{"result":[{"id":4973,"sura":39,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Az-Zumar"},{"id":4974,"sura":39,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Nayo ilishuka Makka"},{"id":4975,"sura":39,"from_aya":1,"to_aya":3,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Mteremsho wa Kitabu hiki umetokana na Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 2. Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa Haki. Basi muabudu Mwenyezi Mungu ukimsafia Dini Yeye tu. 3. Hakika Dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu. Na wale wanaowafanya wenginewe kuwa ni walinzi wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu - Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika wanayohitalifiana. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi aliye mwongo kafiri. "},{"id":4976,"sura":39,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukuu wa Qur-ani na utukufu wa yule aliyeyazungumza na yakateremka kutoka kwake. Na kwamba iliteremka \"kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima,\" ambaye ndiye mwenye uungu kwa viumbe vyote. Hilo ni kwa sababu ya ukuu wake, ukamilifu wake na nguvu yake aliyoshinda kwayo viumbe vyote, na kila kitu kikamdhalilikia. Na anayo hekima kubwa katika kuumba kwake na amri yake. Na Qur-ani hii imeteremka kutoka kwa yule ambaye hizi ndizo sifa zake. Na maneno ni sifa ya yule aliyeyazungumza, nayo sifa hufuata yule anayesifika kwayo. Kwa hivyo, kama vile Mwenyezi Mungu ndiye mkamilifu kwa njia zote, ambaye hana kifani, vile vile maneno yake ni makamilifu kwa njia zote na hayana kifani. Hayo pekee yanatosha kuielezea Qur-ani na kuonyesha daraja yake."},{"id":4977,"sura":39,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Lakini pamoja na hayo, kitabu hiki kiliongeza kuwa wazi katika ukamilifu wake kwa sababu ya yule aliyeteremshiwa, yaani Muhammad - rehema na amani zimshukie - ambaye ndiye mtukufu zaidi katika viumbe vyote, kwa hivyo ikajulikana kuwa ndicho kitabu kitukufu zaidi. Na pia kiliongeza kuwa wazi kwa sababu ya yale ambayo kiliteremka nayo, ambayo ni Haki. Kiliteremka na haki isiyo na shaka yoyote ndani yake, ili kuvitoa viumbe katika giza mbalimbali na kuvipeleka kwenye nuru. Na kilishuka kikiwa na haki katika habari zake za ukweli na hukumu za uadilifu. Kwa hivyo kila kitu ambacho kitabu hiki kinaashiria ndiyo aina kuu zaidi ya haki inayohusiana na mambo yote ya kielimu yanayotakiwa. Basi hakuna chochote kilicho baada ya haki isipokuwa upotofu. Na kwa vile kiliteremka kutoka kwenye haki huku kimejumuisha haki, kikiwa kimeteremka kwa mtukufu zaidi katika viumbe vyote ili kuviongoa viumbe; kikawa kina neema kubwa na kikatukuka. Na ikawa ni lazima kushukuru neema hii kwa kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika dini. Ndiyo maana akasema: \"Basi muabudu Mwenyezi Mungu ukimsafia Dini Yeye tu,\" miongoni mwa sheria za dhahiri na sheria zilizofichika: Uislamu, imani na ihsan, kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu pekee kwa hayo na kuutaka uso wake kwa hayo pasi na kukusudia lengo lingine lolote."},{"id":4978,"sura":39,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} \"Hakika Dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu.\" Huku ni kuthibitisha amri ya kwamba wanapaswa kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, na kubainisha kwamba Yeye Mtukufu ndiye mkamilifu zaidi na ana fadhila juu ya waja wake kwa namna zote. Basi ni yake dini iliyo safi na isiyo na uchafu wowote. Kwani ndiyo dini aliyoiridhia mwenyewe na akaridhia kwamba iwe ndiyo dini ya viumbe wake wateule, na akawaamrisha kuifuata. Kwa sababu inajumuisha kumfanyia Mwenyezi Mungu tu uungu katika upendo, hofu, matumaini, kutubia kwake, na kurejea kwake katika kutimiza mahitaji ya waja wake. Na hayo ndiyo yanayorekebisha nyoyo na kuzitakasa, pasi na kumshirikisha na chochote katika ibada. Kwani Mwenyezi Mungu yuko mbali mno na kuwa na mshirika yeyote na wala haitajii hilo. Kwani shirki huharibu nyoyo, roho, dunia na akhera, na huzitia nafsi katika mashaka makubwa mno. Ndiyo maana, alipoamrisha waja kumpwekesha na kumkusudia Yeye peke yake, akakataza kumshirikisha, na akajulisha ubaya wa wale wanaomshirikisha akisema: \"Na wale wanaowafanya wenginewe kuwa ni walinzi\" kwa kuwaabudu na kuwaomba wakijitafutia udhuru wakisema: \"'Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu.'\" Yaani, ili watufikishie mahitaji yetu kwa Mwenyezi Mungu na kutuombea kwake. Kwa maana sisi tunajua kwamba hivyo vitu haviumbi, haviruzuku, wala havimiliki chochote katika jambo lolote. Watu hawa waliacha yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu ya kumkusudia Yeye tu, na wakathubutu kufanya jambo kubwa kabisa lililoharamishwa, ambalo ni shirki. Na wakamfananisha yule ambaye hakuna kitu kama mfano wake, Mfalme mkuu, na wafalme wengineo. Na wakadai - kwa akili zao mbovu na maoni ya magonjwa - kwamba wafalme, jinsi hawawezi kufikiwa isipokuwa kwa kupitia watu wa hadhi mbele yake, waombezi, mawaziri ambao wanaweza kumfikishia mahitaji ya raia zao na kuwatafutia huruma mbele yao; kwamba Mwenyezi Mungu yuko hivyo! Ulinganisho huu ni mojawapo ya milinganisho potovu zaidi. Kwani unajumuisha ulinganisho kati ya Muumba na kiumbe, pamoja na kwamba imeshathibiti kuwepo tofauti kubwa kati ya viwili hivyo kiakili, kimaandiko na hata kimaumbile ya asili. Kwa maana wafalme walihitaji wapatanishi kati yao na raia wao kwa sababu hawajui hali zao, basi ndiyo wakahitaji mtu wa kuwajulisha hali zao. Na pengine huenda wasiwe na huruma katika nyoyo zao kwa mwenye haja huyo, kwa hivyo wakahitaji mtu wa kuwatafutia huruma mbele yao. Na wanahitaji waombezi na wasaidizi. Na wanawahofu, kwa hivyo ndiyo wanakidhi mahitaji ya wale wanaowaombea ili kuwatuliza mawazo yao. Nao pia ni wahitaji, na wanaweza kuzuiwa kwa sababu wanaogopa umasikini. Na Mola Mlezi Mtukufu ndiye ambaye elimu yake imezunguka mambo yote ya dhahiri na ya ndani, ambaye hahitaji mtu yeyote kumjulisha hali za raia wake na waja wake. Yeye ndiye Mwingi wa kurehemu, Mkarimu atoaye kwa wingi zaidi ya wote, hamhitaji yeyote katika viumbe vyake ili amfanye kuwa na huruma kwa waja wake. Bali Yeye ni Mwenye huruma zaidi kwao kuliko wao wenyewe kwa nafsi zao na kuliko wazazi wao wanavyowahurumia. Naye ndiye anayewahimiza na kuwaita kwenye visababu vya kuwafanya kufikia rehema zake, na anawatakia masilahi ambayo hata wao wenyewe hawajitakii. Naye ndiye Mkwasi, Mwenye ukwasi kamili kabisa. Ambaye kama viumbe vyote tangu vya mwanzo hadi vya mwisho vingekusanyika mahali pamoja, vikamwomba, naye akakipa kila kimoja kilichoomba na kutamani, havingepunguza ukwasi wake hata kidogo, isipokuwa namna inavyopunguka bahari wakati sindano inaingizwa na kutolewa ndani yake. Na waombezi wote wanamuogopa. Hawezi yeyote miongoni mwao kufanya uombezi ila kwa idhini yake, kwani uombezi wote ni wake. Basi kupitia tofauti hizi, unajulikana ujinga wa wale wanaomshirikisha na upumbavu wao mkubwa, na ukubwa wa ujasiri wanaofanya dhidi yake. Na inajulikana hekima ya ukweli kwamba Mwenyezi Mungu hausamehi ushirikina kwa sababu unajumuisha kumtia dosari Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ndiyo maana akasema akihukumu baina ya makundi mawili: wanaomkusudia Yeye peke yake, na wale wanaomshirikisha, maneno ambayo ndani yake kuna tishio kwa washirikina: \"Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika yale wanayohitalifiana.\" Na tayari ilishajulikana kwamba Mwenyezi Mungu alishahukumu kuwa Waumini wanaomkusudia Yeye peke yake watakuwa katika Bustani zenye neema. Naye mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu amemharamishia Bustani za mbinguni, na mahala pake ni Motoni. \"Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi\" kwenye njia iliyonyooka \"aliye mwongo, kafiri.\" Kwa maana anajiwa na mawaidha na ishara mbalimbali lakini haachani na sifa zake hizo. Na Mwenyezi Mungu anamwonyesha ishara mbalimbali lakini anazikanusha, anazikufuru na kuzikadhibisha. Basi huyu atawezaje kupata uwongofu ilhali ameshajifungia mlango na akaadhibiwa kwa Mwenyezi Mungu kuuziza moyo wake? Basi hawezi kuamini."},{"id":4979,"sura":39,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"4. Lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka kuwa na mwana, basi bila ya shaka angeliteua amtakaye katika aliowaumba. Ametakasika na hayo! Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda atakalo."},{"id":4980,"sura":39,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Yaani, \"Lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka kuwa na mwana\" kama wanavyodai hivyo baadhi ya watu wapumbavu, \"basi bila ya shaka angeliteua amtakaye katika aliowaumba\" na wala hangehitaji kuwa na mke. \"Subhanahu (ametakasika)\" mbali na hayo ambayo makafiri wanamdhania, au yale ambayo wavukao mipaka walimnasibisha nayo. \"Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja, Mshindi.\" Yaani, ni Mmoja katika dhati yake, katika majina yake, katika sifa zake na katika vitendo vyake. Hakuna afananaye naye katika chochote miongoni mwa hayo. Ikiwa angekuwa na mwana, basi hilo lingehitajika kwamba mwana huyo anafanana naye katika umoja wake; kwa sababu yeye alitokana naye na ni sehemu yake. Aliyeshinda ulimwengu wote,wa juu na wa chini.Ikiwa angekuwa na mwana, basi hangekuwa miongoni mwa walioshindwa, na angefanyiwa upole na baba yake. Umoja wake na ushindi wake ni mambo yasiyoachana. Kwa maana aliye Mmoja, hawi isipokuwa Mshindi kwa vyote. Naye Mshindi kwa vyote hawi isipokuwa Mmoja tu. Hayo yanapinga uwezekano wa kuwepo mshirika yeyote naye kwa namna zote."},{"id":4981,"sura":39,"from_aya":5,"to_aya":7,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"5. Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchana juu ya usiku. Na amefanya jua na mwezi vitumike. Kila kimojapo kinakwenda kwa kipindi kilichowekewa. Jueni mtanabahi! Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe! 6. Amewaumba kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya mwenziwe katika nafsi ile ile. Na akawaletea wanyama wa mifugo jozi nane. Anawaumba katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyu ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Hapana mungu isipokuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi? 7. Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atawaambia mliyokuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani. "},{"id":4982,"sura":39,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} Mwenyezi Mungu anatujulisha kwamba: \"Aliumba mbingu na ardhi\" kwa hekima na masilahi, na ili awaamrishe na kuwakataza waja, awalipe mazuri na awaadhibu. \"Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchana juu ya usiku.\" Kwani viwili hivyo haviwezi kukutana wakati mmoja, bali kikija kimoja katika hivyo, hicho kingine kinatoweka. \"Na amelitiisha jua na mwezi.\" Alijitenga na mamlaka yake, na \u201cakalitiisha jua na mwezi.\" Vyote viko katika nidhamu iliyoratibiwa vizuri sana. \"Kila kimojapo;\" yaani, jua na mwezi, \"kinakwenda kwa kipindi kilichowekewa\" ambacho ni mwisho wa nyumba hii na wakati itakapoharibiwa. Hapo Mwenyezi Mungu ataharibu mitambo yake, jua lake na mwezi wake. Na atawaanzisha viumbe uumbaji mpya, ili wakae na kutulia katika nyumba ya kubakia; katika Bustani za mbinguni au Motoni. \"Jueni mtanabahi! Yeye ndiye Mwenye nguvu\" ambaye hawezi kushindwa, ambaye alishinda kila kitu, ambaye hakuna linaloshindikana kwake, ambaye kutokana na nguvu zake aliviumba viumbe hivi vikubwa na akavitiisha, vikakwenda kwa amri yake. \"Mwenye kusamehe mno\" dhambi za waja wake waumini waliotubu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu mtukufu: \"Na hakika Mimi ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia, na akaamini, na akatenda mema, tena akaongoka.\" Nami ni Mwenye kusamehe mno mwenye kunishirikisha baada ya kuziona Ishara zangu kubwa, kisha akatubia na kurejea kwangu."},{"id":4983,"sura":39,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} Na katika nguvu zake ni kuwa: \"Amewaumba kutokana na nafsi moja\" pamoja na wingi wenu na kutawanywa kwenu katika ardhi.\" Kisha akamfanya mwenziwe katika nafsi ile ile\" ili apate utulivu kwake, naye mke huyo pia apate utulivu kwake, na neema ikamilike kwa hayo. \"Na akawaletea wanyama wa mifugo jozi nane.\" Kama alivyozitaja katika Surat Al-An'am: \"Wawili katika kondoo na wawili katika mbuzi. Na wawili katika ngamia na wawili katika ng'ombe.\" Hawa aliwataja kwa njia maalumu pamoja na kwamba pia aliwateremsha wanyama wengine kwa sababu ya masilahi ya waja wake kwa sababu ya manufaa yao mengi, ujumla wa masilahi yake na heshima yake. Na kwamba wao tu ndio wanaosifika na mambo ambayo hayapo katika wengineo; kama vile dhabihu, mnyama apelekwaye Makka kama zawadi ya Msikiti Mtukufu, wanyama wachinjwao kwa ajili ya kuzaa mwana, wanyama watolewao Zakaa na wanyama watolewao kwa ajili ya fidia ya mauaji. Alipotaja kuumbwa kwa baba yetu na mama yetu, akataja mwanzo wa kuumbwa kwetu, akasema: \"Anawaumba katika matumbo ya mama zenu umbo baada ya umbo,\" yaani, hatua baada ya hatua, ilhali mko katika hali ambayo hauwagusi mkono wa kiumbe chochote wala haliwaangalii jicho lao lolote. Naye akawalea katika sehemu hiyo finyu \"katika viza vitatu;\" giza la tumbo, giza la tumbo la uzazi, na giza la plasenta. \"Huyu\" ambaye ameziumba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi,akakuumbeni na akakuumbieni wanyama wa mifugo, akakuneemesheni, \"Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi\" anayepaswa kufanyiwa uungu na kuabudiwa. Basi kama vile Yeye ndiye Mmoja tu katika kuumba kwake na malezi yake, bila mshirika yeyote katika hayo, basi Yeye ndiye Mmoja katika uungu wake na hana mshirika yeyote. Ndiyo maana akasema: \"Hapana mungu isipokuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?\" Mkaanza kuabudu viabudiwa visivyo Yeye ambavyo haviendeshi chochote, na wala havina chochote katika jambo hilo, baada ya kubainishiwa kwamba Yeye tu ndiye anayestahiki kukusudiwa!"},{"id":4984,"sura":39,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} \"Mkikufuru, basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi\" wala ukafiri wenu haumdhuru, kama vile hanufaiki na utiifu wenu. Lakini maamrisho yake na makatazo yake kwenu ni katika fadhila zake tu na wema wake juu yenu. \"Lakini hafurahii kufuru kwa waja wake\" kwa sababu ya wema wake mkamilifu juu yao, na kwamba wanajua kuwa ukafiri unawafanya kuwa mashakani kiasi kwamba hawawezi kupata furaha baada yake, na kwa kuwa aliwaumba ili wamuabudu. Hili ndilo kusudi ambalo aliwaumba viumbe kwa ajili yake,kwa hivyo haridhii waache kile alichowaumba kwa ajili yake. \"Na mkishukuru\" Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumpwekesha na kumkusudia Yeye tu katika Dini, \"Yeye hufurahika na hilo kutoka kwenu\" kwa sababu ya rehema yake juu yenu na mapenzi yake kwa kuwafanyia wema na kwa kuwa mnafanya kile alichowaumba kwa ajili yake. Na kama vile hadhuriki na ushirikina wenu wala hanufaiki na matendo yenu na kumpwekesha kwenu,vivyo hivyo, kila mmoja wenu ana matendo yake ya heri na ya shari. \" Wala mbebaji habebi mzigo wa mwengine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi.\" Siku ya Kiyama, \"Hapo atawaambia mliyokuwa mkiyafanya.\" Kwa sababu elimu yake iliyadhibiti yote na kalamu yake ikayaandika zamani, na walinzi wake watukufu wakayaandika, na viungo vyenu vikayashuhudia juu yenu, basi atamlipa kila mmoja wenu kile anachostahiki. \"Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani,\" ya wema na uovu. Kinachokusudiwa hapa ni kujulisha kuhusu kulipwa viumbe kwa uadilifu kamili."},{"id":4985,"sura":39,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"8. Na taabu inapomfikia mtu humwomba Mola wake Mlezi naye ameelekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake, husahau yale aliyokuwa akimwomba zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watu njia yake. Sema: Starehe na ukafiri wako kwa muda mchache. Kwani hakika wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni."},{"id":4986,"sura":39,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukarimu wake kwa mja wake, ihsani yake, wema wake na uchache wa shukrani ya mja wake. Na kwamba wakati madhara yanampata kama vile ugonjwa, umaskini, au kuingia katika dhiki ya baharini au kwingineko, anajua kwamba hakuna awezaye kumwokoa katika hali hii isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Kwa hivyo anamuomba kwa unyenyekevu na kutubia kwake. Na anamuomba msaada katika kuondoa hayo yaliyompata, na anasisitiza kufanya hivyo. \"Kisha\" Mwenyezi Mungu \"akimpa neema kutoka kwake\" kwa kumuondoshea madhara na dhiki iliyokuwa imemsibu, \"husahau yale aliyokuwa akimwomba zamani\" na akawa ni kana kwamba hakupatwa na madhara yoyote, na akaendelea na ushirikina wake. \"Na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watu katika njia yake\" na ajipoteze yeye mwenyewe. \"Sema\" ukimwambia huyu mkaidi aliyebadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru: \"Starehe na ukafiri wako ni kwa muda mchache, kwani hakika wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni.\" Hicho unachostarehe kwacho hakitakusaidia kitu ikiwa utaishia Motoni. \"Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka, kisha yakawafikia waliyokuwa wakiahidiwa. Yatawafaa nini yale waliyostareheshewa?\""},{"id":4987,"sura":39,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"9. Je, afanyaye ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi... Sema: Ati watakuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Hakika wanaokumbuka ni watu wenye akili."},{"id":4988,"sura":39,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} Haya ni maneno yanayohusu tofauti iliyopo kati ya yule atendaye mambo ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu na wale wasiofanya hivyo, na baina ya wenye elimu na wasiokuwa na elimu, na kwamba haya ni miongoni mwa mambo ambayo yalishathibiti kwa njia ya yakini katika akili kwamba yanatofautiana. Kwani mwenye kuyapa mgongo mambo ya kumtii Mola wake Mlezi na akafuata matamanio yake, hawi kama mwenye kumnyenyekea kwa kufanya ibada bora kabisa ambayo ni swala, na nyakati bora zaidi ambazo ni nyakati za usiku. Huyu, Mwenyezi Mungu amemuelezea kwa matendo mengi bora zaidi. Kisha akamuelezea kwa hofu na matumaini, na akataja kwamba hofu hiyo inahusiana na adhabu ya Akhera kwa sababu ya madhambi yake yaliyopita, na kwamba matumaini hayo yanahusiana na rehema ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo akamuelezea kwa matendo ya dhahiri na ya ndani. \"Sema: 'Ati watakuwa sawa wale wanaojua'\" Mola wao Mlezi na wanazijua hukumu zake za kisheria na hukumu zake za kimalipo, siri na hekima alizo nazo katika hayo, \"na wale wasiojua\" kitu chochote katika hayo? Kamwe hawawi sawa kama vile hauwi usiku na mchana, wala mwangaza na giza, wala maji na moto.  \"Hakika wanaokumbuka tu ni watu wenye akili\" safi, werevu. Hao ndio wanaopendelea cha juu kuliko cha chini. Wanaipendelea elimu kuliko ujinga, na kumtii Mwenyezi Mungu kuliko kumuasi. Kwa sababu wana akili zinazowaelekeza kufikiria matokeo ya mambo. Tofauti na yule ambaye hana akili; yeye anayachukua matamanio yake kuwa ndiyo mungu wake."},{"id":4989,"sura":39,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"10. Sema: Enyi waja wangu mlioamini! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu."},{"id":4990,"sura":39,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} Yaani, sema, ukiwaita watukufu zaidi katika viumbe vyote, ambao ni Waumini, ukiwaamrisha kwa amri iliyo bora zaidi, ambayo ni ucha Mungu, ukiwakumbusha sababu inayowalazimu kuwa wacha Mungu, ambayo ni Umola wa Mwenyezi Mungu juu yao, na neema zake ziwe juu yao kama vile neema ya imani. Hiyo inamlazimu mtu kuwa mcha Mungu, kama unavyoweza kusema: 'Ewe mkarimu, toa sadaka! Ewe shujaa, pigana vita.' Na akawatajia malipo ya kuwatia nasati katika dunia, akasema: \"Wale wafanyao wema katika dunia hii\" kwa kumuabudu Mola wao Mlezi watapata \"wema\" kama vile riziki kunjufu, nafsi iliyotulia na moyo mchangamfu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema.\" \"Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu.\" Mkizuiliwa kumwabudu katika nchi moja, basi hamieni nchi nyingine ambapo mtaweza kumuabudu Mola wenu na kusimamisha Dini yenu. Na pale aliposema: \"Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema,\" watu wengine walikuwa na dhana fulani, maana yake ambayo ni kwamba maneno haya ni ya jumla kwa njia ya kwamba kila atendaye mazuri, atapata mema katika dunia hii. Basi vipi kuhusu mtu anayeamini na anaishi katika nchi ambayo anakandamizwa na kuteswa (kiasi kwamba anashindwa kufanya mazuri), je, hatapata hayo? Kwa hivyo, akaiondoa dhana hii kwa kauli yake: \"Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu.\" Hapa pia kuna bishara njema aliyoisema Mtume, rehema na amani zimshukie, kwamba: \"Kundi katika umma wangu litaendelea kushikamana na haki, huku wakiwa washindi, na hatawadhuru wenye kutaka kuwaangusha wala wenye kuwahalifu mpaka itakapofika amri ya Mwenyezi Mungu, nao wako hivyo.\" Aya hii inalizungumzia hilo na kulirejea kwa njia ya karibu, ambayo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alijulisha kwamba ardhi yake ni pana. Kwa hivyo, hata kama mtazuiliwa kiasi gani kumwabudu katika mahali fulani, basi hamieni kwingine. Hili ni la jumla katika nyakati zote na mahali pote. Kila mhamiaji lazima atapata kimbilio kwa Waislamu ambapo ataweza kukimbilia, na mahali ambapo ataweza kuisimamisha dini yake. \"Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hesabu.\" Hili ni la jumla katika kila aina ya subira: kuwa na subira juu ya mipango michungu ya Mwenyezi Mungu; basi hafai kukasirika kwa sababu yake, kuwa na subira juu ya kutomuasi na kuwa na subira katika kumtii; mpaka akatekeleza utiifu apaswavyo. Kwa hivyo ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa waliosubiri ni kwamba atawalipa bila ya hesabu, yaani bila kikomo, wala kipimo, na hilo si isipokuwa kwa sababu ya ubora wa kuwa na subira na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu, na kwamba inasaidia juu ya kila jambo."},{"id":4991,"sura":39,"from_aya":11,"to_aya":16,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"11. Sema: Hakika mimi nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia Dini Yeye tu. 12. Na nimeamrishwa niwe wa mwanzo wa Waislamu. 13. Sema: Hakika mimi ninaogopa adhabu ya Siku Kubwa nikimuasi Mola wangu Mlezi. 14. Sema: Mwenyezi Mungu tu namuabudu kwa kumsafishia Yeye tu Dini yangu. 15. Basi nyinyi abuduni mpendacho badala yake Yeye. Sema: Hakika waliohasirika ni wale waliojihasiri na ahali zao Siku ya Kiyama. Tambueni kuwa hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri. 16. Yatawekwa juu yao matabaka ya moto, na chini yao matabaka. Kwa hayo Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake. Enyi waja wangu! Nicheni Mimi! "},{"id":4992,"sura":39,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} Yaani, \"Sema\" ewe Mtume ukiwaambia watu: \"Hakika mimi nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia Dini Yeye tu.\" Kama ilivyo katika kauli yake mwanzo wa sura hii: \"Basi muabudu Mwenyezi Mungu ukimsafia Dini Yeye tu.\""},{"id":4993,"sura":39,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} \"Na nimeamrishwa niwe wa kwanza wa Waislamu.\" Kwa sababu mimi ndiye mlinganiaji anayeongoza viumbe kwa Mola wao Mlezi, jambo ambalo linahitaji kwamba niwe wa kwanza kutekeleza yale aliyoamrisha na wa kwanza kusilimu. Na jambo hili ni lazima litokee kwa Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake, na pia litokee kwa wale wanaodai kuwa miongoni mwa wafuasi wake. Ni lazima kuwa Waislamu katika matendo ya dhahiri na kumkusudia Mwenyezi Mungu katika matendo ya dhahiri na ya ndani."},{"id":4994,"sura":39,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} \"Sema: 'Hakika mimi ninaogopa nikimuasi Mola wangu Mlezi\" katika yale aliyoniamrisha ya kumkusudia Yeye tu na kuwa Waislamu, \"adhabu ya Siku Kubwa\" ambayo mwenye kumshirikisha atadumu humo milele na anayeasi ataadhibiwa ndani yake."},{"id":4995,"sura":39,"from_aya":14,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14 - 15} \"Sema: 'Mwenyezi Mungu tu namuabudu kwa kumsafishia Yeye tu Dini yangu. Basi nyinyi abuduni mpendacho badala yake Yeye.\" Kama alivyosema: \"Sema: Enyi makafiri! Siabudu mnachokiabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. Wala sitaabudu mnachoabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.\" \"Sema: Hakika waliohasirika\" kwa uhakika ni \"wale waliojihasiri nafsi zao\" kwa kuwa walizinyima thawabu na zikastahiki kwa sababu yao adhabu kali, \"na ahali zao Siku ya Kiyama.\" Yaani, watatenganishwa na huzuni yao na hasara yao itakuwa kubwa. \"Tambueni kuwa hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri,\" ambayo hakuna hasara nyingine mfano wake. Ni hasara inayoendelea ambayo hakuna faida yoyote baada yake, wala hata hakuna usalama."},{"id":4996,"sura":39,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} Kisha akataja ukubwa wa mashaka yatakayowapata, akasema: \"Yatawekwa juu yao matabaka ya moto na chini yao matabaka.\" Kwa hayo tuliyoielezea, adhabu ya wakazi wa Motoni ni mjeledi ambao kwa huo Mwenyezi Mungu anawachungia waja wake kwenda kwenye rehema zake na \"Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake. Enyi waja wangu! Nicheni Mimi,\" na ni karipio kutokana na yale ambayo yanawasababishia adhabu. Ametakasika Yule ambaye amewarehemu waja wake katika kila jambo! Pia amewasahilishia njia zinazofikisha huko na akawahimiza kuzifuata. Akawatia moyo kwa kila kitu ambacho nafsi inatamani sana, na nyoyo zinatulia juu yake. Akawatahadharisha tahadharisho kubwa sana dhidi ya kufanyia kazi mambo yasiyokuwa hilo na akawatajia sababu za kuwakataza hadi wayaache."},{"id":4997,"sura":39,"from_aya":17,"to_aya":18,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"17. Na wale wanaojiepusha na ibada potovu, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja wangu. 18. Ambao husikiliza maneno, wakafuata lililo bora yao. Hao ndio aliowaongoa Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili. "},{"id":4998,"sura":39,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja hali ya wahalifu,akataja hali ya waliotubu na malipo yao, akasema: \"Na wale wanaojiepusha kuabudu Taghuti,\" yaani, chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu. Hii ni mbinu nzuri zaidi ya kuondoa kitu katika vinginevyo ambayo Yeye Mwenye hekima na ajuaye zaidi alitumia hapa. Kwani wale waliojiepusha kuabudu Taghuti ndio wanaofaa kusifiwa peke yao.  \"Na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu\" kwa kumuabudu na kumkusudia Yeye tu katika Dini. Basi dhamira zao zikatoka katika kuabudu masanamu na kwenda katika kumwabudu Mfalme Mjuzi zaidi, na kutoka katika ushirikina na maasia na kuingia katika kumpwekesha na kumtii. \"Watapata bishara njema,\" ambayo kiwango chake hakiwezi kupimwa wala hajui jinsi ilivyo haswa isipokuwa yule aliyewatukuza kwayo. Hili linajumuisha bishara njema katika maisha ya dunia kwa kupewa sifa njema, maoni mazuri na kutunzwa na Mwenyezi Mungu ambayo kwayo wanaona kuwa anakusudia kuwatukuza duniani na akhera. Na pia wanayo bishara njema katika akhera wakati wa kufa, katika kaburi na katika siku ya Kiyama. Na hitimisho la bishara yao njema ni yale ambayo Mola wao Mlezi, Mkarimu atawabashiria ya radhi zake za kuendelea juu yao, wema wake, ihsani yake na kupata amani yake Peponi."},{"id":4999,"sura":39,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} Na alipojulisha kwamba wana bishara njema, Mwenyezi Mungu alimwamrisha kwamba awabashirie na akataja maelezo ambayo kwayo waliistahiki bishara hiyo njema, akasema: \"Basi wabashirie waja wangu. Ambao husikiliza maneno, wakafuata lililobora yao.\" Haya yanajumuisha aina zote za maneno. Wao wanasikiliza yote yanayosemwa ili watofautishe kati ya kile kinachopaswa kupendelewa na kile kinachopaswa kuepukwa. Ndiyo ilikuwa ni sehemu ya azimio lao na sababu na akili ya nzuri ni kwamba wanafuata maneno bora tu, ambayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno ya Mtume Wake. Kama alivyosema katika Sura hii: \"Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana...\" hadi mwisho wa Aya. Kuna suala muhimu katika Aya hii, ambalo ni kwamba pale alipojulisha kuhusu watu hawa waliosifiwa kwamba wanasikiliza yanayosemwa na kufuata yaliyo bora zaidi kati yake, ni kana kwamba ilisemwa: 'Je, ipo njia ya kujua maneno hayo yaliyobora zaidi ili tuweze pia kusifika na sifa za watu wenye akili nzuri hawa, na ili tujue kwamba anayeyapendelea ni miongoni mwa watu wenye akili nzuri?' Ikasemwa: Ndiyo,yaliyobora zaidi ni yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika kauli yake: \"Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana...\" hadi mwisho wa Aya. Hao \"ambao husikiliza maneno, wakafuata lililobora yao,hao ndio aliowaongoa Mwenyezi Mungu\" kufikia maadili na vitendo bora zaidi, \"na hao ndio wenye akili\" safi. Katika akili yao nzuri na azimio lao ni kwamba walitambua kilicho kizuri kutokana na mengineyo yote, na wakapendelea yale yafaayo kuliko mengine yote, na hii ni alama ya kwamba wana akili nzuri,wala hakuna alama ya kuwa na akili nzuri kuliko hii. Kwani yule asiyeweza kutofautisha kati ya maneno mazuri na mabaya si katika watu wenye akili nzuri, au mwenye kuyatofautisha lakini matamanio yake yaliishinda akili yake, kwa hivyo akili yake ikabakia kufuata tu matamanio yake, basi hakupendelea kilichobora zaidi; huyu anakuwa ana akili pungufu."},{"id":5000,"sura":39,"from_aya":19,"to_aya":20,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"19. Je, yule mwenye kustahiki hukumu ya adhabu, je, wewe unaweza kumwokoa aliyomo katika Moto? 20. Lakini waliomcha Mola wao Mlezi watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa; chini yake hupita mito. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. "},{"id":5001,"sura":39,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} Yaani, je yule aliyewajibikiwa neno la adhabu kwa sababu ya kuendelea kwake kupotea na kufanya ukaidi na kukufuru, utamuongozaje? Kwani wewe huna uwezo wa kumwongoa na huwezi kumwokoa aliyemo Motoni."},{"id":5002,"sura":39,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Lakini kushinda kukubwa zaidi na kufuzu kukubwa zaidi ni kwa watu wema, ambao Mwenyezi Mungu amewaandalia mambo makarimu na neema mbalimbali ambazo kiwango chake hakiwezi kupimwa. \"Watapata ghorofa\" za juu, zilizopambwa miongoni kwa uzuri mkubwa, za kifahari kiasi kwamba nje yake inaweza kuonekana kutokea ndani yake na ndani yake kutokea nje yake. Na kutoka kwa kuinuka kwake juu sana zinaonekana kama nyota iliyo mbali zaidi katika upeo wa mashariki au magharibi, na ndiyo maana akasema: \"zilizojengwa juu ya ghorofa\" kwa dhahabu na fedha, na zimepakwa miski yenye harufu nzuri zaidi. \"Chini yake hupita mito\" inayotiririka, inayomwagilia bustani zenye maua na miti safi, inayotoa kila aina ya matunda matamu yaliyoiva. \"Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake\" aliyowaahidi wachamungu, kwa hivyo hakuna budi ataitimiza. Basi nawatimize sifa za uchamungu ili awalipe ujira wao."},{"id":5003,"sura":39,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"21. Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni. Kisha akayapitisha kwenye chemchemi katika ardhi, kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbalimbali? Kisha hunyauka ukaiona imekuwa kimanjano, na kisha huifanya mapepe. Bila ya shaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye akili."},{"id":5004,"sura":39,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawakumbusha wenye ufahamu mkubwa maji aliyoyateremsha kutoka mbinguni, na kwamba aliyapitisha kwenye chemichemi za ardhi, akayahifadhi humo, ambayo inawezekana kuyatoa kwa urahisi sana. \"Kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbali mbali\" kama vile ngano, mahindi, shayiri, mchele na vitu vinginevyo. \"Kisha hunyauka\" inapokomaa au inapotokewa na janga \"ukaiona imekuwa kimanjano, na kisha huifanya mapepe.\" \"Bila ya shaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye akili,\" wanaokumbuka kwayo utunzaji wa Mola wao Mlezi na rehema yake kwa waja wake. Kwa maana aliwafanyia wepesi maji haya na akayahifadhi katika hazina za ardhi kwa ajili ya maslahi yao. Wanakumbuka kwayo ukamilifu wa uwezo wake na kwamba atawahuisha wafu kama alivyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na wanakumbuka kwayo kwamba anayefanya haya ndiye anayestahiki kuabudiwa. Ewe Mwenyezi Mungu! Tujaalie tuwe miongoni mwa wenye ufahamu mkubwa, wale uliowataja na ukawaongoa kwa akili nzuri ulizowapa na ukawaonyesha siri za Kitabu chako na maajabu ya Aya zako ambazo hakuna mwingine aliyeweza kufikia hilo. Wewe ndiye Mpaji."},{"id":5005,"sura":39,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"22. Je, yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfungulia kifua chake kwa Uislamu, na akawa yuko kwenye nuru itokayo kwa Mola wake Mlezi (ni sawa na mwenye moyo mgumu?) Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisizomkumbuka Mwenyezi Mungu! Hao wamo katika upotofu wa dhahiri."},{"id":5006,"sura":39,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} Yaani, je, ni sawa yule ambaye Mwenyezi Mungu amekifungua kifua chake kwa Uislamu, kwa hivyo kikapanuka ili kupokea hukumu za Mwenyezi Mungu na kuzifanyia kazi kwa uwazi, furaha, na ufahamu mzuri wa mambo yake, naye ndiye aliyekusudiwa na kauli yake, \"na akawa yuko kwenye nuru itokayo kwa Mola wake Mlezi,\" ni sawa na asiyekuwa hivyo, ambaye moyo wake ni mgumu? Kama ilivyosema: \"Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisizomkumbuka Mwenyezi Mungu!\" Hazilainiki kwa ajili ya Kitabu chake, wala hazikumbuki aya zake, na wala hazipati utulivu katika kumkumbuka, bali zinajiepusha na Mola wake Mlezi na kuwaelekea wengineo. Hawa wanapatwa na balaa na uovu mkubwa. Na \"hao wamo katika upotofu wa dhahiri.\" Na ni upotofu gani ulio mkubwa zaidi kuliko upotevu wa mwenye kumpa mgongo mlinzi wake, na yule ambaye furaha yote iko katika kurejea kwake, na moyo wake ukawa mgumu usimtaje, na akayaendea kila yenye kumdhuru?"},{"id":5007,"sura":39,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"23. Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa."},{"id":5008,"sura":39,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu Kitabu chake alichokiteremsha kwamba ni \"hadithi nzuri kabisa.\" Kwani hadithi nzuri kabisa ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na kitabu bora zaidi kilichoteremshwa katika maneno ya Mwenyezi Mungu ni Qur-ani hii. Na ikiwa ndiyo nzuri zaidi, basi inajulikana kuwa lafudhi zake ndizo fasaha zaidi na zilizo wazi zaidi, na kwamba maana zake ndizo maana tukufu zaidi. Kwa sababu ndiyo hadithi nzuri zaidi katika maana ya maneno yake. \"Kitabu chenye kufanana\" katika uzuri, kuelewana na kutotofautiana kwa namna yoyote ile, kiasi kwamba kila anapoizingatia mwenye kuzingatia na kuitafakari mwenye kutafakari, anaona namna kinavyoafikiana vyema - hata katika maana zake za ndani zaidi - jambo ambalo linawashangaza watazamaji na anakuwa na uhakika kuwa hakitoki isipokuwa kwa yule ambaye ni Mwenye hekima na ajuaye zaidi. Hii ndiyo maana ya kufanana mahali hapa. Ama katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Yeye ndiye aliyekuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam (zenye maana wazi). Hizo ndizo msingi wa Kitabu hiki. Na ziko nyingine za mifano,\" maana yake ni kwamba zinawachanganya watu wengi kuzifahamu, na kuchanganya huku hakuwezi kuondolewa isipokuwa kwa kuzirudisha kwa aya zilizo wazi. Ndiyo maana akasema: \"Ndani yake zimo Aya muhkam (zenye maana wazi). Hizo ndizo msingi wa Kitabu hiki. Na ziko nyingine za mifano.\" Basi hapa akafanya kufanana huku ni katika baadhi yake, na hapo juu akakifanya chote ni chenye kufanana. Kwa sababu alisema: \"Hadithi nzuri zaidi\" ambayo ni sura na Aya. \"Na kukaririwa;\" yaani, vinakaririwa humo visa, hukumu mbalimbali, ahadi, vitisho, sifa za watu wema na sifa za watu waovu. Na yanakaririwa humo majina na sifa za Mwenyezi Mungu. Hili ni katika utukufu wake na uzuri wake. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alipojua hitaji la viumbe juu ya maana zake zinazotakasa nyoyo, zinazokamilisha maadili, na kwamba maana hizi kwa nyoyo ni kama maji yanyweshwayo miti. Kwa sababu kila wakati miti inapokawia kunyweshwa maji, inapungua na hata labda inaweza kuharibika. Na kila mara inapomwagiliwa maji, inakuwa nzuri na inatoa kila aina ya matunda yenye faida. Basi vile vile moyo daima unahitaji kurudiliwa na maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba ikiwa maana hizo zitarudiwa mara moja tu katika Qur-ani nzima, basi haitauathiri hata kidogo, na hakutakuwa na matokeo yaliyotakiwa kwayo. Ndiyo maana nikachukua njia hii adhimu katika tafsiri hii kwa kufuata mfano wa tafsiri yake. Hutapata ndani yake kuruka kutoka mahali hadi pahali pengine. Bali utapata maelezo ya kila sehemu pamoja na maana yake kamili, bila kuzingatia yale yaliyotangulia, yale yanayofanana nayo, hata kama baadhi ya maeneo yanakuwa yamerefushwa zaidi kuliko mengine na yenye manufaa zaidi. Kwa hivyo, msomaji wa Qur-ani ambaye anatafakari maana zake hafai kuacha kutafakari katika sehemu zake zote. Kwa sababu hilo linamfanya kupata heri nyingi na manufaa tele. Na kwa vile Qur-ani tukufu ina utukufu huu na ukubwa huu, iliathiri nyoyo za wenye ufahamu mkubwa walioongoka. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: \"husisimua kwacho ngozi za wenye kumhofu Mola wao Mlezi,\" kwa sababu ina vitisho na mambo ya kuhofisha yasumbuayo. \"Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu,\" wakati yanapotajwa matumaini na mambo yanyotia moyo. Mara huwahimiza kutenda heri, na wakati mwingine huwatishia wasifanye maovu. \"Hayo\" aliyoyataja Mwenyezi Mungu kuhusiana na athari ya Qur-ani juu yao \"ndiyo uwongofu wa Mwenyezi Mungu\" kwa waja wake, na ambao ni katika fadhila zake na wema wake juu yao. \"Kwa huo humwongoa amtakaye\" katika waja wake. Na inawezekana kwamba kile kinachokusudiwa katika kauli yake: \"hayo\" ni Qur-ani tuliyowaelezea, \"ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu\" ambao hakuna njia nyingine inayoweza kufikisha ielekeayo kwa Mwenyezi Mungu ila kwa hiyo. \"Kwa huo humwongoa amtakaye\" katika waja wake miongoni mwa wale ambao nia zao ni njema. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: \"Mwenyezi Mungu huwaongoa kwayo wenye kufuata radhi yake katika njia za salama.\" \"Na ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, basi hapana wa kumwongoa.\" Kwa sababu hakuna njia inayofikisha kwake ila kwa kuwezesha kwake na kuwezesha kurejea kwenye Kitabu chake. Kwa hivyo, kama hayo hayatotokea, basi hakuna njia iendayo kwenye uwongofu na hakutakuwa na chochote ila upotofu na mashaka yaliyo wazi."},{"id":5009,"sura":39,"from_aya":24,"to_aya":26,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"24. Je, atakayekuwa anapambana kwa uso wake na adhabu mbaya kabisa Siku ya Kiyama, (ni sawa na watenda wema?) Na wataambiwa wenye kudhulumu: Onjeni hayo mliyokuwa mkiyachuma! 25. Waliokuwa kabla yao walikadhibisha, na ikawajia adhabu kutoka pahala wasipopatambua. 26. Basi Mwenyezi Mungu akawaonjesha hizaya katika uhai wa duniani. Na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi; laiti wangelijua! "},{"id":5010,"sura":39,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} Yaani, je, mtu huyu ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa na kumwezesha kufuata njia ifikishayo kwenye makao ya utukufu wake anatoshana na mtu aliye katika upotofu, na akaendelea na ukaidi wake mpaka ikafika Siku ya Kiyama? Basi ikamjia adhabu kubwa, kwa hivyo akaanza kujikinga kwa uso wake, ambao ndio kiungo cha heshima zaidi, na ambao hata adhabu ndogo tu inauathiri vibaya. Siku hiyo akawa anajikinga kwa uso wake kutokana na adhabu; kwani mikono yake na miguu yake itakuwa imefungwa pingu? \"Na wataambiwa wenye kudhulumu\" nafsi zao kwa ukafiri na maasia kwa njia ya kuwakaripia na kuwakemea: \"Onjeni hayo mliyokuwa mkiyachuma!\""},{"id":5011,"sura":39,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} \"Wale waliokuwa kabla yao\" miongoni mwa mataifa \"walikadhibisha\" kama walivyokadhibisha watu hawa, \"basi ikawajia adhabu kutoka pahala wasipopatambua,\" walipokuwa wameghafilika mwanzo wa mchana, au walipokuwa wamelala adhuhuri."},{"id":5012,"sura":39,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} \"Basi Mwenyezi Mungu akawaonjesha\" kwa adhabu hiyo \"hizaya katika uhai wa duniani,\" wakahizika mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya viumbe vyake. \"Na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi; laiti wangelijua!\" Basi na watahadhari watu hawa dhidi ya kuendelea kukadhibisha, wakaja kupatwa na adhabu ile iliyowapata wenzao."},{"id":5013,"sura":39,"from_aya":27,"to_aya":31,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"27. Na bila ya shaka tumewapigia watu mifano ya kila namna katika hii Qur-ani ili wapate kukumbuka. 28. Qur-ani ya Kiarabu isiyo na upogo, ili wamche Mungu. 29. Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanaogombana, na wa mtu mwengine aliyehusika na bwana mmoja tu. Je, wako sawa katika hali zao? Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! Lakini wengi wao hawajui. 30. Kwa hakika wewe utakufa, na wao watakufa. 31. Kisha bila ya shaka mtagombana Siku ya Kiyama mbele ya Mola wenu Mlezi. "},{"id":5014,"sura":39,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba amepiga kila aina ya mfano ndani ya Qur-ani; Mifano ya watu wema, mifano ya watu waovu, mifano ya wale waliompwekesha na wale waliomshirikisha. Kila mfano unaleta karibu uhakika wa mambo na hekima iliyoko ndani yake \"ili wapate kukumbuka\" tunapowabainishia haki, basi wakaijua na wakafanyia matendo mema."},{"id":5015,"sura":39,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} \"Qur-ani ya Kiarabu isiyo na upogo.\" Yenye lafudhi zilizo wazi, yenye maana nyepesi, haswa kwa Waarabu, na isiyokuwa na kasoro wala upungufu kwa namna yoyote ile, katika lafudhi zake wala katika maana zake. Hili linalazimu kwamba imenyooka kikamilifu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: \"Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo. Kimenyooka sawa.\" \"Ili wamche Mungu\" Mtukufu, kwa kuwa tumewarahisishia njia za kielimu za ucha Mungu na za kivitendo za ucha Mungu kwa Qur-ani hii ya Kiarabu iliyonyooka, ambamo Mwenyezi Mungu amepiga kila mifano."},{"id":5016,"sura":39,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Kisha akapiga mfano wa shirki na tauhidi, akasema: \"Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanaogombana.\" Ni wengi, na hawakubaliani katika jambo wala hali yoyote ili aweze kustarehe. Bali wanagombana kwa sababu yake na kila mmoja wao anayo matakwa anayotaka yatekelezwe, naye mwengine anataka kitu tofauti. Basi, je, unadhani itakuwaje hali ya mtu huyu mbele ya washirika hawa wanaogombana? \"Na wa mtu mwengine aliyehusika na bwana mmoja tu\" ambaye tayari alishajua makusudio ya bwana wake na akapata raha kamili. \"Je, wako sawa katika hali zao?\" Hawawi sawa. Basi vile vile, mshirikina ana washirika wanaomgombania. Anamuomba huyu, kisha anamuomba huyu. Kwa hivyo, utamuona hajatulia kokote. Naye anayemkusudia Mola wake Mlezi, Mwenyezi Mungu ameshamuokoa kutokana na ushirikina, basi akawa katika raha na utulivu kamili. \"Je, wako sawa katika hali zao? Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu\" kwa kubainisha haki mbali na batili, na kuwaongoza wasiojua. \"Lakini wengi wao hawajui.\""},{"id":5017,"sura":39,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} \"Kwa hakika wewe utakufa na wao watakufa.\" Yaani, nyinyi nyote mtakufa. Kwani, \"hatukumjaalia mwanadamu yeyote kabla yako kuwa na maisha ya milele. Basi je, ukifa wewe wao wataishi milele?\""},{"id":5018,"sura":39,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} \"Kisha bila ya shaka mtagombana Siku ya Kiyama mbele ya Mola wenu Mlezi\" katika yale mliyokuwa mkihitalifiana ndani yake, naye atahukumu baina yenu kwa hukumu yake ya uadilifu, na atamlipa kila mmoja wenu aliyoyatenda, kwani Mwenyezi Mungu aliyadhibiti na wao wakayasahau!"},{"id":5019,"sura":39,"from_aya":32,"to_aya":35,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"32. Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemsingizia uwongo Mwenyezi Mungu na akaukadhibisha ukweli ulipomfikia? Je, siyo katika Jahannamu makazi ya hao makafiri? 33. Na aliyeuleta ukweli na akausadiki - hao ndio wacha Mungu. 34. Watapata watakachotaka kwa Mola wao Mlezi. Hayo ndiyo malipo ya watendao mema. 35. Ili Mwenyezi Mungu awafutie ukomo wa uovu waliyoufanya na awalipe ujira wao kwa mujibu wa ukomo wa wema waliokuwa wakiutenda. "},{"id":5020,"sura":39,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema akionya na kutahadharisha kwamba hakuna dhalimu mkubwa zaidi \"kuliko yule aliyemsingizia uwongo Mwenyezi Mungu.\" Ima kwa kumnasibisha na kile ambacho hakiufailii ukuu wake au kwa kudai unabii, au kwa kusema kwamba Mwenyezi Mungu alisema hivi au alijulisha hivi au alimhukumu hivi ilhali yeye ni mwongo katika hayo. Huyu imejumuishwa katika kauli yake Mtukufu: \"Na kumsingizia Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua\" ikiwa hajui, vinginevyo, basi hilo ni baya mno. Au \"akaukadhibisha ukweli\" ulioungwa mkono na ushahidi wa wazi \"ulipomfikia\" naye akaukadhibisha. Na ikiwa aliunganisha kati ya kumdanganyishia Mwenyezi Mungu na kukadhibisha ukweli, basi hiyo inakuwa dhuluma juu ya dhuluma.\" Je, siyo katika Jahannamu makazi ya hao makafiri,\" ambamo Mwenyezi Mungu atachukua haki kutoka kwa kila dhalimu na kafiri? \"Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhuluma iliyo kubwa.\""},{"id":5021,"sura":39,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} Na alipomtaja mwongo anayekadhibisha, uhalifu wake na adhabu yake, akamtaja mkweli anayeaminika na ujira wake, akasema: \"Na aliyeuleta ukweli\" katika maneno yake na vitendo vyake. Na hapo wakaingia Manabii na waliochukua nafasi zao miongoni mwa wasemao ukweli katika aliyoyasema juu ya habari za Mwenyezi Mungu, hukumu zake na katika yale aliyoyafanya katika sifa za ukweli, \"na akausadiki.\" Kwa sababu mtu anaweza kuja na ukweli, lakini asiusadiki kwa sababu ya kiburi chake au dharau lake kwa yule aliyeusema na akauleta. Kwa hivyo ni lazima ili mtu asifiwe, awe mkweli na mwenye kusadiki. Ukweli wake unaonyesha elimu yake na uadilifu wake, nako kusadiki kwake kunaonyesha unyenyekevu wake na kutotakabari kwake. \"Hao\" waliowezeshwa kuunganisha mambo mawili haya \"ndio wacha Mungu.\" Kwani sifa zote za uchamungu zinarejea kuwa mkweli katika haki na kuisadiki."},{"id":5022,"sura":39,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} \" Watapata watakachotaka kwa Mola wao Mlezi\" miongoni mwa yale ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio halijawahi kuyasikia, wala hayajawahi kupita kwenye moyo wa mwanadamu yeyote. Kwani kila kitu ambacho mapenzi yao na matamanio yao yataambatana nayo miongoni mwa aina mbalimbali za starehe na matamanio, basi watazipata tayari zimeshatayarishwa kwa ajili yao. \"Hayo ndiyo malipo ya watendao mema,\" wale wanaomuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba wanamuona. Lakini ikiwa hawamwoni, basi Yeye anawaona, na pia wanawafanyia wema waja wa Mwenyezi Mungu."},{"id":5023,"sura":39,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} \"Ili Mwenyezi Mungu awafutie ukomo wa uovu waliyoufanya na awalipe ujira wao kwa mujibu wa ukomo wa wema waliokuwa wakiutenda.\" Matendo ya mwanadamu ya hali tatu: ima ni mbaya zaidi au bora zaidi au si mbaya zaidi wala bora zaidi. Sehemu hii ya mwisho ndiyo inajumuisha yale yanayoruhusiwa ambayo hayaambatani na malipo wala adhabu. Nayo mabaya zaidi yanajumuisha maasia yote. Nayo mazuri zaidi yanajumuisha mambo yote ya utiifu. Kupitia maelezo haya, maana ya Aya hii inadhihirika, na kwamba kauli yake: \"Ili Mwenyezi Mungu awafutie ukomo wa uovu waliyoufanya,\" yaani, madhambi yao madogo na makubwa kwa sababu ya wema wao na uchamungu wao, \"na awalipe ujira wao kwa mujibu wa ukomo wa wema waliokuwa wakiutenda.\" Kwani, \"hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata uzito wa chembe moja. Na ikiwa ni jambo jema, basi Yeye hulizidisha na hutoa kutoka kwake malipo makubwa.\""},{"id":5024,"sura":39,"from_aya":36,"to_aya":37,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"36. Je, Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake? Na ati wanakutishia kwa hao wenginewe wasiokuwa Yeye! Na aliyepotezwa na Mwenyezi Mungu, basi hana wa kumwongoa. 37. Na ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa, basi hana wa kumpotoa. Je, Mwenyezi Mungu si Mwenye nguvu, anayeweza kulipiza? "},{"id":5025,"sura":39,"from_aya":36,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36 - 37} \"Je, Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake?\" Yaani, je, si katika ukarimu wake, kutoa kwake kwa wingi, utunzaji wake mja wake ambaye alimuabudu kikamilifu na akatekeleza amri zake, na akaepuka makatazo yake, hasa kiumbe mkamilifu zaidi katika kumuabudu Mola wake Mlezi, ambaye ni Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake? Mwenyezi Mungu Mtukufu atamtosheleza katika mambo ya dini yake na dunia yake, na atamzuia mbali na wale wanaomtakia mabaya. \"Na ati wanakutishia kwa hao wenginewe wasiokuwa Yeye,\" kama vile masanamu na wenza, kwamba watakufikishia uovu. Lakini hili ni katika ukengeufu wao na upotofu wao. \"Na aliyepotezwa na Mwenyezi Mungu, basi hana wa kumwongoa. Na ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa, basi hana wa kumpotoa.\" Kwa sababu Yeye Mtukufu ndiye ambaye mkononi mwake kuna kuongoa na kupotoa. Naye ndiye ambaye anachotaka, kinakuwa, na asichokitaka hakiwi. \"Je, Mwenyezi Mungu si Mwenye nguvu\" kamili ambazo kwazo alikishinda kila kitu, na kwa nguvu zake humtosheleza mja wake na humzuilia mbali na vitimbi vya maadui zake, \"anayeweza kulipiza\" mwenye kumuasi? Basi jihadharini na sababu za adhabu yake."},{"id":5026,"sura":39,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"38. Na ukiwauliza: Ni nani aliyeziumba mbingu na ardhi. Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Sema: Je, mnawaonaje wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea dhara yake? Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake? Sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Kwake Yeye na wategemee wanaotegemea."},{"id":5027,"sura":39,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} Yaani, ukiwauliza hawa wapotofu wanaokutisha kwa wasiokuwa Mwenyezi Mungu, na ukawathibitishia hoja kutokana nao wenyewe, ukasema: \"Ni nani aliyeziumba mbingu na ardhi?\" Hawataweza kuwathibitishia miungu wao hao chochote katika kuziumba, bali \"bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu\" peke yake ndiye aliyeziumba. \"Sema\" uwaambie kwa njia ya kuwafanya wakiri kutoweza kwa miungu yao baada ya kwisha bainishwa uwezo wa Mwenyezi Mungu: \"Je, mnawaonaje wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru\" kwa ubaya wowote ule, \"wao wanaweza kuniondolea dhara yake\" yote kabisa au hata kuipunguza tu? \"Au akitaka kunirehemu\" kwa rehema ambayo kwayo atanifikishia manufaa katika dini yangu au dunia yangu, \"je, wao wanaweza kuzuia rehema yake\" isinifikie? Watasema: Hao hawawezi kuyaondoa madhara na wala hawawezi kuizuilia rehema yake. Basi waambie baada ya kwamba wameshabainikiwa na hoja ya kukata kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayepasa kuabudiwa, na kwamba Yeye ndiye aliyeumba viumbe wote, Mwenye kunufaisha, kudhuru, na kwamba wasiokuwa Yeye hawawezi kwa namna yoyote ile kuumba wala kunufaisha wala kudhuru, ukiwaonyesha kwamba Yeye atakutosheleza na atakuzuia mbali na vitimbi vyao na njama zao. \"Sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Kwake Yeye na wategemee wanaotegemea\" katika kuwaletea manufaa na kuwakinga mbali na madhara. Kwani Yule mbaye pekee ndiye mwenye uwezo wa kutosheleza, Yeye ndiye atakayenitosheleza dhidi ya kila ninalolijali na nisilolijali."},{"id":5028,"sura":39,"from_aya":39,"to_aya":40,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"39. Sema: Enyi watu wangu! Fanyeni muwezavyo, mimi pia nafanya. Basi mtakuja ona. 40. Ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi na itakayemshukia adhabu ya daima. "},{"id":5029,"sura":39,"from_aya":39,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39 - 40} Yaani, \"Sema\" ukiwaambia ewe Mtume: \"Enyi watu wangu! Fanyeni muwezavyo\" kwa kusalia katika hali zenu mlizoziridhia nafsi zenu za kumuabudu, asiyestahiki ibada yoyote wala hana mamlaka yoyote katika hilo. \"Mimi pia nafanya\" kwa mujibu wa yale niliyokuitieni ya kukusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika dini. \"Basi mtakuja ona\" ni nani atakayekuwa na mwisho mwema, \"na ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi\" katika dunia hii \"na itakayemshukia adhabu ya daima\" ambayo haitawahi kuondoka wala kwisha. Hili ni tishio kubwa kwao, kwani wanajua vyema kwamba wao ndio wanaostahiki adhabu ya milele, lakini dhuluma na ukaidi vikawazuia kuamini."},{"id":5030,"sura":39,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"41. Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa Haki. Kwa hivyo, mwenye kuongoka, ni kwa faida ya nafsi yake. Na mwenye kupotoka, bila ya shaka amepotoka kwa hasara yake. Na wewe si mlinzi juu yao."},{"id":5031,"sura":39,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuwa amemteremshia Mtume wake Kitabu ambacho kina haki katika habari zake, amri zake na makatazo yake, ambacho ndicho kiini cha uwongofu na cha kumfikisha anayetaka kufika kwa Mwenyezi Mungu na katika nyumba ya utukufu wake, na kwamba ushahidi ulisimama kwacho juu ya walimwengu. \"Kwa hivyo, mwenye kuongoka\" kwa nuru yake na akafuata maamrisho yake, basi manufaa ya hayo yanamrudia yeye mwenyewe. \"Na mwenye kupotoka\" baada ya kubainikiwa na uwongofu, \"bila ya shaka amepotoka kwa hasara yake\" wala hamdhuru Mwenyezi Mungu hata kidogo. \"Na wewe si mlinzi juu yao\" wa kuwahifadhia matendo yao, kuwahesabu na kuwalazimisha kufanya utakalo. Badala yake, wewe ni mfikishaji tu unayewafikishia yale uliyoamrishwa."},{"id":5032,"sura":39,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"42. Mwenyezi Mungu huzipokea roho zinapokufa. Na zile zisizokufa wakati wa kulala kwake, huzishika zilizohukumiwa kufa, na huzirudisha nyingine mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri."},{"id":5033,"sura":39,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba Yeye peke yake ndiye anayewaendesha waja wake katika hali zao za kuwa macho na wanapokuwa usingizini, na katika hali zao za uhai na kifo. Akasema: \"Mwenyezi Mungu huzipokea roho zinapokufa\" kifo kikubwa kabisa, kifo cha mauti. Kujulisha kwake kuwa Yeye ndiye huchukua roho, na kwamba Yeye ndiye hufanya hivyo, hakupingani na uhakika kuwa ameweka Malaika wa mauti na wasaidizi wake kufanya hivyo. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: \"Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa juu yenu.\" Pia akasema: \"Mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha, nao hawafanyi kupuuza chochote.\" Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hujifungamanishia vitu kwa kuzingatia kuwa Yeye ndiye Muumbaji na Mwendeshaji mambo, na pia huvifungamanisha na visababu vyake kwa kuzingatia kwamba ni katika ada yake na hekima yake kwamba aliliwekea kila jambo visababu vyake. Na kauli yake: \"Na zile zisizokufa\" kifo kidogo \"wakati wa kulala kwake,\" yaani, anaikamata nafsi ambayo haikufa katika usingizi wake. Lakini \"huzishika zilizohukumiwa kufa\" kati ya nafsi hizi zote, ambazo ni nafsi za wale waliokufa au za wale walioandikiwa kufia kwenye usingizi. \"Na huzirudisha nyingine mpaka ufike wakati uliowekwa.\" \"Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri\" juu ya ukamilifu wa uwezo wake na kuwafufua wafu baada ya kufa kwao. Katika aya hii, kuna ushahidi kwamba roho na nafsi ni mwili ambao unajisimamia kivyake wala hazifanani na mwili, na kwamba zimeumbwa na zinaendeshwa na Mwenyezi Mungu kwa kuzifisha, kuzishikilia, kuziachilia, na kwamba roho za walio hai na wafu zinakutana kaburini kuzungumza, kisha Mwenyezi Mungu anaziachilia roho za waliohai na kuzishikilia roho za wafu."},{"id":5034,"sura":39,"from_aya":43,"to_aya":44,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"43. Au ndio wanachukua waombezi badala ya Mwenyezi Mungu? Sema: Ingawa hawana mamlaka juu ya kitu chochote, wala hawatambui lolote. 44. Sema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa kwake. "},{"id":5035,"sura":39,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapinga wale wanaowafanya waombezi badala yake, wakawa wanajifungamanisha nao, na kuwaomba na kuwaabudu. \"Sema\" ukiwabainishia ujinga wa hivyo wanavyoviabudu na kwamba havistahiki ibada yoyote. \"Ingawa hawana mamlaka juu ya kitu chochote,\" si hata uzito wa chembe mbinguni wala ardhini, wala kidogo zaidi yake, wala kikubwa kuliko hivyo. Hata hawana akili wanayostahiki kusifiwa kwayo, kwa sababu ni vitu visivyo na uhai, kama vile mawe, miti, picha na watu waliokufa. Je, inaweza semwa kwamba anayevichukua akaviabudu ana akili, au yeye ndiye aliyepotea zaidi ya wote, mjinga na dhalimu zaidi yao wote?"},{"id":5036,"sura":39,"from_aya":44,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{44} \"Sema\" ukiwaambia \"Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu,\" kwa sababu mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu na kila muombezi anamhofu, na wala hakuna anayeweza kufanya uombezi kwake isipokuwa kwa idhini yake. Akitaka kumrehemu mja wake anamruhusu mwombezi mtukufu kwake amfanyie uombezi kwa sababu ya kuwarehemu wote wawili. Kisha akathibitisha kwamba uombezi wote ni wake, kwa kauli yake: \"Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi\" pamoja na vyote vilivyomo [ndani yake] kama vile dhati mbalimbali, vitendo na sifa. Basi la lazima ni kuomba uombezi kutoka kwa Yule anayeumiliki na kumfanyia Yeye peke yake ibada. \"Kisha mtarejeshwa kwake.\" Naye atamlipa mwenye kumkusudia Yeye tu ujira mkubwa, na amlipe anayemshirikisha kwa adhabu kali."},{"id":5037,"sura":39,"from_aya":45,"to_aya":46,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"45. Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake, nyoyo za wasioiamini Akhera huchafuka. Na wanapotajwa wenginewe wasiokuwa Yeye, basi wao hufurahi. 46. Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba mbingu na ardhi! Mjuzi wa yasiyoonekana na yanayoonekana! Wewe utahukumu baina ya waja wako katika yale waliyokuwa wakihitalifiana. "},{"id":5038,"sura":39,"from_aya":45,"to_aya":46,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{45 - 46} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja hali ya washirikina na yale uliyoyalazimu ushirikina wao huo, kwamba \"anapotajwa Mwenyezi Mungu\" kwa kuamrisha kwamba apwekeshwe na kumkusudia Yeye tu katika dini, kuacha vyote vinavyoabudiwa badala yake; wao wanachafuka roho, wanajitenga na wanalichukia hilo kwa chuki kubwa zaidi. \"Na wanapotajwa wenginewe wasiokuwa Yeye,\" kama vile masanamu na wenza, na mwitaji akawaita wayaabudu na kuyahimidi \"basi wao hufurahi\" kwa sababu wametajiwa hao ambao wanaabudu, na kwa sababu shirki inaafikiana na matamanio yao. Hali hii ndiyo hali ovu na mbaya zaidi, lakini miadi yao ni Siku ya Malipo. Hapo, haki itachukuliwa kutoka kwao na itaangaliwa: Je, miungu yao hiyo waliyokuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu itawafaa kitu?  Ndiyo maana akasema: \"Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba mbingu na ardhi\" na mwendeshaji wake, \"Mjuzi wa yasiyoonekana,\" ambayo yamefichikana machoni petu na hata hatuyajui, \"na yanayoonekana! Wewe utahukumu baina ya waja wako katika yale waliyokuwa wakihitalifiana.\" Na hakika katika kuhitilafiana kukubwa zaidi ni kuhitilafiana kati ya wale wanaompwekesha Mwenyezi Mungu kwa kumkusudia Yeye tu,wale wasemao: Waliyo juu yake ndiyo haki na kwamba watapata mazuri zaidi Akhera mbali na wengineo, na washirikina waliokufanyia wenza na vitu vya kuabudu, wakakufanya sawa na wale walio duni,wasiotoshana na chochote, wakakupunguzia hadhi zaidi na wakafurahi wanapotajwa miungu yao, na wakachafuka unapotajwa Wewe, na wakadai pamoja na hayo kwamba wao wako kwenye haki na kwamba wengineo wako katika batili, na kwamba watapata mazuri zaidi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Hakika wale walioamini na wale ambao ni Mayahudi, Wasabai, Wakristo, Majusi na wale waliomshirikisha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atawapambanua baina yao Siku ya Kiyama. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu.\" Alitujulisha kwamba atapambanua kati yao baada yake, akasema: \"Hawa ni wagomvi wawili waliogombana kwa ajili ya Mola wao Mlezi. Basi wale waliokufuru watakatiwa nguo za moto na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yanayochemka. Kwa maji hayo vitayeyushwa vilivyomo matumboni mwao na ngozi zao pia. Na kwa ajili yao yatakuwepo marungu ya chuma.\" Mpaka aliposema: \"Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema katika Bustani zipitiwazo na mito kati yake. Watapambwa humo kwa mapambo ya mikononi ya dhahabu na lulu. Na mavazi yao humo ni hariri.\" Na amesema Mtukufu: \"Wale ambao wameamini na hawakuchanganya imani yao na dhuluma - hao ndio watakaopata amani na wao ndio walioongoka.\" Na akasema: \"Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahala pake ni Motoni.\" Katika aya hii, kuna maelezo ya ujumla wa kuumba kwa Mwenyezi, ujumla wa elimu yake na ujumla wa hukumu yake kati ya waja wake. Uweza wake ndio ambao viumbe wanatokana nao. Nayo elimu yake inayokizunguka kila kitu inaashiria kwamba atahukumu baina ya waja wake na kuwafufua, na kwamba anajua matendo yao, mema na mabaya, na kiasi cha malipo yao. Nako kuumba kwake kunaonyesha kwamba anajua yote. Kwani hawezi jua aliyeumba?"},{"id":5039,"sura":39,"from_aya":47,"to_aya":48,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"47. Na lau kuwa wale waliodhulumu wangelikuwa na vyote vilivyomo duniani na pamoja navyo vingine kama hivyo, bila ya shaka wangelivitoa kujikomboa kutokana na adhabu mbaya hiyo Siku ya Kiyama. Na yatawadhihirikia kwa Mwenyezi Mungu wasiyokuwa wakiyatarajia. 48. Na utawadhihirikia ubaya wa yale waliyoyachuma, na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha. "},{"id":5040,"sura":39,"from_aya":47,"to_aya":47,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{47} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuwa Yeye ndiye atakayehukumu kati ya waja wake, na akataja maneno waliyosema washirikina na ubaya wake, ni kana kwamba nafsi zikatazamia yale ambayo Mwenyezi Mungu atawafanyia Siku ya Kiyama, basi akajulisha kuwa watapata \"adhabu\" mbaya; kama walivyosema ukafiri mkubwa na mbaya zaidi. Na hata kama ingechukuliwa kwamba ni vya vyote vilivyo katika ardhi ikijumuisha dhahabu yake, fedha yake, lulu yake, wanyama wake, miti yake, mazao yake na vyombo vyake vyote na mfano wake pamoja navyo, kisha wakavitoa \"Siku ya Kiyama\" ili wajikomboe kwavyo kutokana na adhabu na kuepushwa nayo, haingekubaliwa kwao.Na hakuna chochote kingewafaa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, Siku ambayo haitafaa mali wala watoto isipokuwa atakayemjia Mwenyezi Mungu na moyo safi. \"Na yatawadhihirikia kwa Mwenyezi Mungu wasiyokuwa wakiyatarajia,\" ya ghadhabu na chuki kubwa, ilhali walikuwa wakijihukumia wenyewe vinginevyo."},{"id":5041,"sura":39,"from_aya":48,"to_aya":48,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{48} \"Na utawadhihirikia ubaya wa yale waliyoyachuma. Na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha,\" ya vitisho na adhabu iliyowafikia."},{"id":5042,"sura":39,"from_aya":49,"to_aya":52,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"49. Na dhara inapomgusa mtu, hutuomba. Kisha tunapompa neema zitokazo kwetu, husema: Nimepewa haya kwa sababu ya elimu yangu. Sivyo! Huo ni mtihani! Lakini wengi wao hawajui! 50. Waliyasema haya wale waliokuwa kabla yao, lakini hayakuwafaa waliyokuwa wakiyachuma. 51. Basi ukawasibu uovu wa yale waliyoyachuma. Na wale waliodhulumu miongoni mwa hawa utawasibu uovu wa yale waliyoyachuma vile vile. Nao si wenye kushinda. 52. Kwani wao hawajui kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na akamkadiria? Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaoamini. "},{"id":5043,"sura":39,"from_aya":49,"to_aya":49,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{49} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu hali na maumbile ya asili ya mwanadamu kwamba yanapompata madhara, kama vile maradhi, ugumu au dhiki, \"hutuomba\" akikakamia tumpe afueni kutokana na yale yaliyompata. \"Kisha tunapompa neema zitokazo kwetu\" kwa kumwondolea madhara na ugumu wake, akarejea kwa Mola wake Mlezi akiwa ni kafiri na akakanusha neema yake, na \"husema: Nimepewa haya kwa sababu ya elimu\" ya Mwenyezi Mungu kwamba mimi ninaistahiki kwa sababu mimi ni mtukufu kwake. Au kwa sababu ya elimu ninayo ya kuichuma. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: \"Sivyo! Huo ni mtihani\" ambao Mwenyezi Mungu huwajaribu kwao waja wake ili aone ni nani atakayemshukuru na ni nani atakayemkufuru. \"Lakini wengi wao hawajui!\" Ndiyo maana wanachukulia kuwa mitihani hiyo zawadi, na hawaitofautishi heri tupu mbali na kitu kinachoweza kuwa sababu ya heri au uovu."},{"id":5044,"sura":39,"from_aya":50,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{50} Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: \"Waliyasema haya wale waliokuwa kabla yao\", yaani kauli yao: \"Nimepewa haya kwa sababu ya elimu.\" Basi kauli hii ikaendelea kurithiwa miongoni mwa wale wanaokadhibisha, wakawa hawakiri neema aliyowapa Mola wao Mlezi, na hiyo ikaendelea kuwa ada yao mpaka wakaangamia, na \"hayakuwafaa waliyokuwa wakiyachuma\" adhabu ilipowajia!"},{"id":5045,"sura":39,"from_aya":51,"to_aya":51,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{51} \"Basi ukawasibu uovu wa yale waliyoyachuma.\" Na maana ya maovu hapa ni adhabu. Kwa sababu humfanya mtu ajisikie vibaya na kuhuzunika. \"Na wale waliodhulumu miongoni mwa hawa, utawasibu uovu wa yale waliyoyachuma vile vile.\" Kwa sababu hao si bora kuliko wale, wala hawakuandikiwa vitabuni kuwa hawatatiwa makosani?"},{"id":5046,"sura":39,"from_aya":52,"to_aya":52,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{52} Alipotaja kuwa walidanganywa na mali zao na wakadai kwa ujinga wao kwamba mali hiyo inaashiria hali nzuri ya mwenyewe, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwajulisha kwamba riziki yake haionyeshi hilo, na kwamba \"humkunjulia riziki amtakaye\" miongoni mwa waja wake, wawe wema au wabaya. \"Na akamkadiria\" riziki amtakaye, sawa sawa awe ni mwema au muovu. Riziki yake anawapa viumbe wote, lakini Imani na matendo mema ni mahususi tu kwa viumbe wake waliobora. \"Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaoamini\" na kujua kwamba ukunjufu wa riziki na kukunjwa kwake kunatokana na hekima na rehema ya Mwenyezi Mungu, na kwamba Yeye ndiye anayejua zaidi hali za waja wake. Kwani anaweza kuwakunjia riziki ili kuwafanyia upole; kwa sababu ikiwa angeipanua, wangepitiliza mipaka katika ardhi. Basi kwa kufanya hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawa amezingatia kutengenea kwa dini yao, ambayo ndiyo kiini cha furaha yao na mafanikio yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi."},{"id":5047,"sura":39,"from_aya":53,"to_aya":59,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"53. Sema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 54. Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake, kabla ya kuwajieni adhabu. Kisha hapo hamtanusuriwa. 55. Na fuateni yaliyo bora kabisa katika yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, kabla haijakujieni adhabu kwa ghafla, na hali hamtambui. 56. Isije ikasema nafsi: Ee majuto yangu kwa yale niliyopoteza upande wa Mwenyezi Mungu, na hakika nilikuwa miongoni mwa wanaofanya maskhara! 57. Au ikasema: Ingelikuwa Mwenyezi Mungu ameniongoa, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa wenye kumcha Mungu. 58. Au ikasema inapoona adhabu: Lau kuwa ningelipata fursa nyingine, ningelikuwa miongoni mwa wafanya mema. 59. Wapi! Bila ya shaka zilikujia Ishara zangu, nawe ukazikadhibisha, na ukajivuna, na ukawa miongoni mwa makafiri! "},{"id":5048,"sura":39,"from_aya":53,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{53} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawafahamisha waja wake waliopindukia mipaka juu ya ukubwa wa ukarimu wake, na anawataka watubie kabla ya kufikia hali ambayo hawataweza tena kufanya hivyo. Akasema: \"Sema\" ewe Mtume, na atakayeshika nafasi yako miongoni mwa wale wanaolingania Dini ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwapa habari waja juu ya Mola wao Mlezi: \"Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao\" kwa kufuata madhambi ambayo nafsi zao zinawaitia na kuwania katika mambo yanayomghadhibisha Mjuzi wa ghaibu zote, \"Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu\" mkajitia kwa mikono yenu katika maangamizo, na mkasema: Dhambi zetu zimekuwa nyingi na kasoro zetu zimeongezeka. Hakuna njia ya kuziondoa na wala hakuna njia ya kujiweka mbali nazo, na kwa sababu hiyo mkaendelea kufanya uasi wenu na mambo ya kumfanya Mwingi wa rehema kuwakasirikia. Lakini mjueni Mola wenu Mlezi kwa majina yake yanayoashiria ukarimu wake na kupeana kwake kwa wingi, na jueni kwamba Yeye anasamehe dhambi zote kama vile ushirikina, kuua, uzinzi, riba, dhuluma na madhambi mengineyo makubwa na madogo. \"Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.\" Yaani, hizi ndizo sifa zake za milele na kamwe haziachani naye. Athari zake zinaendelea kupatikana, zikijaza vilivyopo kwa heri usiku na mchana, na Yeye hutoa neema na fadhila kwa waja kwa siri na hadharani. Anapenda kutoa zaidi ya kuliko kuzuilia, na rehema yake ilitangulia na kushinda hasira yake."},{"id":5049,"sura":39,"from_aya":54,"to_aya":54,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{54} Lakini kuna sababu za kupata msamaha wake na rehema yake. Ikiwa mja hatazifanya, basi atakuwa amejifungia mlango mkuu na mtukufu zaidi wa rehema na msamaha wake, ambao hakuna sababu yoyote isipokuwa hiyo - yaani, kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa toba ya kweli, kumuomba dua, kunyenyekea, kumfanyia uungu na kumuabudu Yeye tu. Basi njooni kwenye sababu hii tukufu na njia hii kuu zaidi. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akaamrisha kuharakisha kurejea kwake, akisema: \"Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi\" kwa nyoyo zenu, \"na silimuni kwake.\" Na katika kauli yake: \"Kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake,\" kuna ushahidi wa kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba bila ya ikhlasi matendo ya nje na ya siri hayafai kitu \"kabla ya kukujieni adhabu\" kwa njia ambayo haiwezi kuzuilika. \"Kisha hapo hamtanusuriwa.\""},{"id":5050,"sura":39,"from_aya":55,"to_aya":55,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{55} Ni kana kwamba ilisemwa: Kurejea kwake na kusilimu ni nini? Na ni yapi matendo yake mbalimbali? Mwenyezi Mungu Mtukufu akajibu kwa kusema: \"Fuateni yaliyo bora kabisa katika yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi\" miongoni mwa yale aliyowaamrisha katika matendo ya siri, kama vile kumpenda Mwenyezi Mungu, kumnyenyekea, kumhofu, kumtaraji, kuwanasihi waja wake na kuwapendea heri na kuacha yaliyo kinyume na hayo. Na miongoni mwa matendo ya dhahiri kama vile kuswali, kutoa zaka, kuhiji, kutoa sadaka, na matendo mema mengineyo miongoni mwa yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha. Na hayo ndiyo bora zaidi aliyotuteremshia Mola wetu Mlezi. Kwa hivyo, mwenye kufuatilia maamrisho ya Mola wake Mlezi katika mambo haya na mfano wa hayo ndiye aliyejisalimisha \"kabla haijakukujieni adhabu kwa ghafla na hali hamtambui.\" Yote haya ni himizo la kuharakisha kutumia fursa vyema."},{"id":5051,"sura":39,"from_aya":56,"to_aya":56,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{56} Kisha akawatahadharisha dhidi ya kuendelea kughafilika mpaka ikafika siku watakapojuta, lakini majuto hayo hayatafaa kitu, na \"nafsi ikaja kusema: Ee majuto yangu kwa yale niliyopoteza upande wa Mwenyezi Mungu.\" \"Na hakika nilikuwa\" katika dunia \"miongoni mwa wanaofanya maskhara\" juu ya kulipwa kwa matendo mpaka nikayaona kwa macho yangu."},{"id":5052,"sura":39,"from_aya":57,"to_aya":57,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{57} \"Au ikasema: Ingelikuwa Mwenyezi Mungu ameniongoa, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa wenye kumcha Mungu,\" nikasalimika kutokana na adhabu na nikastahiki malipo mazuri. Neno walilotumia hapa la kutamani, yaani \"lau,\" halikukusudiwa kutumia mipango ya Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo hoja yao juu ya upotofu wao, ambayo ni hoja batili, na Siku ya Kiyama kila hoja batili itaambulia patupu."},{"id":5053,"sura":39,"from_aya":58,"to_aya":58,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{58} \"Au ikasema inapoona adhabu\" na ikajua uhakika kwamba itatokea: \"Lau kuwa ningelipata fursa nyingine\" ya kurejea duniani, basi ningelikuwa\" miongoni mwa wafanya mema.\""},{"id":5054,"sura":39,"from_aya":59,"to_aya":59,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{59} Mungu Mwenyezi Mtukufu alisema kwamba hili haliwezekani wala halifai kitu, na kwamba haya ni matamanio batili ambayo hayana uhakika wowote; kwani mja hataelezewa upya ikiwa atarudishwa baada ya kule kuelezewa kwa kwanza: \"Wapi! Bila ya shaka zilikujia Ishara zangu\" zikionyesha haki kwa njia isiyo na shaka yoyote, \"nawe ukazikadhibisha na ukajivuna\" kuzifuata. \"Na ukawa miongoni mwa makafiri!\" Basi kuomba kurudishwa duniani ni mfano wa mchezo tu. Na kama wangelirudishwa, bila ya shaka wangeyarejea yale yale waliyokatazwa. Na hakika hao ni waongo."},{"id":5055,"sura":39,"from_aya":60,"to_aya":61,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"60. Na Siku ya Kiyama utawaona waliomsingizia uongo Mwenyezi Mungu nyuso zao zimesawijika. Je, si katika Jahannamu makazi ya wanaotakabari? 61. Na Mwenyezi Mungu atawaokoa wenye kujikinga kwa ajili ya kufuzu kwao. Hapana uovu utakaowagusa, wala hawatahuzunika. "},{"id":5056,"sura":39,"from_aya":60,"to_aya":60,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{60} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaeleza juu ya fedheha ya \"wale waliomsingizia uongo Mwenyezi Mungu \" na kwamba nyuso zao Siku ya Kiyama \"zitakuwa nyeusi\" kana kwamba ni usiku totoro. Hivyo ndivyo watakavyowajua watu watakaokuwa hapo siku hiyo. Kwani, haki ni wazi kabisa kana kwamba ni asubuhi. Kama vile walivyofanya uso wa haki kuwa mweusi kwa uongo wao; Mwenyezi Mungu akazifanya nyuso zao kuwa nyeusi kama malipo ya aina sawa na matendo yao. Kwa hivyo, watakuwa na nyuso nyeusi, na watapata adhabu kali katika Jahannamu. Ndiyo maana akasema: \"Je, si katika Jahannamu makazi ya wanaotakabari,\" wakaikataa haki na wakakataa kumuabudu Mola wao Mlezi, na wakamzulia uongo? Ndiyo, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu. Ndani yake kuna adhabu, fedheha na ghadhabu itakayowafikia wafanyao kiburi hao kila kiwango, na haki yote itachukuliwa kutoka kwao. Kusema uwongo juu ya Mwenyezi Mungu kunajumuisha kumfanyia mshirika, mtoto, mke, kusema juu yake mambo yasiyoufailia utukufu wake, au kudai unabii, au kusema katika sheria yake kitu ambacho hakukisema na kusema kuwa alikisema na akakiweka katika sheria."},{"id":5057,"sura":39,"from_aya":61,"to_aya":61,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{61} Alipotaja hali ya wenye kiburi, akataja hali ya wachamungu, akasema: \"Na Mwenyezi Mungu atawaokoa wenye kujikinga kwa ajili ya kufuzu kwao,\" na hilo ni kwa sababu wanacho chombo cha kuokoka ambacho ni ucha Mungu, ambao ndiyo maandalizi bora zaidi wakati wa kila hofu na dhiki. \"Hapana uovu utakaowagusa\" ukawawia vibaya, \"wala hawatahuzunika.\" Hapa akasema kwamba hakuna adhabu na hofu yake itakayowasibu, na hiyo ndiyo amani ya juu kabisa, ambayo itaandamana nao mpaka iwafikishe katika nyumba ya salama. Hapo, watakuwa na amani kutokana na kila ubaya na machukizo, na watakuwa na mng'aro wa neema, watasema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetuondolea huzuni zote. Hakika Mola wetu Mlezi bila ya shaka ni Mwenye kusamehe, Mwenye shukrani sana."},{"id":5058,"sura":39,"from_aya":62,"to_aya":63,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"62. Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu. 63. Yeye anazo funguo za mbingu na ardhi. Na wale waliozikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye kuhasiri. "},{"id":5059,"sura":39,"from_aya":62,"to_aya":62,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{62} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukuu wake na ukamilifu wake unaosababisha hasara kwa wale waliomkufuru. Akasema: \"Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu.\" Maneno haya na mengineyo yanayofanana na hayo ni mengi katika Qur-ani na ni katika mambo yanayoonyesha kwamba vitu vyote - isipokuwa Mwenyezi Mungu - vimeumbwa. Hili ni jawabu kwa kila mtu anayesema kwamba viumbe vingine ni vya azali, kama vile wanafalsafa wanaosema kwamba ardhi na mbingu ni za azali, na wale wanaosema kuwa roho ni za azali, na maneno mengineyo mfano wa hayo ya wana batili ambayo yanajumuisha kupinga kwamba si Mwenyezi Mungu aliyeviumba. Maneno ya Mwenyezi Mungu si katika vitu vilivyoumbwa. Kwa sababu maneno ni sifa ya yule aliyeyazungumza. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na majina yake na sifa zake, ndiye wa kwanza, na hakuna chochote kabla yake. Kwa hivyo, wana itikadi ya Muutazila walioichukua aya hii kuwa hoja juu ya suala kwamba maneno yake yameumbwa ni katika ujinga wao mkubwa zaidi. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu hajaacha kusifika kwa majina yake na sifa zake, wala hakuna sifa mpya miongoni mwa sifa zake iliyojitokeza, na wala hajawahi kutosifika kwa majina yake na sifa zake katika wakati wowote ule. Ushahidi uliopo katika hili ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alijulisha kuhusu nafsi yake Tukufu kwamba Yeye ndiye Muumba wa ulimwengu wote, wa juu na wa chini, na kwamba Yeye ndiye \"Mlinzi juu ya kila kitu.\" Na ulinzi kamili ni jambo ambalo linalazimu kwamba mlinzi huyo ana elimu kamili juu ya kile anachokilinda na kukijua kwa kina, na kwamba anao uwezo kamili juu ya kile anachokilinda; ili aweze kukisimamia kwa kukihifadhi, na pia awe na hekima na ujuzi wa kukisimamia ili aweze kukisimamia na kukiendesha inavyofaa. Kwa hivyo, ulinzi hauwezi kukamilika bila ya haya yote. Basi chochote katika hayo kinapokosekana, basi kinakuwa kimekosekana katika hilo suala nzima. Tayari ilishajulikana na kuthibiti kwamba Mwenyezi Mungu ametakasika mbali na kila upungufu katika sifa zake zote. Kwa hivyo kujulisha kwake kwamba Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu kunaonyesha kwamba anajua kikamilifu vitu vyote, na kwamba ana uwezo wa kuvisimamia na kuviendesha, na kwamba ana hekima kamili ambayo kwayo anaviweka vitu mahali pake."},{"id":5060,"sura":39,"from_aya":63,"to_aya":63,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{63} \"Yeye anazo funguo za mbingu na ardhi.\" Anazijua na anazisimamia. \"Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu hapana wa kuizuia. Na anayoizuia hapana wa kuipeleka isipokuwa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.\" Alipobainisha ukuu wake unaolazimu mioyo imtukuze kwa wingi na kumheshimu, akataja hali ya mtu aliyegeuza suala hili na hakumthamini anavyostahiki. Akasema: \"Na wale waliozikataa Ishara za Mwenyezi Mungu\" zinazoashiria haki ya yakini na njia iliyonyooka, \"hao ndio wenye kuhasiri.\" Walihasiri yale ambayo kwayo nyoyo zanatengenea, kama vile kumfanyia Mwenyezi Mungu uungu na kumkusudia Yeye peke yake, na yale ambayo kwayo ndimi zinatengenea kama vile kuzishughulisha na kumtaja Mwenyezi Mungu, na yale ambayo kwayo viungo vinatengenea kama vile kumtii Mwenyezi Mungu. Wao walibadilisha hayo na wakaweka mahali pake kila chenye kuharibu nyoyo na miili, kwa hivyo wakakosa mabustani ya mbinguni ya neema na badala yake wakapata adhabu iumizayo."},{"id":5061,"sura":39,"from_aya":64,"to_aya":66,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"64. Sema: Je, mnaniamrisha nimuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, enyi majahili? 65. Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa waliokuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu matendo yako yataharibika, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kuhasiri. 66. Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru. "},{"id":5062,"sura":39,"from_aya":64,"to_aya":64,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{64} \"Sema\" ewe Mtume ukiwaambia majahili hao waliokuita uabudu vinyinevyo badala ya Mwenyezi Mungu: \"Je, mnaniamrisha nimuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, enyi majahili?\" Yaani, jambo hili lilitokana na ujinga wenu. Vinginevyo, lau kuwa mngelikuwa mnajua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mkamilifu kwa namna zote, Mwenye kupeana neema zote, ndiye anayestahiki kuabudiwa, si wale walio wapungufu kwa namna zote, wasionufaisha wala kudhuru, basi hamngeniamuru kufanya hivyo. Kwa sababu kumshirikisha Mwenyezi Mungu kunaharibu matendo na hali."},{"id":5063,"sura":39,"from_aya":65,"to_aya":65,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{65} Ndiyo maana akasema: \"Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa waliokuwa kabla yako\" miongoni mwa Manabii wote: \"Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu matendo yako yataharibika.\" Hivi ndivyo Manabii wote waliwaambia watu wao kwamba ushirikina unaharibu matendo yote, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema katika Surat Al-An\u2019am alipowahesabu wengi katika Manabii na Mitume wake, akasema kuwahusu: \"Hiyo ni hidaya ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo humuongoa amtakaye katika waja wake. Na lau wangelimshirikisha, basi yangeliwaharibikia waliyokuwa wakiyatenda.\" Na hapa akasema: \"Na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kuhasiri\" dini yako na akhera yako. Kwa hivyo, kwa kufanya ushirikina, matendo yanabatilika na mtu huyo anastahiki adhabu na mateso."},{"id":5064,"sura":39,"from_aya":66,"to_aya":66,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{66} Kisha akasema: \"Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu.\" Aliposema kuwa watu wajinga wanamuamrisha Mtume kufanya ushirikina, na akaeleza ubaya wake, akamuamrisha akusudiwe Yeye peke yake. Akasema: \"Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu.\" Yaani msujudie Yeye peke yake kwa ibada zako, bila mshirika yeyote, \"na uwe miongoni mwa wenye kushukuru\" Mwenyezi Mungu kwa kukuwezesha kufanya hivyo. Kwani, kama vile Yeye [Mtukufu] anavyoshukuriwa kwa neema za kidunia kama vile afya ya kimwili, usalama, riziki na mengineyo, pia anashukuriwa na kusifiwa kwa neema za kidini, kama vile kumuwezesha mja kumkusudia Yeye tu na uchamungu. Bali, neema za kidini ndiyo neema halisi. Mtu anapotafakari kwamba zimetoka kwa Mwenyezi Mungu, na kumshukuru Mwenyezi Mungu juu yake, anapata usalama kutokana na ugonjwa wa majivuno ambao unawapata wengi wa watendao matendo kwa sababu ya ujunga wao. Vinginevyo, ikiwa mja angejua uhakika wa hali hiyo, hangejivuna kwa neema ambayo inastahili aongeze kushukuru kwa sababu yake."},{"id":5065,"sura":39,"from_aya":67,"to_aya":67,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"67. Na wala hawakumheshimu Mwenyezi Mungu kama anavyostahiki kuheshimiwa. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kiume. Ametakasika na Ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo."},{"id":5066,"sura":39,"from_aya":67,"to_aya":67,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{67} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Hawa washirikina hawakumthamini Mola wao Mlezi \"kama anavyostahiki kuheshimiwa\" wala hawakumtukuza kama anavyostahiki kutukuzwa, bali walifanya yale yanayopingana na hayo kwa kumshirikisha na kile ambacho ni kipungufu katika sifa zake. Ambacho sifa zake hizo ni pungufu kwa namna zote. Na matendo yake hayanufaishi wala hayadhuru, wala hatoi kitu wala hawezi kuzuia chochote, na wala hamiliki chochote katika hayo. Kwa hivyo wakamtoshanisha kiumbe huyu mpungufu na Muumba, Mola Mlezi Mtukufu, ambaye katika utukufu wake wa kushangaza na uwezo wa ushindi ni kwamba Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mshiko wake Yeye Mwingi wa rehema, na kwamba mbingu pamoja na upana wake na ukubwa wake zitakunjwa kwa mkono wake wa kiume. Kwa hivyo, hakuheshimu haki ya kumheshimu mwenye kumtoshanisha na asiyekuwa Yeye, na wala hakuna aliye dhalimu zaidi yake. \"Ametakasika na Ametukuka mbali na hayo wanayomshirikisha nayo.\""},{"id":5067,"sura":39,"from_aya":68,"to_aya":70,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"68. Na litapulizwa barugumu, wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi, isipokuwa aliyemtaka Mwenyezi Mungu. Kisha litapulizwa mara nyingine. Hapo watainuka wawe wanangojea. 69. Na ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi, na Kitabu kitawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa. 70. Na kila nafsi italipwa kwa yale iliyoyafanya, na Yeye anayajua sana wanayoyatenda. "},{"id":5068,"sura":39,"from_aya":68,"to_aya":68,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{68} Mwenyezi Mungu alipowatia hofu juu ya ukuu wake, akawahofisha kwa hali za Siku ya Kiyama, na akawatia moyo na kuwatisha, akisema: \"Na litapulizwa baragumu,\" ambayo ni pembe kubwa sana na hakuna anayejua ukubwa wake isipokuwa Yule aliyeiumba na wale ambao Mwenyezi Mungu aliwajulisha kuihusu miongoni mwa viumbe wake. Kwa hivyo, ataipuliza mmoja wa Malaika aitwaye Israfil, amani iwe juu yake, ambaye ni Malaika wa karibu na Mwenyezi Mungu na ni mmoja wa wale wanaoshikilia 'Arshi ya Mwingi wa rehema. \"Wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi.\" Walipoisikia sauti yake baragumu hiyo, ikawasumbua kwa sababu ya ukali wake na ukubwa wake, na yale wanayojua kwamba hiyo ni utangulizi wake, \"isipokuwa aliyemtaka Mwenyezi Mungu\" miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaimarisha lilipopulizwa, kwa hivyo akasalia hajazimika, kama vile waliokufa kwa ajili ya kupigania dini au baadhi yao na wengineo. Huku ndiko kupuliza kwa kwanza ambako kutawazimisha viumbe na kuwafadhaisha. \"Kisha litapulizwa mara nyingine\" ya pili ambayo nayo ni kwa ajili ya kuwafufua viumbe. \"Hapo watainuka\" watoke makaburini mwao \"wawe wanangojea\" ili wafanyiwe hesabu. Hapo watakuwa tayari wamesharudishiwa maumbile yao ya kimwili na kiroho, na macho yao yamekodoka yanangojea kuona wanafanyiwa nini na Mwenyezi Mungu?"},{"id":5069,"sura":39,"from_aya":69,"to_aya":69,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{69} \"Na ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi.\" Hili linaonyesha kwamba nuru zilizopo zitatoweka Siku ya Kiyama na kupotelea mbali. Kwa maana Mwenyezi Mungu alijulisha kwamba jua litakunjwa, mwezi utapatwa, nyota zitatawanywa, na watu watakuwa gizani. Kisha ardhi itang'aa kwa nuru ya Mola wake Mlezi atakapodhihiri na kushuka ili kuhukumu baina yao. Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawapa nguvu viumbe, na atawaumba kwa namna ya kwamba watakuwa na nguvu ya kutoweza kuunguzwa nuru yake, na pia wataweza kumuona, vinginevyo, nuru yake ni kubwa, kama angeifunua, basi nuru ya uso wake ingeunguza viumbe vyote ambacho inafikia. \"Na Kitabu\" cha matendo \"kitawekwa hapo\" na kikaendezwa ili yasomwe matendo mema na mabaya yaliyo ndani yake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyoogopa kwa yale yaliomo humo. Na watasema: Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika? Na watayakuta yote waliyoyatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.\" Na kwa sababu ya uadilifu kamili na usawa, mtendaji ataambiwa: \"Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhesabu.\" \"Na wataletwa Manabii\" ili waulizwe kama walifikisha ujumbe, na kuhusu kaumu zao, na washuhudie juu yao \"mashahidi\" kutoka kwa Malaika, viungo na ardhi. \"Na patahukumiwa baina yao kwa haki\" na uadilifu kamili na mkuu. Kwa sababu ni hesabu itokayo kwa yule asiyedhulumu hata uzito wa chembe, ambaye amekidhibiti kila kitu, ambaye Kitabu chake - ambacho ni Ubao Uliohifadhiwa - kimedhibiti yote waliyoyafanya, na waandishi watukufu wasiomuasi Mola wao Mlezi, waliandika yote ambayo viumbe waliyafanya, na mashahidi waadilifu zaidi walishuhudia hukumu hiyo. Kwa hivyo, akahukumu kulingana na hayo Yule ambaye anajua kiasi cha matendo na kiasi cha thawabu na adhabu ambazo matendo hayo yanastahiki. Basi atafanya hukumu ambayo viumbe vitaikiri, na vitamkiria Mwenyezi Mungu sifa njema na uadilifu. Kwa hukumu hiyo watatambua ukuu wake, elimu yake, hekima yake na rehema yake, mambo ambayo nyoyo zao hazijawahi kuyafikiria, na ambayo ndimi zao haziwezi kuyaelezea."},{"id":5070,"sura":39,"from_aya":70,"to_aya":70,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{70} Ndiyo maana akasema, \"Na kila nafsi italipwa kwa yale iliyoyafanya, na Yeye anayajua sana wanayoyatenda.\""},{"id":5071,"sura":39,"from_aya":71,"to_aya":75,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"71. Na wale waliokufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapoifikia, itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii? Watasema: Kwani! Lakini limekwishathibiti neno la adhabu juu ya makafiri. 72. Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Basi nayo ni ubaya ulioje wa makazi ya wanaotakabari! 73. Na wale waliomcha Mola wao Mlezi wataongozwa kuendea Peponi kwa makundi, mpaka watakapofikia, nayo milango yake imekwisha funguliwa. Walinzi wake watawaambia: Amani iwe juu yenu! Mmetahirika. Basi ingieni humu mkae milele. 74. Nao watasema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao! 75. Na utawaona Malaika wakizunguka pembeni mwa Kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, wakimtakasa na kumsifu Mola wao Mlezi. Na patahukumiwa baina yao kwa haki na patasemwa: Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote! "},{"id":5072,"sura":39,"from_aya":71,"to_aya":71,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{71} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kwamba atahukumu kati waja wake aliowakutanisha katika uumbaji wake, riziki yake, usimamizi wake na katika mkusanyiko wao mahali ambapo viumbe watasimama Siku ya Kiyama, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawatenganisha katika malipo yao, kama walivyotengana dunia kwa imani, ukafiri, uchamungu na uovu wao. Akasema: \"Na wale waliokufuru wataongozwa kuiendea Jahannamu\" huku wakipigwa mijeledi michungu na Malaika wakali hadi kwenye jela mbaya zaidi na sehemu ya kutisha sana, ambayo ni Jahannamu, ambayo imekusanya kila adhabu, taabu na haina raha yoyote. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: \"Siku watakaposukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu\" kwa watakuwa wamekataa kuingia humo, kwa hivyo wataswagwa kwenda humo \"kwa makundi\" Kila kundi litaingia na kundi linalofanana nalo katika matendo yake na juhudi zake. Hapo watalaaniana wao kwa wao na watatengana wao kwa wao, \"mpaka watakapoifikia itafunguliwa milango yake\" watakapoifikia \"na walinzi wake watawaambia\" wakiwabashiria taabu na adhabu ya milele na yao wakiwakaripia kwa sababu walifanya matendo yaliyowafikisha mahali hapa pabaya \"Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu\" mliowajua na mkajua ukweli wao na mkaweza kujifunza kutoka kwao \"wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi\" ambazo Mwenyezi Mungu aliwatuma nazo, zikibainisha haki ya yakini kwa hoja zilizo wazi zaidi, \"na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii?\" Yaani, haya yaliwalazimu nyinyi kuwafuata na kujihadhari na adhabu ya siku hii kwa kumcha Mungu. Lakini hali yenu ilikuwa tofauti na hali hii. \"Watasema\" wakikiri dhambi zao na kwamba hoja ya Mwenyezi Mungu ilithibiti juu yao. \"Kwani!\" Mitume wa Mola wetu Mlezi walitujia na Ishara zake na hoja zake zilizo wazi, na wakatubainishia kubainisha kukubwa zaidi, na wakatutahadharisha kutokana na siku hii. \"Lakini limekwishathibiti neno la adhabu juu ya makafiri.\" Nalo litathibiti kwa kila aliyezikufuru Aya za Mwenyezi Mungu na akakapinga yale waliyoyaleta Mitume. Basi wakakiri dhambi zao na ikathibitika hoja juu yao."},{"id":5073,"sura":39,"from_aya":72,"to_aya":72,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{72} Kisha wakaambiwa kwa njia ya kudunishwa na kudhalilishwa: \"Ingieni milango ya Jahannamu.\" Kila kundi litaingia kupitia mlango unaowafaa na unaoafikiana na matendo yao, \"mdumu humo\" milele. Hawataondoka humo wala hawatapumzishwa kutokana na adhabu hata saa moja. \"Basi nayo ni mabaya yaliyoje makazi ya wanaotakabari,\" kwa sababu waliifanyia haki kiburi, basi Mwenyezi Mungu akawalipa kwa aina sawa na matendi yao kuwa kuwadunisha, kuwadhalilisha na kuwafedhehesha."},{"id":5074,"sura":39,"from_aya":73,"to_aya":73,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{73} Kisha akasema kuhusu watu wa Peponi: \"Na wale waliomcha Mola wao Mlezi\" kwa kumpwekesha na kumtii, \"wataongozwa\" kwa njia ya heshima, utukufu kama wageni huku wamepanda vipando bora zaidi \"kwenda Pepo kwa makundi\" kwa furaha na kushangilia. Kila kundi litakuwa pamoja na kundi linaloafikiana nalo katika matendo yake na kufanana nalo. \"Mpaka watakapofika\" kwenye maeneo hayo mapana na majumba mazuri, na upepo wake ukawapuliza, na wakati wa umilele wake na furaha yake ukafika, \"nayo milango yake imekwisha funguliwa\" kwa ajili yao ili kuwatukuza viumbe watukufu. \"Walinzi wake watawaambia\" wakiwapongeza na kuwakaribisha: \"Amani iwe juu yenu,\" kutokana na kila taabu, ovu na hali yoyote mbaya. \"Mmetahirika\" nyoyo zenu kwa kumjua Mwenyezi Mungu, kumpenda na kumcha. Na pia ndimi zenu zimetahirika kwa kumtaja Yeye. Na pia viungo vyenu vimetahirika kwa kumtii. \"Basi\" kwa sababu ya kutahirika kwenu \"ingieni humu mkae milele\" kwa sababu ndiyo ni nyumba safi, na wala hawaifailii isipokuwa walio safi. Na akasema kuhusiana na Jahannamu: \"Itafunguliwa milango yake\" na akasema kuhusiana na Pepo \"nayo milango yake imekwisha funguliwa.\" Hili linaashiria kwamba watu wa Motoni, mara watakapoifikia, milango yake itafunguliwa bila ya kungojewa wala kupewa muhula, na ili adhabu yake na joto lake liwe kubwa zaidi kwao inapofunguliwa mbele ya nyuso zao pindi watakapoifikia. Ama Pepo, hayo ni makazi ya juu na ya thamani kubwa, ambayo hayawezi kufikiwa isipokuwa wale ambao walifanya visababu vya kuyafikia. Na pamoja na hayo, ili kuingia humo, watahitaji uombezi wa mbora wa waombezi. Kwa hivyo, haikufunguliwa pindi walipoifikia, bali wataomba uombezi kwa Mwenyezi Mungu kupitia Muhammad \u2013 rehema na amani ziwe juu yake, naye atafanya uombezi huo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ataukubali. Katika Aya hii kuna ushahidi kwamba Jahannam na Pepo zina milango inayofunguka na kufungwa, na kwamba kila moja yake ina walinzi. Nayo ni makazi ambayo ni wale wanaoyastahiki tu wataingia humo."},{"id":5075,"sura":39,"from_aya":74,"to_aya":74,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{74} \"Nao watasema\" watakapoingia na kutulia humo, wakimhimidi Mola wao Mlezi kwa yale aliyowaneemesha na aliyo na kuwaongoa: \"Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetutimizia ahadi yake\" ambayo ni Pepo kupitia ndimi za Mitume wake. Basi tukaamini na tukatengenea, naye akatutimizia yale aliyotuahidi \"na akaturithisha ardhi\" ya Peponi \"tunakaa katika Bustani popote tupendapo.\" Yaani, tunaweza kwenda humo popote tunapotaka, na tunaweza kufurahia humo neema yoyote tunayoitaka, na hakuna kinachoweza kutuzuia tunachokitaka. \"Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao!\" Wale waliofanya bidii katika kumtii Mola wao Mlezi katika muda mfupi wenye mwisho, kwa hivyo wakapata kwa sababu ya hilo heri kubwa yenye kudumu na kuendelea. Haya ndiyo makazi yanayostahiki kusifiwa kwa uhakika, ambayo hapo Mwenyezi Mungu atawatukuza viumbe wake maalumu, naye ambaye ni Mwenye kutoa kwa wingi akaridhia kwamba yawe mashukio yao. Alijenga sehemu ya juu yake, akaifanya kuwa nzuri zaidi, akaipanda kwa mkono wake, na akaijaza kwa rehema yake utukufu wake, kiasi kwamba mtu mwenye huzuni anafurahia kwa baadhi yake tu, dhiki yake inamtoka na utulivu unakamilika."},{"id":5076,"sura":39,"from_aya":75,"to_aya":75,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{75} \"Na utawaona Malaika\" ewe mwenye kuona, siku hiyo kuu \"wakizunguka pembeni mwa Kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu\" wakimtumikia Mola wao Mlezi huku wamenyenyekea kwa sababu ya utukufu wake, wakikiri ukamilifu wake, \"wakimtakasa na kumsifu Mola wao Mlezi\" kutokana na yote yasiyoufailia utukufu wake, miongoni mwa yale ambayo washirikina walimnasibisha nayo na yale ambayo hawakumnasibisha nayo. \"Na patahukumiwa baina yao\" yaani, baina ya viumbe wa mwanzo na wa mwisho \"kwa haki\" isiyo na shaka yoyote wala hataweza kuikataa yule anayelazimika kuilipa, \"Na patasemwa: Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote!\" Hapa haikusemwa ni nani aliyeyasema hayo, ili hilo liashirie kwamba viumbe vyote vitazungumza kwa kumhimidi Mola wao Mlezi na hekima yake kwa yale aliyowahukumia watu wa Peponi na watu wa Motoni, na himdi ya fadhila zake na ukarimu wake, na himdi ya uadilifu wake na hekima yake."},{"id":5077,"sura":39,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya Surat Az-Zumar kwa sifa na msaada wa Mwenyezi Mungu."},{"id":5078,"sura":39,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}