{"result":[{"id":6666,"sura":76,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Al-Insan"},{"id":6667,"sura":76,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":6668,"sura":76,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":6669,"sura":76,"from_aya":1,"to_aya":3,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinachotajwa. 2. Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona. 3. Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru. "},{"id":6670,"sura":76,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Katika Sura hii, Mwenyezi Mungu ametaja hali ya mwanzo, mwisho, na hali ya kati ya mwanadamu: Ametaja kwamba muda mrefu umepita juu yake, nao ni ule uliotangulia kabla ya kuwepo kwake, na hata hakuwa kitu cha kutajwa."},{"id":6671,"sura":76,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Kisha alipotaka kumuumba, alimuumba baba yake, Adam kwa udongo, kisha akawajaalia dhuriya zake \"kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika\" yanayoonwa kwamba ni machafu \"ili tumfanyie mtihani\" kwa hayo. Ili tujue iwapo ataiona hali yake ya mwanzo na kuitambua, au ataisahau na kudanganywa na nafsi yake? Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamuumba na kumpa nguvu za dhahiri na zilizofichika, kama vile kusikia, kuona, na viungo vingine, kwa hivyo alivikamilisha hivyo vote kwa ajili yake na akaviweka salama ili aweze kufikia malengo yake."},{"id":6672,"sura":76,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} Kisha akamtumia Mitume, na akamteremshia vitabu, na akamwongoza kwenye njia ya kumfikisha kwake, na akaifafanua, na akamtia moyo wa kuifuata, na akamwambia yale yatakayokuwa yake atakapoifikia. Kisha akamwambia njia itakayoelekea kwenye maangamizo, na akamtia woga wa kuifuata, na akamwambia yale ambayo yatakuwa yake iwapo ataishika, na akamtia mtihani kwa hayo. Basi watu wakagawanyika wenye kushukuru kwa ajili ya neema za Mwenyezi Mungu juu yake, na ambaye anashika sawasawa yale ambayo Mwenyezi Mungu alimbebesha katika haki zake. Na pia wakawapo wasioshukuru neema ambazo Mwenyezi Mungu amemneemesha; za kidini na za kidunia, na pia anamkufuru Mola wake Mlezi, na anafuata njia ya kumfikisha katika maangamizo. [Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja makundi hayo mawili wakati wa malipo yao, akasema]:"},{"id":6673,"sura":76,"from_aya":4,"to_aya":31,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"4. Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali. 5. Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyochanganyika na kafuri 6. Ni chemchemi watakaoinywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi. 7. Wanatimiza nadhiri, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana. 8. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. 9. Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. 10. Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu. 11. Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha. 12. Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyosubiri. 13. Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali. 14. Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini. 15. Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae. 16. Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo. 17. Na humo watanyweshwa kinywaji kilichochanganyika na tangawizi. 18. Hiyo ni chemchemi iliyo humo inaitwa Salsabil. 19. Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasiopevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizotawanywa. 20. Na utakapoyaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa. 21. Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya atilasi. Na watavishwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa. 22. Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa. 23. Hakika Sisi tumekuteremshia Qur-ani kidogo kidogo. 24. Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimtii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru. 25. Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni. 26. Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu. 27. Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku nzito. 28. Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao. 29. Hakika haya ni mawaidha; basi anayetaka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi. 30. Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye elimu, Mwenye hekima. 31. Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu. "},{"id":6674,"sura":76,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Yaani, hakika Sisi tumewaandalia wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu, na wakakadhibisha Mitume wake, na wakathubutu kumuasi; \"minyororo\" katika Moto wa Jahannamu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!\" Kisha hapa akasema \"na pingu\" ambazo mikono yao itafungwa kwazo hadi shingoni mwao, \"na Moto mkali\" utakachoma miili yao na miili yao. Kila zitakapoiva ngozi zao, tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje hiyo adhabu. Nayo adhabu hii ni ya milele kwao."},{"id":6675,"sura":76,"from_aya":5,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5} Ama \"watu wema\" ambao mioyo yao ni yenye njema kwa sababu ya yale yaliyo ndani yake ya kumjua Mwenyezi Mungu, kumpenda na maadili mema. Basi matendo yao yakawa mema, kwa hivyo ikawaambia kwamba \u201cwatakunywa katika kikombe vya vinywaji\" vitamu vya mvinyo [ambao] umechanganywa na kafuri, ili ichanganyike nayo ili kuipoza na kuvunja ukali wake. Na kafuri hiyo itakuwa na ladha ya hali ya juu, ambayo atakuwa imesalimika mbali na machafu yanayopatikana katika kafuri ya duniani. Kwani kasoro zilizoko duniani haziko katika majina ambayo Mwenyezi Mungu alitaja katika bustani za mbinguni, kama Mwenyezi Mungu alivyosema: \"Katika mikunazi isiyo na miba. Na migomba iliyopangiliwa\" na akasema \"na wake waliotakaswa,\" na akasema \"Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola Mlezi wao.\" Na akasema \"na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia.\""},{"id":6676,"sura":76,"from_aya":6,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6} \"Ni chemchemi watakaoinywa waja wa Mwenyezi Mungu.\" Yaani, hicho kikombe chenye ladha nzuri watakachokunywa, hawataogopa kwamba kitakwisha, bali kina asili isiyokoma, nayo ni chemchemi inayofurika na kutiririka daima, na waja wa Mwenyezi Mungu wataifanya imiminike kwa wingi mahali watakapo na jinsi watakavyo. Wakitaka, wanaitumia kwenye bustani zenye miti mirefu au makonde mazuri, au kati ya pande za makasri yaliyopambwa kifahari na upande wowote wa kifahari wanaouona."},{"id":6677,"sura":76,"from_aya":7,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7} Kisha akataja baadhi ya vitendo vyao, akasema: \"Wanatimiza nadhiri\" waliyojiwekea wenyewe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na maagano mengineyo. Na ikiwa wanatimiza nadhiri ambayo si wajibu katika asili yake isipokuwa kama mtu mwenyewe atajiwajibishia, basi kutakuwa kufanya kwao mambo ya faradhi ya asili ni jambo la awali zaidi na linalostahiki zaidi. \u201cNa wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana.\" Kwa hivyo, wakahofu wasije patwa na uovu wake, basi wakaacha kila sababu ya kuwasababishia hilo."},{"id":6678,"sura":76,"from_aya":8,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{8 - 10} \"Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake\" kwa sababu wametanguliza mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuliko mapenzi ya nafsi zao wenyewe, na wako makini zaidi kuwalisha watu wanaostahiki zaidi na walio wahitaji zaidi miongoni mwao, ambao ni \"masikini, na yatima, na wafungwa\" na kwa utoaji wao huo na kuwalisha kwao huko wanakusudia uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wanasema kwa ulimi wa hali zao: \"Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.\" Yaani, hatutaki malipo ya kimali wala kusifiwa kwa maneno. \"Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida\" nyingi na maovu \"na taabu.\""},{"id":6679,"sura":76,"from_aya":11,"to_aya":11,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11} \"Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo\" na hicho Kitisho Kikubwa hakitawahuzunisha. Na Malaika watawapokea kwa kuwaambia: 'Hii ndiyo Siku yenu mliyokuwa mkiahidiwa!' Na tena \"atawakutanisha na raha\" katika nyuso zao, \"na furaha\" katika nyoyo zao. Hapo atakuwa amewakusanyia neema ya nje na ya ndani."},{"id":6680,"sura":76,"from_aya":12,"to_aya":12,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{12} \"Na atawajazi kwa sababu ya kuwa na subira\" katika kumtii. Wakafanya yale aliyowawezesha, kuwaepusha na kumuasi, na wakaacha kuchukia mipango yake mikali. \"Bustani za Peponi\" zilizokusanya neema, zisizo na kila dhiki na taabu, \"na maguo ya hariri.\" Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Na nguo zao humo ni za hariri.\" Labda Mwenyezi Mungu ameichagua hariri kwa sababu ni nguo zao za dhahiri zinazoonyesha hali ya mwenye kuzivalia."},{"id":6681,"sura":76,"from_aya":13,"to_aya":13,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{13} \"Humo wataegemea juu ya viti vya enzi\" vya sampuli ya kitanda kilichovalishwa vitambaa maridadi. \"Hawataona humo\" Peponi \"jua\" la kuwadhuru kwa joto lake, \"wala baridi kali.\" Badala yake, nyakati zao zote zitakuwa kwenye vivuli vizuri kweli. Si joto wala baridi, ambapo miili yao itafurahia na haitateseka kwa sababu ya joto au baridi."},{"id":6682,"sura":76,"from_aya":14,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{14} \"Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini\" kiasi kwamba anayeyataka ataweza kuyapata akiwa amesimama, amekaa au amelala."},{"id":6683,"sura":76,"from_aya":15,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15 - 16} \"Na watapitishiwa.\" Yaani, watoto na watumishi watawajia mara kwa mara Peponi, \"kwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae. Vya fedha safi kama kiyoo.\" Haya ni katika mambo ya ajabu sana, kwamba fedha ambayo huwa imesongana bila ya kuonekana ndani iwe safi mno kama kioo katika usafi wake na uzuri wake, \"wamevipima kwa vipimo.\" Yaani, walivipima vyombo hivyo vilivyotajwa kulingana na kiwango cha kuwashibisha kiu chao, bila ya kuzidisha wala kupunguza. Kwa sababu ikiwa vingezidi, basi ladha yake ingepungua, na kama vikipungua, basi havingeweza kuwakatia kiu. Lakini inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapa ni: wakazi wa Peponi walivipima kwa kipimo kinacholingana na ladha zao, kwa hivyo vikawajia kulingana na walivyokadiria katika fikira zao."},{"id":6684,"sura":76,"from_aya":17,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17 - 18} \"Na humo watanyweshwa\" katika \"kikombe\" [kilichojaa] mvinyo safi zaidi \"kilicho changanyika na tangawizi\" ili kuifanya ladha na harufu yake kuwa nzuri. \"Hiyo ni chemchemi iliyo humo.\" [Yaani, Peponi] \"inaitwa Salsabil,\" iliitwa hivyo kwa sababu ya ulaini wake, ladha yake na uzuri wake."},{"id":6685,"sura":76,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} \"Na watawazungukia\" wakazi wa Peponi katika vyakula vyao, na vinywaji vyao, na utumishi wao \"wavulana wasiopevuka\" kwa maana waliumbwa huko Peponi waishi milele. Hawabadiliki wala hawakui wakubwa, na ni uzuri wa kiwango cha juu zaidi. \"Ukiwaona\" wakienea katika utumishi wao \"utawafikiri\" kwa sababu ya uzuri wao kwamba ni \"lulu zilizo tawanywa.\" Na hili ni katika jambo la kutimiza starehe ya wakazi wa Peponi; kwamba watumishi wao wawe wavulana wanaoishi milele, ambao wanafurahisha kuwatazama, na wataingia majumbani mwao wakiwa salama kutokana na lawama yoyote, na watawaletea yale wanayoyaitisha na kutakiwa na nafsi zao."},{"id":6686,"sura":76,"from_aya":20,"to_aya":20,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{20} \"Na utakapoyaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.\" Utakuta kwamba kila mmoja wao anayo [makasri na] maskani na vyumba vilivyopambwa na visivyoelezeka, na pia ana bustani nzuri matunda yanayoning'inia chini, matamu, mito itiririkayo, makonde ya ajabu, na ndege waimbao kwa uzuri mkubwa, yale yanayoteka nyoyo na kuzifurahisha nafsi, na pia atakuwa na wake walio wazuri mno na wema, wanaokusanya uzuri wa nje na wa ndani, yale yanayoujaza moyo furaha, raha na starehe kubwa, na kandoni mwake kutakuwa na watoto wasiokufa na watumishi wa kudumu milele, ambao kwao faraja na utulivu itapatikana, na raha na furaha kubwa ya maisha itakamilika. Kisha juu zaidi ya hayo, na kubwa yake zaidi ni kupata radhi za Mola Mwingi wa rehema, kusikia mazungumzo yake, raha ya kuwa karibu naye, kufurahia radhi zake na kuishi milele daima, na pia kuongezeka kwa neema waliyo ndani yake kila wakati. Basi ametakasika Mwenye kumiliki, Mfalme wa Haki, Aliye Wazi, ambaye hazina zake haziishi, na ambaye wema wake haupungui. Na kama vile hakuna mwisho wa sifa zake, hakuna mwisho wa wema na hisani yake."},{"id":6687,"sura":76,"from_aya":21,"to_aya":21,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{21} \"Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi\" na hariri nzito, ambazo ndizo aina bora zaidi za hariri. \"Na watavishwa vikuku vya fedha\" wanaume na wanawake. Hii ni ahadi ambayo Mwenyezi Mungu aliwaahidi, na ahadi yake lazima itatekelezeka. Kwa sababu hakuna aliye mkweli zaidi yake katika usemi na mazungumzo. Na kauli yake: \"Na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa.\" Yaani, hakina uchafu ndani yake kwa namna yoyote ile, na kitawatakasa yaliyomo matumboni mwao kutokana na madhara na uchafu wote."},{"id":6688,"sura":76,"from_aya":22,"to_aya":22,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{22} \"Hakika haya\" malipo makubwa [na kipawa kizuri] hiki \"ni malipo yenu\" kwa yale mliyoyafanya hapo awali. \"Na juhudi zenu zimekubaliwa.\" Yaani, juhudi zenu kidogo Mwenyezi Mungu amekupeni kwazo neema [ya kudumu] isiyohesabika."},{"id":6689,"sura":76,"from_aya":23,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{23} Na kauli yake Mwenyezi Mungu alipotaja neema ya Peponi: \"Hakika Sisi tumekuteremshia Qur-ani kidogo kidogo,\" ina ahadi nzuri na ahadi ya adhabu, na kubainisha kila jambo ambalo waja wanahitaji, na ina amri ya kutekeleza amri na sheria zake kamilifu zaidi na kujitahidi sana katika kuzitekeleza na kuwa na subira kwa hilo."},{"id":6690,"sura":76,"from_aya":24,"to_aya":24,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24} Ndiyo maana akasema: \"Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimtii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru.\" Yaani, kuwa msubirifu kwa hukumu za mipango yake, na usikasirishwe nazo, na hukumu zake za kidini; kwa kuzitekeleza, na kamwe kisikuzuie mbali nazo kizuizi chochote. \"Wala usimtii\" katika wakaidi wanaotaka kukuzuia. \"Wala mwenye kufuru\" kwa maana utii kwa mwenye kufuru, mwovu, mvuka mipaka lazima ni uasi kwa Mwenyezi Mungu. Kwani wao hawaamrishi isipokuwa yale yanayotamaniwa na nafsi zao tu."},{"id":6691,"sura":76,"from_aya":25,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{25} Na kwa kuwa subira inatokana na kumtii Mwenyezi Mungu na kumkumbuka mara kwa mara; Mwenyezi Mungu akaamrisha hilo, akasema: \"Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni.\" Yaani, mwanzo wa siku na mwisho wake, kwa hivyo hilo likajumuisha swala za faradhi, na swala za hiari zinazozifuata, dhikri, kumtakasa, kusema hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kumtukuza katika nyakati hizi."},{"id":6692,"sura":76,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} \"Na usiku msujudie Yeye.\" Na hilo linajumuisha kuswali kwa wingi, \"na umtakase usiku, wakati mrefu.\" Na tayari agizo hili lililo wazi limeshafungiwa na kauli Yake: \"Ewe uliyejifunika! Kesha usiku kucha, ila kidogo tu! Nusu yake, au ipunguze kidogo. Au izidishe...\""},{"id":6693,"sura":76,"from_aya":27,"to_aya":27,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27} Na kauli yake: \"Kwa hakika watu hawa;\" yaani, wale waliokukadhibisha ewe Mtume, baada ya kubainishiwa Aya, na wakati wa moyo na wakaogopeshwa, lakini pamoja na hayo, hayo hayakuwafaa kitu. Bali bado wanapendelea \"maisha ya kidunia\" na wanatulizana juu yake \"na wanaiacha nyuma yao siku nzito.\" Yaani, kwa kuacha kutenda matendo na kuyapuuza kwa ajili ya Siku ya Kiyama, ambayo urefu wake ni miaka hamsini elfu kama mnavyohesabu nyinyi, na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.\" Na tena ni kama kwamba hawakuumbwa isipokuwa kwa ajili ya dunia hii na kudumu humo."},{"id":6694,"sura":76,"from_aya":28,"to_aya":28,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{28} Kisha akatumia ushahidi wa kiakili dhidi yao na wa kuunga mkono kufufuliwa kwao, nao ni ushahidi wa mwanzo wao, akasema: \"Sisi tumewaumba\" baada ya kutokuwepo kwenu \"na tukavitia nguvu viungo vyao\" kama vile mishipa ya fahamu, mishipa ya damu na nguvu zinazoonekana na zisizoonekana, mpaka mwili ukakamilika sawasawa na akaweza kufanya kila alitakalo. Kwa hivyo, aliyewaumba katika hali hii ana uwezo wa kuwarudisha baada ya kufa kwao na kuwalipa. Na aliyewapitisha katika nyumba hii katika awamu hizi zote haimfailii kuwaacha bure bila ya kuamrishwa kukatazwa wala kulipwa mazuri wala kuadhibiwa. Ndiyo maana akasema: \"Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao.\" Yaani, tutawafufua kwa kwa ajili ya ufufuo kwa namna nyingine, na tukurudisheni nyinyi wenyewe hasa, na wao pia wenyewe hasa."},{"id":6695,"sura":76,"from_aya":29,"to_aya":29,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{29} \"Hakika huu ni ukumbusho\" ambao Muumini anakumbushwa kwa huo na kunufaika kwa yaliyo ndani yake ya kuhofisha na pia ya kutia moyo. \"Basi anayetaka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi\" na kumfikisha huko. Kwani Mwenyezi Mungu huweka wazi haki na uwongofu, kisha huwapa watu chaguo kati ya kuongoka kwa hayo au kuyaacha. Ili hilo liwe ni kusimamisha hoja; ili mwenye kuangamia aangamie kwa ushahidi wa wazi, na mwenye kusalia hai asalie hai kwa ushahidi wa wazi."},{"id":6696,"sura":76,"from_aya":30,"to_aya":30,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{30} \"Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu\" kwani utashi wa Mwenyezi Mungu ndio wa kutekelezeka. \"Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye elimu, Mwenye hekima.\" Kwa maana ana hekima katika kuwaongoa wale walioongoka na kuwapoteza waliopotea."},{"id":6697,"sura":76,"from_aya":31,"to_aya":31,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{31} \"Humuingiza amtakaye katika rehema yake\" kwa kumtunza kwa njia mahususi, na humuwezesha kufikia visababu vya kupata furaha, na humuongoza kwenye njia zake. \"Na wenye kudhulumu\" ambao walichagua upotofu badala ya uwongofu, \"amewawekea adhabu iliyo chungu\" kwa sababu ya dhuluma ya na kuvuka kwao mipaka."},{"id":6698,"sura":76,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika tafsiri yake, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu."},{"id":6699,"sura":76,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}