{"result":[{"id":5254,"sura":42,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Ash-Shura"},{"id":5255,"sura":42,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":5256,"sura":42,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu."},{"id":5257,"sura":42,"from_aya":1,"to_aya":9,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Ha Mim 2. 'Ayn Sin Qaf 3. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mwenye hekima anavyokuletea Wahyi wewe na walio kabla yako. 4. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi. Na Yeye ndiye aliye juu zaidi, Mkuu. 5. Zinakaribia mbingu kupasuka juu huko, na Malaika wakimtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi, na wakiwaombea maghfira waliomo kwenye ardhi. Ama hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu sana. 6. Na wale waliowafanya walinzi wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi bora juu yao. Wala wewe si wakili juu yao. 7. Na namna hivi tumekufunulia Qur-ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa Miji na wale walio pembezoni mwake. Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo. Kundi moja litakuwa Peponi na kundi jengine katika Moto wenye mwako mkali. 8. Na Mwenyezi Mungu angelipenda, angewafanya wote umma mmoja, lakini anamwingiza katika rehema yake amtakaye. Na wenye kudhulumu hawana mlinzi wala msaidizi. 9. Au wamechukua walinzi wengine badala yake! Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi hasa. Na Yeye ndiye anayehuisha wafu. Na Yeye ndiye Muweza zaidi wa kila kitu. "},{"id":5258,"sura":42,"from_aya":1,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1 - 5} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatujulisha kwamba aliiteremsha Qur-ani hii tukufu kwa Mtume mtukufu, kama alivyoteremsha ufunuo pia kwa Mitume na Mitume wa kabla yake. Ndani yake kuna maelezo ya fadhila zake kwa kuteremsha Vitabu na kutuma Mitume kabla na baada yake, na kwamba Muhammad \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake \u2013 si wa mwanzo miongoni mwa Mitume, na kwamba njia yake ni njia ile ile ya wale waliotangulia kabla yake, na hali zake zinawiana na hali za Mitume waliotangulia kabla yake, na yale aliyokuja nayo yanafanana na yale waliyokuja nayo. Kwa sababu yote hayo ni haki na ukweli. Na ni ufunuo wa yule ambaye ana sifa ya uungu, utukufu mkubwa, na hekima kubwa, na kwamba ulimwengu wote wa juu na wa chini ni mali yake, na kiko chini ya uendeshaji wake wa kimungu na wa kisheria, na kwamba Yeye ndiye \"Aliye juu zaidi\" kwa dhati yake, cheo chake na ushindi wake. \"Mkuu\" ambaye kwa sababu ya ukuu wake na \"ukubwa wake, \"Zinakaribia mbingu kupasuka juu huko\" licha ya ukubwa wake na licha ya kuwa kwake mkuu, vitu visivyo na uhai \"na Malaika\" watukufu, walio karibu na Mwenyezi Mungu, wananyenyekea kwa utukufu wake na wanatii kwa sababu ya utukufu wake, na wanajisalimisha kwa umola wake \"wakimtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi,\" na wanampa taadhima kutokana na kila upungufu na wanamsifu kwa kila ukamilifu, \"na wakiwaombea maghfira waliomo kwenye ardhi\" kwa sababu ya yale wanayoyafanya miongoni mwa mambo yasiyoufailia ukuu wa Mola wao Mlezi na ukubwa wake, pamoja na kwamba Yeye Mtukufu ni \"Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu sana.\" Ambaye kama si msamaha wake na rehema zake, basi angeharakisha kuwaadhibu viuumbe kwa adhabu ya kuwaangamiza. Na katika kumsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sifa hizi baada ya kutaja kuwa aliwateremshia ufunuo Mitume wote kwa ujumla na kwa Muhammad \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwashukie \u2013 hususan, kuna ishara kwamba Qur-ani hii tukufu ina ushahidi, uthibitisho, ishara zinazoonyesha ukamilifu wa Muumba Mtukufu, na kumsifu kwa majina haya makubwa ambayo yanalazimu nyoyo kujaa kumjua, kumpenda, kumpa taadhima, kumtukuza, kumheshimu na kumfanyia aina zote za ibada za dhahiri na zilizofichikana, na kwamba katika dhuluma kubwa zaidi na maneno machafu zaidi ni kumfanyia wenza, ambao hawawezi kufaidi wala kudhuru, bali wameumbwa, na wanamhitaji Mwenyezi Mungu katika hali zao zote."},{"id":5259,"sura":42,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} Ndiyo maana akaifuata kwa kauli yake:  \"Na wale waliowafanya walinzi wengine badala yake Yeye,\" ambao wanawafanya kuwa walinzi kwa kuwaabudu na kuwatii kama vile wanavyomwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumtii, basi hakika hao waliowachukua ni batili, wala sio walinzi kiuhakika. \"Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi bora juu yao,\" anawahifadhia matendo yao na atawalipa kwa mema yake na maovu yake. \"Wala wewe si wakili juu yao\"  ndiyo uulizwe juu ya matendo yao. Bali wewe ni mfikishaji tu, na tayari ulishafanya kazi yako."},{"id":5260,"sura":42,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Kisha akataja neema yake kwa Mtume wake na kwa watu, ambapo Mwenyezi Mungu aliteremsha \"Qur-ani kwa Kiarabu,\" yenye maneno na maana zilizobainishwa, \"ili uwaonye watu wa Mama wa Miji\" ambao ni Makka tukufu, \"na wale walio pembezoni mwake\" miongoni mwa vijiji vya Waarabu. Kisha onyo hili lienee hadi kwenye viumbe vilivyobakia. \"Na uhadharishe\" watu \"Siku ya Mkutano\" ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho, na uwaambie kwamba \"haina shaka hiyo\" na kwamba viumbe watagawanyika siku hiyo makundi mawili: kundi moja \"litakuwa Peponi.\" Hao ndio waliomuamini Mwenyezi Mungu na wakawasadiki Mitume. Na kundi lingine litakuwa \"katika Moto wenye mwako mkali.\" Na hao ni aina mbalimbali za makafiri wanaokadhibisha."},{"id":5261,"sura":42,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} \"Na\" pamoja na haya, lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka, angeliwafanya watu wote \"umma mmoja\" katika uongofu. Kwa sababu Yeye ndiye Muweza, ambaye hakuna lisilowezekana kwake. Lakini alitaka kumuingiza katika rehema yake amtakaye miongoni mwa viumbe vyake maalumu. Na ama madhalimu ambao hawawezi kutengenea kwa kufanya mambo mema, hao wamenyimwa rehema ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo hawana mlinzi yeyote badala ya Mwenyezi Mungu atakayewalinda ili wapate wanayopenda, wala wa kuwanusuru atakayewaondolea wanayochukia."},{"id":5262,"sura":42,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} Na wale waliojifanyia walinzi badala yake kwa kuwaabudu, basi walifanya kosa baya zaidi; \"Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi hasa\" ambaye mja wake anapaswa kumfanya kuwa Mlinzi wake kwa kumwabudu, kumtii Yeye na kujikurubisha kwake kwa namna yoyote ile iwezekanayo ya kujikurubisha. Naye anawasimamia waja wake kwa ujumla kwa uendeshaji wake na kutekeleza mipango yake juu yao, na anawalinda waja wake waumini hasa kwa kuwatoa katika viza na kuwapeleka kwenye nuru, akiwalea kwa upole wake na kuwasaidia katika mambo yao yote. \"Na Yeye ndiye anayehuisha wafu. Na Yeye ndiye Mweza zaidi wa kila kitu.\" Yaani, Yeye ndiye anayehuisha na kufisha, na kutekeleza mapenzi yake na uwezo wake. Basi Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake, bila mshirika yeyote."},{"id":5263,"sura":42,"from_aya":10,"to_aya":12,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"10. Na mkihitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi ninayemtegemea, na kwake Yeye narejea. 11. Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi. Amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika nyama hoa dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kuona sana. 12. Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi zaidi wa kila kitu. "},{"id":5264,"sura":42,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na mkihitalifiana katika jambo lolote\" katika misingi ya dini yenu na matawi yake, katika yale msiyokubaliana juu yake, \"basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu.\" Inarejeshwa kwenye Kitabu chake na kwa Sunna za Mtume wake. Kwa hivyo, hukumu watakayotoa, basi hiyo ndiyo kweli. Na chochote kilicho kinyume nayo, basi hicho ni batili. \"Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi.\" Yaani, kama vile Yeye Mtukufu ndiye Mola Mlezi, Muumba, Mwenye kuruzuku, Mwendeshaji mambo, basi Yeye ndiye atakayehukumu kati ya waja wake kwa mujibu wa sheria yake katika mambo yao yote. Maana isiyo ya moja kwa moja ya Aya hii tukufu ni kwamba makubaliano ya umma huu ni hoja ya uhakika. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hakutuamrisha kumrudishia isipokuwa yale tuliyohitalifiana juu yake. Kwa hivyo, kile tulichokubaliana juu yake kinautosha umma huu makubaliano yao juu yake. Kwa sababu, umma huu umehifadhiwa kutokana na suala la kukubaliana juu ya kosa, na lazima makubaliano yao yawe kwa mujibu wa yale yaliyomo katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake. Na kauli yake: \"Kwake ndiye ninayemtegemea,\" yaani, nilimtegemea kwa moyo wangu katika kuleta manufaa na kuepusha madhara nikiwa na imani naye Mtukufu anisaidie katika hayo. \"Na kwake Yeye narejea,\" yaani, ninauelekeza moyo wangu na mwili wangu kwake, na ninaelekea katika utiifu wake na kumfanyia ibada. Hii miwili ni misingi ambayo mara nyingi Mwenyezi Mungu anaitaja katika Kitabu chake. Kwa sababu,kwa ujumla wake mja hufikia ukamilifu na pia hukosa ukamilifu kwa kukosa mawili hayo au moja yake. Kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Wewe tu tunakuabudu na Wewe tu tunakuomba msaada,\" na kauli yake, \"Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye.\u201d"},{"id":5265,"sura":42,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} \"Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi.\"  Yaani, Muumba wake kwa uwezo wake, mapenzi yake na hekima yake. \"Amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu\" ili mpate utulivu kwao, na dhuria wenu waenee baina yenu, na muweze kupata manufaa mbalimbali. \"Na katika nyama hoa, dume na jike\" kutoka katika aina zake zote ili waendelee kubakia na kukua kwa manufaa yenu mengi, na ndiyo maana akasema: \"Anakuzidishieni namna hii\" nyinyi na mifugo wenu. \"Hapana kitu kama mfano wake\" katika viumbe vyake, si katika dhati yake, wala katika majina yake, wala katika sifa zake, wala katika vitendo vyake. Kwa sababu majina yake yote ni mazuri zaidi, sifa zake ni sifa za ukamilifu na ukuu, na vitendo vyake Mola Mtukufu ndivyo alivyoumba kwavyo viumbe vikubwa bila ya mshirika yeyote. Basi hapana kitu kama mfano wake kwa sababu ya upekee wake na umoja wake katika ukamilifu kwa namna zote. \"Naye ni Mwenye kusikia mno\" sauti zote kwa lugha mbali mbali, kwa mahitaji mbalimbali. \"Mwenye kuona sana,\" ambaye anaona kutambaa kwa chungu mweusi katika usiku wa giza zaidi juu ya jiwe gumu. Na anaona mtiririko wa chakula kinapopita katika viungo vya wanyama wadogo sana, na mtiririko wa maji yanapopita katika matawi madogo mno. Aya hii na nyinginezo mfano wake ni ushahidi wa dhehebu la Ahlus-Sunna wal-Jamaa katika kuthibitisha sifa na kukanusha kufanana kwake na viumbe, na pia ina jibu kwa wenye kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe katika kauli yake: \"Hapana kitu kama mfano wake,\" na pia kuna jibu kwa wale wanaopinga sifa za Mwenyezi Mungu katika kauli yake: \"Naye ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kuona sana.\""},{"id":5266,"sura":42,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Na kauli yake: 'Yeye ndiye Mwenye mbingu na ardhi.' Yaani, ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, na mkononi mwake ndio kuna funguo za rehema, riziki na neema za dhahiri na zilizofichikana. Kila kiumbe kinamhitaji Mwenyezi Mungu katika kuleta masilahi yao na kuzuia madhara katika hali zote. Mambo hayo hayako katika mkono wa mwingine yeyote. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mwenye kupeana, Mwenye kuzuia, Mwenye kudhuru, Mwenye kunufaisha, ambaye hakuna neema yoyote waliyonayo waja isipokuwa ni kutoka kwake. Na wala hakuna anayeweza kuzuilia maovu isipokuwa Yeye. Na rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu, basi hapana wa kuizuia. Na anayoizuia, hapana wa kuipeleka isipokuwa Yeye. Ndiyo maana akasema, \"Humkunjulia riziki amtakaye\" akampa katika aina mbalimbali za riziki \"na humpimia amtakaye\" ikawa inatosha tu haja yake, si zaidi yake. Na yote haya ni kulingana na elimu yake na hekima yake. Ndiyo maana akasema: \"Hakika Yeye ni Mjuzi zaidi wa kila kitu\" Anazijua hali za waja wake, na anampa kila mmoja wao yale yanayolingana na hekima yake na yanayotaka mapenzi yake."},{"id":5267,"sura":42,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"13. Amekuamrisheni Dini ile ile aliyomuusia Nuhu na tuliyokufunulia wewe, na tuliyowausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayowaitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye."},{"id":5268,"sura":42,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Hii ndiyo neema kubwa kabisa aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu waja wake, kwamba amewawekea sheria ya Dini nzuri kabisa, iliyo bora kabisa, iliyotakasika kabisa na iliyo safi kabisa. Dini ya Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu aliiweka kama sheria kwa ajili ya wateule miongoni mwa waja wake. Bali Mwenyezi Mungu aliiweka kama sheria kwa ajili ya wale walio bora zaidi na walio juu zaidi, ambao ni wale wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume waliotajwa katika aya hii. Ambao ndio wenye daraja ya juu zaidi ya viumbe wote, na wakamilifu zaidi kati yao kwa njia zote. Kwa hivyo, Dini hii ambayo Mwenyezi Mungu amewawekea kama sheria lazima izifailie hali zao na iendane na ukamilifu wao. Bali Mwenyezi Mungu aliwakamilisha na kuwachagua kwa sababu waliitekeleza. Kama si dini ya Uislamu, basi hakuna yeyote angeinuka juu miongoni mwa viumbe. Hiyo ndiyo roho ya furaha na sehemu ya kati ya jiwe la kusagia la ukamilifu. Hayo ndiyo ambayo Kitabu hiki adhimu kinajumuisha na kuyalingania, kama vile kumpwekesha Mwenyezi Mungu, matendo, maadili na adabu mbalimbali. Ndiyo maana akasema kwamba \"shikeni dini sawasawa\" kwa kutekeleza sheria zote za dini, misingi yake na matawi yake. Mnaisimamisha juu ya nafsi zenu wenyewe, na mnajitahidi kuisimamisha kwa wengineo, na mnasaidiana katika wema na uchamungu. Wala hamsaidiani katika dhambi na uadui, \"wala msifarikiane kwayo.\" Yaani, fanyeni makubaliano baina yenu juu ya misingi ya dini na matawi yake, na fanyeni bidii kujihadharini mambo yasije yakawafarakanisha masuala mbalimbali na kuwafanya kuwa makundi makundi, mkawa maadui wenyewe kwa wenyewe licha ya kwamba mnaafikiana katika msingi wa dini yenu. Miongoni mwa aina za kukusanyika pamoja juu ya dini na kutogawanyika ndani yake ni mikusanyiko ya hadhara iliyoamrishwa na sheria. Kama vile mkusanyiko wa Hija, Idi, swala ya Ijumaa, swala tano za kila siku, Jihadi na ibada zinginezo ambazo haziwezi kukamilika wala kutimia isipokuwa kwa kukusanyika pamoja, kutotengana. \"Ni magumu kwa washirikina hayo unayowaitia;\" pale ulipowaita kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumkusudia Yeye peke yake. Kama alivyosema kuwahusu: \"Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake nyoyo za wasioiamini Akhera huchafuka. Na wanapotajwa wenginewe asiyekuwa Yeye basi wao hufurahi.\" Na kusema kwao: \"Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu.\" \"Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye.\" Yaani, anawateuwa miongoni mwa viumbe vyake wale anaowajua kuwa wanafaa kuteuliwa kwa ajili ya ujumbe wake na kuwa vipenzi wake. Na miongoni mwa hilo ni kwamba aliuchagua umma huu na akauboresha kuliko umma nyinginezo zote na akauchagulia dini nzuri na bora zaidi, \"na humwongoa kwake aelekeaye.\" Hii, yaani kurudi kwa Mwenyezi Mungu, ndiyo sababu anayofanya mja na ambayo kupatia kwayo anafikia kuongolewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na pia matamanio ya moyo wake kuelekea kwake na kuukusudia uso wake. Kwa hivyo, nia njema ya mja pamoja na bidii yake katika kutafuta uwongofu ni mojawapo ya sababu za kurahisishiwa kuufikia. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama.\" Katika Aya hii, kuna kwamba Mwenyezi Mungu \"humwongoa kwake aelekeaye\" kwake, pamoja na kauli yake: \"nawe ishike njia ya anayeelekea kwangu.\" Na pamoja na kujua hali za Maswahaba wa Mtume wake, Mwenyezi Mungu awawiye radhi, na wingi wa kurejea kwao kwake, kuna ushahidi kwamba maneno yao ni ushahidi, hasa Mahalifa waongofu wa Mtume wake, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote."},{"id":5269,"sura":42,"from_aya":14,"to_aya":15,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"14. Na hawakufarikiana ila baada ya kuwajia elimu kwa sababu ya husuda iliyokuwa baina yao. Na lau kuwa haikwisha tangulia kauli kutoka kwa Mola wako Mlezi ya kuahirisha mpaka muda maalumu, basi bila ya shaka pangelihukumiwa baina yao. Na hakika wale waliorithishwa Kitabu baada yao wanakitilia shaka inayowahangaisha. 15. Basi kwa haya waite! Nawe simama sawa sawa kama ulivyoamrishwa, wala usiyafuate matamanio yao. Na sema: 'Ninaamini aliyoteremsha Mwenyezi Mungu katika Vitabu. Na nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu. Mwenyezi Mungu ni Mola wetu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Sisi tuna jukumu kwa vitendo vyetu, na nyinyi mna jukumu kwa vitendo vyenu. Hapana kuhojiana baina yetu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu atatukusanya pamoja, na marejeo ni kwake.' "},{"id":5270,"sura":42,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowaamrisha Waislamu kuungana katika dini yao, na akawakataza kutengana, akawaambia wasidanganywe na aliyowateremshia Mwenyezi Mungu katika Kitabu. Kwani, Watu wa Kitabu hawakutawanyika, mpaka Mwenyezi Mungu alipowateremshia Kitabu kinachowataka wakusanyike, lakini wakafanya kinyume na kile kilichoamrishwa na Kitabu chao, na yote hayo ni kwa sababu ya dhuluma na uadui wao. Kwani walichukiana wao kwa wao na wakahusudiana, na ukazuka ugomvi na uadui kati yao, kwa hivyo wakahitilafiana. Basi jihadharini enyi Waislamu msiwe kama wao. \"Na lau kuwa haikwishatangulia kauli kutoka kwa Mola wako Mlezi\" ya kuchelewesha adhabu ya kuwaangamiza hadi muda maalumu, \"basi bila ya shaka palingelihukumiwa baina yao.\" Lakini hekima yake na ustahimilivu wake ulihitaji wacheleweshewe hilo. \"Na hakika wale waliorithishwa Kitabu baada yao\" wakawa mafuatizi wao miongoni mwao wale ambao wamehusishwa na elimu \"wanakitilia shaka inayo wahangaisha.\" Kwa maana, watangulizi wao walitofautiana kwa sababu ya dhuluma na uadui; kwa hivyo wafuatizi wao nao wakahitalifiana kwa sababu ya shaka na kusitasita. Na hao wote ni sawa katika kuhitilafiana kwao kubaya."},{"id":5271,"sura":42,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15} \"Basi kwa haya waite!\" Yaani, kwa ajili ya Dini iliyo madhubuti, na njia iliyonyooka, ambayo Mwenyezi Mungu aliteremsha kwayo vitabu vyake, na akawatuma Mitume wake. Basi waite umma wako kwa hiyo, na wahimize kwayo, na pambana kwa ajili yake wale wasioikubali. \"Nawe simama sawa sawa\" mwenyewe \"kama ulivyoamrishwa\" kwa kuafikiana na amri ya Mwenyezi Mungu; si kwa kupitisha kiwango wala kupuuza, bali kwa kutekeleza sawasawa amri za Mwenyezi Mungu na kuepuka makatazo yake kwa kuendelea daima. Hapa, alimuamuru ajikamilishe mwenyewe kwa kushikamana suala la kusimama sawasawa, na pia akamuamrisha kuwakamilisha wengine kwa kuwalingania kwenye hilo. Na inajulikana vyema kwamba anapoamrishwa Mtume \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake \u2013 basi hiyo pia inakuwa ni amri kwa umma wake ikiwa amri hiyo haikukusudiwa yeye hasa. \"Wala usiyafuate matamanio yao.\" Yaani, matamanio ya wale wanaokengeuka mbali na dini, kama vile makafiri na wanafiki. Ima kwa kuwafuata katika baadhi ya mambo ya dini yao, au kwa kuacha kulingania kwa Mwenyezi Mungu, au kwa kuacha kusimama sawasawa. Kwani, kama utayafuata matamanio yao baada ya kukufikia elimu, hakika hapo utakuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. Hapa, hakusema kwamba usifuate dini yao. Kwa sababu uhakika wa Dini yao aliyowawekea Mwenyezi Mungu ni Dini ya Mitume wote, lakini hawakuifuata. Bali walifuata matamanio yao na wakaifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo. \"Na sema\" uwaambie unapojadiliana nao \"'Ninaamini aliyoteremsha Mwenyezi Mungu katika Vitabu;'\" na majadiliano yako yajengeke juu ya msingi huu mkubwa unayoashiria heshima ya Uislamu, utukufu wake na ushindi wake dini zote, na kwamba dini wanayodai Watu wa Kitabu kuwa wako ndani yake ni sehemu ya Uislamu. Katika hili kuna maelekezo kwamba ikiwa Watu wa Kitabu watafanya majada kwa hoja ya kuamini baadhi ya vitabu au baadhi ya Mitume peke yao, basi hilo halikubaliwi kutoka kwao. Kwa sababu Kitabu wanachokiitia na Mtume wanayemjinasibisha naye ni sharti kwake kwamba awe anaisadiki Qur-ani hii na yule aliyekuja nayo. Kitabu chetu na Mtume wetu hakutuamrisha isipokuwa kuamini Musa, na Isa, na Taurati, na Injili ambavyo kilituambia juu yake, na kikavisadiki, na kikajulisha kwamba hivyo vinakisadikisha na kukubali usahihi wake. Na ama Taurati tu, na Injili, na Musa na Isa, ambavyo hatukuelezwa sifa zake na wala havikukubaliana na kitabu chetu, hivyo hakutuamrishwa kuviamini. Na kauli yake: \"Na nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu\" ninapohukumu katika yale mliyohitalifiana ndani yake. Kwa hivyo, sifai kuzuiwa na uadui wenu na chuki yenu, enyi Watu wa Kitabu, kuwa mwadilifu baina yenu. Na kufanya uadilifu katika kuhukumu baina ya Watu wa Kitabu na watu wengine waliohitilafiana ni kukubali yale waliyo nayo ya haki na kuyakataa waliyo nayo ya batili. \"Mwenyezi Mungu ni Mola wetu Mlezi, na Mola wenu Mlezi.\" Yaani, Yeye ndiye Mola Mlezi wetu sote, nanyi hamumstahiki zaidi kutuliko sisi. \"Sisi tuna jukumu kwa vitendo vyetu na nyinyi mna jukumu kwa vitendo vyenu,\" vya heri na vya shari. \"Hapana kuhojiana baina yetu na nyinyi.\" Yaani, baada ya uhakika kubainika na hali kuwa wazi mbali na batili, na uwongofu mbali na upotofu, basi hakuna nafasi yoyote iliyobakia ya mjadala na mabishano. Kwa sababu, makusudio ya mjadala ni kubainisha haki mbali na batili ili mwenye kutaka usawa apate kuongoka, na ili hoja isimame juu ya mpotevu. Lakini, maana yake si kwamba hairuhusiwi kujadiliana na Watu wa Kitabu. Vipi isiruhusiwe ilhali Mwenyezi Mungu anasema: \"Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa.\" Lakini kinachokusudiwa ni kile tulichotaja. \"Na Mwenyezi Mungu atatukusanya pamoja, na marejeo ni kwake.\" Siku ya Kiyama, na atamlipa kila mmoja kwa matendo yake, na hapo atabainika mkweli kutokana na mwongo."},{"id":5272,"sura":42,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"16. Na wale wanaohojiana juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kukubaliwa, hoja za hawa ni batili mbele ya Mola wao Mlezi, na juu yao ipo ghadhabu, na itakuwa kwao adhabu kali."},{"id":5273,"sura":42,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} Huku ni kuthibitisha kauli yake: \"Hapana kuhojiana baina yetu na nyinyi.\" Na hapa akajulisha kwamba, \"Na wale wanaohojiana juu ya Mwenyezi Mungu\" kwa hoja batili na fikira potofu zenye kupingana \"baada ya kukubaliwa,\" yaani baada ya wale wenye akili na ufahamu mkubwa kumwitikia Mwenyezi Mungu kwa sababu ya yale aliyowabainishia ya Aya za uhakika na hoja zilizo wazi; basi hawa wanaobishana na haki baada ya kudhihirika kwake, \"hoja za hawa ni batili mbele ya Mola wao Mlezi.\" Kwa sababu inajumuisha kuikataa haki, na kila kitu kinachopinga haki ni batili, \"na juu yao ipo ghadhabu\" kwa sababu ya uasi wao na kuzipa kwao mgongo hoja za Mwenyezi Mungu na ishara zilizo wazi na kuzikadhibisha kwao. \"Na itakuwa kwao adhabu kali,\" kwa sababu ndiyo athari ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu juu yao. Basi hii ni adhabu ya kila anayebishana na haki kwa ajili ya batili."},{"id":5274,"sura":42,"from_aya":17,"to_aya":18,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"17. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeteremsha Kitabu kwa Haki na Mizani. Na ni nini kitakachokujulisha ya kwamba pengine Saa ya Kiyama ipo karibu? 18. Wale wasioiamini huihimiza hiyo Saa ifike upesi, lakini wale wanaoamini wanaiogopa na wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli. Ama kwa hakika hao wanaobishana katika habari za hiyo Saa wamo katika upotofu wa mbali kabisa. "},{"id":5275,"sura":42,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuwa hoja zake ziko wazi na zimeshabainika, kiasi kwamba kila aliye na heri ndani yake aliziitikia, akataja asili yake na msingi wake, bali hoja zote alizozifikisha kwa waja zinarejea kwake. Akasema: \"Mwenyezi Mungu ndiye aliyeteremsha Kitabu kwa Haki na Mizani.\" Kwa hivyo, kitabu ni Qur-ani tukufu ambayo iliteremka kwa haki, na inajumuisha haki, ukweli na yakini. Na yote ni aya zilizo wazi na ushahidi wa wazi wa matakwa ya Mwenyezi Mungu na itikadi zote za kidini. Kwa hivyo, ikawa imekuja na masuala bora zaidi na ushahidi ulio wazi zaidi. Na ama mizani hiyo ni uadilifu na kupima kwa mujibu wa mlinganisho sahihi na akili iliyo sawa. Kwani ushahidi wote wa kiakili, kama vile ishara za kiupeo wa macho na za kinafsi, mazingatio ya kisheria, matukio mbalimbali, sababu mbalimbali, hukumu mbalimbali na hekima, vyote vinajumuishwa katika mizani ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiteremsha na akaiweka miongoni mwa waja wake ili wapime kwayo aliyoyathibitisha na aliyoyakanusha miongoni mwa mambo, na ili kwayo wajue ukweli wa yale aliyojulisha na yale ambayo Mitume wake walijulisha. Kwa hivyo, lolote linalotoka nje ya mawili haya - Kitabu na mizani - miongoni mwa yote yaliyosemwa kwamba ni hoja, au uthibitisho au ushahidi au maneno yanayofanana na hayo, hayo ni batili yanayopingana, ambayo misingi yake ilikwisha haribika na mijengo yake na matawi yake yakabomoka. Hayo anayajua mwenye kuyachunguza vyema masuala mbalimbali na namna yanavyochukuliwa, na akajua kutofautisha kati ya hoja iliyo sahihi zaidi kuliko hoja zinginezo, na tofauti iliyoko kati ya hoja na fikira potofu tu. Na ama yule ambaye amedanganyika na maneno yaliyopambwa na maneno yaliyofichwa ukweli wake na ufahamu wake haukupenya ukafika kwenye maana iliyokusudiwa, basi yeye hakika si katika wanasanaa hii, wala si katika mashujaa wa uwanja huu. Kukubaliana kwake na kutokubali kwake ni sawa. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, akiwatia hofu wale wanaotaka Saa ya Kiyama kufika haraka ambao wanaikataa: \"Na ni nini kitakachokujulisha ya kwamba pengine Saa ya Kiyama ipo karibu?\" Yaani, haujulikani umbali wake wala itatokea lini. Inatarajiwa na kuhofiwa kutokea wakati wowote ule."},{"id":5276,"sura":42,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} \"Wale wasioiamini hutaka hiyo Saa ifike upesi\" kwa sababu ya ukaidi, kuikadhibisha na kutaka kumuonyesha Mola wao Mlezi kwamba hawezi kitu. \"Lakini wale wanaoamini wanaiogopa\" kwa sababu ya kuiamini kwao na kujua kwao yale yaliyo ndani yake ya malipo kwa matendo, na hofu yao kwa kumjua kwao Mola wao Mlezi, kwamba huenda matendo yao hayatawaokoa wala kuwaletea furaha. Ndiyo maana akasema: \"na wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli\" isiyo na shaka yoyote. \"Ama kwa hakika hao wanaobishana katika habari za hiyo Saa.\" Baada ya kuwa na shaka nayo, wakashindana na Mitume na wafuasi wao. Wao wamo katika upotofu \"wa mbali kabisa\" ambao hauko karibu na haki. Kwani ni umbali gani ulio mbali zaidi kuliko yule anayeikadhibisha nyumba ambayo ndiyo nyumba kwa hakika? Nayo ndiyo nyumba ambayo aliumbwa kwa ajili ya kuendelea kuwepo na kudumu milele. Nayo ndiyo nyumba ya malipo ambayo Mwenyezi Mungu alitadhihirishia huko uadilifu wake na fadhila yake. Na hakika nyumba hii kwa kulinganishwa na ile ya akhera ni kama mtu aliyepanda kipando, kisha akalala kidogo katika kivuli cha mti, kisha akaondoka na akauacha. Nayo ni nyumba ya kupita, na si nyumba ya kutua humo. Basi wakaisadiki nyumba inayofifia na kuisha kwa kuiona na kuishuhudia, na wakakadhibisha nyumba ya akhera ambayo vilisimulia habari nyingi sana kuhusiana nayo vitabu vya Mwenyezi Mungu, Mitume wake watukufu na wafuasi wao ambao ndio wenye akili kamili zaidi ya viumbe wote, na wenye elimu nyingi zaidi, na wakubwa wao zaidi katika werevu na ufahamu."},{"id":5277,"sura":42,"from_aya":19,"to_aya":20,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"19. Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. Humruzuku amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mtukufu. 20. Mwenye kutaka mavuno ya Akhera, tutamzidishia katika mavuno yake. Na mwenye kutaka mavuno ya duniani, tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu lolote. "},{"id":5278,"sura":42,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya upole wake kwa waja wake ili wamjue, wampende na wautafute upole wake huo na ukarimu wake. Na upole ni miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambao maana yake pia ni Mwenye kuzifahamu zaidi dhamira na siri, ambaye huwafikisha waja wake - haswa Waumini - kwenye yale yanayowafaa kwa namna wasiyoijua wala wasiyoitarajia. Basi katika upole wake kwa mja wake muumini ni kwamba alimuongoza kwenye heri kwa njia ambayo hakumtarajia kwa yale aliyomsahilishia ya sababu ambazo zinamhimiza kufanya hivyo kwa kumtia maumbile ya kupenda haki na kuifuata, na Mwenyezi Mungu kuwaamrisha Malaika wake watukufu kuwatia nguvu waja wake waumini, kuwahimiza kutenda mema na kuweka katika nyoyo zao sifa ya kuipamba haki ili kuwahimiza kuifuata. Na katika upole wake ni kwamba aliwaamrisha Waumini kufanya ibada za kimkusanyiko ambazo kwazo azimio zao zinaimarishwa, hima zao zinakakamishwa na wanahimizwa kushindana katika wema, kuutamani, na kuigana wao kwa wao. Na katika upole wake ni kwamba aliondoa kila sababu inayomzuia kutenda maasi, kiasi kwamba Yeye Mtukufu anapojua kwamba dunia, mali, uongozi na mengineyo katika vitu ambavyo watu wa dunia wanashindana juu yake vitamzuia mja wake kumtii au vitamfanya kughafilika au kumuasi, anamuondolea hivyo na kumkunjia riziki yake, na ndiyo maana akasema hapa: \"Humruzuku amtakaye\" kulingana na hekima yake na upole wake. \"Naye ndiye Mwenye nguvu, Mtukufu.\" Ambaye ana uwezo wote, na hakuna uwezo wala nguvu kwa yeyote yule miongoni mwa viumbe isipokuwa kwa Yeye, ambaye vitu vyote viko chini yake."},{"id":5279,"sura":42,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: \"Mwenye kutaka mavuno ya Akhera,\" basi akaimini na akaisadiki, na akaifanyia bidii kwa matendo yanayoifailia, \"tutamzidishia katika mavuno yake\" kwa kumzidishia matendo yake na malipo yake mazidisho mingi, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na anayeitaka Akhera na akazifanyia juhudi amali zake, naye ni Muumini, basi hao juhudi yao itakuwa ni ya kushukuriwa.\" Na pamoja na hayo, fungu lake la duniani lazima litamjia. \"Na mwenye kutaka mavuno ya duniani\" kwa kuifanya ikiwa dunia ndio makusudio na lengo lake, na wala hakuitangulizia chochote akhera yake wala hakutarajii malipo yake, wala hakuhofu adhabu yake. Basi \"tutampa katika hayo\" fungu lake alilowekewa, \"lakini katika Akhera hana fungu lolote.\" Atanyimwa Bustani ya mbinguni na neema zake, na atastahiki Jahannamu na moto wake. Aya hii ni sawa na kauli yake Mola Mtukufu: \"Wanaotaka maisha ya dunia na pumbao lake tutawalipa humo vitendo vyao kamili. Na wao humo hawatopunjwa.\" Hadi mwisho wa aya hizi."},{"id":5280,"sura":42,"from_aya":21,"to_aya":23,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"21. Au hao wana miungu ya kishirikina waliowatungia dini asiyoitolea idhini Mwenyezi Mungu? Na lau lisingekuweko neno la kupambanua, basi wangelikatiwa hukumu baina yao. Na hakika wenye kudhulumu watapata adhabu chungu. 22. Utawaona hao madhalimu wanavyokuwa na hofu kwa sababu ya waliyoyachuma, nayo yatawafika tu. Na wale walioamini na wakatenda mema watakuwemo katika mabustani ya Peponi. Humo watapata wayatakayo kwa Mola wao Mlezi. Hiyo ndiyo fadhila kubwa. 23. Hayo ndiyo aliyowabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walioamini na wakatenda mema. Sema: 'Sikuombeni malipo yoyote juu yake ila mapenzi katika kujikurubisha. Na anayefanya wema, tutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu mno, Mwenye shukrani sana.' "},{"id":5281,"sura":42,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kuwa washirikina wamewachukua washirika ambao wanawafanya kuwa vipenzi na ambao wanashirikiana nao katika ukafiri na matendo yake. Nao ni kutoka miongoni mwa mashetani wa kibinadamu wanaolingania katika ukafiri, \"waliowatungia dini asiyoitolea idhini Mwenyezi Mungu?\" Kama vile kufanya ushirikina na uzushi, na kuharamisha aliyohalalisha Mwenyezi Mungu, na kuhalalisha aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, na mambo mengineyo yaliyoyatakwa na matamanio yao, licha ya kwamba Dini sahihi si chochote ila yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwawekea waja wake kama sheria ili waifuate na kujiweka kwayo karibu na Yeye. Kanuni ya msingi ni kwamba kila mtu amekatazwa kutungia kitu sheria ambayo haikutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi vipi kuhusu hawa watu waovu, ambao wanashiriki [wao na baba zao] katika ukafiri? \"Na lau lisingekuweko neno la kupambanua, basi wangelikatiwa hukumu baina yao.\" Yaani, lau kuwa si muda maalumu aliouweka Mwenyezi Mungu wa kufarakisha baina ya makundi mbali mbali, na kwamba atawachelewesha hadi waufikie, basi wangelikatiwa hukumu baina yao wakati huu kwa kumfikishia furaha yule aliye katika haki, na kumuangamiza mwana batili, kwa kuwa sababu ya kuwaangamiza tayari imeshapatikana. Lakini mbele yao kuna adhabu chungu katika Akhera, hawa na kila dhalimu."},{"id":5282,"sura":42,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} Na siku hiyo \"utawaona hao madhalimu\" waliojidhulumu wenyewe kwa ukafiri na maasia \"wanavyokuwa na hofu kwa sababu ya waliyoyachuma,\" kwamba wataadhibiwa juu yake. Na kwa vile mwenye hofu huenda yakampata yale anayoyahofu na huenda yasimpate, akajulisha juu ya hilo, akasema: \"nayo yatawafika tu\" kwa sababu walitenda visababu kamili vinavyolazimu waadhibiwe bila pingamizi lolote, kama vile toba au kitu kingine chochote, na wakafika mahali ambapo haiwezekani kupewa muhula. \"Na wale walioamini\" kwa nyoyo Mwenyezi Mungu, Vitabu vyake, Mitume wake na yale waliyokuja nayo \"na wakatenda mema,\" ikijumuisha kila kitendo chema miongoni mwa matendo ya nyoyo na matendo ya viungo miongoni mwa mambo ya wajibu na yale yanayopendekezwa, basi hawa \"watakuwemo katika mabustani ya Peponi.\" Na usiulize juu ya uzuri wa bustani hizo nzuri sana na mito yake inayotiririka, miti mirefu inayofurika, mandhari mazuri, miti yenye matunda, ndege waimbao kwa sauti nzuri za kuimba, kukutana na kila mpendwa na kuchukua sehemu kamili ya urafiki na wendani, bustani ambazo haziongezeki muda huo wote isipokuwa uzuri na urembo, na wakazi wake hawaongezeki isipokuwa hamu kubwa juu ya starehe zake na upendo. \"Humo watapata wayatakayo\" miongoni mwa mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio halijawahi kusikia, wala hata hayajawahi kufikiriwa na moyo wa mwanadamu yeyote. \"Hiyo ndiyo fadhila kubwa.\" Kwani je, kuna ushindi mkubwa zaidi kuliko kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na kufurahia kuwa karibu naye katika nyumba ya utukufu wake?"},{"id":5283,"sura":42,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} \"Hayo ndiyo aliyowabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walioamini na wakatenda mema.\" Bishara hii kubwa ambayo ndiyo bishara kubwa zaidi kuliko zote, aliibashiria Mwingi wa kurehemu, Mwingi wa rehema, kupitia mikono ya mbora zaidi wa viumbe wake kwa watu wenye imani na matendo mema. Hayo ndiyo malengo makubwa zaidi na njia bora zaidi inayofikisha kwayo. \"Sema: 'Siwaombi malipo yoyote juu yake;\" yaani, juu ya kuwafikishia hii Qur-ani na kuwaita katika hukumu zake. Sitaki kuchukua mali zenu, wala kuwatawala na kujipa uongozi juu yenu, wala madhumuni mengineyo yoyote, \"ila mapenzi katika kujikurubisha.\" Inawezekana kwamba kinachokusudiwa ni: Sikuombeni malipo yoyote juu yake, isipokuwa malipo ya aina moja, ambayo ni yenu na yatakunufaisheni, nayo ni kwamba mnipende mimi kama jamaa wenu. Basi mapenzi haya yanakuwa yameongezeka juu ya yale mapenzi ya kwa ajili ya imani. Kwani mapenzi ya imani kwa Mtume na kutanguliza mapenzi yake juu ya vyote vingine vinavyopendwa baada ya kumpenda Mwenyezi Mungu ni wajibu kwa kila Muislamu, na pamoja na hayo, aliwataka hawa wampende pia kwa ajili ya ujamaa. Kwa sababu yeye Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alilingania katika wito wake watu walio karibu naye zaidi, hadi ikasemwa kwamba hakuna katika makabila ya Maquraish isipokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, ana ujamaa na wao. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa ni mapenzi ya dhati kwa Mwenyezi Mungu, ambayo yanaambatana na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kumfikia kwa njia ya kuwa mtiifu kwake, ambayo inaashiria usahihi wake na ukweli wake, na ndiyo maana akasema, \"ila mapenzi katika kujikurubisha\" kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kulingana na kauli zote mbili, jambo hili alilolivua ni ushahidi kwamba yeye hakuombeni kabisa malipo yoyote juu yake, isipokuwa kama ni kitu kinachowanufaisha wao wenyewe; ambacho si malipo hata kidogo kwake, kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa,\" na kama wanavyosema: 'Fulani hana dhambi kwako ila kwa kuwa anakufanyia wema.' \"Na anayefanya wema,\" kama vile Swala, Saumu, Hija, au kuwafanyia viumbe wema, \"tutamzidishia wema\" kwa namna kwamba Mwenyezi Mungu atakipanua kifua chake na amsahilishie mambo yake, na awe ni sababu ya kumuwezesha matendo mengineyo mema, na kwa sababu ya hayo, yanazidi matendo ya Muumini na ananyanyuka juu kwao mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya viumbe vyake, na anapata malipo ya sasa na ya baadaye. \"Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu mno, Mwenye shukrani sana.\" Anasamehe madhambi makubwa, hata yakiwa makubwa kiasi gani, pindi mja anapotubia akayaacha. Na anashukuru kwa matendo machache kwa kupeana ujira mwingi. Basi kwa msamaha wake, Yeye husamehe dhambi na hufunika kasoro za waja. Na kwa shukurani Yake, anakubali matendo mema na kuyazidisha mizidisho mingi."},{"id":5284,"sura":42,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"24. Ati wanasema Amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Mwenyezi Mungu akipenda ataziba moyo wako. Na Mwenyezi Mungu anaufuta upotofu na anaithibitisha Haki kwa maneno yake. Hakika Yeye anayajua yaliyomo vifuani."},{"id":5285,"sura":42,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} Maana yake: Au hawa wanaokadhibisha Mtume \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie \u2013 wanasema kwa ujasiri na uwongo, \"Ati wanasema Amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo?\" Hapa, wakawa wamekuzulia mambo mabaya na maovu zaidi, ambayo ni kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo kwa kudai unabii na kumdanganyishia Mwenyezi Mungu mambo ambayo hayakutoka kwake ilhali wanajua vyema ukweli wake na uaminifu wake. Basi vipi wanafanya ujasiri wa kudanganya kwa njia hii iliyowazi mno? Bali na hata walimfanyia ujasiri huu Mwenyezi Mungu pia. Kwani kwa kusema hivyo, ni kumtia dosari Mwenyezi Mungu; kwa alikuwezesha kutekeleza wito huu mkubwa unaojumuisha - kulingana na madai yao - uharibifu mkubwa katika ardhi. Kwani Mwenyezi Mungu alimuwezesha Mtume kusema wazi wazi wito huu na kuunasibisha naye, kisha akamuunga mkono kwa miujiza dhahiri na hoja zenye ushindi, nusura ya wazi na kumshinda yeyote anayemhalifu. Ilhali Yeye Mtukufu anao uwezo wa kuuvunjilia mbali wito huu kwenye mizizi yake na kiini chake. Hilo lingewezekana kwa kuziba moyo wa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, basi asielewe chochote, wala usiweze kuingiwa na heri yoyote. Na anapozibwa moyo, basi jambo hili lote linashindwa na kukatika. Basi hii ni hoja ya uhakika juu ya usahihi wa yale aliyoyaleta Mtume, na ushahidi wenye nguvu zaidi unaomuunga mkono Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya yale aliyoyasema, na hakuna ushahidi mkuu zaidi wala mkubwa zaidi kuliko huo. Ndiyo kwa sababu ya hekima yake, rehema yake na Sunna yake inayoendelea ni kwamba anaifuta batili na kuiondoa, hata kama ina nguvu katika nyakati fulani, mwisho wake utakuwa ni kupotelea mbali. \"Na anaithibitisha Haki kwa maneno yake\" ya kiulimwengu yasiyobadilika na yasiyogeuka, ahadi yake ya ukweli na maneno yake ya kidini ambayo yanatimiza mambo ya haki aliyoyaweka katika sheria na kuyaimarisha nyoyoni, na kuwafanya wenye ufahamu mkubwa kuona, kiasi kwamba katika jumla ya njia ambazo Yeye Mtukufu anatimiza haki ni kuiwekea batili ili ipingane nayo. Basi inapoipinga, haki inaishambulia batili hiyo kwa hoja zake na ushahidi wake wa wazi, kwa hivyo ikadhihirika kwa nuru yake na uwongofu ambao kwa hayo batili inapotelea mbali na kukatika, na ubatili wake unamdhihirikia kila mtu. Nayo haki pia inamdhihirikia kila mtu wazi wazi. \"Hakika Yeye anayajua yaliyomo vifuani,\" ya heri na mabaya, na yanayoficha bila ya kudhihirishwa."},{"id":5286,"sura":42,"from_aya":25,"to_aya":28,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"25. Naye ndiye anayepokea toba kwa waja wake, na anasamehe mabaya, na anayajua mnayoyatenda. 26. Na anawaitikia wanaoamini na wakatenda mema, na anawazidishia fadhila zake. Na makafiri watakuwa na adhabu chungu. 27. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwakunjulia riziki waja wake, basi bila ya shaka wangelipanda kiburi katika dunia. Lakini anaiteremsha kwa kipimo akitakacho. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona. 28.  Naye ndiye anayeiteremsha mvua baada ya wao kwisha kata tamaa, na hueneza rehema yake. Naye ndiye Mlinzi, Mwenye kusifiwa sana. "},{"id":5287,"sura":42,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} Haya ni maelezo ya ukamilifu wa ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, upana wa wema wake na ukamilifu wa upole wake katika kukubali toba iliyotoka \"kwa waja wake\" pindi wanapoacha dhambi zao, wakajuta juu yake na wakaazimia kutozirudia tena, ikiwa wataukusudia uso wa Mola wao Mlezi kwa hayo. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu anazikubali hata baada ya kupatikana visababu vya kuwaangamiza na kupatwa na adhabu za kidunia na za kidini. Basi anasamehe \"mabaya\" na anayafuta, na pia anafuta athari zake kama vile kutiwa dosari na kupatwa na adhabu ambayo ilikuwa ni lazima wapatwe nayo, kisha mwenye kutubia anarejea kutoka kwake kwa heshima kana kwamba kamwe hakuwahi kufanya ubaya wowote, na anampenda na kumuwezesha kufikia yale yanayomuweka karibu naye. Kwa kuwa toba ni miongoni mwa matendo makubwa ambayo yanaweza kuwa kamili kutokana na kukamilika ikhlasi ya mtu na ukweli wake, na huenda ikawa pungufu yanapokosekana hayo, na hata inaweza kuwa mbovu ikiwa nia yake ni kufikia moja ya malengo ya kidunia, na inajulikana vyema kwamba mahala pake ni moyoni ambapo hakuna anayeujua zaidi ya Mwenyezi Mungu peke yake, akahitimisha Aya hii kwa kusema, \"na anayajua mnayoyatenda.\""},{"id":5288,"sura":42,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaita waja wake wote warejee kwake na watubie kutokana na mapungufu yao. Basi wakagawanyika makundi mawili kulingana na mwitikio wao kwake: Wale walioitikia, na akawaelezea kwa kauli yake, \"Na anawaitikia wanaoamini na wakatenda mema.\" Yaani, walimwitikia Mola wao Mlezi kwa yale aliyowaitia na wanafuata maelekezo yake. Kwa sababu yale waliyo nayo ya imani na matendo mema yanawasukuma kufanya hivyo. Kwa hivyo, wanapomwitikia, Yeye Mwenyezi Mungu anawashukuru, naye ndiye Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kushukuru, na anawazidishia \"katika fadhila zake\" mafanikio na nguvu ya kufanya matendo mema, na pia anawazidishia ujira na kufuzu kukubwa maradufu zaidi ya yale ambayo matendo yao yaliyostahiki. Na ama wale wasiomuitikia Mwenyezi Mungu, na hao ndio wakaidi waliomkufuru Yeye na Mitume wake, watapata adhabu kali duniani na Akhera."},{"id":5289,"sura":42,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} Kisha akataja kuwa katika upole wake kwa waja wake ni kutowapanulia mambo ya kidunia ili yasiwadhuru dini zao. Akasema, \"Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwakunjulia riziki waja wake, basi bila ya shaka wangelipanda kiburi katika dunia.\" Yaani, wangeghafilika wakaacha kumtii Mwenyezi Mungu na wakaanza kufurahia matamanio ya kidunia tu kulingana na matamanio ya nafsi zao, hata kama ni maasia na dhuluma. \"Lakini anaiteremsha kwa kipimo akitakacho\" kulingana na unavyotaka upole wake na hekima yake. \"Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona.\" Ilisimuliwa katika baadhi ya riwaya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, 'Hakika miongoni mwa waja wangu wapo wale ambao imani yao haiwezi kuwa nzuri isipokuwa kwa mali, na kama ningemfanya masikini, basi hilo lingemharibu. Na hakika miongoni mwa waja wangu wapo wale ambao imani yao haiwezi kuwa nzuri isipokuwa kwa umasikini, na kama ningewatajirisha, basi hilo lingewaharibu. Na hakika miongoni mwa waja wangu wapo wale ambao imani yao haiwezi kuwa nzuri isipokuwa kwa afya njema, na kama ningewafanya wagonjwa, basi hilo lingewaharibu. Na hakika miongoni mwa waja wangu wapo wale ambao imani yao haiwezi kuwa nzuri isipokuwa kwa maradhi, na kama ningewaponya, basi hilo lingemharibu. Hakika Mimi ninaendesha mambo ya waja wangu kwa kuwa ninajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Hakika Mimi ni Mwenye habari zote, mwenye kuona yote.'"},{"id":5290,"sura":42,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} \"Naye ndiye anayeiteremsha mvua\" nyingi kwa ajili ya nchi na watu \"baada ya wao kwisha kata tamaa\" na wakadhani kwamba haitawajia, na wakafanya vitendo mbalimbali kwa sababu ya ukame huo, kisha Mwenyezi Mungu akateremsha mvua, \"na akaeneza\" kwa hiyo \"rehema yake\" kwa kuwatolea watu na mifugo vyakula, kwa hivyo likawa jambo la umuhimu mkubwa sana kwao, na wakafurahia hilo furaha kubwa. \"Naye ndiye Mlinzi\" ambaye huwasimamia waja wake kwa kila aina ya usimamizi, na anasimamia masilahi ya mambo ya Dini yao na dunia yao. katika ulezi wake na usimamizi wake, Mwenye kusifiwa sana\" kakatika ulinzi wake na usimamizi, na kwa sababu ukamilifu wake, na kwa sababu ya fadhila alizowafikishia viumbe wake."},{"id":5291,"sura":42,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"29. Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na wanyama aliowaeneza ndani yake. Naye ni Mwenye uweza mkubwa wa kuwakusanya apendapo."},{"id":5292,"sura":42,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Yaani, miongoni mwa ushahidi wa uwezo wake mkubwa ni kwamba atawafufua wafu baada ya kufa kwao ni, \"kuumba mbingu na ardhi\" licha ya ukubwa na upana wake, jambo linaloashiria uwezo wake na upana wa mamlaka yake, na ustadi na usawasawa ulio ndani yake unaashiria hekima yake, na manufaa na masilahi yaliyo ndani yake yanaonyesha rehema yake, na hayo yanaashiria kwamba Yeye ndiye anayestahiki aina zote za ibada, na kwamba uungu wa chochote kisichokuwa Yeye ni batili. \"Na wanyama aliowaeneza ndani yake\" ambao Mwenyezi Mungu aliwafanya kuwa ni masilahi na manufaa kwa waja wake. \"Naye ni Mwenye uweza wa kuwakusanya apendapo\" baada ya kufa kwao ili wasimame katika uwanja wa Kiyama. Kwani, uweza wake na utashi wake unaweza kufanya hivyo. Na kutokea kwake kunategemea kuwepo kwa habari za ukweli, na tayari imeshajulikana kwamba zimekuja habari nyingi sana kutoka kwa Mitume na Vitabu vyao kwamba hilo litatokea."},{"id":5293,"sura":42,"from_aya":30,"to_aya":31,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"30. Na misiba inayowasibu ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi. 31. Na nyinyi hamwezi kushinda katika ardhi. Na wala nyinyi hamna mlinzi wala msaidizi badala ya Mwenyezi Mungu. "},{"id":5294,"sura":42,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kwamba msiba hauwafikii waja wake katika miili yao, mali zao, watoto wao, na katika yale wanayoyapenda na ukawa mkubwa sana kwao isipokuwa kwa sababu ya mabaya waliyoyatanguliza kwa mikono yao, na kwamba yale ambayo Mwenyezi Mungu anayasamehe ni makubwa zaidi. Kwani, hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu waja wake, bali wanajidhulumu wenyewe. \"Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwachukulia ubaya watu kwa waliyoyachuma, basi asingelimuacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja.\""},{"id":5295,"sura":42,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} Kuwapa kwake muda Yeye Mtukufu si kuchelewesha adhabu wala kushindwa kuwaadhibu. Kwamba, \"nyinyi hamwezi kushinda katika ardhi\" bali nyinyi ndio hamna uwezo katika ardhi, na wala hamuwezi kujizuia kutokana na yale anayoyatekeleza Mwenyezi Mungu juu yenu. \"Na wala nyinyi hamna mlinzi\" atakayewalinda na kuwafikishia manufaa, \"wala msaidizi badala ya Mwenyezi Mungu\" anayeweza kukukingeni kutokana na madhara."},{"id":5296,"sura":42,"from_aya":32,"to_aya":35,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"32. Na katika Ishara zake ni vyombo vinavyokwenda na kurejea baharini kama vilima. 33. Akitaka, huutuliza upepo navyo hivyo vyombo husimama tutwe juu ya bahari. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye subira kubwa na akashukuru sana. 34. Au huviangamiza hivyo vyombo kwa sababu ya waliyoyatenda hao watu. Naye husamehe mengi. 35. Na ili wajue wanaojadiliana katika Ishara zetu kwamba hawana pahali popote pa kukimbilia. "},{"id":5297,"sura":42,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} Yaani, miongoni mwa ushahidi wa rehema zake na uangalizi wake mzuri kwa waja wake ni \"vyombo vinavyokwenda na kurejea baharini,\" kama vile safina na maboti ambayo kwa sababu ya ukubwa wake ni \"kama milima\" mikubwa, ambayo Mwenyezi Mungu aliitiishia bahari kuu na akazilinda kutokana na michafuko ya mawimbi, na akazibeba na kuibeba mizigo yenu mingi mpaka nchi na maeneo ya mbali, na akazitiishia njia kuzisaidia kufanya hivyo."},{"id":5298,"sura":42,"from_aya":33,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33 - 34} Kisha akazibainisha njia hizi kwa kauli yake, \"Akitaka, huutuliza upepo\" ambao Mwenyezi Mungu aliufanya kuwa sababu ya kwenda kwake, \"navyo hivyo vyombo vikasimama tutwe juu ya bahari\" bila kusonga mbele wala kurudi nyuma. Hili haliwezi kubatilishwa na motoboti; kwani katika masharti ya kwenda kwake ni uwepo wa upepo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda anavizamisha vyombo hivyo vinavyokwenda na kurejea baharini kwa sababu ya yale waliyoyatenda hao watu wake. Lakini hustahimili na kusamehe mengi. \"Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye subira kubwa na akashukuru sana.\" Yaani, mwenye subira kubwa kwa yale ambayo nafsi yake inayachukia na ni magumu kwake, kwa hivyo akayachukia kwa sababu ya hayo, kama vile ugumu ulioko katika utiifu, au kuzuia hamu ya kuasi, au kujizuia kutoridhika wakati wa msiba. Naye pia ni mwenye kushukuru sana katika hali nzuri nzuri, akakiri neema za Mola wake Mlezi na kumnyenyekea, na anazitumia katika mambo ya kumridhia. Huyu ndiye anayefaidika na Aya za Mwenyezi Mungu. Na ama yule ambaye hana subira na hana shukrani anapopata neema za Mwenyezi Mungu, yeye hupeana mgongo au hukaidi bila ya kufaidika na Aya zake."},{"id":5299,"sura":42,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, \"Na ili wajue wanaojadiliana katika Ishara zetu\" ili wazibatilishe kwa batili zao \"hawana pahali popote pa kukimbilia.\" Yaani, hawatakuwa na mwokozi yeyote atakayewaokoa kutokana na adhabu iliyowapata."},{"id":5300,"sura":42,"from_aya":36,"to_aya":39,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"36. Basi vyote mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu zaidi kwa ajili ya walioamini na wakawa wanamtegemea Mola wao Mlezi. 37. Na wanayoyaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, na wanapokasirika wao husamehe. 38.Na wanaomwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao, na kutokana na tulichowaruzuku wakawa wanatoa. 39. Na ambao wanapofanyiwa jeuri hujitetea. "},{"id":5301,"sura":42,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36} Huku ni kukatisha tamaa na dunia na kuhimiza juu ya Akhera, na kutaja matendo yanayofikisha huko. Akasema, \"Basi vyote mlivyopewa\" kama vile ufalme, uongozi, mali, watoto, afya nzuri na usalama wa kimwili, \"ni starehe ya maisha ya dunia tu,\" zenye kuisha. \"Lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu\" ni cha thawabu na ujira mkubwa, na neema ya kudumu. Na hayo \"ni bora\" kuliko starehe za dunia kwa ubora ambao hakuna ulinganisho kati yake, \"na cha kudumu zaidi,\" kwa sababu ni neema isiyo na usumbufu wowote wala shida, wala haiishi. Kisha akataja yule ambaye malipo haya ni yake, akasema: \"kwa ajili ya walioamini na wakawa wanamtegemea Mola wao Mlezi. \" Yaani, walijumuisha kati ya imani sahihi inayolazimu mtu kutenda matendo ya imani hiyo, ya dhahiri na yaliyofichikana, na kati ya kumtegemea ambako ndio chombo cha kila tendo. Kwani kila tendo ambalo haliambatani na kumtemegea Mwenyezi Mungu, hilo bado halijakamilika. Kwa maana hilo kuteni kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa moyo juu ya kuleta yale anayoyapenda mja na kuzuia anayoyachukia, pamoja na kuwa na imani naye Mtukufu."},{"id":5302,"sura":42,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37} \"Na wanayoyaepuka madhambi makubwa na mambo machafu.\" Tofauti iliyoko baina ya madhambi makubwa na machafu, ijapokuwa yote ni madhambi makubwa, ni kwamba machafu ni madhambi makubwa ambayo kuna ya kuitia kuyafanya katika nafsi kama vile uzinifu na mfano wake, na madhambi makubwa ni yale ambayo sivyo. Hili ni pale mawili haya yanapotajwa kwa pamoja. Na ama linapotenganishwa kila moja yake mbali na jingine, basi hilo pia linaingia katika maana ya lenzake. \"Na wanapokasirika wao husamehe.\" Wao wamejipamba kwa tabia njema na maadili ya heshima, basi ustahamilivu ukawa ndio tabia yao isiyoachana nao, na maadili mema yakawa ndiyo umbile lao la asili, hata mtu akiwakasirisha kwa maneno au matendo, wanaizuia ghadhabu yao, na hawaitekelezi. Bali wanasamehe, na hawakabiliani na aliyewatendea mabaya isipokuwa kwa wema na msamaha, na kuachilia mbali. Kwa hivyo, yakatokana na msamaha huu na kuachilia mbali masilahi mengi na kujizuilia maovu wao wenyewe na pia kuwazuilia wengine, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, \"Zuilia mabaya kwa lililojema zaidi. Hapo, yule ambaye baina yako naye pana uadui, atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.\""},{"id":5303,"sura":42,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} \"Na wanaomwitikia Mola wao Mlezi\" kwa kufuata utiifu wake na wakaitikia wito wake, na makusudio yao yakawa ni radhi zake na lengo lao likawa ni kufikia kuwa karibu naye. Na katika kumuitikia Mwenyezi Mungu ni kusimamisha swala na kutoa zaka. Ndiyo maana akafungamanisha mawili hayo juu yake akitumia mbinu ya kuunganisha kilicho mahsusi kwa cha jumla, kuashiria heshima yake na fadhilla yake. Kwa hivyo akasema: \"Na wakashika Sala\" kwa dhahiri yake na siri yake, za faradhi na za hiyari, \"na kutokana na tulichowaruzuku wakawa wanatoa\" miongoni mwa mambo yanayotolewa kwa faradhi, kama vile zaka na kuwapa matumizi jamaa na wengineo, na pia matumizi yanayopendekezwa kama vile kuwapa sadaka watu wote, \"na mambo yao\" ya kidini na ya kidunia \"yakawa ni kwa kushauriana baina yao.\" Yaani, hakuna hata mmoja wao anayewazuilia wengine kutoa maoni yake juu ya jambo lolote wanaloshirikiana ndani yake, na hili haliwi isipokuwa kutokana na umoja wao, maelewano yao na upendo wao. Na ukamilifu wa akili zao ni kwamba wanapotaka kufanya jambo linalohitaji kutumia fikira na maoni ndani yake, wakakusanyika kwa ajili yake, wakashauriana na kulifanyia utafiti, mpaka masilahi yake yanapowabainikia, wanachukua fursa hiyo na kuianza mara moja, kama vile maoni kuhusu vita vya jihadi, kuwateua wafanyakazi kwa ajili ya uongozi au mahakama, au mambo mengineyo, na kama vile kutafiti masuala ya kidini kwa ujumla. Hayo ni miongoni mwa mambo wanayoshiriki wote ndani yake, na kuyatafiti ili kubainisha yaliyo sahihi ni katika yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu, nayo yanaingia ndani ya aya hii."},{"id":5304,"sura":42,"from_aya":39,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{39} \"Na ambao wanapofanyiwa jeuri\" kutoka kwa maadui zao \"hujitetea\" kwa sababu ya nguvu zao na utukufu wao, na wala hawajidhalilishi wasioweza kujitetea. Basi hapa akawaelezea kwa imani kumtegemea Mwenyezi Mungu, kujiepusha na madhambi makubwa na machafu ambayo kwayo yanafutwa makosa madogo, na pia akawaelezea kwa kufuata kikamilifu kumuitikia Mola wao Mlezi, kusimamisha Swala, kutoa sadaka katika njia za heri, kushauriana katika mambo yao, nguvu na kujitetea dhidi ya maadui zao. Hizi ndizo sifa za ukamilifu ambazo wamezijumuisha. Na inalazimu kutokana na kuwepo kwake ndani yao, kwamba wanafanya yasiyokuwa hayo na kujiepusha kinyume chake."},{"id":5305,"sura":42,"from_aya":40,"to_aya":43,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"40. Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu. 41. Na wanaojitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu. 42. Bali lawama ipo kwa wale wanaowadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika nchi bila ya haki. Hao watapata adhabu iliyo chungu. 43.  Na anayekuwa na subira, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. "},{"id":5306,"sura":42,"from_aya":40,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40} Katika Aya hii, Mwenyezi Mungu ametaja viwango vya adhabu, na kwamba viko katika viwango vitatu: uadilifu, wema na dhuluma. Kiwango cha uadilifu ni kulipa kitendo kibaya kwa kitendo kibaya kama hicho, bila kuongeza wala kupunguza. Nafsi ni kwa nafsi, na kila jeraha kwa jeraha kama hilo, nayo mali inadhaminiwa na kitu mfano wake. Daraja ya wema ni kusamehe na kutengeneza mambo ya aliyetenda mabaya, na ndiyo maana akasema: \"Lakini mwenye kusamehe na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu,\" atamlipa ujira mkubwa na thawabu nyingi. Na Mwenyezi Mungu aliweka sharti la kutengenea katika kusamehe ili kuashiria kwamba ikiwa mkosaji hastahiki kusamehewa, na masilahi ya kisheria yakahitaji kwamba aadhibiwe, basi katika hali hii, haiamrishwi kusamehe. Na katika kuweka malipo ya mwenye kusamehe kwa Mwenyezi Mungu kuna mambo yanayohimiza msamaha, na kwamba mja awatendee viumbe kwa njia ambayo angependa Mwenyezi Mungu aamiliane naye. Kwa hivyo, kama vile anavyopenda Mwenyezi Mungu kumsamehe, basi naye na awasamehe. Na kama vile anavyopenda Mwenyezi Mungu amsamehe, basi naye na awasamehe wengine, kwani malipo ni ya aina sawa na matendo. Na ama kuhusu kiwango cha dhuluma, basi alikitaja katika kauli yake, \"Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.\" Yaani, wale wanaoanzisha kuwadhulumu wengine, au wale wanaomlipa mkosaji zaidi ya kosa lake, basi ziada hiyo ni dhuluma."},{"id":5307,"sura":42,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41} \"Na wanaojitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu.\" Na iliashiria kauli yake, \"Na ambao wanapofanyiwa jeuri,\" na kauli yake, \"Na wanaojitetea baada ya kudhulumiwa,\" kwamba ni lazima dhuluma hiyo iwe imeshafanyika. Na ama kutaka tu kumdhulumu mwengine bila ya kuifanya dhuluma hiyo, basi huyu hatalipwa kwa njia sawa na alivyofanya. Bali ataadhibiwa kwa namna ambayo itamzuia kutokana na maneno au matendo aliyofanya."},{"id":5308,"sura":42,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} \"Bali lawama\" na adhabu ya kisheria \"ipo kwa wale wanaowadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika nchi bila ya haki.\" Na hili linajumuisha kuwadhulumu watu katika damu zao, mali zao na heshima zao. \"Hao watapata adhabu iliyo chungu\" juu ya nyoyo zao na miili yao kulingana na dhuluma yao."},{"id":5309,"sura":42,"from_aya":43,"to_aya":43,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43} \"Na anayekuwa na subira\" juu ya madhara yanayompata kutoka kwa viumbe, \"na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.\" Yaani, ni miongoni mwa mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyahimiza na akayasisitiza, na akajulisha kwamba hawayafikii isipokuwa watu wenye subira na bahati kubwa, na ni miongoni mwa mambo ambayo hawawezeshwi kuyafikia isipokuwa watu wenye azimio na dhamira kubwa na wale wenye akili nzuri na ufahamu mkubwa. Kwani, kuacha kujitetea kwa maneno au vitendo ni katika mambo magumu zaidi juu ya nafsi. Nako kuwa na subira juu ya maudhi na kuachilia mbali, kusamehe na kumkabili kwa wema, ni vigumu zaidi tena ni vigumu zaidi, lakini ni rahisi kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfanyia kuwa jepesi na akapambana na nafsi yake juu ya kusifika kwayo, na akatafuta msaada wa Mwenyezi Mungu katika hilo. Kisha mja anapoonja utamu wake na akapata athari zake, anayapokea kwa kifua kikunjufu, tabia njema na kuyafurahia."},{"id":5310,"sura":42,"from_aya":44,"to_aya":46,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"44. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, hana mlinzi baada yake. Na utawaona wenye kudhulumu watakapoiona adhabu wanasema: 'Je! Ipo njia ya kurudi?' 45. Na utawaona wanapelekwa kwenye Moto, nao wamenyenyekea kwa unyonge, wanatazama kwa mtazamo wa kificho. Na walioamini watasema: 'Hakika wapatao hasara ni hao waliohasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama.' Ama hakika wenye kudhulumu watakuwa katika adhabu ya daima. 46. Wala hawatakuwa na walinzi wa kuwanusuru mbele ya Mwenyezi Mungu. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, hana njia yoyote. "},{"id":5311,"sura":42,"from_aya":44,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{44} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kuwa Yeye ni wa kipekee katika kuongoa na kupotosha, na kwamba \"ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea\" kwa sababu ya udhalimu wake, \"basi hana mlinzi baada yake\" atakayemsimamia mambo yake na kumuongoa. \"Na utawaona wenye kudhulumu watakapoiona adhabu\"  ikionekana kwa muonekano wa kutisha sana, mgumu na mbaya zaidi, watadhihirisha majuto makubwa na huzuni juu ya yale yao yaliyopita. Na \"Je! Ipo njia ya kurudi\" duniani ili tufanye mambo yasiyokuwa yale tuliyokuwa tukifanya? Lakini hili ni kuomba jambo lisilowezekana."},{"id":5312,"sura":42,"from_aya":45,"to_aya":45,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{45} Yaani, \"Na utawaona wanapelekwa kwenye Moto nao wamenyenyekea kwa unyonge\" uliomo ndani ya nyoyo zao, \"wanatazama kwa mtazamo wa kificho\" kwa sababu ya kutisha kwake na hofu waliyo nayo juu yake. \"Na walioamini watasema\" wakati wa mwisho wa viumbe ulipodhihirika na wana ukweli wakabainika mbali na wengineo: \"Hakika wapatao hasara\" kiuhakika \"ni hao waliokhasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama.\" Kwa maana walizikosesha nafsi zao ujira mkubwa na wakapata adhabu iumizayo, na wakatenganishwa wao na ahali zao, wala hawakujumuika tena. \"Ama hakika wenye kudhulumu\" nafsi zao kwa ukafiri na maasia \"watakuwa katika adhabu ya daima.\" Yaani, watatumbukizwa katikati yake na wala hawatatoka humo kamwe, na wala hawatapumzishwa, na humo watakata tamaa."},{"id":5313,"sura":42,"from_aya":46,"to_aya":46,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{46} \"Wala hawatakuwa na walinzi wa kuwanusuru mbele ya Mwenyezi Mungu,\" kama walivyokuwa wakijidai hivyo katika dunia. Basi Siku ya Kiyama itawadhihirikia wao na wengineo kwamba njia walizozitarajia zimekatika, na kwamba ilipowajia adhabu ya Mwenyezi Mungu haikuwezekana kuwaepusha mbali nayo. \"Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, hana njia yoyote\" ya kuongoka. Hawa walipotea pindi walipodai kuwa washirika wao watawanufaisha na kuwaepushia madhara, lakini hapo ukabainika upotofu wao huo."},{"id":5314,"sura":42,"from_aya":47,"to_aya":48,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"47. Muitikieni Mola wenu Mlezi kabla haijafika siku isiyoepukika, itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo hamtakuwa na pa kukimbilia wala hamtakuwa na cha kukingia. 48. Na wakipuuza, basi Sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao. Si juu yako ila kufikisha Ujumbe tu. Na hakika Sisi tukimwonjesha mtu rehema kutoka kwetu, huifurahia. Na akisibiwa na ovu kwa sababu ya iliyoyatanguliza mikono yao, basi hakika mtu huyu anakufuru. "},{"id":5315,"sura":42,"from_aya":47,"to_aya":47,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{47} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waja wake kumuitikia Yeye kwa kutekeleza aliyowaamrisha na kuyaepuka aliyoyakataza, na kwa kuharakisha kufanya hivyo na kutoahirisha \"kabla haijafika siku\" ya Siku ya Kiyama, ambayo ikija haiwezekani kuirudisha nyuma ili kufanya mambo ambayo mtu hakuyafanya. Na mja siku hiyo hatakuwa na kimbilio awezalo kukimbilia ili asifikiwe na Mola wake Mlezi na amkimbie. Bali Malaika watawazunguka viumbe kutokea nyuma yao, na wakanadiwa: \"Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye pande za mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa uwezo wa kufanya hivyo.\" Siku hiyo mja hataweza kukataa yale aliyoyafanya. Bali ikiwa atakataa, basi viungo vyake vitashuhudia dhidi yake. Aya hii na nyinginezo mfano wake zinakemea suala la kuwa na matumaini matupu, na kuamrisha mtu kuchukua fursa katika kila tendo linalomtokea mja. Kwani kuchelewa mambo kuna balaa zake."},{"id":5316,"sura":42,"from_aya":48,"to_aya":48,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{48} \"Na wakipuuza\" yale uliyowajia nayo baada ya kubainishiwa kikamilifu, \"basi Sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao\" ili uyalinde matendo yao na uulizwe juu yake. \"Si juu yako ila kufikisha Ujumbe tu.\" Kwa hivyo ukishafanya kile kilicho juu yako, basi tayari malipo yako yatakuwa kwa Mwenyezi Mungu, sawa waitikie au wapuuze, na hesabu yao iko kwa Mwenyezi Mungu ambaye anawahifadhia vitendo vyao, vidogo na vikubwa, vilivyo dhahiri na vilivyofichikana. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja hali ya mwanadamu, na kwamba Mwenyezi Mungu anapomuonjesha rehema kama vile afya njema ya kimwili, riziki nyingi, heshima na mfano wa hayo \"huifurahia\" kwa sababu ya hayo tu, kisha akatulizana kwa ajili yake na akampuuza yule aliyemneemesha. \"Na akisibiwa na ovu\" kama vile maradhi, ufukara au mengineyo \"kwa sababu ya iliyoyatanguliza mikono yao, basi hakika mtu huyu anakufuru sana.\" neema zilizotangulia na akakasirika sana kwa sababu ya mabaya yaliyompata."},{"id":5317,"sura":42,"from_aya":49,"to_aya":50,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"49. Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume. 50. Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi, Mwenye uweza. "},{"id":5318,"sura":42,"from_aya":49,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{49 - 50} Aya hii ina habari kuhusu upana wa ufalme wake Mtukufu na kutekelezeka kwa uendeshaji wake katika ufalme wake, kama vile kuumba atakavyo na kuendesha mambo yote, kwa kiasi kwamba, kwa sababu ya ujumla wa uendeshaji wake Mtukufu unajumuisha visababu vilivyoumbwa anavyofanya mja. Kwa mfano, kuoa ni kisababu cha kuzaa watoto. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anayewapa watoto atakavyo. Miongoni mwa viumbe wapo wale anaowatunukia watoto wa kike na miongoni mwao wapo wale anaowatunukia watoto wa kiume, na miongoni mwao wapo wale anaowachanganyia wawili hao: wa kiume na wa kike, na miongoni mwao wapo anaowafanya tasa. \"Hakika Yeye ni Mwenye kujua vyema\" kila kitu, \"Mwenye uwezo mkubwa\" juu ya kila kitu. Anawaendesha viumbe wake kwa elimu yake, ustadi wake na uwezo wake."},{"id":5319,"sura":42,"from_aya":51,"to_aya":53,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"51. Na haikuwa kwa mwanadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo), au kwa nyuma ya kizuizi, au kumtuma Mjumbe. Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hekima. 52. Na namna hivi tumekufunulia Qur-ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunamwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyonyooka. 53. Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye tu vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Jueni kuwa mambo yote yanarudi kwa Mwenyezi Mungu. "},{"id":5320,"sura":42,"from_aya":51,"to_aya":51,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{51} Wakati wale waliowakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu, wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu waliposema: \"Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au zikatufikia Ishara?\" Kwa sababu ya kiburi chao, Mwenyezi Mungu akawajibu kwa aya hii tukufu, na kwamba Yeye Mtukufu hawaongeleshi isipokuwa viumbe vyake maalumu: Manabii na Mitume, na watukufu wake miongoni mwa walimwengu, na kwamba hilo huwa kwa moja ya njia hizi: Ima Mwenyezi Mungu amzungumzishe kwa kumteremshia ufunuo wake kwa kutia ufunuo ndani ya moyo wa Mtume bila ya kumtumia Malaika au kusema naye moja kwa moja, \"au\" akazungumza naye kwa maneno moja kwa moja, lakini \"kwa nyuma ya kizuizi.\" Kama ilivyokuwa kwa Musa bin Imran, aliyezungumza moja kwa moja na Mwingi wa rehema. \"Au\" Mwenyezi Mungu akamzungumzisha kupitia Mtume wa kimalaika, akamtumia \"mjumbe\" kama vile Jibril au Malaika wengineo. \"Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake\" Mwenyezi Mungu, na si kwa matamanio yake tu. Yeye Mtukufu ni wa juu zaidi kwa dhati yake, na yuko juu zaidi kwa sifa zake nzuri nzuri, na yuko juu zaidi katika vitendo vyake. Alikishinda kila kitu, na viumbe vyote vinamnyenyekea Yeye. \"Mwenye hekima,\" kwa kuwa anaweka kila kitu mahali pake miongoni mwa viumbe na sheria zake mbalimbali."},{"id":5321,"sura":42,"from_aya":52,"to_aya":52,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{52} \"Na namna hivi\" tulivyowateremshia ufunuo Mitume wa kabla yako, \"tumekufunulia roho (Qur-ani) kwa amri yetu.\" Mwenyezi Mungu ameiita Qur-ani roho kwa sababu roho huhuisha mwili, nayo Qur-ani inahuisha nyoyo na nafsi, na masilahi ya kidunia na ya kidini yanakuwa sawa kwayo. Kwa sababu ndani yake kuna heri nyingi na elimu tele. Nayo ni neema tupu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake na waja wake waumini bila ya wao kufanya sababu yoyote ya kuipata. Ndiyo maana akasema: \"Ulikuwa hujui Kitabu ni nini wala Imani\" kabla ya hicho kuteremshwa kwako, na hata hukuwa unajua Vitabu vilivyotangulia. Bali ulikuwa hujui kusoma na kuandika, kisha kikakukujia Kitabu hiki ambacho \"tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunamwongoa tumtakaye katika waja wetu,\" ambacho wanajiangazia kwacho katika viza vya ukafiri, uzushi na matamanio mabaya yaangamizayo, na kwayo wanajua uhakika wa mambo, na wanaongoka kwayo kufikia njia iliyonyooka. \"Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyonyooka.\" Yaani, unawafafanulia njia hiyo, kuwawekea wazi, [kuwaangazia], kuwahimiza juu yake, kuwakataza kinyume chake na unawakatisha moyo juu yake."},{"id":5322,"sura":42,"from_aya":53,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{53} Kisha akabainisha njia hiyo iliyonyooka, akasema: \"Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye tu vilivyomo mbinguni na katika ardhi,\" ambayo aliwawekea waja wake na akawajulisha kwamba hiyo ndiyo inayofikisha kwake na kwa nyumba ya utukufu wake. \"Jueni kuwa mambo yote yanarudi kwa Mwenyezi Mungu,\" ya heri na maovu, kisha atamlipa kila mmoja kwa matendo yake. Ikiwa ni mazuri, basi kwa uzuri. Na ikiwa ni maovu, basi kwa uovu."},{"id":5323,"sura":42,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya Surat Ash-Shura. Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, mwanzo na mwisho, kwa dhahiri na kwa ndani, kwa sababu ya urahisishaji wake."},{"id":5324,"sura":42,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}