{"result":[{"id":6765,"sura":80,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat 'Abasa"},{"id":6766,"sura":80,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Iliteremka Makka"},{"id":6767,"sura":80,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":6768,"sura":80,"from_aya":1,"to_aya":10,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Alikunja kipaji na akageuka. 2. Kwa sababu alimjia kipofu! 3. Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? 4. Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? 5. Ama ajionaye hana haja, 6. Wewe ndiyo unamshughulikia? 7. Na si juu yako kama hakutakasika. 8. Ama anayekujia kwa juhudi. 9.  Naye anaogopa, 10. Ndiyo wewe unampuuza? "},{"id":6769,"sura":80,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062a\u0645\u0647\u064a\u062f \u0644\u0644\u0622\u064a\u0627\u062a","text":"Sababu ya kuteremshwa aya hizi tukufu ni kwamba alikuja kipofu mmoja miongoni mwa waumini kumwomba Mtume - rehema na amani zimshukie - na ajifunze kutoka kwake, kisha akaja tajiri mmoja, naye Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikuwa na hamu kubwa ya kuwaongoza viumbe, kwa hivyo, yeye Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie - akaegemea na kumsikiliza vyema yule tajiri na akakataa kumsikiliza huyo maskini kipofu; akiwa na matarajio ya kumwongoza tajiri huyo na akitumaini atakasike, lakini Mwenyezi Mungu akamlaumu kwa lawama hii ya upole, akisema:"},{"id":6770,"sura":80,"from_aya":1,"to_aya":10,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1 - 10} \"Alikunja kipaji\" cha uso wake \"na akageuka\" kwa mwili wake kwa sababu alijiwa na kipofu. Kisha akataja manufaa ya kumwelekea, akasema: \"Na nini kitakujuulisha pengine yeye\" yaani kipofu huyo, \"atatakasika\" kwa kujiepusha na tabia mbaya na akasifika kwa sifa nzuri. \"Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?\" Na hii ni faida kubwa, ambayo ndiyo lengo la kuwatuma Mitume, kuwaidhi kwa wale wanaowaidhi, na kukumbusha kwa wale wanaokumbusha. Kwa hivyo, wewe kumwelekea yule ambaye yeye mwenyewe alikuja akilitaka jambo hilo, basi yeye ndiye anayefailia zaidi na anayestahiki zaidi kuelekewa. Na ama kumshughulikia kwako na kumwelekea tajiri na mwenye kujiona kwamba kajitosheleza ambaye haulizi wala kutafuta ushauri wa kisheria (fatwa) kwa sababu hana haja na heri, huku ukimwacha yule aliye muhimu zaidi kuliko yeye, basi haupaswi kufanya hivyo. Kwani hutalaumiwa ikiwa hatatakasika. Kwa maana ikiwa hatatakasika, basi wewe hutaulizwa yale aliyofanya ya uovu. Kwa hivyo hili likaonyesha kanuni inayojulikana sana; kwamba jambo linalojulikana halipaswi kuachwa kwa ajili ya jambo la kufikirika tu, wala kuacha masilahi yenye uhakika kwa ajili ya masilahi ya kufikirika tu, na kwamba mtu anafaa kumshughulikia mtafutaji wa elimu ambaye anaihitaji, mwenye uchu nayo zaidi kuliko wengineye."},{"id":6771,"sura":80,"from_aya":11,"to_aya":32,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"11. Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. 12. Basi anayependa akumbuke. 13. Yamo katika kurasa zilizoheshimiwa. 14. Zilizoinuliwa, zilizotakaswa. 15. Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, 16. Watukufu, wema. 17. Ameangamia mwanaadamu! Nini kinachomkufurisha? 18. Kwa kitu gani amemuumba? 19. Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. 20. Kisha akamsahilishia njia. 21. Kisha akamfisha, akamtia kaburini. 22. Kisha apendapo atamfufua. 23. La! Hajamaliza aliyomuamuru. 24. Hebu mtu na atazame chakula chake. 25. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu. 26. Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu. 27. Kisha tukaotesha humo nafaka. 28. Na zabibu, na mimea ya majani. 29. Na mizaituni, na mitende. 30. Na bustani zenye miti iliyosongana baraabara. 31. Na matunda, na malisho ya wanyama. 32. Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. "},{"id":6772,"sura":80,"from_aya":11,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{11 - 16} Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: \"Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana\" kutoka kwa Mwenyezi Mungu, anawakumbusha kwa huo waja wake na anawabainishia katika Kitabu chake kile wanachokihitaji pamoja na kubainisha uwongofu mbali na upotofu. Kwa hivyo ikishakubainikia hivyo \"basi anayependa akumbuke.\" Yaani, ayafanyie kazi; kama kauli yake Mola Mlezi: \"Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae.\" Kisha akataja mahali pa ukumbusho huu, ukubwa wake, na thamani yake kubwa, akasema: \"Yamo katika kurasa zilizoheshimiwa. Zilizoinuliwa\" cheo na daraja, \"zilizotakaswa\" kutokana na maovu na kutokana na kufikiwa na mikono ya mashetani au hat kuzisikiliza kwa siri. Bali ziko \"mikononi mwa Malaika waandishi\" nao ni malaika ambao ni mabalozi kati ya Mwenyezi Mungu na waja wake. \"Watukufu\" yaani, wenye heri na baraka nyingi. \"wema\" katika nyoyo zao na vitendo vyao. Na haya yote ni kuhifadhi kwa Mwenyezi Mungu Kitabu chake; kwamba aliwafanya mabalozi wake kwa Mitume kuwa Malaika watukufu, wenye nguvu na wacha Mungu, tena hakuwaruhusu mashetani kuwa na njia yoyote kukifikia kitabu chake. Na haya ni katika yale yanayolazimu kukiamini na kukikubali."},{"id":6773,"sura":80,"from_aya":17,"to_aya":23,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17 - 23} Lakini pamoja na hayo, mwanadamu alikataa isipokuwa tu kuwa mtu asiye na shukrani, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: \" Ameangamia mwanaadamu! Nini kinachomkufurisha\" neema ya Mwenyezi Mungu, na ana upinzani mkubwa namna gani huu dhidi ya haki baada ya kuwa wazi. Naye pamoja na hayo yote ni nani? Yeye ndiye kitu dhaifu zaidi. Mwenyezi Mungu alimuumba kutokana na maji ya kudharauliwa, kisha akakadiria uumbaji wake na akamfanya kuwa mwanadamu mkamilifu sawasawa, na akakamilisha nguvu zake za dhahiri na zilizofichika. \"Kisha akamsahilishia njia\" za kidini na za kidunia, akamuongoza kwenye njia sahihi, akaibainishia, na akamtia katika mtihani kwa maamrisho na makatazo. \"Kisha akamfisha, akamtia kaburini.\" Yaani, akamtukuza kwa kumfanya azikwe, na wala hakumfanya kama wanyama wengine wote ambao mizoga yao iko juu ya uso wa ardhi. \"Kisha apendapo atamfufua\" baada ya kufa kwake kwa ajili ya malipo. Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayesimamia uendeshaji wa mwanadamu na kumgeuza katika migeuzo hii. Hakuna mshirika anayeshiriki naye katika hilo, na licha ya hayo yeye hafanyi yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, na hakutekeleza yale aliyomfaradhishia. Bali bado anazembea, huku akitakiwa kutekeleza aliyoamrishwa."},{"id":6774,"sura":80,"from_aya":24,"to_aya":32,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{24 - 32} Kisha Mwenyezi Mungu akamwelekeza kutazama na kufikiria juu ya chakula chake, na jinsi kilivyomfikia baada ya kupitia hatua nyingi, na [Mwenyezi Mungu] akamfanyia wepesi. Akasema: \"Hebu mtu na atazame chakula chake. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu\" juu ya ardhi. \"Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu. Kisha tukaotesha humo\" aina mbalimbali za vyakula vitamu na vizuri, \"nafaka\" zinazojumuisha nafaka za kila namna, \"na zabibu, na mimea ya majani. Na mizaituni, na mitende.\" Hapa ametaja hivi vinne kwa njia hii maalumu kwa sababu ya manufaa yake mengi. \"Na bustani zenye miti iliyo songana barabara. Na matunda, na malisho ya wanyama.\" Ndiyo maana akasema: \"Kwa manufaa yenu na mifugo yenu\" ambayo Mwenyezi Mungu ameiumba na akaitiisha kwa ajili yenu. Kwa hivyo, mwenye kutazama katika neema hizi, hilo linamlazimu kumshukuru Mola wake Mlezi na kufanya juhudi kubwa ya kurejea kwake, kumtii na kusadiki habari zake."},{"id":6775,"sura":80,"from_aya":33,"to_aya":42,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"33. Basi utakapokuja ukelele. 34. Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye. 35. Na mamaye na babaye. 36. Na mkewe na wanawe. 37. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha. 38. Siku hiyo ziko nyuso zitakazonawiri. 39. Zitacheka, zitachangamka. 40. Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi. 41. Giza totoro litazifunika. 42. Hao ndio makafiri watenda maovu. "},{"id":6776,"sura":80,"from_aya":33,"to_aya":42,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{33 - 42} Yaani, utakapokuja ukelele wa Kiyama, ambao kwa sababu ya mahangaiko yake masikio yatapata shida kubwa, na nyoyo zitafadhaika siku hiyo; kutokana na yale watu wataona ya kutisha na haja kubwa ya kuwa matendo mazuri yaliyotangulia. Mtu atawakimbia watu ambao ni wapenzi zaidi kwake na wanaomhurumia zaidi. Atakimbia kutoka kwa kaka yake, mama yake, baba yake, mkewe na watoto wake, kwa sababu \"Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.\" Yaani, nafsi yake itakuwa imemshughulisha, na akajishughulisha na kuiokoa, na hatajali kitu kingine chochote. Hapo viumbe vitagawanyika katika makundi mawili: wenye furaha na wenye huzuni. Ama wenye furaha, nyuso zao \"Siku hiyo zitanawiri\" kwa furaha kutokana na yale waliyoyajua ya wokovu wao na kufuzu kwao kufikia neema. \"Zitacheka, zitachangamka. Na nyuso\" za wana mashakani \"siku hiyo zitakuwa na mavumbi. Giza totoro litazifunika.\" Zitakuwa tayari zimekata tamaa kabisa ya kufikia heri yoyote, na zikajua mashaka yatakayozipata, na maangamio yake. \"Hao\" wenye maelezo haya, \"ndio makafiri watenda maovu.\" Yaani, wale waliokufuru neema ya Mwenyezi Mungu, wakakadhibisha ishara zake, na wakathubutu kufanya aliyoyaharamisha. Tunamwomba Mwenyezi Mungu msamaha na salama. Hakika Yeye ndiye Mpaji, Mkarimu mno."},{"id":6777,"sura":80,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote."},{"id":6778,"sura":80,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"***"}]}