{"result":[{"id":6116,"sura":57,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Surat Al-Hadid"},{"id":6117,"sura":57,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Madina"},{"id":6118,"sura":57,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":6119,"sura":57,"from_aya":1,"to_aya":6,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Kinamsabihi kumtakasa Mwenyezi Mungu kila kilichomo ndani ya mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 2. Yeye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha. Na Yeye ni Mwenye uwezo mno wa kila kitu. 3. Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhahiri na wa Siri, naye ndiye ajuaye zaidi kila kitu. 4.  Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha akainuka juu ya Kitu cha enzi. Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda humo. Naye yu pamoja nanyi popote mlipo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mno mnayoyatenda. 5. Ufalme wa mbingu na ardhi ni wake. Na mambo yote yanarejeshwa kwa Mwenyezi Mungu. 6. Anaingiza usiku katika mchana, na anaingiza mchana katika usiku. Na Yeye ni Mwenye kuyajua mno yaliyomo vifuani. "},{"id":6120,"sura":57,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukuu wake, utukufu wake, na upana wa mamlaka yake, kwamba kila \"kilichomo ndani ya mbingu na ardhi\" miongoni mwa wanyama wanaozungumza [na wasiozungumza] na vitu vinginevyo visivyo na uhai vinamtakasa kwa sifa njema za Mola wao Mlezi na vinamuweka mbali na yote yasiyoufailia utukufu wake, na kwamba vyote vinaunyenyekea Mola wao Mlezi na kutii nguvu zake, na zimedhihiri ndani yao athari za hekima yake. Na ndiyo maana akasema: \"Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.\" Haya yanabainisha ujumla wa viumbe vya juu na vya chini kuhitajia zaidi, Mola wao Mlezi katika hali zao zote, na ujumla wa utukufu wake, ushindi wake juu ya kila kitu, na ujumla wa hekima yake katika uumbaji na amri yake."},{"id":6121,"sura":57,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Kisha akajulisha juu ya ujumla wa ufalme wake, akasema: \"Yeye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha.\" Yaani, Yeye ndiye Muumba wa hayo, Mwenye kuruzuku, Mwenye kuyaendesha kwa uwezo wake, \"Na Yeye ni Mwenye uwezo mno wa kila kitu.\""},{"id":6122,"sura":57,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} \"Yeye ndiye wa Mwanzo\" ambaye hakuna kitu mbele yake. \"Na ndiye wa Mwisho\" ambaye hakuna kitu baada yake. \"Naye ndiye wa Dhahiri\" ambaye juu yake hakuna kitu. \"Na wa Siri\" ambaye hakuna chini yake. \"Naye ndiye ajuaye zaidi kila kitu.\" Elimu yake imezunguka mambo ya dhahiri na ya nje, siri na mambo yaliyofichikana zaidi, yaliyotangulia na ya baadaye."},{"id":6123,"sura":57,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} \"Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita.\" Ya kwanza yake ni Jumapili na ya mwisho yake ni Ijumaa \"kisha akainuka juu ya Kitu cha enzi\" kuinuka kunakolingana na utukufu wake juu viumbe vyake vyote. \"Anayajua yanayoingia katika ardhi\" kama vile nafaka, wanyama, mvua na mengineyo. \"Na yanayopanda kutoka humo\" kama vile mimea, miti, wanyama na mengineyo \"na yanayoteremka kutoka mbinguni\" kama vile Malaika, mipango yake na riziki. \"Na yanayopanda humo\" kama vile Malaika, roho, na dua, matendo na vitu vinginevyo. \"na Yeye yu pamoja nanyi popote mlipo.\" Kama vile kauli yake: \"Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wanne wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo.\" Na upamoja wake huu ni kwa elimu yake na kuona kwake. Ndiyo maana akatishia kwa adhabu na akaahidi ahadi ya kulipa kulingana na matendo, kwa kauli yake: \"Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mno mnayoyatenda.\" Yaani, Yeye Mtukufu anayaona mno matendo mnayoyafanya na yaliyoyasababisha; ya wema na maovu, kisha atakulipeni kwa hayo na amekulindieni."},{"id":6124,"sura":57,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} \"Ufalme wa mbingu na ardhi ni wake;\" ufalme, uumbaji na waja. Yeye huviendesha anavyotaka kwa amri zake alizozipanga awali, na amri zake za kisheria zinazokwenda kwa hekima ya kimungu. \"Na mambo yote yanarejeshwa kwa Mwenyezi Mungu.\" Kisha waja watawasilishwa kwake, naye atampambanua muovu mbali na mwema, na amlipe mwema wema wake, na mbaya kwa ubaya wake."},{"id":6125,"sura":57,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} \"Anaingiza usiku katika mchana, na anaingiza mchana katika usiku.\" Yaani, usiku unaingia katika mchana, kisha unawafunika kwa giza lake, kwa hivyo wanatulia tuli. Kisha mchana unaingilia usiku, na giza lililoko kwenye ardhi linatoweka, na ulimwengu unaangazwa kwa hivyo waja wanatembea huku na kule, wakienda katika masilahi yao na mambo ya maisha yao. Na Mwenyezi Mungu anaendelea kuufunika usiku juu ya mchana, na kuufunika mchana juu ya usiku, na anavizungusha kwa kuongezeka na kupungua, kwa urefu na ufupi, mpaka misimu ipatikane kwa hayo na nyakati zinyooke sawa, ndiyo yapatikane masilahi mbalimbali kwa hayo. Basi ametakasika Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na ametukuka Mwenye ukarimu, Mwenye kutoa kwa wingi, ambaye amewaneemesha waja wake kwa neema za dhahiri na zilizofichika. \"Na Yeye ni Mwenye kuyajua mno yaliyomo vifuani\" mwa walimwengu. Kwa hivyo, anamuwezesha anayejua kwamba anafailia hilo, na anamfelisha anayejua kwamba hafailii kuongolewa."},{"id":6126,"sura":57,"from_aya":7,"to_aya":11,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"7. Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na toeni katika alivyokufanyeni nyinyi kuwa ni waangalizi wake. Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, wana malipo makubwa. 8. Na mna nini hata hamumuamini Mwenyezi Mungu na hali Mtume anakuiteni mumuamini Mola wenu Mlezi? Naye amekwisha chukua ahadi yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. 9. Yeye ndiye anayemteremshia mja wake Aya zinazobainisha wazi ili akutoeni gizani hadi kwenye nuru. Na hakika Mwenyezi Mungu kwenu ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu. 10. Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa miongoni waliotoa kabla ya Ushindi na wakapigana vita. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao walitoa baadaye na wakapigana. Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda. 11. Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, ili amrudishie maradufu, na apate malipo ya ukarimu. "},{"id":6127,"sura":57,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Mwenyezi Mungu anawaamrisha waja wake kumwamini Yeye na Mtume wake na aliyoyaleta, na watoe mali kwa ajili ya njia Yake kutokana na mali ambazo Mwenyezi Mungu ameweka mikononi mwao na akawafanya kuwa wasimamizi juu wake. Ili aone jinsi wanavyofanya matendo. Kisha alipowaamuru kufanya hivyo, akawatia moyo na akawahimiza kufanya hivyo kwa kutaja malipo aliyowapangia, juu yake, akasema: \"Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, wana malipo makubwa.\" Yaani, wale waliojumuisha kati ya kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kutoa mali kwa ajili ya njia yake kwamba watapata malipo makubwa, matukufu ambayo ni kuridhiwa na Mola wao Mlezi na kupata nyumba ya utukufu wake na neema ya milele aliyowaandalia Mwenyezi Mungu Waumini na Mujahidina (wanaopambana kwa ajili yake)."},{"id":6128,"sura":57,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} Kisha akataja sababu itakayowafanya kuamini na kutokuwepo kizuizi cha hilo, akasema: \"Na mna nini hata hamumuamini Mwenyezi Mungu na hali Mtume anakuiteni mumuamini Mola wenu Mlezi? Naye amekwisha chukua ahadi yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini.\" Yaani, ni nini kinakuzuieni kuamini, na hali Mtume Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mbora wa Mitume na mlinganiaji mtukufu zaidi kwa Mwenyezi Mungu anakuiteni? Hili ni katika mambo yanayosababisha kuchukua hatua ya kuitikia wito wake na kuitikia haki aliyokuja nayo, na amechukua ahadi juu yenu na agano madhubuti kwamba mtaamini ikiwa nyinyi ni Waumini."},{"id":6129,"sura":57,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} Pamoja na wema wake huu na kujali kwake, hakutosheka kwa ulinganiaji wa Mtume tu, ambaye ndiye mtukufu zaidi wa walimwengu wote. Bali alimsaidia kwa miujiza na akakuonyesheni ukweli wa yale aliyokuja nayo kwa ishara zilizo wazi. Ndiyo maana akasema: \"Yeye ndiye anayemteremshia mja wake Aya zinazobainisha wazi\" zinazowaonyesha wale wenye wenye akili kwamba kila alichokileta ni sahihi, na kwamba ndiyo haki ya yakini. \"Akutoeni\" kwa kukutumieni Mtume na yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa mkono wake kama vile Kitabu na hekima \"kutoka gizani kuingia kwenye nuru.\" Yaani, kutoka kwenye viza vya ujinga na ukafiri hadi kwenye nuru ya elimu na imani. Haya ni katika rehema na upole wake juu yenu. Ambapo aliwarehemu zaidi waja wake hata kuliko mama kwa mwanawe, \"Na hakika Mwenyezi Mungu kwenu ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu.\""},{"id":6130,"sura":57,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} \"Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu?\" Yaani, ni nini kinachokuzuieni kutumia mali zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu? Nao ni njia za wema zote, na kinawafanya kuwa mabahili. \"Na\" hali ni kwamba hamna chochote, bali \"urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu.\" Kwani mali zote zitatoka katika mikono yenu au nyinyi wenyewe mtaziacha, kisha umiliki wake utamrudia mmiliki wake hasa, Mwenye baraka nyingi, Mtukufu. Kwa hivyo, tumieni fursa kutoa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu madamu bado mna mali mikononi mwenu Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja maelezo ya kina ya matendo kulingana na hali na hekima ya kimwenyezi Mungu, akasema: \"Hawawi sawa miongoni waliotoa kabla ya Ushindi na wakapigana vita. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao walitoa baadaye na wakapigana.\" Kinachokusudiwa hapa na ushindi ni ule ushindi wa Al-Hudaybiyya, yalipofanyika mapatano ya amani baina ya Mtume na Makureshi, ambao ulikuwa katika ushindi mkubwa zaidi kuliko ambao ndani yake ulienea Uislamu, kuchanganyika Waislamu na makafiri, na kuilingania dini bila upinzani. Basi tangia wakati huo watu wakaingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi, na Uislamu ukapata nguvu kubwa sana, na kabla ya ushindi huu, Waislamu hawakuwa na uwezo wa kuilingania dini katika sehemu nyinginezo isipokuwa katika maeneo ambayo watu wake walikuwa wamesilimu kama vile Madina na viunga vyake. Na watu waliosilimu wa Makka na maeneo mengineyo ya washirikina walikuwa wakiadhibiwa na kuogopa. Kwa hivyo akawa aliyesilimu kabla ya ushindi [na akatoa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu] na akapigana vita ni mwenye daraja kubwa zaidi na malipo kuliko yule ambaye hakuwa amesilimu, kupigana vita na kutoa mali isipokuwa baada ya hayo, kama inavyotakiwa na hekima, na ndiyo kwa sababu wengi wa waliotangulia na masahaba bora zaidi walisilimu kabla ya ushindi huu. Na kwa kuwa kuboresha kati ya mambo kunaweza kusababisha ifahamike kwamba kuna upungufu na dosari katika kile ambacho hakikuboreshwa, Mwenyezi Mungu akaondoa hili kwa kauli yake: \"Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema.\" Yaani, wale waliosilimu, wakapigana, na wakatoa mali zao kabla ushindi, na baada yake, wote Mwenyezi Mungu aliwaahidi bustani za mbinguni. Hii inaashiria fadhila za Maswahaba wote, Mungu awe radhi nao, kwani Mwenyezi Mungu alishuhudia imani yao na kuwaahidi Pepo. \"Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda.\" Atamlipa kila mmoja wenu kwa anayoyajua katika matendo yake."},{"id":6131,"sura":57,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} Kisha akawahimiza watu watoe na wapeane katika njia yake; Kwa sababu jihadi inategemea kutoa mali kwa ajili ya kuitayarisha. Basi akasema: \"Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema?\" Ambao huwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu na wenye kuafikiana na radhi za Mwenyezi Mungu, kutokana na mali halali, nzuri na aliyotoa kwa moyo safi. Hili ni katika ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu; ambapo uliuita mkopo, ilhali mali hiyo ni yake, na waja pia ni waja wake, na akaahidi kuizidisha mali hiyo mizidisho mingi naye ndiye Mkarimu, Mpaji. Na mzidisho huo, mahali pake na siku yake ni siku ya Kiyama. Siku ambayo kila mtu atabainika uhitaji wake, na atahitaji malipo mazuri hata kidogo tu. Na ndiyo maana akasema:"},{"id":6132,"sura":57,"from_aya":12,"to_aya":15,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"12. Siku utakapowaona Waumini wanaume na Waumini wanawake, nuru yao iko mbele yao, na kuliani kwao: Furaha yenu leo - Bustani zipitazo mito kati yake, mtakaa humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 13. Siku wanafiki wanaume na wanafiki wanawake watakapowaambia wale walioamini: 'Tungojeni ili tupate mwangaza katika nuru yenu.' Waambiwe: 'Rejeeni nyuma yenu mkaitafute nuru!' Kisha itatiwa baina yao ukuta wenye mlango - ndani yake mna rehema, na nje upande wake wa mbele kuna adhabu. 14. Watawaita wawaambie: 'Kwani hatukuwa pamoja nanyi?' Watawaambia: 'Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkatazamia mabaya (Waumini), na mkatia shaka, na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni mpaka ilipokuja amri ya Mwenyezi Mungu, na mdanganyifu yule akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu. 15. Basi leo haitachukuliwa kwenu fidia, wala kwa wale waliokufuru. Makazi yenu ni Motoni, ndio bora kwenu; na ni marejeo maovu yalioje! "},{"id":6133,"sura":57,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akieleza fadhila ya Imani na kufurahi kukubwa kwa wana imani Siku ya Kiyama: \"Siku utakapowaona Waumini wanaume na Waumini wanawake, nuru yao iko mbele yao, na kuliani kwao.\" Yaani, ikifika Siku ya Kiyama, na jua likakunjwa na mwezi ukapatwa, na watu wakawa gizani, na ikawekwa Sirat (njia iliyoko) kwenye mgongo wa Jahannamu; basi hapo utawaona Waumini wanaume na Waumini wanawake wana nuru yao mbele yao na kuliani kwao, kisha watatembea kwa nuru yao katika hali hiyo inayotisha sana na ngumu, kila mmoja kulingana na imani yake, na hapo watapewa bishara njema iliyo kubwa zaidi, wakiambiwa: \"Furaha yenu leo - Bustani zipitazo mito kati yake, mtakaa humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.\" Ee Mwenyezi Mungu, ni bishara njema iliyo nzuri namna gani hii kwenye nyoyo zao, na yenye ladha zaidi kwenye nafsi zao, ambapo walipata kila wanachotafuta, wanachokipenda, na wakaokoka kutokana na kila uovu na kinachohofiwa."},{"id":6134,"sura":57,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Basi wanaafiki watakapowaona Waumini wanatembea katika nuru yao, ilhali nuru yao imezimwa, na wakabaki gizani wamechanganyikiwa, watawaambia Waumini: \"Tungojeni ili tupate mwangaza katika nuru yenu.\" Yaani, tungojeni tupate kuweze kutoka katika nuru yenu kitu tutakachoweza kutembea kwacho ili tuepuke na adhabu, basi wataambiwa: \"Rejeeni nyuma yenu mkaitafute nuru.\" Yaani, ikiwa hilo linawezekana, na hali ni kwamba hilo haliwezekani, bali ni miongoni mwa yasiyowezekana kamwe. Basi \"ukuta\" wenye kuzuia ulio imara utawekwa baina ya Waumini na wanafiki hao \"wenye mlango - ndani yake mna rehema,\" na huo ni upande wake ulio karibu na Waumini; \"na nje upande wake wa mbele kuna adhabu.\" Nao ni upande wake ulio karibu na wanafiki."},{"id":6135,"sura":57,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} Kisha wanafiki watawaita Waumini, na waseme wakiomba kwa njia ya kusihi na kwa huruma kubwa: \"Kwani hatukuwa pamoja nanyi\" katika dunia, tukisema: Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, tukiswali, tukifunga, tukifanya jihadi, na kukifanya matendo kama yenu? \"Watawaambia: Ndiyo,\" mlikuwa pamoja nasi katika dunia na mkatenda matendo kama sisi kwa dhahiri, lakini matendo yenu yalikuwa matendo ya wanafiki wasio na imani wala nia ya ukweli iliyo nzuri. \"Lakini mlijifitini wenyewe, na mkatazamia mabaya (Waumini), na mkatia shaka\" katika habari za Mwenyezi Mungu zisizo na shaka yoyote; \"na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni.\" Ambapo mlikuwa mkitamani kupata yale watakayopata Waumini, na mkawa hata hamna yakini \"mpaka ilipokuja amri ya Mwenyezi Mungu\" ambayo ni mauti nanyi mko katika hali hiyo ya kukashifiwa; \"na mdanganyifu yule akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu.\" Yaani, Shetani ndiye aliyekupambieni ukafiri na shaka, kwa hivyo mkatulia juu yake, na mkawa na imani na ahadi yake na mkasadiki habari zake."},{"id":6136,"sura":57,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15} \"Basi leo haitachukuliwa kwenu fidia, wala kwa wale waliokufuru.\" Na mkijikomboa kwa dhahabu ya ujazo wa ardhi na mfano wake pamoja nayo, hilo halingekubaliwa kutoka kwenu. \"Makazi yenu ni Motoni ndio bora kwenu na ni marejeo maovu yalioje!\" Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na yule ambaye mizani yake (ya mema) itakuwa hafifu. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! Na nini kitakachokujuilisha nini hiyo? Ni Moto mkali!\""},{"id":6137,"sura":57,"from_aya":16,"to_aya":17,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"16. Je, wakati haujafika bado kwa wale walioamini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyoteremka? Wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao ni  wapotovu. 17. Jueni kwamba Mwenyezi Mungu huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika tumekubainishieni Ishara ili mpate kuzingatia. "},{"id":6138,"sura":57,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} Alipotaja hali ya Waumini wanaume na Waumini wanawake na wanafiki wanaume na wanafiki wanawake katika Akhera, hayo yakawa katika yale yanayoziitia nyoyo kumnyenyekea Mola wao Mlezi na kuunyenyekea ukuu wake, basi Mwenyezi Mungu akawakemea Waumini kwa kutofanya hivyo, akasema: \"Je, wakati haujafika bado kwa wale walioamini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyoteremka?\" Yaani, je, haujafika wakati ambao nyoyo zanafaa kulainika na kuunyenyekea ukumbusho wa Mwenyezi Mungu, nayo ni Qur-ani, na kufuata amri zake na makemeo yake na haki iliyoteremka, ambayo alikuja nayo Muhammad \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Hili ndani yake limo kuwahimiza Waumini kujitahidi kunyenyekea kwa nyoyo zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyoyataremsha ya Kitabu na hekima, na kwamba Muumini akumbuke mawaidha ya kimungu na hukumu za kisheria kila wakati, na wajifanyie hesabu juu yake. \u201cWala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu.\" Yaani, wasiwe kama wale ambao Mwenyezi Mungu aliwateremshia Kitabu kinachohitaji unyenyekevu wa moyo na utiifu kamili, kisha hawakudumu juu yake, wala hawakukaa imara juu yake. Bali muda uliwawia mrefu, wakaendelea kughafilika, na imani yao ikafifia, na yakini yao ikaisha. \"Kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao ni  wapotovu.\" Hayo ni kwa sababu, nyoyo zinahitaji kila wakati kukumbushwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kufanywa kutamka hekima yake, na wala mtu hafai kughafilika mbali na hayo. Kwani hiyo ni sababu ya ugumu wa moyo na ukavu wa jicho."},{"id":6139,"sura":57,"from_aya":17,"to_aya":17,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17} \"Jueni kwamba Mwenyezi Mungu huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika tumekubainishieni Ishara ili mpate kuzingatia.\" Kwa kuwa ishara zinaonyesha akili kufikia kwenye matakwa ya Mwenyezi Mungu, na ambaye ndiye aliyeihuisha ardhi baada ya kufa kwake ana uwezo wa kuwafufua wafu baada ya kufa kwao na kuwalipa kwa matendo yao. Na aliyeihuisha ardhi baada ya kufa kwake kwa maji ya mvua, anaweza kuzifufua nyoyo zilizokufa kwa yale aliyoyateremsha ya haki juu ya Mtume wake. Aya hii inaashiria kwamba hana akili yule ambaye haongokii na ishara (Aya) za Mwenyezi Mungu na hakufuata sheria za Mwenyezi Mungu."},{"id":6140,"sura":57,"from_aya":18,"to_aya":19,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"18. Kwa hakika wanaume wanaotoa sadaka, na wanawake wanaotoa sadaka, na wakamkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, watazidishiwa maradufu na watapata malipo ya ukarimu. 19. Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, hao ndio Masidiqi (wakweli zaidi) na Mashahidi mbele ya Mola wao Mlezi. Wao watapata malipo yao na nuru yao. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ndio wana Motoni. "},{"id":6141,"sura":57,"from_aya":18,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{18} \"Kwa hakika wanaume wanaotoa sadaka, na wanawake wanaotoa sadaka\" kwa wingi \"na wakamkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema\" kwa kutoa na kupeana mali zao katika njia za wema ambazo zitakakuwa akiba zao kwa Mola wao Mlezi, \"watazidishiwa maradufu\" jema moja kwa mara kumi mfano wake, hata mara mia saba, hadi mizidisho mingi, \"na watapata malipo ya ukarimu.\" Nayo ni yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia katika bustani za mbinguni miongoni mwa yale ambayo nafsi haziyajui."},{"id":6142,"sura":57,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} \"Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake\" Imani kwa Masunni ni yale yaliyoashiriwa na Kitabu na Sunna, nayo ni maneno ya moyo na ulimi, na matendo ya moyo, ulimi na viungo. Na hayo yanajumuisha sheria zote za Dini zilizo dhahiri na zilizofichikana, kwa hivyo waliounganisha [baina ya] mambo haya \"hao ndio Masidiqi (wakweli zaidi)\" ambao daraja yao iko juu ya daraja za Waumini wote wa kawaida, lakini chini ya daraja za Manabii. Na kauli yake: \"Na Mashahidi mbele ya Mola wao Mlezi. Wao watapata malipo yao na nuru yao.\" Kama ilivyokuja katika Hadithi sahihi: \u201cHakika kuna ngazi mia moja katika bustani za mbinguni, na umbali ulioko kati ya kila daraja mbili ni kama umbali uliopo kati ya mbingu na ardhi. Mwenyezi Mungu amewaandalia wanaofanya jihadi katika njia yake.\" Haya yanalazimu kwamba wako juu zaidi, na wametukuka zaidi na kwamba wako karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. \"Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ndio wana Motoni.\" Aya hizi zimejumuisha aina za viumbe wanaotoa sadaka, wakweli zaidi, wale waliokufa katika njia ya Mwenyezi Mungu (mashahidi), na watu wa Motoni. Wale watoao sadaka, ni wale ambao walikuwa wakitoa na kuwapa viumbe na pia wakiwafanyia yenye kuwanufaisha kiasi wawezavyo, hasa kuwanufaisha kwa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu. Nao wakweli ni wale waliokamilisha viwango vya imani, matendo mema, elimu yenye manufaa na yakini ya kweli. Nao mashahidi ni wale waliopigana katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kuinua juu neno la Mwenyezi Mungu, wakajitolea nafsi zao na mali zao na wakauawa. Nao watu wa Motoni ni makafiri waliozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu. Na limebakia kundi lingine ambalo Mwenyezi Mungu alilitaja katika Surat Fatir, ambao ni wale wa katikati, ambao walitekeleza mambo ya wajibu na wakaacha yale yaliyoharamishwa. Hata hivyo, hawakufanya sawasawa baadhi ya haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake. Hao pia marejeo yao yatakuwa katika bustani za mbinguni, hata kama baadhi yao wataadhibiwa kwa yale waliyoyafanya."},{"id":6143,"sura":57,"from_aya":20,"to_aya":21,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"20. Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifahirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu. 21. Kimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi, na Bustani ya mbinguni ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu. "},{"id":6144,"sura":57,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Mwenyezi Mungu anajulisha kuhusu uhalisi wa dunia na jinsi ulivyo, na anaelezea madhumuni yake na madhumuni ya wakazi wake, kwamba ni \"mchezo na pumbao.\" Miili huichezea na nyoyo hujifurahisha kwayo, na hili linathibitishwa na yaliyopo na ni ukweli wa wana dunia. Kwani, utawakuta wanapoteza muda wa maisha yao kwa kufanya pumbao za nyoyo zao na kughafilika mbali na suala la kumkumbuka Mwenyezi Mungu na yale yaliyo mbele yao ya ahadi nzuri na vitisho vya kuadhibiwa. Na utawaona wameifanya dini yao kuwa ni mchezo na pumbao. Tofauti na watu ambao wako macho, na wafanyao matendo sana kwa ajili ya akhera. Mioyo yao imejaa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kumjua vyema na upendo. Wameushughulisha wakati wao kwa matendo yanayowaleta karibu na Mwenyezi Mungu, yenye manufaa yanayowahusu wao tu na manufaa yanayowafikia wengine. Na kauli yake: \"Na pambo;\" yaani, kujipamba kwa mavazi, vyakula, vinywaji, vipando, nyumba, makasri na kutafuta heshima na mengineyo. \"Na kujifahirisha baina yenu\" kila mmoja akitaka kuwa mshindi katika mambo yake, na kwamba awe ndiye mwenye umashuhuri zaidi katika hali zake \"na kushindana kwa wingi wa mali na watoto.\" Na hili linathibitishwa na kutokea kwake katika wale wanaoipenda dunia na kuridhika nayo. Tofauti na yule aliyeijua dunia na uhakika wake, basi akaifanya kuwa ni njia tu ya kupitia, na hakuifanya kuwa ni mahali pa kukaa na kutulia, kwa hivyo akashindana katika yale yatakayomuweka karibu na Mwenyezi Mungu, na akachukua njia zitakazomfikisha kwenye makazi ya utukufu wake. Na akimuona mwenye kukithirisha mali na watoto na kushindana naye, yeye anashindana naye katika matendo mema. Kisha akaipigia dunia mfano wa mvua iliyoteremka juu ya ardhi, na ikachanganyika nayo mimea ya ardhi wanayokula kwayo watu na wanyama, mpaka ardhi ilipokamilika katika pambo lake, na mimea yake ikawafurahisha wakulima, ambao hawakuangalia wala hawakuwa na hima juu ya kitu kingine isipokuwa dunia, amri ya Mwenyezi Mungu ikaijia na kuiharibu. Kwa hivyo ikanyauka na kukauka, na kurudi katika hali yake ya mwanzo. Ni kana kwamba hakuna kijani kibichi kilichowahi kuota juu yake, na wala haikuwahi kuwa na mwonekano mzuri mno. Basi dunia pia iko hivyo. Wakati ilikuwa iking'aa kwa mwenye kuitafuta na ikawa na mwonekana mzuri; chochote alichotaka katika mambo yake yanayotakwa, anakipata. Na chochote alicholenga kufanya katika mambo yake anakuta milango yake imefunguliwa sawasawa. Lakini tazama, ikapatwa na yale aliyoipangia Mwenyezi Mungu, nayo yakaiondoa mikononi mwake, au yakamwondoa yeye akaiacha. Kwa hivyo, akaondoka humo mikono mitupu; hakuchukua humo chochote isipokuwa sanda tu. Basi ole wake mwenye kuifanya kuwa ndiyo lengo kubwa zaidi analilotamani, basi akaifanyia matendo na juhudi kubwa. Na ama kuifanyia akhera matendo, hilo ndilo lenye kunufaisha na kuhifadhiwa mwenye kuyafanya matendo hayo na yatafuatana na mja huyo milele, na ndiyo maana Mola Mtukufu akasema: \"Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi.\" Yaani, hali ya Akhera haitoki nje ya mambo mawili: Ima adhabu kali katika moto wa Jahannamu na pingu zake, minyororo yake na vitisho vyake vikubwa kwa yule ambaye dunia ilikuwa ndiyo lengo lake kuu. Kwa hivyo akathubutu kumuasi Mwenyezi Mungu, kukanusha ishara za Mwenyezi Mungu, na kukufuru neema za Mwenyezi Mungu. Au msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa maovu, kuondolewa kwa adhabu mbalimbali, kuridhiwa na Mwenyezi Mungu, na makazi ya kuridhiwa na kuridhia, kwa yule anayemruhusu, ambaye aliijua dunia na akaifanyia Akhera juhudi ipasavyo. Yote hayo ndiyo yanaitia mtu kuipa dunia mgongo na kuitaka sana Akhera, na ndiyo maana akasema: \"Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu.\" Hadanganyiki nayo isipokuwa watu wenye akili dhaifu tu, ambao yule mdanganyifu anawadanganya wamkatae Mwenyezi Mungu."},{"id":6145,"sura":57,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} Kisha akatuamrisha tushindanie msamaha wa Mwenyezi Mungu, radhi yake, na bustani zake za mbinguni, na hiyo yanakuwa kwa kujitahidi kutafuta visababu vya msamaha, kama vile toba ya kweli, kuomba msamaha kwenye manufaa, kujiweka mbali na madhambi na sehemu zake, kushindana kufikia radhi za Mwenyezi Mungu kwa kufanya matendo mema, na kufanyia bidii daima yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu kama vile kumuabudu Muumba kwa uzuri, na kuwafanyia ihsani viumbe katika nyanja mbalimbali za manufaa, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akataja matendo yanayosababisha hayo, akisema: \"Na Bustani ya mbinguni ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake.\" Kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake kunajumuisha misingi ya dini na matawi yake. \"Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye.\" Yaani, haya tuliyokubainishieni na tukataja njia zinazofikisha katika bustani ya mbinguni na njia zinazofikisha katika Moto, na kwamba malipo ya Mwenyezi Mungu ambayo ni mengi na mazuri ni miongoni mwa neema zake kubwa kwa waja wake na fadhila zake. \"Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu.\" Ambaye sifa zake hazihesabiki zikadhibitiwa. Bali Yeye ni kama alivyojisifu mwenyewe, na yuko juu zaidi ya namna ambayo yeyote anamsifu miongoni mwa viumbe vyake."},{"id":6146,"sura":57,"from_aya":22,"to_aya":24,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"22. Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. 23. Ili msihuzunike kwa kilichokupoteeni, wala msijitape kwa alichokupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna akajifahirisha. 24. Ambao wanafanya ubahili, na wanaamrisha watu wafanye ubahili. Na anayegeuka, basi Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa mno. "},{"id":6147,"sura":57,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akijulisha kuhusu ujumla wa mipango yake na kupitisha kwake mambo: \"Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu.\" Hili linajumuisha jumla ya misiba inayowasibu viumbe, ikiwa ni nzuri au mbaya. Yote imeandikwa katika Ubao uliohifadhiwa, kiwe kidogo au kikubwa, na hili ni jambo kubwa lisiloweza kufahamika kikamilifu katika akili za viumbe. Bali nyoyo za wenye akili hustaajabishwa mno nalo, lakini ni rahisi zaidi kwa Mwenyezi Mungu."},{"id":6148,"sura":57,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} Mwenyezi Mungu aliwajulisha waja wake jambo hili ili kanuni hii ikae imara ndani yao, na wajenge juu yake mema na mabaya yaliyowapata. Basi wasihuzunike kwa yale waliyoyakosa, katika yale ambayo nafsi zao ziliyatamani sana na kuwa na shauku nayo. Kwa sababu wanajua kwamba hilo liliandikwa katika Ubao uliohifadhiwa, lazima litekelezeke na litokee, na wala hakuna njia ya kulizuia. Na wala wasifurahi kwa aliyowapa Mwenyezi Mungu, kwa furaha ya kiburi na uovu. Kwa sababu wanajua kwamba hawakuipata kwa uwezo wao wala nguvu zao. Bali waliyapata kwa fadhila na neema ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wanajishughulisha na kumshukuru yule aliyewapa neema hizo na akawazuilia adhabu, na ndiyo maana akasema: \"Na Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna akajifahirisha\" juu ya neema za Mwenyezi Mungu, akawa anajinasibishia neema hizo mwenyewe, na zikampotoa na kumsahaulisha. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: \"Na dhara inapomgusa mtu, hutuomba. Kisha tunapompa neema zitokazo kwetu, husema: 'Nimepewa haya kwa sababu ya elimu yangu.' Siyo hivyo! Huo ni mtihani!\""},{"id":6149,"sura":57,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} \"Ambao wanafanya ubahili, na wanaamrisha watu wafanye ubahili.\" Yaani, wanaunganisha vitu viwili vya kukashifiwa, kila kimoja kinatosha kuwa uovu mkubwa: ubakhili ambao ni kutotekeleza haki za faradhi, na tena wanawaamrisha watu kufanya hivyo. Kwa hivyo, ubakhili wao haukuwatosha wao mpaka wakawaamrisha watu pia kufanya hivyo, na kuwahimiza kufanya tabia hii ya kukadshifiwa, kwa maneno yao na vitendo vyao. Na hili ni katika kupeana kwao mgongo mambo ya kumtii Mola wao Mlezi na kugeuka kwao mbali nayo. \"Na anayegeuka\" akaacha kumtii Mwenyezi Mungu, basi hadhuru yeyote isipokuwa yeye mwenyewe, na wala hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. \"Kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa mno.\" Yule ambaye kujitosheleza kwake ni katika sifa zisizoachana na dhati yake, ambaye miliki ya mbingu na ardhi ni yake, na ndiye aliyewatajirisha waja wake na kuwatosheleza. Naye ni msifiwa mno, Mwenye kila jina zuri, sifa kamili, tendo zuri analostahili kusifiwa juu yake na kutukuzwa."},{"id":6150,"sura":57,"from_aya":25,"to_aya":27,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"25. Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu na ishara waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu amjue anayemnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda. 26. Na bila ya shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim, na tukaweka katika dhuriya zao Unabii na Kitabu. Basi wapo miongoni mwao walioongoka, na wengi katika wao ni wavukao mipaka. 27. Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu, na tukampa Injili. Na tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rehema. Na umonaki (utawa wa mapadri) wameuzua wao. Sisi hatukuwaandikia hayo, ila kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Lakini hawakuufuata inavyotakiwa kuufuata. Basi wale walioamini katika wao tuliwapa ujira wao. Na wengi wao ni wavukao mipaka. "},{"id":6151,"sura":57,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} Anasema Mwenyezi Mungu: \"Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu na ishara waziwazi,\" ambazo ni ushahidi, hoja na ishara zinazoashiria ukweli wa yale waliyokuja nayo na kwamba ni ya haki. \"Na tukateremsha Kitabu pamoja nao.\" Hili linajumuisha vitabu vyote alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuwaongoza viumbe na kuwaelekeza katika yale yatakayowafaa katika dini yao na dunia yao. \"Na mizani\" ambayo ni uadilifu katika kauli na vitendo. Na Dini waliyoileta Mitume yote ni uadilifu na usawa katika maamrisho na makatazo, na katika kuamiliana na viumbe, na katika hukumu za jinai, kulipiza kisasi, adhabu maalumu, mirathi na mambo mengineyo, na hayo ni \"ili watu wasimamie uadilifu\" ili kuisimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu, na kufikia masilahi yao, ambayo hayawezi kuyadhibiti wala kuyahesabu. Hili linaashiria kwamba Mitume walikubaliana katika kanuni za asasi za kisheria, ambazo ni kufanya uadilifu, hata kama aina za uadilifu huo zitatofautiana kulingana na nyakati na hali mbalimbali \"na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi.\" Iwe ala ya vita, kama vile silaha, deraya na vitu vinginevyo. \"Na manufaa kwa watu\" ambayo ni kile kinachoonekana kutokana na manufaa yake katika aina mbalimbali za viwanda, ufundi, vyombo, na mashine za kulima, kiasi kwamba ni mara chache hakuna kitu ambacho hakihitaji chuma. \"Na ili Mwenyezi Mungu amjue anayemnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu.\" Yaani, ili Mwenyezi Mungu Mtukufu aweke mtihani kwa yale aliyoyateremsha katika Kitabu na chuma, ili ibainike ni nani atamnusuru yeye na Mitume wake katika hali ya ghaibu, ambayo imani ina manufaa ndani yake hata kabla ya kuona kwa macho, ambayo yakishapatikana, hapo imani haisaidii kitu. Kwani wakati huo kuamini kunakuwa ni kitu cha lazima. \"Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.\" Yaani, hakuna kinachoweza kumshinda, wala mwenye kukimbia hawezi kumponyoka. Na kutokana na nguvu zake na utukufu wake ni kwamba aliteremsha chuma ambacho hutengeneza kutoka humo vyombo vyenye nguvu. Na kutokana na nguvu zake na utukufu wake ni kwamba ana uwezo wa kuwashinda adui zake. Lakini huwajaribu vipenzi wake kwa maadui wake; ili ajue ni nani atamsaidia kwa ghaibu. Hapa, Mwenyezi Mungu ameiunganisha kati ya Kitabu na chuma. Kwa sababu kwa mambo haya mawili, Mwenyezi Mungu huinusuru Dini yake na kuliinua juu na kulitukuza neno lake kwa Kitabu kuna hoja na ushahidi, na kwa upanga kuna ushindi, Mwenyeezi Mungu akipenda. Na vyote viwili ni vinasimamisha uadilifu na usawa, ambavyo vinatumika kama ushahidi wa hekima ya Muumba na ukamilifu wake na ukamilifu wa sheria yake aliyoiweka juu ya ndimi za Mitume wake."},{"id":6152,"sura":57,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} Na alipotaja unabii wa manabii kwa ujumla wake, akawataja Manabii wawili maalumu watukufu, Nuhu na Ibrahim, ambao Mwenyezi Mungu aliwaweka Unabii na Kitabu katika dhuria zao. \"Na bila ya shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim, na tukaweka katika dhuriya zao Unabii na Kitabu.\" Yaani, Manabii wa mwanzo na wa baadaye, wote walikuwa kutoka katika kizazi cha Nuhu na Ibrahim, amani iwe juu yao, na vivyo hivyo vitabu vyote vilivyoteremshwa, vyote vilikuwa kutoka katika kizazi cha manabii hawa wawili watukufu. \"Basi wapo miongoni mwao.\" Yaani, miongoni mwa wale tuliowatumia Mitume \"walioongoka\" kwa wito wao, wakafuata maamrisho yao, na kuongoka kwa uwongofu wao. \"Na wengi katika wao ni wavukao mipaka\" ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi.\""},{"id":6153,"sura":57,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} \"Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu.\" Mwenyezi Mungu alimtaka hapa kwa jina Isa, amani imshukie, kwa sababu muktadha huu unawahusu Wakristo wanaodai kuwa wanamfuata Yesu (Isa). \"Na tukampa Injili\" ambayo ni miongoni mwa Vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyo bora. \"Na tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rehema.\" Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa wale walioamini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanaosema: 'Sisi ni Manasara.' Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi...\" hadi mwisho wa Aya hizi. Basi ndiyo maana Wakristo walikuwa na mioyo laini kuliko wengineo walipofuata sheria ya Isa, amani iwe juu yake. \"Na umonaki (utawa wa mapadri) wameuzua wao\" wenyewe tu, na wakajitwikisha ibada hiyo, na wakashikamana na matakwa ambayo Mwenyezi Mungu hakuwaandikia wala kuwawekea wala hakuwalazimisha. Nia yao katika hilo ilikuwa kumridhisha Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, \"Hawakuufuata inavyotakiwa kuufuata.\" Hawakuufanya vyema katika njia mbili: ya kwanza ni kwamba waliuzua wenyewe, na ya pili ni kwamba hawakutekeleza yale waliyojiwekea wenyewe. Hali hili ndiyo nyingi zaidi katika hali zao, lakini miongoni mwao wapo wale walio waongofu katika amri ya Mwenyezi Mungu, ndiyo maana akasema: \"Basi wale walioamini katika wao tuliwapa ujira wao.\" Yaani, wale waliomwamini Muhammad \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake \u2013 pamoja na kumwamini Isa. Kila mmoja, alipewa na Mwenyezi Mungu kulingana na imani yake. \"Na wengi wao ni wavukao mipaka.\""},{"id":6154,"sura":57,"from_aya":28,"to_aya":29,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"28. Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na muaminini Mtume wake, atakupeni sehemu mbili katika rehema yake, na atakufanyieni nuru ya kwenda nayo, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu. 29. Ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uwezo wowote juu ya fadhila za Mwenyezi Mungu. Na kwamba fadhila zote zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kuu. "},{"id":6155,"sura":57,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Maneno haya inawezekana kuwa wanaambiwa Watu wa Kitabu waliomuamini Musa na Isa, amani iwe juu yao. Anawaamuru kutenda kulingana matakwa ya imani yao. Kwamba wamche Mwenyezi Mungu na waache kumuasi na wamuamini Mtume Wake Muhammad \u2013 rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie \u2013 na kwamba wakifanya hivyo, Mwenyezi Mungu atawapa \u201csehemu mbili katika rehema yake.\u201d Yaani, mafungu mawili ya malipo. Fungu moja kwa sababu ya kumuamini kwao kwa Manabii wa zamani, na fungu lingine kwa sababu ya kumuamini kwao Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na pia inawezekana kwamba hii ni amri ya jumla, ambayo wanaingia ndani yake Watu wa Kitabu na wengineo, na hili ndiyo maana iliyo dhahiri (sahihi), na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaamrisha kuwa na imani na ucha Mungu, jambo ambalo linajumuisha dini yote, ya dhahiri yake na ya ndani yake, misingi yake na matawi yake, na kwamba ikiwa watatekeleza amri hii kubwa, [Mwenyezi Mungu] atawapa \"sehemu mbili katika rehema yake\" ambazo hakuna anayejua kiasi chake wala maelezo yake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Malipo hayo ni kwa sababu ya imani yao na malipo mengine kwa sababu ya uchamungu wao. Au malipo kwa sababu ya kutii amri na malipo mengine kwa sababu ya kuepuka makatazo. Au uwili uliotajwa hapa unakusudiwa kwamba watapewa kwa kurudia mara baada ya nyingine. \"Na atakufanyieni nuru ya kwenda nayo.\" Yaani, atakupeni elimu, uwongofu na nuru mtakayotembea kwayo katika viza vya ujinga, na atakusameheni mabaya yenu. \"Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.\" Si ajabu kuwa malipo haya ni mengi kama yanatolewa katika fadhila za Mwenye fadhila kubwa, ambaye fadhila zake zimeenea wakazi wa mbinguni na ardhini. Hakuna hata kiumbe mmoja asiye na fadhila zake hata kwa kiasi cha kupepesa jicho, wala kidogo zaidi ya hivyo."},{"id":6156,"sura":57,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Na kauli yake: \"Ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uwezo wowote juu ya fadhila za Mwenyezi Mungu.\" Yaani, tulikuelezeni neema zetu na wema wetu kwa wale walioamini imani ya ujumla, na wakamcha Mwenyezi Mungu, na wakamuamini Mtume wake; ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uwezo wowote ju ya fadhila za Mwenyezi Mungu. Yaani, hawawezi kumzuilia yeyote mbali na Mwenyezi Mungu kwa matamanio yao na akili zao mbovu, kwa kusema kwamba: \"Hataingia Peponi ila aliye Myahudi au Mkristo,\" na wanamtamani kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu] matamanio mabovu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akajulisha kwamba wale wanaomuani Mtume wake Muhammad \u2013 rehema na amani Mwenyezi Mungu zimshukie \u2013 wale wanaomcha Mwenyezi Mungu, kwamba wana dhamana mafungu mawili kutoka kwa rehema yake, nuru na msamaha. Hata wasipopenda hivyo Watu wa Kitabu, na kwamba wajue kuwa: \"Fadhila zote zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa hizo amtakaye\" miongoni mwa wale ambao hekima yake inahitaji kwamba wapewe katika fadhila zake. \"Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kuu\" ambayo haiwezekani kukadiria kiasi chake."},{"id":6157,"sura":57,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya [Surat Al-Hadid], na sifa njema na neema ni za Mwenyezi Mungu]."},{"id":6158,"sura":57,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"******"}]}