{"result":[{"id":7097,"sura":108,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0633\u0645 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Tafsiri ya Surat Al-Kawthar"},{"id":7098,"sura":108,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0645\u0643\u0627\u0646 \u0646\u0632\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0633\u0648\u0631\u0629","text":"Ilishuka Makka"},{"id":7099,"sura":108,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0627\u0644\u0628\u0633\u0645\u0644\u0629","text":"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu"},{"id":7100,"sura":108,"from_aya":1,"to_aya":3,"type":"\u0627\u0644\u0645\u0642\u0637\u0639","text":"1. Hakika tumekupa kheri nyingi. 2. Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi. 3. Hakika anayekuchukia ndiye aliye mpungufu. "},{"id":7101,"sura":108,"from_aya":1,"to_aya":1,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Mtume wake Muhammad - rehema na amani zimshukie - [akimkumbusha neema zake juu yake]: \"Hakika tumekupa heri nyingi\" ambazo miongoni mwake ni yale ambayo Mwenyezi Mungu atampa Nabii wake \u2013 rehema na amani ziwe juu yake \u2013 [Siku ya Kiyama] kutoka kwenye mto uitwao: Al-Kawthar, na kutoka katika hodhi yake ambalo urefu wake ni mwendo wa mwezi mmoja, na upana wake  ni mwendo wa mwezi mmoja. Maji yake ni meupe kuliko maziwa na ni matamu kuliko asali. Vyombo vyake katika wingi wake na kung'aa kwake ni kama idadi ya nyota za mbinguni. Mwenye kunywa humo, hakuwa na kiu kamwe baada ya hapo."},{"id":7102,"sura":108,"from_aya":2,"to_aya":2,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{2} Na alipomtajia wema wake juu yake; akamuamrisha kumshukuru, akasema: \"Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.\" Amezitaja ibada hizi mbili hasa kwa sababu hizo ndizo ibada bora kabisa na mambo matukufu zaidi ya kujiweka kwayo karibu na Mwenyezi Mungu, na kwa sababu swala inajumuisha kunyenyekea moyoni na kwa viungo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na humhamisha kupitia aina mbali mbali za uja. Na katika kuchinja kuna kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu kwa bora zaidi alicho nacho mja miongoni mwa dhabihu, na kutoa mali ambazo roho zimefanywa kuzipenda na kuzifanyia ubahili."},{"id":7103,"sura":108,"from_aya":3,"to_aya":3,"type":"\u062a\u0641\u0633\u064a\u0631 \u0622\u064a\u0629","text":"{3} \"Hakika anayekuchukia\" na kukukashifu na kukupunguzia heshima, \"ndiye aliye mpungufu zaidi\" naye ndiye atakayekatikiwa matendo yake na utajo wake. Na ama Muhammad \u2013 rehema na amani ziwe juu yake, yeye hakika ndiye mkamilifu wa kweli, ambaye ana ukamilifu unaowezekana kwa kiumbe; kwa kuinuliwa utajo wake na wingi wa wasaidizi na wafuasi - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake."},{"id":7104,"sura":108,"from_aya":0,"to_aya":0,"type":"\u0646\u062c\u0648\u0645","text":"* * *"}]}