{"result":[{"id":7087,"sura":107,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Al-Ma'un"},{"id":7088,"sura":107,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":7089,"sura":107,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu"},{"id":7090,"sura":107,"from_aya":1,"to_aya":7,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Je! Umemwona anayekadhibisha Malipo? 2. Huyo ndiye anayemsukuma yatima. 3. Wala hahimizi kumlisha masikini. 4.  Basi, ole wao wanaosali. 5. Ambao wanapuuza Sala zao. 6. Ambao wanajionyesha. 7. Nao huku wanazuia msaada. "},{"id":7091,"sura":107,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema akiwakashifu wale wanaoziacha haki zake na haki za waja wake: \"Je! Umemwona anayekadhibisha Malipo\" baada ya kufufuliwa, akaacha kuyaamini yale yaliyoletwa na Mitume."},{"id":7092,"sura":107,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} \"Huyo ndiye anayemsukuma yatima\" kwa nguvu na kwa ukali, wala hana huruma naye. Kwa sababu ya ugumu wa moyo wake, na kwa sababu hatarajii malipo wala haogopi adhabu."},{"id":7093,"sura":107,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} \"Wala hahimizi\" wengine \"kumlisha masikini\" naye mwenyewe basi ndiyo hata hawalishi masikini."},{"id":7094,"sura":107,"from_aya":4,"to_aya":5,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{4 - 5} \"Basi, ole wao wanaoswali\" lakini \u201cambao wanapuuza Sala zao.\" Yaani, wanaipoteza, wanapuuza wakati wake, na wanaharibu nguzo zake, na hili ni kwa sababu hawajali amri ya Mwenyezi Mungu. Pale ambapo walipuuza swala, ambayo ndiyo tendo muhimu zaidi la utiifu. Na mwenye kusahau swala ndiye anayestahiki kukashifiwa na kulaumiwa. Ama kusahau tu katika swala, hilo analifanya kila mtu, hata Nabii \u2013 rehema na amani ziwe juu yake."},{"id":7095,"sura":107,"from_aya":6,"to_aya":7,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{6 - 7} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawaelezea watu hawa kwamba wanajionyesha, na kwamba ni wagumu na hawana huruma, akasema: \"Ambao wanajionyesha.\" Yaani: wanafanya vitendo kwa ajili ya kujionyesha kwa watu. \"Nao huku wanazuia msaada.\" Yaani, wanazuia kutoa kitu ambacho hakina madhara kwao kukitoa kama vile kuazima au zawadi; kama  vile kuazima chombo, ndoo, shoka, na mambo mengine ambayo ni desturi kuyatoa bure. Lakini watu hawa kutokana na hamu yao kubwa juu ya vitu vyao, wanazuia msaada. Basi vipi wakiambiwa kutoa vilivyo vikubwa zaidi ya hayo? Katika Sura hii kuna kuhimizwa kulisha yatima na masikini, na kuchunga na kuihifadhi swala, na kuifanya kwa kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, na kuhimiza kutenda mema, na kupeana bure mambo mepesi kama vile kuazima chombo, ndoo, kitabu, na mfano wa hivyo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amewakashifu wale wasiofanya hivyo. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi."},{"id":7096,"sura":107,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}