{"result":[{"id":6502,"sura":70,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya surat Al-Ma'arij"},{"id":6503,"sura":70,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":6504,"sura":70,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu."},{"id":6505,"sura":70,"from_aya":1,"to_aya":7,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea. 2. Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia. 3.  Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. 4. Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka hamsini elfu! 5. Basi subiri kwa subira njema. 6. Hakika wao wanaiona iko mbali. 7. Na Sisi tunaiona iko karibu. "},{"id":6506,"sura":70,"from_aya":1,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1 - 4} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akielezea ujinga wa watu wenye ukaidi na kuharakisha kwao adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuifanyia kejeli, usugu, na kuona kwamba wanaweza kumshinda Mwenyezi Mungu: \"Muulizaji aliuliz juu ya adhabu itakayotokea. Kwa makafiri \" kwa sababu walistahiki kuipata kwa ukafiri wao na ukaidi wao. \"ambayo hapana awezaye kuizuia\" kabla ya kuteremka kwake au hata kuiondoa baada ya kushuka kwake. Haya yalikuwa wakati An-Nadhr bin Al-Harith Al-Qurashi au mwengineye miongoni mwa wakaidi alipoomba: \"Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ni kweli itokayo kwako basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tuletee adhabu yoyote iliyo chungu...\" hadi mwisho wa aya hizi. Lakini adhabu hii ni lazima itawapata kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ima wataharakishiwa katika dunia hii, au wataekewa waipate huko Akhera. Na lau wangemjua Mwenyezi Mungu na kujua ukuu wake, upana wa mamlaka yake, na ukamilifu wa majina na sifa zake, basi hawangeharakisha, na wangejisalimisha kwake na wakawa na adabu ipasayo, ndiyo maana Mola Mtukufu akataja katika utukufu wake yale yanayopingana na hayo maneno yao machafu, akasema: \"Mwenye mbingu za daraja. Malaika na Roho hupanda kwenda kwake.\" Yaani: Mwenye ujuu, utukufu, ukuu, na uendeshaji wa viumbe vyote, ambaye Malaika hupanda kwake kutokana na yale aliyoyawekea kusimamia, na pia Roho hupanda kwake. Na jina hili ni jina jumuishi linalojumuisha roho zote; njema na ovu, na hili huwa wakati wa kufa. Ama walio wema, roho zao hupanda kwa Mwenyezi Mungu, na huwapa idhini ya kupita kutoka mbingu kwenda mbingu nyingine, mpaka zifike katika mbingu ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu yuko huko, kisha zinamsalimu Mola wao Mlezi na ninapata fursa ya kuwa karibu naye na kufurahia hilo, kisha zinasifiwa, kutukuzwa, kuwanyiwa wema na kuheshimiwa. Na ama zilizo ovu, hizo hupanda, na zinapofika katika mbingu ya kwanza, zinaomba idhini ya kuingia, lakini haziruhusiwi, kisha zinarudishwa katika ardhi. Kisha akataja umbali ambao Malaika na Roho hupanda ndani yake wakienda kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba wao hupanda katika siku moja kwa sababu ya jinsi alivyowarahisishia na kuwasaidia kuwa wepesi na wa mwendo wa kasi kubwa sana, pamoja na kwamba umbali huu katika safari ya kawaida ni sawa na miaka elfu hamsini, tangu mwanzo wa kupaa hadi kufika kwao pale kwenye kiwango walichowekewa, na pale wanapofikia katika viumbe watukufu wa juu zaidi. Basi ufalme huu mkuu na ulimwengu mkubwa, wa juu wake wote na wa chini wake wote anausimamia Mtukufu aliye juu zaidi. Anazijua hali zao za dhahiri na zilizofichikana, [na anajua] pahali pa kutulia na pa kupita njia, na anawafikishia rehema zake, wema wake na ihsani yake, ambavyo vinawajumuisha wote, na akatekeleza juu yao hukumu yake kulingana na mipango yake, hukumu yake ya kisheria na hukumu yake ya kimalipo. Basi wana taabu wale ambao hawakujua ukuu wake na hawakumheshimu kama alivyostahili, kwa hivyo wakaharakisha adhabu kwa njia ambayo walimfanya Mwenyezi Mungu kwamba hana uwezo na kumjaribu tu. Na ametakasika, Mwingi wa ustahamilivu, ambaye aliwapa muhula na hakuwapuuza, na wakamuudhi, lakini akawafanyia subira, akawapa salama na akawaruzuku! Huu ni uwezekano mmojawapo katika kufasiri Aya hii tukufu. Kwa hivyo kupanda huku kunakuwa ni duniani, kwa sababu muktadha wa kwanza unalionyesha hilo. Na inawezekana kwamba hii ni Siku ya Kiyama, na kwamba Mwenyezi Mungu [Mwenye baraka nyingi] Mtukufu atawadhihirishia waja wake Siku ya Kiyama ukuu wake, utukufu wake na ukubwa wake, ambavyo vitakuwa ni ushahidi mkubwa zaidi juu ya kujua kwake kutokana na watakayoyaona miongoni mwa kupanda kwa Malaika na roho, kupanda na kushuka kulingana na mipango ya Mwenyezi Mungu siku hiyo, ambayo kipimo chake ni miaka elfu hamsini kwa sababu ya urefu wake na ukali wake, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ataihafifisha kwa Muumini."},{"id":6507,"sura":70,"from_aya":5,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5 - 7} Na kauli yake: \"Basi subiri kwa subira njema\" juu ya wito wako kwa watu wako bila ya kulalamika wala kuchoka. Bali endelea na amri ya Mwenyezi Mungu, na waite waja wake kumpwekesha, wala kisikuzuie kile unachokiona cha kukosa kwao utii na kutotaka kwao. Kwani kuna mazuri mengi katika kuwa na subira juu ya hilo. \"Hakika wao wanaiona iko mbali. Na Sisi tunaiona iko karibu.\" Hapa kinachokusudiwa ni ufufuo ambamo ndani yake kuna adhabu ya hao wanaoomba adhabu. Yaani, hali yao ni hali ya mwenye kukanusha hilo, na ni hali ya yule aliyeshindwa na upotofu na ulevi, mpaka yaliyo mbele yake ya kufufuliwa na kutawanyika yakamuwiya mbali mno, ilhali Mwenyezi Mungu anayaona kuwa yako karibu mno. Kwa sababu Yeye ni Mpole, Mstahamilivu, na anajua kwamba ni lazima yatatokea, na [kila] kinachokuja, kiko karibu."},{"id":6508,"sura":70,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"Kisha akataja mahangaiko ya siku hiyo na yale yatakayotokea ndani yake, akasema:"},{"id":6509,"sura":70,"from_aya":8,"to_aya":18,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"8. Siku ambayo mbingu zitakapokuwa kama maadeni iliyoyayushwa. 9. Na milima itakuwa kama sufi. 10. Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. 11. Ijapokuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe. 12. Na mkewe, na nduguye. 13. Na jamaa zake waliokuwa wakimkimu, 14. Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. 15. La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, 16. Unaobambua ngozi ya kichwa! 17. Utamwita kila aliyegeuza mgongo na akageuka. 18. Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. "},{"id":6510,"sura":70,"from_aya":8,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8 - 9} \"Siku\" yaani siku ya Kiyama ambayo yatatokea mambo makubwa haya, \"mbingu zitakapokuwa kama maadeni iliyoyayushwa\" kutokana na kupasuka kwake na kufikiwa na balaa kubwa zaidi. \"Na milima itakuwa kama sufi.\" Kisha baada ya hilo vitakuwa kama mavumbi yaliyotawanywa na kupotelea mbali."},{"id":6511,"sura":70,"from_aya":10,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10 - 14} Ikiwa usumbufu na wasiwasi huu utaipata miili hii mikubwa, migumu, basi je, unamwonaje mja dhaifu ambaye ameuelemesha mgongo wake kwa madhambi na mizigo? Je, si kweli kwamba unafailia zaidi moyo wake kukatikakatika [kusumbukana mno], na kujitenga mbali na kila mtu? Ndiyo maana akasema: \"Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. Ijapokuwa wataonyeshwa waonane.\" Lakini hakutakuwa na nafasi iliyobaki moyoni mwake kumuuliza kuhusu hali yake au ni nini kinachohusiana na usuhuba wao na mapenzi yao, na hatajali isipokuwa yeye mwenyewe tu. \"Atatamani mkosefu\" ambaye alistahiki kuadhibiwa angependa \"lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe. Na mkewe, na nduguye. Na jamaa zake waliokuwa wakimhifadhi\" na kusaidiana wao kwa wao. Lakini siku ya Kiyama, hakuna atakayemnufaisha mwingine, na hakuna atakaemfayia uombezi mwingine isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Bali hata kama mhalifu anayestahili adhabu angejifidia kwa mali zote za duniani ili ajikomboe kutokana na adhabu kisha aokoke yeye, hilo halitamnufaisha kitu."},{"id":6512,"sura":70,"from_aya":15,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15 - 18} \"La!\" Yaani, hakuna hila wala pahali pa kukimbilia, kwani neno la Mola wako Mlezi limeshawafikia, na manufaa ya jamaa na marafiki yametoweka pia. \"Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa. Unaombabua ngozi ya kichwa\" na viungo vinginevyo vinavyoonekana na vilivyofichikana. \"Utamwita kila aliyegeuza mgongo na akageuka\" na akaacha haki. \"Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi\" bila ya kutoa chochote kwayo kile ambacho kingemfaa au kumkinga kutokana na Moto. Basi Moto huo unawaita watu hawa kuuendea, na unajitayarisha kuwaunguza."},{"id":6513,"sura":70,"from_aya":19,"to_aya":35,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"19. Hakika mtu ameumbwa na papara. 20. Inapomgusa shari hupapatika. 21. Na inapomgusa kheri huizuilia. 22. Isipokuwa wanaosali, 23. Ambao wanadumisha Sala zao, 24. Na ambao katika mali yao iko haki maalumu. 25. Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba; 26. Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo. 27. Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. 28. Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. 29. Na ambao wanahifadhi tupu zao. 30. Isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi. 31. Lakini wanaotaka kinyume cha haya, basi hao ndio wanaoruka mipaka. 32. Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, 33. Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, 34. Na ambao wanazihifadhi Sala zao. 35. Hao ndio watakaoheshimiwa Peponi. "},{"id":6514,"sura":70,"from_aya":19,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19 - 21} Haya ni maelezo ya mwanadamu jinsi alivyo; ameielezea hali yake [ya asili] kuwa ni mwenye papara, na akaeleza papara hiyo kwa kusema: \"Inapomgusa shari hupapatika.\" Huingiwa na papara iwapo utampata umasikini au maradhi, au kutoweka kwa mpendwa kama vile mali zake, familia, au mtoto, na wala hafanyi subira na kutosheka kwa yale aliyoyaandikia Mwenyezi Mungu katika hayo. \"Na inapomgusa kheri huizuilia.\" Hatoi katika alichompa Mwenyezi Mungu, wala hamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema na wema wake. Yeye hufanya papara wakati wa shida na hunyimana katika nyakati nzuri."},{"id":6515,"sura":70,"from_aya":22,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22 - 23} \"Isipokuwa wanaosali\" wale walioelezwa kwa maelezo hayo; ikiwa wema utawagusa; wanamshukuru Mwenyezi Mungu na wakatoa katika yale aliyowaruzuku. Na unapowafikia ubaya, wao huwa na subira na kutarajia malipo. Na kauli yake katika kuwaeleza: \"Ambao wanadumisha Sala zao\" kwa wakati wake uliowekwa, pamoja na masharti yake na vyote vya kuikamilisha, na si kama mtu asiyeifanya, au anayeifanya kwa wakati fulani tu, au kuifanya kwa njia pungufu."},{"id":6516,"sura":70,"from_aya":24,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24 - 25} \"Na ambao katika mali yao iko haki maalumu\" kama vile Zaka na sadaka. Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba\" ambaye hata hapewi sadaka."},{"id":6517,"sura":70,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} \"Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo.\" Yaani, wanaamini yale waliyoambiwa na Mitume ya malipo na ufufuo, na wana yakini nayo, kwa hivyo wanajitayarisha kwa ajili ya Akhera, na wanaifanyia bidii ipasavyo. Na kusadiki Siku ya Kiyama kunahitaji kuwasadiki Mitume na vitabu walivyokuja navyo."},{"id":6518,"sura":70,"from_aya":27,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27 - 28} \"Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi.\" Kwa hivyo wanaacha kwa sababu ya hilo kila kitu ambacho kitawaleta karibu na adhabu ya Mwenyezi Mungu. \"Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo.\" Kwa hivyo inapasa kuogopewa na kujitahadharisha nayo."},{"id":6519,"sura":70,"from_aya":29,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29 - 31} \"Na ambao wanahifadhi tupu zao.\" Kwa hivyo, hawaziingizi katika tendo la ndoa la haramu, kama vile zinaa, kulawiti, kujamiiana katika njia ya haja kubwa, au katika hedhi na mfano wake, na pia wanazilinda asimwangalie au kumgusa yule ambaye hairuhusiwi kwake kufanya hivyo, na pia wanaziacha njia zilizoharamishwa zinazoitia kufanya uchafu, \"isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume\" yaani masuria wao. \"Basi hao hawalaumiwi\" kwa kujamiiana nao katika mahali panaporuhusiwa. \"Lakini wanaotaka kinyume cha haya;\" yaani, mwenye kutafuta asiyekuwa mkewe au masuria wake, \"basi hao ndio wanaoruka mipaka\" ya yale aliyoyaruhusu Mwenyezi Mungu na wakaingia katika yale aliyoharamisha. Aya hii inaashiria kuharamishwa kwa ndoa ya muda (Mut'a). Kwa sababu yeye hakukusudiwa kuoelewa na kukaa naye kama mke wala si suria aliyemilikiwa na mkono wake wa kulia."},{"id":6520,"sura":70,"from_aya":32,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32} \"Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao\" na wana bidii katika kuzitekeleza kikamilifu. Hili linajumuisha amana zote zilizo baina ya mja na Mola wake Mlezi, kama vile majukumu ya kisiri ambayo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeyajua tu, na amana zilizoko baina ya mja na viumbe kuhusiana na mali na siri mbalimbali. Na agano linajumuisha agano ambalo alimpa Mweyezi Mungu na agano alilowapa viumbe. Kwa maana, mja ataulizwa juu ya agano,  je alilitimiza kikamilifu au alilikataa na akalifanyia uhaini na akaacha kulitekeleza?"},{"id":6521,"sura":70,"from_aya":33,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33} \"Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao.\" Yaani,   wanashuhudia tu yale wanayoyajua, bila ya kuongeza, kupunguza, wala kuficha, na wala hawampendelei katika hilo jamaa, rafiki wala mfano wa hao, na makusudio yao katika kuufanya ni kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.\" Na akasema \"Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha mno uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu.\""},{"id":6522,"sura":70,"from_aya":34,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34} \"Na ambao wanazihifadhi Sala zao\" kwa kudumu katika hilo kwa njia kamilifu zaidi."},{"id":6523,"sura":70,"from_aya":35,"to_aya":35,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35} \"Hao\" walioelezewa kwa sifa hizo, \"ndio watakaoheshimiwa Peponi.\" Yaani, Mwenyezi Mungu ameshawafikishia utukufu na neema ya milele, miongoni mwa yale ambayo nafsi zinayapenda na macho yanayafurahia, na wao watakaa humo milele. Jumla ya haya ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwaeleza watu wa furaha na wema kwa maelezo haya kamili na maadili ya kuridhisha na yaliyo bora kama vile ibada za kimwili, kama vile sala, kudumu katika kuitekeleza, na matendo ya kimoyo, kama vile kumcha Mwenyezi Mungu, ambako kunaitia katika wema wote, ibada za kimali, itikadi zenye manufaa, na kuamiliana na Mwenyezi Mungu na viumbe vyake kwa njia bora zaidi, kama vile kuwafanyia uadilifu, kuhifadhi haki zao na amana zao, na usafi kamili kwa kulinda sehemu za siri kutokana na yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu Mtukufu."},{"id":6524,"sura":70,"from_aya":36,"to_aya":39,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"36. Wana nini wale waliokufuru wanakutumbulia macho tu? 37. Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! 38. Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? 39. La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanachokijua. "},{"id":6525,"sura":70,"from_aya":36,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{36 - 39} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akieleza kudanganyika kwa makafiri: \"Wana nini wale waliokufuru wanakutumbulia macho tu?\" Na pia ilisemwa kwamba maana yake ni wanakukimbilia. \"Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto!\" Kila mmoja na furahia yale aliyo nayo. \"Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema?\" Ni sababu gani iliwapa matumaini hayo ilhali hawakutanguliza ila ukafiri na kukataa Mola Mlezi wa walimwengu wote? Ndiyo maana akasema: \"La, hasha!\" Mambo si hivyo tu kwa matamanio yao, wala hawawezi kupata wanayoyatamani kwa uwezo wao. \"Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanachokijua.\" Yaani, kutokana na maji yatokayo kwa kuchupa. Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.\" Kwa hivyo, wao ni dhaifu ambao hawawezi kujimilikia manufaa wala madhara, wala kifo, wala uzima, wala ufufuo."},{"id":6526,"sura":70,"from_aya":40,"to_aya":44,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"40. Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza. 41. Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi. 42. Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayoahidiwa, 43. Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo, 44. Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyokuwa wakiahidiwa. "},{"id":6527,"sura":70,"from_aya":40,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40 - 41} Huku ni kuapa kwake Yeye Mtukufu kwa mashariki na magharibi za jua, mwezi na nyota; kwa sababu ya ishara zenye kung'aa zilizo ndani yake kuhusiana na ufufuo na uwezo wake wa kuwabadili kwa mfano wao wenyewe, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: \"Na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilolijua.\" Na akasema \"na Sisi hatushindwi\" tukitaka kumrudisha."},{"id":6528,"sura":70,"from_aya":42,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42} Basi likishakuwa wazi suala la kufufuliwa na kulipwa, na wakaendelea katika kukanusha na kutotii kwao ishara za Mwenyezi Mungu. \"Basi waache wapige porojo na wacheze\" kwa maneno batili na itikadi potofu, na waichezee dini yao, na wale, na wanywe na wastarehe, \"mpaka wakutane na siku yao wanayoahidiwa.\" Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia humo adhabu na balaa kubwa itakayokuwa matokeo ya kuzama kwao katika porojo na kucheza kwao."},{"id":6529,"sura":70,"from_aya":43,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{43 - 44} Kisha akataja hali ya viumbe wanapokutana na siku waliyoahidiwa, akasema: \"Siku watakapotoka makaburini kwa upesi\" kwa kuitikia mwito wa mwitaji, kuyakimbilia, \"kama kwamba wanakimbilia mfundo.\" Hawataweza kukataa kumwendea mwitaji huyo wala hata kukengeuka mbali naye. Bali wanakuja huku wamedhalilika na wametiishwa ili wasimame mbele ya Mola Mlezi wa walimwengu wote. \"Macho yao yatainama, fedheha itawafunika.\" Haya ni kwa sababu ya unyonge na wasiwasi kubwa itakayokuwa imezitawala nyoyo zao na kuzitawala fahamu za nyoyo zao, kwa hivyo macho yao yakanyenyekea, harakati zao zikatulia, na sauti zao zikakatika. Hali hii na mwisho huu ndio siku yao \"waliyokuwa wakiahidiwa.\" na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni lazima itimie."},{"id":6530,"sura":70,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu."}]}