{"result":[{"id":4688,"sura":36,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Yasin"},{"id":4689,"sura":36,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"[Nayo] ilishuka Makka"},{"id":4690,"sura":36,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":4691,"sura":36,"from_aya":1,"to_aya":12,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Ya-Sin 2. Kwa Haki ya Qur-ani yenye hekima! 3. Hakika wewe ni miongoni mwa waliotumwa. 4. Juu ya njia iliyonyooka. 5. Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu. 6. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika. 7. Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini. 8. Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu. 9. Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao. Na tumewafunika macho yao, kwa hivyo hawaoni. 10. Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini. 11. Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman (Mwingi wa rehema), kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema. 12. Hakika Sisi tunawafufua wafu na tunayaandika wanayoyatanguliza, na wanayoyaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari la asili lenye kubainisha. "},{"id":4692,"sura":36,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Hiki ni kiapo kitokacho kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Qur-ani yenye hekima. Ambayo sifa yake ni hekima, ambayo ni kuweka kila kitu mahali pake pafaapo. Kuweka maamrisho na makatazo mahali pake panapofaa, na kuweka malipo ya wema na ya uovu mahali pake panapofaa. Kwa hivyo, hukumu zake za kisheria na za kimalipo zote zina hekima ya hali ya juu. Miongoni mwa hekima za Qur-ani hii ni kwamba inajumuisha kutaja hukumu na hekima yake. Kwa hivyo ikazitanabahisha akili juu ya uwiano na sifa zinazohitaji kuwepo hukumu hiyo juu ya kitu hicho."},{"id":4693,"sura":36,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} \"Hakika wewe ni miongoni mwa waliotumwa.\" Na kwamba wewe Muhammad - rehema na amani zimshukie - si wa kwanza miongoni mwa Mitume. Na pia, ulikuwa na misingi ile ile waliyokuja nayo Mitume wa kabla yako. Na pia, Mwenye kutafakari hali na sifa za Mitume na akajua tofauti iliyoko baina yao na watu wengineo, atajua kwamba wewe Muhammad ni miongoni mwa Mitume bora zaidi kwa sababu ya sifa zako kamilifu na maadili bora. Hapa, haufichikani mfungamano ulioko baina ya kile ambacho Mwenyezi Mungu anaapa juu yake ambacho ni Qur-ani yenye hekima, na ujumbe wa Mtume Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake. Na kwamba hata kama utume wake haukuwa na hoja yoyote wala ushahidi isipokuwa Qur-ani hii yenye hekima, basi hilo tu lingetosha kuwa ushahidi juu ya utume wa Muhammad - rehema na amani zimshukie. Bali Qur-ani tukufu ndiyo ushahidi mkubwa zaidi unaoendelea juu ya utume wa Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake."},{"id":4694,"sura":36,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Kisha akajulisha juu ya sifa kubwa zaidi ya Mtume \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie \u2013 ambayo inaonyesha utume wake. Nayo ni kuwa yuko \"Juu ya njia iliyonyooka\" yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na nyumba ya utukufu wake. Na njia hiyo iliyonyooka inajumuisha matendo, ambayo ni matendo mema yenye kutengeneza moyo, mwili, dunia na Akhera, na maadili mema yanayotakasa nafsi, yanayosafisha moyo na kuongeza malipo. Na hii ndiyo njia iliyonyooka ambayo ndiyo sifa ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na ndiyo sifa ya dini yake aliyokuja nayo. Basi tafakari utukufu wa Qur-ani hii Tukufu. Vipi iliunganisha kati ya kuapa kwa viapo vitukufu na elimu ya Mwenyezi Mungu peke yake inatosha. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu aliweka ushahidi ulio wazi na hoja za kung'aa mahali hapa, juu ya usahihi wa yale aliyoapa kwayo ya kwamba Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake. Jambo ambalo kwalo ametutanabahisha na akatuashiria kwa ishara bora zaidi juu ya kufuata njia yake hii."},{"id":4695,"sura":36,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} Na njia hii iliyonyooka ni \"Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.\" Kwani ni katika njia hii ndiyo aliteremsha Kitabu chake na akakiteremsha kuwa ni njia kwa waja wake, inayowafikisha kwake. Na akakilinda kwa nguvu zake kutokana na mageuzi na mabadiliko. Na akawarehemu waja wake kwacho rehema kwa rehema walizoendelea kuwa nazo mpaka zikawafikisha katika nyumba ya rehema zake. Na ndiyo maana akahitimisha Aya hii kwa majina haya mawili matukufu: Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu."},{"id":4696,"sura":36,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} Mwenyezi Mungu alipoapa kwa ujumbe wake, na kuuthibitisha kwa ushahidi mbalimbali, akataja haja kubwa ya viumbe juu yake, akasema: \"Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika.\" Ambao ni wale Waarabu wasiojua kusoma na kuandika, ambao bado hawakuwa na vitabu na Mitume, ambao walikuwa wamejumuishwa na ujinga na kugubikwa na upotofu, na akili za walimwengu zikawacheka kwa upumbavu wao. Basi Mwenyezi Mungu akawatumia Mtume kutokana nao wenyewe, ili awatakase na awafundishe Kitabu na hekima, ijapokuwa kabla ya hapo walikuwa katika upotofu uliowazi. Alipaswa kuwaonya Waarabu wasiojua kusoma na kuandika na watu wote wanaofanana nao miongoni mwa wale wasiojua kusoma na kuandika, na awakumbushe Watu wa Kitabu vitabu walivyo navyo. Kwa hivyo, Mtume huyu akawa ni neema ya Mwenyezi Mungu juu ya Waarabu hasa na juu ya watu wengine kwa ujumla."},{"id":4697,"sura":36,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Lakini hawa uliotumwa kwao ili uwaonye, baada ya kuwaonya waligawanyika sehemu mbili; kundi lililokataa yale uliyowajia nayo na wala halikukubali maonyo, na hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu alisema juu yao: \"Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini.\" Hilo liliwafika baada ya kufikishiwa haki lakini wakaikataa. Hapo, wakaadhibiwa kwa kuzibwa nyoyo zao."},{"id":4698,"sura":36,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} Akavitaja vizuizi vilivyozuia imani kufika nyoyoni mwao, akasema: \"Hakika sisi tumeweka makongwa shingoni mwao.\" Pingu hizi zilizo shingoni mwao ni kubwa, kiasi kwamba zimefikia videvu vyao na zikaviinua vichwa vyao juu. \"Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu.\" Kwa sababu ya mvuto mkubwa wa pingu iliyo shingoni mwao, hawawezi kuzipunguza."},{"id":4699,"sura":36,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} \"Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao,\" vilivyowazuia kuamini. \"Kwa hivyo hawaoni,\" kwa maana ujinga wao na uovu wao umewafunika kila upande. Kwa hivyo maonyo hayakuwafaa kitu."},{"id":4700,"sura":36,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} \"Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini.\" Na vipi ataamini yule ambaye alizibwa moyo na akaiona haki kuwa ndiyo batili na kwamba batili ndiyo haki?"},{"id":4701,"sura":36,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} Kundi la pili ni wale waliokubali maonyo, nao aliwataja kwa kauli yake: \"Hakika wewe unamwonya.\" Yaani, maonyo yako na mawaidha yako yanamfaa \"mwenye kufuata ukumbusho na akamcha Arrahman (Mwingi wa rehema), kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema kwa sababu ya matendo yake mema na nia yake nzuri."},{"id":4702,"sura":36,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} \"Hakika Sisi tunawafufua wafu\" ili tuwalipe kwa matendo yao. Na tunayaandika wanayoyatanguliza miongoni mwa mambo mema na maovu waliyotenda katika uhai wao, \"na wanayoyaacha nyuma\" ambazo ni athari za heri na athari za shari ambazo walikuwa wao ndio sababu ya kutokea kwake wakati wa uhai wao na baada ya kufa kwao. Na vile vitendo vilivyotokana na maneno yao, vitendo vyao na hali zao. Kila heri aliyofanya mtu kwa sababu ya elimu aliyochukua kwa mtu fulani, au aliyomfundisha, au nasaha, kumuamrisha mema, au kumkataza maovu, au elimu aliyofunza wanafunzi au aliyoandika katika vitabu vyenye kunufaisha wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake. Au akafanya heri kama vile swala, zaka, sadaka, au ihsani, kwa hivyo wengine wakamuiga, au alijenga msikiti au mahali ambapo watu wanakaa na mengineyo; basi hayo yote ni katika athari zake ambazo ameandikiwa, pamoja na matendo yake maovu. Ndiyo maana Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema: \u201cMwenye kuanzisha mwenendo mwema atapata ujira wake na ujira wa mwenye kuutenda mpaka Siku ya Kiyama. Na mwenye kuanzisha mwenendo muovu, basi mzigo wake uko juu yake, na mzigo wa mwenye kuutenda mpaka Siku ya Kiyama.\" Sehemu hii inakuonyesha kiwango cha juu cha kulingania kwa Mwenyezi Mungu na kuongoka kufikia njia yake kwa kila njia inayofikisha kwenye hilo, na kiwango cha chini cha kiongozi wa kulingania kwenye uovu. Na kwamba yeye ndiye kiumbe wa chini kabisa, na mkubwa wao zaidi katika uhalifu, na mwenye madhambi kubwa zaidi yao wote. \"Na kila kitu\" miongoni mwa matendo, makusudio na mambo mengineyo \"tumekihifadhi katika daftari la asili lenye kubainisha.\" Yaani, Kitabu ambacho ni mama wa vitabu vyote, na kwake ndiyo marejeo ya vitabu vilivyo mikononi mwa Malaika, nacho ndio Ubao Uliohifadhiwa."},{"id":4703,"sura":36,"from_aya":13,"to_aya":32,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"13. Na wapigie mfano wa wakazi wa mji walipojiwa na Mitume. 14. Tulipowatumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: \"Hakika sisi tumetumwa kwenu.\" 15. Wakasema: \"Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uongo tu.\" 16. Wakasema: \"Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu.\" 17. Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi. 18. Wakasema: \"Sisi tumeamua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu.\" 19. Wakasema: \"Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu waliopindukia mipaka.\" 20. Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: \"Enyi watu wangu! Wafuateni hawa waliotumwa.\" 21. Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka. 22. Na kwa nini nisimuabudu yule aliyeniumba na kwake nitarejeshwa? 23. Je, niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani (Mwingi wa Rehema) akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa. 24. Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhahiri. 25. Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni! 26. Akaambiwa: \"Ingia Peponi!\" Akasema: \"Laiti kuwa watu wangu wangelijua. 27. Jinsi Mola wangu Mlezi alivyonisamehe, na akanifanya miongoni mwa walioheshimiwa. 28. Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha. 29. Hakukuwa ila ukelele mmoja tu, na mara walizimwa! 30. Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli. 31. Je, hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao. 32. Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu. "},{"id":4704,"sura":36,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Hii inamaanisha kwamba: Hawa wanaokadhibisha ujumbe wako, wanaokataa wito wako, wapigie mfano watakaouzingatia na ambao utakuwa ni mawaidha kwao ikiwa watawezeshwa kufikia heri. Na mfano huo ni watu wa mji fulani na yale waliyoyafanya ya kuwakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu na adhabu na mateso yaliyowafikia. Na ikiwa kungekuwa na faida katika kujua jina la mji huo hasa, basi Mwenyezi Mungu angelitaja jina lake. Kwa hivyo, kujishughulisha na hilo na jambo lolote linalofanana na hilo ni katika kujisumbua tu na mambo ambayo mtu hana elimu yake. Ndiyo maana, ukimsikia mtu akizungumzia mambo hayo, utakuta ndani yake mchanganyiko na tofauti mbalimbali zisizokuwa na uhakika, jambo linalotufanya kujua kwamba njia sahihi ya elimu ni kusimama pamoja na uhakika wa mambo na kuacha kujisumbua na mambo yasiyokuwa na faida, na kwa hayo nafsi inatakasika na elimu yake inaongezeka. Naye mjinga anadhani lililo sahihi ni kuzidisha kutaja kauli zisizo na ushahidi wala uthibitisho wala zisizo na faida isipokuwa kuchanganya akili na kutegemea juu ya mambo yenye kutiliwa shaka. Na ushahidi ni kwamba Mwenyezi Mungu alikifanya kijiji hiki kuwa mfano kwa wale wanaoongeleshwa. \"Walipojiwa na Mitume\" kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; wakiwaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kumkusudia Yeye tu katika Dini, na wakiwakataza kumshirikisha na kumuasi."},{"id":4705,"sura":36,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} \"Tulipowatumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwengine wa tatu.\" Kwa hivyo wakawa Mitume watatu; kutokana na Mwenyezi Mungu kuwajali mno, na kwa sababu ya kuwasimamishia hoja kwa kuwatumia Mitume kwa kufuatanisha. Wakasema: \"Hakika sisi tumetumwa kwenu.\""},{"id":4706,"sura":36,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15} Lakini wao wakawajibu kwa jawabu ambalo bado ni maarufu miongoni mwa wale waliokanusha wito wa Mitume, wakasema: \"Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi.\" Yaani, ni kitu gani kilichokufadhilisheni nyinyi juu yetu na kikawafanya kuwa maalumu zaidi kutuliko sisi? Mitume hao wakawaambia kaumu zao: \"Sisi kweli si chochote ila ni wanadamu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humfanyia hisani amtakaye katika waja wake.\" \"Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu.\" Yaani, walikanusha ujumbe kwa ujumla, kisha wakawapinga hao waliokuwa wanawaongelesha, wakasema: \"Nyinyi mnasema uongo tu.\""},{"id":4707,"sura":36,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} Kwa hivyo, Mitume hao watatu wakasema: \"Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu.\" Na lau kuwa tulikuwa waongo, basi Mwenyezi Mungu angedhihirisha hizaya yetu na angetuharakishia adhabu."},{"id":4708,"sura":36,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} \"Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe wazi wazi.\" Ambako kwa huo mambo yanayohitajika kubainishwa yanawekwa wazi. Na zaidi ya haya miongoni mwa ishara wanazopendekeza wao au kuharakishiwa adhabu, siyo juu yetu, bali kazi yetu ambayo ni kufikisha ujumbe wazi wazi, tayari tumeshaifanya. Kwa hivyo, mkiongoka, basi hiyo ni bahati yenu na kuwezeshwa kwenu. Lakini ikiwa mtapotea, basi hatuna chetu kitu katika jambo hilo."},{"id":4709,"sura":36,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"18. Basi watu wa kijiji hicho wakawaambia Mitume wao: \"Sisi tumeamua kuwa nyinyi ni wakorofi.\" Yaani, hatukuona katika kutujia  kwenu na kuingiliana kwenu nasi isipokuwa uovu tu. Lakini hili ni katika maajabu makubwa zaidi ya yote. Kwamba walimfanya yule aliyewajia na neema kubwa zaidi ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwayo waja wake, na utukufu mkubwa zaidi aliowakirimu kwa huo, na haja yao juu ya hilo iliyokuwa kubwa zaidi ya mahitaji mengine yote, kwamba alikuja na hali ya uovu ambayo iliwazidishia uovu waliokuwa nao, na wakaona mkosi ndani yake. Lakini huko ni kuachiliwa mbali na Mwenyezi Mungu na kutowezeshwa kunaweza kumfanya mtu huyo mambo makubwa zaidi ya anavyoweza kufanyiwa na adui yake. Kisha wakawatishia wakisema: \"Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe.\" Yaani, tutawauwa kwa kuwapiga mawe vibaya kabisa. \"Na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu.\""},{"id":4710,"sura":36,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} Basi Mitume wao hao wakawaambia: \"Ukorofi wenu mnao wenyewe!\" Nao ni ushirikina walionao, na uovu unaopelekea kutokea balaa, adhabu na kuondokewa na mambo wayapendayo na neema. \"Je, ni kwa kuwa mnakumbushwa mambo yenye kutengenea kwenu na bahati yenu nzuri, basi ndiyo mkatuambia hayo mliyosema? Ama nyinyi ni watu waliopindukia mipaka.\" Basi kuwalingania huko hakukuwazidisha isipokuwa kujitenga na kiburi."},{"id":4711,"sura":36,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} \"Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini\" akiwa na hima kubwa ya kuwapa nasaha watu wake, aliposikia yale waliyoyalingania Mitume hao. Kwa hivyo akayaamini, na akajua yale waliwajibu nayo watu wake Mitume hao. Akawaambia: \"Enyi watu wangu! Wafuateni hawa waliotumwa.\" Kwa hivyo akawaamuru wawafuate, akawashauri wafanye hivyo, na akawashuhudilia kwamba ni Mitume."},{"id":4712,"sura":36,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} Kisha akataja kinachounga mkono yale aliyoyashuhudia na kuyalingania, akasema: \"Wafuateni ambao hawakutakini ujira.\" Yaani, wafuateni wale waliokunasihini kwa njia ambayo itakuleteeni heri, na wala hawataki mali zenu wala malipo yoyote kwa nasaha yao waliyowapa wala kuwaelekeza kwao walikowaelekeza. Haya yanalazimu kwamba afuatwe mtu ambaye hizi ndizo sifa zake. Inabakia kusema: Labda analingania bila ya kuomba ujira, lakini hayuko kwenye haki. Basi akazuia hili kwa kauli yake: \"Hali ya kuwa wenyewe wameongoka.\" Kwa sababu hawalinganii isipokuwa kwenye yale ambayo akili timamu inashuhudia uzuri wake, na wala hawakatazi isipokuwa yale ambayo akili timamu inashuhudia kwamba ni mabaya."},{"id":4713,"sura":36,"from_aya":22,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22 - 25} Ni kana kwamba watu wake hawakukubali nasaha yake, bali walimlaumu kwa kuwafuata Mitume hao na kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika Dini. Basi akasema: \"Na kwa nini nisimuabudu yule aliyeniumba na kwake nitarejeshwa?\" Kwani yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa, kwa sababu Yeye ndiye aliyeniumba, na akaniruzuku, na kwake Yeye ndiye marejeo ya viumbe vyote. Kwa hivyo Yule ambaye mkononi mwake ndiko kuko kuumba, kuruzuku na kuhukumu baina ya waja duniani na akhera ndiye anayestahiki kuabudiwa, kusifiwa, na kuhimidiwa na si yule ambaye hamiliki manufaa wala madhara wala kupeana wala kuzuia wala mauti wala uhai wala kufufua. Ndiyo maana akasema: \"Je, niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani (Mwingi wa Rehema) akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu,\" kwa sababu hapana anayeweza kufanya uombezi kwa Mwenyezi Mungu ila kwa idhini yake. Kwa hivyo, uombezi wa hao hautanifaa kitu \"wala hawataniokoa\" kutokana na madhara ambayo Mwenyezi Mungu alinitakia. \"Basi hakika mimi hapo\" ikiwa nikiwaabudu miungu ambao hizi ndizo sifa zao \"nitakuwa katika upotovu ulio dhahiri.\" Basi akaunganisha katika maneno haya kati ya kuwanasihi na kuwashahidilia Mitume hao kwamba ni Mitume, na kwamba ni waongofu. Na kujulisha kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa, na akataja ushahidi juu ya hayo, na kwamba kumuabudu asiyekuwa Yeye ni batili, na akataja ushahidi wa hilo, na akajulisha kwamba wenye kuabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu ni wapotofu, na kutangaza imani yake hadharani pamoja na kuhofu sana kwamba wanaweza kumuua. Alisema: \"Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni!\""},{"id":4714,"sura":36,"from_aya":26,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26 - 27} Kwa hivyo, watu wake wakamuua waliposikia kutoka kwake, na akawaambia yale aliyowaambia. \"Akaambiwa\" papo hapo; \"Ingia Peponi!\" Basi akasema akijulisha kuhusu yale aliyoyafikia ya utukufu kwa sababu ya kumpwekesha kwake Mwenyezi Mungu na kumkusudia katika dini, na kuwanasihi watu wake, baada ya kufa kwake kama alivyowanasihi katika uhai wake: \"Laiti kuwa watu wangu wangelijua. Jinsi Mola wangu Mlezi alivyonisamehe,\" na akaniondoshea aina zote za adhabu \"na akanifanya miongoni mwa walioheshimiwa,\" kwa kila aina ya malipo na mambo ya kufurahisha. Na lau kuwa nyoyo zao zitapata kujua haya, basi hawangeendelea kushikamana na ushirikina wao."},{"id":4715,"sura":36,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Mwenyezi Mungu alisema kuhusu namna walivyoadhibiwa watu wake: \"Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni\" ili liwaangamize. \"Wala si wenye kuteremsha.\" Kwa sababu hakukuwa na haja ya kufanya hivyo, na ukubwa wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ukubwa wa udhaifu wa wanadamu, na kwa sababu kinawatosha hata kitu kidogo tu cha adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu."},{"id":4716,"sura":36,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} \"Hakukuwa ila ukelele mmoja tu\" waliotoa baadhi ya malaika wa Mwenyezi Mungu. \"Na mara walizimwa!\" Nyoyo zao zilichanikachanika ndani ya miili yao, na wakafadhaika kwa sababu ya ukelele huo. Kwa hivyo wakazimika, hawakuweza kutoa sauti wala harakati wala uhai baada ya ufidhuli wao ule na kiburi, na kuwakabili viumbe watukufu zaidi kwa maneno hayo machafu na kuwafanyia jeuri."},{"id":4717,"sura":36,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akiwarehemu waja: \"Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli.\" Yaani, ni upotofu wao upi mkubwa huu, na ukaidi mkubwa huu, na ujinga gani mkubwa huu ambapo waliamua kuwa na sifa hizi mbaya ambazo ndizo sababu ya kuwa mashakani kabisa, na kupata adhabu na mateso."},{"id":4718,"sura":36,"from_aya":31,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31 - 32} \"Je, hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao.\" \"Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu.\" Mwenyezi Mungu anasema: \"Je, hawakuona hawa na kuzingatia ni kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, na kwamba kwao hawatarejea katika dunia?\" Mwenyezi Mungu atawarudisha wote kwa umbo jipya, na atawafufua baada ya kufa kwao, na watahudhuria mbele yake Mtukufu; ili ahukumu baina yao kwa hukumu yake ya uadilifu, ambaye hadhulumu hata uzito wa chembe. Na ikiwa ni jambo jema, basi Yeye atalizidisha na atapeana malipo makubwa kutoka kwake."},{"id":4719,"sura":36,"from_aya":33,"to_aya":36,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"33. Na Ishara hiyo kwao ni ardhi iliyokufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanakula katika hizo! 34. Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemichemi ndani yake. 35. Ili wale katika matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru? 36. Ametakasika yule aliyeumba dume na jike vyote katika vinavyomea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyovijua. "},{"id":4720,"sura":36,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} Yaani, \"Na Ishara hiyo kwao\" juu ya kufufuliwa na kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu kwa malipo ya vitendo hivyo. Mwenyezi Mungu aliiteremshia mvua na akaihuisha baada ya kufa kwake. \"Na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanakula katika hizo!\" Na kila aina ya mazao na mimea wanayokula wanyama wao."},{"id":4721,"sura":36,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} \"Na tukafanya ndani yake;\" yaani, katika ardhi hiyo iliyokufa \"mabustani\" yenye miti mingi, hasa mitende na mizabibu, ambayo ndiyo miti bora zaidi. \"Na tukatimbua ndani yake;\" yaani, katika ardhi \"chemchemi.\" Na tumeifanya katika ardhi hiyo miti na mitende na zabibu."},{"id":4722,"sura":36,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} \"Ili wale katika matunda yake\" kama chakula chao kikuu, na matunda ya kawaida, na kitoweo kwa vyakula vingine na wapate kufurahia. \"Na\" hali ni kwamba matunda haya \"hayakufanywa na mikono yao\" bali ilikuwa ni kazi ya mikono ya Mwenye hekima zaidi ya wote, na mbora wa wanaoruzuku. Pia si mikono yao iliyoyafanya kwa kuyapika au kitu kingine chochote. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyeyaumba matunda haya bila kuhitaji kupikwa wala chochote. Hayo yanachukuliwa tu kutoka kwenye miti yake na kuliwa moja kwa moja. \"Basi je, hawashukuru,\" yule aliyewapa neema hizi na akawajaalia mengi kwa ukarimu mkubwa mambo ambayo kwayo yanatengenea mambo yao ya kidini na ya kidunia? Je, yule aliyeihuisha ardhi baada ya kufa kwake, kisha akaotesha humo mazao, miti, na akatia humo matunda matamu, na akaipasua ardhi kavu iliyokuwa imekufa kwa chemichemi? Kwani huyo hana uwezo wa kuwafufua wafu? Ndiyo, Yeye ni Muweza wa kila kitu."},{"id":4723,"sura":36,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36} \"Ametakasika yule aliyeumba dume na jike vyote katika vinavyomea katika ardhi.\" Basi akavifanya kuwa aina mbalimbali ambazo ni vigumu kuvidhibiti. \"Na katika nafsi zao\" pia akawafanya kuwa wanaume na wanawake, na akatofautisha baina ya maumbile yao, tabia zao, na sifa zao za dhahiri na zilizofichikana. \"Na katika wasivyovijua\" miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa lakini hatujavijua bado. Na pia viumbe ambavyo bado havijaumbwa. Basi ametakasika na kutukuka kuwa na mshirika, msaidizi, waziri, mwenza, mtoto, mwenye jina kama lake, mwenye kulingana naye, au mfano wake katika sifa za ukamilifu wake na sifa za ukuu wake, au kuwepo kitu kinachoweza kumshinda kufanya atakavyo."},{"id":4724,"sura":36,"from_aya":37,"to_aya":40,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"37. Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani. 38. Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua vyema. 39. Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe. 40. Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao. "},{"id":4725,"sura":36,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37} Yaani, \"Na Ishara kwao\" inayoonyesha kutekelezeka kwa mapenzi yake, ukamilifu wa uwezo wake, na kufufua kwake wafu baada ya kufa kwao ni, \"usiku ambao tunauvua humo mchana.\" Yaani, tunauondoa mwangaza mkubwa unaokuwa umetanda kwenye ardhi na tunaubadilisha na giza, \"mara wao wanakuwa gizani.\""},{"id":4726,"sura":36,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} Na vile vile pia tunaliondoa giza hili lililowafunika na kuwajumuisha wote, na tunalichomoza jua.Nalo likaangaza maeneo, kisha viumbe wakatawanyika sehemu mbalimbali kwa ajili ya kutafuta riziki zao na masilahi yao. Ndiyo maana akasema: \"Na jua linakwenda kwa kiwango chake.\" Yaani, kwa daima namna alivyolipangia Mwenyezi Mungu, halikwendi zaidi yake wala halipunguki chini yake, na wala halina uwezo wa kujifanyia kitu lenyewe, wala kuuasi uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. \"Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu\" ambaye kwa nguvu zake, anaviendesha viumbe hivi vikubwa kwa mpango ulio kamili zaidi na nidhamu bora kabisa. \"Mwenye kujua vyema,\" ambaye kwa elimu yake amevifanya kuwa masilahi kwa waja wake na manufaa kwao katika Dini yao na dunia yao."},{"id":4727,"sura":36,"from_aya":39,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39} \"Na mwezi tumeupimia vituo\" ambavyo unashukia kila kituo katika usiku mmoja, \"mpaka\" ukawa mdogo sana, na ukarudi kuwa \"kama karara kongwe.\" Kisha, baada ya hapo ukaendelea kuongezeka kidogo kidogo mpaka nuru yake ikakamilika na mng'aro wake ukawa thabiti."},{"id":4728,"sura":36,"from_aya":40,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40} Na kila moja yake: jua na mwezi, usiku na mchana vimepangwa na Mwenyezi Mungu kwa viwango ambavyo haviwezi kuvizidi, na kila kimoja kina mamlaka yake na wakati wake. Kinapokuwepo, hicho kingine kinakosa kuwepo. Ndiyo maana akasema: \"Haliwi jua kuufikia mwezi.\" Yaani, katika mamlaka yake ambayo ni usiku. Kwa hivyo, jua haliwezi kupatikana usiku, \"wala usiku kuupita mchana\" ukatokea kabla ya kumalizika kwa mamlaka yake. \"Na vyote,\" yaani, jua, mwezi, na nyota, \"vinaogelea katika njia zao\" daima dawamu. Basi yote haya ni ushahidi wa wazi na hoja inayong'aa juu ya ukuu wa Muumba, na ukuu wa sifa zake, hasa sifa ya uwezo, hekima, na elimu katika mahali hapa."},{"id":4729,"sura":36,"from_aya":41,"to_aya":50,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"41. Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuria zao katika jahazi lililosheheni. 42.  Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda. 43. Na tukitaka, tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi. 44. Isipokuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda. 45. Na wanapoambiwa: Jilindeni kutokana na yaliyoko mbele yenu na yaliyoko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa... 46.  Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi isipokuwa wao huwa ni wenye kuipa mgongo. 47. Na wanapoambiwa: Toeni katika aliyokupeni Mwenyezi Mungu, wale waliokufuru huwaambia wale walioamini: Je, tuwalishe wale ambao Mwenyezi Mungu angependa angeliwalisha mwenyewe? Nyinyi hammo isipokuwa katika upotofu ulio dhahiri. 48. Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli? 49. Hawangojei isipokuwa ukelele mmoja tu utakaowachukua nao wamo kuzozana. 50. Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei. "},{"id":4730,"sura":36,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41} Na ushahidi kwao na hoja kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa, kwa sababu Yeye ndiye Mneemeshaji wa neema zote, Mwenye kuepusha adhabu zote, ambaye miongoni mwa neema zake ni \"kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao.\" Wengi katika wafasiri walisema kwamba hili linamaanisha baba zao."},{"id":4731,"sura":36,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} \"Na tukawaumbia\" hawa waliokuja baada yao \"kutoka mfano wake;\" yaani, mfano wa merikebu ile, \"wanavyovipanda.\" Akawa ametaja neema yake juu ya baba zao kwa kuwabeba kwenye merikebu. Kwa sababu neema waliyopewa wao pia ni neema kwa dhuria zao. Mahali hapa ni mojawapo ya mahali pagumu sana kwangu katika kutafsiri. Kwa maana, yale waliyotaja wafasiri wengi kwamba kinachomaanishwa hapa na dhuria ati ni baba zao si jambo la kawaida katika Qur-ani, kutumia neno \u201cdhuriya\u201d kwa mababa. Bali, katika maana hiyo kuna utata, na kuyaondoa maneno kutoka katika mada yake, jambo ambalo linakataliwa na maneno ya Mola Mlezi wa walimwengu wote, na makusudio yake ya kuwabainishia waja na kuwawekea mambo wazi. Kisha kuna uwezekano mwingine bora zaidi kuliko huu, ambao ni kwamba kinachomaanishwa hapa na dhuria ni jenasi yote, na kwamba walimaanishwa wao wenyewe. Kwa sababu wao ndio kizazi cha kibinadamu. Lakini maana hii inapingwa na kauli yake: \"Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda.\" Lakini ikiwa maana ya kauli yake, \"Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda\" ni ngamia ambao ndio merikebu za nchi kavu, basi maana hii ya jenasi inakuwa nyoofu na ya wazi kabisa. Walakini, maneno haya pia yanabaki kuwa ya kutatanisha. Kwani, ikiwa maana hii ingekuwa ndiyo iliyokusudiwa, basi angesema: 'Na Ishara kwao ni kwamba tuliwabeba katika merikebu iliyosheheni, na tukawaumbia mfano wake wanavyovipanda.' Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi uhakika wa hali hii. Nilipofikia mahali hapa katika kuandika; nikadhihirikiwa na maana ambayo haiko mbali na yale aliyokusudia Mwenyezi Mungu. Nayo ni kwamba yule anayejua utukufu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na maelezo yake kamili katika kila njia kinapoeleza mambo ya sasa, yaliyopita na yajayo, na kwamba katika kila maana anataja ile ambayo ni ya juu kabisa na iliyo kamilika kabisa, na pindi zilipokuwa merikebu ni miongoni mwa ishara zake, Mwenyezi Mungu Mtukufu, na neema zake juu ya waja wake tangu alipowaneemesha kwazo, kwa kuzisoma mpaka Siku ya Kiyama, na zimeendelea kuwepo wakati wote mpaka zama za wale walioongeleshwa na Qur-ani, Mwenyezi Mungu Mtukufu alipozungumza nao kwa Qur-ani, na akataja hali ya merikebu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akajua kwamba hizo zitakuwa ishara kubwa zaidi merikebu zitakuja tokea katika zama zisizokuwa zao, pale atakapowafundisha kutengeneza merikebu mbalimbali zikiwemo zile za matanga, za moto, na za angani zinazokwenda angani kama ndege na vile vile vipando vya nchi kavu, ambazo ni ishara kubwa zaidi ambayo haikuwa isipokuwa wakati wa dhuria zao, akatanabahisha katika Kitabu chake juu ya aina miongoni mwa aina za ishara zake. Akasema: \"Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi iliyosheheni\" wapandaji wengi na mizigo. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawabeba na akawaokoa kutokana na kuzama; kwa njia ambazo Mwenyezi Mungu aliwafundisha."},{"id":4732,"sura":36,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} Ndiyo maana aliwatanabahisha juu ya neema yake juu yao, ambapo aliwaokoa kutokana na kuzama majini pamoja na kwamba ana uwezo wa kufanya hivyo. Akasema: \"Na tukitaka, tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia,\" wala hawaokolewi kutokana na yale waliyomo."},{"id":4733,"sura":36,"from_aya":44,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{44} \"Isipokuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda,\" ambapo hatukuwazamisha kwa sababu ya upole wake na kuwastarehesha tu kwa muda; huenda wakarejea au wakatenda yale waliyopuuza kufanya."},{"id":4734,"sura":36,"from_aya":45,"to_aya":45,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{45} \"Na wanapoambiwa: Jilindeni na yaliyoko mbele yenu na yaliyoko nyuma yenu.\" Yaani, wajilinde kutokana na hali ya maisha ya kaburini, Kiyama, na adhabu iliyoko duniani; \"ili mpate kurehemewa.\" Wao wanalipa hilo mgongo na kutolijali kabisa, hata kama zitawajia Ishara zote."},{"id":4735,"sura":36,"from_aya":46,"to_aya":46,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{46} Ndiyo maana akasema: \"Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa ni wenye kuipuuza.\" Na katika kufungamanisha ishara na Mola wao Mlezi kuna ushahidi juu ya ukamilifu na ubainifu wake. Kwa sababu hakuna ishara zilizo wazi na bainifu zaidi kuliko ishara za Mwenyezi Mungu, na kwamba miongoni mwa jumla ya malezi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kuwa aliwafikishia ishara ambazo kwazo wanaweza kuzitumia kuwa ushahidi juu ya yale yenye kuwafaa katika dini yao na dunia yao."},{"id":4736,"sura":36,"from_aya":47,"to_aya":47,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{47} \"Na wanapoambiwa: Toeni katika vile alivyokupeni Mwenyezi Mungu.\" kwani angelitaka, angelikunyang'anyeni \"wale waliokufuru huwaambia wale walioamini\" huku wakiipinga haki na kutumia mipango ya Mwenyezi Mungu kuwa ni ushahidi wa kutofanya hivyo. \"Je, tuwalishe wale ambao Mwenyezi Mungu angependa, angeliwalisha mwenyewe? Nyinyi\" waumini \"hammo ila katika upotofu ulio dhahiri\" kwa maana mnaamrisha hilo. Na hili ni katika mambo yanayoonyesha ujinga wao mkubwa na upumbavu. Kwa maana, mipango ya Mwenyezi Mungu kamwe haifai kuwa ndiyo hoja ya mwenye kutenda maasia, kwani hata kile ambacho Mwenyezi Mungu anataka kinakuwa, na asichotaka hakiwi, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwawezesha waja wake na kuwapa nguvu ambazo kwazo wanaweza kufanya maamrisho na kujiepusha na makatazo. Kwa hivyo, wanapoacha yale waliyoamrishwa; hilo linakuwa kwa sababu ya chaguo lao, siyo kwamba walilazimishwa."},{"id":4737,"sura":36,"from_aya":48,"to_aya":49,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{48 - 49} \"Na wanasema\" kwa njia ya kukadhibisha na pupa: \"Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?\" Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Wasione kwamba hilo haliwezekani; kwani hivi karibuni, \"Hawangojei ila ukelele mmoja tu\" ambao ni kule kupuliza katika Baragumu \"utakaowachukua nao wamo kuzozana\" wanafanya mchezo tu, na wala hilo halikupita mioyoni mwao wanapozozana na kubishana."},{"id":4738,"sura":36,"from_aya":50,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{50} Na ukiwakamata wakati wameghafilika, basi hawatapewa muhula \"Basi hawataweza kuusia;\" yaani, kwa uchache wala kwa wingi, \"wala kwa watu wao hawatarejea.\""},{"id":4739,"sura":36,"from_aya":51,"to_aya":54,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"51. Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi. 52. Watasema: Ole wetu! Ni nani aliyetufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume. 53. Haitakuwa isipokuwa ukelele mmoja tu, mara wote watahudhurishwa mbele yetu. 54. Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda. "},{"id":4740,"sura":36,"from_aya":51,"to_aya":51,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{51} Kupulizwa kwa kwanza katika baragumu kutakuwa kwa ajili ya kutia mahangaiko kwa viumbe na kuwafisha. Lakini kupuliza huku kwa pili, ni kule kwa kuwafufua na kuwatawanya kutoka makaburini mwao.  Basi itakapopulizwa katika baragumu, watatoka \"makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi.\" Na wala hawataweza kungoja wala kuchelewa."},{"id":4741,"sura":36,"from_aya":52,"to_aya":52,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{52} Katika hali hiyo wale waliokadhibisha watahuzunika na kujuta, na watasema: \"Ole wetu! Ni nani aliyetufufua kwenye malazi yetu?\" Yaani, jumo makaburini. Kwa sababu ilisimuliwa katika baadhi ya hadithi kwamba watu wa makaburini watalala kulala fulani muda mfupi tu kabla ya kupulizwa katika baragumu. Wataitikiwa na waambiwe: \"Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume.\" Na leo yamekuwa kweli mnayaona kwa macho. Wala usidhani kuwa kutajwa kwa Mwingi wa Rehema mahali hapa ni kujulisha tu kuhusu ile ahadi yake. Bali ni kufahamisha kwamba siku hiyo kuu wataona rehema yake kwa namna ambayo haikuwahi kuwapitia akilini mwao wala wenye kutarajia hawakuwahi kutarajia. Kama vile kauli yake: \"Ufalme wa haki siku hiyo utakuwa wa Arrahman (Mwingi wa Rehema).\" Na kauli yake, \"Na sauti zote zitamnyenyekea Arrahmani Mwingi wa Rahema.\" Na mfano wa hayo ambapo jina lake 'Arrahmani (Mwingi wa rehema)' limetajwa."},{"id":4742,"sura":36,"from_aya":53,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{53} \"Haitakuwa\" kufufuliwa kutoka makaburini \"isipokuwa ukelele mmoja tu\" alioupuliza Israfil katika baragumu, na miili ikafufuka. \"Mara wote watahudhuruishwa mbele yetu;\" wa mwanzo na wa mwisho, watu na majini. Kisha watafanyiwa hesabu kwa matendo yao."},{"id":4743,"sura":36,"from_aya":54,"to_aya":54,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{54} \"Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu.\" Mema yake hayatapunguzwa kitu wala maovu yake hayataongezwa chochote. \"Wala hamtalipwa ila yale mliyokuwa mkiyatenda\" ya heri na maovu. Basi mwenye kupataya ya heri, basi na amsifu Mwenyezi Mungu. Na mwenye kupata yasiyokuwa hayo, basi kamwe asilaumu isipokuwa yeye mwenyewe tu."},{"id":4744,"sura":36,"from_aya":55,"to_aya":58,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"55. Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi. 56. Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya kifahari. 57. Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakachokitaka. 58. \"Salama!\" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu. "},{"id":4745,"sura":36,"from_aya":55,"to_aya":56,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{55 - 56} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kwamba kila mtu hatalipwa ila kwa aliyoyatenda,akataja malipo ya makundi hayo mawili, na akaanza na malipo ya watu wa Peponi. Akajulisha kwamba siku hiyo watakuwa \u201cshughulini, wamefurahi\" kwa sababu ya kila kitu ambacho nafsi inakitamani, na macho yanakipenda, na yale yanayotamaniwa na wanaoyatamani, na hayo ni pamoja na kuingiliana na wanawali warembo. Kama alivyosema: \"Wao na wake zao\" miongoni mwa hurulaini waliojumuisha kati ya nyuso na miili mizuri na maadili bora \"wamo katika vivuli juu ya viti vya fahari\" vilivyopambwa kwa mavazi mazuri ya urembo, \"wameegemea\" juu yake kuegemea kunakoashiria raha kamili, utulivu na ladha."},{"id":4746,"sura":36,"from_aya":57,"to_aya":57,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{57} \"Watapata humo kila aina ya matunda\" matamu, kama vile zabibu, tini, makomamanga na mengineyo.\" Na watapata kila watakachokitaka.\""},{"id":4747,"sura":36,"from_aya":58,"to_aya":58,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{58} Na pia humo wakapata \"Salama!\" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu. Katika hili kuna ushahidi kwamba Mola Mlezi atawaongelesha watu wa Peponi na kuwapa salamu. Na alilisisitiza hilo kwa maneno yake, \"kauli.\" Kwani Mola Mlezi, Mwingi wa Rehema atakapowasalimia, watapata usalama kamili katika nyanja zote na watapata maamkizi ambayo hakuna maamkizi ya juu zaidi yake wala neema mfano wake. Basi unadhania nini salamu ya Mfalme wa wafalme wote, Mola Mlezi Mkuu, Mpole, Mwingi wa kurehemu kwa watu wa makao yake ya heshima, ambao aliwaridhia, na wala kamwe hatawakasirikia. Na lau si kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliamuru kwamba hawatakufa wala mioyo yao haitatoka katika nafasi zake za furaha kubwa, basi hilo lingetokea. Basi tunamuomba Mola wetu Mlezi asitunyime neema hiyo, na atufurahishe kwa kuutazama uso wake mtukufu."},{"id":4748,"sura":36,"from_aya":59,"to_aya":67,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"59. Na enyi wakosefu! Jitengeni leo! 60. Je, sikuagana nanyi, enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu. 62. Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo njia iliyonyooka. 62. Na bila ya shaka yeye amekwishalipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri? 63. Hii basi ndiyo Jahannamu mliyokuwa mkiahidiwa. 64. Ingieni humo leo kwa vile mlivyokuwa mkikufuru. 65. Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyokuwa wakiyachuma. 66. Na tungelipenda, tungeliyafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wangeionaje? 67. Na tungelitaka, tungewageuza sura hapo hapo walipo, basi wasingeweza kwenda wala kurudi. "},{"id":4749,"sura":36,"from_aya":59,"to_aya":59,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{59} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja malipo ya watu wema, akataja adhabu za wahalifu, \"na\" kwamba wataambiwa Siku ya Kiyama: \"Enyi wakosefu! Jitengeni leo!\" Mbali na Waumini na muwe peke yenu; ili awakemee na kuwakaripia mbele ya viumbe vyote vikiwaona kabla ya kuwaingiza Motoni. Atawaambia:"},{"id":4750,"sura":36,"from_aya":60,"to_aya":60,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{60} \"Je, sikuagana nanyi,\" Yaani, sikuwaamrisheni na kuwausia kupitia ndimi za Mitume wangu, \"na nikakuambieni enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani?\" Yaani, msimtii! Karipio hili linajumuisha kukemea aina zote za ukafiri na maasia; kwa sababu yote hayo ni utiifu kwa Shetani na kumuabudu. \"Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu,\" nikawa nimekuhadharisheni juu yake kwa tahadharisho kubwa kabisa, na nikakuonyeni juu ya kumtii, na nikakujulisheni yale anayowaitia."},{"id":4751,"sura":36,"from_aya":61,"to_aya":61,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{61} \"Na\" nikakuamrisheni kwamba mniabudu mimi kwa kutekeleza amri zangu na kuacha makatazo yangu. \"Hii;\" yaani, kuniabudu huku, kunitii, na kumuasi Shetani \"ndiyo njia iliyonyooka.\" Na mambo yote yanayohusiana na njia iliyonyooka na matendo yake yanarudi kwa mambo mawili haya. Lakini nyinyi hamkushika agano langu wala hamkufanya kulingana na wasia wangu kwenu, bali mlifanya urafiki na adui yenu."},{"id":4752,"sura":36,"from_aya":62,"to_aya":62,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"62. Basi akalipoteza \"kundi kubwa miongoni mwenu.\" \"Je, hamkuwa mkifikiri?\" Yaani, je, hamkuwa na akili inayokuamrisheni kumfanya Mola wenu Mlezi kuwa kipenzi, na kushikamana na haki, na akili hiyo ikakukemeeni kumfanya adui wenu mkubwa kuwa ndiye kipenzi chenu? Basi, ikiwa mngekuwa na akili timamu; kwa nini mlifanya hivyo?"},{"id":4753,"sura":36,"from_aya":63,"to_aya":63,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{63} Basi mlipomtii Shetani, na mkamfanyia uadui Mwingi wa Rehema, na mkakadhibisha kukutana naye, na mkataka Kiyama ambayo ndiyo nyumba ya malipo, na likawa juu yenu neno la adhabu, basi \"hii ndiyo Jahannamu mliyokuwa mkiahidiwa\" nanyi mkaikadhibisha. Basi iangalieni kwa macho yenu wenyewe! Hapo, mioyo yao itafadhaika, nayo macho yao yatakodoka, na watakuwa na hofu kubwa sana."},{"id":4754,"sura":36,"from_aya":64,"to_aya":64,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{64} Kisha haya yatakamilishwa kwa kuamrishwa kwamba waingie Motoni. Wataambiwa: \"Ingieni humo leo kwa vile mlivyokuwa mkikufuru.\" Humo, joto lake litawazunguka, na makali yake yatawafikia kila ncha kwa sababu ya kuzikataa kwenu ishara za Mwenyezi Mungu na kukadhibisha kwenu Mitume wa Mwenyezi Mungu."},{"id":4755,"sura":36,"from_aya":65,"to_aya":65,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{65} Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuelezea hali yao ya kutisha katika nyumba ya dhiki: \"Leo tunaviziba vinywa vyao\" kwa kuwafanya mabubu wasiweze kusema kitu, ili wasiweze kukataa yale waliyofanya miongoni mwa ukafiri na ukadhibishaji. \"Na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.\" Hivyo vyote vitatamkishwa na yule aliyevitamkisha vitu vyote."},{"id":4756,"sura":36,"from_aya":66,"to_aya":66,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{66} \"Na tungelipenda, tungeliyafutilia mbali macho yao,\" kwa kuwaondolea macho yao kama tulivyoondoa kuongea kwao \"wakawa wanaiwania njia\" wakiikimbilia; kwa sababu ndiyo njia inayofikisha Peponi. \"Lakini wangeionaje\" ilhali macho yao yameshaondolewa?"},{"id":4757,"sura":36,"from_aya":67,"to_aya":67,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{67} \"Na tungelitaka, tungewageuza sura hapo hapo walipo, basi wasingeweza kwenda wala kurudi\" nyuma, ili wawe mbali na Moto. Maana yake ni kwamba hawa makafiri lilikwisha wadhibitikia neno la adhabu, na ikabidi waadhibiwe. Na mahali hapo hapatakuwa isipokuwa Moto uliodhihirishwa, ambao hakuna atakayeweza kuokoa isipokuwa kwa kuvuka kupitia juu Sirat (njia iliyoko juu ya Moto), jambo ambalo hawaliwezi isipokuwa watu wa imani ambao wanatembelea katika nuru yao. Ama hawa, hawana agano lolote kwa Mwenyezi Mungu kwamba wataokoka kutokana na Moto. Akitaka, atayafutilia mbali macho yao na akaacha watembee, kwa hivyo wasiweze kuifikia Njia iliyonyooka hata kama wataiwania na kuikimbilia. Na akitaka, anaondoa harakati zao, kwa hivyo wasiweze kwenda mbele wala nyuma. Na maana ya haya ni kwamba hawakuweza kuivuka njia hiyo, kwa hivyo, kamwe hawataokoka."},{"id":4758,"sura":36,"from_aya":68,"to_aya":68,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"68. Na tunayemzeesha, tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii?"},{"id":4759,"sura":36,"from_aya":68,"to_aya":68,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{68} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na tunayemzeesha\" miongoni mwa wanadamu \"tunamrudisha nyuma katika umbo,\" akarudi namna alivyoanza katika hali ya udhaifu wa kiakili na udhaifu wa nguvu. \"Basi je, hawazingatii\" kwamba wanadamu ni wapungufu kwa namna zote, kwa hivyo wakazitumia vyema nguvu zao na akili zao katika kumtii Mola wao Mlezi?"},{"id":4760,"sura":36,"from_aya":69,"to_aya":70,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"69. Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu isipokuwa ni ukumbusho na Qur-ani inayobainisha. 70. Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri. "},{"id":4761,"sura":36,"from_aya":69,"to_aya":69,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{69} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamtakasa Nabii wake Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mbali na walivyomsingizia washirikina kuwa yeye ni mtunzi wa mashairi, na kwamba hayo aliyokuja nayo ni mashairi tu. Akasema: \"Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo,\" kwamba awe mtunga mashairi. Haiwezekani! Kwa sababu yeye ni mwenye hekima, mwongofu, ilhali washairi wamepotea, na wanawafuata wapotevu.Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alivunjilia mbali kila tuhuma ambazo wanazishikilia wale waliopotea mbali na Mtume wake. Alivunjilia mbali uwezekano kwamba yeye ndiye aliyeiandika au kuisoma kutoka kwingine. Kwa hivyo, akajulisha kwamba hakumfundisha ushairi na wala haimfailii kufanya hivyo. \"Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur-ani inayobainisha,\" ambayo kwayo watu wenye akili watakumbuka matakwa yote ya kidini. Kwani inajumuisha hayo yote kwa njia kamilifu zaidi. Na inazikumbusha akili juu ya yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyaweka katika maumbile yao ya asili ya kuamrisha kila jema, na kukataza kila ovu. \"Qur-ani inayobainisha\" yale yanayohitajika kubainishwa. Na ndiyo maana akafuta kinachobainishwa ili hilo lionyeshe kwamba inabainisha haki yote kwa ushahidi wake wa kina na wa jumla, na pia inabainisha batili na ushahidi wa ubatilifu wake. Mwenyezi Mungu aliiteremsha hivyo kwa Mtume wake."},{"id":4762,"sura":36,"from_aya":70,"to_aya":70,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{70} \"Ili imwonye aliye hai\" moyoni, na anayeifahamu. Huyo ndiye anayetakasika kwa Qur-ani hii, na ndiye anayezidi kuwa na elimu na matendo kutokana nayo. Na Qur-ani kwa moyo wake inakuwa kama ilivyo mvua kwa ardhi nzuri, safi. \"Na neno litimie juu ya makafiri,\" kwa kuwa kwayo hoja ya Mwenyezi Mungu ilisimama juu yao, na upinzani wao ukakatika. Basi hawakubakia na udhuru wowote hata mdogo vipi, wala fikira yenye mchanganyiko wanayoweza kuitumia kama ushahidi."},{"id":4763,"sura":36,"from_aya":71,"to_aya":73,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"71. Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki. 72. Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanaowapanda, na baadhi yao wanawala. 73. Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru? "},{"id":4764,"sura":36,"from_aya":71,"to_aya":73,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{71 - 73} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waja wake kutazama mifugo aliyowatiishia na kuwadhalilishia, na akawafanya kuwamiliki, wakiwatii katika kila jambo wanalolitaka kutoka kwao. Na kwamba aliweka manufaa mengi ndani yao, kama vile kuwabeba na kuibeba mizigo yao na bidhaa zao kutoka sehemu moja hadi nyingine, na pia kuwala baadhi yao, na pia wanapata joto kutoka kwao. Pia kutokana na sufu zao, manyoya yao, na nywele zao wanapata vyombo na mapambo ya kutumia kwa muda. \"Basi je, hawashukuru\" Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyeneemesha kwa neema hizi, na wakamfanyia ibada kwa kumkusudia yeye tu, na wala wasizifurahie tu bila ya kuzingatia na kutafakari?"},{"id":4765,"sura":36,"from_aya":74,"to_aya":75,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"74. Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa! 75. Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakaohudhurishwa. "},{"id":4766,"sura":36,"from_aya":74,"to_aya":75,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{74 - 75} Huu ni ufafanuzi wa ubatili wa miungu ya washirikina, waliyoichukua kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ambao walikuwa wakitaraji msaada kutoka kwao na uombezi. Hao kwa hakika, hawana uwezo kabisa. \"Hawataweza kuwasaidia,\" wala wenyewe hawawezi kujinusuru. Na ikiwa hawawezi kuwasaidia, basi watawezaje kuwanusuru? Kuna masharti mawili ya kunusuru, nayo ni uwezo [na nguvu]. Kwa hivyo, ikiwa anaweza, basi inabakia kwamba: Je, anataka msaada kutoka kwa mja wake au la? Na kukanusha uwezo ni kukanusha mambo yote hayo mawili. \"Bali hao ndio watakuwa askari wao watakaohudhurishwa.\" Yaani, wote wawili watahudhurishwa katika adhabu, na watakimbiana wao kwa wao. Je, kwa nini wasijitenge mbali katika dunia na suala la kuwaabudu hawa, na wakamkusudia kwa ibada Yule ambaye mkononi mwake upo ufalme wote, manufaa yote, madhara yote, kutoa na kunyima, naye ndiye Mlinzi na Msaidizi?"},{"id":4767,"sura":36,"from_aya":76,"to_aya":76,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"76. Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayoyaweka siri na wanayoyadhihirisha."},{"id":4768,"sura":36,"from_aya":76,"to_aya":76,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{76} Yaani, yasikuhuzunishe ewe Mtume yale wanayosema hao wanaokadhibisha; miongoni mwa kila maneno ambayo wanamkashifu kwayo Mtume au wanakashifu kwayo yale aliyokuja nayo. \"Hakika Sisi tunayajua wanayoyaweka siri na wanayoyadhihirisha,\" na tutawalipa kulingana na jinsi tunavyowajua. Vinginevyo, maneno yao hayo hayatakudhuru hata kidogo."},{"id":4769,"sura":36,"from_aya":77,"to_aya":83,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"77. Kwani mwanadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndiyo amekuwa ndiye mgomvi wa dhahiri! 78. Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika? 79. Sema: Ataihuisha huyo huyo aliyeiumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba. 80. Aliyekujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha. 81. Kwani aliyeziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi mno. 82. Hakika amri yake anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa. 83. Basi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa. "},{"id":4770,"sura":36,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0622\u064a\u0627\u062a","text":"Aya hizi tukufu zinataja tuhuma za wale wanaokanusha ufufuo na kuzijibu kwa jibu kamili, bora na lililo wazi kabisa."},{"id":4771,"sura":36,"from_aya":77,"to_aya":77,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{77} Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: \"Kwani haoni mwanadamu\" anayepinga ufufuo au anayeshuku hili? Haoni kitu ambacho kinamnufaisha yeye kwa yakini kamili juu ya kutokea kwake, ambacho ni mwanzo wa kuumbwa kwake \"kutokana na tone la manii?\" Kisha kupitia kwake awamu mbalimbali kidogo kidogo, mpaka akawa mkubwa, kisha akawa kijana na akili yake ikakamilika na kuimarika. \"Kisha sasa yeye ndiye amekuwa mgomvi wa dhahiri!\" Baada ya kwamba mwanzo wa kuumbwa kwake ulikuwa kutokana na tone la manii. Basi na aangalie tofauti iliyopo baina ya hali hizi mbili, na ajue kwamba yule aliyemuumba baada ya kutokuwepo anaweza zaidi kumrejesha baada ya kugawanyika na kumung'unyika."},{"id":4772,"sura":36,"from_aya":78,"to_aya":78,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{78} \"Na akatupigia mfano\" ambao haumfailii yeyote kuupiga. Nao ni kuufananisha uwezo wa Muumba na uwezo wa viumbe, na kwamba jambo lisilowezekana kwa uwezo wa viumbe pia haliwezekani kwa uwezo wa Muumba. Basi Mwenyezi Mungu akaufafanua mfano huu kwa kauli yake mwanadamu huyu. \"Akasema:\" Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwishamung'unyika?\" Huku ni kuuliza kwa njia ya kejeli. Huo ndio mchanganyiko wao na fikira yao potofu, nao huo ndio mfano aliotoa Mwenyezi Mungu. Na hilo ni kwamba jambo hili haliwezekani kabisa kulingana na jinsi wanavyojua wanadamu. Lakini kauli hii aliyosema mwanadamu huyu ni kauli iliyotokana na kughafilika kwake na kusahau mwanzo wa kuumbwa kwake. Lau kuwa angeufahamu vyema uumbaji wake baada ya kwamba hakuwa chochote cha kutajwa, kisha akafanywa kuwepo, akaonekana kwa macho, basi hangepinga mfano huu."},{"id":4773,"sura":36,"from_aya":79,"to_aya":79,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{79} Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajibu kuona kwao huku kwamba haliwezekani kwa jawabu la kuponya, la kutosha.Akasema: \"Sema: Ataihuisha huyo huyo aliyeiumba hapo mara ya mwanzo.\" Na hili, kwa kufikiria tu, anajua kwa yakini na bila ya shaka yoyote kwamba yule aliyeiumba mara ya kwanza ana uwezo wa kuirejesha mara ya pili, na hilo ndilo rahisi zaidi mbele ya uwezo ikiwa atafikiria vyema mwenye kufikiria. \"Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.\" Huu pia ni ushahidi wa pili juu ya sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nalo ni kwamba elimu yake, Mwenye nguvu, imewazunguka viumbe wake wote katika hali zao zote katika nyakati zote, na anajua ni nini ambacho ardhi inapunguza miongoni mwa miili ya wafu na ile iliyobakia, na anajua ghaibu na mambo ya dhahiri. Kwa hivyo, mja akiikiri elimu hii kubwa,atajua kwamba hilo ni kubwa zaidi na tukufu zaidi hata kuliko Mwenyezi Mungu kuwafufua wafu kutoka kwenye makaburi yao."},{"id":4774,"sura":36,"from_aya":80,"to_aya":80,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"80. Kisha akataja ushahidi wa tatu, akasema: \"Aliyekujalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.\" Na kama moto mkavu unaweza kutoka katika mti mbichi ambao ni wenye unyevu mkubwa licha ya kuhalifiana kukubwa kwa viwili hivyo, basi kuwatoa wafu makaburini mwao ni mfano tu wa hilo."},{"id":4775,"sura":36,"from_aya":81,"to_aya":81,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{81} Kisha akataja ushahidi wa nne, akasema: \"Kwani aliyeziumba mbingu na ardhi\" pamoja na upana wake na ukubwa wake \"hawezi kuwaumba mfano wao?\" Yaani, kuwarudisha vile walivyokuwa, \"Kwani!\" Yeye anaweza hilo. Kwa maana kuumbwa kwa mbingu na ardhi ni kukubwa kuliko kuumbwa kwa watu. \"Naye ndiye Muumbaji Mkuu, ajuaye zaidi.\" Na huu ndio ushahidi wa tano. Kwani Yeye Mtukufu ndiye Muumbaji wa viumbe vyote vya mwanzo na vya mwisho, vidogo na vikubwa, vyote ni athari miongoni mwa athari za uumbaji wake na uwezo wake, na kwamba hakuna kiumbe kinachoweza kumshinda akitaka kukiumba. Kwa hivyo, kurudisha kwake wafu ni sehemu katika athari za uumbaji wake."},{"id":4776,"sura":36,"from_aya":82,"to_aya":82,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{82} Ndiyo maana akasema: \"Hakika amri yake anapotaka kitu\" chochote \"ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa,\" bila pingamizi lolote."},{"id":4777,"sura":36,"from_aya":83,"to_aya":83,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{83} \"Basi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu.\" Huu ni ushahidi wa sita. Kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mfalme anayemiliki kila kitu, ambaye vyote vilivyomo katika ulimwengu wa juu na wa chini ni mali yake na waja waliotiishwa na wanaoendeshwa, anawaendesha kwa mipango yake ya kimajaliwa, hukumu zake za kisheria, na hukumu zake za kimalipo. Basi kuwarudisha baada ya kufa kwao ili awatekelezee malipo ni katika ukamilifu wa ufalme wake. Na ndiyo maana akasema: \"Na kwake Yeye mtarejeshwa.\" Na hilo halina shaka yoyote, kwa sababu kuna hoja mbalimbali za uhakika na ushahidi unaong'aa juu yake. Basi ametakasika yule ambaye aliweka katika maneno yake mwongozo, uponyaji na nuru."},{"id":4778,"sura":36,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya Surat Yasin Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kama unavyostahiki utukufu wake, ukamilifu wake, ukuu wake na ukubwa wake. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad."},{"id":4779,"sura":36,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}