{"result":[{"id":5079,"sura":40,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Al-Mu'min"},{"id":5080,"sura":40,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":5081,"sura":40,"from_aya":1,"to_aya":3,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Ha, Mim. 2. Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye kujua vyema. 3. Anayesamehe dhambi na anayepokea toba, Mkali wa kuadhibu, Mwenye ukarimu, hakuna mungu ila Yeye; marejeo ni kwake. "},{"id":5082,"sura":40,"from_aya":1,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1 - 3} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu Kitabu chake Kikuu na kwamba kilianzia na kiliteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye anafanyiwa uungu, anayeabudiwa kwa sababu ya ukamilifu wake na upekee wake katika vitendo vyake. \"Mwenye nguvu\" ambaye kwa nguvu zake alikishinda kila kiumbe. \"Ajuaye zaidi\" kila kitu, \"Anayesamehe dhambi\" za wafanyao madhambi \"na anayepokea toba\" za wale wanaotubu, \"Mkali wa kuadhibu\" wale wanaothubutu kufanya dhambi na hawakutubu. \"Mwenye ukarimu\" juu ya walimwengu wote. Alipothibitisha yale aliyothibitisha kuhusu ukamilifu wake, na hilo likamlazimu kwamba Yeye pekee ndiye anayepasa kufanyiwa uungu ambaye anakusudiwa peke yake na matendo, akasema: \"Hakuna mungu ila Yeye; marejeo ni kwake.\" Hapa, uhusiano ulipo kwa kutaja kwamba Qur-ani iliteremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye anasifika kwa sifa hizi ni kwamba sifa hizi zinalazimu kuwepo kwa maana zote zilizomo ndani ya Qur-ani. Kwa maana Qur-ani ima inajulisha kuhusu majina ya Mwenyezi Mungu, sifa zake na vitendo vyake, na haya ni majina, sifa na vitendo. Au ni kujulisha kuhusu ghaibu zilizopita na zijazo, na hayo ni katika mambo ambayo Yule ajuaye zaidi anawafunza waja wake. Au ni kujulisha kuhusu neema zake kubwa, na amri zinazofikisha katika hayo. Hayo yanaonyeshwa na kauli yake: \"Mwenye ukarimu.\" Au ni kujulisha kuhusu adhabu zake kali na maasi yanayozisababisha na kuzilazimu. Haya yanaashiriwa na kauli yake: \"Mkali wa kuadhibu\" Au ni wito kwa wenye dhambi kutubu, kurudi kwake na kutafuta msamaha. Haya yanaashiriwa na kauli yake: \"Anayesamehe dhambi na anayepokea toba, Mkali wa kuadhibu\" Au ni kujulisha kwamba Yeye peke yake ndiye anayepasa kufanyiwa uungu na kuabudiwa, na kusimamisha ushahidi wa kiakili na wa kimaandiko juu ya hayo, na kuhimiza juu yake, kukataza na kuabudu kitu chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha ushahidi wa kiakili na wa kimaandiko juu ya ubovu wake, na kutishia dhidi yake. Haya yanaashiriwa na kauli yake Mola Mtukufu: \"Hakuna mungu ila Yeye.\" Au ni kujulisha kuhusu hukumu yake ya uadilifu na malipo ya wafanyao wema, na adhabu ya wafanyao maasia. Haya yanaashiriwa na kauli yake: \"marejeo ni kwake.\" Haya yote ndiyo mambo ambayo Qur-ani inajumuisha miongoni mwa matakwa ya juu."},{"id":5083,"sura":40,"from_aya":4,"to_aya":6,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"4. Hawazibishi Ishara za Mwenyezi Mungu ila wale waliokufuru; basi kusikughuri wewe kutangatanga kwao katika nchi. 5. Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na makundi mengine baada yao. Na kila taifa lilikuwa na hamu juu ya Mtume wao wamkamate. Na walibishana kwa upotovu ili kuipindua haki. Kwa hivyo niliwakamata. Basi ilikuwaje adhabu yangu! 6. Namna hivi limewathibitikia makafiri neno la Mola wako Mlezi ya kwamba wao ni watu wa Motoni. "},{"id":5084,"sura":40,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba hakuna anayebishana juu ya Aya zake isipokuwa wale waliokufuru, na kinachokusudiwa kubishana hapa ni kubishana ili kuzikanusha Aya za Mwenyezi Mungu na kuzipambanisha na batili. Hayo ni matendo ya makafiri. Ama Waumini, wao wanajisalimisha kwenye haki ili kuipindua batili kwayo. Na wala mtu asidanganywe na hali ya kidunia ya mtu na akafikiri kuwa Mwenyezi Mungu akimpa katika dunia hii ati ni ishara ya kwamba anampenda na kwamba yuko kwenye haki. Ndiyo maana akasema: \"Basi kusikughuri wewe kutangatanga kwao katika nchi\" wakifanya aina mbalimbali za biashara na kuchuma vitu mbalimbali. Bali la wajibu kwa mja ni kwamba awazingatie watu kwa mujibu wa haki na aangalie mambo ya kihakika ya kisheria na awapime watu kwa hayo, na asiipime haki kwa watu kama anavyofanya mtu ambaye hajui wala hata hana akili."},{"id":5085,"sura":40,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} Kisha akawatishia wale wanaojadili Aya za Mwenyezi Mungu ili wazibatilishe, kama walivyofanya wale waliokuwa kabla yao miongoni mwa kaumu mbalimbali kama vile \"kaumu ya Nuhu\" na 'Adi \"na makundi mengine baada yao\" ambayo yalijipanga makundi na wakakusanyika dhidi ya haki ili waipindue na wakakusanyika juu ya batili ili waiunge mkono. \"Na\" kwamba hali yao hiyo na makundi yao hayo yaliwafikisha kiwango kwamba \"kila taifa lilikuwa na hamu juu ya Mtume wao wamkamate\" na wamuue. Hili ndilo jambo la kubwa zaidi wanaloweza kuwafanyia Mitume, ambao ndio viongozi wa watu wema, ambao wako katika haki safi, isiyo na shaka yoyote wala utata. Basi je, kuna chochote baada ya uasi huu, upotofu huu, kuwa mashakani huku isipokuwa adhabu kubwa ambayo hawataepukana nayo? Ndiyo sababu akasema katika adhabu yao ya kidunia na ya kiakhera: \"Kwa hivyo niliwakamata\" kwa sababu ya kukadhibisha kwao na kujiweka kwao makundi. \"Basi ilikuwaje adhabu yangu!\" Ilikuwa adhabu kali na mbaya zaidi. Haikuwa isipokuwa ukelele mmoja tu au kushukiwa na tufani ya changarawe au kuiamuru ardhi ikawadidimiza kuzamishwa baharini, basi wakawa wamezimika."},{"id":5086,"sura":40,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} \"Namna hivi limewathibitikia makafiri neno la Mola wako Mlezi\" kwa sababu ya upotevu wao, na ndiyo maana akasema, \"hakika wao ni watu wa Motoni.\""},{"id":5087,"sura":40,"from_aya":7,"to_aya":9,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"7. Wale wanaobeba 'Arshi, na wale walio pembezoni mwake, wanamsabihi na kumhimidi Mola wao Mlezi, na wanamuamini, na wanawaombea msamaha walioamini kwa kusema: Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe wale waliotubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahanamu. 8. Mola wetu Mlezi! Na waingize katika Bustani za Milele ulizowaahidi. Na uwape haya pia wale waliofanya mema miongoni mwa wazee wao na wake zao na dhuriya zao. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 9. Na waepushe na maovu; kwani umwepushaye maovu siku hiyo, hakika umemrehemu; na huko ndiko kufuzu kukubwa. "},{"id":5088,"sura":40,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya upole wake kamilifu kwa waja wake waumini na sababu za furaha yao ambazo aliwawekea, si wao wanazozitenda, kama vile kuombewa msamaha na malaika walio karibu naye na kuwaombea dua ili watengenee katika dini yao na akhera yao. Hili linajumuisha pia kujulisha kuhusu utukufu wa malaika wabebao kiti chake cha Enzi na wale walio pembezoni mwake, ukaribu wao kwa Mola wao Mlezi na wingi wa ibada zao na kuwanasihi kwa waja wa Mwenyezi Mungu anayapenda, kwa kuwa wanajua kwamba Mwenyezi Mungu anapenda wakifanya hivyo. Akasema: \"Wale wanaobeba kiti chake cha Enzi\" cha Mwingi wa rehema, ambacho ndicho paa la viumbe na ndicho kitu kikubwa zaidi, kipana zaidi, kilicho kizuri zaidi na kilicho karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, ambacho kilienea ardhi, mbingu, na Kursi (mahali ambapo miguu yake inakanyaga). Mwenyezi Mungu aliwakabidhi malaika hawa kukibeba kiti chake kikuu cha enzi. Hapana shaka kuwa wao ni miongoni mwa Malaika wakubwa zaidi na wenye nguvu zaidi. Kuchaguliwa kwao huku na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kukibeba kiti chake cha enzi na kuwapa kipaumbele katika kuwataja, na kujulisha kuhusu ukaribu wao kwake kunaashiria kuwa wao ndio aina bora zaidi ya Malaika, amani iwe juu yao. Mwenyezi Mungu alisema: \"Na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi,\" na \"wale walio pembezoni mwake\" miongoni mwa Malaika walio karibu na Mwenyezi Mungu kwa daraja na ubora, \"wanamtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi.\" Hii ni sifa kwao kwa sababu ya wingi wa kumwabudu kwao Mwenyezi Mungu, hasa kumtakasa na kumhimidi, na matendo mengine yote ya ibada yanayojumuishwa katika kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumsifu. \"Na wanawaombea msamaha wale walioamini.\" Haya ni miongoni mwa manufaa mbalimbali ya Imani na fadhila zake nyingi sana; kwamba Malaika ambao hawana dhambi zozote huwaombea msamaha watu wenye imani. Kwa hivyo, Muumini alijisababishia haya kwa sababu ya imani yake. Na kwa vile msamaha una masharti ambayo hauwezi kutimia ila kwayo - kinyume na yale yanayowajia watu wengi katika akili kwamba, kwa kuuomba tu na kuutaka ndiyo mwisho wake kupata msamaha wa dhambi - Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja jinsi wanavyowaombea msamaha kwa kutaja mambo ambayo hautimii isipokuwa kwayo, akasema: \"Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi.\" Elimu yako imekidhibiti kila kitu, wala chochote cha uzito wa chembe hakiwezi kufichikana kwako katika ardhi wala mbinguni, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa, na rehema yako imekienea kila kitu. Ulimwengu wote, wa juu na wa chini, umejaa rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na zimewaenea. \"Basi wasamehe wale waliotubu\" kutokana na ushirikina na maasia, \"na wakaifuata Njia yako\" kwa kuwafuata Mitume wako kwa kukupwekesha na kukutii, \"na waepushe na adhabu ya Jahannamu.\" Yaani, waepushe na adhabu yenyewe, na waepushe pia visababu vyake."},{"id":5089,"sura":40,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} \"Mola wetu Mlezi! Na waingize katika Bustani za Milele ulizowaahidi\" kupitia ndimi za Mitume wako. \"Na uwape haya pia wale waliofanya mema\" na kwa kuamini \"miongoni mwa wazee wao,wake zao\", marafiki zao \"na dhuriya zao. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu\", Mshindi wa kila kitu. Kwa nguvu zako, unawasamehe madhambi yao na unawaondolea yale wanayohofu, na unawafikisha kwayo kwenye wema wote. \"Mwenye hekima,\" anayeweka vitu mahali pake. Basi hatukuombi, ewe Mola Mlezi, jambo ambalo hekima yako inahitaji vinginevyo, bali tunakuomba kulingana na hekima yako uliyoisema kupitia ndimi za mitume wako na fadhila zako zikahitaji hivyo, kwamba uwasamahe waumini."},{"id":5090,"sura":40,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} \"Na waepushe na maovu;\" yaani, matendo maovu na adhabu yake. \"Kwani umwepushaye maovu siku hiyo\" ya Kiyama \"hakika umemrehemu,\" kwa sababu rehema yako haijaacha kuwafikia waja na hakuna kinachozizuia rehema zako isipokuwa madhambi ya waja na mabaya yao. Na yule ambaye utamwepusha maovu, basi utakuwa umemuwezesha kufikia mazuri na malipo yake mazuri. \"Na huko\" kuondokewa na yanayotaadhariwa kwa kumlinda mja kutokana na maovu na kuweza kupata anachopenda kwa kupata rehema \"ndiko kufuzu kukubwa,\" ambako hakuna kufaulu mfano wake, wala washindani hawashindani kwa ajili ya kizuri zaidi yake. Dua hii kutoka kwa Malaika inajumuisha: Kumjua kwao Mola wao Mlezi kikamilifu na kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa majina yake mazuri zaidi, ambayo anapenda kwamba waja wake wafike kwake kupitia hayo na kuomba dua kwa kutumia majina yanayofailia kitu ambacho wanakiomba kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hapa, walijifikisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia majina yake mawili ambayo ni Mwingi wa rehema na Mwingi wa kurehemu. Hii ni kwa kuwa waliomba dua kwamba wapewe rehema na waondolewe athari za yale ambayo nafsi za wanadamu zilihitaji, ambazo Mwenyezi Mungu alijua kwamba zilikuwa na upungufu kwa kufanya maasia na mambo mengineyo ambayo Mwenyezi Mungu alishayadhibiti kwa elimu yake. Pia inajumuisha ukamilifu wa adabu zao mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kukiri umola wake wa jumla na wa mahususi juu yao. Na kwamba hawana jambo lao katika suala hilo, bali dua yao waliyomuomba Mola wao Mlezi ilitoka kwa yule ambaye ni masikini katika dhati yake kwa namna yoyote ile na hawezi kujisimamia mbali na Mola wake Mlezi kwa hali yoyote ile. Hii sio isipokuwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, ukarimu wake na wema wake. Pia inajumuisha kuafikiana kwao kikamilifu na Mola wao Mlezi kwa kupenda matendo anayoyapenda, ambayo ni ibada wanazozifanya na wanajitahidi sana kama wanavyojitahidi wapenzi, na wakaafikiana naye kuhusiana na wanayoyatenda matendo hayo ambao ni waumini, ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapenda kati ya viumbe wake wote. Kwani Mwenyezi Mungu anawachukia viumbe wote wanaojukumishwa kisheria isipokuwa Waumini miongoni mwao. Na kwa sababu ya upendo wa malaika kwao, walimwomba Mwenyezi Mungu na wakajitahidi kuboresha hali zao. Kumwombea mtu dua ni katika ishara za wazi kabisa za upendo wake juu yake. Kwa sababu mtu hamuombei isipokuwa yule ambaye anampenda. Yale ambayo Mwenyezi Mungu alibainisha na kueleza kwa kina kuhusiana na dua yao - baada ya kauli yake: \"wanawaombea msamaha wale walioamini\" - yanajumuisha tanabahisho nzuri sana juu ya jinsi ya kukitafakari Kitabu chake.Na kwamba mwenye kukitafakari kitabu hiki hafai kusimamia tu kwa lafudhi ya neno peke yake, bali anapaswa kutafakari maana ya lafudhi pia. Ikiwa ataifahamu kwa usahihi namna ilivyo,atalitazama jambo hilo kwa akili yake na atatazama njia zinazolifikia, na yale ambayo hayatimii bila ya hilo, na yale ambayo linategemea juu yake, na awe na hakika kwamba Mwenyezi Mungu alilitaka; kama anao uhakika kwamba alitaka maana yake mahususi inayoashiriwa na neno na lafudhi hiyo. Na yale yanayolazimu kuwa na yakini juu yake kwamba Mwenyezi Mungu alilitaka ni mambo mawili: moja yake ni kwamba ajue na awe na uhakika kwamba ni moja ya mambo yanayotokana na maana yake na ambayo inategemea juu yake. Ya pili ni ajue kwamba Mwenyezi Mungu anajua vyema kila kitu, na kwamba Mwenyezi Mungu amewaamrisha waja wake kukizingatia na kukitafakari Kitabu chake. Mwenyezi Mungu Mtukufu alijua kinachohitajika katika maana hizo, na Yeye ndiye aliyetufahamisha kwamba Kitabu chake ni uwongofu, nuru na ufafanuzi wa kila kitu, na kwamba ndicho chenye maneno yenye ufasaha zaidi na yenye kubainisha kwa kina zaidi. Kwa kupitia hayo, mja anapata elimu kubwa na heri nyingi kulingana na yale ambayo Mwenyezi Mungu amemuwezesha. Katika tafsiri yetu kulikuwa na mengi katika haya ambayo Mwenyezi Mungu ametuneemesha kwayo, na katika baadhi ya aya maana yake inaweza kufichikana kwa yule ambaye hafikirii kwa njia sahihi. Na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atufungulie katika hazina za rehema zake mambo ambayo yatakuwa ni sababu ya kutengenea kwa hali zetu na hali za Waislamu, kwani hatuna ila kushikamana na ukarimu wake na kumfikia kupitia wema wake ambao bado tunaendelea kuupata katika wakati wote. Pia tunamuomba kutokana na fadhila zake kwamba atulinde kutokana na uovu wa nafsi zetu ambao unazuia kuifikia rehema yake. Hakika, Yeye ndiye Mkarimu zaidi, Mpaji zaidi, ambaye alitupa fadhila zake na visababu vya kuzifikia. Aya hii pia inajumuisha kwamba watu wanaokuwa pamoja kama vile mume, mke, mtoto na rafiki wanafaidika kutoka kwa wenzake na unakuwa uhusiano wao huo ndiyo sababu ya kufikia heri ambayo yeye mwenyewe hakuifanya; kama vile Malaika wanavyowaombea Waumini na wale waliofanya mema miongoni mwa wazee wao, wake zao na dhuriya zao. Lakini, pia inaweza kusemwa kwamba ni lazima wao wenyewe wawe wema, kulingana na kauli yake: \"na wale waliofanya mema.\" Ikiwa ni hivyo, basi inakuwa kwamba hayo yote ni matokeo ya matendo yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi."},{"id":5091,"sura":40,"from_aya":10,"to_aya":12,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"10. Kwa hakika wale waliokufuru watanadiwa: Bila ya shaka kukuchukieni Mwenyezi Mungu ni kukubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu, mlipokuwa mnaitwa kwenye Imani nanyi mkakataa. 11. Watasema: Mola wetu Mlezi! Umetufisha mara mbili, na umetuhuisha mara mbili! Basi tunakiri madhambi yetu. Basi je, ipo njia ya kutoka? 12. Hayo ni hivyo kwa sababu mlikuwa akiombwa Mwenyezi Mungu peke yake mnakataa. Na akishirikishwa mnaamini. Basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Mkuu. "},{"id":5092,"sura":40,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu fedheha na hizaya itakayowapata makafiri na maombi yao ya kurejea na kutoka Motoni, na kutowezekana kwa hayo: \"Hakika wale waliokufuru.\" Hili linajumuisha kila aina ya ukafiri, kama vile kumkufuru Mwenyezi Mungu, au vitabu vyake, au Mitume wake, au Siku ya Mwisho. Hilo litatokea watakapokuwa wanaingia Motoni na wakakiri kuwa wanaustahiki kweli kwa sababu ya dhambi na makosa waliyoyafanya. Hapo, watajichukia nafsi zao na kuzikasirikia sana, kisha wanaitwa na kuambiwa: \"Bila ya shaka kukuchukieni Mwenyezi Mungu ni kukubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu.\" Mlipokuwa mnaitwa kwenye Imani nanyi mnakufuru. Wakati Mitume na wafuasi waliwaita ili muamini, na wakawasimamishia hoja zilizo wazi ambazo kwazo haki ilibainika, lakini mkakufuru na mkakata tamaa ya kuamini jambo ambalo Mwenyezi Mungu alikuumbieni kwa ajili yake, na mkatoka katika rehema yake pana, kwa hivyo akakuchukieni. Hayo ni kitu \"kikubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu.\" Basi hali yenu hii iliendelea kuwa hivi kwa hivyo akawachukia na kuwakasirikia, mpaka leo mmepatwa na ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu, wakati Waumini walipata radhi na malipo ya Mwenyezi Mungu."},{"id":5093,"sura":40,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} Basi wakatamani kurejea, na \"wakasema: 'Mola wetu Mlezi! Umetufisha mara mbili,\" wakimaanisha kifo cha kwanza na kuzimia ambako kuko baina ya mipulizo miwili katika baragumu - kulingana na ilivyosemwa, au walimaanisha kutokuwepo kwa kabla ya kuwaumba, kisha akawafisha baada ya kuwaumba; \"Na umetuhuisha mara mbili\", uhai wa duniani na uhai wa Akhera. \"Basi tunakiri madhambi yetu. Basi je, ipo njia ya kutoka?\" Lakini hayo hayakuwafaidi kitu."},{"id":5094,"sura":40,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Walikemewa kwa kutofanya visababu vya wokovu, basi wakaambiwa: \"Hayo ni hivyo kwa sababu mlikuwa akiombwa Mwenyezi Mungu peke yake\" ili apwekeshwe na akusudiwe Yeye tu na kutomshirikisha, \"mnamkufuru.\" Na nyoyo zenu zimechukizwa kwa hayo, na mnajitenga nayo kujitenga kukubwa. \"Na akishirikishwa, mnaamini.\" Haya ndiyo yaliwafikisha mahala hapa, kwani mlikuwa mkikufuru Imani na mnaamini ukafiri. Mkawa mnaridhia maovu na uharibifu duniani na Akhera, na mnachukia mema na ya kuwafanya mtengenee katika dunia na Akhera. Mlikuwa mkipendelea sababu za kujitia mashakani, katika fedheha na ghadhabu, na mnakata tamaa ya kufikia yale ambayo ni sababu ya kufaulu na kushinda. \"Wakiiona njia ya uwongofu, hawaishiki kuwa ndiyo njia lakini wakiiona njia ya upotofu, wanaishika kuwa ndiyo njia.\" \"Basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Mkuu.\" Ni Mtukufu kwa namna zote: kwa dhati yake, cheo na ushindi. Na katika utukufu wa cheo chake ni ukamilifu wa uadilifu wake, na kwamba Yeye huweka vitu mahali pake, na wala hatoshanishi watu wema na waovu. Naye ni Mkubwa ambaye anao ukubwa wote, ukuu na utukufu katika majina yake, sifa zake na vitendo vyake, aliyetakasika mbali na kila kasoro na upungufu. Kwa hivyo, ikiwa hukumu ni yake, na tayari alishawahukumia kwamba mtaishi milele daima, basi hukumu yake haitageuka wala haitabadilika."},{"id":5095,"sura":40,"from_aya":13,"to_aya":17,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"13. Yeye ndiye anayekuonyesheni Ishara zake, na anakuteremshieni kutoka mbinguni riziki. Na hapana anayekumbuka ila anayerejea. 14. Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu, na wangalichukia makafiri. 15. Yeye ndiye Mwenye vyeo vya juu, Mwenye 'Arshi. Hutuma Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake, ili kuonya kwa Siku ya Mkutano. 16. Siku watakayodhihiri wao. Hapana kitakachofichikana chochote chao kwa Mwenyezi Mungu. Ufalme ni wa nani leo? Ni wa Mwenyezi Mungu, Mmoja, Mshindi. 17. Leo kila nafsi italipwa kwa yale iliyochuma. Hapana dhuluma leo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kufanya hesabu. "},{"id":5096,"sura":40,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja neema zake kubwa juu ya waja wake kwamba aliwabainishia haki mbali na batili kupitia yale anayowaonyesha waja wake ya aya zake za kinafsi, za kwenye upeo wa macho na za katika Qur-ani zinazoashiria kila linalotafuta na lililokusudiwa, na zinazobainisha uongofu kutokana na upotofu, kiasi kwamba mwenye kuziangalia na kuzitafakari hawezi kubaki na shaka hata kidogo katika kujua uhakika. Hii ni katika neema zake kubwa juu ya waja wake, kwani hakuiacha haki ikiwa na mchanganyiko na wala hakuliwacha jambo lililo sahihi kuwa na utata wowote. Bali aliweka aina mbalimbali za ishara na akazibainisha Aya mbalimbali ili mwenye kuangamia aangamie kwa hoja zilizowazi, na aishi atakayeishi kwa hoja zilizowazi. Na kila masuala yanavyokuwa matukufu na makubwa zaidi, ushahidi wake unakuwa mwingi na mwepesi zaidi. Hebu tazama suala la upweke wa Mwenyezi Mungu, kwa maana ndilo suala kubwa zaidi, zilikuja hoja nyingi sana juu yake, za kiakili na za kimaandiko, na Mwenyezi Mungu akazipigia mifano na hoja mbalimbali. Basi ndiyo maana akataja na kuashiria mahali hapa baadhi ya ushahidi wake. Alisema: \"Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu.\" Na alipotaja kuwa Yeye huwaonyesha waja wake Ishara zake, akatanabahisha juu ya ishara kubwa, akasema: \"Na anakuteremshieni kutoka mbinguni riziki.\" Yaani, mvua ambayo kwayo mnapata riziki nyinyi na mifugo wenu na mnaishi kwayo. Hilo linaashiria kwamba neema zote zinatoka kwake. Miongoni mwake ni neema za kidini, ambazo ni masuala ya kidini na ushahidi wake, na kufanya matendo mema yanayoufuata ushahidi huo. Na pia kuna neema zote za kidunia kama vile neema zinazotokana na mvua, ambayo kwayo nchi na watu wanakuwa hai. Hili linaonyesha kwa njia ya uhakika kwamba Yeye peke yake ndiye afaaye kuabudiwa, ambaye anafaa kukusudiwa peke yake katika dini, kama vile Yeye peke yake ndiye anayeneemesha. \"Na hapana anayekumbuka\" kwa ishara hizi anapokumbushwa \"ila anayerejea\" kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumpenda, kumnyenyekea na kumtii. Huyu ndiye anayenufaika kwa ishara hizo, nazo zinakuwa ni rehema kwake, na kwazo anazidi kuwa na ufahamu mkubwa."},{"id":5097,"sura":40,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} Na kwa kuwa ishara zinaleta ukumbusho, na kukumbuka kunalazimu kwamba mja amkusudie Mwenyezi Mungu peke yake, akasema: \"Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu.\" Hili linajumuisha kumuomba kwa kumfanyia ibada na kumuomba dua. Ikhlasi inamaanisha kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika ibada zote za faradhi na zinazopendekezwa katika haki za Mwenyezi Mungu na katika haki za waja wake, \"hata kama makafiri watachukia.\" Basi msiwajali, na wala hayo yasikuzuieni mbali na Dini yenu, wala msiijali lawama ya mwenye kuwalaumu kwa sababu ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana, makafiri wanachukia suala la kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake kwa chuki kubwa sana. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake, nyoyo za wale wasioiamini Akhera huchafuka. Na wanapotajwa wenginewe wasiokuwa Yeye, basi wao hufurahi.\""},{"id":5098,"sura":40,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15} Kisha akataja katika utukufu wake na ukamilifu wake unaohitaji kwamba akusudiwe Yeye tu katika ibada, akasema: \"Yeye ndiye Mwenye vyeo vya juu, Mwenye Kiti cha Enzi.\" Aliyeinuka juu ya Kiti chake cha Enzi, ambacho ni chake peke yake, na ambaye aliinuka juu katika vyeo vyake ambavyo kwavyo alijitenga mbali na viumbe vyake, na ni mwenye sifa tukufu, na ambaye dhati yake ilitukuza kiasi kwamba haiwezekani kujikurubisha kwake isipokuwa kwa matendo matakatifu na safi, ambayo ni ikhlasi inayoinua wenyewe viwango mbalimbali na inawaleta karibu naye na kuwaweka juu ya viumbe vyake vyote. Kisha akataja neema yake juu ya waja wake; kuwatumia wajumbe na ufunuo, akasema: \"Hutuma Roho,\" yaani, ufunuo ambao kwa nafsi na nyoyo ni kama roho zilivyo kwa miili. Kama vile mwili bila roho hauwi hai wala hauishi, basi vile vile nafsi na moyo bila roho ya ufunuo haviwezi kutengenea wala kufaulu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu \"hutuma Roho kwa amri yake\" ambayo ndani yake yamo manufaa na masilahi kwa waja wake \"juu ya amtakaye katika waja wake,\" ambao ni Mitume wake aliowaboresha na akawateuwa kwa ajili ya kufikisha ufunuo wake na kuwalingania waja kwake. Faida ya kuwatuma Mitume ni kuwafikishia waja furaha yao katika dini yao, dunia yao na akhera yao, na kuwaondolea mambo ya kuwatia mashakani katika dini yao, dunia yao na Akhera yao. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akasema: \"Ili kuonya\" waja kutokana na \"Siku ya Mkutano\" na kuwahofisha na kuwahimiza juu ya kujitayarisha kwa kufanya visababu vya kuwaokoa kutokana na yatakayotokea humo. Aliita Siku ya Mkutano kwa sababu ni siku hii ambapo Muumba na viumbe watakutana, na viumbe wanakutana wao kwa wao, na watendaji matendo na matendo yao na malipo yao."},{"id":5099,"sura":40,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} \"Siku watakayodhihiri wao\" juu ya ardhi, huku wamekusanyika katika uwanja mmoja usiokuwa na mdidimio wala muinuko. Mwenye kuita ataweza kuwaskizisha wote na mwenye kutazama ataweza kuwaona wote. \"Hapana kitachofichikana chochote chao kwa Mwenyezi Mungu.\" Si wao wenyewe, wala kutoka matendo yao, wala malipo ya matendo hayo. \"Ufalme ni wa nani leo\" hii kuu, iliyokusanya wa kwanza na wa mwisho, wakazi wa mbinguni na watu wa duniani, ambayo ushirika katika umiliki ulikatika na yakakatika mafungamano yao yote, na hakuna kilichobakia isipokuwa matendo mema au mabaya. Ufalme siku hiyo \"ni wa Mwenyezi Mungu Mmoja,\" kwa dhati yake, majina yake, sifa zake na vitendo vyake, na hana mshirika yeyote katika hayo kwa namna yoyote ile. \"Mshindi\" wa viumbe vyote, ambaye viumbe vyote vilijisalimisha kwake, vikamdhalilikia na vikamnyenyekea, haswa katika siku hiyo ambayo nyuso zitamdhalilika yule aliye Hai Milele, Msimamia yote milele. Siku hiyo hakuna nafsi itakayozungumza isipokuwa kwa idhini yake."},{"id":5100,"sura":40,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} \"Leo kila nafsi italipwa kwa iliyochuma\" katika dunia; ya heri na maovu, machache na mengi. \"Hapana dhuluma leo\" juu ya yeyote kwa kuzidishiwa maovu yake au kupunguziwa mema yake. \"Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu.\" Yaani, msione kwamba siku hiyo iko mbali. Kwani anakuja,na kila kinachokuja, kiko karibu. Naye pia ni Mwepesi wa kuwafanyia waja hesabu kwa matendo yao Siku ya Kiyama kwa sababu ya elimu yake iliyozunguka kila kitu na kwa sababu ya ukamilifu wa uwezo wake."},{"id":5101,"sura":40,"from_aya":18,"to_aya":20,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"18. Na waonye siku inayokurubia, wakati nyoyo zitakapofika kooni, nao wamejaa huzuni. Madhaalimu hawatakuwa na rafiki, wala mwombezi wa kuitikiwa. 19. (Mwenyezi Mungu) anajua hiyana ya macho na yale ambayo vifua vinayaficha. 20. Na Mwenyezi Mungu huhukumu kwa haki; lakini hao ambao wao wanawaomba badala yake hawahukumu chochote. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona. "},{"id":5102,"sura":40,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad, rehema na amani zimshukie: \"Na waonye siku inayokurubia,\" na ambayo umefika wakati wa hali zake ngumu, wasiwasi wake mkubwa na mitetemeko yake. \"Wakati nyoyo zitakapofika kooni\" na macho yao yakawa yamekodoka kwa sababu ya hofu kubwa na dhiki, \"nao wamejaa huzuni\" kwa sababu ya yale yaliyo ndani ya nyoyo zao ya hofu kubwa na mambo makubwa yanayowasumbua. Hawatasema ila yule ambaye Mwingi wa rehema atamruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. \"Madhaalimu hawatakuwa na rafiki\" wala jamaa wa karibu, \"wala mwombezi wa kuitikiwa.\" Kwa sababu waombezi hawamuombei yule aliyejidhulumu nafsi yake kwa ushirikina, na hata kama ingechukuliwa kwamba wataweza kufanya uombezi,Mwenyezi Mungu haridhii uombezi wao huo, kwa hivyo hataukubali."},{"id":5103,"sura":40,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} \"(Mwenyezi Mungu) anajua hiyana ya macho\" anapowaangalia kwa siri wale waliokaa pamoja naye \"na yanayoficha vifua\", ambayo mja hajawahi kumwambia yeyote yule. Mwenyezi Mungu Mtukufu anayajua hayo yaliyojificha, kwa hivyo, mambo mengineyo yote yanayoonekana yanafailia zaidi kwamba anayajua vyema."},{"id":5104,"sura":40,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} \"Na Mwenyezi Mungu huhukumu kwa haki.\" Kwa sababu kauli yake ni haki, na hukumu yake ya kisheria ni haki, na hukumu yake ya kimalipo ni haki. Naye amedhibiti kila kitu kwa elimu, na kuandika na kukihifadhi. Naye ametakasika mbali na dhuluma, upungufu na kasoro zinginezo zote. Naye ndiye anayepitisha mipangilio yake ya mambo yote, ambaye anapotaka jambo, linakuwa. Na kile ambacho hakitaki, hakiwi. Naye ndiye anayehukumu baina ya waja wake waumini na makafiri katika dunia hii na kuwatenganisha kwa kuwapa ushindi marafiki zake na vipenzi wake. \"Lakini hao wanaowaomba badala yake hawahukumu chochote\" kwa sababu ya kutoweza kwao, na kwamba hawana utashi juu ya heri na uwezo wa kuifanya. \"Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia\" sauti zote kwa lugha mbalimbali na mahitaji mbalimbali. \"Mwenye kuona\" yaliyokuwepo, yatakayokuwepo, na yanayoonekana na yasiyoonekana, na yale ambayo waja wanayajua na wasiyoyajua. Alisema katika aya ya kwanza katika aya hizi mbili: \"Na waonye siku inayokurubia,\" kisha akaielezea kwa sifa hizi zinazohitaji kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo kuu; kwa sababu inajumuisha mambo ya kutia moyo na vitisho."},{"id":5105,"sura":40,"from_aya":21,"to_aya":22,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"21. Kwani hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Hao walikuwa wamewazidi hawa kwa nguvu na athari katika nchi. Na Mwenyezi Mungu aliwatia mkononi kwa sababu ya madhambi yao. Na wala hapakuwa wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. 22. Hayo ni kwa sababu walikuwa Mitume wao walikuwa wanawajia kwa hoja zilizo wazi, lakini wakawakataa, ndipo Mwenyezi Mungu akawakamata. Bila ya shaka Yeye ni Mwenye nguvu, Mkali wa kuadhibu. "},{"id":5106,"sura":40,"from_aya":21,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21-22} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: \"Kwani hawatembei katika ardhi\" kwa mioyo yao na miili yao, kwa njia ya kuzingatia na kutafakari juu ya athari mbalimbali, kwa hivyo wakaangalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao miongoni mwa wale waliokuwa wakikadhibisha? Wataukuta kwamba ulikuwa mbaya zaidi, kwa kuwa waliangamizwa, wakatiwa hizaya, wakafedheheshwa, ilhali hapo awali walikuwa na nguvu kuliko hawa kwa idadi, maandalizi, ukubwa wa miili \"na athari katika nchi\" kwa ujenzi na upandaji mimea. \"Na Mwenyezi Mungu aliwatia mkononi kwa sababu ya madhambi yao\" walipozikakamia na kuendelea kuzifanya. \"Bila ya shaka Yeye ni Mwenye nguvu, Mkali wa kuadhibu.\" Nguvu zao hizo hazikuwa na manufaa mbele ya nguvu za Mwenyezi Mungu. Bali miongoni mwa kaumu waliokuwa na nguvu zaidi, walikuwa kaumu ya 'Aad, ambao walisema: \"Ni nani mwenye nguvu kutushinda sisi?\" Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawatumia upepo uliodhoofisha nguvu zao hizo na ukawaangamiza wote kabisa."},{"id":5107,"sura":40,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"Kisha akataja mfano wa wale wanaokadhibisha Mitume, ambao ni Firauni na askari wake. Akasema:"},{"id":5108,"sura":40,"from_aya":23,"to_aya":46,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"23. Na kwa yakini tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na uthibitisho ulio wazi. 24. Kumwendea Firauni na Hamana na Qaruni, wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo mkubwa. 25. Basi alipowaletea Haki inayotoka kwetu, walisema: Waueni watoto wanaume wa wale waliomuamini na wawacheni hai wanawake wao. Na haviwi vitimbi vya makafiri ila katika upotovu. 26. Na Firauni akasema: Niachieni nimuue Musa, naye amwite Mola wake Mlezi! Mimi nachelea asije kubadilishieni dini yenu, au akadhihirisha uharibifu katika nchi. 27. Na Musa akasema: Mimi najikinga kwa Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi anilinde na kila mwenye jeuri asiyeiamini Siku ya Hesabu. 28. Na akasema mwanamume mmoja Muumini, aliyekuwa mmoja katika watu wa Firauni aliyeficha Imani yake: Mtamuuwa mtu kwa sababu anasema Mola wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu? Na hali naye amekujieni na hoja zilizo wazi? Na akiwa yeye mwongo, basi uongo wake ni juu yake mwenyewe. Na akiwa mkweli, yatakufikieni baadhi ya hayo anayokuahidini. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi apindukiaye mipaka, mwongo mkubwa. 29. Enyi watu wangu! Leo mna ufalme, mmeshinda katika nchi; basi ni nani atakayenisaidia kutuokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu kama ikitufikia? Firauni akasema: Sikupeni shauri ila ile niliyoiona, wala siwaongozi ila kwenye njia ya uwongofu. 30. Na akasema yule aliyeamini: Enyi watu wangu! Hakika mimi nawahofia mfano wa siku za makundi. 31. Mfano wa hali ya watu wa Nuhu na 'Adi na Thamudi na wale wa baada yao. Na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu waja. 32. Na enyi watu wangu! Hakika mimi nawahofia Siku ya mayowe. 33. Siku mtakapogeuka kurudi nyuma. Hamtakuwa na wa kukulindeni kwa Mwenyezi Mungu. Na mwenye kuhukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi huyo hana wa kumwongoa. 34. Na alikwishawajieni Yusuf zamani kwa dalili zilizo wazi, lakini nyinyi mliendelea katika shaka kwa yale aliyokuleteeni; mpaka alipokufa, mkasema: Mwenyezi Mungu hataleta kabisa Mtume baada yake. Kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha kupotea anayepindukia mipaka katika maasi anayejitia shaka. 35. Hao ambao wanajadiliana katika Ishara za Mwenyezi Mungu pasipo ushahidi wowote uliowafikia, ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya wale walioamini. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu azibavyo kila moyo wa jeuri anayejivuna. 36. Na Firauni akasema: Ewe Hamana! Nijengee mnara ili nipate kuzifikia njia. 37. Njia za mbinguni ili nikamwone Mungu wa Musa. Na kwa hakika mimi bila ya shaka namjua kuwa ni mwongo tu. Na hivi ndivyo Firauni alivyopambiwa ubaya wa vitendo vyake, na akazuiliwa Njia. Na vitimbi vya Firauni havikuwa ila katika kuangamia tu. 38. Na yule aliyeamini alisema: Enyi watu wangu! Nifuateni mimi, nitakuongozeni njia ya uwongozi mwema. 39. Enyi watu wangu! Hakika haya maisha ya dunia ni starehe ipitayo tu, na hakika Akhera ndiyo nyumba ya daima. 40. Mwenye kutenda uovu, hatalipwa ila sawa na huo uwovu wake. Na anayetenda wema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi, waruzukiwe humo bila ya hesabu. 41. Na enyi watu wangu! Kwa nini mimi nakuiteni kwenye uwokofu, nanyi mnaniita kwenye Moto? 42. Mnaniita nimkufuru Mwenyezi Mungu na nimshirikishe na yule ambaye simjui, nami nakuiteni kwa Mwenye nguvu Mwenye kusamehe mno? 43. Bila ya shaka mnayeniitia kumuabudu hastahiki wito duniani wala Akhera. Na hakika marejeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu. Na wanaopindukia mipaka ndio watu wa Motoni! 44. Basi mtayakumbuka ninayokuambieni. Nami namkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu. Hakika Mwenyezi Mungu anawaona vyema waja wake. 45. Basi Mwenyezi Mungu akamlinda na ubaya wa hila walizozifanya. Na adhabu mbaya itawazunguka watu wa Firauni. 46. Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapofika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa! "},{"id":5109,"sura":40,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} Yaani, \"kwa yakini tulimtuma Musa\" bin Imran \"pamoja na Ishara zetu\" kwa watu aina sawa na hawa wanaokadhibisha. Ishara zinazoashiria kwa uhakika yale aliyotumwa nayo na ubatili wa yale ambayo wale aliotumwa kwao wanafanya,ya ushirikina na mambo mengineyo yanayofuatana nao. \"Na uthibitisho ulio wazi,\" yaani, hoja zilizowazi zinazotawala nyoyo na kuzifanya kunyenyekea mbele ya hoja hizo, kama vile nyoka na fimbo, na ishara nyinginezo zilizo wazi ambazo Mwenyezi Mungu alimuunga mkono Musa kwazo na akamuwezesha kuilingania haki."},{"id":5110,"sura":40,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} Wale waliotumiwa Mtume huyu walikuwa \"Firauni na Hamana,\" ambaye alikuwa waziri wake, \"na Qaruni\" ambaye alikuwa katika watu wa Musa, lakini akawafanyia dhuluma kwa mali yake. Wote walimkatalia mbali kwa ukali mkubwa zaidi na wakasema: \"Huyu ni mchawi, mwongo mkubwa.\""},{"id":5111,"sura":40,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} \"Basi alipowaletea Haki inayotoka kwetu\" na Mwenyezi Mungu akamsaidia kwa miujiza ya kung'aa iliyohitaji kusalimu amri kikamilifu, hawakuikabili kwa njia hiyo, na tena haikuwatosha kuiacha tu na kuipa mgongo, wala kuikataa na kuipinga kwa batili, bali hali yao mbaya hiyo iliwafikisha kiwango cha: \"Waueni watoto wanaume wa wale waliomuamini na wawacheni hai wanawake wao. Na haviwi vitimbi vya makafiri ila katika upotovu.\" Kwa kuwa walipanga vitimbi hivi na wakadai kwamba wakiwauwa watoto wao wanaume, basi hawatakuwa na nguvu, na wataendelea kuwa katika utumwa chini ya umiliki wao. Lakini vitimbi vyao hivyo havikuwa \"ila katika upotovu,\" kwani hayakutimia yale waliyokusudia, bali kiliwapata kinyume cha walichokusudia. Mwenyezi Mungu aliwaangamiza na kuwafutilia mbali hadi wa mwisho wao. Kanuni: Zingatia suala hili ambalo limetajwa mara kwa mara katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu ikiwa muktadha unahusu hadithi maalumu au juu ya jambo maalumu, na Mwenyezi Mungu akataka kuhukumu jambo hilo maalum kwa hukumu ambayo sio mahususi kwa hilo tu. Yeye hutaja hukumu hiyo na akaifungamanisha na maelezo ya jumla; ili iwe ni hukumu ya jumla zaidi na ijumuishe suala hilo ambalo mazungumzo hayo yalikuja kwa sababu yake, ili kuzuia hisia kwamba hukumu hii ni maalumu kwa jambo hilo maalumu. Ndiyo maana hakusema: 'Na haviwi vitimbi vyao ila katika upotovu', bali alisema: \"Na haviwi vitimbi vya makafiri ila katika upotovu.\""},{"id":5112,"sura":40,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} Na \"Firauni akasema\" kwa kiburi, kutakabari na kuwahadaa watu wake wapumbavu: \"Niachieni nimuuwe Musa, naye amwite Mola wake Mlezi!\" Yaani, alidai - Mwenyezi Mungu amlaani - kwamba kama haingekuwa ni kwa sababu ya kuzingatia hisia za watu wake, basi angemuua Musa na kwamba hata Musa akimuomba dua Mola wake Mlezi, hilo haliwezi kumzuia kufanya hivyo. Kisha akataja kile kilichomfanya kutaka kumuua Musa, na kwamba alikuwa anawapa watu wake nasaha ya sawasawa na kuwaondolea maovu katika ardhi. Akasema: \"Mimi nachelea aje kukubadilishieni dini yenu\" mnayoifuata, \"au akadhihirisha uharibifu katika nchi.\" Hili ndilo jambo la kushangaza zaidi! Kwamba kiumbe muovu zaidi awe ndiye anayewashauri watu kutomfuata kiumbe bora zaidi. Huku ni kubadilisha mambo ambako hakuingii isipokuwa katika akili za wale ambao Mwenyezi Mungu alisema juu yao: \"Basi aliwachezea watu wake, na wakamtii. Kwa hakika hao walikuwa watu wavukao mipaka.\""},{"id":5113,"sura":40,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} \"Na Musa akasema\" wakati Firauni alipoyasema maneno hayo mabaya ambayo dhuluma yake ndiyo ilimfanya kuyasema, basi Musa akatumia nguvu zake na uwezo wake na akamuomba msaada Mola wake Mlezi: \"Mimi najikinga kwa Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi,\" ambaye kwa umola wake huo anaendesha mambo yote, \"anilinde na kila mwenye jeuri asiyeiamini Siku ya Hesabu.\" Yaani, ambaye kiburi chake na kutoiamini kwake Siku ya Hesabu vinamfanya kutenda maovu na uharibifu. Haya anaingia ndani yake Firauni na wengineo, kama ilivyotajwa hapo nyuma katika kanuni ya hapo awali. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa upole wake akamzuia mbali na kila mwenye jeuri asiyeiamini Siku ya Hesabu, na akamuwekea visababu ambavyo kwavyo alizuilika kutokana na ubaya wa Firauni na wakuu wake na dhulma yao."},{"id":5114,"sura":40,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Miongoni mwa visababu hivyo, ni huyu mwanamume Muumini ambaye anatoka katika familia ya Firauni kutoka katika nyumba ya ufalme, ambaye ililazimu awe katika watu wanaosikizwa maneno yao, hasa ikiwa anadhihirisha kwamba anaafikiana nao, lakini akaficha imani yake. Mara nyingi, wao humzingatia sana kushinda namna ambayo wangemzingatia ikiwa angewahalifu kwa dhahiri. Kama vile Mwenyezi Mungu alivyomzuilia Mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa ami yake, Abu Talib kutokana na Maqureishi; kwa vile Abu Talib alikuwa mkubwa miongoni mwao na alikuwa anaafikiana nao katika dini yao. Na ikiwa angekuwa Mwislamu, basi hangeweza kumzuilia hivyo. Basi mwanamume huyo Muumini aliyewezeshwa na Mwenyezi Mungu, mwenye akili nzuri, mwenye azimio mathubuti, akasema akikemea vitendo vya watu wake na ubaya mkubwa wa yale waliyoyadhamiria kufanya: \"Mtamuua mtu kwa sababu anasema Mola wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu?\" Na kauli hii hakuisema bure tu bila hoja na msingi wowote, ndiyo maana akasema: \"Na hali naye amekukujieni na hoja zilizowazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi.\" Kwa sababu hoja hizo za wazi wazi alizowaletea zilidhihirika baina yao hata kwa wadogo na wazee. Kwa hivyo, hili haliwezi kuwa ndiyo sababu ya kumuua. Kwa nini hamkubatilisha kwanza haki aliyokuja nayo, na akaikabili hoja kwa hoja nyingine yenye kuipinga hoja yake, kisha baada ya hapo mkaangalia je, inaruhusika kumuuwa ikiwa mtamshinda kwa hoja au la? Lakini sasa kwa kuwa hoja yake imedhihirika na uthibitisho wake ukashinda kati yenu, na kumuuwa kuna njia ndefu ya jangwani ambayo zinakatikia hapo shingo za vipando. Kisha akawaambia maneno ya kiakili ambayo yanamshawishi kila mwenye akili nzuri kwa namna yoyote ile. Akasema: \"Na akiwa yeye mwongo, basi uwongo wake ni juu yake mwenyewe. Na akiwa mkweli, yatakufikieni baadhi ya hayo anayokuahidini.\" Yaani, Musa yuko baina ya mambo mawili: ima ni mwongo katika madai yake hayo au ni mkweli. Ikiwa ni mwongo, basi uwongo wake huo uko juu yake, na madhara yake ni juu yake tu, hayatawapata madhara yoyote katika hilo kwa vile mlikataa kumuitikia na kumsadiki. Na kama ni mkweli, na ilhali amekukujieni na hoja zilizo wazi na akakwambieni kwamba msipomuitikia, basi Mwenyezi Mungu atakuadhibuni kwa adhabu ya duniani na adhabu nyingine Akhera, basi lazima yatawapata baadhi ya hayo anayokuahidini, ambayo ni adhabu ya duniani. Haya ni kutokana na akili yake nzuri na upole wake katika kumtetea Musa. Ambapo alikuja na jibu hili, ambalo halikuwachanganya, na akalifanya jambo hilo kuwa kati ya hali hizo mbili na kwamba katika makadirio yote, kumuua kulikuwa ni upumbavu na ujinga. Kisha akahami - Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amghufirie na amrehemu - kwenye jambo ambalo liko juu zaidi ya hilo na kubainisha kwamba Musa yuko karibu na haki. Akasema, \"Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi apindukiaye mipaka\" kwa kuiacha haki na kuishika batili, \"mwongo mkubwa,\" kwa kumnasibishia Mwenyezi Mungu hayo aliyopitiliza mipaka ndani yake. Huyu, Mwenyezi Mungu hawezi kumwongoa kufikia njia iliyosawa. Si katika maana yake wala katika ushahidi wake, wala hawezeshwi kufikia njia iliyonyooka. Yaani, tayari mmeshayaona yale ambayo Musa anayalingania ya haki na kile ambacho Mwenyezi Mungu alimuongoa kukieleza miongoni mwa hoja za kiakili na mambo ya kimiujiza ya mbinguni. Yule ambaye ameongoka hivi, hawezi kuwa katika wavukao mipaka wala mwongo. Huu ni ushahidi juu ya ukamilifu wa elimu yake, akili yake na kumjua kwake vyema Mola wake Mlezi."},{"id":5115,"sura":40,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Kisha akawaonya watu wake, akawanasihi, akawahofisha juu ya adhabu ya Akhera na akawakataza wasidanganywe na ufalme wa dhahiri. Akasema: \"Enyi watu wangu! Leo mna ufalme\" katika dunia hii, \"mmeshinda katika nchi\" juu ya watu walio chini ya utawala wenu, mnawaendesha mtakavyo. Basi chukulieni kwamba hayo yote mnayo nyinyi na yalitimia, lakini hayawezi kutimia. \"Basi ni nani atakayenisaidia kutuokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu kama ikitufikia?\" Hili ni katika njia yake nzuri ya kulingania kwa Mwenyezi Mungu, ambapo aliwaingiza katika jambo hili na pia akajiingiza humo yeye mwenyewe aliposema: \"Kama ikitufikia,\" ili awafahamishe kuwa anawanasihi na pia anajinasihi yeye mwenyewe, na anawapendelea yale anayoipendelea nafsi yake. \"Firauni akasema\" akimpinga katika hayo na kuwahadaa watu wake ili wasimfuate Musa: \"Sikupeni shauri ila ile niliyoiona, wala sikuongozeni ila kwenye njia ya uwongofu.\" Naye alikuwa mkweli katika kauli yake: \"Sikupeni shauri ila ile niliyoiona.\" Lakini aliona nini? Aliona kwamba awachezee watu wake ili wamfuate na ili aweze kusimamisha uongozi wake kwa hao. Na wala hakuona kwamba yeye yuko kwenye haki, bali aliona kwamba haki iko upande wa Musa na akaiikataa hali ya kuwa nafsi yake ina yakini nayo. Naye alidanganya katika kauli yake: \"Wala sikuongozeni ila kwenye njia ya uwongofu.\" Huku ni kupindua uhakika wa mambo. Kwani, kama angewaamrisha wamfuate tu katika ukafiri wake na upotofu wake, basi uovu wa hilo ungekuwa mdogo zaidi. Lakini aliwaamrisha kumfuata na akadai kuwa kumfuata ndio kufuata haki, na kwamba kufuata haki ndiyo kufuata upotofu."},{"id":5116,"sura":40,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} \"Na akasema yule aliyeamini\" akirudia kuwalingania kaumu yake bila kukata tamaa na kuongoka kwao. Hivi ndivyo ilivyo hali ya wale wanaolingania kwa Mwenyezi Mungu. Wanaendelea kulingania kwa Mola wao Mlezi, na hakuna chochote kinachoweza kuwazuia kufanya hivyo, na wala kiburi cha yule wanaowalingania hakiwakatishi tamaa ya kurudia wito. Aliwambia: \"Enyi watu wangu! Hakika mimi nakuhofieni mfano wa siku za makundi.\" Yaani, umma waliokadhibisha ambao walijipanga makundi dhidi ya Manabii wao na wakakusanyika ili kuwapinga."},{"id":5117,"sura":40,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} Kisha akawabainisha akisema: \"Mfano wa hali ya watu wa Nuhu, 'Adi, Thamudi na wale wa baada yao,\" wote walikuwa sawa katika tabia yao ya kukufuru na kukadhibisha, na pia ada ya Mwenyezi Mungu ya kuadhibu duniani kabla ya Akhera. \"Na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu waja\" kwa kuwaadhibu bila kosa lolote walilokosa wala bila uhalifu walioutanguliza."},{"id":5118,"sura":40,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} Alipowahofisha juu ya adhabu za duniani, akawahofisha pia juu ya adhabu ya Akhera, akasema: \"Na enyi watu wangu! Hakika mimi nawahofia Siku ya mayowe\" huko Akhera ambapo wakazi wa Bustani ya mbinguni watakapowaita wakazi wa Motoni: \"Sisi tumekuta yale aliyotuahidi Mola wetu Mlezi kuwa ni kweli.\" Mpaka mwisho wa Aya \"Na watu wa Motoni watawaita watu wa Peponi: Tumiminieni maji au chochote alichokuruzukuni Mwenyezi Mungu. Nao watasema: Hakika Mwenyezi Mungu ameviharamisha hivyo kwa makafiri.\" Na wakati wakazi wa Motoni watakapomwita Malik, mlinzi wa Jahannam: \"Na atufishe Mola wako Mlezi!\" naye atasema: \"Hakika nyinyi mtakaa humo humo!\" Na watakapomwita Mola wao Mlezi: \"Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tukiyarejelea tena, basi kweli sisi ni wenye kudhulumu.\" Basi atawajibu: \"Tokomeeni humo, wala msinisemeshe.\" Na watakapoambiwa washirikina: \"Waiteni hao miungu wa kishirikina wenu! Basi watawaita, lakini hawatawaitikia.\""},{"id":5119,"sura":40,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} Yeye, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, akawahofisha juu ya siku hii mbaya zaidi, na akaona uchungu juu yao ikiwa wataendelea na ushirikina wao huo. Ndiyo maana akasema: \"Siku mtakapogeuka kurudi nyuma\" wakati mnapelekwa Motoni. \"Hamtakuwa na wa kukulindeni kutokana na Mwenyezi Mungu,\" wala nyinyi wenyewe hamtakuwa na nguvu ya kuzuia adhabu ya Mwenyezi Mungu \"Siku zitakapodhihirishwa siri. Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.\" \"Na mwenye kupotezwa na Mwenyezi Mungu, basi huyo hana wa kumwongoa.\" Kwa sababu uwongofu uko mkononi mwa Mwenyezi Mungu tu. Ikiwa atamnyima mja wake uwongofu kwa sababu anajua kuwa haufailii huo kwa sababu ya uovu wake, basi hakuna njia yoyote ya kumuongoa huyo."},{"id":5120,"sura":40,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} \"Na alikwishawajieni Yusuf\" mwana wa Yaaqub, amani iwe juu yao wote wawili, \"zamani\" kabla ya kuja kwa Musa na ushahidi wa wazi unaoonyesha ukweli wake, na akakuamrisheni kumwabudu Mola wenu Mlezi peke yake, bila mshirika yeyote. \"Lakini nyinyi mliendelea katika shaka kwa yale aliyokuleteeni\" katika uhai wake, \"mpaka alipokufa\" shaka yenu hiyo na ushirikina wenu vikazidi, \"mkasema: Mwenyezi Mungu hataleta kabisa Mtume baada yake.\" Yaani, hii ilikuwa ndiyo dhana yenu batili ambayo haimfailii Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu hawezi kuwaacha bure viumbe wake, bila ya kuwaamrisha na kuwakataza, bali huwatumia Mitume wake. Na kudhani kuwa Mwenyezi Mungu hatamtuma Mtume ni upotofu, na ndiyo maana akasema: \"Kama hivyo Mwenyezi Mungu humpoteza yule anayepindukia mipaka katika maasi, anayejitia shaka.\" Hivi ndivyo walivyomuelezea Musa kwa uhakika, ambayo ni maelezo ya kidhuluma na ukaidi. Kwani wao ndio waliopindukia mipaka haki na wakauendea upotofu. Nao ni waongo kwa kuwa walimnasibisha Mwenyezi Mungu na hayo na wakamkadhibisha Mtume wake. Na anayesifika kwa kupitiliza mipaka na uwongo hawezi kuachana na hayo, na wala Mwenyezi Mungu hamwongoi wala hamwezeshi kufikia heri kwa sababu aliikataa haki baada ya kumfikia na akaijua. Kwa hivyo, malipo yake ni kwamba Mwenyezi Mungu anamuadhibu kwa kumnyima uwongofu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Walipopotoka, Mwenyezi Mungu akazipotoa nyoyo zao.\" Na kauli yake: \"Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao. Kama walivyokuwa hawakuamini mara ya kwanza, tunawaacha katika maasi yao wakitangatanga.\" Na kuali yake: \"Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu.\""},{"id":5121,"sura":40,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} Kisha akataja maelezo ya mwongo huyo mwingi kupitiliza kiasi, akasema: \"Hao ambao wanajadiliana katika Ishara za Mwenyezi Mungu\" ambazo zilibainisha haki mbali na batili, na zikawa kama jua kwa macho katika kubainika kwake. Wanabishana juu yake licha ya ubainifu wake, ili wazipinge na wazibatilishe \"pasipo ushahidi wowote uliowafikia.\" Hii ndiyo sifa isiyoachana na kila anayepinga ishara za Mwenyezi Mungu. Haiwezekani kwake kubishana akitumia ushahidi, kwa sababu haki haiwezi kupingwa na mpinzani yeyote; kwa hivyo haiwezi kupingwa kwa ushahidi wa kisheria au wa kiakili hata kidogo. \"Ni chukizo kubwa\" kauli hiyo inayojumuisha kupinga haki kwa batili \"mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya wale walioamini.\" Mwenyezi Mungu ana chuki kubwa zaidi kwa afanyae hivyo, kwa sababu inajumuisha kuikadhibisha haki na kuisadiki batili na kumnasibisha nayo. Hayo yote ni mambo ambayo Mwenyezi Mungu huyachukia zaidi, na anamchukia yule anayesifika nayo, na pia waja wake waumini wanayachukia sana kwa kuafikiana na Mola wao Mlezi. Hawa ndio viumbe maalumu ambao Mwenyezi Mungu aliwaumba. Chuki yao ni ushahidi wa ubaya mkubwa wa wale ambao wao wanawachukia. \"Hivi\" alivyoziba nyoyo za familia ya Firauni, \"ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kila moyo wa jeuri anayejivuna.\" Mwenye kiburi cha kukataa haki na cha kuwadharau viumbe wake, na anayejivuna kwa kufanya dhuluma nyingi na kuvuka kwake mipaka."},{"id":5122,"sura":40,"from_aya":36,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36 - 37} \"Na Firauni akasema\" akimpinga Musa na akikadhibisha wito wake wa kumkiri Mola Mlezi wa walimwengu wote, aliyeinuka juu ya Kiti cha Enzi na aliyetukuka juu ya viumbe vyote: \"Ewe Hamana! Nijengee mnara\" mkubwa mrefu ili nipate kuzifikia njia. \"Njia za mbinguni ili nikamwone Mungu wa Musa. Na kwa hakika mimi bila ya shaka namjua kuwa ni mwongo tu\" katika wito wake kwamba tuna Mola Mlezi, na kwamba yuko juu ya mbingu. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema katika kubainisha kilichompelekea kusema hivyo: \"Na hivi ndivyo Firauni alivyopambiwa ubaya wa vitendo vyake\" na Shetani akaendelea kumpambia hayo, kwa hivyo akawa anayalingania na kuyafanya kuonekana kuwa mazuri mpaka akayaona kwamba ni mazuri, akayalingania na akajadili mjadala wa mwenye haki, ilhali yeye ndiye mharibifu mkubwa zaidi. \"Na akazuiliwa Njia\" ya haki kwa sababu ya batili aliyopambiwa. \"Na vitimbi vya Firauni\" ambavyo alitaka kuipangia njama haki na kuwafanya watu kudhania kuwa yuko katika haki na kwamba Musa yuko katika batili \"havikuwa ila katika kuangamia tu,\" wala havinufaishi isipokuwa kujitia mashakani katika dunia na akhera."},{"id":5123,"sura":40,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} \"Na yule aliyeamini alisema\" akirudia kuwanasihi watu wake: \"Enyi watu wangu! Nifuateni mimi, nitakuongozeni njia ya uwongozi mwema,\" si kama anavyowaambia huyu Firauni. Yeye hakuongozeni isipokuwa kwenye njia ya upotofu na uharibifu."},{"id":5124,"sura":40,"from_aya":39,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39} \"Enyi watu wangu! Hakika haya maisha ya dunia ni starehe ipitayo tu\" ambayo mtu anastarehe kwayo kwa muda kidogo, kisha inakatika na kuishia mbali; kwa hivyo kamwe zisiwadanganye wala zisiwahadae mkayaacha yale mliyoumbwa kwa ajili yake. \"Na hakika Akhera ndiyo nyumba ya daima.\" Basi mnapaswa kuipendelea na kuifanyia matendo ambayo yatawapa furaha huko."},{"id":5125,"sura":40,"from_aya":40,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40} \"Mwenye kutenda uovu\" kama vile shirki, kuvuka mipaka na maasia, \"hatalipwa ila sawa na huo uwovu wake\" ambao utamuwiya vibaya na kumhuzunisha. Kwa sababu malipo ya mabaya ni mabaya. \"Na anayetenda wema, akiwa mwanamume au mwanamke,\" miongoni mwa matendo ya nyoyo, viungo na maneno ya ulimi, \"basi hao wataingia Peponi, waruzukiwe humo bila ya hesabu.\" Yaani, watapewa ujira wao bila ya kikomo wala hesabu. Mwenyezi Mungu atawapa yale ambayo matendo yao hayakuweza kuyafikia."},{"id":5126,"sura":40,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41} \"Na enyi watu wangu! Kwa nini mimi nakuiteni kwenye uwokovu\" kwa yale niliyowaambia \"nanyi mnaniita kwenye Moto\" kwa kuacha kumfuata Nabii wa Mwenyezi Mungu, Musa, amani iwe juu yake?"},{"id":5127,"sura":40,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} Kisha akaeleza hayo akasema: \"Mnaniita ili nimkufuru Mwenyezi Mungu na nimshirikishe na yule ambaye simjui,\" ambaye hastahiki kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu. Kwani kusema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu ndiyo dhambi kubwa na mbaya zaidi. \"Nami nakuiteni kwa Mwenye nguvu\" zote, naye asiyekuwa na kitu chochote mkononi mwake katika jambo hili. \"Mwenye kusamehe mno.\" Ambaye waja wanajifanyia dhuluma nafsi zao, na wakathubutu kufanya yanayomkasirisha, kisha wanapotubu na kurejea kwake, anawafutia mabaya na dhambi zao na akazuia yale yanayotokana nayo ya adhabu za duniani na za akhera."},{"id":5128,"sura":40,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} \" Bila ya shaka mnayeniitia kumuabudu hastahiki wito duniani wala Akhera.\" Yaani, hastahiki kulinganiwa na kuhimiza kumkimbilia katika dunia wala Akhera kwa sababu ya kutoweza kwake na upungufu wake, na kwamba hamiliki uwezo wa kunufaisha wala kudhuru, wala kifo, wala uhai wala kufufua. \"Na hakika marejeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu\" Mtukufu, naye kila mtendaji matendo kwa matendo yake. \"Na kwamba wale wanaopindukia mipaka ndio watu wa Motoni!\" Walipindukia mipaka kwa kufanya ujasiri wa kumuasi na kumkufuru."},{"id":5129,"sura":40,"from_aya":44,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{44} Alipowanasihi, akawatahadharisha na akawaonya, lakini hawakumtii wala hawakukubaliana naye, akawaambia: \"Basi mtayakumbuka ninayokuambieni\" katika nasaha hii na mtaona madhara ya kutoikubali itakapokufikieni adhabu, na mtakaponyimwa ujira mkubwa. \"Nami ninamkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu.\" Yaani, ninamkimbilia na kushikamana naye, na kumuachia mambo yangu yote, na kumtegemea Yeye katika kunifikishia masilahi yangu na kuniepushia madhara yanayonipata kutoka kwenu au kutoka kwa wasiokuwa nyinyi. \"Hakika Mwenyezi Mungu anawaona vyema waja wake.\" Anazijua hali zao na wanayostahiki. Anaijua hali yangu na udhaifu wangu, basi ananilinda kutokana nanyi na ananitosheleza na shari yenu. Na anazijua hali zenu, basi hamuwezi kutenda chochote ila kulingana na utashi wake na mapenzi yake. Kwa hivyo, akikupeni mamlaka juu yangu, basi ni kwa sababu ya hekima yake Mtukufu, na kwa utashi wake na mapenzi yake."},{"id":5130,"sura":40,"from_aya":45,"to_aya":46,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{45 - 46} \"Basi Mwenyezi Mungu akamlinda na ubaya wa hila walizozifanya.\" Yaani, Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu, alimlinda mwanamume huyo muumini aliyemwezesha kutokana na adhabu za yale ambayo Firauni na familia yake walimpangia ya kumwangamiza, kwa sababu alianzisha yale waliyoyachukia na akawaonyesha kwamba anaafikiana kikamilifu na Musa, amani iwe juu yake, na akawalingania katika yale ambayo Musa aliwaitia. Na hili ni jambo ambalo hawawezi kulistahimili, kwani wao ndio waliokuwa na uwezo wakati huo na alikuwa amewakasirisha, kwa hivyo wakamchukia zaidi. Basi wakataka kumfanyia vitimbi, lakini Mwenyezi Mungu akamlinda kutokana na vitimbi vyao na njama zao, na vitimbi na njama zao hizo zikawageukia wenyewe. \"Na adhabu mbaya itawazunguka watu wa Firauni.\" Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwazamisha wote kabisa asubuhi na katika maisha ya kaburini. \"Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itakapofika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!\" Hizi ndizo adhabu mbaya zaidi zinazowapata wale waliokadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu na wakakaidi amri yake."},{"id":5131,"sura":40,"from_aya":47,"to_aya":50,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"47. Na watapohojiana huko Motoni, wanyonge watawaambia wale waliojitukuza: Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu, basi je, hamtuondolei sehemu ya huu Moto? 48. Watasema wale waliojitukuza: Hakika sote sisi tumo humo humo! Kwani Mwenyezi Mungu ameshahukumu baina ya waja! 49. Na wale walio Motoni watawaambia walinzi wa Jahannamu: Mwombeni Mola wenu Mlezi atupunguzie walau siku moja ya adhabu. 50. Nao watasema: Je, hawakuwa wakikufikieni Mitume wenu kwa hoja zilizo wazi? Watasema: Kwani? Watasema: Basi ombeni! Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure. "},{"id":5132,"sura":40,"from_aya":47,"to_aya":47,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{47} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu watu wa Motoni, kuzozana kwao wenyewe kwa wenyewe, kulaumiana kwao,kutafuta kwao msaada kutoka kwa Mlinzi wa Moto na kutokuwa na manufaa yoyote katika kuomba kwao huko. Alisema: \"Na watakapohojiana huko Motoni,\" wafuasi wataweka ushahidi kwamba walidanganywa na wale ambao wao waliwafuata, lakini hao waliofuatwa watajitenga mbali na hao waliowafuata. \"Wanyonge watawaambia wale waliojitukuza\" na wakawalingania katika yale waliyokuwa wakiyafanyia kiburi: \"Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu.\" Mlitupoteza na mkatupambia ushirikina na uovu. \"Basi je, hamtuondolei sehemu ya huu Moto?\""},{"id":5133,"sura":40,"from_aya":48,"to_aya":48,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{48} \"Watasema wale waliojitukuza\" wakibainisha kutoweza kwao na kutekelezeka kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu juu yao wote: \"Hakika sisi sote tumo humo humo! Kwani Mwenyezi Mungu kesha hukumu baina ya waja\" na akamuwekea kila mmoja wao fungu lake la adhabu. Basi hakizidi chochote katika hayo wala hakipunguki, wala hakibadiliki kile alichohukumu Mwenye Hekima."},{"id":5134,"sura":40,"from_aya":49,"to_aya":49,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{49} \"Na wale walio Motoni\" miongoni mwa wale waliotakabari na wanyonge \"watawaambia walinzi wa Jahannamu: 'Mwombeni Mola wenu Mlezi atupunguzie walau siku moja ya adhabu\" ili tupate nafuu kidogo."},{"id":5135,"sura":40,"from_aya":50,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{50} Kisha \"watasema\" wakiwakaripia na wakiwabainishia kuwa uombezi wao huo hautowanufaisha kitu wala dua yao hiyo haitowafaa chochote: \"Je, hawakuwa wakikufikieni Mitume wenu kwa hoja zilizo wazi,\" ambazo kwazo mliweza kuijua haki na njia iliyonyooka, na yale yanayomuweka mtu karibu na Mwenyezi Mungu na yale yanayomuweka mbali zaidi? \"Watasema: Kwani,\" walitujia na hoja zilizowazi, kwa hivyo hoja ya Mwenyezi Mungu ya uhakika ikasimama juu yetu, lakini tukafanya dhuluma na tukaikaidi haki baada ya kudhihirika kwake. \"Watasema\" walinzi hao wa Motoni wakiwaambia watu wa Motoni, huku wakijitenga mbali na suala la kuwaombea dua na kuwafanyia uombezi. \"Basi ombeni\" wenyewe, lakini je, dua hii ina manufaa yoyote au la? Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure.\" Kwa sababu ukafiri huharibu matendo yote na unazuia kukubaliwa dua."},{"id":5136,"sura":40,"from_aya":51,"to_aya":52,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"51. Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na wale walioamini katika uhai wa duniani na siku watakaposimama Mashahidi. 52. Siku ambayo hautawafaa madhalimu udhuru wao, nao watapata laana, na watapata makazi mabaya kabisa. "},{"id":5137,"sura":40,"from_aya":51,"to_aya":51,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{51} Alipotaja adhabu ya watu wa Firauni katika dunia hii, kaburini na Siku ya Kiyama, na akataja hali mbaya zaidi ya watu wa Motoni waliowakadhibisha Mitume wake na wakapigana nao, akasema: \"Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na wale walioamini katika uhai wa duniani\" kwa hoja, uthibitisho, nusura, na katika Akhera kwa hukumu, na tuwalipe mema wafuasi wao na tuwaadhibu wale waliopigana nao kwa adhabu kali."},{"id":5138,"sura":40,"from_aya":52,"to_aya":52,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{52} \"Siku ambayo hautawafaa madhalimu udhuru wao\" watakapoweka udhuru. \"Nao watapata laana, na watapata makazi mabaya kabisa\" kwa wale wanaoishi huko."},{"id":5139,"sura":40,"from_aya":53,"to_aya":55,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"53. Na kwa hakika tulimpa Musa uwongofu, na tukawarithisha Wana wa Israili Kitabu. 54. Ambacho ni Uwongofu na Ukumbusho kwa wenye akili. 55. Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Na omba msamaha kwa dhambi zako, na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi jioni na asubuhi. "},{"id":5140,"sura":40,"from_aya":53,"to_aya":54,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{53 - 54} Alipotaja yale yaliyomfika Musa na Firauni na namna ilivyoishia hali ya Firauni na askari wake, kisha akataja hukumu ya jumla inayomjumuisha yeye na watu wa Motoni.Akataja kuwa alimpa Musa \"uwongofu,\" yaani ishara, elimu ambayo anaongoka kwayo mwenye kuongoka. \"Na tukawarithisha Wana wa Israili Kitabu\" kutoka karne moja hadi nyingine, nacho ni Taurati, ambayo inajumuisha uwongofu ambao ni kujua hukumu za kisheria na mambo mengineyo, na ambacho kinajumuisha kukumbuka heri kwa kuihimiza juu yake na kukumbuka maovu na kutishia dhidi yake; na hilo si kwa kila mtu, bali ni \"kwa wenye akili.\""},{"id":5141,"sura":40,"from_aya":55,"to_aya":55,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{55} \"Basi subiri\" ewe Mtume, kama walivyosubiri wale waliokuwa kabla yako miongoni mwa Mitume wenye stahamala kubwa. \"Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli.\" Haina shaka yoyote, wala si ya uongo kiasi kwamba inakuwa vigumu kwako kuwa na subira. Bali ni haki iliyo safi kabisa na uwongofu safi ambao wenye subira husubiri juu yake, na watu wenye uhafamu mkubwa hujitahidi kushikamana nayo. Kwa hivyo, kauli yake: \"Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli\" ni katika visababu vinavyohimiza juu ya kuwa na subira katika kumtii Mwenyezi Mungu na kujiepusha na anayoyachukia. \"Na omba msamaha kwa dhambi zako\" zinazokuzuia kufuzu na kufikia furaha yako. Basi hapa akawa amemuamrisha kuwa na subira ambamo kunapatikana yale anayopenda mtu, na akamuamrisha pia aombe maghfira ambayo ndani yake kuna kuzuia yote yanayotahadhariwa, na akamuamrisha kumtakasa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumsifu, hasa \"jioni na asubuhi\" ambao ndio wakati bora, na ndani yake kuna mambo mbalimbali ya wajibu na yale yanayopendekezwa, kwa sababu hayo yanasaidia juu ya mambo yote."},{"id":5142,"sura":40,"from_aya":56,"to_aya":56,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"56. Hakika hao wanaobishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu bila ya uthibitisho wowote uliowajia, hawana vifuani mwao ila kutaka ukubwa tu, na wala huo hawaufikilii. Basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona."},{"id":5143,"sura":40,"from_aya":56,"to_aya":56,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{56} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba yeyote anayebishana katika Aya zake ili kuzibatilisha kwa batili bila ya ushahidi wowote wa wazi wala uthibitisho, kwamba hilo linatokana na kiburi kilichomo nyoyoni mwao dhidi ya haki na juu ya yule aliyekuja nayo. Wanataka kuinuka juu yake kwa sababu ya batili waliyonayo. Hili ndilo kusudio lao na nia yao, lakini hili haliwezi kutimia na hawawezi kulifikia. Hili ni andiko lililo wazi na ni bishara njema ya kwamba kila mwenye kubishana na haki atashindwa, na kila anayeifanyia jeuri, basi hatimaye atafedheheka. \"Basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu.\" Hapa, hakutaja kile anachojikinga kutokana nacho ili hilo liwe la jumla. Yaani, jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kiburi kinachopelekea kuifanyia haki jeuri, na jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mashetani wa kiwatu na kijini. Na jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na maovu yote. \"Hakika Yeye ni Mwenye kusikia\" kila sauti pamoja na kutofautiana kwake kwingi. \"Mwenye kuona\" vitu vyote vinavyoonekana, mahali popote na wakati wowote ambao vipo."},{"id":5144,"sura":40,"from_aya":57,"to_aya":59,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"57. Bila ya shaka kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu. Lakini watu wengi hawajui. 58. Na kipofu na mwenye kuona hawalingani; na wale walioamini na wakatenda mema hawalingani na muovu. Ni machache mnayoyakumbuka. 59. Hakika Saa (ya Kiyama) itafika, nayo haina shaka. Lakini watu wengi hawaamini. "},{"id":5145,"sura":40,"from_aya":57,"to_aya":57,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{57} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha yaliyothibiti katika akili kwamba \"kuumba mbingu na ardhi\" pamoja na ukubwa wake na upana wake \"ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu.\" Kwa maana, kwa kulinganisha na uumbaji wa mbingu na ardhi, ni vitu vidogo zaidi. Kwa hivyo, Yule aliyeumba miili mikubwa na akaifanya kuwa sawasawa ana uwezo zaidi na anafailia zaidi kuwarudisha watu baada ya kufa kwao. Huu ni katika ushahidi wa kiakili unaoonyesha ufufuo kwa njia ya uhakika mara tu mwenye akili anapoutazama na akautumia kama ushahidi usio na shaka yoyote wala fikira potofu kwamba yatatokea yale ambayo Mitume walijulisha kuhusu ufufuo. Siyo kila mtu anaiweka akili yake katika hilo na akalitafakari. Ndiyo maana akasema: \"Lakini watu wengi hawajui,\" ndiyo maana hawayazingatii hayo wala hawayaweki maanani."},{"id":5146,"sura":40,"from_aya":58,"to_aya":58,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{58} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: \"Na kipofu na mwenye kuona hawalingani; na wale walioamini na watendao mema hawalingani na muovu.\" Yaani, kama ambavyo hawawi sawa kipofu na mwenye kuona, vile vile hawawi sawa wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na wakatenda mema na wale wanaotakabari wakakataa kumuabudu Mola wao Mlezi na wakaelekea katika kumuasi, wakajitahidi kufanya yenye kumkasirisha. \"Ni machache mnayoyakumbuka.\" Vinginevyo, kama mngekumbuka viwango vya mambo, daraja za heri na shari, na tofauti iliyoko baina ya watu wema na waovu, na mkawa na hima ya juu, basi mngependelea yenye manufaa kuliko yale yenye madhara, na mwongozo kuliko upotofu, na furaha ya kudumu kuliko dunia hii yenye kwisha."},{"id":5147,"sura":40,"from_aya":59,"to_aya":59,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{59} \"Hakika Saa (ya Kiyama) itafika, nayo haina shaka yoyote.\" Hilo walikwisha tujulisha Mitume ambao ndio wakweli zaidi katika viumbe wote, na vikayasema Vitabu vya kutoka mbinguni, ambavyo habari zake zote ni za viwango vya juu zaidi vya ukweli, na ushahidi na ishara za kiupeo wa macho ziliyaashiria. \"Lakini watu wengi hawaamini\" pamoja na mambo haya ambayo yanamlazimu mtu kusadiki na kutii kikamilifu."},{"id":5148,"sura":40,"from_aya":60,"to_aya":60,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahanamu wadhalilike."},{"id":5149,"sura":40,"from_aya":60,"to_aya":60,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{60} Haya ni katika upole wake kwa waja wake na neema yake kubwa. Ambapo aliwalingania katika yale ambayo yatawafaa katika dini yao na dunia yao, na akawaamrisha wamuombe dua ya ibada na dua ya kuomba haja zao mbalimbali, na akawaahidi kuwa atawaitikia, na akawaahidi adhabu wale wanaotakabari wakaacha kufanya hivyo. Akasema: \"Kwa hakika wale ambao wanajivuna wakaacha kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.\" Itakusanywa adhabu juu yao pamoja na kudunishwa yawe malipo ya kutakabari kwao."},{"id":5150,"sura":40,"from_aya":61,"to_aya":65,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"61. Mwenyezi Mungu ndiye aliyewafanyia usiku ili mpate kutulia humo, na mchana wa kuonea. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru. 62. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi, Muumba wa kila kitu. Hapana mungu ila Yeye; basi mnageuzwa wapi? 63. Namna hivi ndivyo walivyogeuzwa wale waliokuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu. 64. Ni Mwenyezi Mungu aliyekufanyieni ardhi kuwa ni pahala pa kukaa, na mbingu kuwa dari. Na akawatia sura, na akazifanya nzuri sura zenu, na akawaruzuku vitu vizuri. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. 65. Yeye ndiye aliye Hai - hapana mungu isipokuwa Yeye. Basi muabuduni Yeye mkimsafishia Dini Yeye. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. "},{"id":5151,"sura":40,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0622\u064a\u0627\u062a","text":"Zingatia Aya hizi tukufu zinazoashiria upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu, ukubwa wa fadhila zake, ulazima wa kumshukuru, ukamilifu wa uwezo wake, ukubwa wa mamlaka yake, upana wa ufalme wake, kuumba kwake kwa jumla kila kitu, ukamilifu wa uhai wake, kusifika kwake kwa sifa zote kamilifu ambazo anasifika kwazo na vitendo vizuri alivyovifanya, ukamilifu wa umola wake na upekee wake katika hilo, na kwamba usimamizi wote katika ulimwengu wa juu na wa chini katika nyakati zilizopita, za sasa na zijazo uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hakuna mwenye amri wala uwezo wowote katika hilo. Inatokana na hili kwamba Yeye Mtukufu ndiye anayepasa kufanyiwa uungu, kuabudiwa peke yake, ambaye hakuna yeyote anastahiki kitu chochote katika ibada kama vile hastahili chochote katika umola wake. Na inatokana na hilo kwamba nyoyo zinapasa kumjua Mwenyezi Mungu sana, kumpenda, kumhofu na kumtumaini. Mambo haya mawili - yaani, kumjua Yeye na kumuabudu - ndiyo ambayo Mwenyezi Mungu aliumba viumbe kwa ajili yake, na ndiyo lengo lililokusudiwa kutoka kwa waja. Haya ndiyo hufikisha kwenye kila heri, kufaulu, kutengenea na furaha ya kidunia na ya kiakhera, ambazo ndizo kipawa adhimu zaidi cha aliye Mkarimu kwa waja wake na ndiyo ladha tukufu zaidi kuliko zote, na ndizo ambazo zikipotea, inapotea kila heri na inakuja kila shari. Basi tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azijaze nyoyo zetu kumjua na kumpenda, na kwamba afanye harakati zetu za ndani na nje kuwa kwa ajili ya uso wake peke yake, za kufuata amri yake. Hashindwi na swali, wala hashindwi kutoa anapoombwa sana."},{"id":5152,"sura":40,"from_aya":61,"to_aya":61,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{61} Basi kauli yake Mwenyezi Mungu: \"Mwenyezi Mungu aliyewafanyia usiku\" kuwa ni giza, \"ili mpate kutulia humo\" na muache harakati zenu nyinyi ambazo ikiwa zingeendelea, basi zingewadhuru. Muda huo mnaenda kwenye malazi yenu, na Mwenyezi Mungu anawawekea usingizi ambao kwa huo moyo na mwili vinapata utulivu. Na hayo ni katika mambo ya lazima anayohitaji mwanadamu, ambayo hawezi kuishi bila hayo, na ndani yake pia kila mpenzi anapata utulivu kwa kipenzi chake, na fikira inakusanyika pamoja, na yanatulia mambo ya kushughulisha. \"Na\" Mwenyezi Mungu Mtukufu akaufanya \"mchana wa kuonea\" ukiangazwa kwa jua linaloendelea kwenda katika kuzunguka kwake. Hapo mnaamka kutoka katika malazi yenu kwenda kwenye shughuli zenu za kidini na za kidunia. Huyu anaweza kumtaja Mwenyezi Mungu na kusoma, na huyu anaweza kuswali, na huyu anaweza kutafuta elimu na kujifunza, na huyu anaweza kununua na kuuza, na huyu anaweza kufanya ujenzi au uhunzi au kuunda vitu, na huyu anaweza kusafiri katika chini kavu au baharini, na huyu anaweza kufanya kilimo, na huyu anaweza kuwatunza wanyama wake. \"Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye fadhila\" kubwa \"juu ya watu,\" kwani aliwaneemesha kwa neema hizi na nyinginezo na akawaepushia adhabu, mambo yanayowalazimu kumshukuru na kumkumbuka kikamilifu. \"Lakini watu wengi hawashukuru\" kwa sababu ya ujinga wao na udhalimu wao. \"Ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru.\" Wale wanaozikubali neema za Mola wao Mlezi, wakamnyenyekea Mwenyezi Mungu, wakampenda na wanazitumia katika kumtii Mola wao Mlezi na kumridhisha."},{"id":5153,"sura":40,"from_aya":62,"to_aya":62,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{62} \"Huyo\" aliyefanya aliyoyafanya \"ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi\" aliye wa pekee katika uungu wake na aliye peke yake katika umola. Kwa sababu kuwa kwake peke yake katika neema hizi ni katika umola wake, na kuhitaji kwake kushukuriwa juu yake ni katika uungu wake. \"Muumba wa kila kitu.\" Hili linathibitisha umola wake. \"Hapana mungu ila Yeye,\" nalo hili linathibitisha kwamba Yeye pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa bila mshirika yeyote. Kisha akataja waziwazi amri ya kumwabudu, akasema: \"Basi mnageuzwa wapi\" mkaacha kumuabudu Yeye peke Yake, bila mshirika, baada ya Yeye kuwabainishia ushahidi wa hayo na akawaangazia njia?"},{"id":5154,"sura":40,"from_aya":63,"to_aya":63,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{63} \"Namna hivi ndivyo walivyogeuzwa wale waliokuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu\" ili iwe ni adhabu ya kukataa kwao ishara za Mwenyezi Mungu na kuwaasi kwao Mitume wake. Walitengwa mbali na suala la kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumkusudia Yeye peke yake, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na ikiteremka Sura, hutazamana wao kwa wao (kama kwamba wanasema:) Je, yuko mtu anakuoneni? Kisha hugeukilia mbali. Mwenyezi amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa hao ni watu wasiofahamu.\""},{"id":5155,"sura":40,"from_aya":64,"to_aya":64,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{64} \"Ni Mwenyezi Mungu aliyewafanyia ardhi kuwa ni pahala pa kukaa,\" ikawa imeandaliwa kwa ajili ya masilahi yenu yote ambayo mnaweza kuilima, kuipanda, kujenga juu yake, kusafiri na kukaa juu yake, \"na mbingu kuwa dari\" ya ardhi ambayo mko ndani yake. Mwenyezi Mungu ameweka humo mambo ya kuwanufaisha kama vile nuru na alama mbalimbali, Ishara zinazowaongoza katika kiza cha bara na bahari. \"Na akawatia sura, na akazifanya nzuri sura zenu.\" Hakuna mnyama mwenye sura nzuri zaidi kuliko wanadamu. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: \"Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lililo bora kabisa.\" Na ukitaka kujua uzuri wa mwanadamu na ukamilifu wa hekima ya Mwenyezi Mungu kuhusiana naye, basi mtazame kiungo kwa kiungo. Je, unapata kiungo chochote kinachomfailia na kinachofaa kuwa katika mahali ambapo si pake? Pia tazama namna ulivyo mwelekeo uliomo mioyoni mwao wa mtu kwa mwengine. Je, unayapata hayo kwa wasiokuwa wanadamu? Na angalia kile ambacho Mwenyezi Mungu amempa yeye tu ambacho ni akili, imani, upendo na kujua, ambayo ndiyo maadili bora zaidi yanayolingana na sura nzuri zaidi. \"Na akakuruzukuni vitu vizuri\" miongoni mwa vyakula, vinywaji, ndoa, mavazi, uwezo wa kuona, kusikia na mengineyo miongoni mwa mambo mazuri ambayo Mwenyezi Mungu amewafanyia wepesi waja wake. Akawafanyia wepesi visababu vyake na akawazuia mbali na mambo maovu yanayopingana na hayo na kuwadhuru miili yao, nyoyo zao na dini zao. \"Huyo\" aliyepanga mambo na akakuneemesheni neema hizi, \"ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.\" Yaani, heri yake na wema wake ni kubwa na nyingi, naye ndiye anayewalea walimwengu wote kwa neema zake."},{"id":5156,"sura":40,"from_aya":65,"to_aya":65,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{65} \"Yeye ndiye aliye Hai\", uhai kamili wenye sifa zake za kidhati ambazo uhai wake hautimii ila kwazo, kama vile kusikia, kuona, uwezo, elimu, usemi na sifa nyinginezo za ukamilifu wake na utukufu wake. \"Hapana mungu isipokuwa Yeye\", ambaye hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila uso wake Mtukufu. \"Basi muabuduni.\" Hili linajumuisha kumuomba dua ya ibaada na dua ya kutaka kitu fulani \"mkimsafishia Dini Yeye\" kwa ibada zote na dua, na kufanya matendo kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani, kilichoamrishwa ni mtu kuwa na Ikhlasi; Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu.\" \"Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote,\" sawa ziwe kwa kauli kama vile viumbe kutamka kwa kumtaja, au kwa vitendo kama vile kumuabudu. Yote haya ni ya Mwenyezi Mungu peke yake. Hana mshirika kwa sababu ya ukamilifu wake katika sifa zake, vitendo vyake na ukamilifu wa neema zake."},{"id":5157,"sura":40,"from_aya":66,"to_aya":68,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"66. Sema: Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ziliponijia hoja zilizo dhahiri kutokana na Mola wangu Mlezi. Na nimeamrishwa nisilimu kwa Mola wa walimwengu wote. 67. Yeye ndiye aliyewaumba kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande la damu, kisha akawatoa katika hali ya mtoto mchanga, kisha mpate kufikilia utu uzima, kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanaokufa kabla, na ili mfikie muda uliokwisha wekwa, na ili mpate kufahamu. 68. Yeye ndiye anayehuisha na anayefisha. Akihukumu jambo liwe, basi huliambia: Kuwa! Likawa. "},{"id":5158,"sura":40,"from_aya":66,"to_aya":66,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{66} Alipotaja amri ya kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, na akataja ushahidi juu yake na hoja zilizowazi, akakataza wazi wazi kuabudu asiyekuwa Yeye, akasema: \"Sema\" ewe Nabii, \"Hakika Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu\" miongoni mwa viabudiwa vyote visivyokuwa Mwenyezi Mungu, na masanamu. Wala mimi sina shaka yoyote juu ya jambo langu hili, bali nina yakini na ufahamu mzuri sana, ndiyo maana akasema: \"ziliponijia hoja zilizo dhahiri kutokana na Mola wangu Mlezi. Na nimeamrishwa nisilimu kwa Mola wa walimwengu wote\" kwa moyo wangu, ulimi wangu na viungo vyangu, ili viwe vitiifu kwa kutenda mambo ya utiifu kwake na kujisalimisha kwa amri yake. Na hii ndiyo amri kuu zaidi kuliko zote, kama vile kukataza kuabudiwa visivyokuwa Yeye ndilo katazo kubwa kuliko makatazo yote."},{"id":5159,"sura":40,"from_aya":67,"to_aya":67,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{67} Kisha ikathibitisha upweke wake huu kwamba Yeye ndiye Muumba wenu na Mtengenezaji wa maumbile yenu. Kwa hivyo, kama alivyokuumbeni peke yake, basi mwabuduni Yeye peke yake; akasema: \"Yeye ndiye aliyewaumba kwa udongo.\" Na hilo lilikuwa kwa kuumba asili yenu na baba yenu Adam, amani iwe juu yake, \"kisha kwa tone la manii.\" Huu ndio mwanzo wa kuumbwa kwa wanadamu wengineo waliobakia. Kwa hivyo akatanabaisha juu ya awamu zilizosalia kama vile pande la damu, kisha pande la nyama, kisha mifupa, kisha kupuliza roho. \"Kisha akakutoeni katika hali ya mtoto mchanga, kisha\" vivyo hivyo mkaendelea kuhama kutoka katika umbo alilowaumba Mwenyezi Mungu mpaka \"mpate kufikilia utu uzima wenu,\" mkapata nguvu ya kiakili, kimwili na nguvu zake zinginezo zote za dhahiri na za ndani, \"kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanaokufa kabla\" ya kufika utu uzima; \"na ili mfikie muda uliokwisha wekwa\" ambapo umri wenu unakuwa umeshaisha. \"Na ili mpate kutumia akili\" kuhusu hali zenu, mkajua kwamba aliyewakuza katika awamu hizi ana uwezo kamili na kwamba Yeye ndiye ambaye hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye tu, na kwamba nyinyi mna upungufu katika namna zote."},{"id":5160,"sura":40,"from_aya":68,"to_aya":68,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{68} \"Yeye ndiye anayehuisha na anayefisha.\" Kwa hivyo, nafsi yoyote haifi kwa sababu fulani au bila ya sababu isipokuwa kwa idhini yake. \"Na wala hapewi umri mwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake, ila yamo hayo katika Kitabu. Hakika hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.\" \"Akihukumu jambo,\" kubwa au dogo \"basi huliambia: Kuwa! Na linakuwa.\" Hapana wa kulizuia wala kulipinga."},{"id":5161,"sura":40,"from_aya":69,"to_aya":76,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"69. Je, huwaoni wale wanaobishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu? Wanageuziwa wapi? 70. Ambao wamekanusha Kitabu na yale tuliyowatuma Mitume wetu. Basi watakuja jua. 71. Zitakapokuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa 72. Katika maji ya moto, kisha wanaunguzwa Motoni. 73. Tena wataambiwa: Wako wapi wale mliokuwa mkiwashirikisha. 74. Badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea, bali tangu zamani hatukuwa tukiomba kitu! Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anawaachia makafiri wapotelee mbali. 75. Haya ni kwa sababu mlikuwa mkijitapa katika ardhi pasipo haki, na kwa sababu mlikuwa mkijishaua. 76. Ingieni kwenye milango ya Jahanamu, mdumu humo milele. Basi ni maovu yaliyoje makazi ya wanaotakabari! "},{"id":5162,"sura":40,"from_aya":69,"to_aya":69,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{69} \"Je, huwaoni wale wanaobishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu\" zilizo wazi kabisa ukastaajabia hali yao mbaya zaidi, \"Wanageuziwa wapi?\" Na wanaenda wapi baada ya maelezo haya kamili? Je, wanazipata kwamba kuna Aya zingine zilizowazi zinazopingana na Aya za Mwenyezi Mungu? Hapana,ninaapa kwa Mwenyezi Mungu. Au wanapata fikira potofu yoyote inayoafikiana na matamanio yao na wanaitumia kufikia batili yao?"},{"id":5163,"sura":40,"from_aya":70,"to_aya":72,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{70 - 72} Basi ni maovu kabisa waliyoyabadili na wakajichagulia wenyewe kwa kukikadhibisha Kitabu kilichowajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwatuma kwayo Mitume wake, ambao ndio bora wa viumbe wote, wakweli wao zaidi na wenye akili bora zaidi yao wote. Basi watu hawa hawana malipo yoyote ila Moto wenye mwako mkali. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawatishia kwa adhabu yake, akasema: \"Basi watakuja jua zitakapokuwa pingu shingoni mwao\" wakashindwa kutembea nazo, \"na minyororo\" ambayo wao na mashetani wao wataunganishwa pamoja \"huku wanabururwa Katika maji ya moto, kisha wanaunguzwa Motoni.\" Kisha watakaripiwa juu ya ushirikina wao na uwongo wao."},{"id":5164,"sura":40,"from_aya":73,"to_aya":74,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{73 - 74} Wataambiwa: \"Wako wapi wale mliokuwa mkiwashirikisha. Badala ya Mwenyezi Mungu?\" Je, waliwanufaisha au kuwaondolea baadhi ya adhabu? \"Watasema: Wametupotea\" na hawapo hapa, na hata wangehudhuria, hawangetusaidia kitu. Kisha wakakataa waliyofanya, wakasema: \"Bali tangu zamani hatukuwa tukiomba kitu!\" Inawezekana kwamba kilichokusudiwa na kukataa kwao huku ni kwamba walidhani kuwa huko kutawanufaisha kitu, na pia inawezekana kwamba - na hii ndiyo maana yake ya dhahiri zaidi - kwamba walikusudia kukiri ubatili wa uungu wa yale waliyokuwa wakiyaabudu, na kwamba hao si washirika wa Mwenyezi Mungu kwa uhakika, bali walipotea na wakakosea kwa kuabudu kisichokuwa na uungu wowote. Hii maana inaashiriwa na kauli yake Mola Mtukufu: \"Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anawapoteza makafiri\" kiasi kwamba wao wenyewe watakiri ubatilifu wake Siku ya Kiyama, na itawadhihirikia maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: \"Na wala hawawafuati hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ni washirika wake; Wao hawafuati ila dhana tu.\" Na hayo yanaashiriwa na kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu: \"Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu.\" Na kauli yake: \"Na ni nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama.\" Hadi mwisho wa Aya hizi."},{"id":5165,"sura":40,"from_aya":75,"to_aya":75,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{75} Na wataambiwa watu wa Motoni: \"Hiyo\" adhabu mliyopewa ya anuwai \"ni kwa sababu mlikuwa mkijitapa katika ardhi pasipo haki, na kwa sababu mlikuwa mkijishaua.\" Yaani, mlikuwa mkifurahia batili yenu na elimu mliyopingana nayo, elimu ya Mitume, na mnajishaua juu ya waja wa Mwenyezi Mungu kwa dhuluma, kuvuka mipaka na uasi, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu mwishoni mwa Sura hii: \"Basi Mitume wao walipowajia kwa ushahidi ulio wazi, walijitapa kwa elimu waliyokuwa nayo.\" Na kama vile watu wa Qaruni walivyomwambia: \"Usijigambe! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaojigamba.\" Hii ndiyo furaha inayokatazwa ambayo inasababisha mtu kuadhibiwa, tofauti na furaha inayosifiwa ambayo Mwenyezi Mungu alisema kuhusiana nayo: \"Sema: 'Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo.\" Ambayo ni kufurahia elimu yenye manufaa na matendo mema."},{"id":5166,"sura":40,"from_aya":76,"to_aya":76,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{76} \"Ingieni kwenye milango ya Jahannamu,\" kila mmoja katika tabaka lake kulingana na matendo yake, \"mdumu humo milele.\" \"Basi ni maovu yaliyoje makazi ya wale wanaotakabari!\" Ni maskani watakayohiziwa, kudunishwa, kuzuiliwa, kuadhibiwa na watakuwa kati ya joto lake na baridi yake kali."},{"id":5167,"sura":40,"from_aya":77,"to_aya":77,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"77. Basi subiri, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Na ama tukikuonyesha baadhi ya yale tuliyowaahidi au tukikufisha, lakini wao watarudishwa kwetu tu."},{"id":5168,"sura":40,"from_aya":77,"to_aya":77,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{77} Yaani, \"basi subiri\" ewe Mtume juu ya kulingania watu wako na maudhi yanayokusibu kutoka kwao, na usubiri kwa msaada wa imani yako. \"Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli.\" Atainusuru dini yake na kuliinua juu neno lake, na atawapa ushindi Mitume wake katika dunia na Akhera.Tafuta msaada juu ya hilo kwa kujua kwamba maadui zako wataadhibiwa duniani na Akhera. Na ndiyo maana akasema: \"Na ama tukikuonyesha baadhi ya yale tuliyowaahidi\" katika dunia, \"au tukikufisha\" kabla ya kuwaadhibu, \"basi kwetu tu ndiko watarudishwa.\" Kisha tutawalipa kwa matendo yao. Basi kamwe usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayoyafanya madhalimu."},{"id":5169,"sura":40,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"Kisha akamliwaza, akamfanya kuwa na subira kwa kuwataja ndugu zake Mitume, akasema:"},{"id":5170,"sura":40,"from_aya":78,"to_aya":78,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"78. Na bila ya shaka tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimulia habari zao, na wengine hatukukusimulia. Na haiwi Mtume alete Ishara yoyote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi ikija amri ya Mwenyezi Mungu, huhukumiwa kwa Haki, na hapo wapotofu watahasiri."},{"id":5171,"sura":40,"from_aya":78,"to_aya":78,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{78} Yaani, \"bila ya shaka tuliwatuma Mitume kabla yako\" kwenda kwa kaumu zao wakiwalingania na wakawa na subira kwa maudhi yao. \"Wengine katika hao tumekusimulia habari zao na wengine hatukukusimulia.\" Na Mitume wote wanaendeshwa na Mwenyezi Mungu, wala hawana uwezo wowote juu ya jambo hili. \"Na haiwi Mtume alete Ishara yoyote\" miongoni mwa ishara za kusikika na za kiakili \"ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.\" Kwa hivyo, mapendekezo ya wenye kuwapendekezea Mitume wao kuwaletea ishara fulani ni dhuluma kwa upande wao, ukaidi na kukadhibisha baada ya Mwenyezi Mungu kuwaunga mkono kwa ishara zinazoonyesha ukweli wao na usahihi wa yale waliyokuja nayo. \"Basi ikija amri ya Mwenyezi Mungu\" ili kukata hukumu kati ya Mitume na maadui zao na ushindi, \"huhukumiwa kwa Haki\" inayoanguka mahali pake na kuafikiana na usahihi kwa kuwaokoa Mitume hao na wafuasi wao na kuwaangamiza wale waliokadhibisha. Ndiyo maana akasema: \"na hapo watahasiri wana batili\" ambao wanasifika kwa batili na hata waliyoyaleta katika elimu, na matendo yote pia ni batili, na lengo lao wanalokusudia ni batili. Basi hao wanaoongeleshwa na wajihadhari wasije wakaendelea na batili yao, wakaja kuhasiri kama walivyohasiri wenzao. Kwani watu hawa si bora kuliko wao na hawakuandikiwa vitabuni kuwa wataokolewa"},{"id":5172,"sura":40,"from_aya":79,"to_aya":81,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"79. Mwenyezi Mungu aliyewajaalia nyama hoa, mifugo, ili muwapande baadhi yao, na muwale baadhi yao. 80. Na katika hao mnayo manufaa kadhaa wa kadhaa, na mnapata kwao haja zilizomo vifuani mwenu; na mnachukuliwa juu yao, na juu ya merikebu. 81. Naye anawaonyesha Ishara zake. Basi Ishara gani za Mwenyezi Mungu mnazozikataa? "},{"id":5173,"sura":40,"from_aya":79,"to_aya":80,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{79 - 80} Mola Mtukufu anawakumbusha waja wake juu ya neema aliyowapa ya wanyama wa mifugo, ambao wananeemeka kwa neema nyingi kutoka kwao. Miongoni mwake ni manufaa ya kuwapanda na kuwabeba, na manufaa ya kula nyama zao na kunywa katika maziwa yao. Na miongoni mwake kuna manufaa ya kupata joto na kutengeneza vyombo na bidhaa mbalimbali kutokana na sufu zao, manyoya yao na nywele zao. Na manufaa mengineyo. \"Na mnapata kwao haja zilizomo vifuani mwenu,\" kama vile kufika nchi za mbali na wamiliki wao kupata furaha kutokana nao. \"Na mnachukuliwa juu yao na juu ya merikebu.\" Mwenyezi Mungu ndiye aliyevitiisha kwa ajili yenu na akaviandalia visababu ambavyo haviwezi kuwapa manufaa haya isipokuwa kwa visababu hivyo."},{"id":5174,"sura":40,"from_aya":81,"to_aya":81,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{81} \"Naye anawaonyesha Ishara zake\" zinazoonyesha upweke wake, majina yake na sifa zake. Hii ni miongoni mwa neema zake kubwa; ambapo aliwafanya waja wake kushuhudia ishara zake za kinafsi na za kiupeo wa macho, na neema zake zinazong'aa. Na akawaorodheshea zote ili wapate kumjua, kumshukuru na kumtaja. \"Basi Ishara gani za Mwenyezi Mungu mnazozikataa?\" Kwani imeshathibiti kwenu kwamba ishara zote na neema zote zinatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa hivyo kukataa hakuna mahali popote wala kuzipa mgongo hakuna nafasi yoyote. Bali zinawalazimu wenye akili ya juu kujitahidi na kufanya uwezo wao katika kumtii na kujitolea kabisa katika kumtumikia Yeye tu."},{"id":5175,"sura":40,"from_aya":82,"to_aya":85,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"82. Kwani hawatembei katika ardhi wakaona namna ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Wao walikuwa wengi kuliko hawa, na wamewashinda kwa nguvu na athari katika nchi. Wala hayakuwafaa hayo waliyokuwa wakiyachuma. 83. Walipowajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, walijitapa kwa elimu waliyokuwa nayo. Basi yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara. 84. Walipoiona adhabu yetu, walisema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni wa pekee, na tunaikataa miungu tuliyokuwa tukiishirikisha naye. 85. Lakini imani yao haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati ambao wamekwishaiona adhabu yetu. Huu ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu uliokuwa kwa waja wake. Na hapo waliokufuru walihasiri. "},{"id":5176,"sura":40,"from_aya":82,"to_aya":82,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{82} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawahimiza wale waliomkadhibisha Mtume wao kuzunguka ardhini kwa miili yao na nyoyo zao, na wawaulize walimwengu \"ili waweze kuona\" kwa njia ya kufikiria na kuchukua yale watakayoyaona kuwa hoja, na siyo kuona kwa kughafilika tu na kupuuza. \"Ulikuwaje mwisho wa wale waliokuwa kabla yao\" miongoni mwa umma waliotangulia, kama vile kina 'Adi, Thamud na wengineo miongoni mwa wale waliokuwa na nguvu zaidi yao na ambao walikuwa na athari kubwa zaidi katika ardhi katika suala la majengo madhubuti, upandaji miti mizuri na mazao mengi? \"Wala hayakuwafaa hayo waliyokuwa wakiyachuma\" wakati walipojiwa na amri ya Mwenyezi Mungu, wala nguvu zao hizo hazikuwafaa kitu, wala hawakuweza kujikomboa kwa mali zao, wala hawakuweza kujikinga kwa ngome zao."},{"id":5177,"sura":40,"from_aya":83,"to_aya":83,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{83} Kisha akataja uhalifu wao mkubwa, akasema: \"Mitume wao walipowajia kwa ushahidi ulio wazi\" kutoka katika Vitabu vya Mwenyezi Mungu na miujiza mikubwa, na elimu yenye manufaa yenye kubainisha uongofu mbali na upotovu na haki mbali na batili, \"wakajitapa kwa elimu waliyokuwa nayo\" ambayo inapingana na dini ya Mitume wao. Na inajulikana vyema kuwa furaha yao hiyo inaashiria ukubwa wa kuridhika kwao nayo, kushikamana kwao nayo na uadui wao dhidi ya haki waliyokuja nayo Mitume wao, na wakaifanya batili kuwa ndiyo haki. Hili ni jambo la jumla katika elimu zote ambazo zilitumika kupinga yale ambayo Mitume walikuja nayo, ambazo aina yake inayostahili zaidi kuingizwa katika hili ni elimu ya falsafa na mantiki ya Kigiriki, ambayo kwayo aya nyingi za Qur-ani Tukufu zilikataliwa na thamani yake ikapungua katika nyoyo, na ushahidi wake wa yakini na wa uhakika mkubwa ukafanywa kuwa ushahidi wa kilafudhi tu usio na yakini yoyote, na zikatangulizwa mbele yake akili za watu wa upumbavu na ubatili. Haya ni miongoni mwa njia kubwa zaidi za kupindukia katika ishara za Mwenyezi Mungu na kuzipinga. Basi Mwenyezi Mungu ndiye tunayemuomba msaada. \"Basi yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara.\" Yaani, adhabu waliyokuwa wakiifanyia mzaha ikawashukia."},{"id":5178,"sura":40,"from_aya":84,"to_aya":84,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{84} \"Walipoiona adhabu yetu,\" wakakiri pale ambapo kukiri hakuwezi kuwafaa, na \"Wakasema: 'Tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni wa pekee na tunaikataa miungu tuliyokuwa tukiishirikisha naye\" miongoni mwa masanamu na vyote vinavyoabudiwa badala yake, na tumejitenga mbali na kila kinachopingana na Mitume miongoni mwa elimu au matendo."},{"id":5179,"sura":40,"from_aya":85,"to_aya":85,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{85} \"Lakini imani yao haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati ambao wamekwishaiona adhabu yetu\" katika hali hiyo, na hii ndiyo \"ada ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa kwa waja wake.\" Ya kwamba wale wanaokadhibisha wanapoteremshiwa adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso yake ikiwa wataamini, Imani yao hiyo haiwezi kuwa sahihi na wala haiwezi kuwaokoa kutokana na adhabu hiyo. Hili ni kwa sababu ilikuwa ni imani ya lazima waliyolazimika kufanya, kwani ilikuwa ni imani baada ya kuona uhakika wa mambo. Lakini imani yenye manufaa, inayomuokoa mwenye kuamini ni imani ya hiari, ambayo ni kuamini mambo ya ghaibu, na hiyo huwa kabla ya kuwepo dalili za adhabu. \"Na hapo wale waliokufuru walihasiri\" Dini yao, dunia yao na akhera yao. Na hata harasa tu katika nyumba hiyo haitoshi, bali lazima watapata hasara ambayo itakuwa mbaya zaidi katika adhabu kali na wadumu milele ndani yake."},{"id":5180,"sura":40,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Mu'min kwa sifa za Mwenyezi Mungu, upole wake na msaada wake, sio kwa uwezo wetu na nguvu zetu. Basi ni zake shukrani na sifa nzuri."},{"id":5181,"sura":40,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"***"}]}