungamane na mapitisho ya Mwenyezi Mungu na kadari yake. \"Na siku hiyo;\" yaani, siku ambayo Warumi watawashinda Waajemi, \"Waumini watafurahi.\" \"Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye.\" Yaani, watafurahia ushindi wao dhidi ya Waajemi, hata kama kila wote wawili ni makafiri, lakini baadhi ya uovu ni rahisi kuliko mwingine. Nao washirikina watahuzunika siku hiyo. \"Naye ndiye Mwenye nguvu\" ambaye ana nguvu ambayo kwayo aliwashinda viumbe wote; humpa ufalme amtakaye, na humwondolea ufalme amtakaye, na humtukuza amtakaye, na humuangusha umtakaye. \"Mwingi wa kurehemu\" waja wake waumini, ambapo amewawekea sababu zinazowafanya wafurahi na kuwasaidia zaidi ya namna ambayo hawakuwa wanatarajia."},{"id":4289,"sura":30,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} \"Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake.\" Kwa hivyo kuweni na yakini na hilo, na uhakika, na jueni kwamba lazima litatokea. Wakati aya hizi, ambazo zina ahadi hii, zilipoteremka, Waislamu walizisadiki, lakini washirikina wakazikufuru, kiasi kwamba baadhi ya Waislamu na baadhi ya washirikina waliwekeana rehani kwa kipindi cha miaka fulani wakichopimiana. Na muda ambao Mwenyezi Mungu aliuweka ulipofika, Warumi wakawashinda Waajemi, na wakawahamisha kutoka katika nchi yao waliyokuwa wamechukua kutoka kwao, na ahadi ya Mwenyezi Mungu ikatimia. Na hili ni katika mambo ghaibu ambayo Mwenyezi Mungu alijulisha kutokea kwake kabla hayajatokea, na yakatokea katika zama za wale ambao Mwenyezi Mungu alijulisha kwamba yatatokea katika wakati wao. \"Lakini wengi wa watu hawajui\" ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Na ndiyo maana lipo kundi miongoni mwao wanaokadhibisha ahadi yake na Ishara zake."},{"id":4290,"sura":30,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Na hawa ambao hawajui undani wa mambo na matokeo yake, lakini \"Wanajua tu hali ya dhahiri ya maisha ya dunia\" Wanaangalia tu sababu, na wanakuwa na uhakika kwamba litatokea jambo hilo ambalo kulingana na wao zimeshapatikana sababu za kutokea kwake, na wanakuwa na uhakika kwamba haliwezi kutokea jambo ambalo hawajaona sababu zake zozote zinazolazimu kutokea kwake. Wao wanasimamia kwenye sababu za mambo tu, na hawaangalii yule anayezisababisha na kuziendesha. \"Na wameghafilika na Akhera.\" Nyoyo zao, matamanio yao na matashi yao yameielekea dunia na matamanio yake na pumbao zake. Kwa hivyo wakatenda kwa ajili ya hayo, na wakayfanyia juhudi, na wakaja nayo na wakaondoka nayo, na akaisahau Akhera; kwa hivyo akawa hata haitamani Pepo wala hahofu na kuuogpa moto, wala haimtishi na kumsumbua kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu na kukutana naye. Na hii ni alama ya kuwa mtu wa mashakani, na sababu yake kuu ni kughafilika na Akhera. Ni katika maajabu kwamba kundi hili la watu, ambao wengi wao wamefikia kiwango cha ufahamu na akili katika sura ya nje ya kiulimwengu kiwango ambacho kinachanganya akili za na kuzishangaza ufahamu mkubwa, na wakaovumbua maajabu ya kiatomiki na kiumeme na vipando vya juu ya ardhi, baharini, na ndege za angani, ambazo walishinda kwazo, na wakasimama wazi na wakajiona na akili zao, na wakaona wengine kwamba hawana uwezo wa kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwawezesha wao, kwa hivyo wakawatazama kwa jicho la dharau, nao pamoja na hayo ndiyo wajinga zaidi ya watu wote katika mambo ya dini yao, na walioghafilika zaidi katika maisha yao ya baada ya kufa, na wasiojua zaidi matokeo yake. Watu wenye ufahamu wa kupenya waliwaona wakiyumbayumba katika ujinga wao, wakitangatanga katika upotovu wao, na wakasitasita katika batili yao, wakamsahau Mwenyezi Mungu, naye akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio waliotoka nje ya mipaka. Kisha wakatazama yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa, na kuwapa uwezo juu yake kama vile fikira za ndani mno za kidunia na mambo yake ya dhahiri, lakini wakanyimwa akili ya juu, kwa hivyo wakajua kuwa jambo hilo ni la Mwenyezi Mungu na kwamba hukumu ni yake katika waja wake; haikuwa isipokuwa ni kuwezesha kwake au kuwaachilia mbali. Kwa hivyo, wakamhofu Mola wao Mlezi na wakamuomba awatimizie yale aliyowatunuku ya nuru ya akili na imani ili waweze kumfikia na waingie katika medani yake. Mambo haya, lau kuwa yaliunganishwa na imani na yakajengwa juu yake; basi yangezaa ustaarabu wa hali ya juu na maisha mazuri. Lakini kwa vile mengi yake yalijengwa juu ya kutokuamini Mwenyezi Mungu; hayakuzaa isipokuwa kuzorota kwa maadili na sababu za kupotelea mbali kuangamia."},{"id":4291,"sura":30,"from_aya":8,"to_aya":10,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"8. Je, hawajifikirii nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo ndani yake isipokuwa kwa Haki na kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukufuru kuwa watakutana na Mola wao Mlezi. 9. Je, hawatembei katika ardhi wakaona ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao, na wakaitimbua ardhi na wakaistawisha zaidi kuliko walivyoistawisha wao. Na Mitume wao wakawajia na ushahidi wa wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini wenyewe walikuwa wakijidhulumu nafsi zao. 10. Kisha ulikuwa mwisho wa wale waliofanya ubaya ni mbaya zaidi kwa sababu  walizikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawa wanazifanyia stihizai. "},{"id":4292,"sura":30,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} Yaani, je, hawakutafakari hawa waliokanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu na kukutana naye \"nafsi zao?\" Kwani katika nafsi zao, zimo ishara ambazo wanajua kwazo kwamba yule aliyewaumba baada ya kutokuwepo kwao, atawarudisha baada ya hayo, na kwamba yule aliyewahamisha kwa awamu kutoka kwenye manii hadi kwenye damu iliyoganda hadi kwenye pande la nyama hadi wakawa wanadamu aliyepuliziwa roho ndani yake, hadi akawa mtoto mdogo hadi akawa kijana hadi akawa mzee hadi akawa mkongwe haifai kuwaacha bure na kuwapuuza; hawakatazwi wala hawaamrishwi, wala hawalipwi mazuri wala hawaadhibiwi. \"Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake isipokuwa kwa Haki.\" Yaani ili awajaribu ni nani miongoni mwenu ndiye mwenye vitendo vizuri zaidi \"na kwa muda maalumu.\" Yaani, uliowekwa kubakia hadi muda ambao dunia itaisha na Kiyama kuja, na ardhi itabadilishwa iwe ardhi nyingine na hata mbingu. \"Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukataa kuwa watakutana na Mola wao Mlezi.\" Na ndiyo maana hawakujiandaa kwa ajili ya kukutana naye, wala hawakuwasadiki Mitume wake waliojulisha juu yake."},{"id":4293,"sura":30,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} Ukafiri huu hautokani na ushahidi wowote, bali ushahidi wa uhakika unaonyesha kuwepo ufufuo na malipo, na ndiyo maana akatanabahisha kwamba wasafiri katika ardhi na wazingatie matokeo ya wale waliokadhibisha Mitume wao na wakaasi amri yao, ambao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko hawa, na wana athari kubwa zaidi juu ya ardhi, kama vile kujenga makasri na majengo ya kifahari, na ambao walipanda miti na mimea, na mitiririko ya mito. Lakini nguvu zao hazikuwafaa kitu, na athari zao hazikuwafaa wakati walipowakadhibisha Mitume wao waliowajia na hoja zilizo wazi zinazoonyesha haki na usahihi wa yale waliyowaletea. Kwani hawa wanapoangalia athari za wale, hawatapata chochote isipokuwa umma waliotoweka, na viumbe walioangamizwa, na nyumba zilizokuwa ukiwa baada yao, na utajo mbaya unaoendelea kutoka kwa viumbe. Na haya ndiyo malipo yaliyoharakishwa, na mfano tu wa adhabu ya Akhera na mwanzo wake. Na umma hawa wote walioangamizwa, Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu kwa maangamizo hayo, bali wao wenyewe walijidhulumu nafsi zao na wakajisababishia kuangamizwa."},{"id":4294,"sura":30,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} \"Kisha ulikuwa mwisho wa wale waliofanya ubaya.\" Yaani, wale wabaya \"ni mbaya zaidi\" ya kutisha, \"kwa sababu kuzikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawa wanazifanyia stihizai.\" Hii ni adhabu ya ubaya wao na dhambi zao. Kisha kejeli hiyo na kukadhibisha huko kulikuwa ni sababu ya adhabu kubwa zaidi na mifano mibaya zaidi."},{"id":4295,"sura":30,"from_aya":11,"to_aya":16,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"11. Mwenyezi Mungu huanzisha uumbaji, tena akaurudisha mara ya pili, na kisha mtarejeshwa kwake. 12. Na siku itakaposimama Saa ya Kiama, wahalifu watakata tamaa. 13. Wala hawatakuwa na waombezi wowote miongoni mwa wale waliokuwa wakiwashirikisha na Mwenyezi Mungu; na wao wenyewe watawakataa hao washirikishwa wao. 14. Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama, siku hiyo watatengana. 15. Ama wale walioamini na wakatenda mema, watafurahishwa katika Bustani. 16. Na ama wale waliokufuru na wakazikanusha Ishara zetu na mkutano wa Akhera, hao basi watahudhurishwa katika adhabu. "},{"id":4296,"sura":30,"from_aya":11,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11 - 13} Mwenyezi Mungu anatujulisha kwamba Yeye ndiye pekee anayeanzisha uumbaji wa viumbe, kisha akavirudisha. Kisha kwake watarejeshwa baada ya kurudishwa kwao, ili awalipe kwa vitendo vyao. Ndiyo maana akataja malipo ya watu waovu, kisha malipo ya watu wema. Akasema, \"Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama,\" na watu wasimame mbele ya Mola Mlezi wa walimwengu wote [na wakione] Kiyama kwa macho yao wenyewe, siku hiyo \"wahalifu watakata tamaa\" juu ya kila heri, na hilo ni kwa sababu hawakuitangulizia siku hiyo isipokuwa uhalifu, ambao ni madhambi kama vile ukafiri, ushirikina na maasi. Kwa hivyo, walipotanguliza sababu za adhabu, na hawakuzichanganya na chochote katika sababu za kulipwa mazuri, wakakata tamaa, wakafilisika, na yakawapotea yale waliyokuwa wakiyazua ya kunufaishwa na washirika wao, na kwamba watawafanyia uombezi. Ndiyo maana akasema, \"Wala hawatakuwa na waombezi wowote miongoni mwa wale waliokuwa wakiwashirikisha na Mwenyezi Mungu; na wao wenyewe watawakataa hao washirikishwa wao.\" Hao washirikina watajitenga mbali na wale ambao wao wenyewe waliwashirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu, na pia wale walioabudiwa watajitenga nao, na watasema: Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi."},{"id":4297,"sura":30,"from_aya":14,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14 - 16} Na siku hiyo watu wema na wabaya watatengana, kama vile matendo yao yalivyotengana katika dunia hii. \"Ama wale walioamini na wakatenda mema,\" waliamini kwa nyoyo zao na wakasadikisha hilo kwa vitendo vizuri \"watafurahishwa katika Bustani,\" yenye kila aina ya mimea na kila aina ya vitu vinavyotamaniwa. Humo watafurahishwa kwa chakula kitamu, vinywaji, wanawali warembo, watumishi, watoto, sauti za kuimba, kusikia maneno mazuri, na mandhari ya ajabu, harufu za kupendeza, furaha na raha ambazo hakuna mtu anayeweza kuzielezea. \"Na ama wale waliokufuru\" na wakakadhibisha neema zake, na wakakabiliana nazo kwa kuzikufuru, \"na wakazikadhibisha Ishara zetu\" ambazo Mitume wetu waliwaletea, \"hao basi watahudhurishwa katika adhabu.\" Jahannam itawazunguka kwa pande zao zote, na adhabu iumizayo itafika kwenye nyoyo zao, na Moto wa Jahannam utabambua nyuso zao, na kukata matumbo yao. Kwa hivyo tofauti kati ya makundi haya mawili iko wapi? Na uko wapi usawa kati ya wenye kufurahishwa na wenye kuadhibiwa?"},{"id":4298,"sura":30,"from_aya":17,"to_aya":19,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"17. Basi Subhanallah (Mtakaseni Mwenyezi Mungu) jioni na asubuhi. 18. Na sifa zote njema ni zake katika mbingu na ardhi, na alasiri na adhuhuri. 19. Hukitoa kilicho hai kutokana na kilichokufa, na hukitoa kilichokufa kutokana na kilicho hai. Na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Na kama hivyo ndivyo mtavyofufuliwa. "},{"id":4299,"sura":30,"from_aya":17,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17 - 18} Huku ni kujulisha juu ya kutakasika kwake mbali na ubaya na upungufu, na utakatifu wake ambao hakuna yeyote anayefanana naye katika kiumbe wake, na kuwaamrisha waja wake wamtakase jioni na asubuhi, na alasiri na adhuhuri. Nyakati hizi tano ndizo nyakati za Swala tano, ambazo Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waja wake kumtakasa ndani yake na kumsifu. Zinaingia ndani yake swala za wajibu kama vile hizo swala tano, na mambo ya kupendekezwa kama vile nyiradi za asubuhi na jioni, na baada ya swala, na pia swala za hiari zinazohusiana nazo. Kwa sababu nyakati hizi ambazo Mwenyezi Mungu alizichagua kwa ajili ya swala za faradhu ndizo nyakati bora zaidi. Kwa hivyo, kumtakasa, kumsifu ndani yake, na kuabudu ndani yake ni bora zaidi kuliko nyakati nyinginezo. Na ikiwa ibada haijumuisha kusema: Ametakasika Mwenyezi Mungu, basi kuifanya iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu kunakuwa kwa kumtakasa Mwenyezi Mungu kwa vitendo vinavyoonyesha kwamba hana mshirika yeyote katika ibada, au yeyote katika kiumbe kustahiki kile anachostahiki Mwenyezi Mungu cha kukusudiwa Yeye tu na kutubia kwake."},{"id":4300,"sura":30,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} \"Hukitoa kilicho hai kutokana na kilichokufa\" kama vile anavyotoa mche katika udongo uliokufa, na masuke kutoka katika punje, mti kutoka katika kokwa, na kifaranga kutoka katika yai, na Muumini kutoka kwa kafiri... na mifano ya hayo. \"Na hukitoa kilichokufa kutokana na kilicho hai\" kinyume na ilivyotajwa. \"Na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake\" mvua inapoiyeshea hali ya kuwa imekufa na imetulia tuli. Hapo, inasisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri. \"Na kama hivyo ndivyo mtavyofufuliwa\" kutoka makaburini mwenu. Huu ni ushahidi wa uhakika na uthibitisho wa wazi kwamba aliyeihuisha ardhi baada ya kufa kwake atawahuisha wafu. Hakuna tofauti yoyote katika kutazama kwa akili kati ya mambo haya mawili, na hakuna sababu yeoye ya kulikataa moja yake pamoja na kuona wazi wazi uwezekano wa linginelo."},{"id":4301,"sura":30,"from_aya":20,"to_aya":21,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"20. Na katika Ishara zake ni kuwa aliwaumba kwa udongo. Kisha mmekuwa watu mliotawanyika kote kote. 21. Na katika Ishara zake ni kuwa aliwaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye ameweka mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaotafakari. "},{"id":4302,"sura":30,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Huu ndio mwanzo wa kuorodheshwa kwa ishara zake zinazoonyesha upekee wake katika uungu, ukamilifu wa ukuu wake, utekelezekaji wa mapenzi yake, na nguvu ya uweza wake, na uzuri wa matendo yake, na upana wa rehema yake na ihsani yake. Alisema, \"Na katika Ishara zake ni kuwa aliwaumba kwa udongo\" kwa kuumba asili ya dhuriya, Adam, amani iwe juu yake. \"Kisha mmekuwa watu mliotawanyika kote kote.\" [Yaani, Yeye ndiye aliyewaumba nyinyi kutokana na asili moja na kiini kimoja], na akawaeneza katika pande mbalimbali za ardhi na sehemu zake. Katika hayo zimo ishara kwamba aliyewaumba kutokana na asili hii na akawaeneza katika pande zote za ardhi ndiye Mola Mlezi anayeabudiwa, Mfalme anayehimidiwa, Mwingi wa kurehemu, Mwingi wa mapenzi, ambaye atawarudisha kwa kuwafufua baada ya kufa kwenu."},{"id":4303,"sura":30,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} \"Na katika ishara zake\" zinazoonyesha rehema yake na uangalizi wake kwa waja wake na hekima yake kubwa na elimu yake iliyozunguka kila kitu, \"ni kuwa aliwaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu\" wanaolingana nanyi, nanyi mnalingana nao, na wanafanana na nyinyi, nanyi mnafanana nao, \"ili mpate utulivu kwao. Naye ameweka mapenzi na huruma baina yenu,\" kwa sababu ya kuwa ameweka katika ndoa mambo yenye kuleta mapenzi na rehema, kwa hivyo mtu akapata kutoka kwa mke wake starehe, raha, na manufaa, kwa kupatikana watoto, kuwalea, na kupata utulivu kwake; basi huwezi kupata mapenzi na rehema iliyopo kati ya wanandoa kwa mtu yeyote yule. \"Hakika katika haya, bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaotafakari\" ishara za Mwenyezi Mungu, na wanatoka kwa kitu kimoja hadi kingine."},{"id":4304,"sura":30,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"22. Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutofautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuao."},{"id":4305,"sura":30,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} Na wajuao ni watu wenye elimu wanaofahamu mazingatio na wanazizingatia ishara mbalimbali, na ishara katika haya ni nyingi. Miongoni mwa ishara za \"kuumba mbingu na ardhi\" na vilivyomo ndani yake ni kwamba hilo linaonyesha ukuu wa mamlaka ya Mwenyezi Mungu na ukamilifu wa uwezo wake, ambaye aliumba viumbe hawa wakuu, na ukamilifu wa hekima yake. Kwa sababu ya ustadi wake mkubwa na upana wa elimu yake; kwa sababu Muumba lazima ajue alichokiumba. \"Je, asijue yule aliyeumba\" na pia linaonyesha ujumla wa rehema yake na fadhila zake; Kwa sababu ya manufaa makubwa ambayo yako ndani yake, na kwamba yeye ni mwenye utashi anayechagua chochote anachotaka; kwa sababu ya umaalumu ulio ndani yake, na kwamba Yeye pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa na kupwekeshwa; kwa sababu yeye pekee ndiye muumbaji; kwa hivyo ni lazima aabudiwe peke yake. Yote haya ni ushahidi wa kimantiki ambao Mwenyezi Mungu amezitanabahisha akili juu yake, na akaziamrisha zitafakari na kutoa mazingatio ndani yake, \"na\" vile vile katika \"kutofautiana ndimi zenu na rangi zenu\" licha ya wingi wenu na tofauti zenu, licha ya kwamba asili yenu ni moja na sehemu za matamshi yenu ni zile zile, lakini pamoja na hayo, huwezi kupata sauti mbili zinazoafikiana kwa namna zote, wala rangi mbili zinazofanana kwa namna zote, walakini utapata tofauti kati yake, jambo ambalo kwalo wanatofautishwa. Hili linaonyesha ukamilifu wa uwezo wake, utekelezekaji wa mapenzi yake, utunzaji wake waja wake na rehema yake kwao, kwa kuweka utofauti huo; ili kufanana kusitokee, kwa hivyo machafuko yakatokea na kusababisha kukosekana malengo mengi na mahitaji."},{"id":4306,"sura":30,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"23. Na katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na mchana, na kutafuta kwenu fadhila zake. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaosikia."},{"id":4307,"sura":30,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} Yaani, kusikiliza kwa kutafakari na kuelewa maana na ishara zilizo katika hilo. Hakika hayo ni ushahidi wa rehema za Mwenyezi Mungu, kama alivyosema, \"Na ni katika rehema zake amekufanyieni usiku na mchana ili mpate kupumzika humo na ili mtafute katika fadhila zake, na ili mpate kushukuru.\" Na ni katika hekima yake kamili. Kwani hekima yake inahitaji kwamba viumbe vikae kwa utulivu muda fulani ili vipumzike na vijikusanye, na visambae katika wakati fulani kwa ajili ya masilahi yao ya kidini na ya kidunia, na hilo haliwezi kutimia isipokuwa kwa kufuatana mchana na usiku juu yao, na mwenye kutendesha hayo peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa."},{"id":4308,"sura":30,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"24. Na katika Ishara zake huwaonyesha umeme kwa kuwatia hofu na tamaa. Na huwateremshia maji kutoka mbinguni, na kwa hayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu watumiao akili."},{"id":4309,"sura":30,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} Yaani, na katika Ishara zake ni kwamba Yeye huwateremshia mvua ambayo kwayo ardhi na waja vinakuwa hai, na huwaonyesha kabla ya kushuka kwake utangulizi wake kama vile ngurumo za radi na umeme, vinavyohofiwa na pia hutia matumaini. \"Hakika katika hayo, zipo Ishara\" zinazoonyesha ujumla ya ihsani yake, na upana wa elimu yake, na ukamilifu wa ustadi wake, na ukubwa wa hekima yake, na kwamba atawahuisha wafu kama alivyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake, \"kwa watu watumiao akili.\" Yaani, wana akili ambazo kwazo wanaelewa yale wanayoyasikia na kuyaona na kuyahifadhi, na huzitumia kuwa ni ushahidi wa yale ambayo ziliwekwa kwa ajili yake."},{"id":4310,"sura":30,"from_aya":25,"to_aya":27,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"25. Na katika Ishara zake ni kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake. Kisha atakapowaita mwito mmoja tu, hapo mtatoka kwenye ardhi. 26. Na ni vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi. Vyote vinamtii Yeye. 27. Na Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyingine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye mwenye mfano bora zaidi katika mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima. "},{"id":4311,"sura":30,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} Yaani, miongoni mwa ishara zake kubwa ni kuwa mbingu na ardhi zilisimama na zikatulia na kuimarika kwa amri yake, na wala hazikutetereka, na mbingu hazikuiangukia ardhi. Kwani kwa uweza wake mkuu ambao kwa huo alizishikilia mbingu na ardhi zisije kuondoka, basi pia anaweza kwa huo huo anapotaka kuwaita viumbe kwa wito mmoja kutoka katika ardhi, tazama, watatoka nje wote. \"Bila ya shaka kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu.\""},{"id":4312,"sura":30,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} \"Na ni vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi\" vyote ni viumbe vyake na miliki yake, na anaendesha bila ya kizuizi chochote, wala msaidizi, wala mpinzani, na vyote vinatii kwa sababu ya utukufu wake na vinanyenyekea kwa sababu ya ukamilifu wake."},{"id":4313,"sura":30,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} \"Na Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyingine.\" Yaani, kuumba viumbe upya baada ya kufa kwao, \"ni jepesi zaidi kwake\" kuliko kuanzisha kuwaumba. Na hili ni kulingana na bongo na akili. Kwani ikiwa Yeye ni muweza wa kuanzisha ambako nyinyi mnakiri hilo, basi ana uwezo wa kurudisha, ambako ni rahisi zaidi na kunakofailia zaidi kuaminiwa. Na alipotaja baadhi ya ishara zake kubwa ambazo kwazo wenye kuzingatia wanazingatia, na Waumini wanakumbuka, na wanapata ufahamu wale walioongoka, akataja amri kubwa na mahitaji makubwa, akasema, \"Naye ndiye mwenye mfano bora zaidi katika mbingu na ardhi.\" Na huo (mfano bora zaidi) ni kila sifa yenye ukamilifu, na ukamilifu unatokana na sifa hiyo, na mapenzi kamili na toba na kurudi kwake kikamilifu ambako kutoka katika nyoyo za waja wake wanaomkusudia yeye tu, na wanamtaja kwa wingi na wakamuabudu. Mfano bora zaidi ndio maelezo yake ya juu kabisa na yale yanayoambatana na hilo. Na ndiyo maana watu wenye elimu walikuwa wakitumia ulinganisho unaofailia zaidi kuhusiana na Muumba. Walikuwa wakisema: kila sifa ya ukamilifu iliyo katika viumbe; basi Muumba wake ndiye anayestahiki zaidi kusifika nayo kwa namna ambayo hakuna yeyote anayeshiriki naye ndani yake. Na kila upungufu ulio katika kiumbe ambao kinawekwa mbali, basi kumuweka Muumba mbali nao kunafailia na kustahili zaidi. \"Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.\" Yaani, ana nguvu kamili na hekima pana, na kwa nguvu zake, aliumba viumbe na akadhihirisha maamrisho, na kwa hekima yake, akaumba sawasawa vile alivyounda na akafanya vizuri aliyafanya kuwa katika sheria."},{"id":4314,"sura":30,"from_aya":28,"to_aya":29,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"28. Amewapigia mfano kutokana na nafsi zenu. Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyowaruzuku, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyoogopana wenyewe kwa wenyewe? Namna hivyo tunazipambanua Aya zetu kwa watu watumiao akili. 29. Bali waliodhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao pasina kujua. Basi ni nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza? Wala hao hawatakuwa na wa kuwanusuru.\" "},{"id":4315,"sura":30,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Huu ni mfano uliopigwa na Mwenyezi Mungu ili kuonyesha ubaya wa ushirikina na uduni wake. Ni mfano kutoka kwa nafsi zenu wenyewe ambao hauhitaji kusafiri na kuondoka na kuwaandaa ngamia. \"Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyowaruzuku.\" Yaani, je, kuna yeyote katika watumwa wenu wa kiume na wa kike anayewashiriki katika riziki zenu, na mkaona kwamba nyinyi na wao ni sawa katika riziki hiyo? \"Mnawaogopa kama mnavyoogopana wenyewe kwa wenyewe?\" Yaani, kama watu huru ambao ni washirika katika uhalisia, ambao wanaogopewa kugawiwa, na kila mmoja wao akachukua mgao wake maalumu? Sivyo hivyo; kwani hakuna hata mmoja katika hao iliyomiliki mikono yenu ya kulia aliye mshirika wenu katika yale aliyowaruzuku Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hilo ni hivyo, hata ingawa si nyinyi mliowaumba na kuwaruzuku, na tena wao pia wanamilikiwa tu kama nyinyi. Basi vipi mnaridhia kumfanyia Mwenyezi Mungu mshirika miongoni mwa viumbe vyake, na kumfanya kuwa katika nafasi yake na kuwa sawa naye katika ibada, na hali nyinyi wenyewe hamridhii kuwa sawa na wale mnaowamiliki? Hili ni miongoni mwa mambo ya kustaajabisha sana, na moja ya mambo yaonyeshayo zaidi upumbavu wa mwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu mshirika, na kwamba alichochukua kuwa ni mshirika nila batili na kitapotelea mbali, hakiwezi kuwa sawa na Mwenyezi Mungu, wala hakistahiki chochote katika ibada. \"Namna hivyo tunazipambanua Aya zetu\" kwa kuzibainisha kwa mifano yake \"kwa watu watumiao akili.\" Na kuelewa uhakika wa mambo na kuujua. Ama yule asiyeelewa; lau angeelezewa Aya kwa undani na akabainishiwa hoja zilizo wazi; hangekuwa na akili ya kuona kile kilicho wazi, wala ufahamu wa kuelewa kile kilichobainishwa. Kwa hivyo, watu wenye akili na ufahamu ndio  wanaoongeleshwa."},{"id":4316,"sura":30,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Ikishajulikana kutokana na mfano huu kwamba anayemfanyia Mwenyezi Mungu mshirika akamuabudu na kumtegemea katika mambo yake, huyo hana haki yoyote katika hayo, basi ni nini kilichomsukuma kufanya jambo hili batili, ambalo ubatili wake uko wazi na uthibitisho wake umedhihirika? Hili lilisababishwa na kufuata kwao matamanio yao, na ndiyo maana akasema, \"Bali waliodhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao pasina kujua.\" Nafsi zao pungufu na ambao upungufu wake umedhihirika na ambazo matamanio yake yamefungamana na mambo ambayo akili ina uhakika kwamba ni mabovu, na pia maumbile ya asili yanayakataa, hayo wanayafanya bila ya elimu yoyote iliyowaelekeza kwayo wala hata hoja iliyowafikisha kwayo. \"Basi ni nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza?\" Yaani, msishangae kutoongoka kwao. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwapoteza kwa dhuluma yao, na hakuna njia yoyote ya kuwaongoa yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza. Kwa sababu hakuna yeyote anayeweza kumpinga Mwenyezi Mungu au kubishana naye katika ufalme wake, \"Wala hao hawatakuwa na wa kuwanusuru;\" neno la adhabu litakapowastahiki, na wakakatikiwa mafungamano yao na njia zao."},{"id":4317,"sura":30,"from_aya":30,"to_aya":32,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"30. Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini kwa unyoofu, ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui. 31. Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na simamisheni Swala, na wala msiwe katika washirikina. 32. Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho. "},{"id":4318,"sura":30,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamrisha kwamba akusudiwe Yeye tu katika kila hali na kuisimamisha Dini yake. Alisema, \"Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini\" ambayo ni Uislamu, Imani, na ihsani, kwa kuelekeza moyo wako, nia yako, na mwili wako katika kusimamisha sheria dhahiri za Dini, kama vile swala, zaka, saumu, Hijja, na mfano ya hayo, na sheria zake zilizofichika, kama vile upendo, hofu, matumaini, kurudi kwa Mwenyezi Mungu, na kufanya kwa uzuri sana sheria zilizo wazi na zilizofichikana; kwa kumwabudu Mwenyezi Mungu ndani yake kana kwamba unamwona. Na ikiwa hamuoni; basi hakika Yeye anakuona. Na hapa Mwenyezi Mungu aliamrisha kuusimamisha uso hasa; kwa sababu kuelekea kwa uso kunafuata kuelekea kwa moyo, na hao mawili yanasababisha mwili pia kufanya juhudi. Na ndiyo maana akasema, \"kwa unyoofu;\" yaani, kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu katika hayo, na kukipa mgongo kila kitu kinginecho. Na jambo hili tulilokuamrisha ndilo \"umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu\" na akaweka katika akili zao uzuri wake, na akawafanya waone yasiyokuwa hilo kuwa ni mabaya. Kwa maana Mwenyezi Mungu ameweka ndani ya nyoyo za viumbe vyote kuzielekea hukumu zote za kisheria zilizo dhahiri na zilizofichikana, na pia akaweka ndani ya nyoyo zao kupenda haki na kuipendelea. Na huu ndio uhakika wa umbile la asili. Na mwenye kutoka katika msingi huu; basi ni kwa sababu ya jambo lililoingia katika umbile lake la asili na likaliharibu, kama alivyosema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, \u201cKila mtoto huzaliwa katika umbile la asili. Kisha wazazi wake wanamfanya kuwa Myahudi, au Mkristo, au Majusi.\u201d \"Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu.\" Yaani, hakuna anayeweza kuwabadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu na akawafanya viumbe katika hali nyingine isipokuwa ile ambayo Mwenyezi Mungu aliwaumbia. \"Hiyo\" ambayo tulikuamrisha \"ndiyo Dini iliyonyooka sawa.\" Yaani, njia iliyonyooka inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na utukufu wake. Kwani, mwenye kuuelekeza uso wake sawasawa kwenye Dini, basi yeye amefuata njia iliyonyooka katika sheria zake zote na njia zake zote, \"Lakini watu wengi hawajui\" Dini hii iliyonyooka sawa, na hata kama wataijua, hawataifuata."},{"id":4319,"sura":30,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} \"Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye\" na hii ndiyo tafsiri ya kusimamisha Dini. Kwani toba ina maana ya moyo kutubia na kuvutiwa kwenye yale yanayompendeza Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hilo linalazimu kwamba mwili utende kulingana na yale yaliyo moyoni, kwa hilo likajumuisha ibada zoye za dhahiri na za ndani, na wala hayo hayatimii isipkuwa kwa kuacha maasi ya dhahiri na ya ndani. Na ndiyo maana akasema, \"Na mcheni Yeye\" Hilo linajumuisha kufanya maamrisho na kuacha makatazo. Na alitaja katika maamrisho swala hasa kwa sababu inaitia kwenye toba na uchamungu, kwa mujibu wa maneno yake Mola Mtukufu, \"na ushike Swala. Hakika Swala inazuilia mambo machafu na maovu.\" Na huku ndiko kumsaidia kwake juu ya uchamungu. Kisha akasema, \"Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa\" Na huku ndiko kumhimiza kwake juu ya kutubu. Na alitaja katika makatazo, katazo la msingi kabisa, ambalo tendo lolote halikubaliki pamoja nalo, nalo ni ushirikina. Akasema, \"Na wala msiwe katika washirikina,\" kwa sababu ushirikina ni kinyume cha toba ambayo roho yake ni kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake kwa namna zote."},{"id":4320,"sura":30,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} Kisha akataja hali ya washirikina na kuonyesha uduni wake na ubaya wake. Akasema, \"Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao,\" ijapokuwa Dini ni moja, ambayo ni kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika ibada. Na washirikina hawa waliigawanya: miongoni mwao wapo wanaoabudu masanamu, na miongoni mwao wapo wanaoabudu jua na mwezi, na miongoni mwao wapo wanaoabudu mawalii (watu walio karibu na Mwenyezi Mungu) na watu wema, na miongoni mwao wapo Mayahudi, na miongoni mwao wapo Wakristo. Na ndiyo maana akasema, \"Na wakawa makundi makundi.\" Yaani, kila kundi miongoni mwa washirikina wakapotea na wakawa washabiki katika kuunga mkono batili waliyo nayo, na kuwapinga wengineo na kuwapiga vita. \"Kila kikundi kinafurahia kilicho nacho\" cha elimu mbalimbali iliyo kinyume na elimu ya Mitume na kwayo wanajihukumu wenyewe kuwa hiyo ndiyo haki na kwamba wengineo wako katika batili. Na katika hilo kuna hatadharisho kwa Waislamu dhidi ya kutawanyika na kutengana makundi makundi, kila kundi likawa linatetea yale waliyo nayo ya haki na batili, kwa hivyo wakawa wamefanana na washirikina katika kugawanyika kwao. Bali Dini ni moja, Mtume ni mmoja, na Mwenyezi Mungu ni mmoja, na katika mambo mengi ya kidini kuna maafikiano baina ya wanachuoni na maimamu, na udugu wa kiimani ulikwisha wekwa na Mwenyezi Mungu na akaufunga vyema kabisa. Basi kwa nini yote haya yanafutwa na unajengwa mgawanyiko na fitina baina ya Waislamu juu ya mambo yaliyofichikana au masuala ya kimatawi yenye utata ambayo kwayo wao kwa wao wanaonana kwamba kila mmoja wao amepotea, na wanajitofautisha baadi yao kutoka kwa wengineo? Je, huu si isipokuwa uchochezi mkubwa wa Shetani na malengo yake makubwa zaidi ambayo kwayo anawapangia njama Waislamu? Je, kujitahidi kuunganisha neno lao na kuondoa tofauti hizi zilizo baina yao zilizojengeka juu ya msingi huo batili, si isipokuwa ndiyo jihadi bora zaidi katika njia ya Mwenyezi Mungu na matendo bora zaidi yanayomuweka mtu karibu na Mwenyezi Mungu? Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoamuru kutubia kwake, na kukawa kutubia huko ni kule kwa hiari, ambako kunakuwa katika hali ya shida, na urahisi, na wingi na dhiki, akataja kutubia kwa kulazimishwa ambako hutokea mtu isipokuwa wakati anapokuwa katika shida na dhiki. Na pindi dhiki hiyo inapomuondokea, anaitupa nyuma ya mgongo wake, lakini toba hii hainufaishi kitu. Akasema:"},{"id":4321,"sura":30,"from_aya":33,"to_aya":35,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"33. Na watu wanapoguswa na madhara, humwomba Mola wao Mlezi huku wanatubu kwake. Kisha akiwaonjesha rehema itokayo kwake, mara kikundi miongoni mwao humshirikisha Mola wao Mlezi. 34. Kwa kuyakufuru yale tuliyowapa. Basi stareheni. Mtakuja jua! Au tumewateremshia hoja ambayo inazungumza juu ya kile walichokuwa wakishirikisha nacho? "},{"id":4322,"sura":30,"from_aya":33,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33 - 34} \"Na watu wanapoguswa na madhara,\" kama vile maradhi au hofu ya kuangamia na mengineyo, \"humwomba Mola wao Mlezi huku wanatubu kwake.\" Na husahau yale waliyokuwa wakimshirikisha nayo katika hali hiyo, kwa sababu wanajua kwao hakuna anayeweza kuondoa madhara isipokuwa Mwenyezi Mungu. Basi \"akiwaonjesha rehema itokayo kwake\" kama vile kuwaponya maradhi yao na huwapa amani kutokana na hofu yao, \"mara kikundi miongoni mwao\" huivunjilia mbali toba hiyo waliyofanya, wakaanza tena kumshirikisha na wale wasio na hifadhi kwao, wala tajiri, masikini, wala tajiri, na yote haya ni kuyakufuru aliyowapa Mwenyezi Mungu na aliyowapa kwa kuwaokoa na kuwaepusha na dhiki na kuwaondolea taabu. Je, hawataitikia baraka hii kubwa kwa shukrani na kuendelea kuwa waaminifu kwake katika hali zote?"},{"id":4323,"sura":30,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} \"Au tumewateremshia hoja\" iliyo dhahiri. Basi hiyo\" hoja \"inazungumza juu ya kile walichokuwa wakishirikisha nacho?\" Na inawaambia: Kuweni imara juu ya ushirikina wenu na endeleeni kuwa na shaka; kwani mliyo juu yake ndiyo Haki, na yale waliyowaitia Mitume ni batili. Basi je, wanayo hoja hiyo ambayo inawafanya kushikamana sawasawa na ushirikina? Ama ushahidi wa kiakili wote na wa kusikia, na vitabu vya mbinguni, na Mitume watukufu, na mabwana wa wanadamu, walikataza kabisa jambo hili, na wakatahadharisha juu ya kufuata njia zake zinazofikisha huko, na wakahukumu kuwa akili na dini ya mwenye kufanya hivyo ni mbovu? Basi ushirikina wa watu hawa hauna hoja yoyote wala uthibitisho, bali ni matamanio tu ya nafsi na uchochezi wa Shetani."},{"id":4324,"sura":30,"from_aya":36,"to_aya":37,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"36. Na tunapowaonjesha watu rehema, huifurahia. Na ukiwasibu ubaya kwa iliyoyatanguliza mikono yao wenyewe, mara wanakata tamaa. 37. Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia amtakaye? Hakika katika hayo, zipo Ishara kwa watu wanaoamini. "},{"id":4325,"sura":30,"from_aya":36,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36 - 37} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu maumbile asili ya watu wengi katika nyakati za mafanikio na shida, kwamba Mwenyezi Mungu anapowaonjesha rehema kutoka kwake, kama vile afya njema, mali, ushindi, na mfano wake; wanayafurahia hayo kwa furaha ya kiburi, si furaha ya shukrani na kujivunia neema ya Mwenyezi Mungu. \"Na ukiwasibu ubaya kwa iliyoyatanguliza mikono yao wenyewe,\" kama vile maasi, \"mara wanakata tamaa\" ya kuondoka kwa ufukara huo, maradhi na mengineyo. Na huu ndio ujinga wao, na kutojua. \"Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia amtakaye?\" Kwa hivyo, halina mahali popote jambo la kukata tamaa baada ya kujua kwamba heri na shari zinatoka kwa Mwenyezi Mungu na kwamba riziki nyingi na chache ni katika mipango yake. Basi ewe mwenye akili usiangalie sababu za mambo tu, bali yaelekeze macho yako kwa aliyeyasababisha mambo hayo, na ndiyo maana akasema, \"Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanaoamini.\" Hao ndio wanaozingatia kwamba Mwenyezi Mungu humkujulia amtakaye na kumkunjia amtakaye, na kwa hayo wanapata kujua hekima ya Mwenyezi Mungu, rehema yake, uwepo wake, na kuivutia mioyo kumwomba Yeye katika mahitaji yote ya riziki."},{"id":4326,"sura":30,"from_aya":38,"to_aya":39,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"38. Basi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni heri kwa wanaotaka uso wa Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waliofaulu. 39. Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnachokitoa kwa Zaka kwa kutaka uso wa Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watakaozidishiwa. "},{"id":4327,"sura":30,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} Yaani, basi mpe jamaa yako wa karibu - kulingana na ukaribu wake na haja yake, - haki yake ambayo Mtunga sheria aliiwajibisha au alihimiza juu yake kama vile kutoa matumizi ya lazima, sadaka, zawadi, wema, salamu, ukarimu, kumsamehe dhambi zake, na kuachilia mbali kuteleza kwake. Na vile vile, mpe masikini aliyetulizwa na umasikini na mahitaji kitu ambacho utamuondolea mahitaji yake hayo na kumzuia kutokana na kuhitaji kwake huko. \"Na msafiri\" mgeni ambaye amekatikiwa hali ya kuwa yuko mbali na nchi yake, ambaye yuko katika hali inayodhaniwa sana kwamba yuko katika ugumu mkubwa, na kwamba hana mali wala mapato yenye kumkimu katika safari yake. Huyu ni tofauti na yule ambaye yuko katika nchi yake. Huyu hata kama hana mali, katika hali nyingi ni lazima anajishughulisha  na kazi ya ufundi au sekta kama hiyo inayoweza kumkidhia mahitaji yake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaweka fungu maalumu la masikini na msafiri katika Zaka. \"Hayo\" ya kuwapa jamaa, masikini, na msafiri \"ni heri kwa wanaotaka\" kwa kitendo hicho \"uso wa Mwenyezi Mungu.\" Yaani, heri nyingi na malipo mengi. Kwa sababu hayo ni miongoni mwa bora ya matendo mema, na yana manufaa yanayowafikia wengine ambayo yaliingia sawasawa mahali pake na ambayo yalifungamana na ikhlasi. Na ikiwa hakuutaka kwayo uso wa Mwenyezi Mungu; basi hayawezi kuwa ni heri kwa mtoaji, hata kama ni heri kwa anayepewa na yenye kumnufaisha, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Hakuna kheri katika mengi ya wanayoshauriana kwa siri, isipokuwa kwa yule anayeamrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu.\" Na maana yake ya kinyume ni kuwa haya yaliyotolewa katika hukumu hii ni mema; kwa sababu ya manufaa yake yanayowafikia wengine, bali mtu afanyaye hayo kwa kutafuta uso wa Mwenyezi Mungu; basi tutakuja mpa ujira mkubwa. Na maneno yake, \"Na hao\" ambao walifanya vitendo hivi na mengineyo kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu, \"ndio waliofaulu\" watakaopata malipo mazuri ya Mwenyezi Mungu na wataokoka kutokana na adhabu yake."},{"id":4328,"sura":30,"from_aya":39,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39} Na alipotaja matendo yanayokusudiwa uso wake, kama vile kutoa kwa ajili ya matumizi; akataja matendo yanayokusudiwa mambo ya kidunia. Akasema, \"Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu.\" Yaani, mlichotoa kutoka katika mali zenu zilizozidi mahitaji yenu, kwa nia ya kuifanya iongezeke, kwa njia ya kumpa mtu ili naye awarudishie kwa zaidi yake; basi malipo ya matendo haya hayaongezeki kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hayana sharti la hilo, ambalo ni ikhlasi. Na mfano wa hilo pia ni matendo yanayokusudiwa kuongeza hadhi ya mtu na kujionyesha kwa watu. Yote haya hayaongezeki kwa Mwenyezi Mungu. \"Lakini mnachokitoa kwa Zaka\" Yaani, mali itakayokutakaseni kutokana na tabia mbaya, itakayosafisha mali zenu kutokana na ubahili, na inaongeza kuzuia mahitaji ya anayepewa. \"kwa kutaka\" kwa hayo \"uso wa Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watakaozidishiwa\" malipo, ambao walichotoa kwa ajili ya matumizi kitazidi kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atakikuza mpaka kiwe kitu kikubwa. Na iliashiria kauli yake, \"Lakini mnachokitoa kwa Zaka\" kwamba kutoa sadaka pamoja na kuwepo na mwenye mahitaji makubwa katika wale walio chini ya yule anayetoa, au ikiwa mtoaji ana deni ambalo bado hajalilipa, naye akatanguliza sadaka mbele ya hayo; basi hiyo sio Zaka ambayo mja atalipwa juu yake. Kitendo chake hiki kinapaswa kuvunjiliwa mbali kwa mujibu wa sheria, kama alivyosema Mwenyezi Mungu kuhusu mwenye kusifiwa: \"Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.\" Kwa hivyo, kutoa mali tu siyo heri, hadi kuwe kwa njia hii, ambayo ni kwa njia ambayo mtoaji anajitakasa."},{"id":4329,"sura":30,"from_aya":40,"to_aya":40,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"40. Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba, kisha akawaruzuku, kisha atawafisha, na kisha atawafufua. Je, yupo yeyote katika hao mnaowashirikisha na Mwenyezi Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye ametakasika, na ametukuka mbali na hayo mnayomshirikisha naye."},{"id":4330,"sura":30,"from_aya":40,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba Yeye peke yake ndiye aliyewaumba, naye ndiye anayewaruzuku, naye ndiye atakayewafisha na kuwahuisha, na kwamba hakuna yeyote katika washirika ambao washirikina wanawaomba anayeshirikiana na Mwenyezi Mungu katika chochote miongoni mwa mambo haya. Basi vipi wanaweza kumshirikiana yule ambaye yuko peke yake katika mambo haya na yule ambaye hana utendaji wowote kwa namna yoyote ile katika hayo? Ametakasika, ametukuka, na yuko juu zaidi ya ushirikina wao huu. Kwa hivyo, hilo halimdhuru kitu, bali msiba wake uko juu yao."},{"id":4331,"sura":30,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"41. Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa yale iliyoyafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonjeshe baadhi ya yale waliyoyatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu."},{"id":4332,"sura":30,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41} Yaani, umekuwa wazi wazi \"Uharibifu barani na baharini\" katika maisha yao, na kuna upungufu ndani yake, na umeingiwa na balaa mbalimbali, na kuna magonjwa na mlipuko wa majanga na mambo mengineyo katika nafsi zao. Hayo ni kutokana na yale yaliyotangulizwa na mikono yao ya matendo mabovu yenye kuharibu maumbile yao. Hayo yaliyotajwa \"ili Mwenyezi Mungu awaonjeshe baadhi ya yale waliyoyatenda.\" Yaani, ili wajue kwamba Yeye ndiye mlipaji wa matendo, basi akawafanyia haraka mfano wa malipo ya matendo yao hapa duniani. \"Huenda wakarejea kwa kutubu\" kutokana na vitendo vyao vilivyowasababishia uharibifu mwingi namna vilivyosababisha, basi hali zao zikaboreshwa, na mambo yao yakanyooka. Ametakasika yule aliyetia neema katika dhiki yake, na akaweka fadhila katika adhabu yake. Sivyo, ikiwa angewaonjesha yote waliyoyachuma, basi hangeacha mnyama yeyote juu ya mgongo wake."},{"id":4333,"sura":30,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"42. Sema: Safirini duniani na muangalie ulikuwaje mwisho wa wale waliotangulia. Wengi wao walikuwa washirikina."},{"id":4334,"sura":30,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} Na amri ya kutembea katika ardhi inajumuisha kutembea kwa miili na kutembea katika nyoyo ili kuangalia na kutafakari mwisho wa wale waliotangulia, \"Wengi wao walikuwa washirikina\" na utapata kwamba mwisho wao ulikuwa mwisho mbaya zaidi, ambayo yalikuwa adhabu ambayo iliwaangamiza, na kufuatwa na shutuma na laana kutoka kwa viumbe vya Mwenyezi Mungu, na fedheha inayoendelea. Kwa hivyo jitahadharini msifanye matendo yao; mkaja fanyiwa mfano wa walivyofanyiwa; kwani, uadilifu wa Mwenyezi Mungu na hekima yake iko katika kila wakati na mahali."},{"id":4335,"sura":30,"from_aya":43,"to_aya":45,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"43. Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini iliyonyooka kabla ya kufika Siku hiyo isiyozuilika, inayotoka kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo watu watatengana. 44. Anayekufuru, basi ukafiri wake utakuwa juu yake mwenyewe. Na anayetenda mema, basi wanazitengezea nafsi zao. 45. Ili awalipe wale walioamini na wakatenda mema kutokana na fadhila yake. Hakika Yeye hawapendi makafiri. "},{"id":4336,"sura":30,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} Yaani, njoo kwa moyo wako na uelekeze uso wako, na jitahidi kwa mwili wako kusimamisha Dini iliyo sawasawa, iliyonyooka, kwa kutekeleza maamrisho yake na makatazo yake kwa bidii na jitihada, na tekeleza mambo yake ya dhahiri na ya siri, na uharakishe kutumia vyema wakati wako, maisha yako, na ujana wako, \"kabla ya kufika Siku hiyo isiyozuilika, inayotoka kwa Mwenyezi Mungu,\" ambayo ni Siku ya Kiyama, ambayo inapokuja, haiwezekani kuirejesha, na wala watendaji hawawezi kuahirishwa ili waendelee kutenda matendo, bali matendo yalishaisha, na hakikubakia isipokuwa kuwalipa watendaji. \"Siku hiyo watu watatengana,\" na watakuja wakiwa mbalimbali huku wametofautiana  ili waonyeshwe matendo yao."},{"id":4337,"sura":30,"from_aya":44,"to_aya":45,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{44 - 45} Basi \"anayekufuru\" miongoni mwao, \"basi ukafiri wake utakuwa juu yake mwenyewe,\" naye mwenyewe ndiye atakayeadhibiwa, na wala hatabeba mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. \"Na anayetenda mema\" miongoni mwa haki za Mwenyezi Mungu, na za waja ambazo ni za wajibu, na zinazopendekezwa, \"basi wanazitengezea nafsi zao.\" Si kwa ajili ya mwingine, na ni akhera yao ambayo wanaiimarisha, na wanajitayarishia kufikia nyumba zake na vyumba vyake, na pamoja na hayo, malipo yao hayatakomea tu kwenye matendo yao, bali Mwenyezi Mungu atawalipa kutokana na fadhila zake kunjufu, na ukarimu wake usio na mipaka malipo ambayo matendo yao hayawezi kufikia. Hayo ni kwa sababu Yeye aliwapenda, na Mwenyezi Mungu anapompenda mja, hummiminia wema wake kwa wingi, na humpa vipawa vya kifahari, na anamneemesha kwa neema za dhahiri na zilizofichika. Na hili ni kinyume na makafiri, hao Mwenyezi alipowachukia mno, akawaadhibu na kuwatesa, lakini hakuwazidishia kama alivyowazidishia wale wa kabla yao. Ndiyo maana akasema, \"Hakika Yeye hawapendi makafiri.\""},{"id":4338,"sura":30,"from_aya":46,"to_aya":46,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"46. Na katika Ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo bishara njema, na ili kuwaonjesha baadhi ya rehema zake, na ili majahazi yaende kwa amri yake; na mtafute kutokana na fadhila yake, na ili mumshukuru."},{"id":4339,"sura":30,"from_aya":46,"to_aya":46,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{46} Yaani, miongoni mwa ishara zinazoonyesha rehema yake na kuwafufuwa kwake wafu, na kwamba Yeye ndiye Mola Mlezi anayeabudiwa na Mfalme Msifiwa, ni kuzituma pepo mbele ya mvua \"ziletazo bishara njema\" kwa kuyatimua mawingu na kuyakusanya, kwa hivyo zikazibashiria nafsi kwa hilo kabla ya kunyesha kwake \"na ili kuwaonjesha baadhi ya rehema zake\" Basi akawateremshia mvua ambayo kwayo nchi na waja vinakuwa hai, na mnaonja katika rehema yake kile mnachojua kwacho kwamba rehema yake ndiyo inayowaokoa waja na kuwaletea riziki, basi mkawa na shauku kubwa ya kuzidisha matendo mema yenye kufungua hazina za rehema. \"na ili majahazi yaende\" baharini \"kwa amri yake\" ya kimajaliwa, \"na mtafute kutokana na fadhila yake\" kwa kujishughulisha na maisha yenu na mambo yenye masilahi kwenu. \"na ili mumshukuru\" aliyewatiishia njia za hayo na akawarahisishia mambo. Na hilo ndilo linalokusudiwa katika neema, kwamba mtu amshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, ili awazidishie katika hizo neema, na azidumishe. Ama kuzikabili neema za Mwenyezi Mungu kwa kukufuru na kufanya maasi, hii ndiyo hali ya mwenye kubadilisha neema za Mwenyezi Mungu kwa ukafiri, na mtihani, na huyo anataka kusababisha neema hiyo kuondoka na kuhama kutoka kwake kwenda kwa mtu mwingine."},{"id":4340,"sura":30,"from_aya":47,"to_aya":47,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"47. Na hakika tulikwisha watuma Mitume kabla yako kwa kaumu zao, na wakawajia kwa hoja zilizo wazi. Tukawaadhibu wale waliofanya uhalifu. Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini."},{"id":4341,"sura":30,"from_aya":47,"to_aya":47,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{47} Yaani, \"Na hakika tulikwisha watuma Mitume kabla yako\" miongoni mwa mataifa yaliyotangulia \"kwa kaumu zao.\" Walipokataa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na wakaikadhibisha haki, kwa hivyo Mitume wao wakawajia wakiwalingania kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na kumkusudia Yeye tu, na kuisadiki haki na kubatilisha yale wanayoyaamini na kutenda ya ukafiri na upotovu, na waliwajia na hoja za wazi na ushahidi wa hayo, lakini hawakuamini na hawakuachana na upotofu wao, \"kwa hivyo, tukawaadhibu wale waliofanya uhalifu\" na tukawanusuru waumini, wafuasi wa Mitume, \"Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.\" Yaani, tulijiwajibishia hilo juu yetu wenyewe, na tukalifanya kuwa moja ya haki zinazopasa kuzitekeleza, na tukawaahidi hilo; na lazima litokee. Basi enyi mnaomkadhibisha Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ikiwa mtaendelea kukadhibisha; mtapatwa na adhabu, na tutamnusuru yeye juu yenu."},{"id":4342,"sura":30,"from_aya":48,"to_aya":50,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"48. Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma pepo zikayatimua mawingu, kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande, basi ukaiona mvua inatoka ndani yake. Anapowafikishia awatakao katika waja wake, mara hao huwa na furaha. 49. Na ingawa kabla ya kuteremshiwa walikuwa wenye kukata tamaa. 50. Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Basi hakika huyo ndiye bila ya shaka mwenye kuhuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu. "},{"id":4343,"sura":30,"from_aya":48,"to_aya":49,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{48 - 49} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu ukamilifu wa uwezo wake na utimilifu wa neema yake kwamba, \"huzituma pepo zikayatimua mawingu\" kutoka ardhini, \"kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande\" yaliyopandana juu kwa juu. \"Basi ukaiona mvua inatoka ndani yake,\" kwa namna ya  matone madogo yaliyotawanyika, na hayateremki maji hayo yote pamoja yakaharibu chochote yanachokifikia. \"Anapowafikishia awatakao katika waja wake, mara hao huwa na furaha,\" wakibashiriana wao kwa wao juu ya kunyesha kwake. Na hilo ni kwa sababu ya mahitaji yao na haja yao kubwa juu yake. Ndiyo maana akasema, \"Na ingawa kabla ya kuteremshiwa walikuwa wenye kukata tamaa,\" kwa sababu ya kuchelewa kwa wakati wa kuja kwake. Na iliponyesha katika hali hiyo, ikawa ina nafasi kubwa sana kwao, na furaha na kuwa na bishara nzuri kwao."},{"id":4344,"sura":30,"from_aya":50,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{50} \"Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake,\" ikasisimka na kututumka, na kuotesha kila namna ya mimea mizuri. \"Basi hakika huyo\" ambaye aliihuisha ardhi baada ya kufa kwake, \"ndiye bila ya shaka mwenye kuhuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu.\" Uwezo wake, Mola Mtukufu, haupingwi na kitu chochote, hata kama ni vigumu mno kwa viumbe wake, na ikawashinda kabisa kuingia katika ufahamu wao, na akili zao zikachanganyikiwa juu yake."},{"id":4345,"sura":30,"from_aya":51,"to_aya":53,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"51. Na tungeutuma upepo na wakauona umekuwa rangi ya manjano, juu ya hayo wangeendelea kukufuru. 52. Kwani wewe hakika huwafanyi maiti wakasikia, wala viziwi wakasikia wito wakishageuka kukupa mgongo. 53. Wala wewe huwaongoi vipofu kutoka katika upotovu wao. Huwasikilizishi isipokuwa wale wanaoziamini Aya zetu. Hao ndio Waislamu, walionyenyekea. "},{"id":4346,"sura":30,"from_aya":51,"to_aya":51,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{51} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu hali ya viumbe na kwamba pamoja na kupewa neema hizi kama vile; kuifufua ardhi baada ya kufa kwake na kueneza rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: kama tungeliuteremshia mmea huu unaotokana na mvua na juu ya mimea yao upepo wenye madhara, wenye kuharibu au kupunguza, \"wakauona umekuwa rangi ya manjano\" tayari umekaribia kuharibika, \"juu ya hayo wangeendelea kukufuru\" na wakasahau neema zilizopita na wakakimbilia kufuru! Hawa hayawafai mawaidha wala kukemewa."},{"id":4347,"sura":30,"from_aya":52,"to_aya":52,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{52} \"Kwani wewe hakika huwafanyi maiti wakasikia, wala viziwi wakasikia wito\" na katika hali inayofailia zaidi \"wakishageuka kukupa mgongo.\" Kwani vizuizi vimeshapatikana kwao vinavyowazuia kufuata na kusikia kwenye manufaa, kama vile kuwepo kwa vizuizi hivi vilivyotajwa hapo juu vinavyozuia kusikia sauti ya kihisia."},{"id":4348,"sura":30,"from_aya":53,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{53} \"Wala wewe huwaongoi vipofu kutoka katika upotovu wao\" kwa sababu hawakubali kuonyeshwa kwa sababu ya upofu wao. Hawana uwezo wowote wa kufanya hilo. \"Huwasikilizishi isipokuwa wale wanaoziamini Aya zetu. Hao ndio Waislamu, walionyenyekea.\" Hao ndio wanaonufaika na kusikiliza uwongofu, ndio wanaoziamini Ishara zetu kwa nyoyo zao, na wanaofuata amri zetu, na wanaojisalimisha kwetu; Kwa sababu wana sababu kubwa sana inayowafanya kukubali nasaha na mawaidha, nayo ni utayari wao wa kuamini kila ishara ya Mwenyezi Mungu, na utayari wao wa kutekeleza amri na makatazo yoyote ya Mwenyezi Mungu wanayoweza kuyafanya."},{"id":4349,"sura":30,"from_aya":54,"to_aya":54,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"54. Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba kutokana na udhaifu, kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye ajuaye zaidi, Mwenye uweza wote."},{"id":4350,"sura":30,"from_aya":54,"to_aya":54,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{54} Mungu Mwenyezi anajulisha juu ya upana wa elimu yake, ukuu wa uwezo wake, na ukamilifu wa hekima yake, kwamba alianzisha uumbaji wa wanadamu kutokana na udhaifu, ambao ni awamu za kwanza za kuumbwa kwake kutokana na manii hadi kwenya pande la damu hadi kwenye pande la nyama hadi akawa mnyama ndani ya matumbo ya uzazi hadi akazaliwa katika umri wa utoto, na wakati huo alikuwa dhaifu sana bila ya kuwa na nguvu na uwezo. Kisha Mwenyezi Mungu akaendelea kuongeza nguvu zake kidogo kidogo, hadi akafikia umri wa ujana, na nguvu zake zikawa sawasawa, basi nguvu zake za dhahiri na zilizofichwa zikakamilika. Kisha akatoka katika awamu hii na akarudi kuwa dhaifu, akawa mzee mkongwe. \"Anaumba atakavyo\" kulingana na hekima yake. Na katika hekima yake ni kwamba anamuonyesha mja udhaifu wake, na kwamba nguvu zake zimezungukwa na madhaifu mawili, na kwamba hana chochote kutokana na nafsi yake isipokuwa upungufu, na lau si kwa sababu ya Mwenyezi Mungu kumtia nguvu, asingepata nguvu na uwezo, na kama nguvu zake zingeendelea kuongezeka, basi angevuka mipaka na akaasi sana, na ili mja ajue ukamilifu wa nguvu za Mwenyezi Mungu, ambazo bado zinaendelea. Anaumba kwazo vitu, na anaendesha kwazo mambo, na wala haziathiriwi na uchovu, wala udhaifu, wala upungufu kwa njia yoyote ile."},{"id":4351,"sura":30,"from_aya":55,"to_aya":57,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"55. Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama, wahalifu wataapa kwamba hawakukaa duniani isipokuwa saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakipotoshwa. 56. Na wale waliopewa elimu na Imani watasema: Hakika nyinyi mlikwisha kaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu mpaka Siku ya kufufuliwa. Basi hii ndiyo Siku ya kufufuliwa! Lakini nyinyi mlikuwa hamuijui. 57. Basi Siku hiyo hautawafaa wale waliodhulumu udhuru wao, wala haitatakiwa toba yao. "},{"id":4352,"sura":30,"from_aya":55,"to_aya":55,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{55} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu Siku ya Kiyama na upesi wa kuja kwake, na kwamba itakapofika Saa, \"wahalifu\" wataapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba \"hawakukaa duniani isipokuwa saa moja tu.\" Watafanya hivyo, ili wakubaliwe udhuru labda udhuru huo uwafae, na kwamba muda wa maisha ya dunia ulikuwa mfupi. Na kwa vile kauli yao hiyo ni uongo na haina uhakika wowote. Yeye Mtukufu akasema, \"Hivyo ndivyo walivyokuwa wakipotoshwa\" walipokuwa duniani, wakaiacha haki waliyokuja nayo Mitume. Na katika Akhera walikataa jambo linalohisiwa ambalo ni kukaa kwa muda mrefu katika dunia hii. Hii ndiyo tabia yao mbaya, na mja atafufuliwa katika hali aliyofia."},{"id":4353,"sura":30,"from_aya":56,"to_aya":56,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{56} \"Na wale waliopewa elimu na Imani watasema;\" yaani, Mwenyezi Mungu aliwaneemesha mawili hayo na yakawa ndiyo sifa yao: kujua haki na kuwa na imani inayolazimu kuipendelea haki. Na ikiwa wanaijua haki na kuipendelea, basi maneno yao lazima yalingane na hali halisi ya mambo, na inayofailia hali zao. Ndiyo maana wakasema kweli, \"Hakika nyinyi mlikwisha kaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu\" aliyowaandikia \"mpaka Siku ya Kiyama.\" Yaani, mliishi maisha umri ambao mwenye kukumbuka anakumbuka, na mwenye kuzingatia anazingatia juu yake mpaka ufufuo ulipotokea, na mkafikia hali hii. \"Basi hii ndiyo Siku ya kufufuliwa! Lakini nyinyi mlikuwa hamuijui.\" Ndiyo maana mliikataa duniani, na mkakataa kukaa kwenu duniani kwa muda ambao mngeweza kurudi kwa Mwenyezi Mungu na kutubu. Basi haukuacha ujinga kuwa ndio kauli mbiu yenu, na athari zake kama vile kukadhibisha na hasara vikawa ndiyo nguo yenu ya juu ya mwili."},{"id":4354,"sura":30,"from_aya":57,"to_aya":57,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{57} \"Basi Siku hiyo hautawafaa wale waliodhulumu udhuru wao,\" wakikadhibisha na wakadai kuwa hakuna ushahidi wowote uliothibiti juu yao, au hawakuweza kuamini, uongo wao huo utadhihirika kwa ushahidi wa watu wenye elimu na imani, na ushahidi wa ngozi zao, mikono yao na miguu yao. Na wakiomba kukubaliwa udhuru, na kwamba warudhishwe na kwamba hawatarejea katika yale waliyokatazwa, hawatawezeshwa kufikia hilo; kwani wakati wa visingizio ulikwisha pita, kwa hivyo udhuru wao hautakubaliwa. \"wala haitatakiwa toba yao.\""},{"id":4355,"sura":30,"from_aya":58,"to_aya":60,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"58. Na hakika tulikwisha wapigia watu kila mfano katika hii Qur-ani. Na ukiwaletea Ishara yoyote, hapana shaka wale waliokufuru watasema, \"Nyinyi si chochote isipokuwa ni wana batili.\" 59. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kwenye nyoyo za wale wasiojua. 60. Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Wala wasikupaparishe hao wasiokuwa na yakini. "},{"id":4356,"sura":30,"from_aya":58,"to_aya":59,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{58 - 59} Yaani, \"Na hakika tulikwisha wapigia watu kila mfano\" kwa sababu ya ulezi wetu mzuri, rehema yetu, wema wetu, na mafunzo yetu mema \"katika hii Qur-ani,\" ambayo inayafanya uhakika kuwa wazi, na mambo yanapata kujulikana, na hoja inakatwa kwa hiyo mifano. Nayo ni ya jumla katika mifano ambayo Mwenyezi Mungu hupiga katika kuleta mambo yasiyoonekana kwa yale yanayoshikika, na katika kupeana habari kuhusu yale yatakayotokea na kuweka wazi uhakika wake hadi yakawa ni kana kwamba yametokea. Na miongoni mwake, ni kwamba mahali hapa, Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaja yatakayotokea Siku ya Kiyama, na hali ya wahalifu ndani yake, na ukubwa wa majuto yao, na kwamba hatakubali udhuru wowote wala hata kutubia kutoka kwao, lakini madhalimu na makafiri walikataa isipokuwa kuipinga haki iliyo wazi, na ndiyo maana akasema, \"Na ukiwaletea Ishara yoyote\" inayoonyesha usahihi wa yale uliyoyaleta, \"hapana shaka wale waliokufuru watasema, \"Nyinyi si chochote isipokuwa ni wana batili,\" wakimaanisha kwamba haki ni batili! Hili ni kwa sababu ya ukafiri wao na ujasiri wao, na Mwenyezi Mungu kuziziba nyoyo zao, na ujinga wao uliopitiliza. Na ndiyo maana akasema, \"Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kwenye nyoyo za wale wasiojua.\" Basi haiingii heri yoyote ndani yake, wala hazifahamu mambo kama yalivyo kihakika, bali zinaona kwamba haki ndiyo batili, nayo batili ndiyo haki."},{"id":4357,"sura":30,"from_aya":60,"to_aya":60,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{60} \"Basi subiri,\" juu ya yale uliyoamrishwa kuyafanya na juu ya kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu, hata ukiwaona wanakugeuzia mgongo, kamwe hayo yasikuzuie. \"Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki\" na haina shaka yoyote juu yake. Na haya ni katika yale yanayomsaidia mtu kuwa na subira. Kwani, mja anapojua kwamba matendo yake hayawezi kupotea, bali atayapata yakiwa kamili; machukizo yoyote anayokutana nayo yanakuwa rahisi kwake, na kila jambo gumu linakuwa rahisi kwake kiasi kwamba anaona matendo yailiyo mengi kwamba ni machache sana. \"Wala wasikupaparishe hao wasiokuwa na yakini.\" Yaani, wale ambao imani yao ni dhaifu, na yakini yao ni chache, na kwa sababu ya hayo maono yao yakawa hafifu, na subira yao ikapunguka. Kwa hivyo jihadhari na watu hawa wasije kukupaparisha. Kwani, ikiwa hutawaweka akilini na ukajihadhari nao, vinginevyo; watakupaparisha na kukufanya usiwe imara katika kufuata maamrisho na kuacha makatazo, nayo nafsi yako itawasaidia katika hili, na itataka ufanane nao na uafikiane nao. Na hili ni katika mambo yanayoonyesha kwamba kila Muumini mwenye yakini na ana akili timamu; ni rahisi sana kwake kuwa na subira. Lakini kila mwenye yakini dhaifu, mwenye akili dhaifu na nyepesi haliwezi hilo. Kwa hivyo, huyo wa kwanza yuko katika nafasi ya kiini cha kitu, naye wa pili ni kama gamba la mbegu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayeombwa msaada juu ya hayo."},{"id":4358,"sura":30,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}