{"result":[{"id":4555,"sura":34,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Saba'"},{"id":4556,"sura":34,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"[Nayo] ilishuka Makka"},{"id":4557,"sura":34,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu."},{"id":4558,"sura":34,"from_aya":1,"to_aya":2,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye ni vyake vyote vilivyo mbinguni na katika ardhi. Na sifa ni zake Yeye katika Akhera. Naye ni Mwenye hekima, Mwenye habari. 2. Anajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda huko. Na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwenye kusamehe. "},{"id":4559,"sura":34,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} \"Alhamdu\" inamanisha kusifu kwa sifa njema na matendo mazuri. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, anasifiwa kwa sifa zake zote kwa sababu ni sifa za ukamilifu. Na anasifiwa kwa matendo yake kwa sababu yanazunguka baina ya fadhila anazosifiwa juu yake na kushukuriwa kwazo, na uadilifu anaosifiwa kwa huo na ambao wanakiri hekima yake ndani yake. Alijisifu mwenyewe hapa kwamba, \u201cni vyake vyote vilivyomo mbinguni na katika ardhi.\" Vyote ni miliki yake na waja wake, na anaviendesha kwa sifa zake. \"Na sifa ni zake Yeye katika Akhera.\" Kwa sababu huko Akhera zitadhihiri sifa zake ambazo hazipo duniani. Ikiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu angeamua kati ya viumbe vyote, na watu na viumbe vyote wakaona kile alichotawala na ukamilifu wa uadilifu wake, na hekima ndani yake; wote wakamsifu kwa hilo, hata watu wa adhabu; hawataingia Motoni ila kwa nyoyo zao zikiwa zimemsifu, na kwamba hayo ni matokeo ya matendo yao, na kwamba Yeye ni mwadilifu katika hukumu yake katika kuwaadhibu. Ama kudhihiri kwa sifa zake katika nyumba ya neema na malipo, hili ni jambo ambalo limeripotiwa katika habari nyingi sahihi na ushahidi mbalimbali wa kusikiwa na kiakili ukakubaliana juu yake. Kwani, wao Peponi wataona mfuatano wa neema za Mwenyezi Mungu, wingi wa heri yake, wingi wa baraka zake, na wingi wa vipawa vyake, kiasi kwamba hayabaki matamanio yoyote wala utashi katika nyoyo za wakazi wa Peponi isipokuwa watakuwa wamepewa zaidi ya walivyotamani na kutaka. Bali watapewa hata heri ambayo hawakuitamani na wala hakikupita kwenye nyoyo zao. Basi unamdhaniaje kumsifu kwao Mola wao Mlezi katika hali hii, pamoja na kwamba katika Pepo vitatokewa vizuizi vyote vinavyozuia kumjua Mwenyezi Mungu na kumpenda, na kumsifu. Na hilo ndilo litakuwa pendwa zaidi na wakazi wa humo kuliko neema zote, na ni lenye kufurahisha zaidi kuliko raha zote? Na kwa sababu hii, watakapomuona Mwenyezi Mungu Mtukufu na kusikia maneno yake atakapozungumza nao, hilo litawastaajabisha wasahau neema zote. Na kumtaja Mola wao Mlezi Peponi kutakuwa ni kama pumzi yenye kuendelea katika kila wakati. Yatakuwa hivyo, na zaidi ni kwamba wakazi wa Peponi watadhihirikiwa humo Peponi kila wakati na ukuu wa Mola wao Mlezi, na utukufu wake, na uzuri wake na upana wa ukamilifu wake, jambo lenye kusababisha wamsifu na wamtaje kwa uzuri kikamilifu. \"Naye ni Mwenye hekima\" katika ufalme wake na usimamizi wake. Mwenye hekima katika amri zake na makatazo yake. \"Mwenye habari\" ambaye anajua siri za mambo na yale yaliyofichikana zaidi."},{"id":4560,"sura":34,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Na ndiyo maana akabainisha kwa kina kwamba ni mwenye kujua kwa kusema, \"Anajua yanayoingia katika ardhi.\" Yaani, kama vile mvua, mbegu na wanyama, \"na yanayotoka humo\" miongoni mwa aina mbalimbali za mimea na aina mbalimbali za wanyama,  \"na yanayoteremka kutoka mbinguni\" kama vile mali, riziki na mapitisho yake \"na yanayopanda huko\" kama vile malaika, roho, na mambo mengine. Na alipotaja viumbe vyake, hekima ya kuhusiana nao, na kujua kwake hali zao; akataja msamaha wake na rehema yake kwao, akasema \"Na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwenye kusamehe.\" Yaani, yule ambaye sifa yake ni rehema na msamaha. Na athari zake hazijaacha kuendelea kuwashukia waja wakati wote kwa mujibu wa yale waliyoyafanya katika mambo yanayolazimu kushuka kwake."},{"id":4561,"sura":34,"from_aya":3,"to_aya":5,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"3. Na walisema wale waliokufuru: \"Haitatufikia Saa ya Kiyama.\" Sema: kwani hapana shaka itakufikieni, ninaapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi, isipokuwa vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha. 4. Ili awalipe wale walioamini na wakatenda mema. Hao watapata msamaha na riziki ya ukarimu. 5. Na wale waliojitahidi kuzipinga Ishara zetu wakaona watashinda, hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu. "},{"id":4562,"sura":34,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} Mwenyezi Mungu alipobainisha ukuu wake kwa yale aliyojielezea nayo, na hili likawa ni sababu ya kumtukuza, kumtakasa na kumwamini; akataja kuwa miongoni mwa aina za watu, kuna kundi ambalo halikumthamini Mola wao kama anavyostahiki kuthaminiwa, wala halikumtukuza kama anavyostahiki kutukuzwa. Bali walimkufuru na wakakanusha uwezo wake wa kuwafufua wafu, na wakakanusha kusimama kwa Saa ya Kiyama, na wakawapinga Mitume wake kwa hayo. \"Na walisema wale waliokufuru\" Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na kwa yale waliyoyaleta, kwa hivyo wakasema kwa sababu ya ukafiri wao, \"Haitatufikia Saa ya Kiyama.\" Yaani, si chochote ila huu uhai wetu wa duniani, tunakufa na tunaishi. Basi Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake kuwajibu kauli yao na kuibatilisha, na kuapa kwa kufufuliwa na kwamba siku hiyo itawajia. Na akaliunga mkono hilo kwa ushahidi ambao mwenye kulikiri, inamlazimu kusadiki kufufuliwa kwa njia ya lazima, na huo ni elimu yake Mtukufu, iliyo pana na ya jumla. Akasema, \"Mwenye kujua ya ghaibu\" ambayo sisi hatuioni wala hatuijui. Basi itakuaje elimu yake kuhusiana na mambo yanayoshuhudiwa? Kisha akasisitiza elimu yake na akasema, \"Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi;\" kila kitu pamoja na dhati zake, sehemu zake, hata sehemu ndogo kabisa. \"Wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi, isipokuwa vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha.\" Yaani, elimu yake iliyadhibiti, na kalamu yake ikayaandika, nayo yako katika kitabu kinachobainisha ambacho ni Ubao Uliohifadhiwa. Basi yule ambaye hakuna kinachoweza kufichika mbali na elimu yake cha uzito wa chembe au kilicho chini ya hivyo katika nyakati zote, na anajua kile ambacho ardhi inapunguza miongoni mwa wale wanaokufa, na kile kinachobakia miongoni mwa miili yao; ana uwezo na anastahili zaidi kuwafufua, na wala kuwafufua si jambo la kushangaza zaidi kuliko elimu hii iliyowazunguka."},{"id":4563,"sura":34,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Kisha akataja makusudio ya kuwafufua viumbe, akasema, \"Ili awalipe wale walioamini\" kwa nyoyo zao, ambao walimsadiki Mwenyezi Mungu na wakawasadiki Mitume wake kwa usadikisho wa uhakika, \"wakatenda mema\" ili kusadikisha imani yao. \"Hao watapata msamaha\" wa dhambi zao. Kwa sababu ya imani yao na matendo yao ulizuilika uovu wote na adhabu ikaepukika, \"na riziki ya ukarimu\" kwa sababu ya wema wao, walifanikiwa kupata kila wanachotafuta na kutamani."},{"id":4564,"sura":34,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} \"Na wale waliojitahidi kuzipinga Ishara zetu wakaona watashinda\" kwa kuzikufuru na kutaka kumshinda yule aliyezileta, na kutaka kumshinda aliyeziteremsha, kama vile walivyoona kwamba hawezi kuwarudisha baada ya kufa. \"Hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu\" yenye kuumiza miili na nyoyo zao."},{"id":4565,"sura":34,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"6. Na wale waliopewa elimu wanaona ya kuwa yale uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ndiyo haki, nayo huongoa kwendea njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa."},{"id":4566,"sura":34,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kukanusha kwa wale waliokanusha suala la kufufuliwa, na kwamba wanayaona yale yaliyoteremshwa kwa Mtume wake kuwa si haki, akataja hali ya wale waliofanikishwa miongoni mwa waja wake, ambao ni watu wa elimu, na kwamba wanayaona yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake miongoni mwa kitabu na habari zilizo ndani yake, kwamba \"ndiyo haki\" na kwamba chochote kinachohalifiana nayo na kupingana nayo ni batili, kwa sababu wamefikia kiwango cha yakini katika elimu, na pia wanaona kwamba katika maamrisho yake na makatazo yake, \"huongoa kwendea njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.\" Hayo ni kwa sababu wana yakini juu ya ukweli wa yale aliyosema kwa pande nyingi: kwa upande mmoja ni kuwa wanajua kwamba aliyeyajulisha ni mkweli, na kwa upande mwingine wa pili ambao ni kwamba yanaafikiana na matukio yaliyotokea na vitabu vilivyotangulia, na kwa upande mwingine ambao ni kwamba wanazishuhudia habari zake ambazo zinatokea na kuonwa kwa macho yao wenyewe, na kwa upande wa yale wanayoyashuhudia miongoni mwa Aya kubwa zinazoyaashiria hayo katika upeo wa macho na katika nafsi zao, na kwa upande wa kuafikiana kwake na yale yanayoonyeshwa na majina yake na sifa zake, na wanaona katika maamrisho na makatazo kwamba yanaongoza kwenye njia iliyonyooka inayojumuisha mambo yenye kila sifa inayoitakasa nafsi, inayoongeza malipo, na yanamfaa mtendaji na wengineo; kama vile ukweli, ikhlasi, kuwafanyia wema wazazi, kuwaunga jamaa, na kuwafanyia wema viumbe wote, na mfano wa hayo. Na yanakataza kila tabia mbaya inayoichafua nafsi, na kuharibu malipo, na kusababisha dhambi kutokana na ushirikina, uzinzi, riba, na dhuluma katika damu, mali, na heshima. Hii ni hadhi kubwa kwa watu wenye elimu,fadhila na ishara. Na kwamba kila mja anavyozidi kuwa na elimu na kusadiki habari za yale aliyoyaleta Mtume, na akawa ni mwenye kujua zaidi hukumu za maamrisho yake na makatazo yake; anakuwa miongoni mwa watu wenye elimu ambao Mwenyezi Mungu aliwafanya kuwa ni hoja kwa yale aliyokuja nayo Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ambao Mwenyezi Mungu aliwatumia kama hoja dhidi ya wale wanaokadhibisha, wakaidi, kama ilivyo katika Aya hii na nyinginezo."},{"id":4567,"sura":34,"from_aya":7,"to_aya":9,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"7. Na wale waliokufuru walisema: Je, tuwajulisheni mtu anayewaambieni kwamba mtakapochambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya? 8. Ama amemzulia Mwenyezi Mungu uongo, au ana wazimu. Bali wale wasioamini Akhera wamo adhabuni na upotofu wa mbali kabisa. 9. Kwani hawaoni yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, ya mbingu na ardhi? Tungelipenda, tungeliwadidimiza ndani ya ardhi, au tungeliwateremshia juu yao vipande vya mbingu. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mja aliyetubia. "},{"id":4568,"sura":34,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Yaani, \"Na wale waliokufuru walisema\" kwa njia ya kukadhibisha na masihara na kuona kwamba hilo haliwezekani, na kutaja njia ya kutowezekana kwake; \"Je, tuwajulisheni mtu anayewaambieni kwamba mtakapochambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya?\" Mtu wanayemkusudia hapa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - na kwamba ni mtu aliyekuja na jambo la kushangaza kutoka kwa mtu kama yeye, hadi akawa, - kwa mujibu wa madai yao - ni jambo la kutazama kwa furaha tena la ajabu wanalolifanyia masihara. Na kwamba vipi anasema kwamba: Mtafufuliwa baada ya kuchambuliwa mapande mapande na kuishia udongoni, na viungo vyenu vikatawanyika, na viungo vyenu vikapotelea mbali!"},{"id":4569,"sura":34,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} Basi mtu huyu anayefanya hivyo: Je, amemzulia \"Mwenyezi Mungu uongo\", kwa hivyo akathubutu kusema aliyoyasema, \"au ana wazimu\" kwani likawa si jambo la kustaajabu. Kwa maana, wazimu ni aina mbalimbali. Na yote haya, wanayafanya kwa njia ya ukaidi na dhuluma, kwani walikwisha jua kwamba yeye ndiye mkweli na mwenye hekima zaidi katika viumbe vya Mwenyezi Mungu. Na katika elimu yao ni kwamba walimwonyesha na kurudia kumfanyia uadui, na wakayatoa maisha yao na mali zao katika kuwazuilia watu mbali naye. Kwa hivyo, ikiwa alikuwa mwongo na wazimu, basi haingewafailia enyi watu wenye akili isiyokuwa safi kusikiliza anachokisema wala kusherehekea wito wake. Kwani haimfailii mwenye akili timamu kujali anachofanya mwendawazimu wala kumwambia maneno magumu. Na lau kuwa si ukaidi wenu na udhalimu wenu, mngefanya haraka kumuitikia na kutii wito wake. Lakini Aya na maonyo hayafai kitu kwa watu wasioamini. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, \"Bali wale wasioiamini Akhera,\" wakiwa miongoni wale waliosema maneno hayo, \"wamo adhabuni na upotofu wa mbali kabisa.\" Yaani, katika mashaka makubwa na upotofu wa mbali usiokaribia usahihi. Na ni mashaka gani na upotevu gani mkubwa zaidi kuliko kukataa kwao uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kufufua, kumkadhibisha kwao Mtume wao aliyeileta habari hiyo, na kumkejeli kwao, na kuwa kwao na uhakika kwamba walichokileta wao ndiyo haki, kwa hivyo, wakaona kwamba haki ndiyo batili, na batili na upotofu ndiyo haki na uwongofu?"},{"id":4570,"sura":34,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} Kisha akawatanabahisha juu ya hoja ya kiakili yenye kuonyesha kwamba ufufuo si jambo ambalo haliwezi kutokea kama wanavyoona kuwa haliwezi kutokea, na kwamba kama watatazama yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, kama vile mbingu na ardhi, wakaona uwezo wa Mwenyezi Mungu ndani yake wenye kuangaza akili, na ukuu wake wenye kustaajabisha wanazuoni wakubwa, na kwamba kuumbwa kwa viwili hivyo, ukubwa wake, na viumbe walio ndani yake ni mambo makubwa zaidi kuliko kuwarudisha watu kutoka makaburini mwao baada ya kufa kwao. Basi je, ni nini kinachowafanya kukadhibisha licha ya kwamba wanasadiki jambo ambalo ni kubwa zaidi kuliko hili? Ndiyo, hiyo ni habari ya ghaibu ambayo bado hawajaiona hadi sasa; basi ndiyo maana wakaikadhibisha. Mwenyezi Mungu akasema, \"Tungelipenda, tungeliwadidimiza ndani ya ardhi, au tungeliwateremshia juu yao vipande vya mbingu.\" Yaani, adhabu; kwa sababu ardhi na mbingu ziko chini uendeshaji wetu. Tukiviamuru, havitaasi. Basi jihadharini dhidi ya kuendelea kukadhibisha, tukaja kuwaadhibu kwa adhabu kali kabisa. \"Hakika katika haya;\" yaani, kuziumba mbingu na ardhi na viumbe vyote vilivyomo \"zipo Ishara kwa kila mja aliyetubia.\" Na kila mja anapokuwa ni wa kurudi kwa Mwenyezi Mungu sana, kunakuwa kufaidika kwake na ishara ni kukubwa zaidi. Kwa sababu mwenye kutubia anaelekea kwa Mola wake Mlezi, tayari utashi wake na hima yake vimeelekea kwa Mola wake Mlezi, na amerejea kwake katika kila jambo miongoni mwa mambo yake, kwa hivyo akawa karibu na Mola wake Mlezi, na akawa hajali kingine isipokuwa kujishughulisha na kumridhisha Yeye, kwa hivyo akawa anawatazama viumbe kwa mtazamo kufikiria na kuzingatia, siyo kutazama kwa kughafilika ambako hakuna faida yoyote."},{"id":4571,"sura":34,"from_aya":10,"to_aya":11,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"10. Na tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, tukasema: \"Enyi milima, karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia.\" Na tukamlainishia chuma. 11. Tukamwambia: \"Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayoyatenda.\" "},{"id":4572,"sura":34,"from_aya":10,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10 - 11} Yaani, tulimneemesha mja wetu na Mtume wetu Daudi, rehema na amani zimshukie, na tukampa elimu yenye manufaa, matendo mema, na neema za kidini na za kidunia, na miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu juu yake. Ni yale ambayo Mwenyezi Mungu alimpa yeye tu miongoni mwa vitu visivyo na uhai, kama vile milima na wanyama kama ndege, vije kukariri pamoja naye kumtakasa Mola wao Mlezi na kumsifu na kumwitikia. Hii ni neema kwake kwamba haya alipewa yeye tu, na wala hakuna aliyewahi kupewa kabla yake wala baada yake, na kwamba hilo likawa ni la kumtia moyo yeye na wengine kumtakasa Mwenyezi Mungu watakapoona vitu hivi visivyo na uhai na wanyama wanamuitikia Mola wao Mlezi kwa kumtakasa na kumtukuza, na kusema kwamba yeye ndiye mkubwa na kumsifu. Hili linakuwa ni katika mambo ambayo yanamchochea mtu kumtaja Mwenyezi Mungu. Na Miongoni mwake ni hilo - kama walivyosema wanazuoni wengi - ilikuwa ni furaha ya sauti ya Daudi. Kwani Mwenyezi Mungu alikuwa amempa sauti nzuri iliyozidi ile ya mtu yeyote. Na alikuwa anaporudiarudia kumtakasa Mwenyezi Mungu, na kusema: hapana mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kumtukuza kwa sauti hiyo ya kupendeza, yenye mvuto, yenye kufurahisha; kila aliyemsikia, kuanzia watu hadi majini, hata ndege na milima, walifurahi na wakamtakasa na kumsifu Mola wao Mlezi. Na miongoni mwake ni labda atapata malipo ya kutakasa kwao huku, kwa sababu yeye ndiye sababu ya wao kufanya hivyo, na walikuwa wakimtakasa Mwenyezi Mungu huku wakimfuata Daudi katika hilo. Na katika fadhila za Mwenyezi Mungu juu yake, ni kwamba alimlainishia chuma ili atengeneze ngao na nguo za chuma pana, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamfundisha jinsi ya kuzitengeneza. Kwamba \"na kadiria sawa katika kuunganisha.\" Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, \"Na tukamfundisha kuunda mavazi ya vita kwa ajili yenu ili yakuhifadhini katika kupigana kwenu. Je, mtakuwa wenye kushukuru?\" Na alipotaja kile alichomneemesha nacho na juu ya familia yake, akamuamuru kumshukuru, na kwamba wafanye matendo mema na wamchunge Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake kwa kuyatengeneza na kuyahifadhi kutokana na yenye kuyaharibu. Kwani Yeye anayaona vyema matendo yao, anayajua na hakuna chochote katika hayo kinachofichikana kwake."},{"id":4573,"sura":34,"from_aya":12,"to_aya":14,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"12. Naye Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyeyushia chemichemi ya shaba. Na katika majini, walikuwako waliokuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anayejitenga na amri yetu katika wao, tunamuonjesha adhabu ya Moto unaowaka. 13. Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na vitu vifananavyo vingine, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yaliyo madhubuti. Enyi watu wa Daudi, fanyeni kazi kwa kushukuru. Na ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru. 14. Na tulipomhukumia kufa, hapana aliyewajulisha kufa kwake ila mnyama wa ardhi aliyekula fimbo yake. Na alipoanguka, majini wakatambua lau kuwa wangelijua ya ghaibu wasingelikaa katika adhabu hiyo ya kufedhehesha. "},{"id":4574,"sura":34,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Alipotaja fadhila zake juu ya Daudi, amani iwe juu yake, akataja neema yake juu ya mwanawe, Suleiman, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na kwamba Mwenyezi Mungu alimtiishia upepo uendao kwa amri yake na ukawa unambeba yeye na kila kilichokuwa pamoja naye na kukata umbali mrefu sana kwa muda mfupi, ukawa unakwenda katika siku moja umbali wa miezi miwili. \"Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyeyushia chemichemi ya shaba.\" Yaani, tukamfanyia wepesi njia za kutengeneza vitu vinavyotengenezwa kutoka humo kama vile vyombo na vitu vingine. Na pia, Mwenyezi Mungu alimtiishia mashetani na majini ambao hawakuweza kuasi amri yake. \"Na kila anayejitenga na amri yetu katika wao, tunamuonjesha adhabu ya Moto unaowaka.\""},{"id":4575,"sura":34,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Na matendo yao yalikuwa kwamba chochote ambacho Suleiman alitaka, walikifanya, kama vile \"mihrabu\" ambao ni kila mjengo unaojengwa, na ambao kwa huo, mijengo mingine inakuwa na nguvu. Hili linaonyesha kwamba kulikuwepo na majengo ya kifahari. \"Na masanamu\", yaani picha za wanyama na vitu visivyo na uhai, kwa kuvitengeneza kwa ustadi mkubwa, na kwamba walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, na kumfanyia kazi Suleimani. \"Na madeste makubwa kama mahodhi\" ambayo walikuwa wamemfanyia Suleiman kwa ajili ya chakula. Kwa sababu alikuwa anahitaji kile ambacho hakuna mtu mwingine alikuwa anakihitaji. \"Na\" wanamtengenezea masufuria \"makubwa\" yasiyoondolewa mahala pake kwa sababu ya ukubwa wake. Kwa hivyo, alipotaja neema zake juu yao, akawaamuru wamshukuru kwa hizo. Kwa hivyo akasema, \"Enyi watu wa Daudi, fanyeni kazi kwa kushukuru.\" Kwa sababu neema hizo ziliwafikia wote, na mengi ya masilahi hayo yalikuwa yanawarudia wote. Kwa hivyo, walipaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa aliyowapa, na pia wamshukuru kwa njia ya kuyakabili yale aliyowaruzuku. \"Ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru.\" Kwani, wengi wao hawakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake alizowaneemesha kwazo, na akawaepusha na adhabu. Shukrani ni kukiri kwa moyo neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuipokea kwa sababu mtu anaihitaji, na kuitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuilinda dhidi ya kuitumia katika uasi."},{"id":4576,"sura":34,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} Kwa hivyo, mashetani wakaendelea kumfanyia kazi Suleiman, rehema na amani ziwe juu yake. Nao walikuwa wamewapotosha watu na kuwaambia kwamba wanajua mambo ya ghaibu, na kwamba walikuwa na uwezo wa kufikia mambo yaliyofichika. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kuwaonyesha waja wake uongo wao katika madai yao haya. Basi wakabakia wakiendelea kufanya kazi yao hiyo. Na Mwenyezi Mungu akapitisha kwamba Suleiman, amani iwe juu yake afe, kwa hivyo akaiegemea fimbo yake. Basi wakawa wanapopita karibu naye hali ya kuwa ameegemea juu yake, wanadhani kwamba yu hai kwa hivyo wanamuogopa. Basi wakawa wanaendelea kufanya kazi zao hivyo hivyo kwa muda wa mwaka mzima, kama ilivyosemwa, mpaka wadudu wa ardhini walipopewa mamlaka kuila fimbo yake. Wakawa wanaila mpaka ikaisha na ikaanguka chini, kwa hivyo Suleiman akaanguka chini pia, nao mashetani wakatawanyika. Kwa hivyo watu wakatambua ya kwamba majini, \"lau kuwa wangelijua ya ghaibu, wasingelikaa katika adhabu hiyo ya kufedhehesha.\" Yaani, kazi ngumu sana juu yao. Na lau kuwa walikuwa wanaijua ghaibu; basi wangejua kifo cha Suleiman, ambacho ndicho kitu kikubwa zaidi walichotaka kujua ili wasalimike kutokana na kile walichokuwemo."},{"id":4577,"sura":34,"from_aya":15,"to_aya":21,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"15. Hakika ilikuwepo Ishara kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika maskani yao - bustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, na mumshukuru. Mji mzuri na Mola Mlezi aliye Msamehevu. 16. Lakini wakayapa mgongo. Kwa hivyo, tukawatumia mafuriko makubwa, na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyingine zenye matunda makali, machungu, na mivinje, na kidogo katika miti ya kunazi. 17. Hayo tuliwalipa kwa sababu ya walivyokufuru. Nasi kwani tunamuadhibu isipokuwa anayekufuru? 18. Na baina yao na miji mingine tuliyoibariki tuliweka miji iliyo dhahiri, na tukaweka humo vituo vya safari. Tukawaambia, \"Nendeni humo usiku na mchana kwa amani.\" 19. Lakini wakasema, \"Mola wetu Mlezi! Weka mwendo mrefu baina ya safari zetu.\" Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi tukawafanya ni masimulizi tu, na tukawatawanya tawanya. Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru mno. 20. Na bila ya shaka Iblisi aliihakikisha ile dhana yake juu yao. Nao walimfuata, isipokuwa kundi katika Waumini. 21. Na yeye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao, isipokuwa kwa sababu ya kuwajaribu ili tumjue ni nani mwenye kuamini Akhera, na ni nani anayeitilia shaka. Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu. "},{"id":4578,"sura":34,"from_aya":15,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15 - 19} Sabaa ni kabila mashuhuri katika viunga vya Yemen, na makazi yao yalikuwa katika mji uitwao Ma'rib. Nao ulikuwa ni miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kwa watu kwa ujumla na hasa kwa Waarabu, na kwamba aliwasimulia katika Qur-ani habari za wale walioangamizwa na kuadhibiwa miongoni mwa wale waliokuwa majirani na Waarabu. Yanashuhudiwa magofu yao, na watu wananukuu habari zao; ili hili liweze kusaidia kusadiki zaidi na liwe karibu zaidi katika kufikisha mawaidha. Akasema, \"Hakika ilikuwepo Ishara kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika maskani yao.\" Na ishara hapa inamaanisha yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha miongoni mwa neema mbalimbali, na akawaepusha kutokana na adhabu, mambo ambayo wanawahitaji kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumshukuru. Kisha akaifafanua ishara hiyo kwa kusema, \"bustani mbili, kulia na kushoto.\" Nao walikuwa na bonde kubwa lenye kujiwa na maji mengi ya mafuriko. Na walikuwa wamejenga bwawa madhubuti lenye kukusanya maji hayo. Kwa hivyo maji hayo ya mafuriko yalikuwa yakija humo, na maji mengi yangekusanyika humo, kisha wanayatawanya katika bustani zao zilizokuwa upande wa kulia na wa kushoto wa bonde hilo. Na zikawa bustani hizo mbili kubwa zinawapa matunda ya kuwatosheleza, na wanafurahia mno. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaamuru kushukuru neema zake alizowapa kwa njia nyingi. Miongoni mwake ni hizi bustani mbili ambazo chakula chao kingi kilikuwa ni kutoka humo. Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu aliifanya nchi yao kuwa nchi nzuri kwa hewa yake nzuri, kutokuwepo na machafuzi yoyote ya hewa, na kuwepo kwa riziki nyingi humo. Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaahidi kwamba wakimshukuru, atawasamehe na kuwarehemu. Na ndiyo maana akasema, \"Mji mzuri na Mola Mlezi aliye Msamehevu.\" Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu alipojua kwamba wanahitaji ardhi iliyobarikiwa kwa ajili ya biashara zao na mapato yao - na ni dhahiri kwamba huu mji ulikuwa miongoni mwa miji ya Sana\u2019a, kama walivyosema zaidi ya mmoja wa wema waliotangulia. Na ikasemwa kwamba ilikuwa huko Shama, - basi Mwenyezi Mungu akawaandalia njia za kurahisisha kuyafikia hayo kwa kuwapa usalama na kuondoa hofu, na kuifanya miji kuwa na mawasiliano, ili wasipate taabu katika kubeba bidhaa na vyakula. Na ndiyo maana akasema, \"Na baina yao na miji mingine tuliyoibariki tuliweka miji iliyo dhahiri, na tukaweka humo vituo vya safari.\" Yaani, safari zilizopangwa wanazozijua na kuzihukumu kwa namna ambayo hawawezi kupotea usiku na mchana. \"Kwa amani.\" Yaani, wakiwa na utulivu katika safari zao, usiku na mchana bila ya hofu yoyote. Na hii ni katika ukamilifu wa neema ya Mwenyezi Mungu juu yao kwamba aliwapa amani kutokana na hofu.  Lakini wakampa mgongo aliyewaneemesha na pia wakakataa kumwabudu. Na wakajivuna na neema hizo na wakachoshwa nazo hadi wakaomba na kutamani kwamba safari zao hizo ziwe mbali kati ya vile miji hiyo ambayo safari ya kati yake ilikuwa rahisi. \"Na wakazidhulumu nafsi zao\" kwa kumkufuru Mwenyezi Mungu na fadhila zake. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaadhibu kwa neema hizi zilizowapotosha; kwa hivyo akaziangamiza. Aliwatumia, \"mafuriko makubwa\" ambayo yaliharibu bwawa lao hilo, na yakaharibu bustani zao. Kwa hivyo, bustani hizo zenye mimea ya kupendeza na miti yenye matunda zikabadilishwa na ikawekwa ndani yake miti isiyofaa. Ndiyo maana akasema, \"na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyingine zenye matunda\" yanayoweza kuliwa lakini yasiyowasaidia kitu katika kukidhi haja yao ya chakula; \"makali, machungu, na mivinje, na kitu kidogo katika miti ya kunazi. Yote hii ni miti mashuhuri, na malipo haya ni ya aina sawa na matendo yao. Kila walivyobadilisha shukrani nzuri kwa ukafiri mbaya; walibadilishiwa neema hizo kwa kile kilichotajwa. Ndiyo maana akasema, \"Hayo tuliwalipa kwa sababu ya walivyokufuru. Nasi kwani tunamuadhibu isipokuwa anayekufuru\" Mwenyezi Mungu na akajivuna na neema yake? Yalipowapata yaliyowapata, walitengana na kutawanyika baada ya kwamba walikuwa pamoja, na Mwenyezi Mungu akawafanya kuwa ni masimulizi tu ambayo watu wanayazungumzia na ndiyo zikawa ndizo hadithi zao za usiku. Na wakawa wanapigiwa mfano, ikasemwa: 'Walitengana kama walivyotengana watu wa Sabaa.' Kila mtu akawa anazungumza juu ya yale yaliyowasibu, lakini hakuna anayefaidika na kupata mafunzo kutoka kwao isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu alisema juu yao: \"Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru.\" Mwenye subira katika machukizo na shida, ambaye anayasubiria kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu, na wala hayachukii, bali anayavumilia, na kushukuru neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na anakiri neema hizo na kuzitambua, na kumsifu aliyemneemesha nazo, na anazitumia katika kumtii. Ndiyo maana, inaposikiwa hadithi yao na kile walichofanya na kile kilichowatokea, inajulikana kwa hayo kwamba adhabu hiyo ni malipo ya kukufuru kwao neema za Mwenyezi Mungu, na kwamba anayefanya mfano wao, atafanyiwa kama walivyofanyiwa wao, na kwamba kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kunahifadhi neema na kuzuia adhabu, na kwamba Mitume wa Mwenyezi Mungu ni wakweli katika yale waliyotuambia, na kwamba malipo ya akhera ni ya kweli, kama ulivyoonekana mfano wake katika dunia hii."},{"id":4579,"sura":34,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Kisha akataja kwamba watu wa Sabaa walikuwa miongoni mwa wale ambao Iblisi alihakikisha ile dhana yake juu yao. Alipomwambia Mola wake Mlezi, \"Ninaapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote. Isipokuwa waja wako waliosafika miongoni mwao.\" Hii ilikuwa tu ni dhana ya Iblisi, wala hata hakuwa na yakini juu ya hilo. Kwa sababu yeye hajui ghaibu, wala haikumjia habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba atawapoteza wote. Isipokuwa wale ambao aliwaepusha kutokana na hilo. Hawa na wengine mfano wao ni miongoni mwa wale ambao Iblisi aliwahakikishia ile dhana yake, na akawaita na kuwapoteza. \"Nao walimfuata, isipokuwa kundi katika Waumini\" katika wale ambao hawakuzikufuru neema za Mwenyezi Mungu; hao hawakuingia katika ile dhana ya Iblisi. Na inawezekana kwamba kisa cha Sabaa kiliishia pale aliposema, \u201cHakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru.\" Kisha akaanza tena na kusema, \"Na bila ya shaka Iblisi aliihakikisha ile dhana yake juu yao.\" Yaani, kwa watu wote, kwa hivyo Aya hii inakuwa ni ya jumla kwa kila aliyemfuata."},{"id":4580,"sura":34,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, \"Na yeye;\" yaani, Iblisi, \"hakuwa na mamlaka yoyote juu yao.\" Yaani, kuwatawala, na kuwakandamiza, na kuwalazimisha juu ya kile anachotaka kutoka kwao, lakini hekima ya Mwenyezi Mungu ililazimu kwamba awe na mamlaka na uwezo wa kuwapotosha wanadamu \"ili tumjue ni nani mwenye kuamini Akhera, na ni nani anayeitilia shaka.\" Yaani, ili watu waweze kupewa mtihani na kwa huo ijulikane mkweli na mwongo. Na ili ajulikane yule ambaye imani yake ni sahihi, anayekuwa thabiti wakati wa mtihani na majaribu na kutupilia mbali fikira potofu za kishetani na ajulikane yule ambaye imani yake si thabiti, ambaye anajisalimisha anapofikiwa na fikira potovu ndogo zaidi na anakubali kufanya kinyume kunapokuwa na sababu ndogo zaidi inayoliitia hilo. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfanya kuwa mtihani na kwake anawafanyia waja wake majaribu ili adhihirike muovu mbali na mwema. \"Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu.\" Anawahifadhi waja wake na anawahifadhia vitendo vyao, na Yeye Mtukufu anahifadhi malipo yao, na atawalipa kwa ukamilifu na ukarimu."},{"id":4581,"sura":34,"from_aya":22,"to_aya":23,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"22. Sema, \"Waiteni wale mnaowadaia kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu. Hawamiliki hata uzito wa chembe katika mbingu wala ardhi. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala Yeye hana msaidizi miongoni mwao.\" 23. Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipokuwa kwa aliyempa idhini. Hata itakapoondolewa hofu kwenye nyoyo zao, watasema: \"Mola wenu Mlezi amesema nini?\" Watasema: \"Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa.\" "},{"id":4582,"sura":34,"from_aya":22,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22 - 23} Yaani, \"Sema\" ewe Mtume, uwaambie wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu na viumbe vingine visivyofaa wala kudhuru, ukiwafanya kukubali kwa lazima kwamba hivyo havina uwezo, na ukibainisha ubatili wa kuviabudu, \"Waiteni wale mnaowadaia kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu,\" mkadai kwamba wao ni washirika wa Mwenyezi Mungu, ikiwa dua yenu ina manufaa yoyote. Wao kwa hakika tayari wana sababu za kutoweza ndani yao na kushindwa kujibu maombi kwa namna yoyote ile. Kwani wao hawana umiliki hata kidogo, kwa kuwa hawamiliki uzito wa chembe katika mbingu na ardhi, kwa kujitegemea wala kwa njia ya ushirika. Na ndiyo maana akasema, \"Wala hawana ushirika wowote humo,\" si mdogo wala mwingi. Inabakia kusema kwamba: Hata hivyo, wanaweza kuwa wasaidizi na mawaziri wa Mmiliki wa kweli; basi dua yao ikawa ni yenye kunufaisha. Kwa kuwa, kwa sababu Mmiliki wa kweli anawahitaji, wanaweza kutimiza mahitaji ya wale wanaofungamana nao. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaikanusha daraja hii, na akasema, \"Wala Yeye\" Mwenyezi Mungu, Mmoja, Mshindi, \"hana msaidizi yeyote miongoni mwao\" anayemsaidia katika kutawala na kuendesha mambo. Basi hakuna kilichobakia isipokuwa uombezi, lakini huo pia akaukanusha kwa kauli yake, \"Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipokuwa kwa aliyempa idhini.\" Hizi ndizo aina za mafungamano wanayofungamana kwayo washirikina na washirika wao na masanamu yao katika wanadamu, miti, mawe na mengineo. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akayakata na kubainisha ubatili wao kwa ubainisho wa kukata kiini cha ushirikina, na wa kukata mizizi yake. Kwa sababu mshirikina huomba na kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu akitarajia kunufaika kutoka kwake, na matarajio haya ndiyo yaliyomfanya kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Basi ikiwa huyo ambaye yeye anamuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu hamiliki manufaa yoyote wala madhara, wala hata si mshirika wa Mmiliki wa kweli wala msaidizi wake, wala hawezi kufanyia wengine uombezi bila ya idhini ya Mmiliki wa kweli. Basi inakuwa dua hii na ibada hii ni upotofu katika akili na batili katika Sheria. Bali, mshirikina huyo anajiwa na kinyume cha yale aliyotaka na aliyokusudiwa. Kwa sababu alikuwa anakusudia kunufaika nayo, lakini Mwenyezi Mungu akabainisha ubatili wake na kutokuwepo kwake, na hata akabainisha katika Aya zingine madhara yake kwa wanaowaabudu, na kwamba Siku ya Kiyama wao kwa wao watakufuriana na kulaaniana, na makaazi yao ni Motoni, na ambao watu watakapokusanywa, watakuwa maadui zao, na wataikataa ibada yao. Inastaajabisha kwamba mshirikina anatakabari kuwafuata Mitume akidai kuwa wao ni wanadamu, na anaridhia kuabudu na kuomba dua miti na mawe. Alitakabari kumkusudia Mfalme, Mwingi wa rehema, Mlipaji, na akaridhia kuwaabudu wale ambao madhara yao yako karibu zaidi kuliko manufaa yake, kutokana na kumtii adui yake mkubwa zaidi, ambaye ni Shetani! Na kauli yake, \"Hata itakapoondolewa hofu kwenye nyoyo zao, watasema: \"Mola wenu Mlezi amesema nini?\" Watasema: \"Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa.\" Inawezekana kwamba wanaokusudiwa hapa ni washirikina; Kwa sababu hao ndio waliotajwa katika matamshi ya wazi ya aya hii. Na kanuni inasema kwamba kivumishi kinarudia yale yaliyo karibu zaidi nacho, kwa hivyo, maana yake inakuwa ni: Siku ya Kiyama itakapofika na hofu ikaondolewa katika nyoyo za washirikina, na wakaulizwa akili zao zilipowarudia kuhusu hali yao ya hapa duniani na kukadhibisha kwao haki waliyoileta Mitume, watakiri kuwa waliyokuwa wakifanya ya ukafiri na ushirikina ni batili, na kwamba aliyoyasema Mwenyezi Mungu na kuambiwa na Mitume wake ndiyo haki, basi yakawadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha zamani, na wakajua kwamba haki ni ya Mwenyezi Mungu, na waliungama dhambi zao. \"Na Yeye ndiye Aliye juu\" kwa dhati yake, juu ya viumbe vyote, na kwa kuwashinda, na kwa hadhi yake ya juu kwa sababu ya sifa zake kuu, tukufu zaidi; \"Mkubwa\" katika dhati yake na sifa zake. Na katika ujuu wake ni kwamba hukumu yake ndiyo yenye kushinda, na nafsi zinanyenyekea kwake kwa ajili yake, hata nafsi za wenye kutakabari na washirikina. Na maana hii ndiyo dhahiri zaidi, nayo ndiyo inayoashiriwa na muktadha huu. Na inawezekana kwamba kilichokusudiwa katika kivumishi kilichotumika ni Malaika, na hilo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu anapozungumza kwa ufunuo; Malaika wanamsikia na wanamuangukia chini Mwenyezi Mungu na kumsujudia. Kisha Jibril anakuwa ndiye wa kwanza kuinua kichwa chake, na Mwenyezi Mungu anazungumza naye kutokana na ufunuo wake atakavyo. Kisha kuzimika huko kunapoondoka katika nyoyo za Malaika na hofu pia ikaisha, wanaulizana wao kwa wao juu ya kauli hiyo ambayo kwayo walizimika: 'Amesema nini Mola wenu Mlezi?'  Basi huambiana wao kwa wao: 'Amesema kweli', ima kwa ujumla; kwa kuwa wanajua kwamba yeye hasemi isipokuwa kweli tu, au wanasema: 'Amesema hivi na hivi,' wakitaja maneno waliyoyasikia kutoka kwake, na kwamba ni kweli. Basi inakuwa maana kulingana na hivi ni kwamba, washirikina walioabudu pamoja na Mwenyezi Mungu miungu hao ambao tumekuelezeeni upungufu wao, na kutoweza kwao kunufaisha kwa njia yoyote ile, namna walivyogeuka na wakaacha kumkusudia Mola Mlezi, Mkuu, aliye juu, Mkubwa, ambaye katika utukufu wake na ukuu wake ni kwamba Malaika watukufu walio karibu sana naye katika viumbe vyote wananyenyekea namna hii na kuzimika wanaposikia maneno yake, na wote wanakiri kwamba Mwenyezi Mungu hasemi isipokuwa kweli tu. Basi wana nini washirikina hawa waliotakabari kumuabudu yule ambaye hadhi yake ni hii, na ukubwa wa ufalme wake na mamlaka yake? Basi Mwenyezi Mungu yuko juu sana, na ni Mkubwa sana mbali na ushirikina wa washirikina, na uzushi wao na uwongo wao."},{"id":4583,"sura":34,"from_aya":24,"to_aya":27,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"24. Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uwongofu au upotofu ulio wazi. 25. Sema: Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya, wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda nyinyi. 26. Sema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki; na Yeye ndiye Hakimu, Mwenye kujua vyema. 27. Sema: Nionyesheni mliowaunganisha naye kuwa washirika. Hasha! Bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima. "},{"id":4584,"sura":34,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwamrisha Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - kumwambia anayemshirikisha Mwenyezi Mungu na kumuuliza juu ya usahihi wa ushirikina wake: \"Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na kwenye ardhi?\" Kwani lazima wakiri kwamba huyo ni Mwenyezi Mungu, na ikiwa hawatakiri; basi \"Sema: Ni Mwenyezi Mungu!\" Hutapata wa kukanusha kauli hii. Basi ikidhihirika kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini, na anawateremshia mvua, na anawaoteshia mimea, na anawapitishia mito, na anawaletea matunda ya miti, na amewaumbia wanyama wote kwa manufaa yenu na riziki zenu; basi kwa nini mnamuabudu pamoja naye yule ambaye hawapei chochote na wala hawanufaishi kwa chochote? Na kauli yake, \"Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uwongofu au upotofu ulio wazi.\" Yaani, moja katika makundi mawili haya, miongoni mwetu na miongoni mwenu, liko kwenye uwongofu na kuwa juu yake, au liko katika upotofu ulio wazi tayari limezama humo. Maneno haya yanasemwa na yule ambaye ukweli umemdhihirikia na usawa umemuwia wazi, na ambaye ana yakini juu ya haki aliyo juu yake na ubatili wa kile ambacho mpinzani wake yuko juu yake. Yaani, tumeeleza ushahidi mbalimbali ulio wazi kwetu na kwenu ambao kwa huo inajulikana kwa elimu ya yakini, isiyo na shaka yoyote ni nani miongoni mwetu aliye kwenye haki na ni nani aliye kwenye batili, na ni nani aliyeongoka na ni nani aliyepotea, kiasi kwamba kuashiria mmoja wetu katika hayo hakuna faida yoyote baada ya hilo. Kwani ukilinganisha baina ya yule anayelingania kumuabudu Muumba wa viumbe vyote, ambaye anaviendesha katika njia za kila aina, mpaji wa neema zote, ambaye aliwaruzuku na kuwafikishia kila aina ya neema na akawaepusha kila adhabu, ambaye sifa zote njema ni zake, na ufalme wote ni wake, na vitu vyote kuanzia Malaika na vyote vilivyo chini yao vinaunyenyekea ukubwa wake na kudhalilikia ukuu wake, na waombezi wote wanamuogopea. Na hakuna anayefanya uombezi miongoni mwao kwake isipokuwa kwa idhini yake yeye aliye juu, Mkubwa katika dhati yake, sifa zake, na vitendo vyake, ambaye ni mwenye ukamilifu wote, utukufu wote, uzuri wote, sifa zote na kuhimidiwa na heshima. Anayelingania kumkaribia yule ambaye hadhi yake ni hii na kumkusudia yeye tu katika matendo, na akataza kuabudu asiyekuwa Yeye, ikilinganishwa na anayekurubisha na vinavyoabudiwa visivyo Mwenyezi Mungu, na masanamu, na makaburi, ambavyo haviumbi wala haviruzuku, wala havijimilikii vyenyewe wala wale wanaoviabudu manufaa wala madhara, wala kifo, wala uhai wala ufufuo. Bali hivyo ni vitu visivyo na uhai ambavyo haviwezi kutumia akili wala havisikii maombi ya wale wanavyoviabudu, na hata kama vingewasikia, basi havingewaitikia. Na Siku ya Kiyama watakufuriana wao kwa wao na watajitenga mbali nao, na watalaaniana, na hata hawana fungu lolote katika ufalme wala ushirika ndani yake, wala kumsaidia Mwenyezi Mungu, na wala hawana uombezi ambao wamejitegemea katika kuufanya isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi huyu mshirikina anamuomba yule ambaye hii ndiyo sifa yake, na anajikurubisha kwake bila kujali ni kiasi gani anaweza, na anamfanyia uadui mwenye kumkusudia Mwenyezi Mungu tu katika dini yake na anampiga vita, na anawakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu waliokuja kwa mafundisho ya kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake. Basi kwa haya itakubainikia ni lipi katika makundi mawili haya lililoongoka na ni lipi potovu, na aliye mashakani na mwenye furaha, na hata hakuna haja ya kuonyeshwa ni nani hasa. Kwa sababu maelezo ya hali tu yako wazi zaidi kuliko kusema kwa maneno."},{"id":4585,"sura":34,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} \"Sema\" ukiwaambia: \"Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya, wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda nyinyi.\" Yaani, kila mmoja wetu ana matendo yake. Hamtaulizwa juu ya makosa yetu na dhambi zetu ikiwa tutatenda dhambi, nasi hatutaulizwa juu ya matendo yenu. Basi na liwe lengo letu na lenu ni kutafuta ukweli na kufuata njia ya usawa, na tuache yale tuliyokuwa tukiyafanya, wala hicho kisiwe kizuizi cha kuwafanya msifuate haki. Kwani hukumu za dunia zinakwenda kwa sura ya nje, na ukweli ndio unaofuatwa, na uwongo unaepukwa. Ama matendo hayo yana nyumba nyingine ambayo atahukumu huko Mbora wa wanaohukumu na kutenganisha kati ya mahasimu, yule ambaye ni Mwadilifu wa waadilifu wote."},{"id":4586,"sura":34,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} Ndiyo maana akasema: \"Sema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki.\" Nayo itakuwa hukumu ambayo kwayo atabainika mkweli na mwongo, na anayestahiki malipo mazuri na anayestahiki adhabu, naye ndiye mbora wa wanaohukumu."},{"id":4587,"sura":34,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} \"Sema, ewe Mtume ukiwaambia wewe na wale watakaochukua nafasi yako. \"Nionyesheni mliowaunganisha naye kuwa washirika;\" yaani, wako wapi? Na iko wapi njia ya kuwajua? Na Je, wako duniani au mbinguni? Kwani ameshatuambia Mjuzi wa ghaibu na yanayoshuhudiwa kuwa Yeye hana mshirika yeyote. \"Nao badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema: \"Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu!\" Sema, \"Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyoyajua...\" hadi mwisho wa Aya. \"Wala hawawafuati hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ni washirika wake. Wao hawafuati ila dhana tu, na hawasemi ila uwongo.\" Hali kadhalika wateule miongoni mwa viumbe wake, kama vile Manabii na Mitume, hawajui mshirika yeyote wake. Basi enyi washirikina, nionyesheni wale mliowaunganisha kwa madai yenu batili kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu! Swali hili hawawezi kulijibu, na ndiyo maana akasema: \"Hasha!\" Yaani, Mwenyezi Mungu hana mshirika yeyote, wala mwenza, wala mpinzani, \"bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu\" ambaye hakuna anayestahiki kufanyiwa uungu wala kuabudiwa isipokuwa Yeye, \"Mwenye nguvu\" ambaye alishinda kila kitu; kila kitu kisichokuwa Yeye kimeshindwa naye, na kinatiishwa na kuendeshwa. \"Mwenye hekima\" ambaye aliumba sawasawa vyote alivyoumba, na akafanya kuwa mazuri yale aliyoweka kuwa sheria. Na hata kama haingekuwa katika hekima na sheria yake isipokuwa kwamba aliamrisha kuwa apwekeshwe na akusudiwe Yeye tu katika dini, na akayapenda hayo na akayafanya kuwa ndiyo njia ya wokovu, na akakataza kumshirikisha na kumfanyia wenza wengine badala yake, na akaifanya hiyo kuwa ndiyo njia ya kuwa mashakani na kuangamia, basi hilo lingetosha kuwa uthibitisho tosha wa ukamilifu wa hekima yake. Basi inakuwaje ilhali kila alichoamrisha na kukataza kinajumuisha hekima?"},{"id":4588,"sura":34,"from_aya":28,"to_aya":30,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"28. Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui. 29. Na wanasema: \"Ahadi hii itakuwa lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?\" 30. Sema: \"Nyinyi mnayo miadi ya Siku ambayo hamtaakhirika nayo kwa saa moja, wala hamtaitangulia.\" "},{"id":4589,"sura":34,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kuwa hakumtuma Mtume wake \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie \u2013 isipokuwa kuwaletea habari njema watu wote kuhusu malipo ya Mwenyezi Mungu, na awajulishe matendo yanayosababisha hilo, na kuwaonya juu ya adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kuwafahamisha matendo yanayosababisha hilo. Nawe huna lako jambo katika suala hilo. Na kila kitu ambacho wale wanaokadhibisha, wakaidi wanakupendekezea sio katika kazi yako. Hilo liko mkononi mwa Mwenyezi Mungu. \"Lakini watu wengi hawajui\" kwa elimu sahihi. Bali ni wajinga au wakaidi ambao hawakufanyia kazi elimu yao, basi ni kana kwamba hawakuwa na elimu. Na katika yale yanayoonyesha kwamba hawajui ni kufanya kwao kule kutoitikiwa na Mtume juu ya yale waliyopendekeza, kuwa ndiyo sababu ya wao kuukataa wito wake."},{"id":4590,"sura":34,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Miongoni mwa waliyopendekeza ni kwamba waharakishiwe adhabu aliyowahadharisha nayo. Akasema: \"Na wanasema: Ahadi hii itakuwa lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?\" Na hii ni dhuluma kutoka kwao. Je, kuna uhusiano gani kati ya ukweli wake na kujulisha kuhusu wakati wa kutokea kwake? Na Je, huku si chochote ila ni kukataa haki na upumbavu katika akili? Je, si kweli kwamba mwonyaji katika mambo ya kidunia ikiwa atawajia watu wanaojua ukweli wake na nasaha zake nzuri, nao wana adui anayetaka kupata fursa kutoka kwao na kujiandaa kwa ajili yao, na mtu huyo akawaambia, 'Nimemwacha adui yenu hali ya kuwa ameshatoka anakuja kuwavamia na kuwatokomeza.' Basi ikiwa baadhi yao watasema, 'Ikiwa wewe ni mkweli, basi tuambie atatufikia saa ngapi? Yuko wapi sasa? Je, huyo mzungumzaji atachukuliwa kuwa na akili timamu au atachukuliwa kwamba ni mpumbavu na kichaa? Huyu mtoa habari anaweza kuwa mkweli au mwongo, na adui anaweza kuonekana kwamba ni adui ya hawa watu lakini si hivyo, na dhamira yake inaweza kudhoofika, na wanaweza kuwa na kizuizi cha kujilinda kwacho. Basi vipi yule ambaye anamkadhibisha mkweli wa viumbe vyote, ambaye amehifadhiwa kusema katika yale anayojulisha, ambaye hasemi kwa matamanio yake kuhusu adhabu yenye yakini, ambayo haiwezi kuzuilika, wala msaidizi kutokana nayo? Je, si kweli kwamba mwenye kukataa habari yake kwa hoja ya kwamba hakusema adhabu hiyo itakuja lini ni katika wapambavu wa wapumbavu wote?"},{"id":4591,"sura":34,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} \"Sema\" ukiwajulisha kuhusu wakati wa kutokea kwake ambao hapana shaka yoyote juu yake. \"Nyinyi mnayo miadi ya Siku ambayo hamtaakhirika nayo kwa saa moja, wala hamtaitangulia.\" Basi itahadharini siku hiyo na mjiandae vyema kwa ajili yake."},{"id":4592,"sura":34,"from_aya":31,"to_aya":33,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"31. Na walisema wale waliokufuru, \"Hatutaiamini Qur-ani hii, wala yale yaliyokuwa kabla yake.\" Na ungeliwaona madhalimu watakaposimamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, wakirudishiana maneno wao kwa wao! Wanyonge wakiwaambia wale waliotakabari, \"Lau kuwa si nyinyi, bila ya shaka tungelikuwa Waumini sisi.\" 32. Na wale waliotakabari watawaambia wanyonge, \"Kwani sisi ndio tuliwazuia na uwongofu baada ya huo kukujieni? Bali nyinyi wenyewe ni wahalifu.\" 33. Na wanyonge wakawaambia wale waliotakabari, \"Bali ni vitimbi vyenu vya usiku na mchana, mlipokuwa mkituamrisha tumkufuru Mwenyezi Mungu, na tumfanyie washirika.\" Nao wataficha majuto watakapoiona adhabu. Na tutaweka makongwa shingoni mwa wale waliokufuru. Kwani wanalipwa isipokuwa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda? "},{"id":4593,"sura":34,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} Mwenyezi Mungu alipotaja kwamba miadi ya wale wanaoharakisha adhabu lazima itokee wakati wake utakapowadia, akataja hapa hali yao siku hiyo, na kwamba lau ungeiona hali yao watakaposimama mbele ya Mola wao Mlezi, na viongozi na wafuasi katika ukafiri na upotofu wakakusanyika pamoja; basi ungeliona jambo kubwa na la kutisha, na ukaona jinsi watakavyogombana, na \"wakirudishiana maneno wao kwa wao!\" Wakasema, \"Wanyonge\" nao ndio wafuasi. \"Wakiwaambia wale waliotakabari\" nao ndio viongozi. \"Lau kuwa si nyinyi, bila ya shaka tungelikuwa Waumini sisi,\" lakini mlizuia baina yetu na Imani, na mkatupambia ukafiri, basi tukakufuateni katika hayo. Na kusudio lao kwa kusema hivi ni kwamba waadhibiwe viongozi badala ya wao kuadhibiwa."},{"id":4594,"sura":34,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} \"Na wale waliotakabari watawaambia wanyonge\" wakiwauliza na kuwajulisha kwamba wote walishiriki katika uhalifu huo. \"Kwani sisi ndio tulikuzuieni na uwongofu baada ya huo kukujieni?\" Yaani, kwa nguvu zetu na kuwatiisha kwa nguvu na kuwashinda, \"bali nyinyi wenyewe ni wahalifu.\" Yaani, wenyewe tu mlichagua kufanya uhalifu wala hamkulazimishwa kuufanya, hata kama tuliwapambia uhalifu huo, lakini hatukuwa na mamlaka yoyote juu yenu."},{"id":4595,"sura":34,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} Kisha wakasema, \"wanyonge wakawaambia wale waliotakabari, \"bali ni vitimbi vyenu vya usiku na mchana, mlipokuwa mkituamrisha tumkufuru Mwenyezi Mungu, na tumfanyie washirika.\" Bali kilichotupata na kutufikia kutoka kwenu cha kutupotosha ni vitimbi mlivyotupangia usiku na mchana. Mlipotufanyia ukafiri kuwa mzuri na mkatuita kwa huo na mkasema, 'Hii ndiyo haki', na mkaitia dosari haki yenyewe, na mkaichanganya na mkadai kuwa ni batili. Basi mkaendelea kutufanyia njama na vitimbi mpaka mkatupoteza na kututia majaribuni. Lakini kugombana kwao huku hakukuwafaidi chochote isipokuwa kukataana wao kwa wao, na majuto makubwa. Na ndiyo maana akasema, \"Nao wataficha majuto watakapoiona adhabu.\" Yaani, ikaisha hoja hiyo waliyoitumia baadhi yao ili kuepuka adhabu, na wakajua kuwa wao ni madhalimu wanaoistahiki, hivyo kila mmoja wao akajuta majuto makubwa mno, na akatamani - kisiri katika nafsi yake mwenyewe, kwa sababu ya hofu ya kufedheheshwa ikiwa watakiri uhalifu huu juu ya nafsi zao - lau kuwa angelikuwa kwenye haki, na lau kuwa aliiacha batili ambayo ilimfikisha kwenye adhabu hii. Katika baadhi ya matukio ya Kiyama na watakapokuwa wanaingia Motoni, watadhihirisha majuto hayo waziwazi. \"Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema, 'Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume!' Ee, ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki...\" hadi mwisho wa Aya. \"Na watasema: Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa na akili, tusingelikuwa katika watu wa Motoni! Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Motoni!\" \"Na tutaweka makongwa shingoni mwa wale waliokufuru.\" Wakafungwa minyororo kama vile anavyofungwa mfungwa atakayefedheheshwa katika jela. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Zitakapokuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa. Katika maji ya moto, kisha wanaunguzwa Motoni...\" hadi mwisho wa Aya. \"Kwani wanalipwa\" katika adhabu hii na mateso, na katika minyororo hii mizito, \"isipokuwa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda?\" Ya kufuru, kuvuka mipaka na kuasi."},{"id":4596,"sura":34,"from_aya":34,"to_aya":39,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"34. Na hatukumtuma mwonyaji yeyote kwenye mji, isipokuwa walisema wale waliojidekeza kwa starehe zao, wa mji huo, \"Hakika sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo.\" 35. Na wakasema, \"Sisi tuna mali nyingi zaidi na watoto, wala sisi hatutaadhibiwa.\" 36. Sema, \"Hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye. Lakini watu wengi hawajui.\" 37. Na si mali zenu wala watoto wenu watakaowasongesha karibu na sisi, muwe karibu sana, isipokuwa yule aliyeamini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu kwa yale waliyoyafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa. 38. Na wale wanaojitahidi kuzipinga Ishara zetu, wakaona watashinda, hao watahudhurishwa kwenye adhabu. 39. Sema: \"Kwa hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye katika waja wake. Na chochote mtakachokitoa, Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanaoruzuku.\" "},{"id":4597,"sura":34,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatujulisha kuhusu hali ya umma waliopita zamani, waliokadhibisha Mitume kwamba ni kama hali ya watu hawa waliopo sasa, wanaomkadhibisha Mtume wao Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - na kwamba Mwenyezi Mungu anapotuma Mtume katika mji miongoni mwa mji, wana starehe yake wanamkadhibisha, wakajivuna kwa neema zao walizopewa na wakajifahirisha kwazo."},{"id":4598,"sura":34,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} \"Na wakasema, \"Sisi tuna mali nyingi zaidi na watoto,' kuliko wale waliofuata haki. \"Wala sisi hatutaadhibiwa.\" Yaani, kwanza, sisi hatutafufuliwa. Lakini ikiwa tutafufuliwa, basi yule aliyetupa mali hizi na watoto katika dunia, atatupa mengi zaidi ya hayo katika akhera na wala hatatuadhibu."},{"id":4599,"sura":34,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36} Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu akawajibu kwamba kumkujulia mtu riziki na kumkunjia si ushahidi wa hayo mliyodai. Kwani, riziki iko chini ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu; akitaka, anamkunjulia mja wake, na akitaka, anamkunjia."},{"id":4600,"sura":34,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37} Na si mali na watoto \"ndizo\" humkurubisha mtu kwa Mwenyezi Mungu, \"akawa karibu sana.\" Bali kinachomkurubisha zaidi ni kuamini yale yaliyoletwa na Mitume na matendo mema, ambayo ni miongoni mwa matakwa ya imani. Hao, wana malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuzidishiwa jema moja kwa mara kumi mfano wake hadi mara mia saba, hadi mizidisho mingi asiyoijua isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake. \"Nao watakuwa salama katika maghorofa,\" mbali na matatizo na masumbuko yenye kuharibu starehe na aina mbalimbali za matamanio wanazozipata, na watakuwa salama kutokana na kuziacha starehe hizi na kuwa na huzuni ndani yake."},{"id":4601,"sura":34,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} Na ama wale wanaojitahidi katika Ishara zetu kwa njia ya kutufanya sisi na Mitume wetu kwamba hatuna uwezo na wakitukadhibisha, \"hao watahudhurishwa kwenye adhabu.\""},{"id":4602,"sura":34,"from_aya":39,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akarudia kusema: \"humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye katika waja wake,\" ili iwe kwamba \"chochote mtakachokitoa\" cha matumizi ya faradhi au yale yanayopendekezwa kwa jamaa, jirani, masikini, yatima, au wengineyo. \"Yeye\" Mtukufu \"atakilipa\" na usidhani kuwa kutoa matumizi ni katika mambo yanayopunguza riziki. Bali mwenye kutoa mali aliahidiwa na yule ambaye humkunjulia riziki amtakaye na kumkunjia amtakaye. \"Naye ni Mbora wa wanaoruzuku,\" basi tafuteni riziki kutoka kwake, na jitahidini kufanya sababu za riziki alizowamrisha."},{"id":4603,"sura":34,"from_aya":40,"to_aya":42,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"40. Na siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia Malaika, \"Je, hawa walikuwa wakikuabuduni?\" 41. Waseme, \"Subhanak (umetakasika). Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao. Bali wao walikuwa wakiwaabudu majini; wengi wao wakiwaamini hao.\" 42. Basi hii leo hataweza yeyote kumletea nafuu wala madhara mwenziwe. Na tutawaambia wale waliodhulumu, \"Onjeni adhabu ya Moto mliokuwa mkiukadhibisha.\" "},{"id":4604,"sura":34,"from_aya":40,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40 - 41} \"Na siku atakayowakusanya wote;\" wale wanaomuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na wale waliokuwa wakiabudiwa kama vile Malaika \"Kisha\" Mwenyezi Mungu \"atawaambia Malaika\" kwa njia ya kuwakemea wale waliokuwa wakiwaabudu, \"Je, hawa walikuwa wakikuabuduni?\" Lakini, wao wakajitenga mbali na ibada yao hiyo na \"Waseme, 'Subhanak (umetakasika),\" kuwa na mshirika na mwenza. \"Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao,\" Sisi wenyewe tunakuhitajia sana, basi vipi tutawaita wengine kutuabudu sisi? Lakini, wao wakajitenga mbali na ibada yao hiyo na \"Waseme, 'Subhanak (umetakasika)\" kuwa na mshirika na mwenza. \"Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao\" Sisi wenyewe tunakuhitajia sana, basi vipi tutawaita wengine kutuabudu sisi? Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo njia iliyonyooka,\" \"wengi wao wakiwaamini hao\" na kuwafuata majini. Kwa sababu imani ni kusadiki kunakomlazimu mtu kutii na kufuata."},{"id":4605,"sura":34,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} Walipojitenga mbali nao, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaambia, \"Basi hii leo hataweza yeyote kumletea nafuu wala madhara mwenziwe.\" Kwani, mafungamani ya baina yenu yameshakatika, nanyi kwa nyinyi mkatengana. \"Na tutawaambia wale waliodhulumu\" kwa kukufuru na kuasi baada ya kuwaingiza Motoni, \"Onjeni adhabu ya Moto mliokuwa mkiukadhibisha.\" Leo mmeuona na mkaingia humo kuwa ni malipo ya kukadhibisha kwenu na adhabu kwa sababu ya yale yaliyosababishwa na kukadhibisha huko ya kutokimbia sababu zake."},{"id":4606,"sura":34,"from_aya":43,"to_aya":45,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"43. Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wanasema: \"Huyu si chochote isipokuwa ni mtu anayetaka kuwazuia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zenu.\" Na wakasema: \"Haya si chochote isipokuwa ni uongo uliozuliwa.\" Na wale waliokufuru waliiambia haki ilipowajia: \"Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio dhahiri.\" 44. Wala hatukuwapa Vitabu wavisome, wala hatukuwatumia mwonyaji kabla yako wewe. 45. Na walikadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Na hawakufikia hata sehemu moja katika kumi ya tulivyowapa hao. Nao waliwakadhibisha Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani! "},{"id":4607,"sura":34,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu hali ya washirikina wanaposomewa Aya za Mwenyezi Mungu zilizo wazi, hoja zake zilizo dhahiri na ushahidi wake wa kukata, zinazoashiria kila heri na kukataza kila maovu, ambayo ndiyo neema kubwa zaidi iliyowajia, inayowahitaji kuitikia kwa kuiamini, kuisadiki, kuifuata, na kujisalimisha kwayo, kwamba wao huikabili kwa kuzuia yanayopasa kukubali, na kumkadhibisha yule aliyewaletea hayo. Na wanasema: \"Huyu si chochote isipokuwa ni mtu anayetaka kuwazuia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zenu.\" Yaani, haya ndiyo makusudio yake anapowaamrisha kumkusudia Mwenyezi Mungu tu, ili muache mila za baba zenu ambao mnawapa taadhima na kutembea nyuma yao. Kwa hivyo, wakaikataa haki kwa sababu ya kauli ya wapotevu, wala hawakutoa ushahidi wowote wala cha kutia shaka. Je, ni shaka gani iliyoko wakati Mitume wanawaamrisha baadhi ya watu wapotofu kufuata haki, nao wakadai kwamba ndugu zao wanaofuata njia yao hawajaacha kuifuata? Huu ndio upumbavu hasa na kuikataa haki kwa sababu ya maneno ya wapotofu. Na ukiitafakari kila haki iliyokataliwa, utakuta kwamba mwisho wake ulikuwa hivi. Haiwezi kukataliwa isipokuwa kwa sababu ya kauli za washirikina wapotofu, wasiomuamini Mwenyezi Mungu, wanafalsafa, Masabii, wale wanaopindukia mipaka katika dini ya Mwenyezi Mungu, waliokengeuka. Hao ndio kiigizo cha kila anayeikadhibisha haki mpaka Siku ya Kiyama. Na walipochukua vitendo vya baba zao kuwa ndivyo hoja, na wakavifanya kuwa ndivyo vya kuyazuia yale ambayo Mitume waliyaleta, wakaitia haki dosari, \"Na wakasema: 'Haya si chochote isipokuwa ni uongo uliozuliwa\" na mwanamume huyu aliyekuja nayo. \"Na wale waliokufuru waliiambia haki ilipowajia: 'Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio dhahiri\" kwa kila mtu. Walisema hivi ili kuikadhibisha haki, na kuwachochea wajinga."},{"id":4608,"sura":34,"from_aya":44,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{44} Na alipobainisha yale waliyoikataa haki kwa sababu yake, na kwamba hayo ni kauli ambazo hata haziwezi kumtia mtu shaka, mbali na kwamba zinaweza kufikia kiwango cha kuwa hoja, akasema kwamba ikiwa mtu atataka kuwasimamishia hoja, wao hawana chochote cha kukitegemea kabisa, \"Wala hatukuwapa Vitabu wavisome\" ili viwe msingi wao, \"wala hatukuwatumia mwonyaji kabla yako wewe.\" Ili kutoka kwa maneno yake na hali zake waweze kupata cha kukanushia yale uliyowaletea. Basi hawana elimu yoyote wala alama ya elimu."},{"id":4609,"sura":34,"from_aya":45,"to_aya":45,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{45} Kisha akawahofisha kwa yale aliyowafanyia umma waliokadhibisha kabla yao, akasema, \"Na walikadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Na hawakufikilia\" hawa wanaoongeleshwa, \"hata sehemu moja katika kumi ya tulivyowapa hao. Nao waliwakadhibisha;\" yaani, umma wa kabla yao \"Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani!\" Yaani, maonyo yangu na adhabu yangu kwao. Kwani alishatujulisha yale aliyowafanyia ya adhabu, na kwamba miongoni mwao wapo waliowagharikishwa, na wapo aliowaangamiza kwa upepo tasa, na kwa ukelele, na kwa tetemeko la ardhi, na kwa kudidimizwa katika ardhi, na kwa kutumwa tufani la kokoto kutoka mbinguni. Basi jihadharini, enyi mnaokadhibisha msije mkaendelea kukadhibisha hivyo akawaangamiza kama alivyowaangamiza wale waliokuwa kabla yenu, na mkapatwa na yale yaliyowapata."},{"id":4610,"sura":34,"from_aya":46,"to_aya":50,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"46. Sema: \"Mimi ninawanasihi kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote isipokuwa ni mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali.\" 47. Sema: \"Ujira niliowaomba ni wenu nyinyi. Sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu.\" 48. Sema: \"Hakika Mola wangu Mlezi anaondoa upotovu kwa haki. Yeye ndiye Mwenye kujua vyema ya ghaibu.\" 49. Sema: \"Kweli imefika, na batili haijitokezi, wala hairudi.\" 50. Sema: \"Ikiwa mimi nimepotea, basi nimepotea kwa kudhuru nafsi yangu mwenyewe. Na ikiwa nimeongoka, basi ni kwa sababu ya kunifunulia Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, aliye karibu.\" "},{"id":4611,"sura":34,"from_aya":46,"to_aya":46,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{46} Yaani, \"Sema: \"Ewe Mtume ukiwaambia hawa wanaokadhibisha, wakaidi, wanaojitahidi kuikanusha haki na kumkashifu yule aliyeileta: \"Mimi ninawanasihi kwa jambo moja tu.\" Na ninawaita kulifuata, ambalo ndiyo njia ya uadilifu wala siwaiti kufuata maneno yangu wala kuyaacha maneno yenu bila sababu ya kufanya hivyo. Na jambo hili ni \"kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja,\" kwa dhamira ya kufuata yaliyo sawa na kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, kwa pamoja, kwa kufanya utafiti na majadiliano, na pia kila mmoja akiwa peke yake, kisha kila mtu ajiongeleshe kuhusiana na hayo. Kwani, mkisimama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wawili wawili na mmoja mmoja, mtaweza kutumia fikira zenu vizuri na kuitafakari hali ya Mtume wenu. Je, yeye ni mwendawazimu na ana sifa za wendawazimu katika anayosema na katika mwonekano wake na tabia zake? Au yeye ni Nabii mkweli, anayewaonya kutokana na yatakayowadhuru ya adhabu kali iliyo mbele yenu? Ikiwa wangeyakubali mawaidha haya na kuyatumia, basi ingewabainikia zaidi kuliko wengine kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake \u2013 si kichaa. Kwa sababu mwonekano wake si kama mwonekano wa vichaa. Bali mwonekano wake ndio mwonekano bora zaidi, na harakati zake ndizo harakati nzuri zaidi, naye ndiye kiumbe mwenye tabia njema zaidi, mtulivu, mnyenyekevu, na mwenye heshima, mambo ambayo hayawi isipokuwa kwa mtu mwenye akili nzuri zaidi ya wote. Kisha, ikiwa wangetafakari mazungumzo yake yenye ufasaha mkubwa, matamshi yake mazuri, na maneno yake ambayo yanaijaza mioyo salama na imani, na yanatakasa nafsi, na yanasafisha mioyo, na yanachochea mtu kuwa na maadili mema, na yanahimiza mtu kuwa na heshima, na yanahofisha dhidi ya tabia mbaya na chafu. Na anapozungumza, macho yalimtazama kwa hofu, heshima na taadhima. Basi je, haya yanafanana na porojo za vichaa na maneno yao yanayofanana na hali zao? Basi kila anayetafakari hali yake na nia yake akiwa na nia ya kuuliza: Je, yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu au la? Sawa atafikiri peke yake au pamoja na mtu mwengine, basi atakuwa na yakini kwamba yeye ni Mtume wa kweli wa Mwenyezi Mungu, na Nabii wake wa kweli. Hasa, watu hawa wanaoongeleshwa, ambao yeye ni mwenzao na wanajua mwanzo na mwisho wa mambo yake."},{"id":4612,"sura":34,"from_aya":47,"to_aya":47,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{47} Na kuna kizuizi kingine kinachozuia nafsi kumfuata mlinganiaji kwenye haki, nacho ni kwamba anachukua mali za wale wanaomwitikia na anachukua ujira kwa sababu ya kuwalingania huko. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akabainisha kujitakasa kwa Mtume wake mbali na jambo hili, akasema: \"Sema: Ujira niliokuombeni,\" juu ya kufuata kwenu haki \"ni wenu nyinyi.\" \"Sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu.\" Yaani, elimu yake imekizunguka kile ninachokilingania. Kama ningekuwa mwongo, basi angenishika kwa adhabu yake. Naye pia ni shahidi juu ya matendo yenu. Atawahifadhia matendo hayo, kisha atawalipa juu yake."},{"id":4613,"sura":34,"from_aya":48,"to_aya":48,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{48} Alipobainisha ushahidi unaoonyesha usahihi wa haki na ubatili wa uongo, Yeye Mtukufu akajulisha kuwa hii ndiyo ada yake na destruri yake, kwamba huitupa haki juu ya batili; na haki hiyo ikaiharibu hiyo batili na kuiondoa. Kwa sababu aliibainisha haki mahali hapa, na akakanusha kwayo kauli za wakadhibishaji, jambo ambalo lilikuwa ni mazingatio kwa wanaozingatia, na ishara kwa wanaotafakari. Kwani, kama unavyoona yametoweka maneno ya wanaokadhibisha, na ukabainika uongo wao na ukaidi wao, nayo haki ikadhihiri na kung'aa, nayo batili ikabatilika na kukomeka kabisa, na hayo ni kwa sababu ya ubainisho wa \"Mwenye kujua vyema ya ghaibu,\" ambaye anajua vilivyomo ndani ya nyoyo kama vile wasiwasi na fikira potofu. Na anajua hoja zinazokabiliana na hayo na kuyazuia. Basi anawafundisha waja wake na kuwabainishia hayo yote."},{"id":4614,"sura":34,"from_aya":49,"to_aya":49,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{49} Ndiyo maana akasema: \"Sema:'Kweli imefika.\" Yaani, amedhihiri na kubainika mpaka ikawa kama jua, na mamlaka yake yakadhihirika, \"na batili haijitokezi, wala hairudi.\""},{"id":4615,"sura":34,"from_aya":50,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"50. Na haki ilipobainika kwa yale aliyolingania Mtume, na wale walioikadhibisha walikuwa wakiizulia kwamba ni upotofu, yeye akawajulisha haki hiyo na akawawekea wazi, na akawabainishia kutoweza kwao kuipinga. Na akawaambia kwamba kumtuhumu kwao kwamba ni mpotofu hakuidhuru haki kwa vyovyote vile wala kuzuia yale aliyokuja nayo. Na kwamba akipotoka - na hasha litokee hili, lakini ilikuwa tu ni njia ya kujiweka katika kiwango kimoja nao ili aweze kujadili nao - basi yeye mwenyewe tu ndiye anayepotea, na si mwengine. \"Na ikiwa nimeongoka,\" basi si kutokana na nafsi yangu mwenyewe, na uwezo wangu na nguvu zangu. Lakini uwongofu wangu ni kwa sababu ya \"kunifunulia Mola wangu Mlezi.\" Kwani Yeye ndiye kiini cha uwongofu wangu kama vile Yeye ndiye kiini cha uwongofu wa watu wengine. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia maneno na sauti zote, yuko karibu na mwenye kumuomba dua na kumuomba kitu na akamuabudu."},{"id":4616,"sura":34,"from_aya":51,"to_aya":54,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"51. Na lau ungeliona watakapobabaika, basi hapana pa kukimbilia! Na watakamatwa mahala pa karibu. 52. Na watasema: \"Tunaiamini!\" Lakini wataipata wapi kutoka huko mahala mbali? 53. Na hapo kabla yake waliikataa, na wakiyatupilia mbali maneno ya ghaibu kutoka mahali mbali. 54. Na watatiliwa kizuizi baina yao na hayo wanayoyatamani, kama walivyofanyiwa wenzao zamani. Hakika hao walikuwa na shaka ya kutia wasiwasi. "},{"id":4617,"sura":34,"from_aya":51,"to_aya":51,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{51} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na lau ungeliona,\" ewe Mtume na yeyote atakayechukua nafasi yako, hali ya hawa waliokadhibisha \"watakapobabaika\" watakapoiona adhabu na yale ambayo Mitume waliwahadithia, na yale waliyoyakadhibisha, ungeliona manadhari makubwa, jambo la kuogofya, na hali ya kuchukiza, na dhiki kubwa mno. Na hapo ndipo itakapowawajibikia adhabu, na hawatakuwa na pa kukimbilia ili kuiepuka. \"Na watakamatwa mahala pa karibu,\" ambapo si mbali na mahali pa adhabu. Bali watachukuliwa na kutupwa Motoni."},{"id":4618,"sura":34,"from_aya":52,"to_aya":52,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{52} \"Na watasema\" katika hali hiyo: tulimuamini Mwenyezi Mungu, na tukayasadiki yale tuliyoyakadhibisha. \"Lakini wataipata wapi\" imani hiyo \"kutoka huko mahala mbali?\" Kwani tayari imeshazuiliwa baina yao na suala la kuamini, na hilo likawa ni miongoni mwa mambo yasiyowezekana katika hali hii."},{"id":4619,"sura":34,"from_aya":53,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{53} Lau wangeamini ilipokuwa bado inawezekana, basi imani yao hiyo ingelikubaliwa. Lakini wao \"hapo kabla yake waliikataa, na wakayatupilia mbali maneno ya ghaibu kutoka mahali mbali,\" walipokuwa wanatupa batili kwenye haki ili kuiangamiza, lakini hakuna njia yoyote ya kufanya hivyo sasa. Kama vile hakuna njia yoyote ya kutupa kitu kutokea mahali pa mbali na kugonga shabaha; basi vile vile haiwezekani kwa batili kuishinda haki au kuiondoa. Bali, batili huwa tu na nguvu wakati haki imeighafilikia. Lakini pindi haki inapodhihiri na kuipinga batili, inaitokomeza."},{"id":4620,"sura":34,"from_aya":54,"to_aya":54,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{54} \"Na watatiliwa kizuizi baina yao na hayo wanayoyatamani\" miongoni mwa starehe, watoto, mali, watumishi na majeshi. Watabakia peke yao na matendo yao, na wakaja kila mmoja peke yake kama walivyoumbwa, na wakaacha nyuma ya migongo yao yale waliyopewa, \"kama walivyofanyiwa wenzao zamani\" katika umma uliotangulia. Wakati walipojiwa na maangamizo, ilizuiliwa kati yao na yale waliyokuwa wanayatamani. \"Hakika hao walikuwa na shaka ya kutia wasiwasi.\" Na ndiyo maana hawakuamini, na wala hawakutubu walipotakiwa kutubu."},{"id":4621,"sura":34,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya Surat Sabaa. Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, na neema na fadhila. Tunaomba msaada kutoka kwake na kwake tunategemea, na tuna imani naye."}]}