{"result":[{"id":6979,"sura":96,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Al-Alaq"},{"id":6980,"sura":96,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":6981,"sura":96,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu"},{"id":6982,"sura":96,"from_aya":1,"to_aya":19,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba. 2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu. 3.  Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! 4. Ambaye amefundisha kwa kalamu. 5. Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui. 6. Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri. 7. Akijiona katajirika. 8. Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. 9. Umemuona yule anayemkataza. 10. Mja anaposali? 11. Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? 12. Au anaamrisha ucha Mungu? 13. Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? 14. Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? 15. Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! 16. Shungi la uwongo, lenye makosa! 17. Basi na awaite wenzake! 18. Nasi tutawaita Mazabania! 19. Hasha! Usimtii! Nawe sujudu na ujongee! "},{"id":6983,"sura":96,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Sura hii ndiyo sura ya kwanza ya Qur-ani iliyoteremshwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie. Ilifunuliwa kwake mwanzoni mwa unabii. Hapo, alikuwa hajui Kitabu ni nini wala imani. Basi Jibril, rehema na amani zimshukie, akamjia na ujumbe, na akamuamuru kusoma, lakini akakataa na akasema: 'Mimi sijui kusoma!' Basi akaendelea naye hivyo mpaka akasoma. Basi Mwenyezi Mungu akamteremshia: \"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba\" viumbe vyote kwa ujumla."},{"id":6984,"sura":96,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Kisha akamtaja mwanadamu hasa, na akataja mwanzo wa kuumbwa kwake \"kwa tone la damu.\" Basi aliyemuumba mwanadamu na akashughulikia suala la kumsimamia, ni lazima amsimamie kwa kumuamrisha na kumkataza, na hilo ni kwa kutuma Mitume na kuteremsha vitabu, na ndiyo maana akaamrisha kusoma baada ya kutaja kuumba kwake mwanadamu."},{"id":6985,"sura":96,"from_aya":3,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3 - 5} Kisha akasema: \"Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!\" Yaani, ana sifa nyingi za upana, ni mwingi wa ukarimu na hisani, na ni Mpaji kwa wingi, ambaye katika ukarimu wake ni kwamba alifundisha aina mbalimbali za elimu, na \"Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui.\" Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alimtoa tumboni mwa mama yake ilhali hajui chochote, na akampa uwezo wa kusikia, kuona, na ufahamu wa moyo, na akamwepesishia njia za elimu. Basi akamfundisha Qur-ani, akamfundisha hekima, na akamfundisha kwa kalamu, [ambayo kwayo zinahifadhiwa elimu] na haki zinawekwa sawasawa, na zinakuwa ni Mitume kwa watu zinazowakilisha mahali pa kuzungumza kwao. Basi sifa njema na neema ni za Mwenyezi Mungu ambaye amewajaalia neema hizi waja wake, ambazo hawawezi kuzilipa wala kushukuru, kisha akawaruzuku mali na riziki nyingi."},{"id":6986,"sura":96,"from_aya":6,"to_aya":8,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6 - 8} Lakini mwanadamu, kwa sababu ya ujinga wake na udhalimu wake; akijiona kajitosheleza; kwa hivyo akavuka mipaka, akafanya udhalimu, akajivuna kufuata uwongofu na akasahau kuwa kwa Mola wake Mlezi \"ndio marejeo\" na wala hakuogopa malipo. Bali huenda akafikia kiwango kwamba yeye mwenyewe aliacha uwongofu na tena akawalingania wengine kuuacha, akawa anakataza watu swala ambayo ndilo tendo bora zaidi la imani."},{"id":6987,"sura":96,"from_aya":9,"to_aya":14,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{9 - 14} Mwenyezi Mungu anamwambia muasi huyu mkaidi: \"Umeona\" ewe mwenye kumkataza mja anaposwali, \"kama yeye\" anayeswali \"yuko juu ya uwongofu\" kujua haki na kuifanyia kazi.  \"Au anaamrisha\" wengine \"ucha Mungu?\" Basi je ni vyema kumkataza yule ambaye anasifika kwa haya? Je, kumkataza si mojawapo ya matendo makuu ya kumpinga Mwenyezi Mungu na kupigana na haki? Kwani katazo halielekezwi isipokuwa kwa yule ambaye hayuko kwenye uwongofu, au anayeamrisha wengine kinyume cha ucha Mungu. \"Umeona\" huyu mwenye kukataza haki \"kama yeye akikanusha na anarudi nyuma\" akaacha amri. Kwani hamuogopi Mwenyezi Mungu na akahofu adhabu yake? \"Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona\" anayoyafanya na kuyatenda?"},{"id":6988,"sura":96,"from_aya":15,"to_aya":16,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{15 - 16} Kisha akamtishia ikiwa ataendelea kuwa hivyo, akasema: \"Kwani! Kama haachi\" hayo anayoyasema na kuyatenda, \"tutamkokota kwa shungi la nywele\" kwa ukali, nalo ni jambo la uhakika. Kwa maana ni \"Shungi la uongo, lenye makosa.\" Ni la uongo katika kile linachosema, na lenye makosa katika kile linachofanya."},{"id":6989,"sura":96,"from_aya":17,"to_aya":18,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{17 - 18} \"Basi na awaite\" huyu aliyestahiki adhabu \"wenzake.\" Yaani, watu wa baraza lake, na sahibu zake, na wote walio karibu naye ili wamsaidie katika yale yaliyomfika. \"Nasi tutawaita Mazabania!\" Yaani, walinzi wa Jahannam ili wamchukue na kumuadhibu. Basi na atazame ni lipi kati ya vikundi viwili hivi ni lenye nguvu na uwezo zaidi. Basi hii ndiyo hali ya mkatazaji huyu na adhabu anayoahidiwa."},{"id":6990,"sura":96,"from_aya":19,"to_aya":19,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{19} Ama hali ya anayekatazwa, Mwenyezi Mungu alimuamrisha kwamba asimsikilize huyu anayemkataza, wala asifuate makatazo yake, akasema: \"Hasha! Usimtii!\" Kwani haamrishi isipokuwa yenye hasara. \"Nawe sujudu\" kwa ajili ya Mola wako Mlezi, \"na jikurubishe\" kwake katika kusujudu na aina nyenginezo za utiifu na kujikurubisha kwake. Hayo yote humleta mtu karibu na radhi zake na kumleta karibu naye. Hili ni la jumla kwa kila mwenye kukataza heri na kwa kila mwenye kukatazwa heri, hata ikiwa sura hii iliteremka kwa sababu ya kisa cha Abu Jahl pale alipomkataa Mtume wa Mwenyezi - rehema na amani zimshukie \u2013 kuswali, akamtesa na kumuudhi."},{"id":6991,"sura":96,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u062e\u0627\u062a\u0645\u0629 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Imekamilika, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote."},{"id":6992,"sura":96,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}