{"result":[{"id":6969,"sura":95,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat At-Tin"},{"id":6970,"sura":95,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":6971,"sura":95,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu"},{"id":6972,"sura":95,"from_aya":1,"to_aya":8,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Ninaapa kwa tini na zaituni! 2.  Na kwa Mlima wa Sinai! 3. Na kwa mji huu wenye amani! 4. Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. 5. Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini! 6. Lakini wale walioamini na wakatenda mema, hao watapata ujira usiokwisha. 7. Basi ni kipi baadaye kitakachokukukadhibishia malipo? 8. Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote? "},{"id":6973,"sura":95,"from_aya":1,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1 - 3} Mwenyezi Mungu aliapa kwa miti hii miwili; kwa sababu ya manufaa mengi ya miti hii na matunda yake, na kwa sababu mamlaka yake katika ardhi ya Sham ndiyo yalikuwa mahala pa unabii wa Isa bin Maryam, amani iwe juu yake \"Na kwa Mlima wa Sinai\" ambapo palikuwa mahali pa unabii wa Musa, amani iwe juu yake. \"Na kwa mji huu wenye amani!\" Nao ni Makka Tukufu, mahala pa unabii pa Muhammad - rehema na amani zimshukie. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akaapa kwa sehemu hizi takatifu ambazo alizichagua na akatuma kutoka hapo manabii bora na watukufu zaidi."},{"id":6974,"sura":95,"from_aya":4,"to_aya":4,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4} Kinachoapwa kwa ajili yake hapa ni kauli yake: \"Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lililo bora kabisa\" na hakukosa chochote anachohitaji, kwa nje na ndani."},{"id":6975,"sura":95,"from_aya":5,"to_aya":6,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{5 - 6} Na licha ya neema hizi kuu, ambazo anapaswa kushukuru kwa sababu yake; viumbe wengi wamepotoka mbali na kutoa shukurani kwa neema hizi, kwa sababu ya wamejishughulisha pumbao na michezo, na wamejiridhisha na mambo duni kabisa na tabia chafu, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawarudisha \"kuwa chini kuliko walio chini\" Motoni, ambapo ni mahali pa watu maasi wanaomuasi Mola wao Mlezi. Isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwa imani,  vitendo vyema na maadili mema ya juu. \"Hao watapata\" kwa sababu ya hayo vyeo vya juu na \"ujira usiokwisha\" Bali ni raha zinazopatikana, furaha za kuwajia mara kwa mara, na neema nyingi za kudumu umilele bila ya kuondoka, matunda yake ni ya daima na pia kivuli chake."},{"id":6976,"sura":95,"from_aya":7,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{7 - 8} \"Basi ni kipi baadaye kitakachokukukadhibishia malipo?\" Yaani, ni nini kinachokufanya kukanusha ewe mwanadamu Siku ya Malipo juu ya matendo? Umeshaziona ishara nyingi za Mwenyezi Mungu zinazokupa yakini, na neema zake ambazo zinaweza kukufanya kutokufuru hata kimoja katika hizo. \"Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?\" Je, hekima yake inaweza kutaka aache viumbe bure, wasiamrishwe wala wasikatazwe, wala wasilipwe mazuri wala wasiadhibiwe? Au yule aliyemuumba mwanadamu hatua baada ya hatua, na akawafikisha neema mbalimbali, heri na wema visivyo na kipimo, na akawalea kwa malezi mazuri ni lazima awarudishe kwenye nyumba ambayo ndiyo makazi yao na marudio yao wanayokwenda na wanayoamini."},{"id":6977,"sura":95,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu."},{"id":6978,"sura":95,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}