{"result":[{"id":6617,"sura":74,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Al-Muddaththir"},{"id":6618,"sura":74,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":6619,"sura":74,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":6620,"sura":74,"from_aya":1,"to_aya":7,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Ewe uliyejigubika! 2. Simama uonye! 3. Na Mola wako Mlezi mtukuze! 4. Na nguo zako, zisafishe. 5. Na yaliyo machafu yahame! 6. Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa. 7. Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri! "},{"id":6621,"sura":74,"from_aya":1,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1 - 2} Hapo awali ilitajwa kuwa al-Muzzammil na al-Muddaththir ni maneno yenye maana sawa, na kwamba Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - afanye bidii katika ibada zinazomfaa yeye tu na zile za kuwafaa wengine pia. Basi ikatangulia hapo awali kwamba ameamrishwa kufanya ibada bora zaidi zenye kumfaa yeye tu na kuwa na subira na juu ya maudhi ya watu wake, na hapa akamuamuru kutangaza wito wake na kutoa onyo waziwazi. Kwa hivyo akasema: \"Simama\" kwa bidii na kwa ukakamavu \"uonye\" watu kwa kauli na vitendo vinavyofanikisha yaliyokusudiwa na pia kubainisha hali ya kile kinachoonywa juu yake, ili hilo liitie zaidi kuachana nalo."},{"id":6622,"sura":74,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} \"Na Mola wako Mlezi mtukuze\" kwa kumpwekesha, na uyafanye makusudio yako katika maonyo yako kuwa ni uso wa Mwenyezi Mungu na kwamba waja wamtukuze na wamuabudu."},{"id":6623,"sura":74,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} \"Na nguo zako, zisafishe.\" Inawezekana kwamba kinachokusudiwa nguo hapa ni matendo yake yote. Na kwamba kuyasafisha ni kuyatakasa na kumsafia Mwenyezi Mungu ndani yake, na kuyatekeleza kwa namna iliyo kamilifu kabisa, na kuyatakasa kabisa mbali na yale yanayoyabatilisha, ya kuyaharibu na yenye kuyapunguza kama vile ushirikina, kujionyesha, unafiki, kiburi, kughafilika na mengineyo miongoni mwa yale ambayo mja ameamrishwa kuepukana nayo katika ibada yake, na hili linajumuisha kutakasa nguo kutokana na najisi. Kwani hilo ni katika mambo yanayosababisha utakaso kamili wa matendo hasa katika swala ambayo wanavyuoni wengi wamesema kuwa kuondoa najisi ni miongoni mwa masharti yake. Na inawezekana kwamba kinachomaanishwa hapa na nguo zake ni nguo zinazojulikana, kwamba ameamrishwa kuzitakasa mbali na najisi kila wakati, haswa wakati wa kuingia katika swala."},{"id":6624,"sura":74,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} Ikiwa ameamriwa kuwa safi kwa nje, basi ni kwa sababu usafi wa nje ni katika utimilifu wa usafi wa ndani: \"Na yaliyo machafu yahame!\" Inawezekana kwamba kinachokusudiwa na uchafu ni masanamu na vyote vinavyoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo akamuamuru kuyaacha na kujiweka mbali nayo, na yote yaliyonasibishwa nayo kama vile maneno au matendo. Na inawezekana kwamba kinachomaanishwa na uchafu ni matendo na maneno yote maovu, kwa hivyo hii inakuwa amri anayoamrishwa kuacha madhambi, madogo na makubwa, ya dhahiri na yaliyofichikana, kwa hivyo inaingia katika hilo ushirikina na yaliyo chini yake."},{"id":6625,"sura":74,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} \"Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa.\" Yaani, usiwape watu neema za kidini na za kidunia ulizowaneemesha kwazo ili uzidishiwe kwa kuneemesha huko. Bali wafanyie wema watu uwezavyo na usahau wema wako kwao, na utafute malipo yako kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wafanye sawa yule uliyemneemesha na yule ambaye hukumneemesha. Na imesemwa kwamba maana yake ni kuwa usimpe mtu kitu ilihali unataka akulipe zaidi ya hicho kitu, basi hili linakuwa ni mahususi kwa Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie."},{"id":6626,"sura":74,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} \"Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!\" Yaani, tarajia malipo ya Mwenyezi Mungu kwa subira yako na uukusudie kwa hilo uso wa Mwenyezi Mungu. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu \u2013  rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie \u2013 akatekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na akachukua hatua ya haraka kufanya hivyo na akawaonya watu wote kwa ishara zilizo wazi juu ya mambo yote ya Mwenyezi Mungu, na akamtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu, akavitaka viumbe vimtukuze, akatakasa vitendo vyake vya nje na vilivyofichikana kutokana na ubaya wote, na akaacha kila kitu kilichoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, na vile vinavyoabudiwa pamoja naye kama vile masanamu na watu wake, na uovu na watu wake. Basi anafaa kupata fadhila kwa hilo baada ya fadhila za Mwenyezi Mungu, bila ya kuwaomba malipo kwa hilo wala shukurani, na akasubiri kwa ajili ya Mola wake Mlezi subira iliyokamilika zaidi. Alikuwa na subira juu ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, na kujiepusha mbali na maasi, na akawa na subira juu ya mipango ya michungu ya Mwenyezi Mungu mpaka akawapiku Mitume wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume. Basi rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na juu yao wote."},{"id":6627,"sura":74,"from_aya":8,"to_aya":10,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"8. Basi litakapopulizwa barugumu, 9. Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu. 10. Kwa makafiri haitakuwa nyepesi. "},{"id":6628,"sura":74,"from_aya":8,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8 - 10} Yaani, linapopulizwa baragumu la kufufuka kutoka makaburini, na viumbe vinakusanywa kwa ajili ya kufufuliwa na kutawanywa. \"Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu\" kwa sababu ya wingi wa mahangaiko na dhiki zake. \"Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.\" Kwa sababu watakata tamaa na wema wote na watakuwa na yakini ya maangamio. Maana yake isiyokuwa na moja kwa moja ni kuwa siku hiyo itakuwa rahisi kwa waumini. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: \"Na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.\""},{"id":6629,"sura":74,"from_aya":11,"to_aya":31,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"11. Niache peke yangu na niliyemuumba. 12. Na nikamjaalia awe na mali mengi. 13. Na wana wanaoonekana. 14. Na nikamtegenezea mambo vizuri kabisa. 15. Kisha anatumai nimzidishie! 16. Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu! 17. Nitamtesa kwa mateso yasiowezekana. 18. Kwani hakika yeye alifikiri na akapima. 19. Basi ameangamia! Vipi alivyopima! 20. Tena ameangamia! Vipi alivyopima! 21. Kisha akatazama. 22. Kisha akakunja kipaji, na akanuna. 23. Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari. 24. Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa. 25. Haya si chochote ila kauli ya binaadamu. 26. Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar. 27. Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? 28. Haubakishi wala hausazi. 29. Unababua ngozi iwe nyeusi. 30. Juu yake wapo kumi na tisa. 31. Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha waliokufuru, wapate kuwa na yakini waliopewa Kitabu, na wazidi Imani wale walioamini, wala wasiwe na shaka waliopewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndiyo kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anayejua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu. "},{"id":6630,"sura":74,"from_aya":11,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11 - 30} Aya hizi ziliteremshwa kuhusu Al-Walid bin Al-Mughirah, ambaye alikuwa mkaidi dhidi ya haki, na ambaye alisimama kukabiliana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kupigana naye na kumpinga. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamkashifu kwa kashfa ambayo hakuwahi kumkashifu mwingineye. Na haya ndiyo malipo kwa wote wanaoikaidi haki na kupingana nayo; kwamba atapata hizaya katika dunia, na tena adhabu ya Akhera ni ya kufedhehesh zaidi. Akasema: \"Niache peke yangu na niliyemuumba\" Yaani: Nilimuumba peke yake, bila ya mali, familia, wala mtu mwingine yeyote. Basi nikaendelea kumlea na kumpa, na nikamjaalia  \"awe na mali nyingi na\" pia nikamfanyia kuwa na \"wana\" wa kiume \"wanaoonekana\" Yaani: waliopo pamoja naye daima, anawafurahia, hutimiza haja zake kupitia kwa hao, na kutafuta msaada kupitia kwao \"Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa\" katika dunia na sababu zake mpaka yakatekelezeka mambo anayotafuta na kutamani. \"Kisha\" pamoja na neema hizi na hivi vyote alivyopewa \"anatumai nimzidishie!'  Yaani anatazamia kupata neema za Akhera kama alivyozipata neema za dunia. \"Hasha!\" Yaani jambo hili si kama alivyokuwa akitaka, bali ni kinyume na aliyoyakusudia na kuyataka. Na hayo ni \"kwa sababu hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!\" Alizijua kisha akazikanusha, na zikamwita kwenye haki, lakini hakunyenyekea kwazo, na bado haikumtosha kujiepusha nazo na kuzipa mgongo. Bali alianza kupigana nao vita na kujitahidi kuzibatilisha, na ndiyo maana akasema juu yake: \"Kwani hakika yeye alifikiri\" ndani ya nafsi yake \"na akapima\" kile alichofikiria ili aseme kauli atakayoibatilisha Qur-ani kwayo. \"Basi ameangamia! Vipi alivyopima! Tena ameangamia! Vipi alivyopima!\"  Kwa sababu alipima kitu kisichokuwa ndani ya upeo wake, na akajiingiza katika kile ambacho yeye wala mfano wake hawawezi kukifikia. \"Kisha akatazama\" cha kusema \"kisha akakunja kipaji, na akanuna\" ili kuikimbia kuichukia haki. \"Kisha akaipa kisogo haki\" na akaenda zake \"na akatakabari\" hili likiwa ni matokeo ya juhudi zake za kiakili, kivitendo na kwa maneno. \"Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa. Haya si chochote ila kauli ya binadamu.\" Yaani, haya si maneno ya Mwenyezi Mungu. Bali ni maneno ya wanadamu, na pia si maneno ya wanadamu wema, bali ni maneno ya waovu miongoni mwao na wasiomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa kila mwongo na mchawi, basi naangamie! Jinsi gani alivyo mbali mno zaidi na usahihi! Na ni mwenye kustahili zaidi vipi hasara na kuangamia! Je, inawezaje kuingia katika akili ya mtu yeyote au kufikiriwa na dhamiri ya mtu yeyote kwamba maneno ya juu kabisa na makuu zaidi, maneno ya Mola Mlezi, Mtukufu, Mwenye heshima, Mkuu kwamba yanafanana na maneno ya viumbe maskini, wapungufu?! Au huyu mwongo mkaidi anathubutu vipi kuelezea maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa maelezo haya? Hastahiki chochote ila adhabu kali [na mateso mazito], na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: \"Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar. Na ni nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? Haubakishi wala hausazi\" mwenye kuadhibiwa. \"Unababua mno ngozi iwe nyeusi.\" Yaani, unawababua na kuwaingiza mno katika adhabu yake, na unawatia wasiwasi kwa ukali wa joto lake na baridi yake kali. \"Juu yake wapo kumi na tisa\" miongoni mwa Malaika, wasimamizi wake, wakali na wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu katika anayowaamrisha na wanafanya wanayoamrishwa."},{"id":6631,"sura":74,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} \"Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika\" kwa sababu ya ukali wao na nguvu zao. \"Wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha waliokufuru.\" Inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapa ni 'isipokuwa kwa ajili wawaadhibu huko Akhera humo motoni na kuwazidishia humo adhabu. Adhabu pia inaitwa fitna (majaribio); kama alivyosema Mwenyezi Mungu: \"Hiyo ni siku watakayoadhibiwa Motoni.\" Inawezekana kuwa kinachomaanishwa hapa ni kwamba hatukukuambieni juu ya idadi yao isipokuwa ili tujue ni nani anayesadiki na ni nani anayekadhibisha. Haya yanaonyeshwa na yale aliyoyataja baada yake katika kauli yake: \"wapate kuwa na yakini wale waliopewa Kitabu, na wazidi Imani wale walioamini.\" Kwa maana, Watu wa Kitabu ikiwa haya yataafikiana na yale waliyo nayo na yakalingana, yakini yao juu ya haki inaongezeka. Nao Waumini kila Mwenyezi Mungu anapoteremsha Aya, wakaiamini na kuisadiki, imani yao inaongezeka. \"Wala wasiwe na shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini.\" Yaani, ili hilo liwaondoshee shaka na kusitasita. Na haya ni malengo makubwa wanayoyachunga mno wenye akili, ambayo ni kujitahidi kuwa na yakini na kuzidisha imani kila wakati na katika kila suala la dini, na kuondosha shaka na fikira potofu zinazojitokeza katika kukabiliana na haki. Basi akayafanya yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake kuwa ni yenye kufanikisha malengo haya makubwa, na yenye kupambanua wakweli mbali na waongo, na ndiyo maana akasema: \"Na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao.\" Yaani, maradhi ya shaka, dhana na unafiki \"na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu?\" Haya ni katika njia ya kuchanganyikiwa na shaka kwa upande wao na kukufuru ishara za Mwenyezi Mungu. Na hili na lile ni sehemu katika kuongoa kwa Mwenyezi Mungu yule ambaye amemuongoa na upotoshaji  wake kwa yule ambaye anampoteza, na ndiyo maana akasema: \"Ndiyo kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye.\" Kwa hivyo yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, anayafanya yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake kuwa ni rehema kwake na kuzidisha imani yake na dini yake, Na yule ambaye amempotosha, anayafanya yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake kuwa ni kuzidisha upotofu juu yake, mkanganyiko na giza kwa upande wake. \"Na hapana yeyote anayejua majeshi ya Mola wako Mlezi\" miongoni mwa Malaika na wengineo \"ila Yeye tu.\" Basi ikiwa nyinyi hamjui majeshi yake, na amekujulisheni hayo Mjuzi mno, Mwenye habari zote, basi lazima muamini habari zake bila ya shaka yoyote wala kusitasita. \"Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binadamu.\" Wala hayakukusudiwa mawaidha haya na ukumbusho kuwa ni upumbavu na mchezo. Bali kilichokusudiwa kwayo ni watu kukumbuka yale yanayowanufaisha, wakayafanya, na yale yanayowadhuru, basi wakayaacha."},{"id":6632,"sura":74,"from_aya":32,"to_aya":56,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"32. Hasha! Naapa kwa mwezi! 33. Na kwa usiku unapokucha! 34. Na kwa asubuhi inapopambazuka! 35. Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa! 36. Ni onyo kwa binaadamu. 37. Kwa anayetaka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa. 38. Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyoyachuma. 39. Isipokuwa watu wa kuliani. 40. Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana 41. Habari za wakosefu: 42. Ni nini kilichokupelekeni Motoni? 43. Waseme: Hatukuwa miongoni waliokuwa wakisali. 44. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini. 45. Na tulikuwa tukizama pamoja na waliozama katika maovu. 46. Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo. 47. Mpaka yakini ilipotufikia. 48. Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi. 49. Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili? 50. Kana kwamba wao ni mapunda waliotimuliwa. 51. Wanaomkimbia simba! 52. Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizofunuliwa. 53. Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera? 54. Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho! 55. Basi anayetaka atakumbuka. 56. Na hawatakumbuka isipokuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye. "},{"id":6633,"sura":74,"from_aya":32,"to_aya":34,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{32 - 34} \"Hasha,\" sivyo hivyo. Kisha Mwenyezi Mungu akaapa kwa mwezi, na kwa usiku wakati wa kucha kwake, na kwa mchana unapopambazuka, kwani hayo yaliyotajwa yanajumuisha ishara kuu za Mwenyezi Mungu zinazoonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu, hekima yake, upana wa mamlaka yake, ujumla wa rehema yake na kujua kwake kila kitu."},{"id":6634,"sura":74,"from_aya":35,"to_aya":37,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{35 - 37} Na kile kilichoapiwa ni kauli yake: \"Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!\" Kwa hivyo, tukikujulisheni juu yake na mkajua vyema jambo lake, basi anayetaka kutangulia miongoni mwenu na kufanya yatakayomweka karibu na Mwenyezi Mungu na kumsogeza karibu mno na radhi zake na nyumba ya utukufu wake, au anayetaka akabaki nyuma katika kile alichoumbwa kwa ajili yake na kile anachokipenda Mwenyezi Mungu na kukiridhia, basi na \nafanye maasi na ajiweke karibu na Jahannam. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye aamini...\" hadi mwisho wa Aya."},{"id":6635,"sura":74,"from_aya":38,"to_aya":48,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{38 - 48} \"Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyoyachuma\" miongoni mwa vitendo viovu na vibaya. Vimefungwa shingoni kwake sawasawa na vikamfanya kustahiki kuadhibiwa kwavyo. \"Isipokuwa watu wa kuliani\" kwani hawakushikwa rahanini. Bali walifunguliwa huru na wakafurahishwa. \"Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana habari za wakosefu.\" Humo watakuwa wamepewa yote waliyoyataka na itawatimia starehe na utulivu, mpaka wakaelekeana kuulizana maswali, kisha mazungumzo hayo yakawapelekea kuuliza juu ya wahalifu. Walifikia hali gani? Je, walipata kile ambacho Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaahidi? Kisha baadhi yao wakaambiana: 'Je, mnawaona?' Basi wakawatazama na wakawaona katikati ya Jahannamu wakiteswa, kwa hivyo wakawaambia: \u201cNi nini kilichokupelekeni Saqr?\u201d Wakasema: \"Hatukuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakisali. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.\" Kwa hivyo hawakumkusudia mwabudiwa peke yake, wala hawakuwa wakiwafanyia wema na kuwanufaisha viumbe wahitaji. \"Na tulikuwa tukizama pamoja na wale waliozama katika maovu\" tukiijadili na kuipinga haki kwayo. \"Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo.\" Hizi ndizo athari za kujizamisha katika batili, ambazo ni kukadhibisha haki. Na katika haki kubwa zaidi ni kuamini katika siku ya malipo, ambayo ndiyo siku ya malipo juu ya matendo na kudhihiri ufalme wa Mwenyezi Mungu na hukumu yake ya uadilifu kwa viumbe vyote. Basi sisi tukaendelea kufanya matendo kulingana na dhehebu hili batili. \"Mpaka yakini ilipotufikia.\" Yaani, mauti. Basi walipokufia katika ukafiri, wakakosa hila yoyote, na mlango wa matumaini ukafungika mbele ya nyuso zao. \"Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi.\" Kwa sababu hawamfanyii uombezi yeyote isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemridhia. Na hao, Mwenyezi Mungu hayaridhii matendo yao."},{"id":6636,"sura":74,"from_aya":49,"to_aya":53,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{49 - 53} Mwenyezi Mungu alipobainisha hatima ya wale waliohalifu kitambo na akabainisha watakachofanyiwa, akawaelekezea hawa waliopo makaripio na lawama, akasema: \"Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?\" Yaani, wanaupinga na na wameghafilika mbali nao. \"Kama kwamba wao\" katika kuukimbia kwao mno \"ni mapunda waliotimuliwa.\" Basi wakakimbizana wao kwa wao, kwa hivyo wakazidi kukimbia. \"Wanaomkimbia simba\" au mwindaji na mpiga mishale anayewataka. Na hali hii ndiyo aina mojawapo kubwa zaidi ya kujiweka mbali na haki, lakini pamoja na kujiweka mbali huku na kupeana mgongo, wanadai madai makubwa. \"Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizofunuliwa\" zimshukie kutoka mbinguni. Anadai kwamba hajisalimishi kwa haki Isipokuwa kwa hilo. Lakini wamesema uwongo. Kwani lau ingewafikia kila ishara, hawangeamini mpaka waione adhabu chungu. Kwa sababu ziliwajia ishara zilizo wazi zinazobainisha na kuiweka wazi haki. Basi ikiwa kulikuwa na wema ndani yao, wangeamini, na ndiyo maana akasema: \"Hasha!\" Yaani, hatuwapi kile walichokiomba, kwani hawakukusudia kwa hilo isipokuwa kuonyesha kwamba Mwenyezi Mungu ameshindwa. \"Kwani wao hawaiogopi Akhera?\" Kwa sababu wangekuwa wanaiogopa, hawangefanya hayo waliyoyafanya."},{"id":6637,"sura":74,"from_aya":54,"to_aya":56,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{54 - 56} \"Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho!\" Hapa, neno huu linawezekana kwamba linarejelea Sura hii au mawaidha yaliyomo ndani yake. \"Basi anayetaka atakumbuka\" kwa sababu ameshambainishia njia, na ushahidi ukamuwia wazi. \"Na hawatakumbuka isipokuwa Mwenyezi Mungu atake.\" Kwani utashi wa Mwenyezi Mungu ni wenye kutekelezeka na ni wa jumla, na hakuna tukio dogo wala kubwa linaloweza kutoka nje yake. Katika hili kuna jibu dhidi ya Al-Qadariyya, ambao hawajumuishi vitendo vya waja chini ya utashi wa Mwenyezi Mungu, na pia Al-Jabriya wanaodai kuwa mja hana dhamira ya kweli au kitendo, lakini badala yake analazimishwa kufanya vitendo vyake. Kwa hivyo, hapa Mwenyezi Mungu Mtukufu amethibitisha kwamba waja wana utashi na wanatenda kiuhakika, lakini akayafanya hayo kuwa chini ya utashi wake, na \"Ucha Mungu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye.\" Yaani, Yeye ndiye anayestahiki kuogopwa na kuabudiwa. Kwa sababu Yeye ndiye Mungu ambaye haipasi kuabudu isipokuwa Yeye, na Yeye ndiye anayestahiki kupeana maghfira kwa wanaomcha na kufuata radhi zake."},{"id":6638,"sura":74,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika (tafsiri yake) na sifa njema na neema ni zake Mwenyezi Mungu."},{"id":6639,"sura":74,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}