{"result":[{"id":6342,"sura":65,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya surat Talaq"},{"id":6343,"sura":65,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Madina"},{"id":6344,"sura":65,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu."},{"id":6345,"sura":65,"from_aya":1,"to_aya":3,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Ewe Nabii! Mtakapowapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi hakika amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jingine baada ya haya. 2.Basi wanapofikia muda wao, ima warejeeni muwaweke kwa wema, au farikianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hayo anaaidhiwa kwayo anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, humtengezea njia ya kutokea. 3. Na humruzuku kutokea asipotazamia. Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu, Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake. "},{"id":6346,"sura":65,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akimwambia Nabii wake [Muhammad] - rehema na amani na Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na akiwaambia Waumini pia: \"Ewe Nabii! Mtakapowapa talaka wanawake.\" Yaani, mnapotaka kuwapa talaka, basi itafuteni talaka hiyo jambo linalokubaliwa kisheria, wala msifanye haraka kutoa talaka wakati sababu yake inapatikana bila ya kuangalia amri ya Mwenyezi Mungu. Bali \"wapeni talaka katika wakati wa eda zao.\" Yaani, ampe talaka hali ya kuwa mke huyo yu safi, na kwamba hakuwa ameingiliana naye katika hali yake ya usafi hiyo. Hii ndiyo talaka ambayo eda yake huwa wazi kabisa. Tofauti na ikiwa atamtaliki akiwa katika hedhi. Hedhi hiyo haitahesabiwa ambayo alimtaliki ndani yake, na hilo litamsababishia eda kuwa ndefu. Vile vile ikiwa atamlatiki hali ya kuwa yu safi lakini aliingiliana naye. Hapo hatakuwa salama kutokana na ujauzito, na wala haitakuwa wazi ni eda ipi atakaa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu aliamrisha uhesabiwe muda wa eda; kwa kuhesabu hedhi ikiwa ni katika wale wanaopata hedhi, au kuhesabu miezi ikiwa si katika wale wanaopata hedhi na wala hana mimba. Kwa maana katika kuihesabu kuna kutimiza haki ya Mwenyezi Mungu, haki ya mume aliyepeana talaka, haki ya yule atakayemuoa baadaye, na haki yake mke huyu ya kupewa matunzo na mengineyo. Kwa hivyo, muda wake wa eda utadhibitiwa vyema, itajulikana hali yake vizuri zaidi, na zitajulikana haki zinazoambatana nayo na kile ambacho ni chake ndani yake. Amri hii ya kuhesabu eda anaambiwa mume na mke ikiwa ni katika wanawake wanaojukumishwa na sheria. Vinginevyo, basi anaambiwa mlezi wake. Na kauli yake: \"Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi.\" Yaani, katika mambo yenu yote, na mhofuni katika mambo ya wake waliopewa talaka. \u201cMsiwatoe katika nyumba zao\" katika muda wa eda. Bali anapaswa kukaa katika nyumba ambayo mume wake alimtaliki akiwa ndani yake. \"Wala wasitoke wenyewe\" ama katazo la kuwatoa, ni kwa sababu kuwapa nyumba ni wajibu wa mume kwa mke ili akamilishe eda yake, ambayo ni moja ya haki zake. Na ama katazo kutoka mwenyewe, ni kwa sababu katika kutoka kwake kuna kupoteza haki ya mume na kutoilinda, na katazo hili la kutomtoa na kutoka kwake katika nyumba litaendelea hadi kukamilika kwa muda wa eda. \"Ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi\" unaohitaji watolewe, kwa manaa unawasababishia watu wa nyumba hiyo madhara ikiwa hatatoka; kama vile madhara kwa maneno na vitendo vichafu. Basi katika hali hii, inaruhusiwa kwa waume kuwatoa. Kwa sababu yeye mwenyewe ndiye aliyejisababishia kutolewa. Na kukalishwa nyumbani alikokuwa amekalishwa kulikuwa kwa sababu ya kumfurahisha mawazo yake na kumfanyia upole. Haya ni kuhusiana na mwanamke aliyetalikiwa talaka ya kurudiana bila ya kufunga nikaa mpya. Ama yule aliyetalikiwa talaka ya kurudiana kwa nikaa mpya, huyo hailazimu kupewa mahali pa kukaa, kwa kwa sababu makazi yatafuatana na kupewa matumizi ya kila siku. Na matumizi ya kila siku ni lazima apewe mwanamke aliyetalikiwa talaka isiyohitaji nikaa mpya ili kurudiana si ile anayohitaji nikaa mpya. \"Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu\" ambayo aliwawekea waja wake na akawawekea hiyo kuwa sheria na akawaamrisha kushikamana nayo na kusimamia hapo, \"Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu\" kwa kutosimamia hapo, bali aliikiuka au aliipuuza sana, \"basi hakika amejidhulumu nafsi yake\" haki yake, na akapoteza fungu lake katika kufuata mipaka ya Mwenyezi Mungu, ambayo ni ndiyo sababu ya kutengenea katika dunia na akhera. \"Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya.\" Yaani, Mwenyezi Mungu ameweka sheria ya eda na akaiweka kuanza baada ya talaka kwa sababu ya hekima mbalimbali kubwa. Miongoni mwake ni kwamba huenda Mwenyezi Mungu akaleta rehema na mapenzi katika moyo wa aliyetoa talaka, kwa hivyo akamrudisha yule aliyempa talaka, kisha wakaendelea kuishi vyema. Na hilo linawezekana katika kipindi cha eda. Au huenda alimpa talaka kutokana na sababu aliyoisababisha mke huyo, kisha ikaisha katika muda wa eda, kwa hivyo, wakarudiana kwa sababu ya kutokuwepo sababu ya talaka ile. Na miongoni mwa hekima ni kwamba muda wa eda utupu wa tumbo lake kutokana na ujauzito wa mumewe."},{"id":6347,"sura":65,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Na kauli yake: \"Basi wanapofikia muda wao.\" Yaani, watakapokaribia karibia kumaliza kipindi cha eda, kwani ikiwa watakuwa wameshatoka katika eda; mume hatakuwa na hiyari baina ya kumshikilia na kumwacha. \"Ima warejeeni muwaweke kwa wema\" si kwa namna ya kuwadhuru na kuwatakia maovu. Kwa sababu, hairuhusiki kuwashikilia kwa njia hii \"au farikianeni nao kwa wema\" isiyo na kudhuriana, bila ya kutukanana, kugombana, au kumshinda na kuchukua kitu katika mali yake. \"Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu\" wa kiume, Waislamu. Kwa sababu huo ushahidi huo kuna kufunga mlango wa mabishano na kila mmoja wao kuficha yale yanayopasa kuwekwa wazi. \"Na simamisheni\" enyi mashahidi \"ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu\" bila ya kuongeza wala kupunguza, na kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala kumwelekea na ushahidi huo jamaa wa karibu kwa sababu ya ujamaa wake wala sahibu kwa sababu ya kumpenda. \"Hayo\" tuliyokutajieni katika hukumu mbalimbali na mipaka, \"anaaidhiwa kwayo anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho\" Kwa maana, kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho inamlazimu mwenye imani hiyo kuaidhika mawaidha ya Mwenyezi Mungu, na kuitangulizia akhera yake matendo mema kiasi awezavyo. Tofauti na yule ambaye imani yake imetoka moyoni mwake. Yeye hajali maovu ambayo anafanya, na hayaheshimu mawaidha ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu ya kutokuwepo cha kumfanya afanya hayo. Na kwa kuwa talaka inaweza kusababisha dhiki, uchungu na huzuni, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaamrisha afanyiwe ucha Mungu, na akawaahidi wale wanaomcha katika talaka na mambo mengine kwamba atampa faraja na njia ya kutokea. Kwa hivyo, mja anapotaka talaka, kisha akaifanya kwa mujibu wa Sheria, kwa kumpa talaka moja nje ya kipindi cha hedhi au hali anapokuwa safi bila ya kuingiliana naye, basi jambo lake halitamuwiya gumu, bali Mwenyezi Mungu atamfanyia faraja na wasaa ambayo kwayo ataweza kurejea kwenye ndoa ikiwa atajutia talaka yake. Na Aya hii, hata ikiwa ni katika muktadha wa talaka na kurejeana baada ya taaka, kitu kinachozingatiwa ni maana ya jumla ya maneno yaliyotumika. Kwa hivyo, kila mwenye kumcha Mwenyezi Mungu Mwenyezi na kushikamana na radhi zake katika hali zake zote, basi hakika Mwenyezi Mungu atamlipa mema duniani na Akhera. Na miongoni mwa thawabu zake ni kumpa faraja na njia ya kutokea katika dhiki na ugumu. Kama vile mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, anamfanyia faraja na njia ya kutokea, basi kile asiyemcha Mwenyezi Mungu, anaanguka kwenye minyororo na pingu ambazo hawezi kujiondoa humo na hata mambo yanayofungamana nayo. Tena zingatia hili katika talaka. Ikiwa mja hamchi Mwenyezi Mungu ndani yake, bali anaifanya kwa njia ya haramu, kama vile kutoa tatu na mfano wake, basi lazima atajuta majuto ambayo hataweza kuyarekebisha na kutoka nje yake."},{"id":6348,"sura":65,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} Na kauli yake: \"Na humruzuku kutokea asipotazamia. Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu\" katika mambo ya dini yake na mambo yake ya kidunia, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kumletea yenye kumanufaisha na kumuepusha mbali na yenye kumdhuru, na akawa na imani naye katika kuyasahilisha hayo, basi \"Yeye humtosha.\" Yaani, atamtosha katika jambo alilomtegemea ndani yake. Na ikiwa jambo liko chini ya Mkwasi, Mwenye nguvu, Mshindi, Mwingi wa kurehemu, basi Yeye yuko karibu na mja kuliko kitu kingine chochote. Lakini labda hekima ya kimungu ikahitaji kulichelewesha hadi wakati ufaao kwake. Kwa ajili hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: \"Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake.\" Yaani, mipango yake na hukumu zake zitekelezeke, lakini amekifanyia \"kila kitu na kipimo chake\" ambao hakiuvuki wala kukipunguza."},{"id":6349,"sura":65,"from_aya":4,"to_aya":5,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"4. Na wale waliosita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi. Na wenye mimba, eda yao mpaka watakapozaa. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi. 5. Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu amekuteremshieni. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, atamfutia maovu yake, na atampa ujira mkubwa. "},{"id":6350,"sura":65,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuwa talaka sahihi iliyoamrishwa ni ile ambayo wanawake wanaweza kuanza eda yao, akataja eda, na akasema: \"Na wale waliosita hedhi miongoni mwa wanawake wenu.\" Yaani, wale waliokuwa wakipata hedhi, kisha hedhi yao ikakatika kwa sababu ya uzee au kitu kingine, na hakuna matumaini ya kurudi kwake. Basi eda yao ni miezi mitatu, kila mwezi inapaswa kuchukuliwa kuwa ni hedhi moja. \"Pamoja na ambao hawapati hedhi.\" Yaani, wasichana wadogo ambao bado hawajapata hedhi, au wanawake watu wazima ambao hawajapata hedhi kabisa. Hao ni kama wanawake walioacha kupata hedhi, eda yao ni miezi mitatu. Ama wale wanaopata hedhi, basi Mwenyezi Mungu akataja eda yao katika kauli yake: \"Na wanawake walioachwa kwa talaka wangoje peke yao mpaka tahara (au hedhi) tatu zipite.\" Na kauli yake: \"Na wenye mimba, eda yao mpaka watakapozaa\" vyote vilivyomo matumboni mwao, kiwe kimoja au vingi, na hapo haitazingatiwa miezi au kitu chochote kile. \"Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi.\""},{"id":6351,"sura":65,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} \"Hiyo\" hukumu ambayo Mwenyezi Mungu amekubainishieni \"ni amri ya Mwenyezi Mungu amekuteremshieni\" ili muifuate, na kuitimiza na kuipa taadhima. \"Na anayemcha Mwenyezi Mungu, atamfutia maovu yake, na atampa ujira mkubwa.\" Yaani, atazuiwa kutokana na yale yaliyoharamishwa na atapata anachotaka."},{"id":6352,"sura":65,"from_aya":6,"to_aya":7,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"6. Wawekeni humo humo mnamokaa nyinyi kwa kiasi cha pato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwapa dhiki. Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwingine. 7. Mwenye wasaa atoe kiasi ya wasaa wake, na mwenye dhiki, atoe katika kile ambacho Mwenyezi Mungu alimpa. Mwenyezi Mungu hamjukumishi mtu ila kwa kiasi cha alichompa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraja. "},{"id":6353,"sura":65,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} Imetajwa hapo awali kuwa Mwenyezi Mungu amekataza kuwatoa wanawake waliopewa talaka majumbani, na hapa akaamrisha wawekwe nyumbani kwa wema. Nayo ni nyumba ambayo watu kama yeye na kama mkewe huishi. Kwa mujibu wa kiasi awezavyo mume. \"Wala msiwaletee madhara kwa kuwapa dhiki\" kwa kauli au vitendo. Ili wapate kuchoka na kuondoka nyumbani kabla ya kumaliza eda yao, na hapo mnakuwa ndio mumewatoa. Jumla ya hayo ni kwamba aliwakataza kuwatoa na akawakataza kutoka nje, na akawaamrisha kuwafanya waishi katika njia ambayo haitawaletea madhara wala taabu, na hilo ni kulingana na desturi. \"Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue.\" Hilo ni kwa sababu ya mimba iliyomo tumboni mwake ikiwa ni mwanamke aliyetalikiwa talaka isiyo ya kurudiana, na kwa sababu yake mwenyewe na mimba yake ikiwa ni talaka ya kurudiana, na mwisho waa matunzo hayo ni mpaka ajifungue. Basi wakishajifungua, ima watawanyonyesha watoto wao au la. \"Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao\" kama walivyosikilizana ikiwa watasikilizana juu ya kiwango maalumu. Vinginevyo, basi atapewa ujira kama ule wanaopewa mfano wake. \"Na shaurianeni kwa wema\" wenye manufaa na masilahi katika dunia na akhera. Kwa maana kughafilika katika kushauriana yaliyo mema kunasababisha madhara na maovu anayojua Mwenyezi Mungu pekee. Na katika kushauriana kuna ushirikiano katika wema na ucha Mungu. Na katika kinachonasibiana na hali hii ni kwamba wanandoa wanapotengana wakati wa eda, hasa ikiwa mtoto amezaliwa kati yao, mara nyingi hutokea migogoro na ugomvi juu ya matunzo ya mke huyu na mtoto kwa sababu ya chuki iliyoko kati yao, kwa hivyo mambo mengi yanaathiriwa na hayo. Basi kila mmoja wao anafaa kushauri kwa wema na kuishi kwa uzuri, siyo kugombana kupingana au kugombana. \"Na mkiona uzito kati yenu\" ikiwa wanandoa hao hawatakubaliana juu ya kumnyonyesha mtoto wake, \"basi amnyonyeshee mwanamke mwengine\"\nasiyekuwa yeye, \"wala hapana ubaya kwenu mkitoa mlichoahidi kwa mujibu wa ada.\" Hili ni pale mtoto anakubali kunyonya mtu asiyekuwa mama yake. Lakini ikiwa hakubali isipokuwa titi la mama yake, basi mama yake tu ndiye atakayemnyonyesha, na itamlazimu kufanya hivyo ikiwa atakataa, na atastahiki ujira mfano wa ule wanaopewa mfano wake ikiwa hawakuwa hawatakubaliana juu ya ujira maalumu. Hili limechukuliwa kutoka katika Aya hii tukufu kulingana na maana yake. Kwa maana, mtoto alipokuwa tumboni mwa mama yake kwa kipindi chote cha ujauzito, hakukuwa na njia ya kutoka humo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akamuamrisha mlinzi wake kumpa matumizi ya kila siku. Basi pale alipozaliwa na kukawa na uwezekano wa kunyonyeshwa na mama yake au na wengineo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaruhusu mambo yote hayo mawili. Basi ikiwa yuko katika hali ambayo hawezi kunyonyeshwa isipokuwa na mama yake tu, basi hilo linakuwa sawa na wakati alivyokuwa tumboni, na mama yake anakuwa ndiye peke yake anayeweza kumnyonyesha."},{"id":6354,"sura":65,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaweka kipimo cha mali ya matumizi ya kila siku kulingana na hali ya mume, akasema: \"Mwenye wasaa atoe kiasi ya wasaa wake.\" Yaani, tajiri na atoe  kutoka katika utajiri wake, wala asitoe matumizi kama ya masikini. \"Na mwenye dhiki, atoe katika kile ambacho Mwenyezi Mungu alimpa. Mwenyezi Mungu hamjukumishi mtu ila kwa kiasi cha alichompa.\" Haya yanafailiana na hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema zake. Ambapo alimuamrisha kila mmoja kulingana na hali yake, na akamwepesishia mwenye uzito, na kwamba hamtwiki ila kile alichompa, sawa iwe ni katika mlango wa kutoa matumizi ya kila siku au mengineyo. \"Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraja.\" Hii ni bishara njema kwa wale walio katika matatizo kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaondolea dhiki na ugumu wake. Kwa maana pamoja na dhiki kuna wepesi. Hakika pamoja na dhiki kuna wepesi."},{"id":6355,"sura":65,"from_aya":8,"to_aya":12,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"8. Na miji mingapi iliyovunja amri ya Mola wake Mlezi na Mitume wake, basi tuliihisabia hisabu ngumu na tukaiadhibu kwa adhabu kali. 9. Basi ikauonja ubaya wa mambo yake; na mwisho wa mambo yao ilikuwa hasara. 10. Mwenyezi Mungu aliwaandalia adhabu kali. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, mlioamini! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteremshieni Ukumbusho. 11. Mtume anayekusomeeni Aya za Mwenyezi Mungu zinazobainisha, ili kuwatoa wale walioamini na wakatenda mema kutoka vizani kuwapeleka kwenye nuru. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema, atamwingiza katika Bustani za mbinguni zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Mwenyezi Mungu amekwisha mpa riziki nzuri. 12. Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba mbingu saba, na ardhi kwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka baina yake, ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza mno juu ya kila kitu, na kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kukijua vilivyo kwa elimu yake. "},{"id":6356,"sura":65,"from_aya":8,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8 - 10} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya maangamizo yake mataifa yenye nguvu na karne ambazo ziliwakadhibisha Mitume, na kwamba wingi wao na nguvu zao havikuwafaa kitu ilipowajia hesabu kali na adhabu chungu, na kwamba Mwenyezi Mungu akawaonjesha adhabu iliyotokana na matendo yao mabaya. Na pamoja na adhabu ya dunia, basi hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia adhabu kali katika Akhera. \"Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili.\" Yaani, enyi watu wenye akili zinazozifahamu ishara na mazingatio ya Mwenyezi Mungu, na kwamba yule aliyeziangamiza karne zilizopita kwa sababu ya kukadhibisha kwao, basi wale wa baada yao watakuwa mfano wao, na hakuna tofauti baina ya makundi mawili haya."},{"id":6357,"sura":65,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} Kisha akawakumbusha waja wake yale walioteremshiwa ya Kitabu chake alichokiteremsha kwa Mtume wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ili kuwatoa watu katika viza vya ujinga, ukafiri na uasi na kuwaingiza kwenye nuru ya elimu, imani na utii. Kwa hivyo, miongoni mwa watu wapo wanaoiamini, na miongoni mwao wapo wasioiamini.\" Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema\" miongoni mwa mambo ya wajibu na yale yanayopendekezwa \"atamwingiza katika Bustani za mbinguni zipitazo mito kati yake\" ambayo ndani yake kuna raha ya milele ambayo jicho halijawahi kuona, wala sikio halijawahi kusikia, wala moyo wa mwanadamu haujapata kuyaona; \"wadumu humo milele. Mwenyezi Mungu amekwishampa riziki nzuri.\" Yaani, na asiyemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hao ndio watu wa Motoni, na humo watakaa milele."},{"id":6358,"sura":65,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema kwamba ameziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na ardhi saba na vilivyomo ndani yake na vilivyomo baina yake, na akateremsha amri ambayo ni sheria na hukumu za dini alizoziteremsha kwa Mitume wake ili kuwakumbusha na kuwaaidhi waja wake, pamoja na amri za kiulimwengu na zile za mipango ya Mwenyezi Mungu ambazo kwazo Yeye huwaendesha viumbe. Yote haya ni ili waja wamjue na wajue kwamba uweza wake umekizunguka kila kitu na elimu yake imekizingira kila kitu. Kwa hivyo, ikiwa watamjua kwa majina yake mazuri na sifa zake takatifu, watamwabudu, watampenda, na watatimiza haki zake, na hayo ndiyo lengo lililokusudiwa katika uumbaji na amri: Kumjua Mwenyezi Mungu na kumuabudu. Basi wakafanya hayo wale waliowezeshwa miongoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu, nao madhalimu wakayapa kisogo."},{"id":6359,"sura":65,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya sura hii, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu."},{"id":6360,"sura":65,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}