{"result":[{"id":5426,"sura":44,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya surat Ad-Dhukhan"},{"id":5427,"sura":44,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":5428,"sura":44,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu."},{"id":5429,"sura":44,"from_aya":1,"to_aya":16,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Ha Mim 2. Ninaapa kwa Kitabu kinachobainisha. 3. Hakika Sisi tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji. 4. Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima. 5. Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma. 6. Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 7. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini. 8. Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo. 9 Lakini wao wanacheza katika shaka. 10. Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri. 11. Utakaowafunika watu. Hii ni adhabu chungu! 12. Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. 13. Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha. 14. Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: 'Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.' 15. Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile! 16. Siku tutakayoyashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa. "},{"id":5430,"sura":44,"from_aya":1,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1 - 3} Hiki ni kiapo kwa Qur-ani juu ya Qur-ani. Kwa hivyo aliapa kwa Kitabu kinachobainisha kila kinachohitaji kuelezwa kwamba alikiteremsha: \"katika usiku uliobarikiwa.\" Yaani: wenye heri na baraka nyingi, nao ni Usiku wa Cheo (Lailatul-Qadr) ambao ni bora kuliko miezi elfu moja. Basi aliteremsha maneno bora zaidi katika usiku na michana bora zaidi kwa kiumbe bora zaidi kwa lugha ya Waarabu watukufu; ili kuwaonya watu waliogubikwa na ujinga na wakasifika mno na hali ya kuwa mashakani, ili waangazwe na nuru yake, wachukue uongofu wake, na watembelee nyuma yake, ili wapate heri ya duniani na akhera, na ndiyo maana akasema: \"Hakika Sisi ni Waonyaji.\""},{"id":5431,"sura":44,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} \"Katika usiku huu\" mtukufu ambao iliteremka humo Qur-ani, \"hubainishwa kila jambo la hekima.\" Yaani: linapitishwa na kuandikwa kila jambo linalohusiana na mipango ya Mwenyezi Mungu na la kisheria. Uandishi huu na kupambanua huku unaokuwa katika usiku huu wa Cheo ni miongoni mwa uandishi unaoandikwa na kutofautishwa, kwa hivyo ukawiana na uandishi ule wa kwanza ambao Mwenyezi Mungu aliandika kuhusiana na hatima za viumbe, muda wao, riziki zao, matendo yao, na hali zao. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka Malaika kuandika yale yatakayompata mja akiwa ndani ya tumbo la mama yake. Kisha akaweka baada ya kutoka kwake humo na kuja duniani waandishi watukufu ili waandike na kuhifadhi matendo yake. Kisha Yeye Mtukufu katika usiku wa Cheo anapitisha yatakayotokea katika mwaka huo, na yote haya ni katika ukamilifu wa elimu yake, ukamilifu wa hekima yake, kuhifadhi sawasawa kwake, na utunzaji wake Mtukufu wa viumbe vyake."},{"id":5432,"sura":44,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} \"Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma\" Mitume na kuteremsha Vitabu. Na Mitume wanafikisha tu amri za aliyewatuma na wanapeana habari za mipango yake."},{"id":5433,"sura":44,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} \"Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi.\" Yaani: kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu, ambavyo bora zaidi yake ni Qur-ani, ni rehema itokayo kwa Mola Mlezi wa waja kwa waja wake. Na Mwenyezi Mungu hakuwahi kuwarehemu waja wake kwa rehema kubwa kuliko kuwaongoza kwa Vitabu na Mitume, na kila heri wanayoipata duniani na Akhera, basi ni kwa ajili ya hilo na kwa sababu yake. \"Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua zaidi.\" Yaani, anasikia vyema sauti zote, na anajua mambo yote ya dhahiri na yaliyofichika. Naye Mtukufu alijua haja kubwa ya waja wake juu ya Mitume wake na Vitabu vyake, basi akawarehemu kwa hivyo na kuvifanya kuwa neema kwao. Kwa hivyo,ni za Mwenyezi Mungu sifa njema, neema na wema."},{"id":5434,"sura":44,"from_aya":7,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7 - 8} \"Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina ya viwili hivyo.\" Yaani, Muumba wake, msimamizi wake, na anayeviendesha atakavyo, \"ikiwa nyinyi mna yakini.\"  Yaani, ikiwa mnayajua hayo elimu yenye kumfanya mtu kuwa na yakini. Basi jueni kwamba Mola Mlezi wa viumbe ndiye Mungu wavyo wa haki, na ndiyo maana akasema: \"Hakuna mungu ila Yeye.\" Yaani, hakuna anayefaa kuabudiwa kwa haki ila Uso wake. \"Anahuisha na anafisha;\" yaani, Yeye pekee ndiye mwenye anayeendesha suala la kufufua na kufisha, na atakukusanyeni baada ya kufa kwenu na atakulipeni kwa matendo yenu, ikiwa ni heri, basi kwa heri. Na ikiwa ni shari, basi kwa shari. \"Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo.\" Yaani, Mola Mlezi wa wa mwanzo na wa mwisho. Anayewalea kwa neema zake, anayewazuilia adhabu."},{"id":5435,"sura":44,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipothibitisha umola wake na uungu wake kwa njia inalazimu mtu kuwa na elimu kamili na kuondoa shaka, akajulisha kwamba makafiri pamoja na kubainisha huku: \"wanacheza katika shaka\" na mambo ya kuwatia utata, huku wameghafilika mbali na yale waliyoumbwa kwa ajili yake, na wamejishughulisha na mchezo wa batili ambao hauwaletei isipokuwa madhara tu."},{"id":5436,"sura":44,"from_aya":10,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10 - 16} \"Basi ingoje\" adhabu itakayowapata hao. Kwa maana wakati wake umekaribia na umefika. \"Siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri. Utakaowafunika watu\" na wataambiwa: \"Hii ni adhabu chungu!\" Wafasiri walitofautiana kuhusu maana ya moshi huu: Ikasemwa kwamba ni moshi utakaowafunika watu na kuwagubika wote Moto utakapowakaribia wahalifu Siku ya Kiyama, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwatishia kwa adhabu Siku ya Kiyama, na akamuamuru Nabii wake awangojee siku hiyo. Maana hii inaungwa mkono na ukweli kwamba njia hii ndiyo njia ya Qur-ani ya kuwatishia makafiri, kutowaharakisha, kuwatia hofu kubwa kwa siku hiyo na adhabu yake, na kumliwaza Mtume na waumini kwamba wawangojee wale waliowatia udhia. Maana hii pia inaungwa mkono na ukweli kwamba alisema katika Aya hii: \"Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha.\" Haya wataambiwa makafiri Siku ya Kiyama watakapoomba kurejea katika dunia, lakini wataambiwa: Tayari wakati wa kurudi umeshapita. Na ikasemwa kwamba maana yake ni yale yaliyowasibu makafiri wa Kiquraishi walipokataa kuamini na wakaifanyia kiburi haki, kwa hivyo Nabii - rehema na amani zimshukie - akawaapiza na akasema: \"Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie dhidi yao kwa miaka (ya ukame) kama miaka (ya ukame) ya Yusuf.\" Basi Mwenyezi Mungu akawaletea njaa kubwa, hata wakala maiti na mifupa; kiasi kwamba wakaanza kuona kilicho kati ya mbingu na ardhi kama mwonekano wa moshi, lakini haukuwa moshi, na hiyo ilitokana na ukali wa njaa hiyo. Basi inakuwa kauli yake: \"siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri\" na maana kwamba hayo ni kulingana na macho yao wanavyoona, na wala si moshi kwa uhakika. Basi wakaendelea kuwa katika hali yao hii mpaka wakaomba Mtume wa Mwenyezi Mungu \u2013 rehema na amani ziwe juu yake - rehema na kwamba awaombee kwa Mwenyezi Mungu ili Mwenyezi Mungu awaondolee balaa hiyo, [hivyo akamwomba Mola wake Mlezi]; basi Mwenyezi Mungu akaiondoa kwao. Kwa hivyo kwa msingi huu inakuwa kauli yake: \"Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile\" ni kujulisha kwamba Mwenyezi Mungu atawaondolea balaa hiyo, ni tishio kwao kwamba wasije rudi kwenye kiburi na kukadhibisha, na kujulisha juu ya kutokea kwake, nayo ikatokea, na kwamba Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa mshambulio mkubwa. Walisema kwamba hili lilikuwa vile vita vya Badr, lakini kauli hii ina maana ya mbali iliyo dhahiri. Na ikasemwa kuwa maana yake ni kwamba hii ni moja ya alama za Saa ya Kiyama, na kwamba katika zama za mwisho utatokea moshi utakaochukua pumzi za watu, lakini Waumini watasibiwa na hilo kama mwonekano wa moshi tu. Na kauli sahihi zaidi ni ile ya kwanza. Na katika aya hii kuna uwezekano kwamba kinachomaanishwa na kauli yake: \"Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri. Utakaowafunika watu. Hii ni adhabu chungu! Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha. Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: 'Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu\" kwamba haya yote yatatokea Siku ya Kiyama, na kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile. Siku tutakayoyashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa,\" ni yale yaliyowapata Maquraishi kama ilivyotangulia kutajwa awali. Ikiwa Aya hizi zilieleweka kwamba zina maana hizi mbili, basi hautapata chochote katika maneno yake chenye kuzuilia hilo, badala yake utayapata yanaingiliana nayo kuingiliana kukamilifu, na hili ndilo la sahihi zaidi kulingana na mimi, Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi."},{"id":5437,"sura":44,"from_aya":17,"to_aya":33,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"17 Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu. 18. Akasema: 'Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu. 19. Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi. 20. Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe. 21. Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.' 22. Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: 'Hakika watu hawa ni wakosefu.' 23. Mwenyezi Mungu akasema: 'Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa. 24. Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao ni jeshi litakalozamishwa.' 25. Mabustani mangapi na chemchemi ngapi waliziacha! 26. Na mimea na vyeo vitukufu! 27. Na neema walizokuwa wakijistareheshea! 28. Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe. 29. Basi mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula. 30. Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha, 31. Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka. 32. Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe. 33. Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi. "},{"id":5438,"sura":44,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kukadhibisha kwa wale waliomkadhibisha Mtume Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake, - akataja kuwa wao walikuwa na watangulizi waliokadhibisha, basi akataja kisa chao na Musa, na yale aliyowafikishia Mwenyezi Mungu, ili hawa wanaokadhibisha wakomeke mbali na yale wanayoyafanya, akasema: \"Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni\" kwa kuwatuma Mtume wetu Musa bin Imran, Mtume mtukufu ambaye alikuwa na utukufu na maadili mema ambayo hayakuwa kwa mwengineye."},{"id":5439,"sura":44,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} Akamwambia Firauni na wakuu wake: \"Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu\" yaani Wana wa Israili na muwaachilie huru na usiwaadhibu adhabu yako hiyo kali. Kwani wao ni ukoo wangu na bora zaidi wa walimwengu wa zama zao, na nyinyi mmewadhulumu na kuwatumikisha bila haki. Kwa hivyo, waachilieni wamuabudu Mola wao Mlezi. \"Kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu.\" Yaani, Mtume kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote, mwaminifu kwa yale aliyonituma nayo, siwafichi chochote katika hayo, wala siongezi, wala sipunguzi. Na hili linalazimu watu kumtii kikamilifu."},{"id":5440,"sura":44,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} \"Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu\" kwa kuacha kumwabudu na kujikweza juu ya waja wa Mwenyezi Mungu. \"Hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi.\"  Na huo ni miujiza ya kung'aa na ushahidi wa ushindi alioufanya."},{"id":5441,"sura":44,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Basi wakamkadhibisha na wakataka mno kumuuwa. Kwa hivyo, akakimbilia kwa Mwenyezi Mungu kutokana na uovu wao, na akasema: \"Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe\" mkaniuwa vibaya zaidi kwa kunipiga mawe."},{"id":5442,"sura":44,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} \"Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.'\" Yaani, mna viwango vitatu: Kuniamini. Na hilo ndilo ninalokukusudia kwenu. Ikiwa hamtafikia kiwango hiki, basi jitengeni mbali nami, msinidhuru wala nisiwadhuru. Basi nilindeni kutokana na shari yenu. Lakini hakikutokea kwao kiwango hicho cha kwanza wala cha pili. Bali walibakia wakisitasita na wakimfanyia Mwenyezi Mungu ukaidi, wakimpigana vita Nabii wake Musa, amani iwe juu yake, bila ya kumuwezesha kuwatoa watu wake, Wana wa Israili."},{"id":5443,"sura":44,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} \"Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: 'Hakika watu hawa ni wahalifu.'\" Yaani, wamefanya uhalifu unaolazimu waharakishiwe adhabu. Basi yeye amani iwe juu yake akajulisha juu ya hali yao. Na huku ni kuomba dua kwa kutumia hali, njia ambayo ni bora zaidi hata kuliko kuzungumza. Kama alivyosema kujihusu mwenyewe, yeye amani iwe juu yake: \"Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji wa heri utakayoniteremshia.\""},{"id":5444,"sura":44,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} Basi Mwenyezi Mungu akamwamuru atembee na waja wake usiku, na akamwambia kwamba Firauni na watu wake watamfuata."},{"id":5445,"sura":44,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} \"Na iache bahari vivyo hivyo imeachana.\" Haya ni kwa sababu Musa alipowaongoza Wana wa Israili kama alivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, kisha Firauni akawafuata, basi Mwenyezi Mungu akamuamuru Musa aipige bahari, naye akaipiga na ikawa njia kumi na mbili, na maji kati ya njia hizo yakawa kama milima mikubwa. Basi Musa na watu wake wakapitia humo. Walipotoka humo, Mwenyezi Mungu alimwamuru kuiacha vivyo hivyo; ili Firauni na askari wake wapitie humo. \"Hakika wao ni jeshi litakalozamishwa majini.\" Kwa hivyo, walipotoka kaumu ya Musa wote na wakaingia humo watu wa Firauni, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiamrisha kuwafunika, kwa hivyo wakazama wote majini, na wakaacha yale waliyostareheshwa kwayo katika uhai wa duniani, na Mwenyezi Mungu akawarithisha hayo Wana wa Israili, ambao walikuwa watumwa wao."},{"id":5446,"sura":44,"from_aya":25,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25 - 28} Ndiyo maana akasema: \"Mabustani mangapi na chemchemi ngapi waliziacha!. Na mimea na vyeo vitukufu! Na neema walizokuwa wakijistareheshea! Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe.\" Na katika Aya nyingine alisema: \"Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili.\""},{"id":5447,"sura":44,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} \"Basi mbingu wala ardhi havikuwalilia\" wala kuwahuzunukia kwa sababu ya kutengana nao Mwenyezi Mungu alipowaharibu na kuwaangamiza. Bali kila moja na hivyo kilifurahia kuangamizwa kwao na kuharibiwa kwao, hata mbingu na ardhi. Kwa sababu hawakuacha ila athari zinazozifanya nyuso zao kuwa nyeusi na kuwasababishia laana na kuchukiwa na walimwengu wote. \"Wala hawakupewa muhula\" kabla ya kuadhibiwa. Bali waliuawa mara moja."},{"id":5448,"sura":44,"from_aya":30,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30 - 31} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaambia Wana wa Israili juu ya neema yake, akasema: \"Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha\" ambayo walikuwa ndani yake \"Ya Firauni\" Kwani alikuwa akiwauwa watoto wao wa kiume na anawaacha hai wanawake wao. \"Hakika yeye alikuwa jeuri\" na kutakabari katika ardhi bila ya haki, \"katika wenye kupindukia mipaka\" ya Mwenyezi Mungu kwa kufanyia ujasiri maharamisho yake."},{"id":5449,"sura":44,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} \"Na tuliwakhiari kwa elimu yetu\" kwani tulijua kwamba walistahiki fadhila hiyo \"kuliko walimwengu wengineo\" wa zama zao, na wale waliokuwa kabla yao na baada yao. Mpaka Mwenyezi Mungu alipowaleta umma wa Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - basi wao wakawa bora kuliko walimwengu wote, na Mwenyezi Mungu akawafanya kuwa umma bora kabisa waliotolewa watu, na akawaneemesha kwa yale ambayo hakuwahi kuwaneemesha wengineo."},{"id":5450,"sura":44,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} \"Na tukawapa\" Wana wa Israili \"katika ishara\" na miujiza inayong'aa na iliyo dhahiri. Ishara hizi ni \"zenye majaribio yaliyo wazi.\" Yaani, tuliwapa wema mwingi ulio dhahiri na ambao ni hoja dhidi yao juu ya usahihi wa yale aliyokuja nayo Nabii wao Musa, amani ziwe juu yake."},{"id":5451,"sura":44,"from_aya":34,"to_aya":37,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"34. Hakika hawa wanasema: 35. 'Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi. 36. Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.' 37. Je, ni wao bora au watu wa Tubbaa' na waliokuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu. "},{"id":5452,"sura":44,"from_aya":34,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34 - 35} Mwenyezi Mungu anajulisha kwamba: \"Hakika hawa\" wanaokadhibisha wanasema wakikatalia mbali suala la ufufuo na kuwatawanya viumbe: \"'Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.'\" Yaani, si chochote ila ni maisha ya dunia, na hakutakuwa na ufufuo wala kuwatawanya viumbe huko akhera, wala Bustani za mbinguni wala Moto."},{"id":5453,"sura":44,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36} Kisha wakasema kwa kumfanyia ujasiri Mola wao Mlezi na kuona kwamba hawezi kitu: \"'Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.'\" Haya ni katika mapendekezo ya watu wajinga wakaidi ambayo ni ya mbali mno. Kwani kuna uhusiano gani kati ya ukweli wa Mtume \u2013 rehema na amani ziwe juu yake \u2013 na kwamba hawezi kuwa mkweli hadi awaletee baba zao? Kwani ishara zilishasimama juu ya ukweli wa yale aliyowaletea na zikasimuliwa kwa idadi kubwa sana kwa kila namna?"},{"id":5454,"sura":44,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37} Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: \"Je, ni wao bora.\" Yaani, hawa wanaoongeleshwa \"au watu wa Tubbaa' na waliokuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wahalifu?\" Wao si bora kuliko wale, kwani wameshiriki katika uhalifu. Basi na watarajie maangamizi kama yale yaliyowapata ndugu zao wahalifu."},{"id":5455,"sura":44,"from_aya":38,"to_aya":42,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"38. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo. 39. Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui. 40. Hakika siku ya Uamuzi ni wakati uliowekwa kwa wao wote. 41. Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa. 42. Isipokuwa atakayemrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu mno. "},{"id":5456,"sura":44,"from_aya":38,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38 - 39} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu ukamilifu wa uwezo wake na ukamilifu wa hekima yake, na kwamba hakuziumba mbingu na ardhi kwa ajili ya mchezo wala kwa pumbao, wala bure bila manufaa, na kwamba hakuziumba \"ila kwa Haki.\" Yaani, kuviumba kwenyewe ni kwa Haki, na uumbaji wake umejumuisha haki, na kwamba aliviumba ili vimuabudu Yeye pekee, bila mshirika, na ili awaamrishe waja wake na awakataze, na awalipe mazuri na awaadhibu; \"lakini wengi wao hawajui.\" Kwa hivyo, hawakutafakari katika kuumbwa mbingu na dunia."},{"id":5457,"sura":44,"from_aya":40,"to_aya":40,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40} \"Hakika siku ya Uamuzi\" ambayo ni Siku ya Kiyama, ambayo Mwenyezi Mungu atapambanua baina ya wa mwanzo na wa mwisho na baina ya waliohitilafiana, \"ni wakati uliowekwa kwa wao wote.\" Mwenyezi Mungu atawakusanya wote humo, na atawahudhurisha wao na matendo yao, na atawalipa juu yake."},{"id":5458,"sura":44,"from_aya":41,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{41} \"Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote\" wala jamaa hatamfaa jamaa yake kitu. \"Wala hawatanusuriwa\" na kuzuiliwa mbali na adhabu ya Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mtukufu. Kwa sababu hakuna yeyote miongoni mwa viumbe aliye na mamlaka yoyote juu ya jambo hilo."},{"id":5459,"sura":44,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} \"Isipokuwa atakayemrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu mno.\" Huyo ndiye atakayenufaika na kuinuka juu kwa sababu ya rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambazo alijisababishia na akazifanyia juhudi namna zinavyostahiki katika dunia hii. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:"},{"id":5460,"sura":44,"from_aya":43,"to_aya":50,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"43. Hakika Mti wa Zaqqum 44. Ni chakula cha mwenye dhambi. 45. Kama shaba iliyoyeyushwa, hutokota matumboni. 46. Kama kutokota kwa maji ya moto. 47. (Itasemwa): 'Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu! 48. Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayochemka.' 49. Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu! 50. Hakika haya ndiyo mliyokuwa mkiyatilia shaka. "},{"id":5461,"sura":44,"from_aya":43,"to_aya":50,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43 - 50} Alipotaja Siku ya Kiyama na kwamba atapambanua kati ya waja wake siku hiyo, akataja mgawanyiko wao katika makundi mawili: Kundi la kwenda katika Bustani za mbinguni, na kundi la kwenda Motoni, nao ni wakosefu waliofanya kufuru na maasia, na kwamba chakula chao ni \"mti wa Zaqqum.\" Mti muovu na mbaya zaidi, na kwamba ladha yake ni \"kama shaba iliyoyeyushwa\" ndani ya matumbo yao. \"Kama kutokota kwa maji ya moto.\" Na mhalifu ataambiwa: \"Onja\" adhabu hii chungu na kali sana. \"Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!\" Kwani ulidai kwamba wewe ni mwenye nguvu, kwa hivyo utazuilika na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kwamba wewe ni mtukufu kwa Mwenyezi Mungu, na wala Yeye hawezi kukutia katika adhabu. Basi leo imekudhihirikia kuwa wewe ni mtu dhalili, anayefedheheshwa, aliye duni sana. \"Hakika haya\" ya adhabu kubwa \"ndiyo mliyokuwa mkiyatilia shaka.\" Lakini sasa mmeshajua kwamba ni haki ya yakini."},{"id":5462,"sura":44,"from_aya":51,"to_aya":59,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"51. Hakika wacha Mungu watakuwa katika mahali pa amani. 52. Katika mabustani na chemchemi. 53. Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana. 54. Hivi ndivyo itakavyokuwa, na tutawaoza mahurilaini. 55. Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani. 56. Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu. 57. Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 58. Basi tumeifanya nyepesi hii Qur-ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka. 59. Ngoja tu, na wao wangoje pia. "},{"id":5463,"sura":44,"from_aya":51,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{51 - 53} Haya ni malipo ya wale wanaomcha Mwenyezi Mungu, walioogopa ghadhabu yake na adhabu yake kwa kuacha dhambi na kufanya vitendo vya utiifu. Pindi walipoepushwa mbali na ghadhabu na adhabu, wakapata ridhaa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na malipo mazuri makubwa katika kivuli vikubwa mno, katika miti mingi na matunda mengi, na chemchemi zinazotiririka na mito inayopita chini yao, wakiifanya imiminike kwa wingi katika Bustani za mbingu za neema. Mwenyezi Mungu alifungamanisha neema za Bustani hizi kwa sababu kila kitu kilichomo ndani yake ni neema, furaha kamili kwa namna zote, hakuna kitu cha kuhuzunisha wala kuchukiza kwa namna yoyote ile, na nguo zao zitakuwa zimetengenezwa kwa hariri ya kijani iliyotengenezwa kwa hariri laini na hariri nzito ya atilasi miongoni mwa yale yanayotamaniwa na nafsi zao \"wakielekeana\" nyoyoni mwao na nyuso zao, wakiwa katika raha kamili, utulivu, upendo, kuishi kwa uzuri na tabia njema."},{"id":5464,"sura":44,"from_aya":54,"to_aya":54,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{54} \"Hivi ndivyo itakavyokuwa\" neema kamili na furaha kamili \"na tutawaoza mahurilaini.\" Nao ni wanawake warembo muno ambao kwa sababu ya urembo wao na uzuri wao huyafanya macho kushangazwa mno, akili kuduwaa na moyo kutekwa na ukamilifu wao. Nao ni wenye macho makubwa, mazuri mno."},{"id":5465,"sura":44,"from_aya":55,"to_aya":55,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{55} \"Humo watataka kila aina ya matunda\" miongoni mwa yale yaliyo na jina katika dunia na yasiyo na jina wala mfano wake katika dunia hii. Basi kwa namna yoyote ile watakavyoomba aina yoyote ile ya matunda, wataletewa mara hiyo hiyo bila juhudi yoyote wala kujisumbua, huku wakiwa wamesalimika kutokana na suala la kukatikiwa na hayo, na watakuwa salama kutokana na madhara yake, salama kutokana na kila cha kutia huzuni, na salama kutokana kuondoka humo, na kutokana na kifo."},{"id":5466,"sura":44,"from_aya":56,"to_aya":56,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{56} Ndiyo maana akasema: \"Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza\" ya duniani, na wala humo hakuna mauti yoyote. Kwa hivyo wakapata kwa ukamilifu kila kitu walichokipenda, walichokitafuta \"na (Mwenyezi Mungu) atawalinda kutokana na adhabu ya Jahannamu.\""},{"id":5467,"sura":44,"from_aya":57,"to_aya":57,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{57} \"Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi\" kwa kuwapa neema hizo na kuwaondolea adhabu. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliyewawezesha kufikia matendo mema, ambayo kwayo walipata heri ya Akhera, na akawapa yale ambayo matendo yao hayakuyafikia. \"Huko ndiko kufuzu kukubwa.\" Na kweli ni kufuzu gani ni kukubwa zaidi kuliko kupata radhi ya Mwenyezi Mungu, Pepo yake kusalimika kutokana na adhabu yake na ghadhabu yake?"},{"id":5468,"sura":44,"from_aya":58,"to_aya":58,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{58} \"Basi tumeifanya nyepesi hii Qur-ani kwa ulimi wako\" ambao ndio fasaha zaidi kuliko ndimi zote na ambao ndio bora zaidi. Basi kwa huo, maneno yake yakafanywa kuwa wepesi, na maana zake pia zikafanywa kuwa nyepesi \"ili wapate kukumbuka\" yenye manufaa kwao, wakayafanya. Na yenye madhara kwao, basi wakayaacha."},{"id":5469,"sura":44,"from_aya":59,"to_aya":59,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{59} \"Basi ngoja tu\" yale aliyokuahidi Mola wako Mlezi ya heri na ushindi. \"Hakika wao pia wanangoja\" yale yatakayowapata ya adhabu, lakini kuna tofauti kubwa baina ya kungonja huku kuwili: Mtume wa Mwenyezi Mungu na wafuasi wake wanatazamia heri duniani na Akhera, naye aliye kinyume chao anangojea uovu duniani na Akhera."},{"id":5470,"sura":44,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya surat Ad-Dukhan, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu na neema."},{"id":5471,"sura":44,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}