{"result":[{"id":6385,"sura":67,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya surat Al-Mulk"},{"id":6386,"sura":67,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":6387,"sura":67,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu."},{"id":6388,"sura":67,"from_aya":1,"to_aya":4,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Ametukuka ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uwezo mno juu ya kila kitu. 2. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu,  Mwenye msamaha mno. 3. Aliyeumba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudia kutazama! Je, unaona kosa lolote? 4. Tena rudia kutazama mara mbili, kutazama kwako kutakurejelea mwenyewe hali ya kuwa kumehizika, kumechoka. "},{"id":6389,"sura":67,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} \"Ametukuka ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote.\" Yaani, ni Mkuu na ametukuka, na heri yake ni nyingi na wema wake umeenea. Katika ukuu wake ni kwamba mkononi mwake kuna ufalme wa ulimwengu wa juu na wa chini. Yeye ndiye aliyeuumba na anauendesha atakavyo kwa hukumu zake za alizozipanga na za kidini zinazofuata hekima yake. Na miongoni mwa ukuu wake ni ukamilifu wa uwezo wake ambao kupitia kwa huo anaweza kila kitu na kupitia kwa huo ameumba viumbe vikubwa alivyoumba kama vile mbingu na ardhi."},{"id":6390,"sura":67,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Na \"ameumba mauti na uhai.\" Yaani, amewapangia waja wake kuwafanya kuwa hai kisha atawafisha \"ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi.\" Yaani, vilivyokusudiwa Yeye tu, na vilivyo sahihi zaidi. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaumba waja wake na akawaweka kwenye nyumba hii ya duniani, na akawaambia kuwa watahamishwa kutoka humo, na akawaamrisha na kuwakataza, na akawajaribu kwa matamanio ya nafsi yanayowapingana na amri yake. Kwa hivyo, mwenye kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na akatenda mema, Mwenyezi Mungu atamlipa malipo mema katika nyumba hizi mbili. Na mwenye kufuata matamanio ya nafsi na akatupa amri ya Mwenyezi Mungu, atampata malipo mabaya kabisa. \"Na Yeye ni Mwenye nguvu\" ambazo kwazo alikishinda kila kitu, na viumbe vyote vikamnyenyekea. \"Mwenye msamaha mno\" kwa wale waliofanya mabaya, waliopuuza, waliotenda dhambi, hasa wakitubu na wakamrudia. Basi hapo kwa hakika atawasamehe madhambi yao, hata yakifika kwenye sehemu ya juu zaidi ya mbingu, na zitafunikwa kasoro zao, hata kama ni za kujaza dunia."},{"id":6391,"sura":67,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} \"Aliyeumba mbingu saba kwa matabaka.\" Yaani, kila moja ikiwa juu ya nyenzake, na wala si tabaka moja tu, na akaziumba kwa uzuri mkubwa mno na ustadi wa hali ya juu. \"Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema.\" Yaani, huwezi kuona kasoro na upungufu. Na ikiwa upungufu haupo kwa namna yoyote ile, basi unakuwa uumbaji huo ni mzuri mkamilifu, unaolingana sawasawa katika kila njia, katika rangi yake, mwonekano wake, kuinuka juu kwake, na vilivyomo kama vile jua [na mwezi] na sayari zenye mwangaza. Vile visivyosonga miongoni mwake na vile vinavyosonga. Na pindi ukamilifu wake ulipokua jambo linalojulikana, Mwenyezi Mungu Mtukufu akatuamuru kuziangalia mara kwa mara na kutafakari katika pande zake. Akasema: \"Hebu rudia kutazama!\" Yaani, rudia kutazma kwa kuzingatia. \"Je, unaona kosa lolote?\""},{"id":6392,"sura":67,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} \"Tena rudia kutazama mara mbili, kutazama kwako kutakurejelea mwenyewe hali ya kuwa kumehizika, kumechoka.\" Yaani, bila ya kuona kasoro yoyote hata kama utakuwa makini namna gani."},{"id":6393,"sura":67,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"Kisha akataja waziwazi uzuri wake, akasema:"},{"id":6394,"sura":67,"from_aya":5,"to_aya":11,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"5. Na kwa hakika tumeipamba mbingu ya chini kabisa kwa mataa, na tumeyafanya ili kuwapigia mashetani, na tumewaandalia adhabu ya Moto wenye mwako mkali. 6. Na kwa wale waliomkufuru Mola wao Mlezi ipo adhabu ya Jahannamu. Na ni marejeo maovu yalioje hayo! 7. Watakapotupwa humo, watausikia mngurumo wake na huku inafoka. 8. Inakaribia kupasuka kwa hasira. Kila mara likitupwa kundi humo, walinzi wake huwauliza: 'Kwani hakukujieni mwonyaji?' 9. Watasema: 'Kwani! Ametujia mwonyaji, lakini tulimkadhibisha, na tukasema: 'Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamumo ila katika upotovu mkubwa!'' 10. Na watasema: 'Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa tukitumia akili, tusingelikuwa katika watu wa Moto wenye mwako mkali!' 11. Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Moto wenye mwako mkali! "},{"id":6395,"sura":67,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} Yaani, tumeipamba \"mbingu ya chini kabisa\" mnayoiona na inayofuatana na dunia yenu, \"kwa mataa\" ambayo ni nyota zinazotofautiana katika nuru na mwangaza wake. Kwa maana lau si nyota zilizomo ndani yake, basi mbingu ingelikuwa ni dari yenye giza isiyo na uzuri wala urembo. Lakini Mwenyezi Mungu alizifanya nyota hizi kuwa pambo la mbingu, uzuri, nuru, na mwongozo wa kutuongoza katika viza vya nchi kavu na baharini. Na kauli yake kwamba ameipamba mbingu iliyo chini kabisa kwa mataa haipingani na ukweli kwamba kuna nyota nyingi juu ya mbingu ya saba. Kwani mbingu ni kitu kinachoweza kuonyesha kilicho nyuma yake, na kwa hilo linapatikana pambo kwa mbingu ya chini kabisa, hata kama sayari hizo hazimo ndani yake. \"Na tumeyafanya;\" yaani, mataa haya kuwa kitu cha \"kuwapigia mashetani\" ambao wanataka kusikiliza kwa siri habari za mbinguni. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akazifanya nyota hizi kuwa ni ulinzi wa mbingu kutokana na mashetani kuiba habari za mbinguni na kupeleka dunia. Basi vimondo hivi vya nyota vinavyorushwa vimetayarishwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani kwa ajili ya mashetani, \"na tumewaandalia\" huko Akhera \"adhabu ya Moto wenye mwako mkali,\" kwa sababu walimuasi Mwenyezi Mungu na wakawapoteza waja wake."},{"id":6396,"sura":67,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} Ndiyo maana wafuasi wao miongoni mwa makafiri ni mfano wao, Mwenyezi Mungu aliwaandalia adhabu ya Moto wenye mwako mkali. Ndiyo maana akasema: \"Na kwa wale waliomkufuru Mola wao Mlezi ipo adhabu ya Jahannamu. Na ni marejeo maovu yalioje hayo,\" ambayo wakazi wake watadhalilishwa huko kukadhilishwa kukubwa kabisa."},{"id":6397,"sura":67,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} \"Watakapotupwa humo\" kwa njia ya kudunishwa na kufedheheshwa \"watausikia mngurumo wake na huku inafoka.\""},{"id":6398,"sura":67,"from_aya":8,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8} \"Inakaribia kupasuka kwa hasira\" yake juu ya makafiri. Basi unadhani watakapoingia humo itawafanyia nini? Kisha akataja karipio la walinzi wake kwa wale walioingia humo, akasema: \u201cKila mara likitupwa kundi humo, walinzi wake huwauliza: 'Kwani hakukujieni mwonyaji?'\" Yaani, hali yenu hii na kustahiki kwenu huku kuingia Motoni ni kana kwamba hamkufahamishwa kuhusu hilo wala waonyaji hawakukutahadharisheni dhidi yake."},{"id":6399,"sura":67,"from_aya":9,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9} \"Watasema: 'Kwani! Ametujia mwonyaji, lakini tulimkadhibisha, na tukasema: 'Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamumo ila katika upotovu mkubwa!\" Basi wakawa wamejumuisha kati ya kukadhibisha kwao mahususi na kukadhibisha kwao kwa jumla yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, na pia hilo halikuwatosha, mpaka walipotangaza upotovu wa Mitume waonyaji, ilhali wao ndio waongofu wanaoongoza, na tena haikuwatosha kuona kwamba Mitume hao ni wapotofu tu, bali waliona kwamba wako katika upotofu mkubwa. Je, ni ukaidi upi, na kiburi kipi, na dhuluma ipi inayofanana na hayo?"},{"id":6400,"sura":67,"from_aya":10,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10} \"Na watasema\" wakikiri kutostahiki kwao uwongofu na kuelekea kisawasawa, \"Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa tukitumia akili, tusingelikuwa katika watu wa Moto wenye mwako mkali!\" Basi wakawa wamejikanushia njia za uwongofu, ambazo ni kusikia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na wakaja nayo Mitume, na akili inayomnufaisha mwenyewe na kumfahamisha uhakika wa mambo na kupendelea heri na kukomeka mbali na yote yenye mwisho wa kukashifiwa. Kwa hivyo hawakuweza kusikia wala hawakuweza kutumia akili. Hili ni kinyume na watu wa yakini na elimu na mabwana wa ukweli na imani. Kwani waliiunga mkono imani yao kwa ushahidi wa kusikia, basi wakayasikia yaliyotoka kwa Mwenyezi Mungu, na akaja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu ya elimu, maarifa na matendo, na pia ushahidi wa kiakili unaojulisha na kutofautisha kati ya uongofu na upotofu, uzuri na ubaya, heri na uovu, nao katika imani yao wako kulingana na yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu ya kufuata yale yaliyowafikia kwa njia ya kiakili na kwa njia ya kimaandiko. Basi ametakasika yule anayempa amtakaye tu fadhila zake, na kumneemesha amtakaye katika waja wake, na anawaachilia mbali wasioifailia heri."},{"id":6401,"sura":67,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu hao watakaoingia Motoni waliokiri dhuluma yao na ukaidi wao: \"Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Moto wenye mwako mkali!\" Basi hao ni wenye wana mashakani makubwa yaliyoje na walio katika maangamivu makubwa yaliyoje, ambapo walikosa thawabu za Mwenyezi Mungu, na wakawa katika wale watakaodumu katika moto wenye mwako mkali ambao mwako wake utachoma mno miili yao na kufikia mioyo yao."},{"id":6402,"sura":67,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"12. Hakika wale wanaomwogopa Mola wao Mlezi kwa ghaibu, watapata maghfira na ujira mkubwa."},{"id":6403,"sura":67,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} Alipotaja hali ya watu wa mashakani, walio waovu, akataja maelezo ya watu wema wenye furaha, akasema: \"Hakika wale wanaomwogopa Mola wao Mlezi kwa ghaibu.\" Yaani, katika hali zao zote, hata katika hali ambayo hawezi akawaona isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee, hawamfanyii maasia, wala hawafanyi chini ya namna alivyowaamrisha. \"Watapata maghfira\" ya dhambi zao, na ikiwa Mwenyezi Mungu atawasamehe dhambi zao, atawalinda kutokana na uovu wake na atawalinda kutokana na adhabu ya Jahannamu \"na wana ujira mkubwa.\" Na hayo ni yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu katika bustani za mbinguni ya neema ya kudumu, na ufalme mkubwa, na starehe zenye kuendelea kuwafikia, na makasri na majumba yaliyoinuka juu, na hurulaini wazuri, na wajakazi na watoto wadogo, na kubwa zaidi kuliko hilo ni radhi za Mwingi wa rehema ambazo atawapa wakazi wa bustani za mbinguni."},{"id":6404,"sura":67,"from_aya":13,"to_aya":14,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"13. Na ficheni kauli zenu, au zidhihirisheni wazi; hakika Yeye anajua mno yaliyomo vifuani. 14. Asijue yule aliyeumba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari? "},{"id":6405,"sura":67,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} Huku ni kujulisha anakojulisha Mwenyezi Mungu juu ya upana wa elimu yake, na ujumuishaji wa upole wake. Akasema, \"Na ficheni kauli zenu, au zidhihirisheni wazi.\" Yaani, yote hayo ni kitu kimoja kwake, hakuna chochote kinachofichikana kwake katika hayo. Kwani, \"hakika Yeye anajua mno yaliyomo vifuani.\" Yaani, yaliyomo ya nia mbalimbali na utashi. Basi vipi kuhusu maneno na vitendo vinavyosikika na kuonekana?"},{"id":6406,"sura":67,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} Kisha akasema akibainisha ushahidi wa kiakili juu ya elimu yake: \"Asijue yule aliyeumba.\" Vipi asivijue yule aliyeumba viumbe, akavikamilisha sawasawa na akaviumba kuwa vizuri zaidi, vipi asivijue \"naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari?\" Ambaye ujua wake na kuwa kwake na habari ya kila kitu kunafikia kila kitu, kiasi kwamba anafahamu vyema siri, dhamiri, vilivyofichikana na ghaibu zote. Na Yeye ndiye \"anayejua siri na kilicho chini zaidi kuliko siri.\" Na katika maana za Al-Latwif (Mpole), ni kwamba Yeye ndiye mwenye kumfanyia upole mja wake na kipenzi chake, kwa hivyo unamfikishia wema na ukarimu kutokea pale asipotambua, na anamkinga mbali na uovu kutokea pale asipotarajia, na anampandisha daraja za juu kwa sababu ambazo hata mja mwenyewe hazijui, kiasi kwamba humwonjesha mambo anayochukia ili amfikishe kwenye mapenzi makubwa na mambo matukufu yanayotafutwa."},{"id":6407,"sura":67,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"15. Yeye ndiye aliyeidhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndiyo kufufuliwa."},{"id":6408,"sura":67,"from_aya":15,"to_aya":15,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15} Yaani, yeye ndiye aliyeitiisha ardhi kwa ajili yenu na akaifanya kuwa dhalili. Ili mpate kutoka kwayo yale yanayofungana na mahitaji yenu kama vile kupanda mimea, kujenga, kulima, na njia ambazo kwazo inawezekana kufika katika pande na nchi za mbali mno. \"Basi tembeeni katika pande zake\" ili mtafute riziki na kuchuma. \"Na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa.\" Yaani, baada ya kutoka katika nyumba hii ambayo Mwenyezi Mungu ameifanyia mtihani na cha kuwafikishia nyumba ya Akhera, mtafufuliwa baada ya kufa kwenu na mtakusanywa kwa Mwenyezi Mungu; ili awalipe kwa matendo yenu mema na mabaya."},{"id":6409,"sura":67,"from_aya":16,"to_aya":18,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"16. Je, mmesalimika kutokana na aliyeko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika! 17. Au mnadhani mko salama kutokana na aliyeko juu ya kuwa Yeye hatakupelekeeni kimbunga chenye changarawe? Basi mtajua vipi maonyo yangu? 18. Na bila ya shaka walikwisha kanusha wale waliokuwa kabla yao; basi kulikuwaje kukasirika kwangu? "},{"id":6410,"sura":67,"from_aya":16,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{16} Hili ni tishio na ahadi ya adhabu kwa anayeendelea na kupotoka kwake, kuvuka mipaka na uasi wake, ambao unamsababishia mateso na kufikiwa na adhabu. Akasema: \"Je, mmesalimika kutokana na aliyeko juu\" ambaye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, aliye juu ya viumbe vyake, \"kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika\" pamoja nanyi, na kuyumbayumba ili muangamie na mharibike kabisa?"},{"id":6411,"sura":67,"from_aya":17,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17 - 18} \"Au mnadhani mko salama kutokana na aliyeko juu ya kuwa Yeye hatakupelekeeni kimbunga chenye changarawe\" ili Mwenyezi Mungu akulipizeni kisasi? \"Basi mtajua vipi maonyo yangu?\" Yaani, mtajua namna yatavyokufikieni yale waliyokuhadharisheni Mitume na Vitabu? Kwa hivyo, msidhani kwamba kutawanufaisha kitu kusalimika kwenu kutokana na Mwenyezi Mungu ni kukuadhibuni kwa adhabu kutoka ardhini na kutoka mbinguni. Kwani mtapata mwisho wa mambo yenu ukiwa mbaya mno sawa muda wenu uwe mrefu au mfupi. Kwa maana wale waliokuwa kabla yenu walikadhibisha kama mlivyokadhibisha, kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaangamiza. Basi tazameni jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaonya. Aliwaharakishia adhabu ya duniani kabla ya adhabu ya Akhera. Basi jihadhari yasije yakakupateni yale yaliyowapata."},{"id":6412,"sura":67,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"19. Kwani hawawaoni ndege walioko juu yao namna wanavyozikunjua mbawa zao, na kuzikunja? Hawashikilii ila Mwingi wa rehema. Hakika Yeye ni Mwenye kuona mno kila kitu."},{"id":6413,"sura":67,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} Hii ni lawama na kuhimiza kuangalia hali ya ndege aliowatiisha Mwenyezi Mungu na akawatiishia anga na hewa. Wao hutandaza ndani yake mbawa zao ili waruke na wanazibana ili wasimame, basi hubaki wakipaa angani wakienda huku na kule ndani yake kulingana na mapenzi na mahitaji yao. \"Hawashikilii ila Mwingi wa rehema\" Yeye ndiye aliyewatiishia anga, na akaifanya miili yao na mbawa zao kuwa tayari kwa ajili ya kupaa. Kwa hivyo, mwenye kutazama hali ya ndege na kuizingatia, hilo litamwelekeza kwenye uwezo wa Muumba na uangalizi wake wa kiungu, na kwamba Yeye ni Mmoja na wa Pekee, ambaye haifai kuabudu isipokuwa Yeye. \"Hakika Yeye ni Mwenye kuona mno kila kitu.\" Yeye ndiye anayewaendesha waja wake kulingana na yale yanayowafailia na kulingana na hekima yake."},{"id":6414,"sura":67,"from_aya":20,"to_aya":21,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"20. Au ni lipi hilo jeshi lenu la kukunusuruni badala ya Mwingi wa Rehema? Hakika makafiri hawamo ila katika udanganyifu. 21. Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki yake? Bali wao wanakakamia tu katika jeuri na kujiweka mbali. "},{"id":6415,"sura":67,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaambia wale wanaoikataa amri yake na wakaiacha haki: \"Au ni lipi hilo jeshi lenu la kukunusuruni badala ya Mwingi wa Rehema\" ikiwa atakutakieni mabaya akawaondoleeni hayo? Yaani, ni nani atakayekusaidieni dhidi ya maadui zenu kando na Mwingi wa Rehema? Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anayesaidia, mwenye kutukuza na kufedhehesha. Na wasiokuwa Yeye miongoni mwa viumbe kama wangeungana pamoja ili kumsaidia mja, hawangemnufaisha kwa uzito wa chembe dhidi ya adui yeyote yule. Kwa hivyo, kuendelea kwa makafiri juu ya ukafiri wao baada ya kujua kwamba hakuna wa kuwanusuru isipokuwa Mwingi wa Rehema ni kudanganyika na ni upumbavu."},{"id":6416,"sura":67,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} \"Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki yake?\" Yaani, riziki zote zimetoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, kama akikunyimeni riziki, basi ni nani anayeweza kuiachilia ikawafikia? Kwa maana, viumbe hawana uwezo wa kujiruzuku. Basi vipi watawaruzuku wengine? Kwa hivyo, Mwenye kuruzuku, Mwenye kuneemesha, ambaye haiwafikii neema waja isipokuwa huwa imetoka kwake, ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake, lakini makafiri \"wanakakamia tu katika jeuri\" na kutolainika mbele ya haki \"na kujieka mbali\" na haki hiyo."},{"id":6417,"sura":67,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"22. Je, anayekwenda akisinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi, au yule anayekwenda sawasawa katika Njia iliyonyooka?"},{"id":6418,"sura":67,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} Yaani ni yupi kati ya wanaume hawa wawili ndiye aliyeongoka zaidi? Yule ambaye amepotelea katika upotofu na akazama katika ukafiri, moyo wake tayari umeshabadilika, kwa hivyo haki kwake ikawa ndiyo batili, nayo batili ikawa ndiyo haki, ama yule anayeijua haki, akaipendelea, akaifanyia kazi, na akawa anatembelea katika njia iliyonyooka katika maneno yake, matendo yake, na hali zake zote? Kwa kuangalia tu hali ya wanaume hao wawili, inajulikana tafauti baina yao na kujulikana yule aliyeongoka na aliyepotea. Na hali ni ushahidi mkubwa zaidi kuliko maneno."},{"id":6419,"sura":67,"from_aya":23,"to_aya":26,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"23. Sema: Yeye ndiye aliyekuumbeni tangu mwanzo, na akakupeni masikio na macho, na nyoyo. Ni kidogo kabisa shukrani zenu. 24. Sema: Yeye ndiye aliyekutawanyeni katika ardhi, na kwake mtakusanywa. 25. Na wanasema: Lini ahadi hii, ikiwa mnasema ukweli? 26. Sema: Hakika elimu ya hayo iko kwa Mwenyezi Mungu; na hakika mimi ni mwonyaji wa wazi tu mwenye kubainisha. "},{"id":6420,"sura":67,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akieleza kuwa Yeye pekee ndiye anayefaa kuabudiwa, na kuwalingania waja Wake kumshukuru na kumpwekesha katika ibada: \"Yeye ndiye aliyekuumbeni\" baada ya kutokuwa kwenu kitu; bila ya msaidizi yeyote, na alipokuumbeni, akakukamilishieni kuwepo kwenu kwa kuwapa uwezo wa kusikia, kuona, na mioyo. Na hivi vitatu ndivyo viungo bora kabisa vya mwili na nguvu kamili za mwili, lakini nyinyi pamoja na neema hizi, \"Ni kidogo kabisa shukrani zenu.\""},{"id":6421,"sura":67,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} \"Sema: Yeye ndiye aliyekutawanyeni katika ardhi\" katika maeneo yake, na akakuwekeni kuishi katika pande zake, na akawaamrisheni na akakukatazeni, na akakumiminieni neema mnazofaidika kwazo, kisha baada ya hayo atakukusanyeni Siku ya Kiyama, lakini ahadi hii ya kuwalipa wanaipinga watu hawa wakaidi."},{"id":6422,"sura":67,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} \"Na wanasema\" kwa njia ya kukadhibisha: \"Lini ahadi hii, ikiwa mnasema ukweli?\" Walifanya kuwaambia kwao wakati wa kuja kwake ati ndiyo alama ya ukweli wao, na hii ni dhuluma na ukaidi."},{"id":6423,"sura":67,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} Kwa maana \"hakika elimu ya hayo iko kwa Mwenyezi Mungu tu.\" Si kwa yeyote miongoni mwa viumbe vyote, na hakuna uhusiano wowote baina ya habari hii na kutoa kwao (Mitume) habari za kuja kwake. Kwa maana ukweli unajulikana kwa ushahidi wake, na tayari Mwenyezi Mungu ameshaweka ushahidi huo na uthibitisho wa usahihi wake ambao haiwezi kubakia shaka yoyote pamoja nao kwa yule  anayetega sikio naye yuko anashuhidia sawasawa."},{"id":6424,"sura":67,"from_aya":27,"to_aya":30,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"27. Lakini watakapoiona karibu, nyuso za wale waliokufuru zitahuzunishwa, na itasemwa: Hayo ndiyo mliyokuwa mkiyaomba mno. 28. Sema: Mwaonaje, ikiwa Mwenyezi Mungu ataniangamiza mimi na wale walio pamoja nami, au akiturehemu, ni nani atakayewalinda makafiri mbali na adhabu chungu? 29. Sema: Yeye ndiye Mwingi wa Rehema; tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea. Basi mtakuja jua ni nani aliye katika upotovu ulio dhahiri. 30. Sema: Mwaonaje, yakiwa maji yenu yamedidimia chini, ni nani atakueleteeni maji yanayomiminika? "},{"id":6425,"sura":67,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} Maana yake ni kwamba mahali walipokanushwa makafiri na wakadanganyika napo ni wakati walipokuwa katika dunia hii. Lakini itakapofika Siku ya Malipo, wataiona adhabu \"karibu\" sana nao, na hilo litawahuzunisha, kuwatisha mno na kuwatia wasiwasi, na nyuso zao zitabadilika kwa sababu yake, na watakemewa kwa sababu ya kukanusha kwao, na wataambiwa: \"Hayo ndiyo mliyokuwa mkiyaomba mno.\" Leo mmeiona kwa macho yenu, na jambo hilo limekwisha kubainikieni wazi, na njia za mahusiano zenu zimeshakukatikieni, na hakikubakia isipokuwa kuikabili adhabu."},{"id":6426,"sura":67,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Na kwa vile wale waliomkadhibisha Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - wale walioukataa wito wake wanamngojelea kuangamia, na wanamtarajia kupatilizwa na siku zinaposonga, Mwenyezi Mungu akamwamrisha kuwaambia: 'Hakika nyinyi hata kama matamanio yenu yatatimia, na \"Mwenyezi Mungu akaniangamiza mimi na wale walio pamoja nami\" hilo halitakuwa na faida yoyote kwenu. Kwa sababu mlizikufuru Aya za Mwenyezi Mungu, na mkastahiki adhabu. Basi ni nani atakayekuepusheni \"mbali na adhabu chungu\" ambayo tayari imeshakuwa lazima itakufikieni. Kwa hivyo, juhudi zenu na hamu yenu kubwa ya kuona nikiangamia haina faida yoyote kwenu."},{"id":6427,"sura":67,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} Na kutokana na kusema kwao: 'Hakika wao wako kwenye uwongofu, naye Mtume amepotea' na wakairudia na kuiendeleza, na wakajadili juu yake na wakapigana vita. Basi Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kuwajulisha kuhusu hali yake na hali ya wafuasi wake, ambayo kwayo uwongofu wao na uchamungu wao utadhihirika kwa kila mtu, ambayo ni kwamba waseme, \"tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea.\" Na imani inajumuisha kusadiki kwa ndani na matendo ya ndani na nje. Na kwa kuwa kupatikana kwa matendo na ukamilifu wake kunasimama juu ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akachagua suala la kumtegemea kati ya matendo mengine yote. Vinginevyo, huko pia kunaingia katika imani, na ni miongoni mwa mahitaji yake, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: \"Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini.\" Kwa hiyo, ikiwa hii ndiyo hali ya Mtume na hali ya waliomfuata, nayo ndiyo hali inayotakiwa ili mtu afaulu na kupata furaha kunategemea juu yake, na hali ya maadui zake ni kinyume chake, kwani wao hawana imani wala kumtegemea Mwenyezi Mungu, basi kwa hilo inajulikana ni nani yuko kwenye uwongofu na ni nani yuko katika upotofu ulio wazi."},{"id":6428,"sura":67,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} Kisha akajulisha kwamba Yeye tu ndiye mwenye neema zote, hasa maji ambayo kwayo Mwenyezi Mungu aliumba kila kiumbe kilicho uhai, akasema: \"Sema: Mwaonaje, yakiwa maji yenu yamedidimia chini, ni nani atakueleteeni maji yanayomiminika,\" ambayo kwayo mtakunywa na kuwanywesha mifugo wenu, miti yenu na mimea yenu? Huku ni kuuliza kwenye maana ya kukanusha. Yaani, hakuna awezaye kufanya hivyo isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu tu."},{"id":6429,"sura":67,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri ya surat Al-Mulk, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu."}]}