{"result":[{"id":6743,"sura":79,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsir ya Surat An-Naziat"},{"id":6744,"sura":79,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":6745,"sura":79,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":6746,"sura":79,"from_aya":1,"to_aya":14,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Ninaapa kwa wanaokomoa kwa nguvu. 2. Na kwa wanaotoa kwa upole. 3. Na wanaoogelea sawasawa. 4. Wakishindana mbio kweli kweli. 5. Wakidabiri mambo. 6. Siku kitakapotetemeka cha kutetemeka. 7. Kifuate cha kufuatia. 8. Siku hiyo nyoyo zitapigapiga. 9. Macho yatainama chini. 10. Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza? 11. Hata tukiwa mifupa iliyobunguliwa? 12. Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye hasara! 13. Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu. 14. Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano! "},{"id":6747,"sura":79,"from_aya":1,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1 - 5} Hivi ni viapo kwa Malaika watukufu na vitendo vyao vinavyoashiria utiifu wao kamili kwa amri za Mwenyezi Mungu na uharaka wao katika kuzitekeleza. Inawezekana kwamba yule kinachokusudiwa na viapo hivi ni malipo na ufufuo; kwa ushahidi wa kutajwa hali za siku ya Kiyama baada ya hapo. Na inawezekana kwamba kinachoapiwa na kinachokusudiwa na viapo hivi ni kitu kimoja, nao ni Malaika. Kwa sababu kuwaamini ni miongoni mwa nguzo sita za imani, na kwa sababu kutajwa kwa vitendo vyao hapa kunajumuisha malipo ambayo Malaika husimamia wakati wa kufa kwa viumbe, na kabla yake, na baada yake. Akasema, \"Ninaapa kwa wanaokomoa kwa nguvu.\" Hao ni Malaika wanaozitoa roho kwa nguvu, mpaka roho itoke na ilipwe kwa matendo yake. \"Na kwa wanaotoa kwa upole.\" Nao pia ni Malaika wanaovuta roho kwa nguvu na ukakamavu, au ukakamavu huo huwa wanapotoa roho za Waumini, nayo nguvu huwa wanapotoa roho za makafiri. \"Na wanaoogelea sawasawa\" angani, wakipanda na kushuka. \"Wakishindana mbio kweli kweli\" wenzao huku wakiharakisha kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, na kuwatangulia mashetani katika kufikisha ufunuo kwa Mitume wa Mwenyezi Mungu; ili wasiusikilize kwa siri. \"Wakidabiri mambo\" nao ni wale Malaika ambao Mwenyezi Mungu aliwaweka wasimamie mambo mengi ya ulimwengu wa juu na wa chini, kama vile mvua, mimea [na miti], pepo, bahari, vijusi matumboni mwa mama, wanyama, bustani za mbinguni, Moto wa mbinguni na vitu vinginevyo."},{"id":6748,"sura":79,"from_aya":6,"to_aya":9,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6 - 9} \"Siku kitakapotetemeka cha kutetemeka\" ambayo ni kuja kwa Saa (ya Kiyama), \"Kifuate cha kufuatia\" Yaani, mtetemeko mwingine unaoifuata na kuja baada yake. \"Siku hiyo nyoyo zitapigapiga\" kwa sababu ya ukali wa yale ambayo zinayaona na kukisikia. \"Macho yatainama chini\" huku yamedhalilika, kutwezwa, kwa sababu nyoyo zao zitakuwa zimetawaliwa na hofu na majuto makubwa."},{"id":6749,"sura":79,"from_aya":10,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{10 - 14} \"Sasa wanasema\" makafiri hapa duniani kwa njia ya kukadhibisha \"Hata tukiwa mifupa iliyobunguliwa? Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye hasara!\" Yaani, waliona kwamba haliwezekani kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua na kuwarudisha baada ya kuwa mifupa iliyooza, kwa sababu ya ujinga wao kuhusiana na uwezo wa Mwenyezi Mungu na kwa kumdharau Yeye! Mwenyezi Mungu alisema katika kufafanua wepesi wa jambo hili: \"Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu.\" Ambapo itapulizwa katika baragumu, na hapo viumbe vyote \"watakuwa kwenye uwanda wa mkutano\" wamesimama wakingoja. Kisha Mwenyezi Mungu atawakusanya pamoja, na kuhukumu kati yao kwa hukumu yake ya uadilifu, na awalipe."},{"id":6750,"sura":79,"from_aya":15,"to_aya":26,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"15. Je! Imekufikia hadithi ya Musa? 16. Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la Tuwaa, akamwambia: 17. Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri. 18. Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa? 19. Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha. 20. Basi alimwonyesha Ishara kubwa. 21.Lakini aliikadhibisha na akaasi. 22. Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi. 23. Akakusanya watu akanadi. 24. Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa. 25. Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo. 26. Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanaoogopa. "},{"id":6751,"sura":79,"from_aya":15,"to_aya":25,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15 - 25} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - \"Je! Imekufikia hadithi ya Musa?\" Swali hili linahusu jambo kubwa ambalo ni la yakini kutokea kwake. Yaani, je, ilikufikia hadithi yake \"Mola wake Mlezi alipomwita katika bonde takatifu la T'uwaa?\" Napo ni pale mahali alipozungumza naye Mwenyezi Mungu, akamneemesha kwa utume, na akamtuma kwa ufunuo, na akamteua, na akamwambia: \"Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri.\" Yaani, basi mkamkataze uasi wake, na ushirikina, na uovu wake kwa maneno laini na ya upole, labda atakumbuka au akaogopa. \"Umwambie: Je, unapenda kujitakasa?\" Yaani, je, hutaki jambo la kusifiwa lililo zuri ambalo watu wenye ufahamu mzuri hushindana ndani yake? Nalo ni kwamba ujitakase kutokana na uchafu wa ukafiri na kuvuka mipaka na kuelekea kwenye imani na matendo mema. \"Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi\" kwa kukubainishia pahala pa radhi zake na pahala pa ghadhabu yake \"upate kumcha\" Mwenyezi Mungu utakapojua njia iliyonyooka. Lakini Firauni akakataa yale ambayo Musa alimwitia, \"Basi alimwonyesha Ishara kubwa.\" Nazo zilikuwa aina mbalimbali za ishara kubwa kubwa. \"Basi akaitupa fimbo yake, na mara ikawa nyoka dhahiri. Na akatoa mkono wake, mara ukawa mweupe kwa watazamao.\" Lakini Firauni \"aliikadhibisha\" haki \"na akaasi\" amri. \"Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi\" za kupinga na kupigana na haki. \"Akakusanya\" askari wake \"akanadi. Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.\" Kwa hivyo, wakamtii na kukiri batili yake hivyo wakati alipowachezea mchezo huo. \"Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.\" Yaani, Mwenyezi Mungu aliifanya adhabu yake kuwa ni mwongozo, karipio na ufafanuzi wa adhabu ya dunia na akhera."},{"id":6752,"sura":79,"from_aya":26,"to_aya":26,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{26} \"Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanaoogopa.\" Kwa maana anayemcha Mwenyezi Mungu ndiye anayefaidika na Ishara na mazingatio. Ikiwa ataona adhabu ya Firauni; atajua kwamba [kila mtu] aliyekuwa na kiburi, akaasi, na akapigana na Mfalme Mkuu, atamuadhibu katika dunia na Akhera. Lakini yule ambaye hofu ya Mwenyezi Mungu iliondoka moyoni mwake, basi hata kama atajiwa na ishara zote, hataziamini."},{"id":6753,"sura":79,"from_aya":27,"to_aya":33,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"27. Je, ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliyeijenga! 28. Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. 29. Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake. 30. Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. 31. Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake. 32. Na milima akaisimamisha imara. 33. Kwa nafuu yenu na mifugo yenu. "},{"id":6754,"sura":79,"from_aya":27,"to_aya":33,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{27 - 33} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akiwabainishia ushahidi wazi wale wanaokanusha ufufuo na wanaokataa suala la Mwenyezi Mungu kurejesha miili: \"Je, ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi\" watu \"au mbingu\" zenye maumbile makubwa, ya nguvu, zilizoinuka juu sana? \"Yeye\" Mwenyezi Mungu \"ndiye aliyeijenga! Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri\" na ukamilifu wa hali ya juu unaozichanganya akili na kuzishangaza nyoyo. \"Na akautia giza usiku wake\" nalo likatanda pande zote za mbingu, kwa hivyo uso wa ardhi ukawa giza. \"Na akautokeza mchana wake\" jua lilipochomoza, kwa hivyo watu wakaenea kwa ajili ya masilahi ya dini yao na dunia yao. \"Na juu ya hivyo\" baada ya kuumbwa mbingu \"ameitandaza ardhi\" na kutia humo manufaa yake, kama alivyofasiri hilo kwa kauli yake: \"Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake. Na milima akaisimamisha imara.\" Na suala la kuitandaza ardhi kulikuwa baada ya kuumba mbingu. Kama ilivyo katika maandiko ya Aya hizi tukufu. Na ama kuumbwa kwa ardhi yenyewe, huko kulitangulia kuumbwa mbingu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: \"Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliyeumba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote...\" mpaka aliposema: \"Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa hiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu. Basi akazifanya mbingu saba...\" Kwa hivyo, yule aliyeziumba mbingu kubwa na mianga na miili iliyomo ndani yake, na ardhi yenye mavumbi na nene, na mahitaji ya lazima na manufaa ya viumbe, ni lazima atawafufua viumbe waliojukumishwa kisheria ili awalipe kwa matendo yao. Kwa hivyo, aliyefanya wema, basi atalipwa na wema. Naye aliyefanya ubaya, basi kamwe asilaumu isipokuwa yeye mwenyewe tu."},{"id":6755,"sura":79,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"Ndiyo maana baada ya haya akataja kuja kwa Saa (ya Kiyama) kisha malipo, akasema:"},{"id":6756,"sura":79,"from_aya":34,"to_aya":41,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"34. Basi itakapofika hiyo balaa kubwa, 35. Siku ambayo mtu atakumbuka aliyoyafanya, 36. Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona, 37. Basi ama yule aliyezidi ujeuri, 38. Na akakhiari maisha ya dunia, 39. Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! 40. Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, 41. Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake! "},{"id":6757,"sura":79,"from_aya":34,"to_aya":36,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{34 - 36} Yaani, wakati Ufufuo Mkuu na Dhiki Kuu itakapokuja, wakati huo kila dhiki itakuwa rahisi. Kisha baba hatamjali mtoto wake, na rafiki hatamjali rafiki yake, na kila apendwaye hatampenda kipenzi chake, na \"mtu atakumbuka aliyoyafanya\" katika dunia ya heri na maovu, na atatamani kuongezewa uzito wa chembe katika matendo yake mema, na atahuzunika na kupata wasiwasi mkubwa kutokana na kuongezeka uzito wa chembe katika matendo yake mabaya, na atajua wakati huo kuwa kiini cha faida yake na hasara yake ni yale aliyofanya katika dunia, na kila njia na mafungamano aliyokuwa nayo hapa duniani yatakatika isipokuwa matendo. \"Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona\" ili kila mmoja aione. Kwani itakuwa tayari imeandaliwa wakazi wake ili iwachukue, huku ikingojea amri ya Mola wake Mlezi."},{"id":6758,"sura":79,"from_aya":37,"to_aya":39,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{37 - 39} \"Basi ama yule aliye zidi ujeuri\" kwa kuvuka mipaka kwa kuthubutu kufanya maasi makubwa na hakukomekea kwenye mipaka aliyowekewa na Mwenyezi Mungu, \"na akakhiari maisha ya dunia\" kuliko ya akhera, kwa hivyo akajitahidi kwa ajili yake, na akamaliza wakati wake katika kufuata mazuri yake na matamanio yake, na akaisahau Akhera na kuifanyia kazi, \"kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!\""},{"id":6759,"sura":79,"from_aya":40,"to_aya":41,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{40 - 41} \"Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi\" kwa hivyo, hofu hii akaathiri katika moyo wake, basi \"na akajizuilia nafsi yake\" na matamanio yake, ambayo yanaizuia kumtii Mwenyezi Mungu, kwa hivyo matamanio yake hayo yakawa yanafuata yale aliyoyaleta Mtume, na akapigana na matamanio na vivutio viovu vinavyozuia kufanya wema, \"Basi huyo, Pepo\" yenye kila heri, furaha na neema \"itakuwa ndiyo makaazi yake!\""},{"id":6760,"sura":79,"from_aya":42,"to_aya":46,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"42. Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini? 43. Una nini wewe hata uitaje? 44. Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake. 45. Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuihofu. 46. Ni kama kwamba wao siku watakapoiona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake. "},{"id":6761,"sura":79,"from_aya":42,"to_aya":44,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{42 - 44} Maana yake ni kwamba wanakuuliza wenye ukaidi wanaokadhibisha ufufuo \"Saa (ya Kiyama)\" na kwamba \"itakuwa lini?\" Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kauli yake: \"Una nini wewe hata uitaje?\" Yaani, kuna faida gani kwako na kwao katika kuitaja na kujua muda wa kuja kwake? Hakuna natija katika hilo, na ndiyo sababu hii, kwa kuwa kujua kwa waja kuhusu Saa ya Kiyama hakuna masilahi yao ya kidini wala ya kidunia, bali masilahi yao ni katika kuwaficha wasiijue, basi akaficha elimu ya hilo mbali na viumbe vyote na akajiwekea Yeye tu elimu ya hilo, akasema: \"Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.\" Yaani, kwake ndiyo ujua wake unaishia, kama alivyosema katika Aya nyingine: \u201cWanakuuliza hiyo Saa (ya mwisho) itakuwa lini? Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye.\""},{"id":6762,"sura":79,"from_aya":45,"to_aya":46,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{45 - 46} \"Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuihofu.\" Yaani: Kuonya kwako kutawanufaisha wale tu wanaoogopa kuja kwa Saa (ya Kiyama) na wanaogopa kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio hawajishungulishi isipokuwa kujitayarisha kwa ajili yake na kuifanyia kazi. Ama wale wasioiamini, hao asiwajali wala usugu wao. Kwa maana ni usugu unaotokana na kukadhibisha na ukaidi. Na ikifikia hali hii, basi kumjibu ni bure tu, ambako ametakasika mbali nako mbora zaidi wa wanaohukumu."},{"id":6763,"sura":79,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote."},{"id":6764,"sura":79,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}