{"result":[{"id":5472,"sura":45,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya surat Al-Jathiya"},{"id":5473,"sura":45,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":5474,"sura":45,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu."},{"id":5475,"sura":45,"from_aya":1,"to_aya":11,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1.  Ha, Mim. 2. Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 3. Hakika katika mbingu na ardhi ziko Ishara kwa Waumini. 4. Na katika umbo lenu na katika wanyama aliowatawanya, zimo Ishara kwa watu wenye yakini. 5. Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayoiteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili. 6. Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayoiamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake? 7. Ole wake kila mzushi mwenye dhambi! 8. Anayesikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anashikilia yale yale aliyokatazwa, na anajivuna, kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu chungu! 9. Na anapokijua kitu kidogo katika Aya zetu, hukifanyia mzaha. Watu hao ndio watakaokuwa na adhabu ya kufedhehesha. 10. Na nyuma yao ipo Jahanamu. Na waliyoyachuma hayatawafaa hata kidogo, wala walinzi waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu. Na watapata adhabu kubwa. 11. Huu ni uwongofu. Na wale wale waliozikataa Ishara za Mola wao Mlezi watapata adhabu inayotokana na ghadhabu, iliyo chungu. "},{"id":5476,"sura":45,"from_aya":1,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1 - 2} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu habari inayojumuisha amri ya kuitukuza Qur-ani na kuitunza. Nayo ni kwamba: \"Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu\" mwenye kufanyiwa uungu, anayeabudiwa. Kwa sababu ana sifa za ukamilifu, na ndiye mwenye neema peke yake, ambaye ni Mwenye nguvu kamili na hekima timilifu."},{"id":5477,"sura":45,"from_aya":3,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3 - 5} Kisha akaunga mkono hili kwa ishara za kwenye upeo wa macho na za kinafsi kama vile kuumba mbingu na ardhi, na aliyoyaeneza miongoni mwa wanyama, na aliyoyaweka ndani yake ya manufaa, na maji aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ambayo kwayo Mwenyezi Mungu huhuisha ardhi na waja. Zote hizi ni ishara zilizo wazi na ushahidi wa wazi wa ukweli wa Qur-ani hii tukufu na usahihi wa hekima zilizo ndani yake na hukumu zake mbalimbali, ambazo pia zinaashiria ukamilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ufufuo na kuwatawanya viumbe siku ya Kiyama."},{"id":5478,"sura":45,"from_aya":6,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6 - 10} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawagawanya watu kulingana na kunufaika na Ishara zake au la katika makundi mawili. Kundi la watu wanaozitumia kama ushahidi na kuzitafakari, na kunufaika nazo na kuinuka juu. Na hawa ni wanaomwamini Mwenyezi Mungu, Malaika wake, vitabu vyake, Mitume wake, na Siku ya Mwisho kwa imani kamili, ambayo iliwafikisha katika kiwango cha yakini. Kwa hivyo imani hiyo ikawatakasa akili, ikawaongeza maarifa na ufahamu wao na elimu zao. Na kuna kundi ambalo linasikia ishara za Mwenyezi Mungu kusikia kwa kuwasimamishia tu hoja, kisha wanazipa mgongo na kufanya kiburi kana kwamba hawakuzisikia. Kwa sababu hazikuutakasa moyo wake wala kuusafisha. Bali kwa sababu ya kuzifanyia kwake kiburi, akazidi kupotoka, na kwamba anapojua chochote katika Ishara za Mwenyezi Mungu, anazifanyia mzaha, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akamtishia kwa adhabu kali. Akasema: \"'Ole wake kila mzushi mwenye dhambi!'\" Yaani, mwongo mkubwa katika anayoyasema, mwenye dhambi sana katika vitendo vyake, na akajulisha kuwa atapata adhabu chungu, na kwamba \"nyuma yao ipo Jahannamu,\" ambayo inatosha kuwaadhibu vikali mno, na kwamba \"waliyoyachuma hayatawafaa hata kidogo\" miongoni mwa mali \"wala walinzi waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu.\" Kwa hivyo, wakawa wamewatupa katika wakati ambao waliwahitaji sana, ikiwa wangeweza kuwanufaisha."},{"id":5479,"sura":45,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} Alipofafanua ishara zake za ki Qur-ani na za kuonekana kwa macho, na kwamba watu katika hizo wamegawanyika makundi mawili, akajulisha kwamba Qur-ani hii inayojumuisha mambo haya makubwa ni uwongofu. Akasema: \"Huu ni uwongofu.\" Haya ni maelezo ya jumla ya Qur-ani yote. Kwa maana inaongoza kwenye kumjua Mwenyezi Mungu kwa sifa zake takatifu na matendo yake yenye kusifiwa, na inaongoza kwenye kuwajua Mitume wake, vipenzi wao na maadui zao na sifa zao, na inaongoza kwenye matendo mema, na inalingania kwa hayo na kubainisha matendo mabaya na kuyakataza, na inaongoza katika kubainisha malipo ya matendo, na inabainisha malipo ya duniani na akhera. Kwa hivyo, wale walioongoka waliongoka kwayo, nao basi wakafanikiwa na kuwa na furaha. \"Na wale wale waliozikataa Ishara za Mola wao Mlezi\" zilizo wazi wazi na za uhakika kabisa, ambazo hakuna mwenye kuzikataa isipokuwa mwenye dhuluma kubwa mno na ukazidi upotofu wake, \"watapata adhabu inayotokana na ghadhabu, iliyo chungu.\""},{"id":5480,"sura":45,"from_aya":12,"to_aya":13,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"12. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeifanya bahari ikutumikieni, ili humo zipite merikebu kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na ili mpate kushukuru. 13. Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofikiri. "},{"id":5481,"sura":45,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu fadhila zake juu ya waja wake na wema wake kwao kwa kuitiisha bahari ili vitu vinavyopandwa, kama vile mashua na merikebu, viweze kwenda kwa amri yake na wepesishaji wake, \"na ili mtafute fadhila yake\" kwa aina mbalimbali za biashara na namna mbalimbali za kuchuma, \"na ili mpate kushukuru\" Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa maana, ikiwa mtamshukuru, akakuzidishieni neema zake na akakulipeni malipo makubwa kwa kushukuru kwenu."},{"id":5482,"sura":45,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} \"Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake.\" Yaani, hayo yote ni kutokana na fadhila zake na wema wake. Hayo yanajumuisha vyombo vilivyo mbinguni na duniani, na vyote alivyoweka humo Mwenyezi Mungu kama vile jua, mwezi, sayari zisizosonga na zenye kusonga, na aina mbalimbali za wanyama, miti, mazao, aina mbalimbali za madini na mambo mengineyo ambayo yametayarishwa kwa ajili ya masilahi ya wanadamu ambayo wanayahitaji sana. Hayo yote yanawalazimu kufanya juhudi kubwa zaidi katika kushukuru neema zake, na kwamba fikira zao zizame katika kuzingatia ishara zake na hekima zake, na ndiyo maana akasema: \"Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofikiri.\" Kwa ufupi, uumbaji wake, uendeshaji wake na kuvitiisha kwake vyote vinaonyesha kutekelezeka kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na ukamilifu wa uwezo wake. Na ustadi mkubwa ulio ndani yake, usawasawa wake, ufundi wake wa hali ya juu na maumbile yake mazuri zaidi, yote haya yanaashiria ukamilifu wa hekima yake na elimu yake. Na upana wake, ukubwa wake na wingi wake vinaashiria upana wa ufalme wake na mamlaka yake. Na mambo maalumu yaliyomo, na vitu vilivyo kinyume cha vingine ni ushahidi kwamba Yeye ndiye anafanya kabisa anachotaka. Na manufaa yaliyo ndani yake na masilahi ya kidini na kidunia ni ushahidi wa upana wa rehema yake, ujumla wa fadhila zake na wema wake, na upole wake mkubwa na wema wake, na hayo yote yanaashiria kwamba Yeye peke yake ndiye anayestahiki kufanyiwa uungu na kuabudiwa, ambaye haifai kufanywa ibada wala kujidhalilisha wala kumpenda isipokuwa Yeye, na kwamba Mitume wake ni wakweli katika yale waliyokuja nayo. Huu ni ushahidi wa kiakili ulio wazi, ambao haukubali shaka au kusitasita kokote."},{"id":5483,"sura":45,"from_aya":14,"to_aya":15,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"14. Waambie walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyokuwa wakiyachuma. 15. Mwenye kutenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kutenda uovu ni juu yake mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi. "},{"id":5484,"sura":45,"from_aya":14,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14 - 15} Mwenyezi anaamrisha waja wake waumini kuwa na maadili mema na kuwa na subira juu ya udhia wa wale wanaomshirikisha, wale \"wasiozitaraji siku za Mwenyezi Mungu,\" yaani malipo yake mazuri, na wala hawaogopi namna anavyowafanyia wale wanaomuasi. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa kila watu \"kwa waliyokuwa wakiyachuma.\" Basi, enyi kundi la Waumini atakulipeni thawabu nyingi kwa Imani yenu, msamaha wenu, na subira yenu, na ikiwa wao wataendelea kukadhibisha kwao huko, basi haitakupateni adhabu kali na hizaya kali itakayowapata wao, na ndiyo maana akasema: \"Mwenye kutenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kutenda uovu ni juu yake mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi.\""},{"id":5485,"sura":45,"from_aya":16,"to_aya":17,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"16. Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu, hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote. 17. Na tukawapa maelezo wazi ya amri. Basi hawakuhitalifiana ila baada ya kuwajia elimu kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyokuwa wakihitilafiana. "},{"id":5486,"sura":45,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} Yaani, tuliwaneemesha Wana wa Israili neema ambazo hawakuwahi kupewa wasiokuwa wao miongoni mwa watu, na tukawapa \"Kitabu;\" yaani, Taurati, Injili, kuhukumu baina ya watu, na unabii waliokuwa tofauti sana na watu wengine. Na unabii huo ukawa katika kizazi cha Ibrahim, amani iwe juu yake, ambao wengi wao walikuwa katika Wana wa Israili. \"Na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri\" kama vile vyakula, vinywaji na mavazi, na tukawateremshia Manna na Salwa. \"Na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote.\" Yaani, juu ya viumbe wengineo kwa neema hizi. Ila umma huu unatoka katika ujumla huu wa kimatamshi, kwani wao ndio umma bora kabisa uliowahi kutolewa kwa ajili ya watu. Na muktadha unaonyesha kwamba kinachokusudiwa ni kingine kisichokuwa umma huu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu anatusimulia yale aliyowaneemesha kwayo Wana wa Israili na akawatofautisha na watu wengine (wa zama zao). Na pia, fadhila ambazo kwazo Wana wa Israili walifanywa kuwa bora ni kama vile Kitabu, hekima, Unabii na sifa nyinginezo zote zinazopatikana katika umma huu, na umma huu ukawazidi kwa fadhila nyingi sana. Kwa maana, sheria ya Wana wa Israili ni sehemu katika sheria hii. Kwa maana Kitabu hiki ndicho kinachotawala vitabu vyote vilivyotangulia, naye Muhammad \u2013 rehema na amani ziwe juu yake \u2013 anawasadikisha Mitume wote."},{"id":5487,"sura":45,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} \"Na tukawapa\" Wana wa Israili \"maelezo wazi\" yanayobainisha haki kutokana na batili \"ya amri\" inayohusiana na mipango ya Mwenyezi Mungu ambayo Mwenyezi Mungu aliwafikishia. Na maelezo hayo ni miujiza waliyoiona kupitia mkono wa Musa, amani iwe juu yake. Neema hizi alizowapa Mwenyezi Mungu Wana wa Israili zilihitaji wazitekeleze kwa ukamilifu kabisa, na kwamba waungane juu ya haki ambayo Mwenyezi Mungu aliwabainishia. Lakini jambo hilo likawa kinyume, wakayafanyia kinyume na inavyolazimu, na wakahitilafiana katika yale waliyoamrishwa kuungana ndani yake, na ndiyo maana akasema: \"Basi hawakuhitalifiana ila baada ya kuwajia na elimu;\" yaani, inayofanya wasitofautiane. Na kilichowafanya kutofautiana ni ukandamizaji na dhuluma ya wenyewe kwa wenyewe. \"Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyokuwa wakihitalifiana\" ili apambanue aliye kwenye haki na aliye katika batili, na apambanue aliyehitilafiana kwa sababu ya matamanio au kitu chenginecho."},{"id":5488,"sura":45,"from_aya":18,"to_aya":19,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"18. Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasiojua kitu. 19. Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika wenye kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki msaidizi wa wamchao. "},{"id":5489,"sura":45,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} Yaani, kisha tukakuwekeeni sheria kamili inayolingania kwenye kila heri, na inakataza kila ovu. \"Basi ifuate,\" kwani katika kuifuata kuna furaha ya milele, kutengenea na mafanikio. \"Wala usifuate matamanio ya wasiojua kitu.\" Yaani, wale ambao matamanio yao hayafuati elimu. Nao ni kila mwenye kuhalifu sheria ya Mtume \u2013 rehema na amani ziwe juu yake \u2013 katika matamanio yake na utashi wake. Hayo ni katika matamanio ya wale wasiojua."},{"id":5490,"sura":45,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} \"Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu.\" Yaani, hawatakunufaisha kwa Mwenyezi Mungu, wakakufikishia heri na kukuondolea uovu ikiwa utawafuata katika matamanio yao, na wala hamfai kukubaliana nao na kuwafanya wasaidizi wako. Kwa sababu wewe na wao mnatofautiana sana, na wao wenyewe kwa wenyewe ni vipenzi wanaosaidiana. \"Na Mwenyezi Mungu ni rafiki msaidizi wa wamchao.\" Anawatoa katika giza mbalimbali hadi kwenye nuru kwa sababu ya uchamungu wao na kumtii kwao."},{"id":5491,"sura":45,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"20. Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uwongofu na rehema kwa watu wenye yakini."},{"id":5492,"sura":45,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Yaani, \"hii\" Qur-ani Tukufu na Ukumbusho wenye hekima \"ni dalili zilizo wazi kwa watu wote.\" Yaani, kwazo watu wanaweza kuona kwa uwazi kila jambo, na kwa hayo manufaa yanawafikia Waumini, \"na\" uwongofu na rehema \"kwa watu wenye yakini.\" Basi kwa hizo wanaongoka kwenye njia iliyonyooka katika misingi ya Dini na matawi yake, na wanapata kwayo heri na furaha katika dunia na akhera, nayo ni rehema. Kwa hivyo nafsi zao zinatakasika kwayo, inazitia nguvu akili zao, inawazidishia imani na yakini, na hoja inasimama kwayo mwenye kuendelea kuasi na akafanya ukaidi."},{"id":5493,"sura":45,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"21. Je, wanadhani wale wanaotenda maovu kuwa tutawafanya wawe sawa sawa na wale walioamini, na wakatenda mema, uhai wao na kufa kwao? Ni hukumu mbaya mno wanayoihukumu!"},{"id":5494,"sura":45,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} Yaani, au je, wale watendao mabaya, madhambi mengi na wakapuuza sana haki za Mola wao Mlezi wanadhani kwamba \"tutawafanya kama walioamini na wakatenda mema?\" Wale waliotekeleza haki za Mola wao Mlezi, wakajiweka mbali na mambo yanayomkasirisha na wakaendelea kupendelea mambo yanayomridhisha na wakaacha matamanio yao wenyewe. Yaani, je, wanadhani kwamba watakuwa \"sawa sawa\" na wao hapa duniani na akhera? Ni kibaya muno walichofikiri na kudhani, na ni hukumu mbaya muno hiyo wanayoihukumu! Kwani ni hukumu inayopingana na hekima ya Mbora zaidi wa wanaohukumu na Mbora zaidi wa wafanyao uadilifu, na inapingana na akili timamu na maumbile asili yaliyonyooka, na inapingana na yale yaliyoteremshwa katika vitabu na yakasemwa na Mitume. Bali hukumu iliyoko ya uhakika kabisa ni kwamba waumini wanaotenda mema watapata ushindi, kufaulu, furaha na malipo ya sasa na ya baadaye, kila mmoja kulingana na wema wake. Na kwamba watendao mabaya watapata ghadhabu, fedheha, adhabu na kuwa mashakani duniani na akhera."},{"id":5495,"sura":45,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"22. Na Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili kila nafsi ilipwe yale iliyoyachuma. Nao hawatadhulumiwa."},{"id":5496,"sura":45,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} Yaani, Mwenyezi Mungu aliziumba mbingu na ardhi kwa hekima, na ili aabudiwe Yeye peke yake, bila ya mshirika yeyote. Kisha baada ya hayo atawalipa wale walioamrishwa kumwabudu, akawaneemesha kwa neema za dhahiri na zilizofichika. Je, walimshukuru Mungu Mwenyezi Mtukufu na kutekeleza waliyoamrishwa? Au walikufuru na wakastahiki malipo ya mwenye kukufuru?"},{"id":5497,"sura":45,"from_aya":23,"to_aya":26,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"23. Je, umemwona aliyefanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akampoteza pamoja na kuwa ana elimu, na akaziba masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi ni nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Je, hamkumbuki? 24. Na walisema: 'Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinachotuangamiza isipokuwa dahari.' Lakini wao hawana elimu ya hayo, ila wao wanadhani tu. 25. Na wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema: 'Waleteni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wasemao kweli.' 26. Sema: 'Mwenyezi Mungu anawahuisha, kisha anawafisha, kisha anawakusanya Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui.' "},{"id":5498,"sura":45,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} Mwenyezi Mungu anasema: \"Je, umemwona\" mtu mpotovu ambaye \"aliyafanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake?\" Basi kila anachokitamani, anakifanya. Sawa kiwe ni cha kumridhisha Mwenyezi Mungu au ni cha kumchukiza. \"Na Mwenyezi Mungu akampoteza pamoja na kuwa ana elimu,\" au Mwenyezi Mungu akampoteza baada ya kujua kwamba hafailii uwongofu, wala hawezi kutakasika kwa huo. \"Na akaziba masikio yake,\" kwa hivyo hawezi kusikia yatakayomnufaisha, \"na moyo wake,\" kwa hivyo hawezi kuelewa mambo ya heri, \"na akambandika vitanga machoni mwake\" vikamzuilia kuona haki. \"Basi ni nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu?\" Ilhali Mwenyezi Mungu ameshamfungia milango ya uwongofu na akamfungulia milango ya upotofu, na wala Mwenyezi Mungu hakumdhulumu, lakini yeye mwenyewe ndiye aliyejidhulumu, na akajisababishia kunyimwa rehema za Mwenyezi Mungu. \"Je, hamkumbuki\" yenye kuwanufaisha mkayafuata, na yenye kuwadhuru, mkayaepuka?"},{"id":5499,"sura":45,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} \"Na walisema\" wale waliokanusha kufufuliwa: \"Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinachotuangamiza isipokuwa dahari.\" Yaani, mazoea na mambo kutendeka kulingana na kwenda kwa usiku na mchana, watu wanakufa na wengine wanaishi. Na chenye kufa, hicho hakirudi kwa Mwenyezi Mungu wala hakilipi kwa matendo yake. Lakini kauli yao hii ilitokana na sintojua yao, \"ila wao wanadhani tu.\" Basi wakapinga viumbe kurudishwa Siku ya Kiyama, na wakawakadhibisha Mitume wakweli bila ya ushahidi uliowaonyesha hayo wala hoja. Haya si chochote ila ni dhana tu na kupinga mambo bila ya uhakika wowote."},{"id":5500,"sura":45,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: \"Na wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema: 'Waleteni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wasemao kweli.\" Huku ni kufanya kwao ujasiri dhidi ya Mwenyezi Mungu, kwa kupendekeza pendekezo hili na kudai kwamba ukweli wa Mitume wa Mwenyezi Mungu unategemea kuwaleta baba zao, na kwamba hata ikiwa watawajia na kila ishara, hawataamini, isipokuwa ikiwa Mitume watawafuata katika yale waliyoyasema. Lakini wao ni waongo katika hayo waliyoyasema. Makusudio yao makubwa ni kukataa wito wa Mitume, siyo kueleza haki."},{"id":5501,"sura":45,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: \"Sema: 'Mwenyezi Mungu anawahuisha, kisha anawafisha, kisha anawakusanya Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui.\" Vinginevyo, ikiwa kujua kwa Siku ya Mwisho kungefika kwenye nyoyo zao, basi wangeufanyia matendo na kujiandaa vyema kwa ajili yake."},{"id":5502,"sura":45,"from_aya":27,"to_aya":37,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"27. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama, siku hiyo wataangamia wenye kushikamana na upotovu. 28. Na utauona kila umma umepiga magoti, na kila umma utaitwa kwenda kusoma kitabu chake: Leo mtalipwa mliyokuwa mkiyatenda. 29. Hiki kitabu chetu kinasema juu yenu kwa haki. Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika mliyokuwa mkiyatenda. 30. Ama walioamini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawatia katika rehema yake. Huko ndiko kufuzu kuliko wazi. 31. Na ama waliokufuru wataambiwa: 'Kwani hamkuwa mkisomewa Aya zangu nanyi mkapanda kichwa, na mkawa watu wakosefu?' 32. Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Saa haina shaka, nyinyi mlikuwa mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini. 33. Basi ubaya wa yale waliyoyatenda utawadhihirikia, na yatawafika yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara. 34. Na itasemwa: 'Leo tunawasahau kama nyinyi mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wa kuwanusuru.' 35. Hayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao. 36. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote. 37. Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. "},{"id":5503,"sura":45,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27}  Mwenyezi Mungu anajulisha juu ya upana wa ufalme wake na kwamba Yeye peke yake ndiye anayeendesha na kusimamia mambo yote wakati wote, na kwamba \"siku itakaposimama Saa ya Kiyama\" na viumbe vikusanywe kwa ajili ya kisimamo cha siku hii, hasara kubwa itawafikia wanabatili. Wale walioleta batii ili kuiangusha kwayo haki, na matendo yao yalikuwa ni batili kwa kuwa yalifungamana na batili. Hiyo ndiyo siku ambayo hakika mbalimbali zitabainika na ipotelee mbali batili, kisha watakosa malipo mazuri na wapate adhabu iumizayo."},{"id":5504,"sura":45,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeleza ukali na mahangaiko ya Siku ya Kiyama ili waja wajihadhari nayo na wajiandae kwa ajili yake. Akasema: \"Na utauona\" ewe mwenye kuona siku hiyo, \"kila umma umepiga magoti\" kwa hofu, kufadhaika na kungojea hukumu ya Mfalme, Mwingi wa rehema. \"Kila umma utaitwa kwenda kusoma kitabu chake.\" Yaani, kwenye sheria ya Mtume wao aliyewajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na je waliitekeleza; ili wapate malipo mazuri na wokovu? Au waliipoteza; kwa hivyo wapate hasara? Basi umma wa Musa wataitwa kwenye sheria ya Musa, na umma wa Isa utaitwa vivyo hivyo, na umma wa Muhammad utaitwa vivyo hivyo, na wengineo vile vile. Kila umma utaitwa kwenye sheria yake ambayo ulijukumishwa.' Huu ni uwezekano mmoja wa maana za Aya hii, nao ndio wenye maana sahihi yenyewe, usio na shaka yoyote. Na inawezekana kwamba kile kinachokusudiwa na kauli yake: \"Na kila umma utaitwa kwenda kusoma kitabu chake,\" ni kitabu cha matendo yake waliyoandikiwa; mema na mabaya, na kwamba kila mtu atalipwa kwa aliyoyafanya yeye mwenyewe. Kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Anayetenda mema, basi anajitendea mwenyewe nafsi yake. Na mwenye kutenda uovu, basi ni juu ya nafsi yake vile vile.\" Na inawezekana kwamba maana zote mbili zimekusudiwa na Aya hii."},{"id":5505,"sura":45,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Haya yanaonyeshwa na kauli yake: \"Hiki kitabu chetu kinasema juu yenu kwa haki.\" Yaani, hiki ni Kitabu chetu tulichowateremshia, kinachoamua [baina yenu] kwa haki, ambayo ni uadilifu. \"Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika mliyokuwa mkiyatenda.\" Basi hiki hapa ni kitabu cha matendo yenu."},{"id":5506,"sura":45,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Ndiyo maana akabainisha kwa kina yale ambayo Mwenyezi Mungu atawafanyia makundi mawili hayo akisema: \"Ama walioamini na wakatenda mema\" kwa Imani ya sahihi, wakasadikisha imani yao kwa matendo mema ya lazima na yasiyokuwa ya lazima, \"Mola wao Mlezi atawatia katika rehema yake\" ambayo mahali pake ni katika Bustani za mbinguni, na vilivyomo ndani yake vya neema ya kudumu na uhai ulio salama. \"Huko ndiko kufuzu kuliko wazi\" ambako kunapomtokea mja, basi anakuwa amepata kila heri, na akazuilika na kila ovu."},{"id":5507,"sura":45,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} \"Na ama waliokufuru\" Mwenyezi Mungu wataambiwa kwa kukemewa na kukaripiwa: \"Kwani hamkuwa mkisomewa Aya zangu nanyi,\" na zikawaonyesha yenye heri kwenu na zikakukatazeni yenye kuwadhuru, na hii ndiyo neema kubwa zaidi iliyowahi kuwafikia lau mngewezeshwa kuzikubali. Lakini mlizifanyia kiburi, mkazipa mgongo na mkazikufuru, basi mkawa mmefanya kosa kubwa zaidi na uhalifu mkubwa zaidi. Kwa hivyo, leo mtalipwa kwa yale mliyokuwa mkitenda.'"},{"id":5508,"sura":45,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} Na watakaripiwa pia kwa kauli yake: \"Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Saa haina shaka, nyinyi mlikuwa mkisema\" kwa njia ya kukanusha: \"Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini.\" Basi hii ndiyo hali yao katika dunia, na hali ya kufufuliwa ni kukanusha, na wakaikataa kauli ya yule aliyeyaleta."},{"id":5509,"sura":45,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: \"Basi ubaya wa yale waliyoyatenda utawadhihirikia.\" Yaani, itawadhihirikia adhabu ya vitendo vyao Siku ya Kiyama, \"na yatawafika yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara\" katika dunia hii. Kwani walikuwa wakifanyia masihara kutokea kwake na pia walikuwa wakimfanyia masihara aliyekuwa na habari hii."},{"id":5510,"sura":45,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} \"Na itasemwa: 'Leo tunawasahau,\" na tunawaacha katika adhabu \"kama nyinyi mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii.\" Kwani, malipo ni ya aina sawa na matendo, \"na mahali penu ni Motoni.\" Yaani, hapo ndipo mahali mtakapokaa na ndiyo maishio yenu, \"wala hamna wa kuwanusuru\" atakayewanusuru kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuwakinga adhabu yake."},{"id":5511,"sura":45,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} \"Hayo\" yaliyowapata ya adhabu ni kwa sababu \"nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu\" ingawa zilihitaji kuwa mtu kuzikakamia na kuzifanyia bidii na kuzipokea kwa furaha na bishara njema. \"Na maisha ya dunia yakawadanganya\" kwa mapambo yake na matamanio yake, basi kila mmoja akatulizana juu yake, na mkayafanyia matendo mbalimbali, na mkaacha kufanyia matendo nyumba ya kubakia milele.' \"Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao\" na tena hawatarejeshwa duniani ili wafanye mema."},{"id":5512,"sura":45,"from_aya":36,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36} \"Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu\" kama upasavyo utukufu wa uso wake na ukubwa wa mamlaka yake, \"Mola Mlezi wa mbingu na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote.\" Yaani, ana sifa njema kwa sababu ya umola wake juu ya viumbe vyote, ambapo aliwaumba, akawalea, akawaneemesha kwa neema za dhahiri na zilizofichika."},{"id":5513,"sura":45,"from_aya":37,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37} \"Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi.\" Yaani, ni wake utukufu, ukuu na heshima kubwa. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu anasifika kwa sifa njema za ukamilifu, anapendwa na anatukuzwa. Na pia Yeye ni mwenye ukubwa, ukuu na heshima kubwa mno. Kwani, ibada imejengwa juu ya nguzo mbili: kumpenda Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea. Na mawili hayo yanatokana na kujua sifa njema za Mwenyezi Mungu, utukufu wake na ukubwa wake. \"Naye ni Mwenye nguvu,\" aliyeshinda kila kitu. \"Mwenye hekima,\" anayeweka vitu mahali pake pa sawasawa. Kwa hivyo, hawezi kuweka sheria alizoweka isipokuwa kwa hekima na masilahi, na wala haumbi anachokiumba isipokuwa kwa masilahi na manufaa."},{"id":5514,"sura":45,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya surat Al-Jathiya, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na neema na fadhila."},{"id":5515,"sura":45,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}