{"result":[{"id":5564,"sura":47,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Al-Qital"},{"id":5565,"sura":47,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Madina"},{"id":5566,"sura":47,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":5567,"sura":47,"from_aya":1,"to_aya":3,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao. 2. Na wale walioamini, na wakatenda mema, na wakaamini yale aliyoteremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi - atawafutia makosa yao na ataitengeneza hali yao. 3. Hayo ni kwa sababu wale waliokufuru wamefuata upotovu, na wale walioamini wamefuata Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowapigia watu mifano yao. "},{"id":5568,"sura":47,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Aya hizi zinajumuisha kutajwa malipo ya Waumini, adhabu ya wafanyao maasi, sababu ya hayo, na kuwalingania viumbe kuzingatia hayo. Mwenyezi Mungu akasema: \"Wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu\" Hawa ndio viongozi wa ukafiri na maimamu wa upotofu, ambao walichanganya kati ya kumkufuru Mwenyezi Mungu na ishara zake na kujizuilia wao wenyewe na wengineo mbali na njia ya Mwenyezi Mungu, ambayo ni kuamini yale waliyoyalingania Mitume na kuifuata. Basi hawa \"Yeye\" Mwenyezi Mungu \"atavipotoa vitendo vyao\" na kuwatia mashakani kwa sababu yake. Na hili linajumuisha matendo yao waliyoyafanya kwa ajili ya kufanya vitimbi dhidi ya haki na vipenzi wa Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu akatia vitimbi vyao hivyo kwenye koo zao, kwa hivyo hawakupata chochote katika yale waliyokusudia, na vitendo vyao wanavyotarajia kulipwa juu yake, Mwenyezi Mungu ataviharibu. Na sababu yake ni kwamba walifuata batili, ambao ni kila lengo ambalo mja hataki kwalo uso wa Mwenyezi Mungu, kama vile kuabudu masanamu na miungu. Na kwa sababu matendo yaliyofanywa kwa ajili ya kuunga mkono batili ni batili pia, basi matendo yanayofanywa kwa ajili yake ni batili pia."},{"id":5569,"sura":47,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Ama \"wale walioamini\" katika yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume wake kwa ujumla na kwa Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - hasa  \"na wakatenda mema\" kwa kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu zilizoko juu yao na haki za waja wake za lazima na zisizokuwa za lazima, \"atawafutia makosa yao\" madogo na makubwa. Na wakishasamehewa makosa yao, watakuwa wameokoka na adhabu ya duniani na ya Akhera, \"na ataitengeneza vizuri hali yao\" ya kidini, kidunia, nyoyo zao, na matendo yao, na atazitengeneza thawabu zao kwa kuzikuza na kuzitakasa, na atatengeneza hali zao zote kuwa nzuri."},{"id":5570,"sura":47,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} Sababu ya hayo ni kwamba waliifuata haki, ambayo ni ukweli na yakini, na yale yaliyomo ndani ya Qur-ani hii tukufu iliyotoka kwa Mola wao Mlezi, ambaye aliwanyanyua kwa fadhila zake na akawalea kwa neema zake, na akawaendesha kwa upole wake. Basi Yeye Mtukufu akawalea kwa haki, hivyo wakaifuata, kwa hivyo mambo yao yakatengenea. Na kwa kuwa lengo lililokusudiwa kwao lilihusiana na haki inayonasibishwa na Mwenyezi Mungu, Mwenye kubakia, wa Haki, aliye wazi, njia hiyo ikawa nzuri na ya kudumu, na yenye malipo ya kubakia. \"Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowapigia watu mifano yao.\" Ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaeleza watu wema na watu waovu, na akawatajia sifa za kila mmoja ambazo kwazo wanajulikana na ni maalumu kwao tu. Ili mwenye kuangamia aangamie kwa hoja iliyo wazi, na mwenye kusalia hai asalie hai kwa hoja iliyo wazi."},{"id":5571,"sura":47,"from_aya":4,"to_aya":6,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"4. Basi mnapowakuta wale waliokufuru, wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha, wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndivyo hivyo. Na lau angelitaka Mwenyezi Mungu, angeliwashinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu awatie mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na wale waliouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, hatayapoteza matendo yao. 5. Atawaongoza na awatengezee hali yao. 6. Na atawaingiza katika Pepo aliyowajuulisha. "},{"id":5572,"sura":47,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akiwaelekeza waja wake katika yale yaliyo mazuri kwao kuwapa ushindi dhidi ya maadui zao: \"Basi mnapowakuta wale waliokufuru\" katika vita, basi piganeni nao kweli kweli kwa kupigana shingo zao mpaka muwadhoofishe na mvunje nguvu zao na mbatilishe maovu yao. Mkifanya hivyo na mkaona kwamba kuwashikilia mateka ndilo bora zaidi, \"wafungeni pingu sawasawa.\" Hilo ni ili wasikimbie wakatoroka, na kwa kufanya hivyo, Waislamu wanakuwa na utulivu kutokana na vita vyao na uovu wao. Na hapo mna hiyari baina ya kuwaachilia bure bila ya kulipa mali wala kujikomboa, au mnaweza kuwataka wajikomboe kwa kujinunua wenyewe, au wenzao wawanunue kwa mali au kwa mateka Mwislamu waliye naye. Jambo hili litaendelea hivi \"mpaka vita vipoe\" kwa kuweka mkataba wa amani. Kwa maana kila nafasi ina maneno yake maalumu, na kila hali ina hukumu yake. Hali iliyotangulia hapo juu ni ikiwa tu kuna vita. Lakini ikiwa katika wakati mwingine hakuna vita kwa sababu yoyote ile, basi hakutakuwa na mauaji wala mateka. \"Ndivyo hivyo\" ilivyo hukumu iliyotajwa katika kuwajaribu Waumini kwa makafiri na kuhitalifiana kwa siku mbalimbali baina yao na wao kwa wao kushindana. \"Na lau angelitaka Mwenyezi Mungu, angeliwashinda mwenyewe.\" Kwani kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu, na anaweza kuwafanya makafiri wasishinde hata mahali pamoja mpaka Waislamu waangamize vitu vyao vizuri vyote. \"Lakini haya ni kwa sababu awatie mitihani nyinyi kwa nyinyi\" ili Jihadi iweze kusimama imara, na kwa hilo zibainike hali za waja wa ukweli na  waongo, na ili anayeamini aamini imani sahihi kwa elimu ya sawasawa, siyo imani iliyojengeka juu ya kuwafuata wenye ushindi tu. Hiyo hakika ni imani dhaifu sana, ambayo mwenyewe hawezi kudumu juu yake wakati wa majaribio na misiba. \"Na wale waliouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu\"  watapata thawabu nyingi na ujira mzuri, na hao ndio wale waliopigana na wale ambao waliamrishwa kupigana nao; ili neno la Mwenyezi Mungu liwe ndilo la juu zaidi. Hao, Mwenyezi Mungu \"hatayapoteza matendo yao.\" Yaani hatayaangusha na kuyabatilisha, bali atayakubali na kuyakuza kwa ajili yao na ataonyesha matokeo ya matendo yao katika dunia hii na akhera."},{"id":5573,"sura":47,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} \"Atawaongoza\" wafuate njia yenye kufikisha katika Bustani ya mbinguni, \"na awatengezee hali yao kuwa nzuri.\" Yaani, hali na mambo yao, na malipo yao yatakuwa mazuri na kamili, bila ya ubaya wowote wala dhiki kwa namna yoyote ile."},{"id":5574,"sura":47,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} \"Na atawaingiza katika Pepo aliyowajuulisha.\" Yaani: Kwanza alibainishia kwa kuwafanya kuwa na shauku kubwa nayo, akawaelezea namna ilivyo, na kuwatajia matendo yanayowafikisha huko, ambayo miongoni mwake ni kuuawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, na akawawezesha kufanya aliyowaamrisha akawahimiza zaidi kufanya hivyo, kisha watakapoingia Peponi, atawajulisha nyumba zao na neema za milele zilizomo humo na maisha ya amani."},{"id":5575,"sura":47,"from_aya":7,"to_aya":9,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"7. Enyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu, naye atawanusuruni na ataiimarisha miguu yenu. 8. Na wale waliokufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao. 9. Hayo ni kwa sababu waliyachukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao. "},{"id":5576,"sura":47,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Hii ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Waumini kumnusuru Mwenyezi Mungu kwa kushikamana sawasawa katika dini yake, kuilingania, na kupigana jihadi dhidi ya maadui zake, na kuukusudia uso wa Mwenyezi Mungu katika hayo. Kwani katika hakika wakifanya hivyo, Yeye atawanusuru na aifanye miguu yao kuwa imara. Yaani, anazifunga nyoyo zao kwa subira, utulivu mkubwa, uthabiti, na ataifanya miili yao kuwa na subira kwa hayo, na kuwasaidia dhidi ya maadui zao. Hii ni ahadi kutoka kwa Mwingi wa Ukarimu ambaye ni mkweli katika ahadi yake kwamba mwenye kumnusuru kwa kauli na matendo, Mola wake atamnusuru na amrahisishie njia za ushindi, kama vile uthabiti na mambo mengineyo."},{"id":5577,"sura":47,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} Ama wale waliomkufuru Mola wao Mlezi na wakainusuru batili, wamo katika mashaka makubwa na kurudi nyuma katika mambo yao na kuachiliwa mbali bila ya kusaidiwa, \"na atavipoteza vitendo vyao.\" Yaani, atavibatilisha vitendo vyao walivyoipangia njama dhidi ya haki, basi vitimbi vyao hivyo vikarejea kooni mwao, na vikabatilika vitendo vyao walivyodai kuwa wanatafuta uso wa Mwenyezi Mungu kwavyo."},{"id":5578,"sura":47,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} Huko kupotoshwa na kutiwa mashakani kwa wale waliokufuru ni kwa sababu wao \"waliyachukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu\" katika Qur-ani ambayo [Mwenyezi Mungu] aliiteremsha kwa ajili ya kuwatengeneza waja wake na kwa ajili ya kufaulu kwao, lakini wao hawakuikubali. Bali walikereka nayo na kuichukia, \"basi akaviangusha vitendo vyao.\""},{"id":5579,"sura":47,"from_aya":10,"to_aya":11,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"10. Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mifano ya hayo. 11. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini. Na makafiri hawana mlinzi. "},{"id":5580,"sura":47,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} Yaani kwa nini hawa wanaomkadhibisha Mtume \u2013 rehema na amani zimshukie \u2013 hawatembei \"wakaona ulikuwaje mwisho wa wale waliokuwa kabla yao?\" Kwani hawatapata mwisho wao chochote isipokuwa ulikuwa mwisho mbaya zaidi. Kwa maana hawageuki kuliani wala kushotoni ila wataona wameshapotelea mbali na kuangamia, na wakaang'olewa kabisa kabisa na kukadhibisha kwao na ukafiri wao, basi wakazimika. Na Mwenyezi Mungu akaziharibu mali zao na makazi yao, na hata akaviharibu vitendo vyao na njama zao. Basi makafiri katika kila wakati na sehemu wanayo matokeo mabaya sawa na adhabu hizi kubwa na adhabu hizi mbaya zaidi. Ama Waumini, Mwenyezi Mungu Mtukufu huwaepusha adhabu na huwapa malipo mengi."},{"id":5581,"sura":47,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} \"Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini.\" Basi akawachunga kwa rehema yake, na akawatoa katika giza mbalimbali na akawapeleka kwenye nuru, na akasimamia malipo yao na ushindi wao. \"Na kwamba makafiri\" waliomkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambapo walikata ulinzi wa Mwenyezi Mungu kutoka kwao, na wakajiweka mbali wenyewe na rehema yake \"hawana mlinzi\" anayeweza kuongoza kufikia njia za amani, na kuwaokoa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso yake. Bali walinzi wao ni Taghut (mashetani na waovu wote), ambao wanawatoa kwenye nuru na kuwaingiza katika giza mbalimbali. Hao ndio wenza  wa Moto, humo watadumu milele."},{"id":5582,"sura":47,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"12. Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema katika Bustani za mbinguni zipitiwazo na mito kati yake. Na wale waliokufuru hujifurahisha na hula kama walavyo wanyama, na Moto ndio makazi yao."},{"id":5583,"sura":47,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuwa Yeye ndiye mlinzi wa Waumini, akataja watakayofanyiwa Akhera ya kuingia katika Bustani zipitazo mito kati yake, zinyweshazo bustani hizo zinazong'aa kwa uzuri, na miti mizuri yenye matunda. Zina kila jozi yenye furaha, na kila tunda lenye ladha. Na alipotaja kwamba makafiri hawana mlinzi, akasema kwamba wameachiwa wenyewe, kwa hivyo hawakusifika kwa sifa za heshima wala sifa za kibinadamu. Bali walishuka kutoka huko matabaka, na wakawa kama wanyama wasio na akili wala heshima. Bali hima yao kuu katika maisha yao na lengo lao ni kufurahia starehe za dunia na matamanio yake. Kwa hivyo utaona harakati zao za nje na za ndani zikizungukia hapo bila kuvuka kwenda kwenye mambo ya heri na furaha, na ndiyo maana Moto utakuwa makazi yao yaliyoandaliwa kwa ajili yao. Hawatatoka humo wala hawatapunguziwa katika adhabu yake."},{"id":5584,"sura":47,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"13. Na ni miji mingapi iliyokuwa na nguvu zaidi kuliko mji wako huu uliokutoa? Tuliwateketeza na wala hawakuwa na yeyote wa kuwanusuru."},{"id":5585,"sura":47,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Yaani, ni miji mingapi miongoni mwa miji ya wale waliokadhibisha ilikuwa ni yenye nguvu zaidi kuliko mji wako kwa mali, watoto, wasaidizi, majengo na ala mbalimbali, tuliwaangamiza walipowakadhibisha Mitume wetu, na wala mawaidha hayakuwafaa kitu. Kwa hivyo hatukuwapata wakiwa na yeyote wa kuwanusuru, na wala nguvu zao hazikuwafaa chochote mbele ya adhabu ya Mwenyezi Mungu. Basi vipi hali ya hawa wanyonge wana kijiji chako walipokufukuza katika mji wako, wakakukadhibisha na wakakufanyia uadui, ilhali wewe ndiye mbora wa Mitume wote na mbora wa wa mwanzo na wa mwisho? Je, wao hawastahiki zaidi kuangamizwa na kuadhibiwa kuliko wengineo, lau kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakumtuma Mtume wake kwa rehema na kutokuwa na haraka juu ya kila kafiri na mwenye kukataa?"},{"id":5586,"sura":47,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"14. Je, yule aliye kwenye ubainifu kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama yule aliyepambiwa uovu wa vitendo vyake, na wakafuata matamanio yao?"},{"id":5587,"sura":47,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} Yaani: Hawi sawa mwenye ufahamu mzuri wa mambo ya dini yake katika elimu na vitendo. Aliijua haki na akaifuata, na akataraji aliyowaahidi Mwenyezi Mungu wana haki. Yeye hawi sawa na mtu ambaye ni kipofu wa moyo, aliyeikataa haki, akaipotosha, na akafuata matamanio yake bila ya uwongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na pamoja na hayo anaona kwamba ayafanyayo hayo ndiyo haki. Basi ni tofauti kubwa iliyoje hii kati ya makundi haya mbili! Wana haki na wana upotovu."},{"id":5588,"sura":47,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"15. Mfano wa Bustani ya mbinguni waliyoahidiwa wachamngu, ina mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa yasiyoharibika ladha yake, na mito ya mvinyo wenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakaodumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayochemka ya kuwakatakata matumbo yao?"},{"id":5589,"sura":47,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15} Yaani mfano wa Bustani ya mbinguni aliyowaandalia Mwenyezi Mungu waja wake walioogopa ghadhabu yake na wakafuata radhi yake, \"ina mito ya maji yasiyovunda.\" Si kwa uvundo wala kwa harufu inayonuka ya kuoza, wala si machungu, wala hayakuchafuliwa. Bali hayo ndiyo maji safi zaidi, yenye harufu nzuri zaidi, na ladha nzuri zaidi ya kunywa. \"Na mito ya maziwa yasiyoharibika ladha yake\" kwa kuchacha wala kitu kingine chochote. \"Na mito ya mvinyo wenye ladha kwa wanywao.\" Yaani, mnywaji wake atafurahia ladha yake nzuri sana, si kama mvinyo wa dunia hii, ambao ladha yake inachukiwa, unaumiza kichwa, na kuvuruga akili. \"Na mito ya asali iliyosafishwa mno\" kutokana na nta yake na uchafu wake wote. \"Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda\" kama vile mitende, mizabibu, tufaha, mikomamanga, mikorogo, tini, na mengineyo miongoni mwa yale yasiyokuwa na mfano wake hapa duniani. Basi kipendwa hiki kinachotafutwa tayari wameshakipata. Kisha akasema: \"Na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi\" ambayo kwayo yataondoka kila yanayokimbiwa. Basi huyu ndiye aliye bora zaidi au ni  wale \"watakaodumu Motoni\" ambao joto lake ni kali sana, na adhabu yake inazidishwa maradufu \"na wakinyweshwa\" humo \"maji yanayochemka\" mno \"na yakawakatakata matumbo yao.\" Basi ametakasika Yule aliyetofautisha baina ya nyumba mbili hizi, malipo mawili haya, watendao wawili hawa na matendo mawili haya."},{"id":5590,"sura":47,"from_aya":16,"to_aya":17,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"16. Na wapo miongoni mwao wanaokusikiliza, mpaka wakiondoka kwako, huwauliza waliopewa elimu: 'Amesema nini sasa hivi?' Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu ameziba nyoyo zao, na wakafuata matamanio yao. 17. Na wale walioongoka anawazidishia uongofu na anawapa uchamungu wao. "},{"id":5591,"sura":47,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Na miongoni mwa wanaafiki yupo \u201cwanaokusikiliza,\u201d mnayoyasema; kusikiza si kwa kuridhia na kunyenyekea, bali nyoyo zao zikajiepusha nayo, na kwa ajili hiyo akasema: \"mpaka wakiondoka kwako, huwauliza waliopewa elimu\" juu ya yale uliyoyasema na yale waliyoyasikia katika yale wasiyokuwa na hamu nayo: \"Amesema nini sasa hivi?\" Hili ni la kuwakashifu mno, kwa maana ikiwa walikuwa na hamu kubwa ya kufanya mema, wangempa vyema masikio yao, na nyoyo zao zingemuelewa, na viungo vyao vingemfuata. Lakini wao wako kinyume na hali hii, na ndiyo maana akasema: \"Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu ameziba nyoyo zao.\" Yaani, aliwafungia milango ya heri ambayo kupitia hiyo inaifikia nyoyo. Na hilo ni kwa sababu ya kufuata kwao matamanio yao ambayo ndani yake hawatamani ila batili tu."},{"id":5592,"sura":47,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} Kisha akabainisha hali ya walioongoka, na akasema: \"Na wale walioongoka\" kwa Imani, utiifu, na kuyafuata anayoyaridhia Mwenyezi Mungu \"anawazidishia uongofu\" iwe ni shukrani yake kwao juu ya hayo, \"na anawapa ucha Mungu wao.\" Yaani, huwaongoza kwenye heri na kuwalinda kutokana na maovu. Basi hapa akataja malipo mawili kwa walioongoka: elimu yenye manufaa na matendo mema."},{"id":5593,"sura":47,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"18. Kwani wanangojea jengine isipokuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla? Na hakika alama zake zimekwishakuja. Na itakapowajia, kutawafaa nini kukumbuka kwao?"},{"id":5594,"sura":47,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} Maana yake ni kwamba hawa wanaokadhibisha wanangoja lingine \"isipokuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla\" hali ya kuwa hawajui? \"Na hakika alama zake zimekwisha kuja.\" Yaani, ishara zake zinazoashiria ukaribu wake. \u201cNa itakapowajia, kutawafaa nini kukumbuka kwao?\" Hayo yatakuwa yameshachelewa na wakati wa kukumbuka umeshapita. Kwani, walipewa umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka, na akawajia Mwonyaji? Basi katika haya kuna kutia hamu ya kujiandaa kabla ya kifo kuja ghafla. Kwa sababu, kifo cha mtu ndiyo kusimama kwa Saa yake (ya Kiyama)."},{"id":5595,"sura":47,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"19. Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa."},{"id":5596,"sura":47,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} Kuwa na elimu kunalazimu mtu kukiri kwa moyo na kujua vyema maana ya kile anachotakiwa kukifanya, na utimilifu wake ni mtu kufanya matendo kulingana na matakwa yake. Na kujua huku ambako Mwenyezi Mungu aliamrisha ambako ni kujua upweke wa Mwenyezi Mungu, ni wajibu wa mtu binafsi kwa kila mwanadamu, hautoki wajibu huu kwa yeyote yule, bali kila mtu analazimika kujua hivyo. Na njia ya kujua kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu ni mambo mbalimbali: Moja yake - bali kubwa yake zaidi - ni kuyatafakari majina yake, sifa zake, na vitendo vyake vinavyoashiria ukamilifu wake, ukuu wake, na utukufu wake. Hayo kwa hakika yanalazimu mtu kujitahidi mno kumfanyia Mwenyezi Mungu uungu na kumwabudu Mola Mlezi, Mkamilifu, ambaye ni zake sifa njema zote, taadhima, utukufu na uzuri. La pili ni kujua kwamba Yeye ndiye wa pekee katika kuumba na kuendesha mambo. Kwa hivyo inajulikana kwa hayo kwamba Yeye ndiye wa pekee katika uungu. La tatu ni kujua kwamba Yeye ni wa pekee katika neema za dhahiri na zilizofichika, za kidini na za kidunia. Hayo yanalazimu moyo kufungamana naye, kumpenda na kumfanya uungu Yeye peke yake, bila ya mshirika yeyote. La nne ni yale tunayoyaona na kuyasikia juu ya malipo kwa vipenzi wake wanaompwekesha kwamba atawanusuru na kuwapa neema za sasa hivi, na kuwaadhabu maadui zake wanaomshirikisha. Hayo yanamfanya mtu kujua kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahili ibada zote. La tano ni kujua sifa za masanamu na wale wafanywao kuwa wenza wa Mwenyezi Mungu ambao waliabudiwa pamoja na Mwenyezi Mungu na wakachukuliwa kuwa miungu, na kwamba wana mapungufu kwa namna zote, wao wenyewe ni wahitaji sana, hawajimilikii wenyewe wala hawamilikii wale wanaowaabudu manufaa yoyote, madhara, mauti, uhai wala ufufuo, na hawawezi kuwanusuru wale wanaowaabudu, wala kuwanufaisha kwa uzito wa chembe katika kuwaletea heri au kuwazuilia uovu. Kwani kujua hivyo kunalazimu mtu kujua kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu na ubatili wa uungu wa kitu chochote kisichokuwa Yeye. La sita ni kukubaliana kwa Vitabu vya Mwenyezi Mungu juu ya hilo. La saba ni kwamba viumbe maalumu ambao ndio viumbe kamili zaidi katika suala la maadili, akili, rai, kuwa katika usahihi na elimu - nao ni Mitume, Manabii wanaomuabudu Mola wao Mlezi tu - walimshuhudilia Mwenyezi Mungu hilo. La nane ni ushahidi mbalimbali wa kiupeo wa macho na wa kibinafsi ambao Mwenyezi Mungu aliusimamisha juu ya upweke wake ni ushahidi mkubwa zaidi, na huo wenyewe tu kwa kuutazama unalingania hilo kwa sababu ya yale aliyoweka Mwenyezi Mungu ndani yake ya maumbile yenye ustadi mkubwa, hekima yake kubwa zaidi na maajabu ya uumbaji wake. Hizi ndizo njia ambazo Mwenyezi Mungu alizitumia zaidi katika kuwalingania viumbe kwa hizo katika kudhibitisha suala kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, na akaziweka wazi kabisa katika Kitabu chake na akazirudia, na mja anapozitafakari baadhi yake, lazima atakuwa na yakini na elimu ya hilo. Basi itakuwaje kama utakutana na ushahidi huu, na ukakubaliana na ushahidi wa upweke wake ukasimama kutokea kila upande? Hapo, imani na ujuzi wa jambo hili vitakuwa imara katika moyo wa mja, kiasi kwamba utakuwa kama milima dhabiti isiyotikisika kwa sintowazi na dhana potofu, na wala haiongezeki licha ya kurudiarudia kwa batili na sintowazi isipokuwa kukua sawasawa na kukamilika. Hili ni hivyo, na zaidi ni kwamba ukiangalia ushahidi mkubwa na jambo kubwa - ambao ni kuitafakari Qur-ani hii tukufu na kuzitafakari Aya zake, kwani huo ndilo lango kuu kujua elimu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na elimu hiyo inapatikana humo kwa maelezo ya kina kwa namna ambayo haiwezi kupatikana mahali pengine. Na kauli yake: \"Na omba maghufira kwa dhambi zako.\" Yaani, Mwombe Mwenyezi Mungu msamaha kwa dhambi zako, kwa kufanya visababu vya msamaha, kama vile toba, kuomba dua ya msamaha, kutenda matendo mema yenye kufuta dhambi, na kuacha madhambi, na kusamehe makosa. \"na\" pia omba msamaha \"kwa ajili ya Waumini wanaume na Waumini wanawake.\" Kwani, sababu ya imani yao wanakuwa na haki juu ya kila Mwislamu mwanamume na mwanamke, na miongoni mwa haki zao ni kuwaombea dua na kuwaombea msamaha kwa madhambi yao. Na ikiwa aliamrishwa kuwaombea msamaha, ambako kunajumuisha kuwafutia madhambi na adhabu yake, basi miongoni mwa mambo yanayofungamana na hilo ni kuwapa ushairi mzuri, na kuwapendea heri anayojipendea mwenyewe, na kuwachukia ubaya anaojichukia mwenyewe, kuwaamrisha kuwafanya yenye heri kwao, na kuwakataza na yale yenye madhara kwao, na kusamehe makosa yao na mapungufu yao, na kufanya hima kubwa ya kuwakusanya kwa njia ya kuziunganisha nyoyo zao, na kuwaondolea yale yenye kinyongo ambayo yanaweza kusababisha uadui na kutengana kwao; mambo ambayo kwa hayo yanazidi madhambi yao na maasia. \"Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi\" na mkakaa ili kupumzika. Kwa hili anajua harakati zenu na kutulia kwenu, kisha atakulipeni kwa hayo malipo kamili."},{"id":5597,"sura":47,"from_aya":20,"to_aya":23,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"20. Na Waumini wanasema: 'Kwa nini haiteremshwi Sura?' Na inapoteremshwa Sura madhubuti na ikatajwa ndani yake habari ya vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anayezimia kwa sababu ya mauti. Basi ni bora kwao. 21. Utiifu na kauli njema. Na jambo likishaazimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka itakuwa ni heri kwao. 22. Basi mnatarajia kwamba mkigeuka mkaenda zenu kwamba ndio mtafanya uharibifu katika nchi na muwatupe jamaa zenu? 23. Hao ndio aliowalaani Mwenyezi Mungu, na akawatia uziwi, na akawapofua macho yao. "},{"id":5598,"sura":47,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: \"Na Waumini wanasema\" kwa kuzifanyia haraka amri ngumu: \"Kwa nini haiteremshwi Sura?\" Yaani, yenye amri ya kupigana vita. \"Na inapoteremshwa Sura madhubuti.\" Yaani, yenye kuwajibisha kuitekeleza, \"na ikatajwa ndani yake habari ya vita\" jambo ambalo ndilo gumu zaidi kwa nafsi, wale wanyonge wa imani hawawezi kuwa na msimamo imara katika kutekeleza maamrisho haya. Na ndiyo maana akasema: \"Utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anayezimia kwa sababu ya mauti,\" kwa sababu ya kuchukia kwao hayo na ugumu wake juu yao, na hili ni kama kauli ya Mwenyezi Mungu: \"Je, huwaoni wale walioambiwa: 'Izuieni mikono yenu, na mshike Sala na mtoe Zaka.' Na walipoamrishwa kupigana, mara kundi moja kati yao liliwaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu, au kwa hofu kubwa zaidi.\""},{"id":5599,"sura":47,"from_aya":20,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20 - 21} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawahimiza wafanye yanayoifailia zaidi hali yao, akasema: \"Basi ni bora kwao. Utiifu na kauli njema.\" Yaani, ni bora kwao kutekeleza amri iliyopo sasa juu yao, na kuziunganisha hima zao juu yake, na wasiombe kuwekewa sheria ya yale yatakayowawia magumu, na wafurahie usalama wa Mwenyezi Mungu na msamaha wake, \"Na jambo likishaazimiwa.\" Yaani, jambo zito na lisiloepukika likishawajia katika hali hii, basi lau \u201cwakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu\u201d kwa kutafuta msaada wake na kujitahidi kulitekeleza, \u201cbila ya shaka itakuwa ni heri kwao\u201d kuliko hali yao ya awali, na hilo ni kutokana na mambo kadhaa: miongoni mwake ni kwamba mja ni mpungufu katika kila namna, hana uwezo wowote isipokuwa Mwenyezi Mungu akimsaidia; basi na asiombe zaidi ya yale aliyojukumishwa tayari. Na miongoni mwake ni kwamba ikiwa nafsi yake itafungamana na wakati ujao, basi atadhoofika kufanya matendo ya katika wa sasa na pia wakati ujao. Ama wakati wa sasa, hilo ni kwa sababu hima yake tayari imeshahama hadi kwingine, na matendo hufuatana na hima. Na ama siku zijazo, huo hautakuja isipokuwa itakuwa hima yake juu ya ukakamavu itakuwa tayari imeshapunguka, kwa hivyo hataweza kusaidiwa juu yake. Na miongoni mwake ni kwamba mja anayetarajia matarajio ya wakati ujao, pamoja na kwamba ni mzembe wa kufanya matendo katika wakati uliopo, ni sawa na yule anayejigamba ambaye anajiona kwamba ana uhakika juu ya uwezo wake wa kushughulikia mambo yake ya baadaye. Huyo anafailia zaidi kuachiliwa mbali na asiweze kufanya alichokusudia na akaizoesha nafsi yake juu yake. Kwa hivyo, kinachopaswa kufanywa na mja ni kukusanya hima yake, mawazo yake na ukakamavu wake katika wakati wake wa sasa, na kufanya majukumu yake kulingana na uwezo wake. Kisha wakati wowote unapofika, anaupokea kwa ukakamavu na azimio kubwa, iliyounganishwa na sio iliyotengana, akitafuta msaada wa Mola wake Mlezi katika hilo. Mtu huyu anastahili zaidi kufanikishwa na kuwekwa katika usawa katika mambo yake yote."},{"id":5600,"sura":47,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja hali ya mwenye kuacha kumtii Mola wake Mlezi, na kwamba hageuki akaenda kwenye heri, bali anageuka kwenda kwenye uovu, akasema: \"Basi mnatarajia kwamba mkigeuka mkaenda zenu kwamba ndio mtafanya uharibifu katika nchi na muwatupe jamaa zenu?\" Yaani, ni vitu viwili tu: Ima kushikamana na kumtii Mwenyezi Mungu na kufuata amri zake, basi hiyo ndiyo heri na kuwa katika njia ya sawasawa na kufaulu. Au kuyapa mgongo na kuacha kumtii Mwenyezi Mungu, basi hapo hakuna chochote ila uharibfu katika dunia kwa kufanya maasia na kukata mahusiano ya kifamilia."},{"id":5601,"sura":47,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} \"Hao ndio\" wale waliofanya uharibifu katika ardhi, na wakakata jamaa zao kwa hivyo \"aliowalaani Mwenyezi Mungu,\" kwa kuwaweka mbali na rehema zake na wakawa karibu na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu \"na akawatia uziwi, na akawapofua macho yao.\" Yaani, aliwafanya wasikie yenye kuwafaa wala hata hawayaoni. Kwani wana masikio, lakini hawasikii kwa kusikia kwa kutii na kukubali, bali wanasikia kusikia kwa kuwasimamishia hoja ya Mwenyezi Mungu juu yao. Na wana macho lakini hawaoni kwayo mazingatio na ishara, na wala hawaangalii kwayo hoja mbalimbali na ushahidi ulio wazi."},{"id":5602,"sura":47,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"24. Je, hawaizingatii hii Qur-ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli zake?"},{"id":5603,"sura":47,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} Yaani, kwa nini hawa wanaokipa mgongo Kitabu cha Mwenyezi Mungu hawakizingatii na kukitafakari ipasavyo? Kwani ikiwa walikitafakari, kingewaonyesha kila heri, na kingewahadharisha na kila shari, na kingezijaza nyoyo zao imani na sehemu zao za ndani mno kwa yakini, na kingewafikisha kwenye mambo yatafutwayo ya hali ya juu na tunu za thamani kubwa, na kingewabainishia njia inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na Bustani zake za mbinguni, na vyenye kuikamilisha na vyenye kuiharibu, na njia ifikishayo kwenye adhabu, na kwa kitu kipi inaepukwa, na kingewajulisha Mola wao Mlezi, kwa majina yake, na sifa zake, na wema wake, na kingewapa shauku kubwa ya kufikia thawabu nyingi, na kingewahofisha mno adhabu kali zaidi. \"Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli zake?\" Yaani, ziliifunga pamoja na yale yaliyomo ya kupeana mgongo, kughafilika na kupinga, kwa hivyo zikafungika kwa hivyo, heri haiwezi kuingia humo kabisa? Hii ndiyo hali halisi."},{"id":5604,"sura":47,"from_aya":25,"to_aya":28,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"25. Kwa hakika wale wanaorudi nyuma baada ya uwongofu kwisha wabainikia, Shetani huyo amewashawishi na amewaghuri. 26. Hayo ni kwa sababu waliwaambia wale waliochukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu: 'Tutakutiini katika baadhi ya mambo.' Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao. 27. Basi itakuwaje Malaika watakapowafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao! 28. Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yale yaliyomchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayomridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao. "},{"id":5605,"sura":47,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaeleza kuhusu hali ya wale walioritadi wakaacha uwongofu na imani na wakageuka kwenye visigino vyao wakaenda katika upotofu na ukafiri, si kwa sababu ushahidi uliowaelekeza kufanya hivyo wala hoja. Lakini ilikuwa tu kushawishiwa na adui wao, Shetani ambaye aliwapambia na akawatia matarajio marefu. \"Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shetani hawaahidi ila udanganyifu.\""},{"id":5606,"sura":47,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} Na \"hayo ni kwa sababu\" ya kuwa uwongofu ulikwisha wabainikia, lakini wakakata tamaa nao na wakaukataa. \"Wakawaambia wale waliochukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu\" miongoni mwa wale wanaosimama kidete katika kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Mtume wake, \"Tutakutiini katika baadhi ya mambo.\" Yaani, yale yatakayoafikiana na matamanio yao, basi ndiyo sababu Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa upotofu na kudumu katika yale yatakayowafikisha kwenye mashaka ya milele na adhabu ya kudumu milele, \"na Mwenyezi Mungu anajua siri zao.\" Kwa hivyo akawafedhehesha kwa hizo, na akawazibainisha kwa waja wake Waumini; wasije wasidanganyike nazo."},{"id":5607,"sura":47,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} \"Basi itakuwaje\" hali yao mbaya zaidi na mwonekano wao wa kutisha mno \"Malaika watakapowafisha,\" kwa kuchukua roho zao \"wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao\" kwa marungu makali mno!"},{"id":5608,"sura":47,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} \"Hiyo\" adhabu waliyostahiki na wakaipata ni kwa sababu \"wao waliyafuata yale yaliyomchukiza Mwenyezi Mungu\" miongoni mwa kila ukafiri, kutoka katika mipaka ya Mwenyezi mungu na uasi. \"Na wakachukia yanayomridhisha\" wakakosa kabisa kutaka yale yenye kuwaweka karibu naye; \"basi akaviangusha vitendo vyao.\" Na hili ni tofauti na yule anayefuata yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu na akachukia yanayomkasirisha. Huyu Mwenyezi Mungu atamfutia madhambi yake na amzidishie maradufu malipo yake mazuri."},{"id":5609,"sura":47,"from_aya":29,"to_aya":31,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"29. Je, wenye maradhi nyoyoni mwao wanadhani kwamba Mwenyezi Mungu hatazidhihirisha chuki zao? 30. Na tungelipenda, tungelikuonyesha hao na ungeliwatambua kwa alama zao. Lakini bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu. 31. Na bila ya shaka tutawajaribu mpaka tuwajue wapignao Jihadi katika nyinyi na wanaosubiri. Nasi tutazifanyia mtihani habari zenu. "},{"id":5610,"sura":47,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Je, wenye maradhi nyoyoni mwao wanadhani\" maradhi ya kuwa na shaka au matamanio ya nafsi, kwamba Mwenyezi Mungu hatatoa nje kinyongo na uadui ulio katika nyoyo zao dhidi ya Uislamu na watu wake! Hii ni dhana ambayo haifailii hekima ya Mwenyezi Mungu. Ni lazima kupambanua mkweli na mwongo, na hilo ni kwa kupima kupeana mtihani kwa misukosuko ambayo mwenye kubakia imara ndani yake na imani yake ikadumu humo, basi yeye ndiye Muumini wa kweli. Na mwenye kurudishwa nyuma nayo kwa visigino vyake, akawa hana subira juu yake, na pindi mtihani ulipomjia, alipapatika na imani yake ikadhoofika, na kinyongo kilichokuwa moyoni mwake na unafiki wake ukatoka nje na ukabainika wazi. Hivi ndivyo inavyohitajika katika hekima ya kimungu."},{"id":5611,"sura":47,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Ijapokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: \"Na tungelipenda, tungelikuonyesha hao na ungeliwatambua kwa alama zao\"  zilizo kama michoro kwenye nyuso zao. \"Lakini bila ya shaka, utawajua kwa namna ya msemo wao.\" Kwani ndimi ndizo zenye kudhihirisha uzuri na uovu ulio katika nyoyo. \"Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu\" na atawalipa kwa hivyo."},{"id":5612,"sura":47,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} Kisha akataja mtihani mkubwa zaidi anaowajaribu kwa huo waja wake, ambao ni kipigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, akasema: \"Na bila ya shaka, tutawajaribu\" imani yenu na subira yenu \"mpaka tuwajue wapiganao Jihadi katika nyinyi na wanaosubiri. Nasi tutazifanyia mtihani habari zenu.\" Basi anayetekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na akapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kunusuru Dini yake na kunyanyua neno lake, basi huyo ndiye Muumini wa kweli. Na mwenye kujitia uvivu katika hilo, huo utakuwa ni upungufu katika imani yake."},{"id":5613,"sura":47,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"32. Kwa hakika wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakapinzana na Mtume baada ya uwongofu kwishawabainikia, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao."},{"id":5614,"sura":47,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} Hili ni ahadi ya adhabu kali kwa wanaojumuisha kila aina ya uovu, kama vile kumkufuru Mwenyezi Mungu na kuwazuilia viumbe njia ya Mwenyezi Mungu aliyoiweka iwe ni ya kuwafikisha kwake, \"na wakapinzana na Mtume baada ya uwongofu kwisha wabainikia\" kwa makusudi na kwa ukaidi, si kwa kutojua, na upotofu. Basi \"hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote\" na wala ufalme wake hautapungua kwa hayo. \"Naye ataviangusha vitendo vyao\" walivyovifanyia juhudi katika kubwa katika kuunga mkono batili, kwa namna kwamba havitawazalia chochote isipokuwa kuambulia patupu na kupata hasara, na tena matendo yao wanayoyatarajia hayatakubaliwa; kwa sababu hawakutekeleza sharti lake."},{"id":5615,"sura":47,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"33. Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume, wala msiviharibu vitendo vyenu."},{"id":5616,"sura":47,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha Waumini kutekeleza amri ambayo kwayo [mambo yao] yatakamilika na watapata furaha yao ya kidini na ya kidunia, ambayo ni kumtii Yeye na kumtii Mtume wake katika misingi ya dini na matawi yake. Na utiifu ni kutekeleza amri na kujiepusha na makatazo kwa namna ilivyoamrishwa kwa kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake na kumfuta Mtume kikamilifu. Na kauli yake: \"Wala msiharibu vitendo vyenu\" inajumuisha kuviharibu baada ya kuvifanya; kwa kufanya jambo linaloviharibu, kama vile kujisifia, kujivuna, kujigamba, na kutafuta sifa, na kutenda maasi ambayo yanapunguza matendo na kuharibu thawabu zake. Na inajumuisha kukataza kuviharibu vinapokuwa bado vinafanywa kwa kuvikatisha au kufanya chochote cha kuviharibu. Kwa hivyo, yenye kubatilisha Swala, Saumu, Hija, na mengineyo yote yanaingia katika hili na yamekatazwa. Manazuoni wa elimu ya Fiqh wanaitumia Aya hii kuwa ni ushahidi wa kuharamisha kukatisha Swala za faradhi, na kuchukia kukatisha Swala za hiyari bila ya kuwepo jambo la kuruhusu kufanya hivyo. Ikiwa Mwenyezi Mungu alikataza kubatilisha matendo, basi hiyo ni amri ya kuyafanya kuwa mazuri, makamilifu, na kuyatekeleza kwa namna ambayo ni sahihi kwa elimu na vitendo."},{"id":5617,"sura":47,"from_aya":34,"to_aya":35,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"34. Hakika wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao. 35. Basi msilegee na mkataka suluhu, maana nyinyi ndio mtakaoshinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatawanyima malipo ya vitendo vyenu. "},{"id":5618,"sura":47,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} Aya hii, na ile iliyo katika Surat Al-Baqarah, kauli: \"Na yeyote katika nyinyi akiacha Dini yake akafa naye ni kafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika duniani na Akhera\" zinafungia kila aya ambayo haikufungiwa ambayo ndani yake kuna kuharibu matendo kwa ukafiri, hizo zimefungiwa kwa sharti kwamba afe katika hali hiyo. Na akasema hapa: \"Hakika wale waliokufuru\" Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, \"na wakazuilia\" viumbe \"njia ya Mwenyezi Mungu\" kwa kuwavunja moyo wa kukubali haki na kuwalingania kwenye batili na kuwapambia batili hiyo \"kisha wakafa na hali ya kuwa makafiri\" bila ya kutubu wakaacha ukafiri huo, \"basi Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao\" si kwa uwombezi wala kwa njia nyingine yoyote; kwa sababu imeshahakikika kwamba wataadhibiwa, wakakosa malipo mzuri, ikawa ni lazima watakaa milele katika Jahanamu, na wakafungiwa rehema ya Mwingi wa rehema, Mwingi wa kusamehe. Maana isiyokuwa ya moja kwa moja Aya hii tukufu ni kwamba wakitubia hayo kabla ya kufa kwao, basi Mwenyezi Mungu atawasamehe, na atawarehemu, na atawaingiza katika Bustani za mbinguni, hata kama walimalizia maisha yao katika kumkufuru, na kuzuilia njia yake na kumuasi. Basi ametakasika Yule aliyewafungulia waja wake milango ya rehema na wala hakumfungia yeyote maadamu bado yu hai na anaweza kutubia. Na ametakasika, Mstahamilivu, ambaye hawaharakishii adhabu wale wanaofanya maasi, bali huwaacha salama na kuwaruzuku kana kwamba hawakumuasi, licha ya uwezo wake mkubwa juu yao."},{"id":5619,"sura":47,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: \"Basi msilegee\" mkaacha kupigana vita na adui zenu, mkashindwa na hofu. Bali subirini, kuweni imara, na zizoesheni nafsi zenu kupigana vita na kukakamia hilo kwa kutafuta radhi za Mola wako Mlezi na kuwa kuwa mwaminifu kwa Uislamu na kumkasirisha Shetani. \"Na mkataka suluhu\" kati yenu na adui zenu kwa kutaka kupumzika tu. Na hali ni kwamba \"nyinyi ndio mtakaoshinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatawanyima malipo ya vitendo vyenu.\" Basi mambo haya matatu, kila kimojawapo kinahitaji subira na kutokadhoofika, na kwamba wao ndio wa juu kabisa; Yaani, tayari wanavyo visababu vya ushindi na waliahidiwa ahadi ya kweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwani mtu hadhoofiki isipokuwa ikiwa ni dhalili zaidi kuliko wengineo na dhaifu zaidi kwa idadi au maandalizi, nguvu, ndani na nje. Ya pili ni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja nao. Kwani wao ni Waumini, na Mwenyezi Mungu yu pamoja na Waumini kwa msaada wake, nusura yake na kuwaunga mkono, na hayo yanalazimu wawe na nyoyo imara na kuwa na ujasiri wa kukabiliana na adui yao. La tatu ni kwamba Mwenyezi Mungu hatawapunguzia chochote katika vitendo vyao, bali atawapa ujira wao kikamilifu na kuwazidishia katika fadhila zake, hasa juu ya ibada ya jihadi. Kwani kutoa matumizi kwa sababu yake kunazidishwa mizidisho mara mia saba hadi mizidisho nyingi sana, na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: \"Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa, kwa ajili ya Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaendi mahali panapowaghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kwa sababu ya hayo kuwa ni kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya mema. Wala hawatoi cha kutoa kidogo wala kikubwa, wala hawalivuki bonde, ila huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu awalipe bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.\" Basi mja anapojua kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi matendo na juhudi zake, hilo linamfanya kuwa mkakamavu na kufanya juhudi katika yale ambayo yatamletea malipo mazuri. Kwa hivyo itakuwaje ikiwa vitu hivi vitatu vitakutana? Hayo yanamsababishia kuwa mkakamavu kikamilifu. Kwa hivyo haya ni katika mbinu ambayo Mwenyezi Mungu humtia moyo, na kuwakakamua, na kuzipa nguvu nafsi zao juu ya yale yenye kuwafanya watengenee na kuwafanya wafaulu."},{"id":5620,"sura":47,"from_aya":36,"to_aya":38,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"36. Hakika uhai wa duniani ni mchezo na pumbao. Na mkiamini na mkamcha Mungu, Mwenyezi Mungu atakupeni ujira wenu, wala hatakutakeni mali zenu. 37. Na akikutakeni hizo na kukushikilieni, mtafanya ubahili, na atatoa undani wa chuki zenu. 38. Angalieni! Nyinyi hawa mnaitwa mtumie mali katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanaofanya ubahili. Na anayefanya ubahili, basi anajifanyia ubahili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka, atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi. "},{"id":5621,"sura":47,"from_aya":36,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36 - 37} Huku ni Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwavunja moyo waja juu ya maisha ya dunia; kwa kuwaambia ukweli kuhusu jambo lake. Kwamba ni mchezo na pumbao. Ni mcheza katika miili na pumbao nyoyoni. Hivyo basi, mja hataacha kuendelea kufanya pumbao katika mali yake, watoto wake, mapambo yake, na starehe zake kama vile wanawake, vyakula, vinywaji, makazi, vikao, mandhari na uongozi, na akaendelea kucheza katika kila matendo yasiyo na faida yoyote. Bali, anazunguka tu kati ya kutofanya chochote, kughafilika, na kufanya maasia, mpaka anapomaliza maisha yake ya kidunia na wakati wake ukamjia; na tazama, mambo hayo yatampa mgongo, na kumuacha, na wala mja hakupata manufaa yoyote kutokana nayo. Bali hasara yake na kunyimwa kwake kukamdhihirikia, na adhabu yake ikamjia. Haya yanamfanya mwenye akili kukata tamaa nayo na kutoyataka na kutoyajali kabisa. Badala yake, anachopaswa kujishughulisha nayo ni yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika kauli yake: \"Na mkiamini na mkamcha Mungu\" na kuamini Malaika wake, Vitabu vyake, Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na kufanya yanayompendeza Yeye daima, pamoja na kuacha kumuasi. Basi hayo ndiyo yanayomnufaisha mja, na ndilo ambalo mtu anapaswa kushindana ndani yake na kujitahidi na kufanya juhudi kubwa katika kuyatafuta, na hayo ndiyo malengo ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake; kwa kuwafanyia rehema na wema; ili awalipe malipo mazuri mengi, na ndiyo maana akasema: \"Na mkiamini na mkamcha Mungu, Mwenyezi Mungu atakupeni ujira wenu, wala hatakutakeni mali zenu.\" Yaani, Mwenyezi Mungu hataki kuwajukumisha yale yatakayowalemea na kuwadhuru kwa kuchukua mali zenu na kuwaacha bila mali au kuwapunguzia mali hizo kiasi kwamba mtadhurika. Ndiyo maana akasema: \"Na akikutakeni hizo na kukushikilieni, mtafanya ubahili, na atatoa undani wa chuki zenu\" mtakapoombwa kitu ambacho mnachukia kukitoa."},{"id":5622,"sura":47,"from_aya":38,"to_aya":38,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38} Ushahidi wa kwamba Mwenyezi Mungu akikutakeni mali zenu na akakushikilieni katika kuziomba kwamba mtazizuia, ni kwamba, nyinyi \"mnaitwa mtumie mali katika njia ya Mwenyezi Mungu\" kwa njia hii yenye masilahi yenu ya kidini na ya kidunia, \"na wapo katika nyinyi wanaofanya ubahili.\" Basi je, ingekuwaje kama angewaomba mali zenu kwa kitu ambacho hamuoni ndani yake masilahi yenu ya sasa? Je, haitakuwa ni karibu zaidi kwamba mngekataa kufanya hivyo? Kisha akasema: \"Na anayefanya ubahili, basi anajifanyia ubahili mwenyewe.\" Kwa sababu amejizuilia ujira wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akakosa heri nyingi, na wala hatamdhuru Mwenyezi Mungu chochote kwa kuacha kutoa mali yake. Kwani \"Mwenyezi Mungu\" ndiye \"Asiye mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji\" mnaomhitajia katika wakati wenu wote katika mambo yenu yote. \"Na mkigeuka\" mkaacha kumuamini Mwenyezi Mungu na kutekeleza yale anayowaamrisha ''atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi\" katika kupeana migongo. Bali watakuwa wakimtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: \"Enyi mlioamini! Atakayeiacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anaowapenda nao wanampenda.\""},{"id":5623,"sura":47,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Qital, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu,  Mola Mlezi wa viumbe wote."},{"id":5624,"sura":47,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}